Sera ya Mpango wa Wasanidi Programu

(kuanza kutumika tarehe 31 Mei, 2024, isipokuwa ibainishwe vinginevyo)

Tujenge chanzo cha programu na michezo kinachoaminika zaidi ulimwenguni

Ubunifu wako huleta mafanikio tunayoshiriki, lakini ubunifu huo huambatana na majukumu. Sera hizi za Mpango wa Wasanidi Programu pamoja na Mkataba wa Usambazaji kwa Wasanidi Programu, huhakikisha kuwa tunashirikiana kusambaza programu zinazoaminika na zilizobuniwa kwa ustadi kwa zaidi ya watu bilioni moja kupitia Google Play. Tunakualika usome sera zetu hapa chini.

Maudhui yenye Vikwazo

Watu kutoka ulimwenguni kote hutumia Google Play kufikia programu na michezo kila siku. Kabla ya kutuma programu, jiulize iwapo imetimiza masharti ya Google Play na inatii sheria za mahali ulipo.

Kuhatarisha Maisha ya Watoto

Programu ambazo hazizuii watumiaji kutengeneza, kupakia au kusambaza maudhui yanayowezesha unyanyasaji wa watoto zitaondolewa mara moja kwenye Google Play. Hii ni pamoja na maudhui yote yanayoonyesha unyanyasaji wa watoto kingono. Ili uripoti maudhui yaliyo kwenye bidhaa ya Google yanayoweza kumnyanyasa mtoto, bofya Ripoti matumizi mabaya. Iwapo utapata maudhui mahali pengine kwenye intaneti, tafadhali wasiliana moja kwa moja na shirika husika katika nchi yako

Tunazuia matumizi ya programu ili kuwahatarisha watoto. Ikiwa ni pamoja na lakini si tu, matumizi ya programu kuendeleza tabia za kuwanyemelea watoto, kama vile:

  • Matendo yasiyofaa yanayowalenga watoto (kwa mfano, kuwapapasa au kuwagusa).
  • Kumpevua mtoto (kwa mfano, kuanzisha urafiki na mtoto mtandaoni ili kuwezesha mtagusano wa kingono mtandaoni na/au kubadilishana picha za ngono na mtoto huyo mtandaoni au nje ya mtandao).
  • Kuwafanya watoto wachukuliwe kwa mtazamo wa kingono (kwa mfano, picha zinazoonyesha, kuhimiza au kuendeleza unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto au kuwaonyesha watoto kwa namna inayoweza kusababisha unyanyasaji wa watoto kingono).
  • Dhuluma inayohusiana na masuala ya ngono (kwa mfano, kumtishia au kumhadaa mtoto kwa kutumia uwezo halisi au unaokisiwa wa kufikia picha nyeti za mtoto).
  • Ulanguzi wa mtoto (kwa mfano, utangazaji au kumshawishi mtoto kwa ajili ya biashara ya unyanyasaji wa kingono).

Tutachukua hatua stahiki, ikiwemo kutoa ripoti katika shirika la National Center for Missing & Exploited Children, iwapo tutatambua maudhui yanayoonyesha unyanyasaji wa watoto kingono. Ikiwa unaamini kuwa mtoto yupo hatarini, amenyanyaswa au ni mhasiriwa wa ulanguzi, wasiliana na wakala wako wa sheria katika eneo mahususi na shirika la usalama wa watoto lililoorodheshwa hapa.

Mbali na hayo, programu zinazowavutia watoto lakini zina maudhui ya watu wazima haziruhusiwi, ikiwa ni pamoja na, lakini si tu:

  • Programu zenye vurugu zilizokithiri, maudhui ya kutisha na ya umwagaji damu katika kiwango kikubwa.
  • Programu zinazoonyesha au kuhimiza shughuli hatarishi na za kudhuru.

Pia, haturuhusu programu zinazotangaza maudhui ya kujidunisha mwonekano au kujidharau ikiwa ni pamoja na programu zinazoonyesha utengenezaji wa viungo bandia, kupunguza uzito na marekebisho mengine ya urembo katika mwonekano wa mtu, kwa lengo la burudani.


Maudhui Yasiyofaa

Ili kudumisha usalama na heshima kwenye mfumo wa Google Play, tumebuni viwango vinavyobainisha na kuzuia maudhui ambayo hayafai au yanayodhuru watumiaji wetu.

Maudhui ya Ngono na Lugha Chafu

Haturuhusu programu ambazo zina maudhui ya ngono au lugha chafu au zinazoyatangaza ikiwa ni pamoja na ponografia au maudhui au huduma yoyote inayolenga kuchochea ngono. Haturuhusu programu au maudhui ya programu ambayo yanaonekana kutangaza au kuchochea kitendo cha ngono ili kulipwa. Haturuhusu programu ambazo zina maudhui yanayohusiana na tabia za kunyemelea kingono au kuyatangaza au kusambaza maudhui ya ngono yanayotayarishwa bila idhini. Maudhui yaliyo na picha za uchi yanaweza kuruhusiwa iwapo lengo lake la msingi ni kuelimisha, kuelezea uhalisia, sayansi au sanaa na ikiwa yana sababu.

Programu za katalogi—programu zinazoorodhesha majina ya vitabu au video kama sehemu ya katalogi pana ya maudhui—huenda zikasambaza majina ya vitabu (ikijumuisha vitabu pepe na vitabu vya kusikiliza) au video yanayojumuisha maudhui ya ngono mradi masharti yafuatayo yametimizwa:

  • Majina ya vitabu au video zenye maudhui ya ngono yanawakilisha sehemu ndogo ya katalogi ya jumla ya programu
  • Programu haitangazi majina ya vitabu au video zenye maudhui ya ngono. Majina haya bado yanaweza kuonekana kwenye mapendekezo kulingana na historia ya mtumiaji au wakati wa matangazo ya bei ya jumla. 
  • Programu haisambazi jina la kitabu au video yoyote yenye maudhui yanayohatarisha maisha ya watoto, ponografia au maudhui mengine yoyote ya ngono yaliyobainishwa kisheria kuwa si halali.
  • Programu inawalinda watoto kwa kuwazuia kufikia majina ya vitabu au video zenye maudhui ya ngono

Iwapo programu ina maudhui ambayo yanakiuka sera hii lakini maudhui hayo yanaonekana yanafaa katika eneo fulani, programu hiyo inaweza kupatikana kwa watumiaji katika eneo hilo, lakini haitapatikana kwa watumiaji kwenye maeneo mengine.

Ili kudumisha usalama na heshima kwenye mfumo wa Google Play, tumebuni viwango vinavyobainisha na kuzuia maudhui ambayo hayafai au yanayodhuru watumiaji wetu.
  • Kuonyesha uchi au picha zinazochochea ngono ambapo mhusika hajavaa chochote, ameficha kidogo au amevaa nguo isiyoficha uchi kabisa, na/au hali ambapo nguo aliyovaa haikubaliki katika muktadha husika wa umma.
  • Maonyesho, uhuishaji au michoro ya matendo ya ngono au picha zinazochochea ngono au kuonyesha sehemu za mwili zinazochochea ngono.
  • Maudhui yanayoonyesha au yanatumia visaidizi vya ngono, mwongozo wa ngono, vifaa vya ngono na mandhari ya ngono yasiyo halali.
  • Maudhui ya uzinifu au lugha chafu – ikiwa ni pamoja na, lakini si tu, maudhui ambayo yanaweza kuwa na lugha chafu, matusi, maandishi yenye lugha chafu, maneno muhimu ya ngono au ya watu wazima kwenye ukurasa wa programu katika Google Play au ndani ya programu.
  • Maudhui yanayoonyesha, yanayoeleza au yanayoshawishi watu kufanya vitendo vya kuingilia wanyama.
  • Programu zinazohimiza burudani inayohusiana na ngono, huduma za ukahaba au huduma zingine ambazo zinaweza kubainishwa kuwa za ngono au zinachochea ngono ili kulipwa, ikiwa ni pamoja na, lakini si tu kufidiwa kwa kufanya mapenzi au mipango ya kingono ambapo mshiriki mmoja anatarajiwa au anakisiwa kutoa pesa, zawadi au usaidizi wa kifedha kwa mshiriki mwingine (“uchumba wa kulipwa”).
  • Programu zinazoshusha hadhi ya watu au kuwatumia kama vifaa, kama vile programu zinazodai kuwavua watu nguo au kuona ndani ya nguo, hata kama zimewekwa lebo ya programu za mizaha au burudani. 
  •  Maudhui au tabia ambazo zinajaribu kutishia au kunyanyasa watu katika namna ya kingono, kama vile picha zinazochochea ngono, kamera iliyofichwa, maudhui ya ngono yaliyotayarishwa bila idhini kupitia teknolojia ya kubadilisha sura au teknolojia kama hiyo au maudhui yanayoonyesha unyanyasaji.

Matamshi ya Chuki

Haturuhusu programu ambazo zinaendeleza vurugu, kuhimiza chuki kati ya watu au makundi kwa misingi ya rangi, kabila, dini, ulemavu, umri, uraia, hali ya kuwa mwanajeshi mstaafu, mwelekeo wa kingono, jinsia, utambulisho wa kijinsia, matabaka na hali ya uhamiaji au sifa nyinginezo zinazohusiana na ubaguzi au utengaji wa kimfumo.

Programu zilizo na maudhui ya EDSA (maudhui ya Kielimu, Filamu za Hali Halisi, Sayansi au Sanaa) yanayohusiana na Nazi yanaweza kuzuiwa katika nchi fulani, kwa mujibu wa sheria na masharti husika.

Ili kudumisha usalama na heshima kwenye mfumo wa Google Play, tumebuni viwango vinavyobainisha na kuzuia maudhui ambayo hayafai au yanayodhuru watumiaji wetu.
  • Maudhui au mazungumzo yanayodai kuwa kikundi cha watu wanaolindwa hakina utu, ni dhaifu au kinafaa kuchukiwa.
  • Programu zilizo na maudhui ya chuki, hoja za ubaguzi au nadharia kuhusu kikundi kinacholindwa kuwa na sifa mbaya (k.m. hasidi, fisadi, uovu n.k.) au zinazodai kwa njia dhahiri au isiyo dhahiri kuwa kikundi hicho ni tisho kwa usalama wa wengine.
  • Maudhui au matamshi yanayohimiza watu wengine waamini kuwa watu wanapaswa kuchukiwa au kubaguliwa kwa sababu ni washiriki wa kikundi kinacholindwa.
  • Maudhui yanayohimiza ishara za chuki kama vile bendera, ishara, alama za cheo, vifaa au tabia zinazohusiana na makundi ya chuki.

Vurugu

Haturuhusu programu zinazoonyesha au zinazohimiza vurugu iliyokithiri au shughuli zingine hatari. Tunaruhusu programu zinazoonyesha maudhui ya kubuni yenye vurugu katika muktadha wa mchezo, kama vile katuni, uwindaji au uvuvi. 
 
Ili kudumisha usalama na heshima kwenye mfumo wa Google Play, tumebuni viwango vinavyobainisha na kuzuia maudhui ambayo hayafai au yanayodhuru watumiaji wetu.
  • Maonyesho dhahiri au maelezo ya vurugu za kihalisia au vitisho vya vurugu kwa mtu au mnyama yeyote.
  • Programu ambazo zinaendeleza hali ya kujiumiza, kujitia kitanzi, matatizo ya kula, michezo ya kusakamwa au matendo mengine ambayo yanasababisha kifo au majeraha makali.

Itikadi Kali yenye Vurugu

Haturuhusu mashirika ya kigaidi, makundi au mashirika mengine hatari ambayo yamejihusisha, yamejiandaa au yamedai kuhusika katika vitendo vya vurugu dhidi ya raia kuchapisha programu kwenye Google Play kwa sababu yoyote ile, ikiwemo kusajili wanachama.

Haturuhusu programu zilizo na maudhui yanayohusiana na itikadi kali ya vurugu au maudhui yanayohusiana na kupanga, kuandaa au kusifu vurugu dhidi ya raia, kama vile maudhui yanayoendeleza vitendo vya kigaidi, kuchochea vurugu au kusherehekea mashambulizi ya kigaidi. Ikiwa unachapisha maudhui yanayohusiana na itikadi kali ya vurugu kwa sababu za elimu, makala ya hali halisi, sayansi au sababu ya kisanii, kumbuka kutoa muktadha husika wa EDSA.

Matukio Nyeti

Haturuhusu programu zisizojali hisia za wengine au zinazonufaika na tukio nyeti lenye athari kubwa ya kijamii, kitamaduni au kisiasa, kama vile dharura za umma, majanga ya asili, dharura za afya ya umma, mapigano, vifo au matukio mengine ya kuhuzunisha. Tunaruhusu programu zilizo na maudhui yanayohusiana na tukio nyeti iwapo yana maudhui ya EDSA (Maudhui ya Kielimu, Filamu Tahakiki, Sayansi au Sanaa) au yanalenga kuwaarifu watumiaji au kuwahamasisha kuhusu tukio nyeti. 
Ili kudumisha usalama na heshima kwenye mfumo wa Google Play, tumebuni viwango vinavyobainisha na kuzuia maudhui ambayo hayafai au yanayodhuru watumiaji wetu.
  • Kukosa kujali hisia za wengine kuhusiana na kifo cha mtu halisi au kundi la watu kutokana na kujiua, kutumia dawa kupita kiasi, sababu za kiasili, n.k.
  • Kukataa kutokea kwa tukio kubwa la kuhuzunisha ambalo limerekodiwa kwenye vyanzo vya kuaminika.
  • Kuonekana kuwa unafaidika kutokana na tukio nyeti ilhali waathiriwa hawapati manufaa yoyote.

Uchokozi na Unyanyasaji

Haturuhusu programu zinazojumuisha au zinazohimiza vitisho, unyanyasaji au uchokozi.
Ili kudumisha usalama na heshima kwenye mfumo wa Google Play, tumebuni viwango vinavyobainisha na kuzuia maudhui ambayo hayafai au yanayodhuru watumiaji wetu.
  • Kuchokoza waathiriwa wa mizozo ya kidini au kimataifa.
  • Maudhui yanayonuia kudhulumu wengine kama vile kutoza kwa nguvu, usaliti n.k.
  • Kuchapisha maudhui kwa kusudi la kudunisha mtu hadharani.
  • Kunyanyasa waathiriwa au marafiki na familia za waathiriwa wa mkasa mkuu.

Bidhaa Hatari

Haturuhusu programu zinazowezesha uuzaji wa vilipuzi, bunduki, risasi au vifuasi vingine vya bunduki.

  • Vifuasi visivyoruhusiwa ni pamoja na vile vinavyowezesha bunduki kuiga ufyatuaji wa kiotomatiki au kugeuza bunduki ifyatue kiotomatiki (k.m hifadhi ya risasi, risasi zinazofyatuliwa kwa haraka, zana za kubadilisha ufyatuaji), na zana za kubebea risasi zilizo na zaidi ya risasi 30.

Haturuhusu programu zinazotoa maelezo kuhusu utengenezaji wa vilipuzi, bunduki, risasi, vifaa vya bunduki vinavyodhibitiwa au silaha zingine. Hii inajumuisha maelezo kuhusu jinsi ya kugeuza bunduki ifyatue kiotomatiki au iige ufyatuaji wa kiotomatiki.

Bangi

Haturuhusu programu zinazoendeleza uuzaji wa bangi au bidhaa zenye bangi, bila kujali uhalali wake.
Ili kudumisha usalama na heshima kwenye mfumo wa Google Play, tumebuni viwango vinavyobainisha na kuzuia maudhui ambayo hayafai au yanayodhuru watumiaji wetu.
  • Kuwaruhusu watumiaji waagize bangi kupitia kipengele cha kikapu cha ununuzi wa ndani ya programu.
  • Kuwasaidia watumiaji kupanga usafirishaji au uchukuaji wa bangi.
  • Kuendeleza uuzaji wa bidhaa zilizo na kemikali ya THC (Tetrahydrocannabinol), zikiwemo bidhaa kama vile mafuta ya CBD yaliyo na kemikali za THC.

Tumbaku na Pombe

Haturuhusu programu zinazoendeleza uuzaji wa tumbaku (ikijumuisha sigara za kielektroniki na vifaa vya kuvuta mihadarati) au kuhimiza matumizi mabaya au yasiyoruhusiwa ya tumbaku au pombe.
Maelezo ya ziada
  • Kuonyesha au kuhimiza matumizi au uuzaji wa tumbaku au pombe kwa watoto hakuruhusiwi.
  • Kudai kuwa matumizi ya tumbaku yanaweza kuboresha hali ya mtu kwa misingi ya kijamii, kingono, kitaaluma, kimawazo au riadha hakuruhusiwi.
  • Kuonyesha unywaji wa pombe kupita kiasi bila madhara yoyote, ikiwa ni pamoja na maonyesho ya kunywa pombe nyingi zaidi, kunywa kwa mfululizo au mashindano ya kunywa pombe bila madhara yoyote hakuruhusiwi.
  • Matangazo, ofa au kuangazia bidhaa za tumbaku kwa njia dhahiri (ikiwa ni pamoja na matangazo, mabango, aina na viungo vya tovuti za kuuza tumbaku) hakuruhusiwi.
  • Tunaweza kuruhusu uuzaji wa muda mfupi wa bidhaa za tumbaku katika programu za kusafirisha vyakula, katika maeneo fulani, kulingana na ulinzi na uthibitishaji wa umri (kama vile ukaguzi wa vitambulisho wakati wa kusafirishiwa).

Huduma za Fedha

Haturuhusu programu ambazo zinaonyesha watumiaji huduma na bidhaa za kifedha ambazo ni hatari au zinapotosha.

Kwa madhumuni ya sera hii, tutachukulia huduma na bidhaa za kifedha kuwa zile ambazo zinahusiana na usimamizi au uwekezaji wa pesa na sarafu za dijitali, ikiwa ni pamoja na ushauri wa binafsi.

Iwapo programu yako inajumuisha au inatangaza huduma na bidhaa za kifedha, ni lazima utii kanuni za jimbo na za mahali ulipo katika eneo au nchi yoyote ambako programu yako inalenga—kwa mfano, weka ufumbuzi mahususi unaotakikana kwa mujibu wa sheria za mahali ulipo.

Programu yoyote iliyo na vipengele vya kifedha ni sharti ijaze Fomu ya Taarifa ya Vipengele vya Kifedha ndani ya Dashibodi ya Google Play.

Biashara ya Kubahatisha

Haturuhusu programu ambazo zinawawezesha watumiaji kufanya biashara za kubahatisha.

Mikopo binafsi

Fasili yetu ya mikopo ya binafsi ni mtu binafsi, shirika au huluki kukopesha mteja binafsi pesa katika hali isiyojirudia, si kwa madhumuni ya kulipia mali isiyohamishika au elimu. Wateja wanaopokea mikopo ya binafsi huhitaji maelezo kuhusu ubora, sifa, ada, ratiba ya kulipa, hatari na manufaa ya aina za mikopo ili kufanya maamuzi ya busara kuhusu iwapo watachukua mkopo.

  • Mifano: Mikopo ya binafsi, mikopo inayolipwa ukipokea mshahara, mikopo kati ya mtu na mwenzake, mikopo ya kuweka rehani cheti cha umiliki wa gari
  • Mifano ambayo haijajumuishwa: Rehani, mikopo ya magari, mikopo yenye kiasi kinachoweza kurudiwarudiwa (kama vile kadi za mikopo, kutoa pesa za ziada kwenye akaunti)

Programu ambazo zinatoa mikopo ya binafsi, ikiwa ni pamoja na, lakini si tu, programu ambazo zinatoa mikopo moja kwa moja, zinazotangaza mikopo na zinazounganisha wateja na washirika wengine wanaotoa mikopo, zinapaswa kuweka Aina ya Programu kuwa "Fedha" katika Dashibodi ya Google Play na zifumbue maelezo yafuatayo katika metadata ya programu:

  • Vipindi vya chini na juu zaidi vya kulipa mikopo
  • Kiwango cha Juu Zaidi cha Asilimia ya Mwaka (APR), ambacho kwa kawaida hujumuisha asilimia ya riba pamoja na ada na gharama zingine za mwaka, au ada nyingine kama hizo zinazohesabiwa kwa mujibu wa sheria za mahali ulipo
  • Mfano unaoonyesha jumla ya gharama ya mkopo, zikiwemo ada kuu na ada zote zinazotozwa
  • Sera ya faragha ambayo inafumbua kwa uwazi kuhusu matukio ya kufikia, kukusanya, kutumia na kutuma data ya mtumiaji ambayo ni nyeti na binafsi, kutegemea masharti yaliyoainishwa kwenye sera hii

Haturuhusu programu zinazotangaza mikopo ya binafsi inayohitaji kumaliza kulipwa ndani ya siku 60 au chache zaidi kuanzia tarehe ambapo mkopo ulitolewa (tunaiita mikopo hii "mikopo ya binafsi ya kipindi kifupi").

Hali zisizofuata kanuni kwa sera hii zitazingatiwa kwa programu za mikopo binafsi zinazofanya kazi katika nchi ambapo kanuni mahususi zinaruhusu kwa udhahiri mbinu kama hizo za ukopeshaji wa muda mfupi chini ya mifumo ya kisheria iliyoidhinishwa. Katika hali hizi chache, hali zisizofuata kanuni zitatathminiwa kwa mujibu wa sheria za mahali ulipo na mwongozo wa unaotumika wa udhibiti wa nchi husika.

Ni lazima tuweze kutambua ikiwa kuna uhusiano kati ya akaunti yako ya msanidi programu na leseni au hati zozote zilizotolewa zinazothibitisha uwezo wako wa kutoa huduma za mikopo ya binafsi. Huenda ukaombwa maelezo ya ziada au hati ili kuthibitisha kuwa akaunti yako inatii sheria na kanuni zote za mahali ulipo.

Programu za mikopo ya binafsi, programu zenye lengo la msingi la kuwezesha upatikanaji wa mikopo ya binafsi (kwa mfano, zinazowashawishi au kuwavutia wateja) au programu za mikopo ya vifuasi (vikokotoo vya mikopo, mwongozo wa mikopo, n.k.) haziruhusiwi kufikia data nyeti, kama vile picha na anwani. Ruhusa zifuatazo haziruhusiwi:

  • Read_external_storage
  • Read_media_images
  • Read_contacts
  • Access_fine_location
  • Read_phone_numbers
  • Read_media_videos
  • Query_all_packages
  • Write_external_storage

Programu zinazotumia API au taarifa nyeti zinasimamiwa na sheria na masharti ya ziada. Tafadhali angalia Sera ya ruhusa ili upate maelezo zaidi.

Mikopo ya binafsi yenye APR ya juu

Nchini Marekani, haturuhusu programu za mikopo ya binafsi ambapo kiwango cha Asilimia ya Kila Mwaka (APR) ni asilimia 36 au zaidi. Ni lazima programu za mikopo ya binafsi nchini Marekani zionyeshe kima cha juu cha APR, kilichohesabiwa kwa mujibu wa Sheria ya Ukopeshaji wa Kweli (TILA).

Sera hii inatumika kwenye programu zinazotoa mikopo moja kwa moja, zinazotangaza mikopo na zinazounganisha wateja na watu au mashirika mengine ya kukopesha.

Masharti ya nchi mahususi

Programu za mikopo ya binafsi zinazolenga nchi zilizoorodheshwa lazima zitii masharti ya ziada na kutoa hati za ziada kama sehemu ya taarifa ya vipengele vya Kifedha ndani ya Dashibodi ya Google Play. Unapopokea ombi kutoka kwa Google Play, ni lazima utoe maelezo ya ziada au hati zinazohusiana na namna unavyotii kanuni zinazotumika na masharti ya utoaji leseni.

  1. India
    • Ikiwa umepewa leseni na Benki Kuu ya India (RBI) kutoa mikopo ya binafsi, ni sharti utume nakala ya leseni ili tuikague.
    • Ikiwa huhusiki moja kwa moja katika shughuli za kukopesha pesa na unatoa tu mfumo wa kuwezesha ukopeshaji wa pesa unaofanywa na Kampuni za Fedha Zisizo Benki (NBFC) au benki kwa watumiaji, utahitaji kueleza hali hiyo kwa usahihi katika taarifa.
      • Pia, majina yote ya NBFC na benki zilizosajiliwa lazima yafumbuliwe kwa njia dhahiri kwenye maelezo ya programu yako.
  2. Indonesia
    • Ikiwa programu yako inajihusisha na shughuli za Huduma za Ukopeshaji Pesa Kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa mujibu wa Kanuni ya OJK Nambari 77/POJK.01/2016 (kadri inavyoweza kurekebishwa mara kwa mara), lazima uwasilishe nakala ya leseni yako halali ili tuikague.
  3. Ufilipino
    • Kampuni zote za ufadhili na ukopeshaji zinazotoa mikopo kwa kutumia Mifumo ya Ukopeshaji Mtandaoni (OLP) lazima zipate Namba ya Usajili wa SEC na Namba ya Cheti cha Uidhinishaji (CA) kutoka kwenye Tume ya Soko la Hisa na Ubadilishaji nchini Ufilipino (PSEC).
      • Pia, unapaswa kufumbua Jina la Shirika lako, jina la biashara, Namba ya Usajili wa PSEC, na Cheti cha Uidhinishaji ili Uendeshe Kampuni ya Ufadhili/Ukopeshaji (CA) kwenye maelezo ya programu yako.
    • Programu zinazojihusisha na shughuli za kuchangisha pesa kwa kutoa mikopo, kama vile ukopeshaji kati ya watu au mashirika (P2P) au kama ilivyofafanuliwa chini ya Sheria na Kanuni Zinazoongoza Kuchangisha pesa (Sheria ya CF), lazima zichakate miamala kupitia watu au mashirika yaliyosajiliwa na PSEC kutekeleza CF.
  4. Naijeria
    • Wakopeshaji Pesa Kidijitali (DML) lazima wafuate na wakamilishe LIMITED INTERIM REGULATORY/ REGISTRATION FRAMEWORK AND GUIDELINES FOR DIGITAL LENDING, 2022 (kadri inavyoweza kurekebishwa mara kwa mara) ya Tume ya Kitaifa ya Ushindani na Ulinzi wa Watumiaji (FCCPC) ya Naijeria ili kupata barua ya idhini iliyothibitishwa kutoka FCCPC.
    • Wakusanyaji wa mikopo lazima watoe hati na/au cheti kwa ajili ya huduma za ukopeshaji kidijitali na maelezo ya mawasiliano ya kila DML iliyoshirikishwa.
  5. Kenya
    • Watoa Huduma za Mikopo Dijitali (DCP) wanapaswa kukamilisha mchakato wa usajili wa DCP ili wapate leseni kutoka Benki Kuu ya Kenya (CBK). Unapaswa kutoa nakala ya leseni yako kutoka CBK kama sehemu ya kuthibitisha taarifa zako.
    • Ikiwa huhusiki moja kwa moja katika shughuli za kukopesha pesa na unaweka tu mfumo wa kuwezesha ukopeshaji wa pesa unaofanywa na Watoa Huduma za Mikopo Dijitali kwa watumiaji, utahitaji kueleza hali hiyo kwa usahihi katika taarifa na utoe nakala ya leseni ya DCP ya washirika husika.
    • Kwa sasa, tunapokea tu taarifa na leseni kutoka kwa huluki zilizochapishwa chini ya Orodha ya Watoa Huduma za Mikopo Dijitali kwenye tovuti rasmi ya CBK.
  6. Pakistani
    • Kila mkopeshaji wa Kampuni za Fedha Zisizo Benki (NBFC) anaweza tu kuchapisha Programu moja ya Ukopeshaji Kidijitali (DLA). Wasanidi programu wanaojaribu kuchapisha zaidi ya Programu moja ya Ukopeshaji Kidijitali (DLA) kwa kila Kampuni za Fedha Zisizo Benki (NBFC) wanahatarisha kufungiwa akaunti yao ya msanidi programu na akaunti zingine zozote zinazohusiana.
    • Ni lazima uwasilishe uthibitisho wa idhini kutoka Tume ya Soko la Hisa na Ubadilishaji nchini Pakistani (SECP) ili kutoa au kuwezesha huduma za ukopeshaji dijitali nchini Pakistani.
  7. Tailandi
    • Programu za mikopo binafsi zinazolenga Tailandi, zenye kiwango cha riba asilimia 15 au zaidi, ni sharti zipate idhini halali kutoka Benki ya Tailandi (BoT) au Wizara ya Fedha (MoF). Ni sharti wasanidi programu watoe hati zinazothibitisha uwezo wao wa kutoa au kuwezesha mikopo binafsi nchini Tailandi. Hati inapaswa kujumuisha:
      • Nakala ya leseni iliyotolewa na Benki ya Tailandi ya kuendesha biashara kama mtoa huduma wa mikopo binafsi au shirika dogo la kifedha.
      • Nakala ya leseni yake ya biashara ya fedha ya Pico iliyotolewa na Wizara ya Fedha ili kufanya biashara kama biashara ya kutoa mikopo ya Pico au Pico-plus.
Ili kudumisha usalama na heshima kwenye mfumo wa Google Play, tumebuni viwango vinavyobainisha na kuzuia maudhui ambayo hayafai au yanayodhuru watumiaji wetu.

Mashindano, Michezo na Kamari za Pesa Halisi

Tunaruhusu programu za kamari zinazotumia pesa halisi, matangazo yanayohusiana na kamari za pesa halisi, mipango ya kutuza uaminifu iliyo na matokeo ya michezo na programu za michezo dhahania ya muda mfupi zinazotimiza masharti fulani.

Programu za Kamari

Kwa kutegemea masharti na utii wa sera zote za Google Play, tunaruhusu programu zinazowezesha au kuruhusu kamari ya mtandaoni katika nchi mahususi, ilimradi Msanidi Programu akamilishe mchakato wa kutuma ombi kwa programu za kamari zinazosambazwa kwenye Google Play, ni mhudumu aliyeidhinishwa na serikali na/au mamlaka husika ya serikali inayosimamia kamari katika nchi mahususi na anatoa leseni halali ya kuendesha shughuli katika nchi mahususi kwa aina ya bidhaa ya kamari ya mtandaoni ambayo angependa kutekeleza. 

Tunaruhusu tu programu za kamari zilizoidhinishwa au kupewa leseni halali zilizo na aina zifuatazo za bidhaa za kamari ya mtandaoni 

  • Michezo ya Kasino ya Mtandaoni
  • Kuwekea Michezo Dau
  • Mashindano ya Farasi (ambayo yanadhibitiwa na kupewa leseni kando na Kuwekea Michezo Dau)
  • Bahati nasibu
  • Michezo Dhahania ya Muda Mfupi

Lazima programu zinazostahiki zitimize masharti yafuatayo:

  • Ni sharti msanidi programu akamilishe mchakato wa kutuma ombi ili aweze kusambaza programu kwenye Google Play;
  • Ni sharti programu itii sheria zote husika na viwango vya sekta katika kila nchi ambapo inasambazwa;
  • Ni lazima msanidi programu awe na leseni halali ya kamari kwa kila nchi au jimbo/eneo ambako programu imesambazwa;
  • Msanidi programu hafai kutoa aina ya bidhaa ya kamari inayozidi maelezo kwenye leseni ya kamari;
  • Lazima programu izuie watumiaji ambao hawajafikisha umri unaotakikana kuitumia;
  • Lazima programu izuie ufikiaji na utumiaji kutoka nchi, majimbo/maeneo, au maeneo ya kijiografia ambayo hayajaruhusiwa kwa mujibu wa leseni ya kamari iliyotolewa na msanidi programu;
  • Programu HAIPASWI kununuliwa kama programu inayolipishwa kwenye Google Play wala kutumia mfumo wa Kutozwa kupitia Google Play;
  • Ni lazima programu ipakuliwe na kusakinishwa bila malipo kutoka kwenye Duka la Google Play;
  • Ni lazima programu ipewe ukadiriaji wa AO (Watu Wazima Pekee) au ukadiriaji wa IARC unaolingana na huo; na
  • Ni lazima programu na uorodheshaji wake katika Google Play zitoe maelezo kwa njia dhahiri kuhusu uchezaji kamari kwa kuwajibika.

Programu nyingine za Mechi, Mashindano na Michezo ya Pesa Halisi

Kwa programu nyingine zote ambazo hazitimizi masharti ya kujiunga kwa programu za kamari zilizobainishwa hapo juu na ambazo hazijumuishwi kwenye "Majaribio Mengine ya Michezo ya Pesa Halisi" iliyobainishwa hapa chini, haturuhusu maudhui au huduma zinazowezesha au zinazoruhusu uwezo wa mtumiaji kuweka dau, kubahatisha au kushiriki kwa kutumia pesa halisi (ikiwa ni pamoja na vipengee vilivyo ndani ya programu vinavyonunuliwa kwa pesa) ili kupokea zawadi yenye thamani ya pesa halisi. Orodha hii inajumuisha, lakini si tu, kasino za mtandaoni, kuwekea michezo dau, bahati nasibu na michezo inayokubali pesa na hutoa zawadi za pesa taslimu au tuzo nyingine halisi (isipokuwa programu zinazoruhusiwa chini ya masharti ya Mipango ya Kudumisha Uaminifu katika Michezo yaliyofafanuliwa hapa chini).

Mifano ya ukiukaji

  • Michezo inayokubali pesa ili kutoa fursa ya kushinda tuzo halisi au ya kifedha
  • Programu zilizo na vipengele au vipengee vya usogezaji (k.m. vipengee vya menyu, vichupo, vitufe, mionekano ya wavuti, n.k.) zinazotoa mwito wa kuchukua hatua ya kuweka dau, kubahatisha au kushiriki katika michezo au mashindano kwa kutumia pesa halisi, kama vile programu zinazoalika watumiaji “KUWEKA DAU!” au “KUJISAJILI!” au “KUSHINDANA!” katika mashindano ili kupata fursa ya kushinda zawadi za pesa taslimu.
  • Programu zinazokubali au kudhibiti wanaoweka dau, sarafu za ndani ya programu, ushindi au kuweka pesa za kamari, au kupata zawadi halisi au yenye thamani ya pesa.

Majaribio Mengine ya Michezo ya Pesa Halisi

Tunaweza kufanya majaribio ya muda mfupi mara mojamoja kwa aina fulani za michezo ya pesa halisi katika baadhi ya maeneo. Ili upate maelezo, rejelea ukurasa huu wa Kituo cha Usaidizi. Jaribio la Michezo ya Kreni Mtandaoni nchini Japani liliisha tarehe 11 Julai 2023. Kuanzia tarehe 12 Julai 2023, huenda programu za Michezo ya Kreni Mtandaoni zikaorodheshwa kwenye Google Play duniani kote kwa kutegemea sheria inayotumika na masharti fulani.

Mipango ya Kudumisha Uaminifu katika Michezo

Panaporuhusiwa na sheria na bila kutegemea masharti ya ziada ya leseni za kamari au michezo, tunaruhusu mipango ya kudumisha uaminifu inayowapa watumiaji zawadi halisi au zenye thamani ya pesa, kwa mujibu wa masharti yafuatayo ya kujiunga kwenye Duka la Google Play:

Kwa programu zote (za michezo na zisizo za michezo):

  • Lazima manufaa au zawadi za mpango wa kudumisha uaminifu ziwe za ziada na zitegemee muamala wowote unaostahiki wa kifedha ndani ya programu (ambapo muamala wa kifedha unaotimiza masharti lazima uwe muamala halali tofauti wa kutoa huduma na bidhaa za mpango wa kudumisha uaminifu pekee) na hazipaswi kutegemea ununuzi wala kuwekwa vinginevyo kwenye hali yoyote ya ubadilishaji kwa kukiuka masharti ya sera ya Mashindano, Michezo na Kamari za Pesa Halisi.
    • Kwa mfano, hakuna sehemu ya muamala wa kifedha unaotimiza masharti unaopaswa kuwakilisha ada au kuweka dau ili kushiriki katika mpango wa kudumisha uaminifu na muamala wa kifedha unaotimiza masharti haupaswi kusababisha ununuzi wa bidhaa au huduma kwa bei ya juu kuliko kawaida.

Kwa programu za Michezo:

  • Zawadi au pointi za uaminifu zilizo na manufaa au zawadi zinazohusiana na miamala ya pesa inayoruhusiwa, zinaweza tu kutolewa au kutumiwa kwa msingi wa uwiano usiobadilika, ambako uwiano huo umebainishwa kwa uwazi kwenye programu na pia kwenye kanuni rasmi zinazopatikana hadharani katika mpango. Pia, upataji wa manufaa au thamani ya matumizi haupaswi kuwekewa dau, kutolewa kama zawadi au kutegemea utendaji wa mchezo au matokeo ya bahati nasibu.

Kwa programu zisizo za Michezo:

  • Pointi au zawadi za kudumisha uaminifu zinaweza kuhusishwa na mashindano au matokeo ya bahati nasibu iwapo zinatimiza masharti yaliyo hapa chini. Mipango ya kudumisha uaminifu iliyo na manufaa au zawadi zinazohusiana na miamala ya kifedha inayoruhusiwa inapaswa:
    • Kuchapisha sheria rasmi za mpango ndani ya programu.
    • Kwa mipango inayohusisha mifumo ya vibadala, bahati nasibu au zawadi za nasibu: onyesha kwenye sheria na masharti rasmi ya programu 1) thamani za mipango yoyote ya zawadi inayotumia thamani zisizobadilika ili kubaini zawadi na 2) mbinu za kuchagua (k.m. vibadala vinavyotumiwa kubaini zawadi) kwa mipango mingine yote kama hiyo.
    • Kubainisha idadi mahususi ya washindi, tarehe ya mwisho ya kujiunga na tarehe ya kutoa zawadi, kwa kila tangazo, kwa mujibu wa sheria na masharti rasmi ya mpango unaotoa bahati nasibu, droo au matangazo mengine kama haya.
    • Kurekodi uwiano wowote usiobadilika wa pointi za uaminifu au ujumlishaji na utumiaji wa zawadi za uaminifu kwa njia ya wazi katika programu na pia kwenye sheria na masharti rasmi ya programu.
Aina ya programu iliyo na mpango wa kudumisha Uaminifu Kudumisha uaminifu katika michezo na zawadi zinazoweza kubadilika Zawadi za kudumisha uaminifu kulingana na uwiano au ratiba isiyoweza kubadilishwa Sheria na Masharti ya mpango wa kudumisha uaminifu yanahitajika Lazima Sheria na Masharti yaonyeshe thamani au mbinu ya kuchagua ya fursa yoyote kulingana na mpango wa kudumisha uaminifu
Mchezo Hairuhusiwi Inaruhusiwa Sharti ijazwe Haitumiki (Programu za michezo haziruhusiwi kuwa na vipengele vya bahati nasibu katika mipango ya kudumisha uaminifu)
Si ya Michezo Inaruhusiwa Inaruhusiwa Sharti ijazwe Inahitajika

 

Matangazo ya Kamari au Michezo inayotumia Pesa Halisi na Mashindano ndani ya Programu zinazosambazwa kwenye Google Play

Tunaruhusu programu ambazo zina matangazo ya kamari, mashindano na michezo ya pesa halisi ikiwa zinatimiza masharti yafuatayo:

  • Ni lazima matangazo na programu (ikijumuisha watangazaji) zitii sheria zote husika na viwango vya sekta katika nchi yoyote ambako matangazo yanaonyeshwa;
  • Lazima programu zitimize masharti yote yanayotumika ya leseni za matangazo katika nchi husika kuhusu bidhaa na huduma zote zinazohusiana na kamari, ambazo zinatangazwa;
  • Programu haipaswi kuonyesha tangazo la kamari kwa watu walio na umri wa chini ya miaka 18;
  • Programu haipaswi kujumuishwa kwenye mpango wa Programu za Familia Yote;
  • Programu haipaswi kulenga watu walio na umri wa chini ya miaka 18;
  • Ni lazima tangazo lionyeshe kwa njia ya wazi maelezo kuhusu uchezaji wa kamari kwa kuwajibika kwenye ukurasa wake wa kutua, ukurasa wa programu inayotangazwa katika Google Play au katika programu, iwapo unatangaza Programu ya Kamari (kama ilivyobainishwa hapo juu);
  • Programu haipaswi kutoa maudhui ya kuiga kamari (k.m. programu za kasino ya kijamii; programu zilizo na mashine pepe ya kuweka pesa);
  • Programu hazipaswi kuwa na utendaji unaoruhusu mashindano, bahati nasibu au kamari au mchezo unaotumia pesa halisi au utendaji saidizi (k.m utendaji unaosaidia kuweka dau, malipo, ufuatiliaji wa thamani au alama za spoti, au usimamizi wa fedha za kushiriki);
  • Maudhui ya programu hayapaswi kutangaza au kuelekeza watumiaji kwenye huduma za mashindano au bahati nasibu, kamari au michezo inayotumia pesa halisi

Programu zinazotimiza tu masharti yote katika sehemu iliyoorodheshwa (hapo juu) ndizo zinaweza kuonyesha matangazo ya mashindano au bahati nasibu, kamari au michezo inayotumia pesa halisi. Programu za Kamari Zinazokubaliwa (kama ilivyobainishwa hapo juu), au Programu za Spoti Dhahania za Muda Mfupi zinazokubaliwa (jinsi ilivyobainishwa hapa chini) zinazotimiza masharti ya kwanza hadi sita hapo juu, zinaweza kuonyesha matangazo ya mashindano au bahati nasibu, kamari au michezo inayotumia pesa halisi.

Mifano ya ukiukaji

  • Programu ambayo imebuniwa kwa watumiaji wa umri wa chini na huonyesha tangazo linaloendeleza huduma za kamari
  • Mchezo wa kasino wa kuiga ambao hutangaza au huelekeza watumiaji kwenye kasino za pesa halisi
  • Programu ya ufuatiliaji wa thamani za spoti ambayo ina matangazo yaliyojumuishwa na ambayo imeunganishwa kwenye tovuti ya kuweka dau katika spoti
  • Programu zilizo na matangazo ya kamari ambayo yanakiuka sera yetu ya Matangazo Yanayopotosha, kama vile matangazo yanayoonekana kwa watumiaji kama vile vitufe, aikoni au vipengee vingine vinavyoshirikisha mtumiaji ndani ya programu

Programu za Michezo Dhahania ya Muda Mfupi (DFS)

Tunaruhusu tu programu za spoti dhahania za muda mfupi (DFS), kama ilivyobainishwa na sheria ya mahali ulipo, iwapo zinatimiza masharti yafuatayo:

  • Programu inapaswa iwe 1) inasambazwa tu nchini Marekani au 2) inaruhusiwa kwa mujibu wa masharti ya Programu za Kamari na mchakato wa kutuma ombi uliobainishwa kwa nchi zisizo Marekani;
  • Ni lazima wasanidi programu wakamilishe mchakato wa kutuma ombi la DFS na likubaliwe ili waweze kusambaza programu kwenye Google Play;
  • Ni lazima programu itii sheria zote husika na viwango vya sekta katika nchi ambako inasambazwa;
  • Ni lazima programu zizuie watoto ili wasiendeleze shughuli zozote zinazohusu pesa katika programu;
  • Programu HAZIPASWI kununuliwa kama programu zinazonunuliwa kwenye Google Play, au kutumia huduma ya Kutozwa kupitia Google Play;
  • Ni lazima programu ipakuliwe na kusakinishwa bila malipo katika Duka la Google Play;
  • Ni lazima programu ipewe ukadiriaji wa AO (Watu Wazima Pekee) au ukadiriaji wa IARC unaolingana na huo
  • Ni lazima programu na uorodheshaji wake katika Google Play zitoe maelezo kwa njia dhahiri kuhusu uchezaji kamari kwa kuwajibika;
  • Ni lazima programu zitii sheria zote husika na viwango vya sekta katika nchi ambapo zinasambazwa;
  • Ni lazima wasanidi programu wawe na leseni halali ya kila eneo au jimbo la Marekani ambapo leseni inatakiwa ili kutumia programu za michezo dhahania ya muda mfupi;
  • Ni lazima programu zizuie matumizi yake katika maeneo au majimbo ya Marekani ambapo wasanidi programu hawana leseni inayohitajika ya programu za michezo dhahania ya muda mfupi;
  • Ni lazima programu zizuie matumizi yake katika maeneo au majimbo ya Marekani ambapo programu za michezo dhahania ya muda mfupi haziruhusiwi.

Shughuli Zinazokiuka Sheria

Haturuhusu programu zinazowezesha au kuendeleza shughuli zinazokiuka sheria.
Ili kudumisha usalama na heshima kwenye mfumo wa Google Play, tumebuni viwango vinavyobainisha na kuzuia maudhui ambayo hayafai au yanayodhuru watumiaji wetu.
  • Kuwezesha uuzaji au ununuzi wa dawa za kulevya.
  • Inayoonyesha au inayohamasisha watoto kutumia au kuuza dawa za kulevya, pombe au tumbaku.
  • Maagizo ya kupanda au kutengeneza dawa za kulevya.

Maudhui Yaliyozalishwa na Watumiaji

Maudhui yaliyozalishwa na watumiaji (UGC) ni maudhui ambayo watumiaji huchangia kwenye programu. Maudhui hayo huonekana au kufikiwa na angalau kikundi fulani cha wanaotumia programu.

Programu ambazo zinajumuisha au zinaangazia maudhui yaliyozalishwa na watumiaji, ikijumuisha programu ambazo ni vivinjari au viteja maalumu ili kuwaelekeza watumiaji kwenye mfumo wa maudhui yaliyozalishwa na watumiaji, lazima zitekeleze udhibiti imara, wenye ufanisi na endelevu katika maudhui yaliyozalishwa na watumiaji ambao:

  • Unahitaji watumiaji wakubali sheria na masharti ya programu na/au sera ya watumiaji kabla ya watumiaji kuunda au kupakia maudhui yaliyozalishwa na watumiaji (UGC);
  • Unabainisha maudhui na matendo yasiyofaa (kwa njia inayotii Sera za Mpango wa Wasanidi Programu wa Google Play), na kuzizuia kwenye sheria na masharti ya programu au sera za mtumiaji;
  • Unafanya udhibiti wa maudhui yaliyozalishwa na watumiaji kadiri inavyofaa na kulingana na aina za maudhui yaliyozalishwa na watumiaji yanayopangishwa na programu. Hii inajumuisha kutoa mfumo wa ndani ya programu kwa kuripoti na kuzuia maudhui yasiyofaa yaliyozalishwa na watumiaji na watumiaji, na kuchukua hatua dhidi ya maudhui yaliyozalishwa na watumiaji au watumiaji panapofaa. Hali tofauti za maudhui yaliyozalishwa na watumiaji zinaweza kuhitaji juhudi tofauti za udhibiti. Kwa mfano:
    • Programu zenye maudhui yaliyozalishwa na watumiaji zinazotambua kundi mahususi la watumiaji kupitia njia kama vile uthibitishaji wa watumiaji au usajili wa nje ya mtandao (kwa mfano, programu zinazotumika kwa upekee katika shule au kampuni mahususi, nk.) ni sharti zitoe utendaji wa programu ili kuripoti maudhui na watumiaji.
    • Vipengele vya maudhui yaliyozalishwa na watumiaji vinavyowawezesha watumiaji kuwasiliana moja kwa moja na watumiaji mahususi (kwa mfano, ujumbe wa moja kwa moja, kutambulisha, kutaja, nk) ni sharti vitoe utendaji wa programu wa kuzuia watumiaji.
    • Programu zinazotoa uwezo wa kufikia maudhui yaliyozalishwa na watumiaji yanayoweza kufikiwa na umma, kama vile programu za mitandao jamii na blogu, lazima zitekeleze utendaji wa programu wa kuripoti watumiaji na maudhui, na kuzuia watumiaji.
    • Katika hali ya programu za uhalisia ulioboreshwa (AR), ni lazima udhibiti wa maudhui yaliyozalishwa na watumiaji (ikiwa ni pamoja na mfumo wa kuripoti wa ndani ya programu) uwajibikie matukio yenye utata ya maudhui yaliyozalishwa na watumiaji katika uhalisia ulioboreshwa (kwa mfano, picha ya uhalisia ulioboreshwa wa maudhui dhahiri ya ngono) na data nyeti ya eneo la kurekodi uhalisia ulioboreshwa (kwa mfano, maudhui ya uhalisia ulioboreshwa yaliyorekodiwa katika eneo linalolindwa, kama vile makao ya kijeshi, au mali ya binafsi ambapo hatua ya kurekodi uhalisia ulioboreshwa inaweza kusababisha matatizo kwa mmiliki wa mali);
  • Inaweka kinga za kuzuia uchumaji wa mapato ndani ya programu ili kuzuia matendo ya watumiaji yasiyofaa.

Maudhui ya ngono ya kuambatana

Maudhui ya ngono yanachukuliwa kuwa “ya kuambatana" kama yanajitokeza kwenye programu ya maudhui yaliyozalishwa na watumiaji ambayo (1) hutoa ufikiaji wa maudhui yasiyo ya ngono, na (2) haitangazi wala kupendekeza maudhui ya ngono. Maudhui ya ngono yanabainishwa kuwa si halali chini ya sheria inayotumika na maudhui yanayohatarisha maisha ya watoto hayachukuliwi kuwa ni “ya kuambatana” na hayaruhusiwi.

Programu za maudhui yaliyozalishwa na watumiaji zinaweza kuwa na maudhui ya ngono ya kuambatana kama masharti yote yafuatayo yametimizwa:

  • Maudhui kama hayo hufichwa kwa chaguo msingi nyuma ya vichujio ambavyo huhitaji angalau vitendo viwili vya mtumiaji ili kuzima kabisa (kwa mfano, nyuma ya kiunganishi cha kufumba msimbo au kuzuiwa kutoka kwenye utazamaji kwa chaguomsingi isipokuwa iwapo "utafutaji salama" umezimwa).
  • Watoto, kama inavyofafanuliwa katika Sera ya familia, wamezuiwa waziwazi wasifikie programu yako kwa kutumia mifumo ya kuchagua umri kama vile kuchagua umri au mfumo unaofaa kama inavyofafanuliwa na sheria inayotumika.
  • Programu yako hutoa majibu sahihi kwenye dodoso la daraja ukadiriaji wa maudhui kuhusu maudhui yaliyozalishwa na watumiaji, jinsi sera ya daraja la maudhui inavyotaka.

Programu ambazo lengo lake la msingi ni kuangazia maudhui yenye utata yaliyozalishwa na watumiaji, zitaondolewa kwenye Google Play. Aidha, programu ambazo lengo lake la msingi ni kupangisha maudhui yenye utata yaliyozalishwa na watumiaji, au ambazo zinakuza umaarufu miongoni mwa watumiaji kuwa ni sehemu ambapo maudhui kama hayo huendelezwa, pia zitaondolewa kwenye Google Play.

Ili kudumisha usalama na heshima kwenye mfumo wa Google Play, tumebuni viwango vinavyobainisha na kuzuia maudhui ambayo hayafai au yanayodhuru watumiaji wetu.
  • Kutangaza maudhui ya ngono dhahiri yanayozalishwa na watumiaji, ikiwa ni pamoja na kutumia au kuruhusu vipengele vinavyolipishwa ambavyo lengo lake kuu ni kuhimiza usambazaji wa maudhui yenye utata.
  • Programu zilizo na maudhui yanayozalishwa na watumiaji (UGC) zisizo na kinga za kutosha dhidi ya vitisho, unyanyasaji, au uchokozi, hasa unaoelekezwa kwa watoto.
  • Machapisho, maoni, au picha zilizo ndani ya programu ambazo zinalenga kunyanyasa au kulenga mtu mwingine kwa matusi, mashambulizi kwa kukusudia, au kejeli.
  • Programu ambazo zimeshindwa kabisa kushughulikia malalamiko ya watumiaji kuhusu maudhui yenye utata.

Maudhui na Huduma za Afya

Haturuhusu programu zinazoonyesha watumiaji maudhui na huduma hatari za afya. 

Iwapo programu yako inajumuisha au inatangaza maudhui na huduma za afya, unapaswa kuhakikisha kwamba programu yako inatii sheria na kanuni zozote zinazotumika.

Programu za Afya

Ikiwa programu yako inafikia data ya afya na ni programu ya afya au inatoa vipengele vinavyohusiana na afya, ni lazima itii Sera zilizopo za Wasanidi Programu wa Google Play, ikiwa ni pamoja na Sera dhidi ya Matumizi Mabaya ya Vifaa, Faragha na Udanganyifu na Matukio Nyeti, pamoja na masharti yaliyo hapa chini:

  • Taarifa Kuhusu Dashibodi:
    • Nenda kwenye Ukurasa wa maudhui ya programu (Sera > Maudhui ya programu) kwenye Dashibodi ya Google Play kisha uchague aina ambazo programu yako inajihusisha nazo.
  • Sera ya Faragha na Masharti ya Ufumbuzi Dhahiri:
    • Ni lazima programu yako ichapishe kiungo cha sera ya faragha katika sehemu iliyobainishwa kwenye Dashibodi ya Google Play na kiungo au maandishi ya sera ya faragha ndani ya programu yenyewe. Tafadhali hakikisha kuwa sera yako ya faragha inapatikana kwenye URL inayotumika, inayoweza kufikiwa na umma na isiyo na mipaka pepe (hatukubali PDF) na haiwezi kubadilishwa (kwa mujibu wa Sehemu ya Usalama wa Data).
    • Ni lazima sera ya faragha ya programu yako, pamoja na ufumbuzi wowote wa ndani ya programu, ifafanue kwa kina ufikiaji, ukusanyaji, matumizi na kuruhusu ufikiaji wa data ya mtumiaji ambayo ni ya binafsi au nyeti, lakini si tu data iliyofumbuliwa katika sehemu ya Usalama wa Data hapo juu. Kwa utendaji au data yoyote inayodhibitiwa na ruhusa hatari au ruhusa za programu inapotumika, ni sharti programu itimize masharti ya idhini na ufumbuzi dhahiri yanayotumika.
    • Ruhusa ambazo hazihitajiki katika utendaji wa msingi wa programu ya afya hazipaswi kuombwa na ruhusa zisizotumika lazima ziondolewe. Ili upate orodha ya ruhusa zinazochukuliwa kuwa katika upeo wa data nyeti inayohusiana na afya, angalia Aina za programu za afya na maelezo ya ziada.
    • Iwapo programu yako si programu ya afya kwa msingi, lakini ina vipengele vinavyohusiana na afya na inafikia data ya afya, bado ipo katika upeo wa sera ya Programu za Afya. Inapaswa kumwelezea mtumiaji kwa njia ya wazi uhusiano kati ya utendaji wa msingi wa programu na ukusanyaji wa data inayohusiana na afya (kwa mfano, watoa huduma za bima, programu za michezo zinazokusanya data ya shughuli za mtumiaji kama njia ya kuendeleza uchezaji nk.). Ni lazima sera ya faragha ya programu ionyeshe matumizi haya.
  • Masharti ya ziada:
    Ikiwa programu yako ya afya inastahiki mojawapo ya hali zifuatazo, ni lazima utii masharti husika pamoja na kuchagua aina inayofaa katika Dashibodi ya Google Play:
    • Programu za afya zinazoshirikiana na Serikali: Iwapo una ruhusa kutoka kwa serikali au shirika la afya linalotambuliwa, ya kubuni na kusambaza programu kwa kushirikiana nalo, ni sharti uwasilishe uthibitisho wa kustahiki kupitia Fomu ya Arifa ya Mapema.
    • Programu za Kufuatilia Waliotangamana na Aliyeambukizwa au za Hali ya Afya: Ikiwa programu yako ni ya kufuatilia waliotangamana na aliyeambukizwa na/au ya hali ya afya, tafadhali chagua “Kuzuia Ugonjwa na Afya ya Umma” kwenye Dashibodi ya Google Play, kisha uweke maelezo yanayohitajika kupitia fomu ya arifa ya mapema hapo juu.
    • Programu Zinazoendesha Utafiti Unaohusu Binadamu: Ni lazima programu zinazoendesha utafiti unaohusu afya ya binadamu zifuate sheria na kanuni zote; ikiwa ni pamoja na, lakini si tu, kupata idhini ya washiriki au, ikiwa washiriki ni watoto, zipate idhini kutoka kwa mzazi au mlezi wao. Programu za Utafiti wa Afya zinapaswa pia zipate idhini kutoka Bodi ya Ukaguzi wa Mashirika (IRB) na/au kamati huru za maadili zinazolingana isipokuwa ziruhusiwe kutopata idhini hii. Uthibitishaji wa idhini kama hizi unapaswa kutolewa ukihitajika.
    • Programu za SaMD au Kifaa cha Matibabu: Programu ambazo zinachukuliwa kuwa ni vifaa vya matibabu au SaMD zinapaswa kupata na kuhifadhi barua ya idhini au hati nyingine ya idhini ambayo imetolewa na mamlaka au taasisi ya serikali inayohusika na usimamizi na utiifu wa programu za afya. Uthibitishaji wa idhini kama hizi unapaswa kutolewa ukihitajika.

Data ya Health Connect

Data inayofikiwa kupitia Ruhusa za Health Connect huchukuliwa kuwa data binafsi na nyeti ya mtumiaji inayotegemea sera ya Data ya Mtumiaji na kutegemea masharti ya ziada.

Dawa zinazotolewa kwa maagizo ya daktari

Haturuhusu programu zinazowezesha uuzaji au ununuzi wa dawa zinazotolewa kwa maagizo ya daktari bila agizo la daktari.

Dawa ambazo Hazijaidhinishwa

Google Play hairuhusu programu ambazo zinatangaza au kuuza dawa ambazo hazijaidhinishwa, bila kujali madai yoyote ya kisheria. 
Ili kudumisha usalama na heshima kwenye mfumo wa Google Play, tumebuni viwango vinavyobainisha na kuzuia maudhui ambayo hayafai au yanayodhuru watumiaji wetu.
  • Bidhaa zote zilizo kwenye orodha hii ambayo haijataja vipengele vyote vya dawa za matibabu na vibadala vya mlo ambavyo havijaruhusiwa.

  • Bidhaa zilizo na "ephedra".

  • Bidhaa zilizo na homoni inayotolewa na mfuko wa uzazi (hCG), kwa minajili ya kupunguza au kudhibiti uzito au zinapotangazwa pamoja na steroidi za kuongeza nguvu mwilini.

  • Vibadala vya mlo au mitishamba iliyo na kemikali hatari au za matibabu.

  • Madai ya afya yanayopotosha au yasiyo sahihi, ikiwa ni pamoja na madai kuwa bidhaa inafanya kazi kama dawa zinazotolewa kwa maagizo ya daktari au dawa zinazodhibitiwa.

  • Bidhaa ambazo hazijaidhinishwa na serikali zinazotangazwa kwa njia inayodai kuwa ni salama au zina ufanisi katika kuzuia au kutibu ugonjwa au maradhi fulani.

  • Bidhaa ambazo zimepewa onyo au kudhibitiwa na serikali au mamlaka yoyote.

  • Bidhaa zenye majina yanayokanganya kwa kuwa yanafanana na dawa inayodhibitiwa au kibadala cha mlo au dawa ya matibabu ambayo haijaidhinishwa.

Kwa maelezo zaidi kuhusu dawa za matibabu na vibadala vya mlo tunavyovifuatilia ambavyo havijaidhinishwa au vinapotosha, tafadhali tembelea www.legitscript.com.

Maelezo ya Kupotosha ya Afya

Haturuhusu programu zenye madai ya afya yanayopotosha ambayo yanakinzana na makubaliano ya kimatibabu yaliyopo au yanayoweza kusababisha madhara kwa watumiaji.
Ili kudumisha usalama na heshima kwenye mfumo wa Google Play, tumebuni viwango vinavyobainisha na kuzuia maudhui ambayo hayafai au yanayodhuru watumiaji wetu.
  • Madai yanayopotosha kuhusu chanjo, kama vile chanjo zinaweza kubadili Vinasaba (DNA) vya mtu.
  • Utetezi wa matibabu hatari, yasiyoidhinishwa.
  • Utetezi wa mbinu zingine hatari za kiafya, kama vile tiba ya kubadili mwelekeo au utambulisho wa kijinsia.

Utendaji wa Kimatibabu

Haturuhusu programu zenye vipengele vya matibabu au utendaji unaohusiana na afya ambavyo vinapotosha au vinaweza kudhuru. Kwa mfano, haturuhusu programu ambazo zinadai kuwa zina utendaji wa upimaji wa oksijeni ambao unafanywa ndani ya programu. Programu za Kupima Oksijeni ni lazima zitumiwe na maunzi ya nje, kifaa cha kuvaliwa au vitambuzi maalumu vya simu mahiri vilivyobuniwa ili vitumike katika utendaji wa upimaji wa oksijeni. Pia, programu hizi zinazotumika ni lazima ziwe na makanusho katika metadata inayosema kuwa hazijakusudiwa kwa matumizi ya matibabu, zimeundwa kwa madhumuni ya jumla ya siha na ustawi, si kifaa cha matibabu na lazima zifichue ipasavyo muundo wa maunzi/kifaa kinachooana.

Malipo - Huduma za Kimatibabu

Miamala inayohusu huduma za kimatibabu zinazodhibitiwa hazipaswi kutumia mfumo wa utozaji wa Google Play. Kwa maelezo zaidi, angalia Fahamu Sera ya Malipo ya Google Play.

Maudhui yanayotokana na Rekodi ya makundi ya miamala

Teknolojia ya rekodi ya makundi ya miamala inapoendelea kubadilika kwa kasi, tunalenga kutoa jukwaa kwa wasanidi programu kustawi katika uvumbuzi na kuimarisha ubunifu wa hali ya juu kwa ajili ya watumiaji.

Kwa madhumuni ya sera hii, tunachukulia maudhui yanayotoka kwenye rekodi ya makundi ya miamala kuwa vipengee vya dijitali vyenye tokeni vinavyolindwa kwenye rekodi ya makundi ya miamala. Ikiwa programu yako ina maudhui yanayotokana na rekodi ya makundi ya miamala, ni lazima utii masharti haya.

Ubadilishaji wa Sarafu ya Dijitali na Programu za Kuhifadhi Sarafu Dijitali

Ununuzi, umiliki au ubadilishanaji wa sarafu za dijitali unapaswa kufanywa kupitia huduma zilizoidhinishwa katika maeneo yanayodhibitiwa.

Ni lazima pia utii kanuni zinazotumika za eneo au nchi yoyote ambayo programu yako inalenga na usichapishe programu yako mahali ambapo bidhaa na huduma zako zimepigwa marufuku. Google Play inaweza kukuomba utoe maelezo ya ziada au hati zinazohusiana na namna unavyotii kanuni zinazotumika na masharti ya utoaji leseni.

Uchumaji wa sarafu za dijitali

Haturuhusu programu zinazochuma sarafu za dijitali kwenye vifaa. Tunaruhusu programu zinazodhibiti kwa umbali uchumaji wa sarafu za dijitali.

Masharti ya Uwazi kwa Usambazaji wa Vipengee vya Dijitali vyenye Tokeni

Iwapo programu yako inauza au kuwawezesha watumiaji kujipatia Vipengee vya Dijitali vyenye Tokeni, ni lazima utangaze kupitia fomu ya taarifa ya Vipengele vya Fedha kwenye ukurasa wa Maudhui ya Programu katika Dashibodi ya Google Play.

Unapounda bidhaa ya ndani ya programu, lazima uonyeshe katika maelezo ya bidhaa kuwa inawakilisha Kipengee cha Dijitali chenye Tokeni. Kwa mwongozo wa ziada, angalia Kuunda bidhaa ya ndani ya programu.

Huwezi kutangaza au kuhimiza mapato yoyote yanayoweza kutokana na kucheza au shughuli za biashara.

Masharti ya Zaida ya Matumizi ya kanuni na vipengele vya michezo ya NFT

Kama inavyohitajika katika Sera ya Mashindano, Michezo na Kamari za Pesa Halisi ya Google Play, programu za kamari zinazojumuisha vipengee dijitali vyenye tokeni, kama vile NFT, zinapaswa kukamilisha mchakato wa kutuma maombi.

Kwa programu nyingine zote ambazo hazitimizi masharti ya kujiunga kwa programu za kamari na hazijabainishwa katika Majaribio Mengine ya Michezo ya Pesa Halisi, kitu chochote cha thamani ya fedha hakipaswi kukubaliwa badala ya nafasi ya kupata NFT ya thamani isiyojulikana. NFT zinazonunuliwa na watumiaji zinapaswa kutumiwa au kutumika katika mchezo ili kuboresha hali ya utumiaji ya mtumiaji au kuwasaidia watumiaji kuendeleza mchezo. NFT hazipaswi kutumika kuweka dau au kubahatisha ili kupata fursa ya kushinda zawadi zenye thamani ya pesa halisi (ikiwa ni pamoja na NFT zingine).

Ili kudumisha usalama na heshima kwenye mfumo wa Google Play, tumebuni viwango vinavyobainisha na kuzuia maudhui ambayo hayafai au yanayodhuru watumiaji wetu.
  • Programu zinazouza vifurushi vya NFT bila kufichua maudhui na thamani mahususi za NFT.
  • Michezo ya kasino ya kijamii ya kulipa ili ucheze, kama vile mashine za kuweka sarafu, ambazo huzawadi NFT.

Maudhui Yanayotayarishwa na AI

Kadri miundo ya AI zalishi inavyoendelea kupatikana kwa upana zaidi kwa wasanidi programu, unaweza kutumia miundo hii katika programu zako kuongeza ushirikishaji na kuboresha hali ya utumiaji. Google Play inataka kukusaidia kuhakikisha maudhui yanayotayarishwa na AI ni salama kwa watumiaji wote na kuwa maoni ya watumiaji yanatumika katika uvumbuzi wa kuwajibika.

Maudhui Yanayotayarishwa na AI

Maudhui yanayotayarishwa na AI ni maudhui ambayo yanazalishwa na miundo ya AI zalishi kulingana na vidokezo vya watumiaji. Mifano ya maudhui yanayotayarishwa na AI ni pamoja na:

  • Vijibu vya gumzo vya AI zalishi vya mazungumzo ya maandishi, ambapo kuwasiliana na kijibu cha gumzo ni utendaji wa msingi wa programu.
  • Picha zinazotayarishwa na AI kulingana na maandishi, picha au vidokezo vya sauti

Ili kuhakikisha usalama wa mtumiaji na kwa mujibu wa Matumizi ya Sera ya Google Play, programu zinazotayarisha maudhui kwa kutumia AI ni sharti zitii sera zilizopo za Wasanidi Programu wa Google Play, ikiwa ni pamoja na kutoruhusu na kuzuia uzalishaji wa Maudhui Yaliyozuiwa, kama vile maudhui yanayowezesha unyanyasaji wa watoto na maudhui yanayowezesha Tabia Danganyifu.

Programu zinazotayarisha maudhui kwa kutumia AI ni sharti ziwe na vipengele vya ndani ya programu vya kuripoti watumiaji vinavyoruhusu watumiaji kuripoti au kutia alama maudhui ya kukera kwa wasanidi programu bila kuhitaji kufunga programu. Wasanidi programu wanapaswa kutumia ripoti za watumiaji ili kutekeleza udhibiti na kuchuja maudhui katika programu zao.


Mali ya Uvumbuzi

Haturuhusu programu au akaunti za wasanidi programu zinazokiuka haki za uvumbuzi za watu wengine (ikiwa ni pamoja na chapa za biashara, hakimiliki, hataza, siri za biashara na haki zingine za umiliki) Pia haturuhusu programu zinazohimiza au kushawishi ukiukaji wa haki za uvumbuzi.

Tutajibu taarifa dhahiri za madai ya ukiukaji wa hakimiliki. Kwa maelezo zaidi au kuwasilisha ombi la DMCA (Sheria ya Milenia ya Hakimiliki Dijitali), tafadhali tembelea taratibu zetu za hakimilki.

Ili uwasilishe malalamiko kuhusu uuzaji au matangazo ya uuzaji wa bidhaa ghushi ndani ya programu, tafadhali wasilisha onyo la bidhaa ghushi.

Kama wewe ni mmiliki wa Chapa ya Biashara na unaamini kuna programu kwenye Google Play inayokiuka haki zako za chapa ya biashara, tunakuhimiza uwasiliane na msanidi programu moja kwa moja ili utatue tatizo lako. Ikiwa huwezi kutatua tatizo na msanidi programu, tafadhali tuma malalamiko kuhusu chapa ya biashara kupitia fomu hii.

Ikiwa una hati iliyoandikwa inayothibitisha kuwa una ruhusa ya kutumia mali ya uvumbuzi wa wengine katika programu au orodha yako ya duka (kama vile Majina ya chapa na nembo na vipengee vya picha), wasiliana na timu ya Google Play kabla ya kuchapisha programu yako ili kuhakikisha kuwa programu hiyo haikataliwi kwa misingi ya ukiukaji wa haki za uvumbuzi.

Matumizi Yasiyoidhinishwa ya Maudhui yenye Hakimiliki

Haturuhusu programu zinazokiuka hakimiliki. Kubadilisha maudhui yenye hakimiliki bado kunaweza kusababisha ukiukaji. Huenda wasanidi programu wakahitajika kutoa ushahidi wa haki zao za kutumia maudhui yaliyo na hakimiliki.

Tafadhali kuwa makini unapotumia maudhui yanayolindwa kwa hakimiliki ili kuonyesha utendaji wa programu yako. Kwa jumla, njia ya uhakika ni kutengeneza programu ambayo ni halisi.

Ili kudumisha usalama na heshima kwenye mfumo wa Google Play, tumebuni viwango vinavyobainisha na kuzuia maudhui ambayo hayafai au yanayodhuru watumiaji wetu.
  • Sanaa ya jalada ya albamu za muziki, michezo ya video na vitabu.
  • Picha za matangazo kutoka filamu, televisheni au michezo ya video.
  • Kazi za sanaa au picha kutoka vitabu vya vibonzo, katuni, filamu, video za muziki, au runinga.
  • Nembo za vyuo na timu za michezo ya kulipwa.
  • Picha zilizochukuliwa kutoka akaunti ya mitandao jamii ya mtu mashuhuri.
  • Picha za kitaalamu za watu mashuhuri.
  • Utoaji wa "sanaa ya mashabiki" isiyoweza kutofautishwa na kazi halisi iliyo na hakimiliki.
  • Programu ambazo zina sauti zinazocheza klipu za sauti kutoka maudhui yenye hakimiliki.
  • Utoaji tena wa tafsiri kamili za vitabu ambavyo havipo wazi kutumiwa na umma.

Zinazoshawishi Ukiukaji wa Hakimiliki

Haturuhusu programu zinazohimiza au kushawishi ukiukaji wa hakimiliki. Kabla ya kuchapisha programu yako, tafuta njia ambazo programu yako inaweza kuwa inahimiza ukiukaji wa hakimiliki na upate ushauri wa kisheria ikibidi.
Ili kudumisha usalama na heshima kwenye mfumo wa Google Play, tumebuni viwango vinavyobainisha na kuzuia maudhui ambayo hayafai au yanayodhuru watumiaji wetu.
  • Programu zinazotiririsha maudhui zinazoruhusu watumiaji kupakua nakala ya maudhui yenye hakimiliki bila idhini.

  • Programu zinazowahimiza watumiaji kutiririsha na kupakua kazi zenye hakimiliki, ikiwa ni pamoja na muziki na video, ikiwa ni ukiukaji wa sheria ya hakimiliki inayotumika:

     

    ① Maelezo yaliyo kwenye ukurasa huu wa programu katika Google Play yanahimiza watumiaji kupakua maudhui yenye hakimiliki bila idhini.
    ② Picha za skrini zilizo kwenye ukurasa wa programu katika Google Play zinahimiza watumiaji kupakua maudhui yenye hakimiliki bila idhini.

Ukiukaji wa chapa ya biashara

Haturuhusu programu zinazokiuka chapa za biashara za wengine. Chapa ya biashara ni neno, ishara, au mchanganyiko unaotambulisha chanzo cha bidhaa au huduma. Mmiliki wa chapa akishapata chapa ya biashara, ana haki za kipekee za kutumia kwa ajili ya bidhaa au huduma mahususi.

Ukiukaji wa hakimilki ya chapa ya biashara ni kutumia chapa ya biashara isivyofaa au bila idhini kwa namna inayoweza kusababisha utata kuhusu chanzo cha bidhaa hiyo. Ikiwa programu yako inatumia chapa za biashara za mtu mwingine katika namna inayoweza kuleta utata, programu yako inaweza kusimamishwa.

Ghushi

Haturuhusu programu zinazouza au kutangaza uuzaji wa bidhaa ghushi. Bidhaa ghushi zina nembo au chapa ya biashara ambayo inafanana na chapa halisi au huwezi kutofautisha kwa urahisi chapa hizo. Bidhaa ghushi huiga vipengele vya chapa ya bidhaa halisi ili ziweze kuonekana kama bidhaa halisi ya mmiliki wa chapa hiyo.

Faragha, Ulaghai na Matumizi Mabaya ya Kifaa

Tumejitolea kulinda faragha ya watumiaji na kutoa mazingira salama kwa watumiaji wetu. Haturuhusu programu zinazopotosha, kulaghai au kulenga kutumia vibaya mtandao, kifaa au data yoyote ya binafsi.

Data ya Watumiaji

Ni lazima uwe muwazi unaposhughulikia data ya watumiaji (kwa mfano, maelezo yanayokusanywa kutoka kwa mtumiaji au kuhusu mtumiaji ikiwa ni pamoja na maelezo ya kifaa). Hii inamaanisha kufumbua uwezo wa kufikia kukusanya, kutumia, kushughulikia na kushiriki data ya mtumiaji kutoka kwenye programu yako na kudhibiti matumizi ya data kwa madhumuni ya kutii sera yaliyofumbuliwa. Tafadhali kumbuka kuwa kushughulikia data yoyote nyeti au binafsi ya mtumiaji pia hutegemea masharti ya ziada katika sehemu ya "Data Binafsi na Nyeti ya Mtumiaji" hapo chini. Masharti haya ya Google Play yanatumika pamoja na masharti yoyote yanayobainishwa na sheria husika za faragha na ulinzi wa data.

Ikiwa unajumuisha msimbo wa wahusika wengine (kwa mfano, SDK) kwenye programu yako, ni lazima uhakikishe kuwa msimbo wa wahusika wengine unaotumika kwenye programu yako, na desturi za wahusika wengine kuhusiana na data ya mtumiaji, zinatii Sera za Mpango wa Wasanidi Programu wa Google Play, ambazo zinajumuisha matumizi na masharti ya ufumbuzi. Kwa mfano, ni lazima uhakikishe kuwa watoa huduma wako wa SDK hawauzi data nyeti ya mtumiaji kwenye programu yako. Masharti haya yanatumika bila kujali kama data ya mtumiaji inahamishwa baada ya kutumwa kwenye seva, au kwa kupachika msimbo wa wahusika wengine katika programu yako.

Data Binafsi na Nyeti ya Mtumiaji

Data ya mtumiaji ambayo ni nyeti na ya binafsi hujumuisha, lakini si tu, taarifa binafsi inayoweza kumtambulisha mtu, maelezo ya fedha na malipo, maelezo ya uthibitishaji, orodha ya anwani, anwani, mahali kifaa kilipo, data inayohusiana na SMS pamoja na simu, data ya afyadata ya Health Connect, orodha ya programu nyinginezo zilizopo kwenye kifaa, maikrofoni, kamera na data nyingine nyeti ya matumizi au ya kifaa. Iwapo programu yako inashughulikia data nyeti na ya binafsi, ni sharti:

  • Udhibiti jinsi unavyoikusanya, kuifikia, kuitumia na kuishiriki data nyeti na binafsi inayopatikana kupitia programu kwa utendajikazi wa programu na huduma, pamoja na kutii sera kwa madhumuni yanayotarajiwa na mtumiaji:
    • Ni lazima programu zinazoendeleza utumiaji wa data nyeti na binafsi ya mtumiaji kwa ajili ya kuonyesha matangazo zitii Sera ya Matangazo ya Google Play.
    • Pia, unaweza kuhamisha data jinsi inavyohitajika kwa watoa huduma au kwa madhumuni ya kisheria kama vile kutii ombi halali la serikali, sheria zinazotumika au kama sehemu ya muungano au ununuzi wa kibiashara ulio na ilani halali ya kutosha kwa watumiaji.
  • Ushughulikie kwa usalama data yote ya mtumiaji ambayo ni nyeti na ya binafsi, ikiwa ni pamoja na kuituma kupitia usimbaji fiche wa kisasa (kwa mfano, kupitia HTTPS).
  • Utumie ombi la ruhusa za programu inapotumika zinapopatikana, kabla ya kufikia data inayodhibitiwa na ruhusa za Android.
  • Usiuze data ya watumiaji iliyo ya binafsi na nyeti.
    • "Mauzo" yanamaanisha kubadilishana au kuhamisha data binafsi na nyeti ya mtumiaji kwenda kwa mhusika mwingine kwa ajili ya malipo.
      • Uhamisho wa data binafsi na nyeti ulioanzishwa na mtumiaji (kwa mfano, mtumiaji anapotumia kipengele cha programu kuhamisha faili kwenda kwa mhusika mwingine au mtumiaji anapochagua kutumia programu mahususi ya utafiti), hakuchukuliwi kuwa ni mauzo.

Masharti ya Idhini na Ufumbuzi Dhahiri

Katika hali ambapo uwezo wa programu yako kufikia, kukusanya, kutumia au kushiriki data nyeti na binafsi ya mtumiaji unaweza usiwe ndani ya matarajio ya mtumiaji wa bidhaa au kipengele husika (kwa mfano, ikiwa ukusanyaji wa data unafanyika chinichini wakati mtumiaji hatumii programu yako), ni lazima utimize masharti yafuatayo:

Ufumbuzi dhahiri: Ni lazima utoe ufumbuzi wa ndani ya programu kuhusu jinsi unavyofikia data, kuikusanya, kuitumia na kuishiriki. Ufumbuzi wa ndani ya programu:

  • Ni lazima uwe ndani ya programu yenyewe wala si kwenye maelezo ya programu au tovuti pekee;
  • Ni lazima uonyeshwe katika matumizi ya kawaida ya programu, yaani mtumiaji asihitajike kwenda katika menyu au mipangilio;
  • Ni lazima ufafanue data inayofikiwa au kukusanywa;
  • Ni sharti ueleze jinsi data itakavyotumika/au kushirikiwa;
  • Hauwezi kuwekwa kwenye sera ya faragha na masharti pekee; na
  • Hauwezi kujumuishwa kwenye ufumbuzi mwingine usiohusiana na ukusanyaji wa data ya watumiaji iliyo binafsi na nyeti.

Idhini na ruhusa za programu inapotumika: Maombi ya idhini ya mtumiaji ya ndani ya programu na maombi ya ruhusa za programu inapotumika lazima yatanguliwe papo hapo na ufumbuzi wa ndani ya programu unaotimiza masharti ya sera hii. Ombi la programu la idhini:

  • Ni sharti liwasilishe kidirisha cha kuonyesha idhini kwa njia dhahiri na bayana;
  • Ni sharti liombe kitendo cha kuidhinisha cha mtumiaji (kwa mfano, gusa ili ukubali, tia alama kwenye kisanduku cha kuteua);
  • Halipaswi kufasili maelekezo kwa njia tofauti na ufumbuzi (ikiwa ni pamoja na kugusa ili kufunga au kubonyeza kitufe cha kurudi nyuma au cha ukurasa wa mwanzo) kuwa idhini;
  • Halipaswi kutumia ujumbe unaoondolewa baada ya muda fulani au unaojiondoa kiotomatiki kuwa mbinu ya kupata idhini ya mtumiaji; na
  • Ni lazima litolewe na mtumiaji kabla ya programu yako kuanza kukusanya au kufikia data nyeti na binafsi ya mtumiaji.

Programu zinazotegemea misingi mingine ya kisheria ili kuchakata data nyeti na binafsi ya mtumiaji bila idhini, kama vile sababu halali chini ya EU GDPR, lazima zitii mahitaji yote ya kisheria yanayotumika na kutoa ufumbuzi unaofaa kwa watumiaji, ikiwa ni pamoja na ufumbuzi wa ndani ya programu kama inavyohitajika chini ya sera hii.

Ili utimize masharti ya sera, inapendekezwa kwamba utumie mfano wa muundo ufuatao wa Ufumbuzi Dhahiri panapohitajika:

  • “[Programu hii] hukusanya/hutuma/husawazisha/huhifadhi [aina ya data] ili kuwezesha  ["kipengele"], [katika hali unayotaja]."
  • Mfano: “Programu ya Fitness Funds hukusanya data ya mahali ili kuwezesha huduma ya ufuatiliaji wa siha hata wakati programu imefungwa au haitumiki na hutumiwa pia kusaidia katika utangazaji.” 
  • Mfano: “Programu ya Call Buddy hukusanya, kusoma na kuandika data ya rekodi ya nambari za simu ili kuwezesha huduma ya upangaji wa anwani hata wakati programu haitumiki.”

Ikiwa programu yako itajumuisha msimbo wa wahusika wengine (kwa mfano, SDK) ambayo imeundwa kukusanya data nyeti ya mtumiaji kwa chaguomsingi, ni lazima, ndani ya wiki 2 baada ya kupokea ombi kutoka Google Play (au ikiwa ombi la Google Play litatoa muda mrefu zaidi, ndani ya kipindi hicho), utoe ushahidi wa kutosha unaoonyesha kuwa programu yako inatimiza masharti ya Idhini na Ufumbuzi Dhahiri wa sera hii, ikijumuisha jinsi unavyofikia data, kuikusanya, kuitumia au kuishiriki kupitia msimbo wa wahusika wengine.

Ili kudumisha usalama na heshima kwenye mfumo wa Google Play, tumebuni viwango vinavyobainisha na kuzuia maudhui ambayo hayafai au yanayodhuru watumiaji wetu.
  • Programu ambayo inakusanya data ya mahali kifaa kilipo lakini haina ufumbuzi dhahiri unaofafanua kipengele ambacho kinatumia data hii na/au kuonyesha matumizi ya programu chinichini.
  • Programu ambayo ina ruhusa ya programu inapotumika ambayo inaomba ufikiaji wa data kabla ya kutoa ufumbuzi dhahiri unaobainisha matumizi ya data husika.
  • Programu ambayo inafikia rekodi ya programu zilizosakinishwa na mtumiaji na haitunzi data hii kama ya binafsi au nyeti kwa mujibu wa Sera ya Faragha iliyo hapo juu, kushughulikia data na masharti ya Idhini na Ufumbuzi Dhahiri.
  • Programu ambayo inafikia data ya kitabu cha nambari za simu au cha anwani za mtumiaji na haitunzi data hii kama ya binafsi au nyeti kwa mujibu wa Sera ya Faragha iliyo hapo juu, kushughulikia data na masharti ya Idhini na Ufumbuzi Dhahiri.
  • Programu inayorekodi skrini ya mtumiaji na haishughulikii data hii kama data nyeti au ya binafsi kwa mujibu wa sera hii.
  • Programu inayokusanya data ya mahali kifaa kilipo na haifumbui matumizi yake kwa kina na kupata idhini kwa mujibu wa masharti yaliyo hapo juu.
  • Programu inayotumia ruhusa zinazodhibitiwa katika hali ya chinichini kwenye programu ikiwa ni pamoja na kwa malengo ya kufuatilia, kufanya utafiti au kutangaza na haifumbui matumizi yake kwa kina na kupata idhini kwa mujibu wa masharti yaliyo hapo juu. 
  • Programu iliyo na SDK inayokusanya data nyeti na binafsi ya mtumiaji na haishughulikii data hii kwa mujibu wa Sera hii ya Data ya Mtumiaji, ufikiaji, kushughulikia data (ikiwa ni pamoja na kutoruhusu mauzo) na masharti ya idhini na ufumbuzi dhahiri.

Rejelea kwenye makala haya ili upate maelezo zaidi kuhusu Masharti ya Idhini na Ufumbuzi Dhahiri.

Masharti ya Ufikiaji wa Data Binafsi na Nyeti

Mbali na masharti yaliyo hapo juu, jedwali lililo hapa chini linafafanua masharti ya shughuli mahususi.

Shughuli  Masharti
Programu yako inashughulikia maelezo kuhusu fedha au malipo au nambari za utambulisho zinazotolewa na serikali Programu yako haipaswi kufumbua hadharani data yoyote ya watumiaji ambayo ni ya binafsi na nyeti inayohusiana na shughuli za fedha au malipo au nambari zozote za utambulisho zinazotolewa na serikali.
Programu yako inashughulikia anwani za mawasiliano au orodha ya anwani isiyo ya umma Haturuhusu uchapishaji au ufumbuzi wa anwani za watu zisizo za umma bila idhini.
Programu yako ina kingavirusi au vipengele vya usalama, kama vile kingavirusi, kinga ya programu hasidi au vipengele vinavyohusiana na usalama Ni lazima programu yako ichapishe sera ya faragha ambayo (pamoja na ufumbuzi wowote wa ndani ya programu) inafafanua aina ya data ya watumiaji inayokusanywa na kusambazwa na programu yako, namna inavyotumika na aina ya watu inaoshiriki nao.
Programu yako inalenga watoto Programu yako haipaswi kuwa na SDK ambayo haijaidhinishwa katika matumizi ya huduma zinazolenga watoto. Angalia sehemu ya Kubuni Programu za Watoto na Familia ili upate masharti na lugha ya sera yote. 
Programu yako hukusanya au kuunganisha vitambulishi vya kifaa vinavyoendelea kuwepo (k.m., IMEI, IMSI, Nambari ya Ufuatiliaji ya SIM, n.k.)

Vitambulishi vya vifaa vinavyoendelea kuwepo havipaswi kuunganishwa kwenye data nyingine ya watumiaji ambayo ni ya binafsi na nyeti au vitambulishi vya vifaa vinavyoweza kubadilishwa, isipokuwa kwa madhumuni ya 

  • Huduma za kupiga simu zinazohusiana na utambulisho wa SIM (k.m., huduma ya kupiga simu kupitia Wi-Fi iliyounganishwa na akaunti ya kampuni inayokupa huduma), na
  • Programu za biashara za kudhibiti vifaa zinazotumia hali ya mmiliki wa kifaa.

Matumizi haya lazima yafumbuliwe kwa njia dhahiri kwa watumiaji jinsi ilivyobainishwa kwenye Sera ya Data ya Watumiaji.

Tafadhali soma nyenzo hii ili upate vitambulishi maalum mbadala.

Tafadhali soma Sera ya matangazo ili upate mwongozo wa ziada kuhusu kitambulishi cha kifaa kwa ajili ya matangazo kwenye Android.

Sehemu ya usalama wa data

Lazima wasanidi programu wote wajaze kwa uwazi na usahihi sehemu ya Usalama wa data ya kila programu kwa kutoa ufafanuzi kuhusu ukusanyaji, utumiaji na kushiriki data ya mtumiaji. Msanidi programu anawajibikia usahihi wa lebo na kusasisha maelezo haya. Panapofaa, lazima sehemu hiyo ilingane na ufumbuzi uliofanywa kwenye sera ya faragha ya programu. 

Tafadhali rejelea makala haya ili upate maelezo ya ziada kuhusu kujaza Sehemu ya Usalama wa Data.

Sera ya Faragha

Ni lazima programu zote zichapishe kiungo cha sera ya faragha katika sehemu iliyobainishwa kwenye Dashibodi ya Google Play na kiungo au maandishi ya sera ya faragha ndani ya programu yenyewe. Ni lazima sera ya faragha pamoja na ufumbuzi wowote wa ndani ya programu, ifafanue kwa kina jinsi programu yako inavyofikia, kukusanya, kutumia na kushiriki data ya mtumiaji, lakini si tu data iliyofumbuliwa kwenye sehemu ya Usalama wa Data. Sharti ijumuishe: 

  • Maelezo ya msanidi programu na mtu wa kuwasiliana naye kuhusu faragha au utaratibu wa kuuliza maswali.
  • Kufumbua aina ya data binafsi na nyeti ya mtumiaji ambayo programu yako hufikia, kukusanya, kutumia na kushiriki; na washirika wowote ambao utashiriki nao data yoyote nyeti au ya binafsi ya watumiaji.
  • Utaratibu salama wa kushughulikia data binafsi na nyeti ya mtumiaji.
  • Sera ya msanidi programu ya kuhifadhi na kufuta data.
  • Kuweka lebo kwa uwazi kuwa ni sera ya faragha (kwa mfano, iwe na maandishi “sera ya faragha” katika mada).

Huluki (kwa mfano, msanidi programu, kampuni) iliyotajwa kwenye ukurasa wa programu katika Google Play inapaswa ionekane katika sera ya faragha au lazima jina la programu litajwe kwenye sera ya faragha. Programu zisizofikia data yoyote nyeti na ya binafsi ya mtumiaji zinapaswa pia kuwasilisha sera ya faragha. 

Tafadhali hakikisha kuwa sera yako ya faragha inapatikana kwenye URL inayotumika, inayoweza kufikiwa na umma na isiyo na mipaka pepe (hatukubali PDF).

Masharti ya Kufuta Akaunti

Ikiwa programu yako huwaruhusu watumiaji kufungua akaunti kutoka ndani ya programu yako, basi ni lazima pia kuwaruhusu watumiaji kuomba akaunti zao zifufutwe. Watumiaji wanapaswa kuwa na chaguo linaloweza kutambulika kwa urahisi la kuanzisha ufutaji wa akaunti ya programu kutoka ndani na nje ya programu yako (k.m. kwa kutembelea tovuti yako). Kiungo cha nyenzo hii ya wavuti kinapaswa kuwekwa ndani ya sehemu ya fomu ya URL iliyobainishwa ndani ya Dashibodi ya Google Play.

Unapofuta akaunti ya programu kutokana na ombi la mtumiaji, unapaswa pia kufuta data ya mtumiaji inayohusiana na akaunti hiyo ya programu. Kufunga akaunti kwa muda, kuzima au "kusimamisha" akaunti ya programu si sawa na kufuta akaunti. Ikiwa utahitaji kuhifadhi data fulani kwa sababu halali kama vile madhumuni ya usalama, kuzuia ulaghai au kutii mamlaka, unapaswa uwataarifu watumiaji wako kwa njia ya uwazi kuhusu taratibu zako za kuhifadhi data (kwa mfano, ndani ya sera yako ya faragha).

Ili upate maelezo zaidi kuhusu masharti ya sera ya kufuta akaunti, tafadhali kagua makala haya ya Kituo cha Usaidizi. Kwa maelezo ya ziada kuhusu kusasisha fomu yako ya usalama wa data, tembelea makala haya.

Matumizi ya Kitambulisho Kilichowekwa na Programu

Android italeta kitambulisho kipya ili kusaidia katika matumizi ya hali muhimu kama vile takwimu na kuzuia ulaghai. Sheria na masharti ya vitambulisho hivi yapo hapo chini.

  • Matumizi: Kitambulisho kilichowekwa na programu hakipaswi kutumiwa katika kuweka mapendeleo ya matangazo na kupima matangazo. 
  • Kuhusisha maelezo yanayoweza kumtambulisha mtu au vitambulishi vingine: Kitambulisho kilichowekwa kwenye programu huenda hakijaunganishwa na vitambulishi vyovyote vya Android (k.m., AAID) au data yoyote ya binafsi na nyeti kwa madhumuni ya matangazo.
  • Uwazi na idhini: Ilani ya faragha inayojitosheleza kisheria lazima itolewe kwa mteja kuhusu ukusanyaji na utumiaji wa kitambulisho kilichowekwa na programu na pia kujitolea kwako kuzingatia masharti haya, ikiwa ni pamoja na sera ya faragha. Ni sharti upate idhini ya kisheria ya mtumiaji panapohitajika. Ili upate maelezo zaidi kuhusu viwango vyetu vya faragha, tafadhali kagua sera yetu ya Data ya Mtumiaji.

EU-U.S., Swiss Privacy Shield (Mifumo ya Faragha ya Uswizi, Marekani-Umoja wa Ulaya)

Ukiwa unaweza kufikia, kutumia au kuchakata maelezo ya binafsi yaliyo kwenye Google na ambayo yanatambulisha mtu kwa njia ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja na ikiwa maelezo hayo yametoka Umoja wa Ulaya au Uswizi ("Taarifa Binafsi kutoka Umoja wa Ulaya"), basi ni sharti:

  • Itii sheria, kanuni, amri na masharti yote ya faragha, usalama na ulinzi wa data husika;
  • Ifikie, kutumia au kuchakata Taarifa Binafsi ya Umoja wa Ulaya kwa madhumuni ambayo yanalingana tu na idhini iliyotolewa na mshirika ambaye anahusiana na Taarifa Binafsi ya Umoja wa Ulaya;
  • Itekeleze hatua za kiufundi na za kimashirika zinazofaa ili kulinda Taarifa Binafsi ya Umoja wa Ulaya dhidi ya kupotea, kutumiwa vibaya na kuharibiwa, kubadilishwa, kufumbuliwa na kufikiwa kwa njia isiyoruhusiwa au kuidhinishwa; na
  • Itoe kiwango sawa cha ulinzi kwa mujibu wa Kanuni za Privacy Shield (Mfumo wa Faragha).

Unapaswa kufuatilia jinsi unavyotii masharti haya kila wakati. Iwapo hutaweza kutimiza masharti haya wakati wowote ule (au iwapo kuna uwezekano mkubwa kuwa hutaweza kuyatimiza), unapaswa kutuarifu mara moja kwa kutuma barua pepe kwa data-protection-office@google.com na uache kuchakata Taarifa Binafsi za Umoja wa Ulaya mara moja au uchukue hatua zinazofaa za kurejesha kiwango cha ulinzi wa kutosha.

Kuanzia tarehe 16 Julai 2020, Google haitegemei tena EU-U.S. Privacy Shield (Mfumo wa Faragha wa Ulaya-Marekani) ili kuhamisha data binafsi ambayo imetoka nchi washirika katika Makubaliano ya Kiuchumi ya Ulaya au Uingereza kwenda Marekani. (Pata maelezo zaidi.)  Maelezo zaidi yanapatikana katika Kifungu cha tisa cha DDA.


Ruhusa na API Zinazofikia Maelezo Nyeti

Maombi ya ruhusa na API zinazofikia maelezo nyeti lazima ziwe bayana kwa mtumiaji. Unapaswa tu kuomba ruhusa na API zinazofikia maelezo nyeti zinazohitajika kutekeleza vipengele au huduma za sasa katika programu yako ambazo umezitangaza kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play. Hupaswi kutumia ruhusa au API zinazofikia maelezo nyeti ambazo zinakupa ufikiaji wa data ya vifaa au ya watumiaji kwa madhumuni yasiyofichuliwa, yasiyotekelezwa au yasiyoruhusiwa au kwenye vipengee ambavyo haviruhusiwi. Huruhusiwi kuuza wala kushiriki data binafsi au nyeti inayofikiwa kupitia ruhusa au API zinazoweza kufikia maelezo nyeti.

Omba ruhusa au API zinazofikia maelezo nyeti ili ufikie data husika (kupitia maombi endelevu), ili watumiaji waweze kuelewa kwa nini programu yako inaomba ruhusa. Tumia data kwa madhumuni ambayo mtumiaji ameidhinisha pekee. Kama ungependa kutumia data kwa madhumuni mengine baadaye, lazima uwaombe watumiaji idhini na uhakikishe wanakubali kabisa matumizi ya ziada.

Ruhusa Zinazodhibitiwa

Mbali na maelezo yaliyo hapo juu, ruhusa zinazodhibitiwa ni ruhusa ambazo zimebainishwa kuwa Hatari, Maalum,  Saini au jinsi inavyobainishwa hapa chini. Ruhusa hizi zinategemea vidhibiti na masharti ya ziada yafuatayo:

  • Data ya kifaa au ya mtumiaji inayofikiwa kupitia Ruhusa Zilizodhibitiwa inachukuliwa kuwa data nyeti na binafsi. Masharti ya Sera ya Data ya Mtumiaji yatatumika.
  • Heshimu uamuzi wa watumiaji iwapo watakataa ombi la kutoa Ruhusa Inayodhibitiwa na watumiaji hawapaswi kulazimishwa au kulaghaiwa ili watoe idhini ya ruhusa zozote zisizo muhimu. Ni lazima ujitahidi kuwakubali watumiaji ambao hawatoi uwezo wa kufikia ruhusa nyeti (kwa mfano, kumruhusu mtumiaji aweke mwenyewe nambari ya simu iwapo hajaruhusu ufikiaji wa Rekodi ya Nambari za Simu).
  • Haturuhusu kabisa matumizi ya ruhusa kwa njia inayokiuka sera za programu hasidi za Google Play (ikiwa ni pamoja na Matumizi Mabaya ya Ufikiaji Maalum).

Ruhusa fulani Zinazodhibitiwa zinaweza kutegemea masharti ya ziada jinsi inavyoelezewa kwa kina hapa chini. Lengo la masharti haya ni kulinda faragha ya mtumiaji. Tunaweza kuruhusu hali kadhaa zisizofuata masharti yaliyo hapa chini katika matukio ambayo hutokea kwa nadra, ambapo programu zinatoa kipengele cha lazima au muhimu zaidi na katika hali ambapo hakuna njia mbadala ya kutoa kipengele hicho. Tunatathmini hali pendekezwa zisizofuata kanuni kwa kuzingatia uwezekano wa kuathiri faragha au usalama wa watumiaji.

Ruhusa za SMS na Rekodi ya Nambari za Simu

Ruhusa za SMS na Rekodi ya Nambari za Simu huchukuliwa kuwa data ya mtumiaji ambayo ni nyeti na ya binafsi kwa mujibu wa sera ya Taarifa Binafsi na Nyeti na masharti yafuatayo:

Ruhusa Zinazodhibitiwa Masharti
Kikundi cha ruhusa za Rekodi ya Nambari za Simu (k.m. READ_CALL_LOG, WRITE_CALL_LOG, PROCESS_OUTGOING_CALLS) Sharti iwe imesajiliwa kikamilifu kuwa kidhibiti chaguomsingi cha Simu au Programu ya Mratibu kwenye kifaa.
Kikundi cha ruhusa za SMS (k.m. READ_SMS, SEND_SMS, WRITE_SMS, RECEIVE_SMS, RECEIVE_WAP_PUSH, RECEIVE_MMS) Sharti iwe imesajiliwa kikamilifu kuwa kidhibiti chaguomsingi cha SMS au Programu ya Mratibu kwenye kifaa.

 

Programu zisizo na uwezo wa kidhibiti chaguomsingi cha SMS, Simu au Programu ya Mratibu hazipaswi kutangaza matumizi ya ruhusa zilizo hapo juu kwenye faili ya maelezo. Uwezo huu unajumuisha maandishi ya kishikilia nafasi kwenye faili ya maelezo. Vile vile, ni lazima programu ziwe zimesajiliwa kuwa kidhibiti chaguomsingi cha programu ya Mratibu, SMS au Simu kabla ya kudokezea watumiaji wakubali mojawapo ya ruhusa zozote zilizo hapo juu na sharti ziache mara moja kutumia ruhusa zikiacha kuwa kidhibiti chaguomsingi. Matumizi na hali zisizofuata kanuni zinazoruhusiwa zinapatikana kwenye ukurasa huu wa Kituo cha Usaidizi.

Programu zinaweza kutumia tu ruhusa (na data yoyote inayotokana na ruhusa) ili kutoa utendaji wa msingi wa programu ulioidhinishwa. Utendaji wa msingi unafafanuliwa kuwa lengo kuu la programu. Hili linaweza kujumuisha vipengele vya msingi, ambavyo vinapaswa kurekodiwa kwa njia dhahiri katika maelezo ya programu. Bila vipengele vya msingi, programu “haijakamilika” au inachukuliwa kuwa haiwezi kutumika. Uhamishaji, kushiriki au matumizi yaliyoidhinishwa ya data hii ni sharti yatoe tu huduma au vipengele vya msingi katika programu na matumizi yake hayapaswi kuenezwa kwa madhumuni mengine yoyote (k.m. madhumuni ya utangazaji au uuzaji, kuboresha programu au huduma nyingine). Hupaswi kutumia njia mbadala (ikiwa ni pamoja na ruhusa, API au vyanzo vya wengine) ili kupata data inayohusishwa na ruhusa za SMS au Rekodi ya Nambari za Simu.

Ruhusa za Mahali

Data ya mahali kifaa kilipo huchukuliwa kuwa data ya mtumiaji ambayo ni nyeti na ya binafsi kwa mujibu wa sera ya Taarifa Binafsi na Nyeti na Sera ya Ruhusa ya Kubainisha Mahali Chinichini na masharti yafuatayo:

  • Programu hazipaswi kufikia data inayolindwa kwa ruhusa za mahali (k.m., ACCESS_FINE_LOCATION, ACCESS_COARSE_LOCATION, ACCESS_BACKGROUND_LOCATION) baada ya kutohitajika tena kutekeleza huduma au vipengele vya sasa katika programu yako.
  • Usiwahi kuomba ruhusa za mahali kutoka kwa watumiaji kwa lengo kuu la kuonyesha matangazo au takwimu. Programu ambazo zinaendeleza matumizi yanayoruhusiwa ya data hii kwa kuonyesha matangazo ni lazima zitii Sera yetu ya Matangazo.
  • Programu zinapaswa kuomba kiwango cha chini zaidi kinachohitajika cha ufikiaji (yaani, cha juujuu badala ya kuwa ya kina, na ufikiaji wakati programu inatumika badala ya chinichini) ili kutoa kipengele au huduma ya sasa inayotaka data ya mahali na watumiaji wanapaswa kutarajia kuwa kipengele au huduma hiyo inahitaji kiwango cha data ya mahali kilichoombwa. Kwa mfano, tunaweza kukataa programu zinazoomba au kufikia data ya mahali chinichini bila kutoa sababu za kutosha.
  • Ufikiaji wa data ya mahali chinichini unapaswa tu kutumika kutoa vipengele muhimu kwa mtumiaji na vinavyohusiana na utendakazi wa msingi wa programu.

Programu zinaruhusiwa kufikia data ya mahali kwa kutumia ruhusa ya huduma ya ufikiaji wakati programu inatumika (programu ina uwezo wa ufikiaji wakati inatumika tu, k.m., "inapotumika") ikiwa matumizi haya:

  • yameanzishwa kuendeleza kitendo cha ndani ya programu kilichoanzishwa na mtumiaji na
  • yanasimamishwa mara moja baada ya programu kukamilisha matumizi yaliyokusudiwa na kitendo kilichoanzishwa na mtumiaji.

Ni lazima programu zilizobuniwa kwa ajili ya watoto zitii sera ya Programu za Familia Yote.

Ili upate maelezo zaidi kuhusu masharti ya sera, tafadhali angalia makala haya ya usaidizi.

Ruhusa ya Kufikia Faili Zote

Sifa za faili na saraka kwenye kifaa cha mtumiaji huchukuliwa kuwa data ya mtumiaji ambayo ni nyeti na ya binafsi kwa mujibu wa sera ya Taarifa Binafsi na Nyeti na masharti yafuatayo:

  • Programu zinapaswa tu kuomba idhini ya kufikia hifadhi ya kifaa kwa namna ambayo inahitajika ili programu ifanye kazi na hazipaswi kuomba idhini ya kufikia hifadhi ya kifaa kwa niaba ya programu yoyote ya wengine kwa madhumuni yoyote ambayo hayahusiani na utendaji ulio muhimu kwa mtumiaji katika programu.
  • Vifaa vya Android vinavyotumia toleo la R au matoleo mapya, vitahitaji ruhusa ya MANAGE_EXTERNAL_STORAGE ili kudhibiti idhini ya kufikia hifadhi inayoshirikiwa. Ni lazima programu zote zinazolenga toleo la R na zinazoomba idhini ya kufikia hifadhi iliyoshirikiwa (“Ufikiaji wa faili zote”) zipite ukaguzi unaofaa wa ufikiaji kabla ya kuchapishwa. Ni lazima programu zinazokubaliwa kutumia ruhusa hii ziwaombe watumiaji kwa njia ya wazi kuwasha kipengele cha “Ufikiaji wa faili zote” kwenye programu yao chini ya mipangilio ya “Ufikiaji maalum wa programu”. Ili upate maelezo zaidi kuhusu masharti ya R, tafadhali angalia makala haya ya usaidizi.

Ruhusa ya Uonekanaji wa Kifurushi (Programu)

Orodha ya programu zilizosakinishwa iliyotumwa kutoka kwenye kifaa huchukuliwa kuwa data ya mtumiaji ambayo ni nyeti na ya binafsi kwa mujibu wa sera ya Maelezo Nyeti na ya Kibinafsi  na masharti yafuatayo:

Programu ambazo zina lengo kuu la kufungua, kutafuta au kufanya kazi na programu zingine kwenye kifaa, zinaweza kupata ruhusa inayofaa upeo wa uonekanaji kwenye programu zingine zilizosakinishwa kwenye kifaa jinsi inavyobainishwa hapa chini:

  • Uonekanaji mpana wa programu: Uonekanaji mpana ni uwezo wa programu wa kuona kwa kina (au “upana”) programu zilizosakinishwa ("vifurushi") kwenye kifaa.
    • Kwa programu zinazolenga API ya kiwango cha 30 au cha juu, uonekanaji mpana kwenye programu zilizosakinishwa kupitia ruhusa ya QUERY_ALL_PACKAGES unatekelezwa tu katika matumizi mahususi ambapo ufahamu na/au uwezo wa kufanya kazi pamoja na programu yoyote au zote kwenye kifaa unahitajika ili programu ifanye kazi. 
    • Matumizi ya njia mbadala za kukadiria kiwango cha uonekanaji mpana zinazohusishwa na ruhusa ya QUERY_ALL_PACKAGES pia yanatekelezwa tu kwenye utendakazi wa msingi wa programu inayotumiwa na mtumiaji na uwezo wa kufanya kazi pamoja na programu zozote zilizogunduliwa kupitia njia hii.
    • Tafadhali angalia makala haya ya Kituo cha Usaidizi ili ujue hali za matumizi yanayoruhusiwa katika ruhusu ya QUERY_ALL_PACKAGES.
  • Uonekanaji mdogo wa programu: Uonekanaji mdogo wa programu ni wakati ambapo programu inapunguza uwezo wa kufikia data kwa kutuma hoja za programu mahususi kutumia njia zinazolengwa zaidi (badala ya “pana”) (k.m. kutuma hoja za programu mahususi ambazo zinatimiza taarifa ya faili ya maelezo ya programu yako). Unaweza kutumia njia hii ili kutuma hoja za programu katika hali ambapo programu yako ina uwezo wa kufanya kazi na programu zingine unaotii sera au kudhibiti programu hizi. 
  • Ni lazima uonekanaji kwenye orodha ya programu zilizosakinishwa kwenye kifaa uhusiane moja kwa moja na lengo kuu au utendakazi wa msingi ambao watumiaji hufikia ndani ya programu yako. 

Hupaswi kuuza au kushiriki data ya orodha ya programu iliyotumwa kutoka kwenye programu zinazosambazwa na Google Play kwa ajili ya takwimu au madhumuni ya uchumaji wa mapato ya matangazo.

API ya Ufikivu

API ya Ufikivu haitumiki:

  • Kubadilisha mipangilio ya mtumiaji bila ruhusa yake au zuia uwezo wa mtumiaji kuzima au kuondoa huduma au programu yoyote isipokuwa inapoidhinishwa na mzazi au mlezi kupitia programu ya kidhibiti cha wazazi au wasimamizi walioidhinishwa kupitia programu ya usimamizi wa biashara; 
  • Kukwepa vidhibiti vya faragha na arifa vilivyojumuishwa kwenye Android; au
  • Kubadilisha au kutumia kiolesura kwa udanganyifu au vinginevyo kwa njia inayokiuka Sera za Wasanidi Programu katika Google Play. 

API ya Ufikivu haijabuniwa na haiwezi kuombwa kwa ajili ya kurekodi simu ya sauti kutoka mbali. 

Ni lazima utumiaji wa API ya Ufikivu urekodiwe kwenye ukurasa wa programu katika Google Play.

Mwongozo wa IsAccessibilityTool

Programu ambazo utendaji wa msingi unanuia kuwasaidia walemavu kwa njia ya moja kwa moja zinatimiza masharti ya kutumia IsAccessibilityTool ili ziweze kujibainisha hadharani inavyofaa kuwa programu za ufikivu.

Programu zisizotimiza masharti ya IsAccessibilityTool hazipaswi kutumia kitia alama na lazima zitimize masharti muhimu ya ufumbuzi na idhini kama inavyobainishwa katika Sera ya Data ya Mtumiaji kwa vile utendaji unaohusiana na ufikivu si bayana kwa mtumiaji. Tafadhali rejelea makala ya kituo cha usaidizi ya API ya Huduma ya Ufikivu ili upate maelezo zaidi.

Ni lazima programu zitumie API na ruhusa zinazohusisha vipengele vichache zaidi badala ya API ya Ufikivu inapowezekana ili kufikia utendaji unaohitajika. 

Omba Ruhusa ya Kusakinisha Vifurushi

Ruhusa hii ya REQUEST_INSTALL_PACKAGES inaruhusu programu kuomba usakinishaji wa vifurushi vya programu.​​ Ili utumie ruhusa hii, utendaji wa msingi wa programu yako lazima ujumuishe:

  • Kutuma au kupokea vifurushi vya programu; na
  • Kuruhusu usakinishaji wa vifurushi vya programu unaoanzishwa na mtumiaji.

Utendaji unaoruhusiwa unajumuisha:

  • Kuvinjari au kutafuta katika wavuti
  • Huduma za mawasiliano zinazoruhusu viambatisho
  • Kushiriki, kuhamisha au kudhibiti faili
  • Kudhibiti kifaa cha kampuni
  • Kuhifadhi nakala au kurejesha vipengee
  • Uhamishaji kwenye Kifaa au Simu
  • Programu inayotumika kudhibiti Jam inayosawazisha simu na kifaa cha kuvaliwa au kifaa cha IoT (kwa mfano, saa mahiri au televisheni inayoweza kuunganisha kwenye intaneti)

Utendaji wa msingi unafafanuliwa kuwa ni lengo kuu la programu. Utendaji wa msingi, pamoja na vipengele vyovyote vya msingi vinavyojumuisha utendaji huu wa msingi lazima vitangazwe na kuonyeshwa kwa njia dhahiri kwenye maelezo ya programu.

Huruhusiwi kutumia REQUEST_INSTALL_PACKAGES kufanya masasisho binafsi, marekebisho au kuunganisha APK nyingine kwenye faili ya kipengee isipokuwa kwa madhumuni ya usimamizi wa kifaa. Masasisho yote au usakinishaji wa vifurushi ni lazima zitii sera ya Google Play Dhidi ya Matumizi Mabaya ya Vifaa na Mtandao na lazima zianzishwe na ziendeshwe na mtumiaji.

Ruhusa za Health Connect kutoka Android

Data inayofikiwa kupitia Ruhusa za Health Connect huchukuliwa kuwa data ya mtumiaji ambayo ni nyeti na ya binafsi kwa mujibu wa sera ya Data ya Mtumiaji na masharti ya ziada yafuatayo:

Ufikiaji na Matumizi Sahihi ya Health Connect

Maombi ya kufikia data kupitia Health Connect lazima yawe dhahiri na yanaeleweka. Health Connect inapaswa tu kutumika kwa mujibu wa sera, sheria na masharti yanayotumika pamoja na hali zilizoidhinishwa, kama ilivyobainishwa katika sera hii. Hatua hii inamaanisha kwamba unapaswa tu kuomba idhini ya kufikia ruhusa wakati programu au huduma yako itatimiza moja kati ya hali za matumizi zilizoidhinishwa.

Hali za matumizi zilizoidhinishwa ili kufikia Ruhusa za Health Connect ni:

  • Programu au huduma zenye kipengele kimoja au zaidi chenye manufaa kwa afya na siha ya mtumiaji kupitia kiolesura kinachoruhusu moja kwa moja watumiaji waweke rekodi zao za kila siku, kuripoti, kufuatilia na/au kuchanganua mazoezi yao ya mwili, kulala, ustawi wa akili, lishe, vipimo vya afya, maelezo ya kimaumbile na/au maelezo mengine yanayohusiana na afya au siha pamoja na vipimo.
  • Programu au huduma zenye kipengele kimoja au zaidi chenye manufaa kwa afya na siha ya mtumiaji kupitia kiolesura kinachoruhusu watumiaji wahifadhi mazoezi yao ya mwili, kulala, ustawi wa akili, lishe, vipimo vya afya, maelezo ya kimaumbile na/au maelezo mengine yanayohusiana na afya au siha pamoja na vipimo kwenye simu na/au kifaa chao cha kuvaliwa na kushiriki data yao na programu zingine kwenye kifaa zinazotimiza hali hizi za matumizi.

Health Connect ni mfumo wa madhumuni ya jumla wa kuhifadhi na kushiriki data ambao huruhusu watumiaji wakusanye data ya afya na siha kutoka vyanzo mbalimbali kwenye kifaa chao cha Android kisha kushiriki na wengine watakapoamua. Data huenda ikatoka kwenye vyanzo mbalimbali kama itakavyoamuliwa na watumiaji. Wasanidi programu wanapaswa kutathmini iwapo Health Connect ni sahihi kwa matumizi wanayokusudia na kuchunguza pamoja na kuhakiki chanzo na ubora wa data yoyote kutoka Health Connect inayohusiana na madhumuni yoyote, hasa kwa matumizi ya utafiti, afya au tiba.

  • Programu zinazoendesha utafiti unaohusu afya wenye washiriki ambao ni binadamu, unaotumia data kutoka Health Connect zinapaswa kupata idhini kutoka kwa washiriki au ikiwa washiriki ni watoto, idhini kutoka kwa mzazi au mlezi. Idhini hii inapaswa kujumuisha (a) aina, madhumuni na muda wa utafiti; (b) utaratibu, hatari na manufaa kwa mshiriki; (c) maelezo kuhusu usiri na ushughulikiaji wa data (ikiwa ni pamoja na ushiriki wowote na wengine); (d) mtu wa kuwasiliana naye endapo kuna maswali kutoka kwa mshiriki; na (e) mchakato wa kujiondoa. Programu zinazoendesha utafiti unaohusu afya yenye washiriki ambao ni binadamu, unaotumia data kutoka Health Connect zinapaswa kupata idhini kutoka bodi ya kujitegemea yenye lengo la 1) kulinda haki, usalama na ustawi wa washiriki na 2) yenye mamlaka ya kuchunguza, kubadilisha na kuidhinisha utafiti wenye washiriki ambao ni binadamu. Ushahidi wa uthibitisho unapaswa kutolewa utakapohitajika.
  • Pia, ni jukumu lako kuhakikisha kwamba unatii mahitaji yoyote ya mamlaka za usimamizi au sheria ambazo huenda zikatumika kulingana na matumizi uliyokusudia ya Health Connect pamoja na data yoyote kutoka Health Connect. Isipokuwa kama ilivyobainishwa dhahiri katika lebo au taarifa zilizotolewa na Google kwa bidhaa na huduma mahususi za Google, Google haiidhinishi matumizi ya au kuthibitisha usahihi wa data yoyote iliyo katika Health Connect kwa matumizi na madhumuni yoyote, hasa, kwa matumizi ya utafiti, afya au tiba. Google inakanusha dhima zote zinazohusiana na matumizi ya data inayopatikana kupitia Health Connect.

Matumizi yaliyowekewa Vizuizi

Unapotumia Health Connect kwa matumizi yanayofaa, matumizi yako ya data iliyofikiwa kupitia Health Connect pia yanapaswa kutii masharti yaliyo hapa chini. Masharti haya yanatumika kwenye data ghafi iliyopatikana kutoka Health Connect pamoja na data iliyojumlishwa, isiyomtambulisha mtu au iliyotokana na data hiyo ghafi.

  • Fanya utumiaji wako wa data ya Health Connect uwe tu kwa ajili ya utoaji au uboreshaji wa hali yako ya matumizi yanayofaa au vipengele vinavyoonekana na ni dhahiri katika kiolesura cha programu inayoomba.
  • Hamishia tu kwa wengine data ya mtumiaji:
    • Ili kutoa au kuboresha hali yako ya matumizi yanayofaa au vipengele ambavyo vipo dhahiri katika kiolesura cha programu inayoomba na kwa idhini ya mtumiaji pekee;
    • Kwa madhumuni ya usalama, ikiwa ni lazima (kwa mfano, kuchunguza matumizi mabaya);
    • Ili kutii sheria na/au kanuni zinazotumika; au,
    • Kama sehemu ya muungano wa kibiashara, ununuzi wa biashara au kuuza mali za msanidi programu baada ya kupata idhini dhahiri ya awali kutoka kwa mtumiaji.
  • Usiruhusu binadamu asome data ya mtumiaji, isipokuwa:
    • Idhini dhahiri ya kusoma data mahususi imetolewa na mtumiaji;
    • Ni lazima kwa madhumuni ya usalama, (kwa mfano, kuchunguza matumizi mabaya);
    • Ili kutii sheria zinazotumika; au,
    • Data (ikiwa ni pamoja na data iliyotokana na data ghafi) inajumlishwa na kutumika katika shughuli za ndani kwa mujibu wa mahitaji ya faragha pamoja na mahitaji mengine ya kisheria yanayotumika katika eneo la mamlaka.

Uhamishaji, matumizi au uuzaji mwingine wowote wa data ya Health Connect hauruhusiwi, ikiwa ni pamoja na:

  • Kuhamisha au kuuza data ya mtumiaji kwenda kwa wengine kama vile mifumo ya utangazaji, madalali wa data au wauzaji wowote wa taarifa.
  • Kuhamisha, kuuza au kutumia data ya mtumiaji ili kuonyesha matangazo, ikijumuisha matangazo yaliyowekewa mapendeleo au yanayotegemea mambo yanayomvutia mtumiaji.
  • Kuhamisha, kuuza au kutumia data ya mtumiaji ili kubaini ustahili wa mikopo au kwa madhumuni ya kukopesha.
  • Kuhamisha, kuuza au kutumia data ya mtumiaji na bidhaa au huduma yoyote inayoweza kutimiza masharti ya kuwa kifaa cha matibabu kwa mujibu wa Kifungu cha 201(h) cha Sheria ya Marekani ya Chakula, Dawa na Vipodozi iwapo data ya mtumiaji itatumiwa na kifaa cha matibabu ili kutekeleza utendaji wake uliodhibitiwa.
  • Kuhamisha, kuuza au kutumia data ya mtumiaji kwa madhumuni yoyote au kwa njia yoyote inayohusu Maelezo ya Afya Yaliyolindwa (kama ilivyobainishwa na HIPAA) isipokuwa endapo ulipokea idhini kwa maandishi hapo awali kutoka Google kwa ajili ya matumizi hayo.

Uwezo wa kufikia Health Connect haupaswi kutumika kinyume cha sera hii au sera pamoja na sheria na masharti mengine ya Health Connect yanayotumika, ikiwa ni pamoja na madhumuni yafuatayo:

  • Usitumie Health Connect kusanidi au kujumuisha katika, programu, mazingira au shughuli ambazo matumizi au kutokufanikiwa kwa Health Connect huenda kukatarajiwa kusababisha kifo, majeraha ya mwili au uharibifu wa mali au mazingira (kama vile utengenezaji au uendeshaji wa vituo vya nyuklia, udhibiti wa safari za ndege, mifumo ya kusaidia kuokoa uhai au ya silaha).
  • Usifikie data yoyote iliyopatikana kupitia Health Connect kwa kutumia programu zisizokuwa na kiolesura. Ni lazima programu zionyeshe aikoni inayotambulika vizuri kwenye trei ya programu, mipangilio ya programu ya kifaa, aikoni za arifa, n.k.
  • Usitumie Health Connect na programu zinazosawazisha data kati ya vifaa au mifumo isiyooana.
  • Health Connect haiweza kuunganisha kwenye programu, huduma au vipengele ambavyo vinalenga watoto pekee. Health Connect haijaidhinishwa kwa ajili ya huduma zinazolenga watoto.

Taarifa ya kuidhinisha kwamba matumizi yako ya data ya Health Connect yanatii vikwazo vya Matumizi yaliyowekewa Vizuizi inapaswa ifichuliwe katika programu yako au kwenye tovuti inayomilikiwa na huduma yako ya wavuti au programu; kwa mfano, kiungo katika ukurasa wa kwanza kinachoelekeza kwenye ukurasa maalumu au sera ya faragha inayosema: "Matumizi ya taarifa kutoka Health Connect yanatii sera ya Ruhusa za Health Connect, ikiwa ni pamoja na masharti ya Matumizi yaliyowekewa Vizuizi."

Upeo wa kiwango cha chini

Unaweza tu ukaomba idhini ya kufikia ruhusa ambazo ni muhimu kwenye utekelezaji wa programu au utendaji wa huduma yako. 

Hatua hii inamaanisha:

  • Usiombe idhini ya kufikia maelezo ambayo huyahitaji. Omba tu idhini ya kufikia ruhusa ambazo zinahitajika ili kutekeleza vipengele au huduma za bidhaa yako. Ikiwa bidhaa yako haihitaji kufikia ruhusa mahususi, hupaswi kuomba idhini ya kufikia ruhusa hizi.

Ilani Wazi na Sahihi pamoja na Udhibiti

Health Connect hushughulikia data ya afya na siha, inayojumuisha maelezo nyeti na ya binafsi. Programu na huduma zote lazima zijumuishe sera ya faragha, inayopaswa kufumbua kwa kina jinsi programu au huduma yako inavyokusanya, kutumia na kushiriki data ya mtumiaji. Hatua hii inajumuisha aina ya washirika ambao hutumiwa data ya mtumiaji, jinsi unavyotumia data, jinsi unavyoihifadhi na kuilinda na kuhusu kile kinachofanyika kwenye data iwapo akaunti itafungwa na/au kufutwa.

Mbali na masharti yaliyo chini ya sheria inayotumika, unapaswa pia utii masharti yafuatayo:

  • Ni sharti utoe ufumbuzi kuhusu jinsi unavyoifikia data, kuikusanya, kuitumia na kuishiriki. Ufumbuzi huo:
    • Ni lazima uwakilishe kwa usahihi utambulisho wa programu au huduma inayotaka iwe na uwezo wa kufikia data ya mtumiaji;
    • Ni lazima utoe maelezo sahihi na yaliyodhahiri yanayofafanua aina za data inayofikiwa, inayoombwa na/au inayokusanywa;
    • Ni lazima ufafanue jinsi data itakavyotumika na/au kushirikiwa: Ikiwa utaomba data kwa sababu moja, lakini data hiyo pia ikatumika kwa sababu ya pili, unapaswa kuwaarifu watumiaji kuhusu hali zote mbili za matumizi.
  • Ni sharti utoe hati ya usaidizi kwa mtumiaji inayoeleza jinsi watumiaji wanaweza kudhibiti na kufuta data yao kutoka kwenye programu yako.

Kushughulikia Data kwa Usalama

Unapaswa kushughulikia kwa usalama data yote ya mtumiaji. Chukua hatua adilifu na zinazofaa ili kulinda programu na mifumo yote inayotumia Health Connect dhidi ya ufikiaji, ubadilishaji, ufumbuzi, kupotea, kuharibiwa, au matumizi kwa njia isiyoidhinishwa au inayokiuka sheria.

Mbinu za usalama zinazopendekezwa hujumuisha utekelezaji na udumishaji wa Mfumo wa Usimamizi wa Usalama wa Taarifa kama ilivyoainishwa kwenye ISO/IEC 27001 pamoja na kuhakikisha kwamba programu au huduma yako ya wavuti ipo imara na haina matatizo ya kawaida ya usalama kama yalivyobainishwa na OWASP Top 10.

Kulingana na API inayofikiwa pamoja na idadi ya ruhusa zilizotolewa kwa mtumiaji au watumiaji, tutahitaji programu au huduma yako ipitie tathmini ya usalama ya mara kwa mara na ipokee Barua ya Tathmini kutoka kwa wahusika wengine waliyobainishwa ikiwa bidhaa yako inahamisha data kutoka kwenye kifaa cha mtumiaji.

Kwa maelezo zaidi kuhusu masharti ya programu zinazounganisha kwenye Health Connect, tafadhali angalia makala haya ya usaidizi.

Huduma ya VPN

VpnService ni daraja la msingi kwa ajili ya programu kuendeleza na kutengeneza huduma yazo zenyewe za VPN. Programu zinazotumia VpnService tu, ambazo pia zina utendaji wa msingi wa VPN ndizo zinaweza kuunda njia salama ya upitishaji wa data kwenye seva ya mbali katika kifaa chenyewe. Hali zisizofuata kanuni hujumuisha programu zinazohitaji seva ya mbali kwa ajili ya utendaji wa msingi kama vile:

  • Programu za vidhibiti vya wazazi na udhibiti wa kibiashara.
  • Ufuatiliaji wa matumizi ya programu.
  • Programu za usalama wa kifaa (kwa mfano, kingavirusi, kidhibiti cha vifaa vya mkononi, kinga mtandao).
  • Zana zinazohusiana na mtandao (kwa mfano, ufikiaji wa mbali).
  • Programu za kuvinjari kwenye wavuti.
  • Programu za mtoa huduma zinazohitaji kutumia utendaji wa VPN ili kutoa huduma za simu na muunganisho.

VpnService haiwezi kutumika:

  • Kukusanya data binafsi na nyeti ya mtumiaji bila ufumbuzi dhahiri na idhini.
  • Kuelekeza kwingine au kubadilisha shughuli za mtumiaji kutoka programu zingine kwenye kifaa kwa madhumuni ya uchumaji wa mapato (kwa mfano, kufanya ionekane kuwa mtumiaji ameangalia matangazo akiwa kwenye nchi tofauti na aliyopo).

Programu zinazotumia VpnService zinapaswa:

Ruhusa ya Kengele Sahihi

Ruhusa mpya itakayoongezwa ya USE_EXACT_ALARM, itazinduliwa ambayo itatoa uwezo wa kufikia utendaji sahihi wa kengele katika programu kuanzia Android 13 (kiwango lengwa cha API 33). 

USE_EXACT_ALARM ni ruhusa inayodhibitiwa na programu zinapaswa tu kubainisha ruhusa hii ikiwa utendaji wake wa msingi unaonyesha hitaji la kufikia utendaji sahihi wa kengele. Programu zitakazoomba ruhusa hii inayodhibitiwa, zitakaguliwa na zile ambazo hazitatimiza kigezo cha hali ya matumizi yanayokubalika hazitaruhusiwa kuchapisha kwenye Google Play.

Hali za matumizi zinazokubalika kutumia Ruhusa ya Kengele Sahihi

Programu yako inapaswa tu kutumia utendaji wa USE_EXACT_ALARM wakati utendaji msingi wa programu yako kwa mtumiaji unahitaji vitendo vinavyolingana kwa usahihi na saa, kama vile:

  • Ni programu ya kengele au ya kupima muda.
  • Ni programu ya kalenda inayoonyesha arifa za tukio.

Ukiwa una hali ya matumizi kwa ajili ya utendaji sahihi wa kengele ambayo haipo hapa juu, unapaswa kutathmini iwapo unaweza kutumia SCHEDULE_EXACT_ALARM kama chaguo mbadala.

Ili upate maelezo zaidi kuhusu utendaji sahihi wa kengele, tafadhali angalia mwongozo huu wa msanidi programu.

Ruhusa ya Utaratibu wa Kuratibu Skrini Nzima

Kwa programu zinazolenga toleo la Android 14 (kiwango lengwa cha API 34) na zaidi, USE_FULL_SCREEN_INTENT ni ruhusa ya ufikiaji wa programu maalum. Programu zitaruhusiwa tu kiotomatiki kutumia ruhusa ya USE_FULL_SCREEN_INTENT ikiwa utendaji wa msingi wa programu unapatikana chini ya moja ya aina zilizo hapa chini zinazohitaji arifa za kipaumbele cha juu:

  • kuweka kengele
  • kupokea simu zinazopigwa au simu za video

Programu zinazoomba ruhusa hii zitakaguliwa na zile ambazo hazitimizi kigezo cha hapo juu hazitapewa ruhusa hii kiotomatiki. Kwa hivyo, lazima programu ziombe ruhusa kutoka kwa mtumiaji ili kutumia USE_FULL_SCREEN_INTENT.

Kama kikumbusho, matumizi yoyote ya ruhusa ya USE_FULL_SCREEN_INTENT lazima yatii Sera zote za Google Play za Wasanidi Programu, ikiwa ni pamoja na sera za Programu za Simu Zisizotakikana, Matumizi Mabaya ya Kifaa na Mtandao na Matangazo. Arifa za utaratibu wa kuratibu skrini nzima hazipaswi kuathiri, kukatiza, kuharibu au kufikia kifaa cha mtumiaji kwa njia ambayo haijaidhinishwa. Pia, programu hazipaswi kuathiri programu nyingine au urahisi wa kutumia kifaa.

Pata maelezo zaidi kuhusu ruhusa ya USE_FULL_SCREEN_INTENT katika Kituo chetu cha Usaidizi.


Matumizi Mabaya ya Kifaa na Mtandao

Haturuhusu programu zinazoingilia, zinazokatiza, zinazoharibu au zinazofikia katika njia isiyoidhinishwa kifaa cha mtumiaji, vifaa vingine au kompyuta, seva, mitandao, Kusano ya Kusanifu Programu (API), au huduma, ikiwa ni pamoja na, lakini siyo tu, programu nyingine kwenye kifaa, huduma yoyote ya Google, au mtandao wa mtoa huduma usioidhinishwa.

Ni lazima programu kwenye Google Play zitii masharti chaguomsingi ya uboreshaji wa mfumo wa Android yanayopatikana katika Mwongozo wa Ubora wa Programu za Msingi katika Google Play.

Programu inayosambazwa kupitia Google Play haifai kujirekebisha, kujibadilisha au kujisasisha kwa kutumia mbinu yoyote isipokuwa utaratibu wa kusasisha wa Google Play. Pia, programu haipaswi kupakua msimbo unaoweza kutekelezwa (k.m., faili za dex, JAR, .so) kutoka chanzo kingine isipokuwa Google Play. Masharti haya hayatumiki kwenye msimbo unaotumika katika mtambo pepe au kitafsiri ambapo mojawapo inatoa idhini inayodhibitiwa ya kufikia API za Android (kama vile JavaScript katika kivinjari au mwonekano wa wavuti). 

Programu au msimbo wa wengine (k.m., SDK) zilizo na lugha zinazotafsiriwa (JavaScript, Python, Lua, n.k.) zinazopakiwa wakati zinatumika (k.m., zisizofungashwa pamoja na programu) hazipaswi kuruhusu ukiukaji wa sera za Google Play unaoweza kutokea.

Haturuhusu msimbo ambao unaleta au kusababisha uwezekano wa kuathiriwa kiusalama. Angalia Mpango Wetu wa Kuimarisha Usalama wa Programu ili upate maelezo kuhusu matatizo ya hivi majuzi ya usalama yaliyoripotiwa kwa wasanidi programu.

Ili kudumisha usalama na heshima kwenye mfumo wa Google Play, tumebuni viwango vinavyobainisha na kuzuia maudhui ambayo hayafai au yanayodhuru watumiaji wetu.

Mifano ya ukiukaji wa kawaida wa Matumizi Mabaya ya Vifaa na Mtandao:

  • Programu zinazozuia au kuingilia jinsi programu nyingine inavyoonyesha matangazo.
  • Programu zinazotumiwa kidanganyifu katika michezo zinazoathiri uchezaji wa programu nyingine.
  • Programu zinazowezesha au kutoa maelekezo ya jinsi ya kuvamia huduma, programu au maunzi, au zinazokwepa ulinzi wa kiusalama.
  • Programu zinazofikia au zinazotumia huduma au API katika njia inayokiuka sheria na masharti.
  • Programu ambazo hazitimizi masharti ya kuwekwa kwenye orodha ya zilizoruhusiwa na hujaribu kukwepa udhibiti wa nishati ya mfumo.
  • Programu ambazo zinaendeleza huduma za seva mbadala kwa washirika wengine zinaweza tu kufanya hivyo katika programu ambapo hayo ndiyo madhumuni ya msingi kwa watumiaji wa programu.
  • Programu au msimbo wa wengine (kwa mfano, SDK) zinazopakua msimbo unaoweza kutekelezwa, kama vile faili za dex au msimbo halisi, kutoka kwenye chanzo kingine tofauti na Google Play.
  • Programu zinazosakinisha programu zingine kwenye kifaa bila idhini ya mtumiaji.
  • Programu zinazounganisha au kuendeleza usambazaji au usakinishaji wa programu hasidi.
  • Programu au msimbo wa wengine (kwa mfano, SDK) zilizo na mwonekano wa wavuti zenye Kiolesura cha JavaScript kinachopakia maudhui ya wavuti yasiyoaminika (kwa mfano, http:// URL) au URL ambazo hazijadhibitishwa zinazotoka kwenye vyanzo visivyoaminika (kwa mfano, URL zenye Utaratibu wa kuratibu usioaminika).
  • Programu zinazotumia ruhusa ya utaratibu wa kuratibu skrini nzima ili kulazimisha mtumiaji atumie arifa au matangazo yanayokatiza mtumiaji.

Matumizi ya Huduma ya Wakati Programu Inatumika

Ruhusa ya Huduma Inayoendeshwa Programu Inapotumika huhakikisha matumizi yanayofaa yanayowalenga watumiaji ya huduma zinazoendeshwa programu inapotumika. Kwa programu zinazolenga toleo la Android 14 na matoleo mapya zaidi, ni lazima ubainishe aina sahihi ya huduma inayoendeshwa programu inapotumika kwa kila huduma inayoendeshwa programu inapotumika ambayo inatumika kwenye programu yako na ubainishe ruhusa ya huduma inayoendeshwa programu inapotumika inayofaa kwa aina hiyo. Kwa mfano, ikiwa hali ya utumiaji wa programu yako inahitaji ramani ya kutambulisha mahali, ni lazima ubainishe ruhusa ya FOREGROUND_SERVICE_LOCATION kwenye faili ya maelezo ya programu yako.

Programu huruhusiwa tu kubainisha ruhusa ya huduma inayoendeshwa programu inapotumika ikiwa matumizi:

  • hutoa kipengele ambacho ni cha manufaa kwa mtumiaji na muhimu kwa utendaji wa msingi wa programu
  • huanzishwa na mtumiaji au yanaonekana kwa mtumiaji (kwa mfano, sauti inayotokana na kucheza wimbo, kutuma maudhui kwenye kifaa kingine, arifa sahihi na ya wazi ya mtumiaji, ombi la mtumiaji la kupakia picha kwenye wingu).
  • yanaweza kusimamishwa au kusitishwa na mtumiaji
  • hayawezi kukatizwa au kuahirishwa na mfumo bila kusababisha hali mbaya ya utumiaji au kusababisha kipengele kinachotarajiwa cha mtumiaji kutofanya kazi kama ilivyokusudiwa (kwa mfano, simu inatakiwa kupigwa mara moja na isiweze kuahirishwa na mfumo).
  • ni ya kutekeleza tu ilimradi ni muhimu kukamilisha jukumu

Hali zifuatazo za huduma inayoendeshwa programu inapotumika hazifuati vigezo vya hapo juu:

Matumizi ya huduma inayoendeshwa programu inapotumika yamefafanuliwa zaidi hapa.

Majukumu ya Uhamishaji wa Data unaoanzishwa na mtumiaji

Programu huruhusiwa tu kutumia API ya majukumu ya uhamishaji wa data unaoanzishwa na mtumiaji ikiwa matumizi:

  • yanaanzishwa na mtumiaji
  • ni ya majukumu ya uhamishaji wa data ya mtandao
  • ni ya kutekeleza tu ilimradi ni muhimu kukamilisha uhamishaji wa data

Matumizi ya API za Uhamishaji wa Data unaoanzishwa na Mtumiaji yamefafanuliwa zaidi hapa.

Masharti ya Flag Secure

FLAG_SECURE ni alama ya onyesho inayobainishwa katika msimbo wa programu ili kuashiria kuwa kiolesura chake kinajumuisha data nyeti inayokusudiwa kudhibitiwa kwenye mfumo salama wakati programu inatumika. Alama hii imebuniwa ili kuzuia data isionekane kwenye picha za skrini au isitazamwe kupitia skrini zisizo salama. Wasanidi programu hubainisha alama hii pale maudhui ya programu hayapaswi kutangazwa, kutazamwa au vinginevyo kuenezwa nje ya programu au kifaa cha mtumiaji.

Kwa madhumuni ya usalama na faragha, programu zote zinazosambazwa kwenye Google Play zinapaswa kuheshimu taarifa ya FLAG_SECURE ya programu zingine. Inamaanisha, programu hazipaswi kuwezesha au kuunda njia za kukwepa mipangilio ya FLAG_SECURE kwenye programu zingine.

Programu zinazotimiza masharti ya kuwa Zana ya Ufikivu hazijumuishwi katika masharti haya, ilimradi hazienezi, hazihifadhi au kuweka maudhui yanayolindwa na FLAG_SECURE katika akiba ili kufikiwa nje ya kifaa cha mtumiaji.

Programu Zinazotekeleza Metadata ya Android iliyo kwenye Kifaa

Programu za metadata ya Android zilizo kwenye kifaa hutoa mazingira yanayoiga sehemu kamili au vifungu vya mfumo wa uendeshaji wa Android unaotumika. Hali ya matumizi katika mazingira haya huenda isifanane na ya kifurushi kamili cha vipengele vya usalama vya Android, ndio maana wasanidi programu wanaweza kuchagua kuweka kitia alama cha faili ya maelezo ya mazingira salama ili kuwasiliana na metadata ya Android iliyo kwenye kifaa kuwa hazipaswi kufanya kazi katika mazingira yaliyoigwa ya Android.

Kitia Alama cha Faili ya Maelezo ya Mazingira Salama

REQUIRE_SECURE_ENV ni kitia alama kinachoweza kubainishwa katika faili ya maelezo ya programu ili kuashiria kuwa programu hii haipaswi kutekelezwa kwenye programu za metadata ya Android iliyo kwenye kifaa. Kwa madhumuni ya usalama na faragha, programu zinazotoa metadata ya Android iliyo kwenye kifaa ni sharti ziheshimu programu zote zenye taarifa ya kitia alama hiki na:
  • Kagua faili za maelezo ili ubaini programu zinazokusudia kupakia katika metadata ya Android iliyo kwenye kifaa kwa ajili ya kitia alama hiki.
  • Kutopakia programu zilizobainisha kitia alama hiki katika metadata ya Android iliyo kwenye kifaa.
  • Kutofanya kazi kama seva mbadala kwa kukatiza au kutekeleza API kwenye kifaa ili zionekane kana kwamba zimesakinishwa kwenye metadata.
  • Kutowezesha, au kuunda njia mbadala za kukwepa kitia alama (kama vile, kupakia toleo la zamani la programu ili kukwepa kitia alama cha sasa cha REQUIRE_SECURE_ENV cha programu).
Pata maelezo zaidi kuhusu sera hii kwenye Kituo chetu cha Usaidizi.

Tabia Danganyifu

Haturuhusu programu zinazojaribu kuwapotosha watumiaji au kuendeleza mienendo isiyo ya kweli ikiwa ni pamoja na programu zilizobainishwa kuwa haziwezi kufanya chochote. Ni lazima programu itoe ufumbuzi, maelezo na picha au video sahihi ya utendaji wake kwenye sehemu zote za metadata. Programu hazipaswi kujaribu kuiga utendaji au maonyo kutoka mifumo ya uendeshaji au programu zingine. Ni lazima mabadiliko yoyote ya mipangilio ya kifaa yafanywe baada ya kupata idhini ya mtumiaji na yawe rahisi kutenduliwa na mtumiaji.

Madai Yanayopotosha

Haturuhusu programu zilizo na maelezo au madai ya udanganyifu au yanayopotosha, ikiwa ni pamoja na maelezo, jina, aikoni na picha za skrini.
Ili kudumisha usalama na heshima kwenye mfumo wa Google Play, tumebuni viwango vinavyobainisha na kuzuia maudhui ambayo hayafai au yanayodhuru watumiaji wetu.
  • Programu zinazowakilisha kwa uongo au zisizobainisha kwa uwazi utendaji wake:
    • Programu inayoeleza kuwa ni mchezo wa mbio za magari katika maelezo na picha zake za skrini, lakini ni mchezo wa chemsha bongo unaotumia picha ya gari.
    • Programu inayodai kuwa ni programu ya kingavirusi, lakini iliyo na mwongozo wa maandishi pekee unaoelezea jinsi ya kuondoa virusi.
  • Programu zinazodai utendaji ambao hauwezi kutekelezwa kama vile programu za kufukuza wadudu, hata zikionyeshwa kama za mzaha, bandia, utani n.k.
  • Programu ambazo hazijapangwa vizuri, ikiwa ni pamoja na, lakini si tu, ukadiriaji au aina ya programu.
  • Maudhui yanayopotosha au ya udanganyifu yanayoweza kuathiri michakato ya kupiga kura au kuhusu matokeo ya uchaguzi.
  • Programu ambazo zinadai kwa njia ya udanganyifu kushirikiana na huluki ya serikali au kutoa au kutekeleza huduma za serikali ilhali hazijaidhinishwa kwa njia sahihi.
  • Programu zinazodanganya kuwa ni programu rasmi za huluki inayotambulika. Majina kama "Programu Rasmi ya Justin Bieber" hayaruhusiwi bila ruhusa au haki zinazohitajika.

(1) Programu hii ina madai ya matibabu au yanayohusiana na afya (Tibu Saratani) ambayo yanapotosha.
(2) Programu hizi zinadai utendaji ambao hauwezi kutekelezwa (kutumia simu yako) kama kifaa cha kupima pumzi.

Mabadiliko Danganyifu ya Mipangilio ya Kifaa

Haturuhusu programu zinazofanya mabadiliko ya mipangilio au vipengele vya kifaa cha mtumiaji nje ya programu bila mtumiaji kufahamu na kutoa ridhaa yake. Mipangilio na vipengele vya kifaa vinajumuisha mipangilio ya mfumo au kivinjari, alamisho, njia za mkato, aikoni, wijeti na upangaji wa programu kwenye skrini ya kwanza.

Zaidi ya hayo, haturuhusu:

  • Programu zinazorekebisha mipangilio au vipengele vya kifaa kwa idhini ya mtumiaji lakini katika njia ambayo si rahisi kutenduliwa.
  • Programu au matangazo yanayorekebisha mipangilio au vipegele vya kifaa kama huduma kwa watu wengine au kwa madhumuni ya utangazaji.
  • Programu zinazopotosha watumiaji kuondoa au kuzima programu za wengine au kurekebisha mipangilio au vipengele vya kifaa.
  • Programu zinazohimiza au kutoa motisha kwa watumiaji kuondoa au kuzima programu za wengine au kurekebisha mipangilio au vipengele vya kifaa isipokuwa kama sehemu ya huduma ya usalama inayoweza kuthibitishwa.

Kuendeleza Mienendo Isiyo ya Kweli

Haturuhusu programu ambazo zinawasaidia watumiaji kuwapotosha wengine au zina utendaji danganyifu kwa njia yoyote, ikijumuisha: programu ambazo zinatengeneza au kusaidia kutengeneza kadi za vitambulisho, nambari za usalama wa jamii, pasipoti, vyeti, kadi za mikopo, akaunti za benki, na leseni za udereva. Lazima programu ziwe na maelezo sahihi ya ufumbuzi, mada, ufafanuzi na picha/video kuhusu maudhui na/au utendaji wa programu na zinapaswa kufanya kazi kwa uadilifu na usahihi jinsi inavyotarajiwa na mtumiaji.

Nyenzo za ziada za programu (kwa mfano, vipengee vya mchezo) zinaweza tu kupakuliwa iwapo zinahitajika kwa matumizi ya watumiaji wa programu. Nyenzo zilizopakuliwa ni sharti zitii sera zote za Google Play na kabla ya kuanza kupakua, lazima programu iwatumie watumiaji kidokezo na ibainishe wazi ukubwa wa faili ya kupakuliwa.

Dai lolote kuwa programu inatumika kwa ajili ya "utani", "sababu za burudani" (au maneno kama hayo) halizuii programu kufuata sera zetu.

Ili kudumisha usalama na heshima kwenye mfumo wa Google Play, tumebuni viwango vinavyobainisha na kuzuia maudhui ambayo hayafai au yanayodhuru watumiaji wetu.
  • Programu zinazoiga tovuti au programu nyingine ili kufanya watumiaji wafichue taarifa za binafsi au za uthibitishaji.
  • Programu ambazo zinaonyesha nambari za simu, anwani (ambazo hazijathibitishwa au halisi) au taarifa zinazoweza kuwatambulisha watu au mashirika bila idhini.
  • Programu ambazo zina utendaji tofauti kulingana na jiografia ya watumiaji, vigezo vya vifaa au data nyingine ambayo mtumiaji anategema ambapo tofauti hizo hazijatangazwa kwa uwazi kwa watumiaji kwenye ukurasa wa programu katika Google Play.  
  • Programu ambazo hubadilisha matoleo kwa kiasi kikubwa bila kumwarifu mtumiaji (k.m., sehemu ya ‘ni nini kipya’) na kusasisha ukurasa wa programu katika Google Play.
  • Programu zinazojaribu kubadilisha au kufumba msimbo wa vitendo wakati wa ukaguzi.
  • Programu zilizo na faili za kupakuliwa zinazotokana na Mtandao wa Kuwasilisha Maudhui (CDN) ambazo hazimtumii mtumiaji kidokezo wala kubainisha ukubwa wa faili ya kupakuliwa kabla ya kupakua.

Maudhui Yaliyobadilishwa

Haturuhusu programu zinazotangaza au zinazosaidia kuanzisha maelezo au madai ya uongo au ya kupotosha yanayowasilishwa kupitia picha, video na/au maandishi. Haturuhusu programu zilizobainishwa kuwa zinaeneza au kuendeleza picha, video na/au maandishi ya kupotosha, ambazo zinaweza kusababisha madhara kutokana na tukio nyeti, siasa, masuala ya jamii au masuala mengine yanayohusu umma.

Programu zinazobadilisha au kuathiri maudhui, zaidi ya marekebisho ya kawaida na yanayokubaliwa kwa uhariri kwa ajili ya ubora au kueleweka vizuri, lazima zifumbue kwa uwazi au ziweke alama maalum kwenye maudhui yaliyobadilishwa iwapo mtu wa kawaida anaweza kukosa kuelewa kuwa maudhui yamebadilishwa. Hali maalum zinaweza kuwekwa kwa manufaa ya umma au tashtiti au bezo dhahiri.

Ili kudumisha usalama na heshima kwenye mfumo wa Google Play, tumebuni viwango vinavyobainisha na kuzuia maudhui ambayo hayafai au yanayodhuru watumiaji wetu.
  • Programu zinazomweka mtu mashuhuri kwenye maandamano wakati wa tukio nyeti la kisiasa.
  • Programu zinazotumia watu mashuhuri au maudhui kutoka kwenye tukio nyeti kutangaza uwezo wa kubadilisha maudhui ndani ya ukurasa wa programu katika Google Play.
  • Programu zinazobadilisha klipu za maudhui ili kuiga matangazo ya habari.

    (1) Programu hii hutoa utendaji wa kubadilisha klipu za maudhui ili kuiga matangazo ya habari na kuweka watu maarufu kwenye klipu bila alama maalum.

Uwazi wa Utendaji

Utendaji wa programu yako unapaswa kuwa wazi kwa kiasi kikubwa kwa watumiaji; usijumuishe vipengele vyovyote vilivyofichwa, visivyotumika au visivyoorodheshwa katika programu yako. Mbinu za kukwepa maoni ya watumiaji kuhusu programu haziruhusiwi. Huenda programu zikahitajika kutoa maelezo ya ziada ili kuhakikisha usalama wa watumiaji, uadilifu wa mfumo na utiifu wa sera.

Uwakilishi wa uongo

Haturuhusu programu au akaunti za wasanidi programu ambazo:

  • zinaiga mtu au shirika lolote, au zinazowakilisha kwa njia ya uongo au zinazoficha umiliki au lengo la msingi. 
  • zinahusika katika shughuli zinazolenga kuwapotosha watumiaji. Hii ni pamoja na, lakini si tu, programu au akaunti za wasanidi programu zinazowakilisha kwa uongo au zinazoficha nchi zinakosanidiwa na zinazoelekeza maudhui kwa watumiaji walio katika nchi nyingine.
  • zinashirikiana na programu, tovuti, watoa huduma au akaunti nyingine kuficha au kuwakilisha utambulisho wa programu au msanidi programu kwa njia ya uongo au maelezo mengine, ambapo maudhui ya programu yanahusiana na siasa, masuala ya kijamii au mambo yanayohusiana na umma.

Sera ya Google Play ya kiwango lengwa cha API

Ili kuwapa watumiaji ulinzi na hali salama ya utumiaji, Google Play inahitaji viwango lengwa vya API vifuatavyo kwa programu zote:

Programu mpya na masasisho ya programu LAZIMA yalenge Kiwango cha API ya Android katika mwaka mmoja wa toleo kuu la mfumo wa uendeshaji wa Android wa hivi karibuni. Programu mpya na masasisho ya programu ambayo yameshindwa kutimiza masharti haya yatazuiwa kuwasilisha programu kwenye Dashibodi ya Google Play.

Programu zilizopo za Google Play ambazo hazijasasishwa na zisizolenga Kiwango cha API katika miaka miwili ya toleo kuu la Android la hivi karibuni, hazitapatikana kwa watumiaji wapya wenye vifaa vinavyotumia matoleo mapya zaidi ya mfumo wa uendeshaji wa Android. Watumiaji ambao walisakinisha programu hapo awali kutoka Google Play wataendelea kuwa na uwezo wa kugundua, kusakinisha upya na kutumia programu kwenye toleo lolote la mfumo wa uendeshaji wa Android ambao programu hiyo itakubali.

Ili upate ushauri wa kiufundi kuhusu jinsi ya kutimiza masharti ya kiwango lengwa cha API, tafadhali soma mwongozo wa uhamishaji

Ili upate rekodi halisi ya maeneo uliyotembelea na hali zisizofuata kanuni, tafadhali rejelea makala haya ya Kituo cha Usaidizi.

Masharti ya SDK

Mara nyingi wasanidi programu hutegemea msimbo wa washirika wengine (kwa mfano, SDK) ili kuunganisha huduma na utendaji wa msingi katika programu zao. Unapojumuisha SDK kwenye programu yako, unakusudia kuhakikisha kuwa unawalinda watumiaji wako na programu yako inakuwa salama dhidi ya athari zozote za kiusalama. Katika sehemu hii, tunafafanua jinsi baadhi ya masharti yetu yaliyopo ya faragha na usalama yanavyotumika kwenye muktadha wa SDK na yanavyobuniwa ili kuwasaidia wasanidi programu kuunganisha kwa usalama SDK kwenye programu zao.

Ukijumuisha SDK kwenye programu yako, una wajibu wa kuhakikisha kuwa msimbo wa washirika wao wengine na kanuni zake hazisababishi programu yako ikiuke Sera za Mpango wa Wasanidi Programu wa Google Play. Ni muhimu kufahamu jinsi SDK zilizojumuishwa kwenye programu yako zinavyoshughulikia data ya mtumiaji na kuhakikisha unafahamu ruhusa ambazo zinatumia, data zinazokusanya na sababu ya kukusanya.  Kumbuka kwamba, ukusanyaji na ushughulikiaji wa data ya mtumiaji unaofanywa na SDK lazima uendane na matumizi ya data yaliyobainishwa yanayotii sera ya programu yako.

Ili kusaidia kuhakikisha matumizi yako ya SDK hayakiuki masharti ya sera, soma na uelewe sera zifuatazo kwa ukamilifu wake na uzingatie baadhi ya masharti yake yaliyopo kuhusiana na SDK zilizo hapa chini:

Sera ya Data ya Mtumiaji

Ni lazima uwe muwazi kuhusu jinsi unavyoshghulikia data ya watumiaji (kwa mfano, maelezo yanayokusanywa kutoka kwa mtumiaji au kuhusu mtumiaji ikiwa ni pamoja na maelezo ya kifaa). Hali hiyo inamaanisha kufumbua uwezo wa kufikia, kukusanya, kutumia, kushughulikia na kushiriki data ya mtumiaji kutoka kwenye programu yako pamoja na kudhibiti matumizi ya data kwa madhumuni ya kutii sera yaliyofumbuliwa.

Ikiwa unajumuisha msimbo wa washirika wengine (kwa mfano, SDK) kwenye programu yako, ni lazima uhakikishe kuwa msimbo wa washirika wengine unaotumika kwenye programu yako na kanuni za washirika wengine zinazohusiana na data ya mtumiaji kwenye programu yako, zinatii Sera za Mpango wa Wasanidi Programu wa Google Play, ambazo zinajumuisha matumizi na masharti ya ufumbuzi. Kwa mfano, ni lazima uhakikishe kwamba watoa huduma wako wa SDK hawauzi data binafsi au nyeti ya mtumiaji kutoka kwenye programu yako. Masharti haya yanatumika bila kuzingatia iwapo data ya mtumiaji inahamishwa baada ya kutumwa kwenye seva au kwa kupachika msimbo wa washirika wengine katika programu yako.

Data Nyeti na Binafsi ya Mtumiaji

  • Dhibiti jinsi ya unavyoifikia, kuikusanya, kuitumia na kushiriki data nyeti na binafsi ya mtumiaji inayopatikana kupitia utendaji wa programu na huduma pamoja na madhumuni ya utii wa sera yanayotarajiwa na mtumiaji:
    • Programu zinazoendeleza matumizi ya data nyeti na binafsi ya mtumiaji kwa lengo la kuonyesha matangazo lazima zitii Sera ya Matangazo ya Google Play.
  • Shughulikia kwa usalama data yote ya mtumiaji ambayo ni nyeti na ya binafsi, ikiwa ni pamoja na kuituma kupitia usimbaji fiche wa kisasa (kwa mfano, kupitia HTTPS).
  • Tumia ombi la ruhusa za programu zinapotumika zinapopatikana, kabla ya kufikia data inayodhibitiwa na ruhusa za Android.

Uuzaji wa Data Nyeti na Binafsi ya Mtumiaji

Usiuze data nyeti na binafsi ya mtumiaji.

  • "Uuzaji" unamaanisha kubadilishana au kuhamisha data nyeti na binafsi ya mtumiaji kwenda kwa mshirika mwingine kwa kusudi la kupata pesa.
    • Uhamisho wa data binafsi na nyeti unaoanzishwa na mtumiaji (kwa mfano, mtumiaji anapotumia kipengele cha programu kuhamisha faili kwenda kwa washirika wengine au mtumiaji anapochagua kutumia programu mahususi ya utafiti), hakuchukuliwi kuwa ni uuzaji.

Masharti ya Ufumbuzi Dhahiri na Idhini

Katika hali ambapo uwezo wa programu yako kufikia, kukusanya, kutumia au kushiriki data nyeti na binafsi ya mtumiaji huenda usiwe ndani ya matarajio husika ya mtumiaji wa bidhaa au kipengele mahususi, lazima utimize masharti ya idhini na ufumbuzi dhahiri ya Sera ya Data ya Mtumiaji.

Iwapo programu yako itajumuisha msimbo wa washirika wengine (kwa mfano, SDK) ambayo imeundwa kwa ajili ya kukusanya data binafsi au nyeti ya mtumiaji kwa chaguomsingi, ni lazima, ndani ya wiki 2 baada ya kupokea ombi kutoka Google Play (au ikiwa ombi la Google Play litatoa muda mrefu zaidi, ndani ya kipindi hicho), utoe ushahidi wa kutosha unaoonyesha kuwa programu yako inatimiza masharti ya Idhini na Ufumbuzi Dhahiri wa sera hii, ikijumuisha jinsi unavyofikia data, kuikusanya, kuitumia au kuishiriki kupitia msimbo wa washirika wengine.

Kumbuka kuhakikisha kuwa matumizi yako ya msimbo wa washirika wengine (kwa mfano, SDK) hayasababishi programu yako ikiuke Sera ya Data ya Mtumiaji.

Rejelea makala haya ya Kituo cha Usaidizi ili upate maelezo zaidi kuhusu Masharti ya Idhini na Ufumbuzi Dhahiri.

Mifano ya ukiukaji unaosababishwa na SDK

  • Programu iliyo na SDK inayokusanya data nyeti na binafsi ya mtumiaji na haishughulikii data hii kwa mujibu wa masharti ya Sera hii ya Data ya Mtumiaji ya ufikiaji, kushughulikia data (ikiwa ni pamoja na kutoruhusu uuzaji) na masharti ya idhini na ufumbuzi dhahiri.
  • Programu inayojumuisha SDK ambayo inakusanya data nyeti na binafsi ya mtumiaji kwa chaguomsingi inayokiuka masharti ya sera hii inayohusu idhini ya mtumiaji na ufumbuzi dhahiri. 
  • Programu iliyo na SDK inayodai kukusanya data nyeti na binafsi ya mtumiaji ikikusudia tu kutoa utendaji wa kupambana na ulaghai na matumizi mabaya ya programu, lakini SDK pia inashiriki data inayokusanya na washirika wengine kwa ajili ya utangazaji au takwimu. 
  • Programu inayojumuisha SDK ambayo inahamisha taarifa za vifurushi ambavyo mtumiaji amesakinisha bila kufuata mwongozo wa ufumbuzi dhahiri na au mwongozo wa sera ya faragha

Masharti ya Ziada ya Ufikiaji wa Data Binafsi na Nyeti

Jedwali lililo hapa chini linaelezea masharti ya shughuli mahususi.

Shughuli  Masharti
Programu yako hukusanya au kuunganisha vitambulishi vya kifaa vinavyoendelea kuwepo (k.m., IMEI, IMSI, Nambari ya Ufuatiliaji ya SIM, n.k.)

Vitambulishi vya vifaa vinavyoendelea kuwepo havipaswi kuunganishwa kwenye data nyingine ya watumiaji ambayo ni ya binafsi na nyeti au vitambulishi vya vifaa vinavyoweza kubadilishwa, isipokuwa kwa madhumuni ya:

  • Huduma za kupiga simu zilizounganishwa na utambulisho wa SIM (k.m., huduma ya kupiga simu kupitia Wi-Fi iliyounganishwa na akaunti ya kampuni inayotoa huduma) na
  • Programu za biashara za kudhibiti vifaa zinazotumia hali ya mmiliki wa kifaa.

Matumizi haya lazima yafumbuliwe kwa njia dhahiri kwa watumiaji jinsi ilivyobainishwa kwenye Sera ya Data ya Watumiaji.

Tafadhali soma nyenzo hii ili upate vitambulishi maalum mbadala.

Tafadhali soma Sera ya matangazo ili upate mwongozo wa ziada kuhusu kitambulisho cha matangazo kwenye vifaa vya Android.
Programu yako inalenga watoto Programu yako inaweza tu kujumuisha SDK zenye uthibitishaji wa kujifanyia ili zitumike katika huduma zinazowalenga watoto. Angalia Mpango wa SDK ya Matangazo ya Familia yenye Uthibitishaji wa Kujifanyia ili uone lugha na masharti yote ya sera. 

 

Mifano ya ukiukaji unaosababishwa na SDK

  • Programu inayotumia SDK ambayo inaunganisha Kitambulisho cha Android na Data ya Mahali 
  • Programu yenye SDK inayounganisha AAID kwenye vitambulishi vya kifaa vinavyoendelea kuwepo kwa lengo lolote la utangazaji au takwimu. 
  • Programu inayotumia SDK inayounganisha AAID na anwani ya barua pepe kwa madhumuni ya kutoa takwimu.

Sehemu ya usalama wa Data

Wasanidi programu wote lazima wakamilishe kujaza kwa uwazi na usahihi sehemu ya Usalama wa data ya kila programu kwa kutoa ufafanuzi kuhusu ukusanyaji, matumizi na kushiriki data ya mtumiaji. Hii ni pamoja na data inayokusanywa na kushughulikiwa kupitia maktaba au SDK zozote za washirika wengine zinazotumiwa katika programu zao. Msanidi programu anawajibikia usahihi wa lebo na kusasisha maelezo haya. Panapofaa, ni lazima sehemu hiyo ilingane na ufumbuzi uliofanywa kwenye sera ya faragha ya programu.

Tafadhali rejelea makala haya ya Kituo cha Usaidizi ili upate maelezo zaidi kuhusu kukamilisha Sehemu ya usalama wa data.

Angalia Sera yote ya Data ya mtumiaji.

Sera ya Ruhusa na API Zinazofikia Maelezo Nyeti

Maombi ya ruhusa na API zinazofikia maelezo nyeti lazima yawe bayana kwa mtumiaji. Unapaswa tu kuomba ruhusa na API zinazofikia maelezo nyeti zinazohitajika kutekeleza vipengele au huduma za sasa katika programu yako ambazo umezitangaza kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play. Hupaswi kutumia ruhusa au API zinazofikia maelezo nyeti ambazo zinakupatia ufikiaji wa data ya vifaa au ya mtumiaji kwa madhumuni yasiyofichuliwa, yasiyotekelezwa au vipengele ambavyo havijaruhusiwa. Huruhusiwi kuuza wala kushiriki data binafsi au nyeti inayofikiwa kupitia ruhusa au API zinazoweza kufikia maelezo nyeti kwa lengo la kurahisisha uuzaji.

Angalia sera yote ya Ruhusa na API Zinazofikia Taarifa Nyeti.

Mifano ya ukiukaji unaosababishwa na SDK

  • Programu yako inajumuisha SDK ambayo inaomba kufikia data ya mahali katika hali ya chinichini kwa madhumuni yasiyoruhusiwa au yasiyofichuliwa. 
  • Programu yako inajumuisha SDK ambayo inahamisha IMEI iliyotolewa kwenye ruhusa ya Android ya read_phone_state bila idhini ya mtumiaji.

Sera ya Programu Hasidi

Sera yetu ya programu hasidi ni rahisi, inabainisha kuwa mfumo wa Android, ikiwa ni pamoja na Duka la Google Play na vifaa vya watumiaji, havifai kuwa na shughuli za kihasidi (yaani, programu hasidi). Kupitia kanuni hii kuu, tunajitahidi kuwapatia mfumo salama wa Android watumiaji wetu na vifaa vyao vya Android.

Programu hasidi ni msimbo wowote unaoweza kuhatarisha mtumiaji, data ya mtumiaji au kifaa. Programu hasidi ni pamoja na, lakini si tu, Programu Zinazoweza Kudhuru (PHA), mfumo wa jozi au ubadilishaji wa mifumo, zikiwemo aina kama vile programu za Trojan, za wizi wa data binafsi na za vidadisi, tunaendelea kusasisha na kuweka aina mpya.

Angalia Sera yote ya programu hasidi.

Mifano ya ukiukaji unaosababishwa na SDK

  • Programu inayokiuka miundo ya ruhusa za Android au inayoiba vitambulisho (kama vile tokeni za OAuth) kwenye programu zingine.
  • Programu zinazotumia vibaya vipengele ili kuzizuia zisiondolewe au kukomeshwa.
  • Programu inayozima SELinux.
  • Programu yako inajumuisha SDK ambayo inakiuka muundo wa ruhusa za Android kwa kupata ufikiaji maalum kupitia ufikiaji wa data ya kifaa kwa dhumuni lisilofichuliwa
  • Programu yako inajumuisha SDK iliyo na msimbo ambao unawalaghai watumiaji wajisajili au wanunue maudhui kupitia malipo ya simu zao za mkononi.

Programu za kutoa ruhusa maalum zinazozibua vifaa bila ruhusa ya mtumiaji zinaainishwa kuwa programu zenye idhini maalum ya kudhibiti.

Sera ya Programu za Simu Zisizotakikana

Utendaji na ufumbuzi dhahiri

Misimbo yote inapaswa kutenda ilivyowaahidi watumiaji. Programu zinapaswa kutekeleza utendaji wote unaotajwa. Programu hazipaswi kuwachanganya watumiaji. 

Mifano ya ukiukaji:

  • Ulaghai wa matangazo
  • Kuhadaa Watu

Kulinda data ya watumiaji

Kuwa wazi kuhusu matukio ya ufikiaji, matumizi, ukusanyaji na kushiriki data nyeti na binafsi ya mtumiaji. Matumizi ya data ya mtumiaji ni lazima yatii Sera zote husika za Data ya Mtumiaji, zinapotumika na uchukue tahadhari zote kulinda data hiyo.

Mifano ya ukiukaji:

  • Ukusanyaji wa Data (linganisha Vidadisi)
  • Matumizi mabaya ya Ruhusa Zinazodhibitiwa

Angalia sera yote ya Programu za Simu Zisizotakikana

Sera ya Matumizi Mabaya ya Vifaa na Mtandao

Haturuhusu programu zinazoingilia, zinazokatiza, zinazoharibu au zinazofikia kwa njia isiyoidhinishwa kifaa cha mtumiaji, vifaa vingine au kompyuta, seva, mitandao, Kusano ya Kusanifu Programu (API) au huduma, ikiwa ni pamoja na, lakini si tu, programu nyingine katika kifaa, huduma yoyote ya Google au mtandao wa mtoa huduma ulioidhinishwa.

Programu au msimbo wa washirika wengine (k.m., SDK) zilizo na lugha zinazotafsiriwa (JavaScript, Python, Lua, n.k.) zinazopakiwa wakati zinatumika (k.m., zisizofungashwa pamoja na programu) hazipaswi kuruhusu ukiukaji wa sera za Google Play unaoweza kutokea.

Haturuhusu msimbo ambao unaleta au kusababisha uwezekano wa kuathiriwa kiusalama. Angalia Mpango wa Kuimarisha Usalama wa Programu ili upate maelezo kuhusu matatizo ya hivi karibuni ya usalama yaliyoripotiwa kwa wasanidi programu.

Angalia sera yote ya Matumizi Mabaya ya Vifaa na Mtandao.

Mifano ya ukiukaji unaosababishwa na SDK

  • Programu ambazo zinaendeleza huduma za seva mbadala kwa washirika wengine zinaweza tu kufanya hivyo katika programu ambapo hilo ndilo dhumuni la msingi kwa watumiaji wa programu.
  • Programu yako inajumuisha SDK ambayo inapakua msimbo unaoweza kutekelezwa, kama vile faili za dex au msimbo wa ndani, kutoka katika chanzo kingine tofauti na Google Play.
  • Programu yako inajumuisha SDK ambayo ina mwonekano wa wavuti ulio na Kiolesura cha JavaScript kinachopakia maudhui ya wavuti yasiyoaminika (k.m., http://URL) au URL zisizothibitishwa zilizopatikana kupitia vyanzo visivyoaminika (k.m., URL zinazopatikana kupitia utaratibu ambao hauaminiki).
  • Programu yako inajumuisha SDK ambayo ina msimbo uliotumika kusasisha APK yake
  • Programu yako inajumuisha SDK ambayo inasababisha athari za kiusalama kwa watumiaji kwa kupakua faili kupitia muunganisho usio salama.
  • Programu yako inatumia SDK ambayo ina msimbo wa kupakua au kusakinisha programu kutoka vyanzo visivyojulikana nje ya Google Play.

Sera ya Tabia Danganyifu

Haturuhusu programu zinazojaribu kuwadanganya watumiaji au kuruhusu tabia danganyifu ikiwa ni pamoja na, lakini si tu kwa programu zilizobainishwa kuwa haziwezi kufanya kazi. Ni lazima programu itoe ufumbuzi, maelezo na picha au video sahihi ya utendaji wake kwenye sehemu zote za metadata. Programu hazipaswi kujaribu kuiga utendaji au maonyo kutoka mifumo ya uendeshaji au programu zingine. Ni lazima mabadiliko yoyote ya mipangilio ya kifaa yafanywe baada ya kupata idhini ya mtumiaji na yawe rahisi kutenduliwa na mtumiaji.

Angalia Sera kamili ya Tabia Danganyifu.

Uwazi wa Tabia

Utendaji wa programu yako unapaswa kuwa wazi kwa kiasi kikubwa kwa watumiaji; usijumuishe vipengele vyovyote vilivyofichwa, visivyotumika au visivyoorodheshwa katika programu yako. Mbinu za kukwepa maoni ya watumiaji kuhusu programu haziruhusiwi. Huenda programu zikahitajika kutoa maelezo ya ziada ili kuhakikisha usalama wa watumiaji, uadilifu wa mfumo na utii wa sera.

Mfano wa ukiukaji uliosababishwa na SDK

  • Programu yako inajumuisha SDK inayotumia mbinu za kukwepa maoni ya watumiaji kuhusu programu.

Je, Sera zipi za Wasanidi Programu kwa kawaida zinahusiana na ukiukaji unaosababishwa na SDK?

Ili kukusaidia uhakikishe kuwa msimbo wowote wa washirika wengine unaotumiwa na programu yako unatii Sera za Mpango wa Wasanidi Programu wa Google Play, tafadhali rejelea sera zifuatazo kikamilifu:

Ingawa sera hizi kwa kawaida zinatumika katika suala husika, ni muhimu kukumbuka kwamba msimbo wa SDK wenye hitilafu unaweza kusababisha programu yako ikiuke sera tofauti ambayo haijarejelewa hapo juu. Kumbuka kukagua na kufahamu sera zote kwa ukamilifu wake kwa kuwa ni wajibu wako ukiwa msanidi programu kuhakikisha SDK zako zinashughulikia data ya programu yako katika hali inayotii sera.

Ili upate maelezo zaidi, tafadhali tembelea Kituo chetu cha Usaidizi.


Programu hasidi

Sera yetu ya programu hasidi ni rahisi. Inabaini kuwa mfumo wa Android, ikiwa ni pamoja na Duka la Google Play na vifaa vya watumiaji, havifai kuwa na shughuli za kihasidi (yaani programu hasidi). Kupitia kanuni hii kuu, tunajitahidi kutoa mfumo salama wa Android kwa watumiaji wetu na vifaa vyao vya Android.

Programu hasidi ni msimbo wowote unaoweza kuhatarisha mtumiaji, data ya mtumiaji au kifaa. Programu hasidi ni pamoja na Programu Zinazoweza Kudhuru (PHA), mfumo wa jozi au ubadilishaji wa mifumo, zikiwemo aina kama vile programu za Trojan, za wizi wa data binafsi na za vidadisi na tunaendelea kusasisha na kuweka aina mpya.

Ingawa programu hasidi hutofautiana katika uwezo na aina, kwa kawaida zina mojawapo ya malengo yafuatayo:

  • Kuhatarisha ukamilifu wa kifaa cha mtumiaji.
  • Kupata udhibiti wa kifaa cha mtumiaji.
  • Kuruhusu utendaji unaodhibitiwa kwa mbali ili mshambulizi aweze kufikia, kutumia au kukagua kifaa kilichoathiriwa.
  • Kusambaza data ya binafsi au kitambulisho kutoka kwenye kifaa bila ufumbuzi na idhini inayofaa.
  • Kusambaza taka au amri kutoka kwenye kifaa kilichoathiriwa ili kuathiri mitandao na vifaa vingine.
  • Kulaghai watumiaji.

Programu, mfumo wa jozi au ubadilishaji wa mfumo unaweza kuwa hatari, kwa hivyo unaweza kusababisha shughuli za kihasidi, hata kama haukukusudiwa kuwa hatari. Hii ni kwa sababu programu, mifumo ya jozi au ubadilishaji wa mfumo unaweza kufanya kazi kwa namna tofauti kulingana na vipengee mbalimbali. Kwa hivyo, kitu ambacho ni hatari kwa kifaa kimoja cha Android huenda kisihatarishe kifaa kingine cha Android. Kwa mfano, kifaa kinachotumia toleo jipya la Android hakiathiriwi na programu hatari zinazotumia API zilizoacha kutumika katika kutekeleza shughuli za kihasidi lakini kifaa ambacho bado kinatumia toleo la awali zaidi la Android kinaweza kuwa hatarini. Programu, mfumo wa jozi au ubadilishaji wa mfumo huripotiwa kuwa programu hasidi au PHA iwapo inahatarisha kwa uwazi vifaa na watumiaji wote wa Android au baadhi yao.

Aina za programu hasidi zilizo hapa chini, zinaonyesha imani yetu ya msingi kwamba ni sharti watumiaji waelewe jinsi vifaa vyao vinavyotumiwa na wadumishe mfumo salama unaoruhusu uvumbuzi imara na hali ya utumiaji inayoaminika.

Tembelea Google Play Protect ili upate maelezo zaidi.

Matendo fiche

Msimbo unaoruhusu utekelezaji wa shughuli zisizotakikana, zinazoweza kuwa hatari au zinazodhibitiwa kwa mbali kwenye kifaa.

Shughuli hizi zinaweza kuwa matendo ambayo yanaweka programu, mfumo wa jozi au ubadilishaji wa mfumo kwenye mojawapo ya aina nyingine za programu hasidi iwapo zitatekelezwa kiotomatiki. Kwa jumla, matendo fiche ni maelezo ya jinsi shughuli ambayo huenda ni hatari inaweza kutokea kwenye kifaa na hivyo hailingani kabisa na aina kama vile ulaghai wa malipo au vidadisi vya kibiashara. Kwa hivyo, kikundi cha matendo fiche, katika hali fulani, huchukuliwa na Google Play Protect kuwa uwezekano wa kuathiriwa.

Ulaghai wa Malipo

Msimbo ambao humtoza mtumiaji kiotomatiki kwa njia ya ulaghai kimakusudi.

Ulaghai wa malipo ya kifaa cha mkononi hufanyika katika aina tatu - Ulaghai kupitia SMS, Ulaghai kupitia Simu na Ulaghai kupitia Ada.

Ulaghai kupitia SMS
Msimbo ambao huwatoza watumiaji wakituma SMS zinazolipishwa bila idhini yao au hujaribu kubadilisha shughuli zake za SMS kwa kuficha makubaliano ya ufumbuzi au ujumbe wa SMS kutoka kwa mtoa huduma za simu, unaomwarifu mtumiaji kuhusu gharama au kuthibitisha usajili.

Baadhi ya misimbo, hata kama hufichua kiufundi tabia za kutuma SMS, huanzisha tabia nyingine ambazo huruhusu ulaghai kupitia SMS. Mifano ni pamoja na kuficha sehemu za makubaliano ya ufumbuzi kutoka kwa mtumiaji, kuzifanya zisiweze kusomeka na kuzuia ujumbe wa SMS kwa njia ya masharti kutoka kwa mtoa huduma za simu, unaomfahamisha mtumiaji kuhusu gharama au kuthibitisha usajili.

Ulaghai kupitia Simu
Msimbo ambao huwatoza watumiaji kwa kupiga simu kwa nambari zinazolipishwa bila idhini ya mtumiaji.

Ulaghai kupitia Ada
Msimbo ambao huwalaghai watumiaji wajisajili au wanunue maudhui kupitia malipo ya simu zao za mkononi.

Ulaghai kupitia Ada hujumuisha aina yoyote ya malipo isipokuwa SMS na simu zinazolipishwa. Mifano ya ulaghai huu ni pamoja na malipo ya moja kwa moja kupitia mtoa huduma wa simu, mlango wa mtandao usiotumia waya (WAP) na uhamishaji wa salio la kupiga simu katika kifaa cha mkononi. Ulaghai wa WAP ni mojawapo ya aina maarufu za Ulaghai kupitia Ada. Ulaghai wa WAP unaweza kujumuisha hatua ya kuwalaghai watumiaji wabofye kitufe kwenye Mwonekano wa Wavuti unaoonekana ambao ulipakiwa kwa siri. Baada ya kutekeleza kitendo, usajili unaojirudia huanzishwa na mara nyingi SMS au barua pepe ya uthibitishaji hutekwa ili kuwazuia watumiaji wasitambue muamala wa kifedha.

Programu za kudadisi

Msimbo unaokusanya data nyeti au binafsi ya mtumiaji kutoka kwenye kifaa kisha kutuma data hiyo kwa mshirika mwingine (biashara au mtu mwingine) kwa madhumuni ya ufuatiliaji.

Ni lazima programu zitoe ufumbuzi dhahiri wa kutosha na zipate idhini kama inavyotakiwa kwa mujibu wa Sera ya Data ya Mtumiaji.

Mwongozo kwa ajili ya Programu za Ufuatiliaji

Programu ambazo zimebuniwa na kutangazwa mahususi kwa ajili ya kufuatilia mtu mwingine, kwa mfano wazazi kufuatilia watoto wao au udhibiti wa kibiashara kwa ajili ya ufuatiliaji wa wafanyakazi, ndiyo programu pekee za ufuatiliaji zitakazokubalika, ilimradi programu hizo zinatii masharti yaliyofafanuliwa hapa chini. Programu hizi hazipaswi kutumiwa kufuatilia mtu yeyote mwingine (kwa mfano, mume au mke) hata kama akijua na kukuruhusu, bila kujali iwapo arifa ya kudumu inaonyeshwa. Ni lazima programu hizi zitumie kitia alama cha metadata cha IsMonitoringTool kwenye faili ya maelezo ili ziweze kujibainisha inavyofaa kuwa programu za ufuatiliaji.

Programu za ufuatiliaji zinapaswa kutii masharti yafuatayo:

  • Programu hazipaswi kuwasilishwa kama suluhisho la upelelezi au uchunguzi wa siri.
  • Lazima programu zisijifiche au kuficha utendaji wa kufuatilia au kujaribu kupotosha watumiaji kuhusu utendaji kama huo.
  • Lazima programu ziweke arifa ya kudumu wakati wote programu inapotumika na ziwe na aikoni ya kipekee inayotambulisha programu kwa uwazi.
  • Lazima programu zifumbue utendaji wa ufuatiliaji kwenye maelezo ya Duka la Google Play.
  • Programu na kurasa za programu katika Google Play hazipaswi kujumuisha njia zozote za kuwasha au kufikia utendaji ambao unakiuka sheria na masharti haya, kama vile kuunganisha kwenye APK isiyoruhusiwa, ambayo imepangishwa nje ya Google Play.
  • Programu zinapaswa kutii sheria zozote zinazotumika. Unawajibika kibinafsi kubaini uhalali wa programu yako kulingana na mahali inapolengwa kwenda kutumika.
Tafadhali rejelea makala ya Matumizi ya Kitia alama cha isMonitoringTool ya Kituo cha Usaidizi ili upate maelezo zaidi.

Kuzuiwa kwa Huduma (DoS)

Msimbo ambao, bila ufahamu wa mtumiaji, hutekeleza shambulizi la kuzuiwa kwa huduma (DoS) au ni sehemu ya shambulizi linalosambazwa la DoS dhidi ya mifumo na nyenzo nyingine.

Kwa mfano, hali hii inaweza kutokea kwa kutuma kiwango cha juu cha maombi ya HTTP ili kusababisha kazi zaidi kwenye seva za mbali.

Vipakuaji Hatari

Msimbo ambao si hatari, lakini hupakua PHA nyingine.

Msimbo unaweza kuwa kipakuaji hatari iwapo:

  • Kuna sababu ya kuaminika kuwa ulitengenezwa kusambaza PHA na umepakua PHA au una msimbo ambao unaweza kupakua na kusakinisha programu; au
  • Angalau asilimia tano ya programu zilizopakuliwa na msimbo huo ni PHA, kutokana na angalau programu 500 zilizopakuliwa ambazo zilichunguzwa (programu 25 zilizopakuliwa zilikuwa za PHA).

Programu za kushiriki faili na vivinjari vikuu havichukuliwi kuwa vipakuaji hatari mradi:

  • Hazisababishi upakuaji bila kumshirikisha mtumiaji; na
  • Programu zote zinazopakuliwa za PHA zinatokana na idhini ya watumiaji.

Hatari Isiyo ya Android

Msimbo ulio na hatari zisizo za Android.

Programu hizi haziwezi kusababisha madhara kwa kifaa au mtumiaji wa Android, lakini zina vipengele ambavyo vinaweza kuwa hatari kwa mifumo mingine.

Wizi wa data ya binafsi

Msimbo unaojifanya kutoka kwenye chanzo kinachoaminika, huomba kitambulisho cha uthibitishaji cha mtumiaji au maelezo ya kulipa na kutuma data hiyo kwa wengine. Aina hii pia hutumika kwa msimbo ambao huingilia usambazaji wa kitambulisho cha mtumiaji kinapotumwa.

Kwa kawaida, wizi wa data binafsi hulenga vitambulisho vya benki, nambari za kadi za mikopo na vitambulisho vya akaunti za mtandaoni za michezo na mitandao jamii.

Matumizi Mabaya ya Haki Maalum

Msimbo unaoathiri kuaminika kwa mfumo kwa kuingia katika programu ya sehemu ya majaribio, kupata haki za kipekee au kubadilisha au kuzima uwezo wa kufikia vipengele vinavyohusiana na usalama wa msingi.

Mifano ni kama:

  • Programu inayokiuka miundo ya ruhusa za Android au inayoiba vitambulisho (kama vile tokeni za OAuth) kwenye programu nyingine.
  • Programu zinazotumia vibaya vipengele ili kuzizuia zisiondolewe au kukomeshwa.
  • Programu inayozima SELinux.

Programu za kutoa haki maalum zinazozimbua vifaa bila ruhusa ya mtumiaji zinaainishwa kuwa programu kudhibiti.

Programu za kudai kikombozi

Msimbo unaochukua udhibiti kiasi au kamili wa kifaa au data iliyo kwenye kifaa na kumtaka mtumiaji kulipa au kutekeleza kitendo fulani ili kutoa udhibiti.

Baadhi ya programu za kudai kikombozi husimba data iliyo kwenye kifaa kwa njia fiche na kudai malipo ili kusimbua data na/au kuzuia vipengele vya msimamizi wa kifaa ili isiondolewe na mtumiaji wa kawaida. Mifano ni kama:

  • Kumfungia mtumiaji nje ya kifaa chake na kudai pesa ili kurejesha udhibiti wa mtumiaji.
  • Kusimba kwa njia fiche data kwenye kifaa na kudai malipo, ili kusimbua data ile.
  • Kuweka vipengele vya udhibiti wa sera za kifaa na kuzuia uwezo wa kuondolewa na mtumiaji.

Msimbo unaosambazwa na kifaa ambao lengo lake la msingi ni udhibiti wa kifaa uliopunguzwa unaweza kutengwa kwenye kikundi cha programu za kudai kombozi mradi zinatimiza masharti ya udhibiti na kufunga kwa usalama na masharti ya ufumbuzi na idhini kamili ya mtumiaji.

Kufikia faili za mfumo

Msimbo ambao hudhibiti kifaa.

Kuna tofauti kati ya msimbo hasidi na msimbo usio hasidi ambao hudhibiti. Kwa mfano, programu zisizo hasidi ambazo hudhibiti humruhusu mtumiaji afahamu mapema kuwa huwa zitadhibiti kifaa na hazitekelezi vitendo vingine vinavyoweza kuwa na madhara, ambavyo vinatumika katika aina nyingine za PHA.

Programu hasidi ambazo hudhibiti hazimfahamishi mtumiaji kuwa zitadhibiti kifaa au humfahamisha mtumiaji mapema kuhusu kudhibiti lakini pia hutekeleza vitendo vingine ambavyo vinatumika katika aina nyingine za PHA.

Taka

Msimbo unaotuma ujumbe ambao mtumiaji hajaomba atumiwe kwenye anwani yake au unaotumia kifaa kutuma barua taka.

Vidadisi

Vidadisi ni mienendo, misimbo au programu hasidi zinazokusanya, kuondoa au kutuma data ya mtumiaji au ya kifaa isiyohusiana na utendaji wa kutii sera.

Mienendo au misimbo hasidi inayoweza kuzingatiwa kuwa ya kumdadisi mtumiaji au kuondoa data bila ilani au idhini inayofaa pia huchukuliwa kuwa vidadisi.

Kwa mfano, ukiukaji wa vidadisi ni pamoja na, lakini si tu:

  • Kurekodi sauti au kurekodi simu zinazopigwa
  • Kuiba data ya programu
  • Programu iliyo na msimbo hasidi wa wengine (kwa mfano, SDK) unaotuma data kutoka kwenye kifaa kwa njia ambayo mtumiaji hakutarajia na/au bila ilani au idhini inayofaa.

Ni lazima programu zote zitii Sera zote za Mpango wa Wasanidi Programu wa Google Play, ikiwa ni pamoja na sera za data ya mtumiaji na ya kifaa kama vile Programu za Simu Zisizotakikana, Data ya Mtumiaji, Ruhusa na API Zinazofikia Taarifa Nyeti na Masharti ya SDK.

Trojan

Msimbo unaoonekana kufaa, kama vile mchezo unaodai kuwa mchezo, lakini unatekeleza matendo yasiyotarajiwa dhidi ya mtumiaji.

Uainishaji huu kwa kawaida hutumiwa na mkusanyiko wa aina nyingine za PHA. Trojan ina kipengele kisicho na madhara na kipengele hatari kilichofichwa. Kwa mfano, mchezo unaotuma ujumbe wa SMS unaolipiwa kutoka kwenye kifaa cha mtumiaji chinichini na bila mtumiaji kujua.

Dokezo la Programu Zisizo za Kawaida

Programu mpya na nadra zinaweza kuainishwa kuwa zisizo za kawaida iwapo Google Play Protect haina maelezo ya kutosha kuidhinishwa kuwa salama. Hii haimaanishi kuwa programu ni hatari, lakini bila ukaguzi zaidi haiwezi kuidhinishwa kuwa salama.

Kidokezo kuhusu Aina ya Matendo Fiche

Uainishaji wa kundi la programu hasidi ya matendo fiche hutegemea jinsi msimbo unavyotenda. Masharti muhimu ya msimbo wowote kuainishwa kuwa tendo fiche ni kuwa unaruhusu matendo ambayo yataweka msimbo huo kwenye mojawapo ya aina za programu hasidi unapotekelezwa kiotomatiki. Kwa mfano, iwapo programu inaruhusu upakiaji unaobadilika wa msimbo na msimbo uliopakiwa unatoa SMS, itaainishwa kuwa programu hasidi yenye matendo fiche.

Hata hivyo, iwapo programu inaruhusu utekelezaji wa jumla wa msimbo na hatuna sababu zozote za kuamini kuwa utekelezaji huu wa msimbo uliwekwa kutekeleza shughuli za kihasidi, basi programu itachukuliwa kuwa inaweza kuathiri wala si programu hasidi yenye matendo fiche na msanidi programu ataombwa airekebishe.

Programu fichamizi

Programu inayotumia mbinu mbalimbali za ukwepaji ili kumpa mtumiaji utendaji tofauti au bandia wa programu. Programu hizi hujibainisha kama programu au michezo halali ili zisionekane kuwa hatari kwenye maduka ya programu na hutumia mbinu kama vile ufumbaji wa msimbo, upakiaji wa msimbo unaobadilika au uwasilishaji wa maudhui tofauti kwa watu na mitambo ya kutambaa ili kuonyesha maudhui hasidi.

Programu hasidi za ufichaji ni sawa na aina nyingine za PHA, hasa programu hasidi ya Trojan, tofauti kuu ikiwa ni mbinu zinazotumiwa kufumba msimbo wa shughuli hasidi.


Uigaji

Haturuhusu programu zinazopotosha watumiaji kwa kuiga mtu mwingine (k.m. msanidi programu,  kampuni, shirika jingine) au programu nyingine.  Usidai kuwa programu yako inahusiana au imeidhinishwa na mtu, ilhali si kweli.  Kuwa makini usitumie aikoni, maelezo, mada au vipengele vya ndani ya programu ambavyo vinaweza kuwapotosha watumiaji kuhusu uhusiano wa programu yako na mtu au programu nyingine.
 
Ili kudumisha usalama na heshima kwenye mfumo wa Google Play, tumebuni viwango vinavyobainisha na kuzuia maudhui ambayo hayafai au yanayodhuru watumiaji wetu.
  • Wasanidi programu ambao wanadai kuwa na uhusiano na kampuni, msanidi programu, huluki au shirika jingine kwa njia ya uongo.

    ① Jina la msanidi programu lililoorodheshwa kwenye programu hii linaonyesha uhusiano rasmi na Google, ingawa uhusiano kama huo haupo.

  • Programu ambazo aikoni na majina yazo huashiria uhusiano na kampuni, msanidi programu, huluki au shirika jingine kwa njia ya uongo.

    ①Programu inatumia nembo ya kitaifa na kupotosha watumiaji waamini kwamba ina uhusiano na serikali.
    ②Programu inaiga nembo ya huluki ya biashara kuashiria kwa njia ya uongo kuwa ni programu rasmi ya kampuni husika.

  • Majina na aikoni za programu zinazofanana kwa ukaribu na zile za bidhaa au huduma zilizopo kiasi kwamba watumiaji wanaweza kupotoshwa.


    ①Programu inatumia nembo ya tovuti maarufu ya sarafu ya dijitali katika aikoni yake ili iashirie kwamba yenyewe ndiyo tovuti rasmi.
    ②Programu inaiga mhusika au jina la kipindi maarufu cha televisheni katika aikoni yake na kupotosha watumiaji kudhani kwamba ina uhusiano na kipindi cha televisheni.

  • Programu zinazodanganya kuwa ni programu rasmi za huluki inayotambulika. Majina kama "Programu Rasmi ya Justin Bieber" hayaruhusiwi bila ruhusa au haki zinazohitajika.

  • Programu zinazokiuka Mwongozo wa Biashara wa Android.

Mobile Unwanted Software

Hapa Google, tunaamini kuwa tukimzingatia mtumiaji, mengine yote yatatekelezwa. Katika Kanuni zetu za Programu na Sera ya Programu Isiyotakikana, tunatoa mapendekezo ya jumla kuhusu programu inayotoa hali bora ya utumiaji. Sera hii hutokana na Sera ya Google ya Programu Isiyotakikana kwa kubainisha kanuni za mfumo wa Android na Duka la Google Play. Programu inayokiuka kanuni hizi inaweza kuwa hatari kwa hali ya utumiaji na tutachukua hatua kulinda watumiaji dhidi yake.

Kama ilivyotajwa kwenye Sera ya Programu Isiyotakikana, tumegundua kuwa programu nyingi zisizotakikana huonyesha sifa moja au zaidi za msingi zinazofanana:

  • Ni ya kupotosha, inaahidi uboreshaji wa thamani ambao haiwezi kutekeleza.
  • Hujaribu kuwalaghai watumiaji kuisakinisha au hujificha katika programu nyingine ya kusakinishwa.
  • Haimfahamishi mtumiaji kuhusu kanuni na utendaji wake.
  • Huathiri mfumo wa mtumiaji kwa njia zisizotarajiwa.
  • Hukusanya au kutuma maelezo ya faragha bila kumfahamisha mtumiaji.
  • Hukusanya au kutuma maelezo ya faragha bila kushughulikiwa kiusalama (k.m. kutuma kupitia HTTPS)
  • Huunganishwa na programu nyingine na uwepo wake haufumbuliwi.

Kwenye vifaa vya mkononi, programu ni msimbo katika muundo wa programu, mfumo wa jozi, ubadilishaji wa mfumo, n.k. Ili kuzuia programu ambayo ni hatari kwa mfumo wa programu au inayokatiza hali ya utumiaji, tutachukua hatua kwa msimbo unaokiuka kanuni hizi.

Hapa chini, tunafafanua Sera ya Programu Isiyotakikana ili kubainisha utendaji wake kwenye programu ya simu. Sawa na ilivyo kwenye sera hiyo, tutaendelea kuboresha sera hii ya Programu Isiyotakikana ya Simu ili kushughulikia aina mpya za matukio ya matumizi mabaya.

Utendaji na ufumbuzi wazi

Misimbo yote inapaswa kutenda ilivyowaahidi watumiaji. Programu zinapaswa kutekeleza utendaji wote unaotajwa. Programu hazipaswi kuwachanganya watumiaji. 

  • Programu zinapaswa kuwa wazi kuhusu utendaji na malengo.
  • Kwa njia dhahiri na wazi, elezea mtumiaji mabadiliko kwenye mfumo yatakayosababishwa na programu. Waruhusu watumiaji kukagua na kuidhinisha chaguo na mabadiliko yote ya usakinishaji. 
  • Programu hazipaswi kuwakilisha kwa njia ya uongo hali ya kifaa cha mtumiaji, kwa mfano kudai kuwa mfumo uko katika hali hatari ya usalama au umeathiriwa na virusi.
  • Usitumie shughuli zisizo sahihi zilizobuniwa ili kuongeza watazamaji wa tangazo na/au walioshawishika.
  • Haturuhusu programu ambazo huwapotosha watumiaji kwa kuiga mtu mwingine (k.m. msanidi programu, kampuni, shirika jingine) au programu nyingine. Usidokeze kuwa programu yako inahusiana au imeidhinishwa na mtu, ilhali si kweli.

Mifano ya ukiukaji:

  • Ulaghai wa matangazo
  • Kuhadaa Watu

Kulinda data na faragha ya mtumiaji

Toa maelezo bayana kuhusu ufikiaji, matumizi, ukusanyaji na utumaji wa data nyeti na binafsi ya mtumiaji. Matumizi ya data ya mtumiaji ni lazima yatii sera zote husika za Data ya Mtumiaji, zinapotumika na yatilie maanani tahadhari zote za kulinda data hiyo.

  • Wape watumiaji fursa ya kukubali ukusanyaji wa data yao kabla ya kuanza kukusanya na kuituma kutoka kwenye kifaa, ikiwa ni pamoja na data kuhusu akaunti za wengine, barua pepe, namba ya simu, programu zilizowekwa kwenye vifaa, faili, data ya mahali na data nyingine yoyote nyeti na ya binafsi ambayo mtumiaji hatarajii ikusanywe.
  • Data nyeti na ya binafsi ya mtumiaji inayokusanywa inapaswa kushughulikiwa kwa njia salama, ikiwa ni pamoja na kutumwa kupitia usimbaji fiche wa kisasa (kwa mfano, kupitia HTTPS).
  • Ni lazima programu, ikiwa ni pamoja na programu za vifaa vya mkononi, zitume tu data nyeti na ya binafsi ya mtumiaji kwenye seva jinsi inavyohusiana na utendaji wa programu.
  • Usiwaombe au kuwadanganya watumiaji wazime vipengele vya ulinzi wa usalama wa kifaa kama vile Google Play Protect. Kwa mfano, hupaswi kutoa zawadi au vipengele vya ziada vya programu kwa watumiaji ili wazime Google Play Protect.

Mifano ya ukiukaji:

  • Ukusanyaji Data (linganisha Vidadisi)
  • Matumizi mabaya ya Ruhusa Zinazodhibitiwa

Mifano ya sera za Data ya Mtumiaji:

Usidhuru hali ya utumiaji wa vifaa vya mkononi 

Hali ya utumiaji inapaswa kuwa dhahiri, rahisi kueleweka na kulingana na chaguo zinazofanywa na mtumiaji. Inapaswa kuwasilisha kwa njia ya uwazi uboreshaji wa thamani kwa mtumiaji na isikatize hali ya utumiaji iliyotangazwa au inayopendelewa.

  • Usionyeshe matangazo yanayoonyeshwa kwa watumiaji kwa njia zisizotarajiwa, ikiwemo kuathiri au kuingilia urahisi wa kutumia vipengele vya kifaa, au kuonyesha nje ya mazingira ya programu bila kuweza kuondolewa kwa urahisi wala maelezo na idhini ya kutosha.
  • Programu hazipaswi kuingilia programu nyingine au kuathiri urahisi wa kutumia kifaa
  • Tukio la kuondoa programu, panapohitajika, linapaswa kuwa wazi. 
  • Programu ya kifaa cha mkononi haipaswi kuiga vidokezo kutoka mfumo wa uendeshaji wa kifaa au programu nyingine. Usizuie arifa za mtumiaji kutoka programu nyingine au mfumo wa uendeshaji, hasa zinazomfahamisha mtumiaji kuhusu mabadiliko katika mfumo wake wa uendeshaji. 

Mifano ya ukiukaji:

  • Matangazo yanayokatiza mtumiaji
  • Matumizi Yasiyoidhinishwa au Uigaji wa Mfumo wa Utendaji

Vipakuaji Hatari

Msimbo ambao si programu isiyotakikana, lakini hupakua programu zingine zisizotakikana za vifaa vya mkononi (MUwS).

Msimbo unaweza kuwa kipakuaji hatari iwapo:

  • Kuna sababu ya kuaminika kuwa ulitengenezwa kusambaza MUwS na umepakua MUwS au una msimbo ambao unaweza kupakua na kusakinisha programu; au
  • Angalau asilimia tano ya programu zilizopakuliwa na msimbo huo ni MUwS, kutokana na angalau programu 500 zilizopakuliwa ambazo zilichunguzwa (programu 25 zilizopakuliwa zilikuwa za MUwS).

Programu za kushiriki faili na vivinjari vikuu havichukuliwi kuwa vipakuaji hatari mradi:

  • Hazisababishi upakuaji bila kumshirikisha mtumiaji; na
  • Programu zote zinazopakuliwa zinatokana na idhini ya watumiaji.

Ulaghai wa Matangazo

Ulaghai wa matangazo hauruhusiwi kabisa. Uonyeshaji wa tangazo unaobuniwa kwa madhumuni ya kulaghai kituo cha matangazo kiamini kuwa utazamaji unatokana na watumiaji kuvutiwa ni ulaghai wa tangazo, ambayo ni aina ya utazamaji usio sahihi. Ulaghai wa matangazo unaweza kuwa kizalia cha wasanidi programu wanaotekeleza matangazo kwa njia zisizoruhusiwa, kama vile kuonyesha matangazo yaliyofichwa, kubofya matangazo kiotomatiki, kubadilisha au kurekebisha maelezo na kuweka vitendo visivyo vya kibinadamu (programu za kutambaa, vijibu, n.k.) au shughuli za kibinadamu zilizobuniwa kuonyesha utazamaji wa matangazo usio sahihi. Utazamaji usio sahihi na ulaghai wa matangazo ni hatari kwa watangazaji, wasanidi programu na watumiaji, na husababisha kupoteza imani kwa muda mrefu katika mfumo wa Matangazo kwenye vifaa cha mkononi.
Ili kudumisha usalama na heshima kwenye mfumo wa Google Play, tumebuni viwango vinavyobainisha na kuzuia maudhui ambayo hayafai au yanayodhuru watumiaji wetu.
  • Programu inayoweka matangazo ambayo hayaonekani kwa mtumiaji.
  • Programu inayobuni kiotomatiki mibofyo kwenye matangazo bila nia ya mtumiaji au yanayoweka trafiki sawa ya mtandao ili kupeana mibofyo kwa ulaghai.
  • Programu inayotuma mibofyo bandia ya maelezo ya usakinishaji ili kulipwa kwa usakinishaji ambao haukutoka kwenye mtandao wa mtumaji. 
  • Programu inayochomoza matangazo wakati mtumiaji hayuko karibu na kiolesura cha programu.
  • Uwakilishi wa uongo wa hesabu ya matangazo kwenye programu, k.m. programu ambayo inawasiliana na vituo vya matangazo na kudai kuwa inatekeleza kwenye kifaa cha iOS wakati inatekelezwa kwenye kifaa cha Android, programu ambayo ina jina la uongo la kifurushi ambalo linatumiwa kuchuma mapato.

Matumizi Yasiyoidhinishwa au Uigaji wa Mfumo wa Utendaji

Haturuhusu programu au matangazo yanayoiga au kukatiza utendaji wa mfumo, kama vile arifa au maonyo. Arifa za ngazi ya mfumo zinaweza kutumika kwa vipengele muhimu vya programu pekee, kama vile programu ya ndege inayowaarifu watumiaji kuhusu ofa maalum, au mchezo unaowaarifu watumiaji kuhusu ofa za ndani ya mchezo.

Ili kudumisha usalama na heshima kwenye mfumo wa Google Play, tumebuni viwango vinavyobainisha na kuzuia maudhui ambayo hayafai au yanayodhuru watumiaji wetu.
  • Programu au matangazo yanayowasilishwa kupitia arifa ya mfumo au tahadhari:
    ① Arifa ya mfumo inayoonyeshwa katika programu hii inatumika kuonyesha tangazo.
 

Kwa mifano ya ziada inayohusu matangazo, tafadhali rejelea Sera ya matangazo.

 


Social Engineering

We do not allow apps that pretend to be another app with the intention of deceiving users into performing actions that the user intended for the original trusted app.


Haturuhusu programu zilizo na matangazo yanayopotosha au yanayokatiza mtumiaji. Lazima matangazo yaonyeshwe ndani ya programu inayoyaonyesha. Tunachukulia matangazo yanayoonyeshwa kwenye programu yako kama sehemu ya programu yako. Matangazo yanayoonyeshwa kwenye programu yako ni lazima yatii sera zetu zote. Ili upate sera kuhusu matangazo ya kamari, tafadhali bofya hapa.
Google Play hutumia mbinu mbalimbali za uchumaji mapato ili kunufaisha wasanidi programu na watumiaji, ikiwa ni pamoja na usambazaji unaolipiwa, bidhaa za ndani ya programu, usajili na miundo inayotegemea matangazo. Ili kuboresha hali ya matumizi, tunahitaji utii sera hizi.

Malipo

  1. Sharti wasanidi programu wanaotoza gharama za upakuaji wa programu kwenye Google Play watumie mfumo wa utozaji wa Google Play kama njia ya kulipia miamala hiyo.
  1. Ni lazima programu zinazosambazwa kupitia Google Play zinazohitaji au zinazokubali malipo ili kufikia vipengele au huduma za ndani ya programu, ikiwa ni pamoja na utendaji wowote wa programu, maudhui au bidhaa zozote dijitali (kwa jumla “ununuzi wa ndani ya programu”), zitumie mfumo wa utozaji wa Google Play kwa miamala hiyo isipokuwa Kifungu cha 3, 8 au 9 kitumike.

    Mifano ya vipengele vya programu au huduma zinazohitaji utumiaji wa mfumo wa utozaji wa Google Play ni pamoja na, lakini si tu, ununuzi wa ndani ya programu wa:

    • Vipengee (kama vile sarafu pepe, maisha ya ziada, muda wa ziada wa kucheza, vipengee vya programu jalizi, herufi na ishara);
    • huduma za usajili (kama vile maudhui ya siha, mchezo, kuchumbiana, elimu, muziki, video, uboreshaji wa huduma na huduma zingine za usajili);
    • maudhui au utendaji wa programu (kama vile toleo la programu lisilo na matangazo au vipengele vipya ambavyo havipatikani katika toleo lisilolipishwa); na
    • huduma na programu za wingu (kama vile huduma za kuhifadhi data, programu za tija za biashara na programu za usimamizi wa fedha).
  1. Mfumo wa utozaji wa Google Play haupaswi kutumiwa katika hali ambapo:
    1. malipo yanatumiwa kimsingi kwa:
      • ununuzi au ukodishaji wa bidhaa halisi (kama vile vyakula, mavazi, vifaa vya nyumbani, vifaa vya kielektroniki);
      • ununuzi wa huduma halisi (kama vile huduma za usafiri, usafi, nauli ya ndege, uanachama kwenye ukumbi wa mazoezi, usafirishaji wa chakula, tiketi za matukio ya moja kwa moja); au
      • malipo ya bili za kadi za mikopo au malipo ya utumiaji wa huduma (kama vile huduma za kebo na mawasiliano);
    2. malipo yanajumuisha malipo kupitia programu ya wakala, minada ya mitandaoni na michango isiyotozwa kodi;
    3. malipo ni ya maudhui au huduma zinazowezesha uchezaji kamari mtandaoni, kama ilivyofafanuliwa kwenye sehemu ya Programu za Kamari za sera ya Mashindano, Michezo na Kamari za Pesa Halisi;
    4. malipo yanafanyika kwenye aina yoyote ya bidhaa ambayo haikubaliki chini ya Sera za Maudhui za Kituo cha Malipo kwenye Google.
      Kumbuka: Katika baadhi ya masoko, tunatumia Google Pay kwa programu zinazouza bidhaa halisi na/au huduma. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea Ukurasa wetu wa wasanidi programu kwenye Google Pay.
  1. Mbali na hali zilizofafanuliwa katika Kifungu cha 3, 8 na 9, programu hazipaswi kuwaelekeza watumiaji kwenye njia nyingine ya kulipa isipokuwa mfumo wa utozaji wa Google Play. Marufuku haya ni pamoja na, lakini si tu, kuwaelekeza watumiaji kwenye njia zingine za kulipa kupitia:
    • Maelezo ya ukurasa wa programu katika Google Play;
    • Matangazo ya ndani ya programu yanayohusiana na maudhui yanayoweza kununuliwa;
    • Vitufe, viungo, kutuma ujumbe, matangazo au miito mingine ya kuchukua hatua, mionekano ya wavuti ya ndani ya programu; na
    • Taratibu za kiolesura za ndani ya programu, ikijumuisha kufungua akaunti au taratibu za kujisajili, ambazo huelekeza watumiaji kutoka kwenye programu kwenda kwenye njia ya kulipa kando na mfumo wa utozaji wa Google Play kama sehemu ya taratibu hizo.
  1. Sarafu pepe za ndani ya programu zinapaswa kutumika tu kwenye programu au mchezo ambako zilinunuliwa.

  1. Ni lazima wasanidi programu wawafahamishe watumiaji kwa njia ya wazi na sahihi kuhusu sheria na masharti na bei za programu yao au vipengele vyovyote vya ndani ya programu au usajili unaotolewa kwa ununuzi. Ni lazima bei za ndani ya programu zilingane na bei zilizoonyeshwa kwenye kiolesura cha Malipo kupitia Play kwa watumiaji. Kama maelezo ya bidhaa yako kwenye Google Play yanahusu vipengele vya ndani ya programu ambavyo vinaweza kuhitaji ada maalum au ya ziada, ni lazima maelezo ya programu yako katika Google Play yawaarifu watumiaji wazi kuwa malipo yanahitajika ili kufikia vipengele hivyo.

  1. Michezo na programu zinazotoa mbinu ya kupokea bidhaa pepe za ununuzi kwa unasibu ikiwa ni pamoja na, lakini si tu, “masanduku ya hazina” zinapaswa kufumbua kwa uwazi uwezekano wa kupokea bidhaa kabla ya ununuzi na karibu na wakati wa kununua.

  1. Isipokuwa hali zilizofafanuliwa katika Kifungu cha 3 zitumike, wasanidi wa programu zinazosambazwa kupitia Google Play zinazohitaji au zinazokubali malipo kutoka kwa watumiaji walio kwenye nchi au maeneo haya ili wafikie ununuzi wa ndani ya programu, huenda wakawapa watumiaji mfumo mbadala wa utozaji kwenye programu pamoja na mfumo wa utozaji wa Google Play kwa miamala hiyo iwapo watajaza kikamilifu fomu ya taarifa ya malipo kwa kila mpango husika na wakubali sheria na masharti ya ziada ya mpango yaliyojumuishwa humo.

  1. Huenda wasanidi wa programu zinazosambazwa na Google Play wakawaelekeza watumiaji walio kwenye nchi washirika katika Makubaliano ya Kiuchumi ya Ulaya (EEA) nje ya programu, ikijumuisha kutangaza ofa za vipengele na huduma za kidijitali za ndani ya programu. Wasanidi programu wanaowaelekeza watumiaji wa EEA nje ya programu sharti wajaze kikamilifu fomu ya taarifa ya programu husika na wakubali sheria na masharti ya ziada na masharti ya programu yaliyojumuishwa humo.

Kumbuka: Ili uone rekodi ya maeneo uliyotembelea na maswali yanayoulizwa sana kuhusu sera hii, tafadhali tembelea Kituo chetu cha Usaidizi.

Matangazo

Ili kudumisha hali bora ya utumiaji, tunazingatia maudhui ya tangazo lako, hadhira, hali ya utumiaji, tabia, pamoja na usalama na faragha. Tunazingatia matangazo na ofa husika kama sehemu ya programu yako, lazima pia yafuate sera zingine zote za Google Play. Pia tuna masharti ya ziada kwa matangazo ikiwa unachuma mapato ya programu inayolenga watoto kwenye Google Play.

Unaweza pia kupata maelezo zaidi kuhusu sera zetu za Utangazaji wa Programu na Ukurasa wa Programu katika Google Play hapa, ikiwa ni pamoja na jinsi tunavyoshughulikia mbinu zinazopotosha za utangazaji.

Maudhui ya Tangazo

Matangazo na ofa husika ni sehemu ya programu yako na lazima yafuate sera zetu za Maudhui Yaliyozuiwa. Masharti ya ziada yanatumika ikiwa programu yako ni ya kamari.

Matangazo Yasiyofaa

Matangazo pamoja na ofa zinazohusishwa nayo (kwa mfano, tangazo linaloshawishi mtumiaji kupakua programu nyingine) yanayoonyeshwa ndani ya programu yako yanapaswa kufaa daraja la maudhui la programu yako, hata kama maudhui yenyewe yanatii sera zetu.
Ili kudumisha usalama na heshima kwenye mfumo wa Google Play, tumebuni viwango vinavyobainisha na kuzuia maudhui ambayo hayafai au yanayodhuru watumiaji wetu.
  • Matangazo yasiyofaa kwa daraja la maudhui ya programu

① Tangazo hili halifai (Kijana) kwa daraja la maudhui la programu (Kila mtu)
② Tangazo hili halifai (Watu wazima) kwa daraja la maudhui la programu (Kijana)
③ Ofa ya tangazo hili (tangazo linaloshawishi upakuaji wa programu inayowalenga Watu wazima) haifai daraja la maudhui la programu ya michezo ya video ambako tangazo hilo limeonyeshwa (Kila mtu)

Masharti ya Matangazo ya Familia

Ikiwa unachuma mapato ya programu inayolenga watoto kwenye Google Play, ni muhimu programu yako ifuate Masharti ya Matangazo ya Familia na Sera ya Uchumaji wa Mapato.

Matangazo Yanayopotosha

Matangazo hayapaswi kuiga kiolesura cha kipengele cha programu yoyote, kama vile arifa au vipengele vya onyo vya mfumo wa uendeshaji. Ni lazima iwe dhahiri kwa mtumiaji ni programu gani inayoonyesha kila tangazo.

Ili kudumisha usalama na heshima kwenye mfumo wa Google Play, tumebuni viwango vinavyobainisha na kuzuia maudhui ambayo hayafai au yanayodhuru watumiaji wetu.
  • Matangazo yanayoiga kiolesura cha programu:

    ① Aikoni ya alama ya kuuliza katika programu hii ni tangazo linalomwelekeza mtumiaji kwenye ukurasa wa kutua wa nje.

  • Matangazo yanayoiga arifa ya mfumo:

    ① ② Mifano iliyo hapo juu inaonyesha matangazo yanayoiga arifa mbalimbali za mifumo.


    ① Mfano wa hapo juu unaonyesha sehemu ya kipengele inayoiga vipengele vingine lakini inamwelekeza tu mtumiaji kwenye tangazo moja au matangazo kadhaa.

Matangazo Yanayokatiza Mtumiaji

Matangazo yanayokatiza mtumiaji ni matangazo ambayo yanaonyeshwa kwa watumiaji kwa njia zisizotarajiwa, ambazo zinaweza kusababisha watumiaji kubofya bila kukusudia, au kukatiza au kuathiri urahisi wa kutumia vipengele vya kifaa.

Programu yako haipaswi kumlazimisha mtumiaji abofye tangazo au kutuma taarifa binafsi kwa madhumuni ya utangazaji kabla aweze kutumia programu kikamilifu. Matangazo yanapaswa tu kuonyeshwa ndani ya programu inayoyaonyesha na hayapaswi kuathiri programu, matangazo au utendakazi mwingine wa kifaa, ikiwa ni pamoja na milango na vitufe vya kifaa au mfumo. Hii inajumuisha matangazo yaliyowekelewa juu, vipengele vinavyoshirikiana au makundi ya matangazo yaliyotengenezwa kuwa wijeti. Ikiwa programu yako inaonyesha matangazo ambayo yanakatiza matumizi ya kawaida, lazima yawe rahisi kuondoa bila adhabu.

Ili kudumisha usalama na heshima kwenye mfumo wa Google Play, tumebuni viwango vinavyobainisha na kuzuia maudhui ambayo hayafai au yanayodhuru watumiaji wetu.
  • Matangazo yanayoonyeshwa kwenye skrini nzima au yanayokatiza matumizi ya kawaida na hayatoi njia ya wazi ya kuondoa tangazo:

    ① Tangazo hili halina kitufe cha kuliondoa.

  • Matangazo yanayomlazimisha mtumiaji kubofya kwa kutumia kitufe cha uongo cha kuondoa, au kwa kufanya matangazo yaonekane ghafla katika maeneo ya programu ambapo mtumiaji hugusa kwa utendaji mwingine:

    ① Tangazo hili linatumia kitufe cha uongo cha kuliondoa.

    ② Tangazo hili huonyeshwa ghafla katika eneo ambako mtumiaji amezoea kugusa kwa utendaji wa ndani ya programu.

  • Matangazo yanayoonekana nje ya programu inayoyaonyesha:

    ① Mtumiaji anaenda kwenye skrini ya kwanza kutoka kwenye programu hii na tangazo linatokea kwa ghafla kwenye skrini ya kwanza.

  • Matangazo yanayoanzishwa na kitufe cha ukurasa wa mwanzo au vipengele vingine vilivyoundwa mahususi kwa ajili ya kuondoka kwenye programu:

    ① Mtumiaji anajaribu kuondoka kwenye programu na kwenda kwenye skrini ya kwanza, lakini badala yake, utaratibu unaotarajiwa unakatizwa na tangazo.

Better Ads Experiences

Wasanidi programu wanapaswa kutii mwongozo wa matangazo ufuatao ili wahakikishe hali za matumizi zenye ubora wa hali ya juu kwa ajili ya watumiaji, wanapotumia programu za Google Play. Huenda matangazo yako yasionyeshwe kwa watumiaji kwa njia zisizotarajiwa kama ifuatavyo:

  • Matangazo ya katikati ya skrini nzima ya kila muundo (video, GIF, yasiyobadilika, n.k.) yanayoonekana bila kutarajiwa, kwa kawaida wakati mtumiaji amechagua kufanya jambo lingine, hayaruhusiwi. 
    • Matangazo yanayotokea wakati wa uchezaji, kama mwanzoni mwa kiwango cha mchezo au mwanzoni mwa sehemu ya maudhui hayaruhusiwi. 
    • Matangazo ya katikati ya skrini nzima yanayotokea kabla ya skrini ya programu inayopakia (skrini ya utangulizi) hayaruhusiwi.
  • Matangazo ya katikati ya skrini nzima ya kila muundo yasiyoweza kufungwa baada ya sekunde 15 hayaruhusiwi. Matangazo ya katikati ya skrini nzima ya kujijumuisha au matangazo ya katikati ya skrini nzima yasiyokatiza vitendo vya watumiaji (kwa mfano, baada ya skirini ya alama katika programu ya mchezo) yanaweza kuendelea kuonyeshwa kwa zaidi ya sekunde 15.

Sera hii haitumiki kwa matangazo ya zawadi ambayo watumiaji wamejijumuisha kwa njia dhahiri (Kwa mfano, tangazo ambalo wasanidi programu wameliweka dhahiri kwa mtumiaji kutazama ili kufikia kipengele fulani cha mchezo au kipande cha maudhui). Pia, sera hii haitumiki kwenye uchumaji wa mapato na utangazaji ambao haukatizi matumizi ya kawaida ya programu au uchezaji (kwa mfano, maudhui ya video yenye matangazo ndani yake, matangazo ya mabango yasiyo ya skrini nzima).

Kanuni hizi zimetokana na mwongozo wa Better Ads Standards - Mobile Apps Experiences. Kwa maelezo zaidi kuhusu Better Ads Standards, tafadhali rejelea Coalition of Better Ads.
Ili kudumisha usalama na heshima kwenye mfumo wa Google Play, tumebuni viwango vinavyobainisha na kuzuia maudhui ambayo hayafai au yanayodhuru watumiaji wetu.
  • Matangazo yasiyotarajiwa yanayotokea wakati wa uchezaji au mwanzoni mwa sehemu ya maudhui (kwa mfano, baada ya mtumiaji kubofya kitufe na kabla ya kitendo kilichokusudiwa na hatua hiyo kuanza kufanya kazi). Matangazo haya huwa hayajatarajiwi na watumiaji, kwa kuwa watumiaji hutegemea kuanza mchezo au kutangamana na maudhui.

    ① Tangazo lisilobadilika ambalo halijatarajiwa hutokea wakati wa uchezaji, mwanzoni mwa ngazi ya mchezo.

    ② Tangazo la video ambalo halijatarajiwa hutokea mwanzoni mwa sehemu ya maudhui.
  • Tangazo la skrini nzima hutokea wakati wa uchezaji na haliwezi kufungwa baada ya sekunde 15.

    ①  Tangazo la katikati hutokea wakati wa uchezaji na haliwapatii watumiaji chaguo la kuliruka ndani ya sekunde 15.

Zinazolenga Matangazo

Haturuhusu programu ambazo huonyesha matangazo ya katikati mara kwa mara yanayowazuia watumiaji kutumia programu na kufanya shughuli ndani ya programu.
Ili kudumisha usalama na heshima kwenye mfumo wa Google Play, tumebuni viwango vinavyobainisha na kuzuia maudhui ambayo hayafai au yanayodhuru watumiaji wetu.
  • Programu ambapo tangazo la katikati linaonyeshwa kwa mfululizo baada ya kitendo cha mtumiaji (ikiwa ni pamoja na, lakini si tu kubofya, kutelezesha kidole, n.k.).

    ① Ukurasa wa kwanza wa ndani ya programu una vitufe mbalimbali vya kutumia. Mtumiaji anapobofya Anzisha programu ili atumie programu, tangazo la katikati huibuka. Baada ya tangazo kufungwa, mtumiaji hurudi kwenye programu kisha hubofya Huduma ili aanze kutumia huduma, ila tangazo jingine la katikati linaonyeshwa.


    ② Kwenye ukurasa wa kwanza, mtumiaji anaongozwa ili abofye Cheza kwa kuwa ni kitufe pekee cha kutumia programu. Mtumiaji anapokibofya, tangazo la katikati linaonyeshwa. Baada ya tangazo kufungwa, mtumiaji hubofya Anzisha kwa kuwa ni kitufe pekee anachoweza kutumia na tangazo jingine la katikati linaonyeshwa.

Uchumaji wa Mapato kwa Kutumia Kipengele cha Kufunga Skrini

Kama lengo la kipekee la programu si kufunga skrini, programu hazipaswi kuanzisha matangazo au vipengele ambavyo vinachuma mapato kwa kutumia kipengele cha kufunga skrini ya kifaa.

Ulaghai wa Kimatangazo

Ulaghai wa kimatangazo hauruhusiwi. Kwa maelezo zaidi, rejelea Sera yetu dhidi ya ulaghai wa kimatangazo.

Matumizi ya Data ya Mahali kwa Ajili ya Matangazo

Programu zinazoendeleza matumizi ya data ya mahali kifaa kilipo kutokana na ruhusa ya kuonyesha matangazo zinategemea sera ya Maelezo Nyeti na ya Binafsi na ni lazima pia zitii masharti yafuatayo:

  • Ni lazima utumiaji au ukusanyaji wa data ya mahali kifaa kilipo kutokana na ruhusa kwa madhumuni ya matangazo uwe dhahiri kwa mtumiaji na urekodiwe kwenye sera ya faragha ambayo ni lazima ifuatwe na programu, ikiwa ni pamoja na kuunganisha kwenye sera zozote za faragha zinazohusiana za kituo cha matangazo kinachoshughulikia matumizi ya data ya mahali.
  • Kwa mujibu wa masharti ya Ruhusa za Mahali unapaswa kuomba tu ruhusa za mahali ili utekeleze vipengele au huduma za sasa za ndani ya programu yako na hupaswi kuomba ruhusa za data ya mahali kifaa kilipo kwa matumizi ya matangazo pekee.

Matumizi ya Kitambulisho cha Kifaa cha Android kwa Ajili ya Matangazo

Toleo la 4.0 la Huduma za Google Play lilianzisha API mpya na Kitambulisho kwa ajili ya matumizi ya watoa huduma ya matangazo na uchanganuzi. Sheria na masharti ya vitambulisho hivi yapo hapo chini.

  • Matumizi. Kitambulisho cha kifaa kwa ajili ya matangazo ya Android (AAID) lazima kitumike tu kwa utangazaji na takwimu za watumiaji. Ni lazima hali ya mipangilio ya “Jiondoe kwenye Matangazo Yanayotegemea Mambo Yanayokuvutia” au “Jiondoe kwenye Mapendeleo ya Matangazo" ithibitishwe kila mara unapofikia kitambulisho.
  • Kuhusisha maelezo yanayoweza kumtambulisha mtu au vitambulishi vingine.
    • Matumizi ya matangazo: Kitambulishi cha matangazo hakipaswi kuunganishwa kwenye Vitambulishi vya kifaa vinavyoendelea kuwepo (kwa mfano: SSAID, anwani ya MAC, IMEI, n.k.) kwa madhumuni yoyote ya utangazaji. Kitambulishi cha matangazo kinaweza tu kuunganishwa kwenye maelezo yanayoweza kumtambulisha mtu binafsi kupitia idhini dhahiri ya mtumiaji.
    • Matumizi ya takwimu: Kitambulishi cha matangazo hakipaswi kuunganishwa kwenye maelezo yanayoweza kumtambulisha mtu binafsi au kuhusishwa na vitambulishi vyovyote vya kifaa vinavyoendelea kuwepo (kwa mfano: SSAID, anwani ya MAC, IMEI, n.k.) kwa madhumuni yoyote ya takwimu. Tafadhali soma sera ya Data ya Mtumiaji ili upate mwongozo wa ziada kuhusu vitambulishi vya kifaa vinavyoendelea kuwepo.
  • Kuheshimu chaguo za mtumiaji.
    • Kitambulishi cha matangazo kikiwekwa upya, hakipaswi kuhusishwa na kitambulishi cha awali au data iliyotokana na kitambulishi cha awali cha matangazo bila idhini dhahiri ya mtumiaji.
    • Lazima utii mipangilio ya mtumiaji ya "Jiondoe kwenye Matangazo Yanayotegemea Mambo Yanayokuvutia" au "Jiondoe kwenye Mapendeleo ya Matangazo". Iwapo mtumiaji ameweka mipangilio hii, hupaswi kutumia kitambulisho cha kifaa kwa ajili ya matangazo kuunda wasifu wa mtumiaji kwa madhumuni ya kutangaza au kulenga watumiaji na matangazo yanayotegemea mambo yanayowavutia. Shughuli zinazoruhusiwa ni pamoja na matangazo ya kimuktadha, masafa ya uelekezi, kufuatilia hali ya kushawishika, kuripoti na usalama na kugundua ulaghai.
    • Kwenye vifaa vipya, mtumiaji anapofuta kitambulishi cha matangazo cha Android, kitambulishi hicho kitaondolewa. Majaribio yoyote ya kufikia kitambulishi yatapokea mifuatano ya sufuri. Kifaa kisicho na kitambulishi cha matangazo hakipaswi kuunganishwa na data iliyohusiana au kutokana na kitambulishi cha awali cha matangazo.
  • Uwazi kwa watumiaji. Arifa ya faragha ya kisheria inayojitosheleza lazima itolewe kwa ukusanyaji na matumizi ya kitambulishi cha kifaa kwa ajili ya matangazo na kuzingatia masharti haya. Ili upate maelezo zaidi kuhusu viwango vyetu vya faragha, tafadhali kagua sera yetu ya Data ya Mtumiaji.
  • Kufuata sheria na masharti. Kitambulishi cha matangazo kinaweza tu kutumika kwa mujibu wa Sera ya Mpango wa Wasanidi Programu wa Google Play. Mshirika yeyote utakayekishiriki naye katika kipindi cha biashara yako pia anatarajiwa kutii sera hii. Programu zote zinazopakiwa au kuchapishwa kwenye Google Play zinapaswa kutumia kitambulisho cha matangazo (kinapopatikana kwenye kifaa) badala ya vitambulishi vyovyote vingine vya kifaa kwa madhumuni yoyote ya matangazo.
Kwa maelezo zaidi, rejelea sera ya Data ya Mtumiaji.

Usajili

Wewe, ukiwa msanidi programu, hupaswi kuwapotosha watumiaji kuhusu huduma zozote za usajili au maudhui unayotoa ndani ya programu yako. Ni muhimu zaidi kuelezea ofa yako kwa njia dhahiri katika matangazo yoyote ya ndani ya programu au skrini za utangulizi. Haturuhusu programu ambazo zinawahadaa watumiaji kufanya ununuzi wa kilaghai au wa uongo (ikiwa ni pamoja na usajili au ununuzi wa ndani ya programu).

Ni lazima uelezee kwa uwazi kuhusu ofa yako. Hii ni pamoja na kuwa dhahiri kuhusu sheria na masharti ya ofa, ikiwa ni pamoja na bei ya usajili, kipindi cha kutuma bili na iwapo usajili unahitajika ili kutumia programu. Watumiaji hawapaswi kutekeleza hatua yoyote ya ziada ili kusoma maelezo.

Lazima usajili utoe manufaa ya kudumu au yanayojirudia kwa watumiaji katika kipindi chote cha usajili na haupaswi kutumiwa kutoa manufaa dhahiri ya wakati mmoja kwa watumiaji (kwa mfano, SKU ambazo zinatoa sarafu/masalio ya wakati mmoja ya ndani ya programu au viboreshaji vya mchezo vya matumizi ya mara mmoja). Usajili wako unaweza kutoa kichocheo au bonasi za ofa, lakini lazima vitu hivi visaidie katika kutoa manufaa ya kudumu au yanayojirudia katika kipindi chote cha usajili. Bidhaa ambazo hazitoi manufaa ya kudumu na yanayojirudia lazima zitumie bidhaa ya ndani ya programu badala ya bidhaa inayolipiwa.

Hupaswi kubadilisha au kutoa sifa za uongo kuhusu manufaa ya wakati mmoja kwa watumiaji kama usajili. Hii ni pamoja na ubadilishaji wa usajili kuwa ofa ya wakati mmoja (kwa mfano, kughairi, kuacha kuendesha huduma au kupunguza manufaa yanayojirudia) baada ya mtumiaji kununua usajili.

Ili kudumisha usalama na heshima kwenye mfumo wa Google Play, tumebuni viwango vinavyobainisha na kuzuia maudhui ambayo hayafai au yanayodhuru watumiaji wetu.
  • Usajili wa kila mwezi ambao hauwafahamishi watumiaji kuwa utasasishwa kiotomatiki na kutozwa kila mwezi.
  • Usajili wa kila mwaka ambao unaonyesha kwa njia dhahiri bei yake kwa misingi ya ada ya kila mwezi.
  • Bei za usajili na sheria na masharti ambayo hayajajanibishwa kikamilifu.
  • Matangazo ya ndani ya programu ambayo hayaonyeshi kwa njia dhahiri kuwa mtumiaji anaweza kufikia maudhui bila kujisajili (ikiwa yapo).
  • Majina ya SKU ambayo hayaonyeshi vizuri hali ya usajili, kama vile "Jaribio Lisilolipishwa," au “Jaribu uanachama wa Premium - furahia kwa siku tatu bila malipo,” kwa usajili ulio na gharama inayojirudia kiotomatiki. 
  • Skrini nyingi kwenye utaratibu wa ununuzi ambazo zinasababisha watumiaji kubofya kitufe cha 'jisajili' kimakosa.
  • Usajili ambao hautoi manufaa ya kudumu au yanayojirudia — kwa mfano, kutoa vito 1,000 kwa mwezi wa kwanza, kisha kupunguza manufaa hayo kuwa kito kimoja kwa miezi inayofuata ya usajili.
  • Kuhitaji mtumiaji ajisajili kwenye usajili unaosasishwa kiotomatiki ili kupata manufaa ya wakati mmoja na kughairi usajili wa mtumiaji bila idhini yake baada ya kununua bidhaa.
Mfano wa 1:

① Kitufe cha 'Ondoa' hakionekani vizuri na huenda watumiaji wasifahamu kuwa wanaweza kufikia utendaji bila kukubali ofa ya usajili.

② Ofa inaonyesha tu bei kwa misingi ya kila mwezi na huenda watumiaji wasifahamu kuwa wanaweza kutozwa bei ya miezi sita wakati wanapojisajili.

③ Ofa inaonyesha tu bei ya utangulizi na huenda watumiaji wasifahamu ada ambayo watatozwa kiotomatiki mwishoni mwa kipindi cha utangulizi.

④ Ofa inapaswa kujanibishwa kwa lugha iliyotumiwa katika sheria na masharti ili watumiaji waweze kufahamu maelezo yote ya ofa.

 

Mfano wa 2:

① Mibofyo inayojirudia katika eneo sawa la kitufe husababisha mtumiaji kubofya kimakosa kitufe cha mwisho cha “endelea” ili kujisajili.

② Kiasi ambacho watumiaji watatozwa baada ya kipindi cha jaribio kuisha hakisomeki vizuri, hali ambayo inaweza kufanya watumiaji wafikirie kuwa mpango haulipishwi

Majaribio Yasiyolipishwa na Ofa za Utangulizi

Kabla ya mtumiaji kujiandikisha kwenye usajili wako: Ni lazima uelezee kwa njia dhahiri na sahihi sheria na masharti ya ofa yako, ikiwa ni pamoja na muda, bei na ufafanuzi wa huduma au maudhui yanayoweza kufikiwa. Hakikisha kuwa unawaruhusu watumiaji kufahamu wakati ambapo jaribio lisilolipishwa litabadilika kuwa usajili unaolipishwa, gharama ya usajili unaolipishwa na kwamba mtumiaji anaweza kughairi iwapo hangependa kuanza kulipia usajili.
Ili kudumisha usalama na heshima kwenye mfumo wa Google Play, tumebuni viwango vinavyobainisha na kuzuia maudhui ambayo hayafai au yanayodhuru watumiaji wetu.
  • Ofa ambazo hazifafanui kwa njia dhahiri muda wa jaribio lisilolipishwa au bei ya utangulizi.
  • Ofa ambazo hazifafanui kwa njia dhahiri kuwa mtumiaji ataandikishwa kiotomatiki katika usajili unaolipishwa mwishoni mwa kipindi cha ofa.
  • Ofa ambazo hazionyeshi kwa njia dhahiri kuwa mtumiaji anaweza kufikia maudhui bila jaribio lisilolipishwa (ikiwa lipo).
  • Bei na sheria na masharti ya ofa ambayo hayajajanibishwa kikamilifu.
 

① Kitufe cha 'Ondoa' hakionekani vizuri na huenda watumiaji wasielewe kuwa wanaweza kufikia utendaji bila kujisajili kwenye jaribio lisilolipishwa.

② Ofa huangazia jaribio lisilolipishwa na huenda watumiaji wasielewe kuwa watatozwa kiotomatiki baada ya kipindi cha kujaribu kuisha.

③ Ofa haitaji kipindi cha jaribio na huenda watumiaji wasielewe muda wa kutumia bila malipo maudhui yanayohitaji usajili.

④ Ofa inapaswa kujanibishwa kwa lugha iliyotumiwa katika sheria na masharti ili watumiaji waweze kufahamu maelezo yote ya ofa.

Kughairi na Kudhibiti Usajili pamoja na Kurejesha Pesa za Usajili

Ikiwa unauza usajili ndani ya programu zako, unapaswa kuhakikisha kuwa programu zako zinafumbua kwa uwazi namna mtumiaji anavyoweza kudhibiti au kughairi usajili wake. Unapaswa pia ujumuishe kwenye programu yako uwezo wa kufikia njia iliyo rahisi kutumia ya mtandaoni ya kughahiri usajili. Katika mipangilio ya akaunti ya programu yako (au ukurasa sawa na huo), unaweza kutimiza masharti haya kwa kujumuisha:

  • Kiungo cha Kituo cha Usajili cha Google Play (kwa programu zinazotumia mfumo wa utozaji wa Google Play); na/au
  • ufikiaji wa moja kwa moja kwenye mchakato wako wa kughairi.

Mtumiaji akighairi usajili alionunua kupitia mfumo wa utozaji wa Google Play, sera yetu ya jumla ni kuwa mtumiaji huyo hatarejeshewa pesa kwa kipindi cha bili cha sasa, lakini ataendelea kupokea maudhui ya usajili wake kwa kipindi cha bili kilichosalia, bila kuzingatia tarehe ya kughairi. Hatua ya mtumiaji kughairi usajili itatekelezwa baada ya kipindi cha bili cha sasa kukamilika.

Unaweza (ukiwa mtoa huduma za maudhui au mtoa idhini ya kufikia) kutekeleza sera nyumbufu zaidi ya kurejesha pesa moja kwa moja kati yako na watumiaji wako. Ni wajibu wako kuwaarifu watumiaji kuhusu mabadiliko yoyote kwenye sera za kurejesha pesa, kughairi na kujisajili na kuhakikisha kuwa sera hizo zinatii sheria zinazotumika.


Mpango wa SDK ya Matangazo ya Familia yenye Uthibitishaji wa Kujifanyia

Iwapo unaonyesha matangazo katika programu yako na hadhira inayolengwa na programu yako inajumuisha watoto pekee kama ilivyoelezewa katika Sera ya Familia, basi ni lazima utumie tu matoleo ya SDK za matangazo zenye uthibitishaji wa kujifanyia unaotii sera za Google Play, ikiwa ni pamoja na Masharti ya SDK ya Matangazo ya Familia yenye Uthibitishaji wa Kujifanyia yaliyo hapa chini.

Iwapo hadhira inayolengwa na programu yako inajumuisha watumiaji watoto na watu wazima, unapaswa kuhakikisha kuwa matangazo yanayoonyeshwa kwa watoto yanatoka kwenye mojawapo ya matoleo haya ya SDK ya matangazo yenye uthibitishaji wa kujifanyia (kwa mfano, kwa kutumia hatua za kuchagua umri).

Kumbuka ni wajibu wako kuhakikisha kwamba matoleo yote ya SDK unayotumia kwenye programu yako, ikiwa ni pamoja na matoleo ya SDK ya Matangazo yenye Uthibitishaji wa Kujifanyia yanatii sera, sheria na kanuni zote zinazotumika mahali ulipo. Google haitoi dhamana au uwakilishi wowote kuhusu usahihi wa maelezo ambayo hutolewa na SDK za matangazo katika mchakato wa uthibitishaji wa kujifanyia.

Matumizi ya SDK za matangazo ya Familia zenye uthibitishaji wa kujifanyia yanahitajika tu ikiwa unatumia SDK za matangazo ili kuonyesha matangazo kwa watoto. Mipango ifuatayo inaruhusiwa bila uthibitishaji wa kujifanyia wa SDK ya matangazo katika Google Play, hata hivyo, bado ni wajibu wako kuhakikisha kuwa maudhui ya matangazo yako na mbinu za ukusanyaji wa data zinatii Sera ya Data ya Watumiaji na Sera ya Familia ya Google Play:

  • Matangazo ya Ndani ya Kampuni ambapo unatumia SDK kudhibiti utangazaji katika vyombo mbalimbali vya habari, kuhusu programu yako au bidhaa na maudhui mengine unayomiliki.
  • Kuingia katika mpango wa ofa za moja kwa moja na watangazaji ambapo unatumia SDK kudhibiti orodha ya bidhaa.

Masharti ya SDK ya Matangazo ya Familia yenye Uthibitishaji wa Kujifanyia

  • Fafanua matendo na maudhui ya matangazo yasiyofaa na uyazuie kupitia sheria na masharti au sera ya SDK ya matangazo. Ufafanuzi unapaswa kutii Sera za Mpango wa Wasanidi Programu wa Google Play.
  • Tengeneza mbinu ya kukadiria faili za matangazo kulingana na makundi yanayoambatana na umri. Ni lazima makundi yanayofaa umri yajumuishe angalau makundi ya 'Kila Mtu' na 'Watu Wazima'. Mbinu ya ukadiriaji inapaswa kuafikiana na mbinu ambayo Google hutoa kwa SDK baada ya kujaza fomu ya kutuma ombi hapa chini.
  • Waruhusu wachapishaji, kwa misingi ya kila ombi au kila programu, waombe hali ya 'ichukuliwe kama inayowalenga watoto' katika uonyeshaji wa matangazo. Hali kama hiyo ni lazima itii sheria na kanuni zinazotumika, kama vile Sheria ya Marekani ya Kulinda Faragha ya Watoto Mtandaoni (COPPA) na Sheria ya Jumla ya Ulinzi wa Data (GDPR) ya Umoja wa Ulaya. Google Play inahitaji SDK za matangazo ili izime matangazo yaliyowekewa mapendeleo, utangazaji unaotegemea mambo yanayomvutia mtumiaji na kutangaza tena ikiwa sehemu ya hali ya 'ichukuliwe kama inayowalenga watoto'.
  • Waruhusu wachapishaji wachague miundo ya matangazo inayotii sera ya Matangazo ya Familia na Uchumaji Mapato kwenye Google Play na itimize masharti ya Mpango wa Programu Zilizoidhinishwa na Walimu
  • Hakikisha kuwa wakati hali ya uwekaji zabuni katika wakati halisi inatumika kuonyesha matangazo kwa watoto, faili za matangazo ziwe zimekaguliwa na viashirio vya faragha viwe vimetangazwa kwa wanaoweka zabuni.
  • Ipatie Google maelezo ya kutosha, kama vile kuwasilisha programu ya majaribio na maelezo yaliyobainishwa kwenye fomu ya ombi hapa chini, ili ithibitishe sera ya SDK ya matangazo inatii masharti yote ya uthibitishaji wa kujifanyia pamoja na kujibu kwa wakati unaofaa maombi yoyote ya baadaye ya maelezo, kama vile kuwasilisha matoleo mapya ili kuthibitisha toleo la SDK ya matangazo linatii masharti yote ya uthibitishaji wa kujifanyia na kuwasilisha programu ya majaribio.
  • Jifanyie uthibitishaji kuwa matoleo yote mapya yanatii Sera za Mpango wa Wasanidi Programu wa Google Play, ikiwa ni pamoja na Masharti ya Sera ya Familia.

Kumbuka: SDK za Matangazo za Familia zenye Uthibitishaji wa Kujifanyia zinapaswa zionyeshe matangazo yanayotii sheria na kanuni zote zinazohusu watoto ambazo zinaweza kutumika kwa wachapishaji husika.

Maelezo zaidi kuhusu kuziwekea alama maalum faili za matangazo na kuwasilisha programu ya majaribio yanaweza kupatikana hapa.

Yafuatayo ni masharti ya upatanisho kwa mifumo ya matangazo inapoonyesha matangazo kwa watoto:

  • Tumia tu SDK za Matangazo za Familia zenye Uthibitishaji wa Kujifanyia au uweke kinga zinazohitajika kuhakikisha kuwa matangazo yote yanayoonyeshwa kutoka kwenye upatanisho yanatii masharti haya; na
  • Tuma maelezo yanayohitajika kwenye mifumo ya upatanisho ili kuashiria daraja la maudhui la tangazo na hali yoyote inayotumika ya 'ichukuliwe kama inayowalenga watoto'.

Wasanidi programu wanaweza kupata orodha ya SDK za Matangazo ya Familia zenye Uthibitishaji wa Kujifanyia na wanaweza kuangalia aina za matoleo mahususi ya SDK hizo za matangazo ambazo zimejifanyia uthibitishaji ili zitumike kwenye programu za Familia. hapa.

Wasanidi programu pia wanaweza kushiriki fomu hii ya ombi na watoa huduma wa SDK za matangazo ambao wangependa kujifanyia uthibitishaji.


Matangazo na Ukurasa wa Programu katika Google Play

Utangazaji na uonekanaji wa programu yako huathiri ubora wa duka kwa kiasi kikubwa. Usitumie kurasa za programu katika Google Play zenye taka, matangazo duni na mbinu bandia za kuimarisha uonekanaji wa programu yako kwenye Google Play.

Utangazaji wa Programu

Haturuhusu programu zinazojihusisha moja kwa moja au kwa njia zisizo za moja kwa moja au zinazonufaika kutokana na mbinu za utangazaji (kama vile matangazo) zinazotumia udanganyifu au zinazodhuru watumiaji au mfumo wa wasanidi programu. Mbinu za utangazaji ni za udanganyifu au zinadhuru iwapo matendo au maudhui yake yanakiuka Sera zetu za Mpango wa Wasanidi Programu.

Ili kudumisha usalama na heshima kwenye mfumo wa Google Play, tumebuni viwango vinavyobainisha na kuzuia maudhui ambayo hayafai au yanayodhuru watumiaji wetu.
  • Kutumia matangazo ya udanganyifu kwenye tovuti, programu, au vipengele vingine, ikiwa ni pamoja na arifa zinazofanana na arifa na tahadhari za mfumo.
  • Kutumia matangazo yenye maudhui ya ngono dhahiri ili kuelekeza watumiaji kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play ili wapakue.
  • Mbinu za utangazaji au usakinishaji zinazowaelekeza kwingine watumiaji kwenye Google Play au kupakua programu bila mtumiaji kuchukua hatua.
  • Matangazo yasiyoidhinishwa yanayotumwa kupitia huduma za SMS.
  • Picha au maandishi yaliyo kwenye jina, aikoni ya programu au jina la msanidi programu yanayoonyesha utendaji au nafasi ya duka, bei au maelezo ya ofa au ambayo yanaashiria uhusiano na mipango iliyopo ya Google Play.

Ni wajibu wetu kuhakikisha kuwa mitandao ya matangazo, washirika au matangazo yoyote yanayohusiana na programu yako yanatii sera hizi.


Metadata

Watumiaji hutegemea maelezo ya programu yako ili yawasaidia kuelewa utendaji na malengo yake. Haturuhusu programu zilizo na metadata inayopotosha, iliyo na miundo isiyo sahihi, isiyo na maelezo, isiyo muhimu, iliyopita kiasi au isiyofaa, ikiwa ni pamoja na, lakini si tu, maelezo ya programu, jina la msanidi programu, mada, aikoni, picha za skrini na picha za matangazo. Ni lazima wasanidi programu watoe maelezo dhahiri na yaliyoandikwa vizuri ya programu yao. Haturuhusu pia maoni ya watumiaji yasiyowatambulisha au yasiyojulikana katika maelezo ya programu.

Jina lako la msanidi programu, aikoni na jina la programu huwasaidia watumiaji kutafuta na kupata maelezo kuhusu programu yako. Usitumie emoji, vikaragosi au herufi maalum zinazorudiwa katika vipengele hivi vya metadata. Usitumie HERUFI KUBWA PEKEE isipokuwa iwe sehemu ya jina la biashara yako. Haturuhusu ishara za kupotosha katika aikoni za programu, kwa mfano: kiashirio cha nukta cha kuonyesha ujumbe mpya wakati hamna ujumbe mpya na ishara za kupakua au kusakinisha wakati programu haihusiani na upakuaji wa maudhui. Jina la programu yako halipaswi kuzidi herufi 30. Usitumie maandishi au picha kwenye jina la programu, aikoni au jina la msanidi programu inayoonyesha utendaji wa duka au nafasi, bei au maelezo ya utangazaji au inayopendekeza mahusiano na mipango iliyopo ya Google Play.

Mbali na masharti yaliyobainishwa hapa, huenda Sera mahususi za Wasanidi Programu kwenye Google Play zikakuhitaji uweke maelezo ya ziada ya metadata.

Ili kudumisha usalama na heshima kwenye mfumo wa Google Play, tumebuni viwango vinavyobainisha na kuzuia maudhui ambayo hayafai au yanayodhuru watumiaji wetu.

        ① Maoni ya Watumiaji Yasiyowatambulisha au Yasiyojulikana
        ② Ulinganishaji wa Data ya programu au biashara
        ③ Makundi ya maneno na orodha za maneno wima au mlalo

 

        ① HERUFI KUBWA PEKEE ingawa si sehemu ya jina la biashara
        ② Mifuatano ya herufi maalum ambazo hazifai kwenye programu
        ③ Matumizi ya emoji, vikaragosi (ikiwa ni pamoja na kaomoji) na herufi maalum
        ④ Ishara za kupotosha
        ⑤ Maandishi ya kupotosha

 

  • Picha au maandishi yanayoonyesha nafasi au utendaji wa duka, kama vile aikoni za zawadi za 'Programu bora ya mwaka,' 'Inayoongoza,' 'Bora zaidi kwenye Google Play 20XX,' 'Maarufu,' n.k.

  • Picha au maandishi yanayoonyesha maelezo ya ofa na bei, kama vile 'punguzo la asilimia 10,' 'zawadi ya pesa ya $50,' 'hailipishwi kwa muda mfupi pekee,' n.k.

  • Picha au maandishi yanayoonyesha programu za Google Play, kama vile 'Chaguo za Wahariri,' 'Mpya,' n.k.

Ifuatayo ni mifano ya video, picha au maandishi yasiyofaa kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play:

  • Video au picha zenye maudhui yanayochochea ngono. Usichapishe picha zinazoonyesha matiti, matako, sehemu za siri au maudhui yoyote ya uchi, iwe ni mifano au viungo halisi.
  • Kutumia lugha chafu na lugha nyingine isiyofaa katika hadhira ya jumla kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play. 
  • Picha za ukatili zinazoonyeshwa katika aikoni za programu, picha za matangazo au video.
  • Maonyesho ya matumizi ya dawa za kulevya. Ni sharti maudhui ya EDSA (Maudhui ya Kielimu, Filamu Tahakiki, Sayansi au Sanaa) utakayoweka kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play yafae hadhira ya jumla.

Ifuatayo ni mifano ya mbinu bora:

  • Angazia mambo mazuri kuhusu programu yako. Shiriki mambo ya kuvutia na yanayosisimua kuhusu programu yako ili uwasaidie watumiaji waelewe kinachofanya programu yako iwe maalum.
  • Hakikisha jina na maelezo ya programu yako yanaelezea kwa usahihi utendaji wa programu yako.
  • Epuka kutumia maneno muhimu au marejeleo yanayorudiwarudiwa au yasiyohusiana.
  • Fupisha maelezo ya programu yako na uyafanye dhahiri. Maelezo mafupi husababisha hali bora ya watumiaji, hasa kwenye vifaa vilivyo na skrini ndogo. Maelezo marefu zaidi, ya kina, yenye miundo isiyo sahihi au yanayorudiwa yanaweza kusababisha ukiukaji wa sera hii.
  • Kumbuka kuwa ni sharti ukurasa wa programu katika Google Play ufae hadhira ya jumla. Usitumie maandishi, picha au video zisizofaa kwenye ukurasa wa programu yako katika Google Play na utii mwongozo uliotolewa hapa juu.

Ukadiriaji wa Watumiaji, Maoni na Mara Ambazo Programu Imesakinishwa

Wasanidi programu hawapaswi kujaribu kutumia hila ili kuathiri mahali ambapo programu itawekwa katika Google Play. Hali hii inajumuisha, lakini si tu, kuongeza ukadiriaji wa bidhaa, maoni au idadi ya mara ambazo programu imesakinishwa kwa njia zisizoruhusiwa kama vile kwa ulaghai au uhamasishaji wa maoni na ukadiriaji au kuwahimiza watumiaji kusakinisha programu zingine kama utendaji mkuu wa programu.

Ili kudumisha usalama na heshima kwenye mfumo wa Google Play, tumebuni viwango vinavyobainisha na kuzuia maudhui ambayo hayafai au yanayodhuru watumiaji wetu.
  • Kuwaomba watumiaji wakadirie programu yako kwa kuwapa zawadi:


        ① Arifa hii inawapatia watumiaji punguzo wanapofanya ukadiriaji wa juu.
     
  • Kuwasilisha ukadiriaji mara kwa mara kwa kujifanya kuwa mtumiaji mpya ili kushawishi uwekaji wa programu kwenye Google Play.
     
  • Kuwasilisha au kuwahimiza watumiaji kuwasilisha maoni yaliyo na maudhui yasiyofaa, ikiwa ni pamoja na washirika, kuponi, misimbo ya michezo, anwani za barua pepe au viungo vinavyoelekeza kwenye tovuti au programu zingine:

        ② Maoni haya yanawahimiza watumiaji watangaze programu ya RescueRover kwa kuwapa ofa ya kuponi.

Ukadiriaji na maoni ni vigezo vya ubora wa programu. Watumiaji hutegemea kuwa ukadiriaji na maoni ni halisi na faafu. Zifuatazo ni baadhi ya mbinu bora za kutumia unapojibu maoni ya watumiaji:

  • Lenga hoja zilizozungumzwa kwenye maoni ya mtumiaji na usiombe upewe ukadiriaji wa juu.
     
  • Jumuisha marejeo ya nyenzo muhimu kama vile anwani ya usaidizi au ukurasa wa Maswali Yanayoulizwa Sana.

Daraja la Maudhui

Madaraja ya maudhui kwenye Google Play hutolewa na Muungano wa Kimataifa wa Ukadiriaji wa Maudhui kulingana na Umri (IARC) na yamebuniwa kuwasaidia wasanidi programu kutoa habari kuhusu madaraja ya maudhui yanayofaa watumiaji katika maeneo waliko. Mamlaka ya kimaeneo ya IARC hudumisha mwongozo ambao hutumika kubaini kiwango cha ukomavu wa maudhui kwenye programu. Haturuhusu programu ambazo hazina daraja la maudhui kwenye Google Play.

Jinsi daraja la maudhui linavyotumika

Daraja la maudhui hutumika kuwafahamisha wateja, haswa wazazi, kuhusu maudhui ambayo huenda hayafai ndani ya programu. Pia, husaidia kuchuja au kuzuia maudhui yako kwenye maeneo au watumiaji mahususi ambapo itahitajika kisheria na kutathmini ufaafu wa programu yako katika mipango maalum ya wasanidi programu.

Jinsi daraja la maudhui linavyokabidhiwa

Ili upokee ukadiriaji wa maudhui, ni lazima ujaze dodoso la ukadiriaji kwenye Dashibodi ya Google Play lililo na maswali kuhusu hali ya maudhui ya programu yako. Programu yako itakabidhiwa daraja la maudhui kutoka mamlaka mbalimbali za ukadiriaji kulingana na majibu utakayojaza kwenye dodoso. Usipotoa maelezo sahihi kuhusu maudhui ya programu yako, inaweza kuondolewa au kusimamishwa. Kwa hivyo, ni muhimu utoe majibu sahihi katika dodoso la ukadiriaji wa maudhui.

Ili kuzuia programu yako isiorodheshwe kuwa “Haijakadiriwa”, ni lazima ujaze dodoso la daraja la maudhui kwa kila programu mpya unayowasilisha kwenye Dashibodi ya Google Play, pamoja na programu zote zilizoko zinazotumika kwenye Google Play. Programu zisizo na daraja la maudhui zitaondolewa kwenye Duka la Google Play.

Ukibadilisha maudhui au vipengele vya programu yako ambavyo vitaweza kuathiri majibu kwenye dodoso ya ukadiriaji, ni lazima uwasilishe dodoso jipya la ukadiriaji wa maudhui katika Dashibodi ya Google Play.

Tembelea Kituo cha Usaidizi ili upate maelezo zaidi kuhusu mamlaka mbalimbali za ukadiriaji na jinsi ya kujaza dodoso la ukadiriaji wa maudhui.

Rufaa za ukadiriaji

Ikiwa unapinga ukadiriaji uliokabidhiwa programu yako, unaweza kukata rufaa moja kwa moja kwa mamlaka ya ukadiriaji ya IARC ukitumia kiungo ulichotumiwa kupitia barua pepe yenye cheti chako.

News

Programu ya Habari ni programu ambayo:

  • Inajibainisha kama programu ya "Habari" kwenye Dashibodi ya Google Play, au
  • Inajiorodhesha katika aina ya programu za “Habari na Magazeti” katika Duka la Google Play na inajieleza kuwa “habari” kwenye jina lake la programu, aikoni, jina la msanidi programu au maelezo.

Mifano ya programu zilizo katika aina ya programu za “Habari na Magazeti” zinazotimiza masharti ya kuwa programu za Habari:

  • Programu zinazojieleza kama "habari" kwenye maelezo ya programu, ikiwa ni pamoja na, lakini si tu:
    • Habari za hivi punde
    • Gazeti
    • Habari zinazojiri
    • Habari za mahali ulipo
    • Habari za kila siku
  • Programu yenye neno “Habari” kwenye majina ya programu, aikoni, au jina la msanidi programu.

Hata hivyo, ikiwa programu zina maudhui yaliyobuniwa kimsingi na mtumiaji (k.m., programu za mitandao ya kijamii), hazipaswi kujibainisha kuwa programu za Habari na hazichukuliwi kuwa ni programu za Habari.

Programu za habari zinazohitaji mtumiaji anunue uanachama ni lazima ziweke toleo la kukagua kwanza maudhui ya ndani ya programu kwa watumiaji kabla ya kununua. 

Ni lazima programu za habari:

  • Zitoe maelezo ya umiliki kuhusu programu na chanzo cha makala ya habari ikiwa ni pamoja na, lakini si tu, mchapishaji halisi au mwandishi wa kila makala. Katika hali ambapo si kawaida kuorodhesha waandishi binafsi wa makala, ni lazima programu ya habari iwe asasi halisi inayochapisha makala husika. Tafadhali kumbuka kwamba viungo vya akaunti za mitandao ya kijamii si njia za kutosha za kutoa maelezo ya mwandishi au mchapishaji. 
  • Ziwe na tovuti au ukurasa maalumu wa ndani ya programu ambao umewekewa lebo kuwa una anwani ya mawasiliano, ni rahisi kupatikana (k.m., imeunganishwa katika sehemu ya chini ya ukurasa wa kwanza au katika sehemu ya viungo muhimu vya tovuti) na inatoa anwani sahihi ya mawasiliano ya shirika la kuchapisha habari, ikijumuisha ama anwani ya barua pepe au nambari ya simu ya mtu wa kuwasiliana naye. Tafadhali kumbuka kuwa viungo vya akaunti za mitandao ya kijamii si njia za kutosha za kutoa anwani ya mawasiliano ya mchapishaji.

Programu za habari hazipaswi:

  • Kuwa na makosa mengi ya tahajia na/au sarufi,
  • Kuwa tu na maudhui ambayo hayabadiliki (k.m., maudhui ambayo yamekuwepo kwa zaidi ya miezi mitatu), au
  • Kuwa na utangazaji wa washirika au mapato ya matangazo kama madhumuni yake ya msingi.  

Tafadhali kumbuka kuwa programu za Habari zinaweza kutumia matangazo na miundo mingine ili kuchuma mapato ilimradi lengo kuu la programu si kuuza bidhaa na huduma au kuzalisha mapato ya utangazaji.

Ni lazima programu za habari ambazo zinajumlisha maudhui kutoka vyanzo tofauti vya uchapishaji ziwe na uwazi kuhusu chanzo cha uchapishaji wa maudhui kwenye programu na ni lazima kila chanzo kitimize mahitaji ya sera za Google News.

Tafadhali soma makala haya ili upate njia bora ya kutoa maelezo yanayohitajika. 


Taka na Utendaji wa Msingi

Ni lazima programu ziwape watumiaji huduma za msingi na hali bora ya utumiaji. Programu zinazoacha kufanya kazi, kuonyesha utendaji ambao haulingani na hali bora ya utumiaji au kutuma taka kwa watumiaji au Google Play, hazileti manufaa yoyote kwenye orodha ya programu.

Taka

Haturuhusu programu zinazotuma taka kwa watumiaji au Google Play. Kwa mfano, programu zinazowatumia watu ujumbe au programu ambazo hawajaomba au programu zinazojirudia au zenye ubora wa chini.

Ujumbe Taka

Haturuhusu programu zinazotuma SMS, barua pepe, au ujumbe mwingine kwa niaba ya mtumiaji bila kumpa mtumiaji uwezo wa kuthibitisha maudhui na mpokeaji anayetumiwa.
Ili kudumisha usalama na heshima kwenye mfumo wa Google Play, tumebuni viwango vinavyobainisha na kuzuia maudhui ambayo hayafai au yanayodhuru watumiaji wetu.
  • Wakati mtumiaji anabonyeza kitufe cha ‘Kushiriki’, programu ilituma ujumbe kwa niaba ya mtumiaji bila kumpa uwezo wa kuthibitisha maudhui na wapokeaji waliolengwa:

Takwimu za Kuangaliwa kwenye Wavuti na Taka Husika

Haturuhusu programu ambazo lengo lake la msingi ni kuelekeza watumiaji kwenye tovuti au kutoa mwonekano wa wavuti bila ruhusa kutoka kwa mmiliki wa tovuti au msimamizi.
Ili kudumisha usalama na heshima kwenye mfumo wa Google Play, tumebuni viwango vinavyobainisha na kuzuia maudhui ambayo hayafai au yanayodhuru watumiaji wetu.
  • Programu ambayo lengo lake la msingi ni kuelekeza watumiaji kwenye tovuti ili kupokea mapato kutokana na watu kujiunga au kununua bidhaa au huduma kwenye tovuti hiyo.
  • Programu ambazo lengo lake la msingi ni kutoa mwonekano wa wavuti bila ruhusa:

         ① Programu hii inaitwa “Ted’s Shopping Deals” na inatoa mwonekano wa wavuti wa Google Shopping.

Maudhui Yanayojirudia

Haturuhusu programu zinazotoa huduma sawa na programu zingine ambazo tayari zinapatikana kwenye Google Play. Programu zinapaswa kuwanufaisha watumiaji kwa kubuni maudhui au huduma za kipekee.
Ili kudumisha usalama na heshima kwenye mfumo wa Google Play, tumebuni viwango vinavyobainisha na kuzuia maudhui ambayo hayafai au yanayodhuru watumiaji wetu.
  • Kuiga maudhui kutoka kwenye programu zingine bila kuongeza thamani au maudhui yoyote mapya.
  • Kuunda programu nyingi zenye maudhui, utendaji na hali ya utumiaji unaofanana sana. Ikiwa kila programu ina maudhui machache, tunawashauri wasanidi programu waunde programu moja inayojumuisha maudhui hayo yote.

Utendaji wa Msingi

Hakikisha kuwa programu yako inatoa hali ya utumiaji ambayo ni bora, thabiti na inayoshirikisha.
Ili kudumisha usalama na heshima kwenye mfumo wa Google Play, tumebuni viwango vinavyobainisha na kuzuia maudhui ambayo hayafai au yanayodhuru watumiaji wetu.
  • Programu ambazo zimebuniwa ili kutofanya kazi wala kutekeleza jukumu lolote

Huduma Zinazokatizwa

Haturuhusu programu zinazoacha kufanya kazi, kulazimisha kufunga, kusitisha shughuli au kufanya kazi kwa njia isiyo ya kawaida.
Ili kudumisha usalama na heshima kwenye mfumo wa Google Play, tumebuni viwango vinavyobainisha na kuzuia maudhui ambayo hayafai au yanayodhuru watumiaji wetu.
  • Programu ambazo hazisakinishwi
  • Programu zinazosakinishwa, lakini hazipakii
  • Programu zinazopakia, lakini hazifanyi kazi

Mipango Mingine

Mbali na kutii sera za maudhui zilizobainishwa kwingineko kwenye Kituo hiki cha Sera, programu ambazo zimebuniwa kwa ajili ya mipango mingine ya Android na kusambazwa kupitia Google Play zinaweza pia kuongozwa na masharti ya sera maalum za programu. Hakikisha kuwa umekagua orodha iliyo hapa chini ili ubaini ikiwa mojawapo ya sera hizi inatumika kwenye programu yako.

Programu za Android zinazofunguka papo hapo

Lengo letu kwa Programu za Android Zinazofunguka Papo Hapo ni kuunda mazingira bora na rahisi kwa watumiaji, na wakati huo huo kutii sera za usalama na faragha kwa kiwango cha juu. Sera zetu zimeundwa kutimiza lengo hilo.

Ni lazima wasanidi programu wanaochagua kusambaza Programu za Android zinazofunguka papo hapo kupitia Google Play watii sera zifuatazo, kando na Sera za Mpango wa Wasanidi Programu.

Kitambulisho

Kwa programu zinazofunguka papo hapo zinazojumuisha kipengele cha maelezo ya kuingia katika akaunti, ni sharti wasanidi programu wajumuishe Smart Lock ya Manenosiri.

Uwezo wa Kutumia Viungo

Wasanidi wa Programu za Android Zinazofunguka Papo Hapo wanapaswa kutoa uwezo unaofaa wa kutumia viungo vya programu zingine. Iwapo programu za msanidi zinazofunguka papo hapo au zilizosakinishwa zina viungo ambavyo vinaweza kuelekeza kwenye programu inayofunguka papo hapo, ni lazima msanidi programu aelekeze watumiaji kwenye programu hiyo inayofunguka papo hapo badala ya, kwa mfano, kufungua viungo katika Mwonekano wa Wavuti.

Maelezo ya Kiufundi

Ni lazima wasanidi programu watii masharti na maelezo ya kiufundi ya Programu za Android zinazofunguka papo hapo, yaliyotolewa na Google, kadri yanavyobadilishwa mara kwa mara, ikiwa ni pamoja na zilizoorodheshwa kwenye hati yetu ya umma.

Kutoa Huduma ya Usakinishaji wa Programu

Programu inayofunguka papo hapo inaweza kumpa mtumiaji programu ambayo anaweza kusakinisha, lakini hili halipaswi kuwa lengo kuu la programu inayofunguka papo hapo. Wasanidi programu wanapotoa huduma ya usakinishaji:

  • Wanapaswa kutumia aikoni ya Usanifu Bora ya "pakua programu" na lebo ya "sakinisha" katika kitufe cha kusakinisha.
  • Hawapaswi kuwa na zaidi ya vidokezo 2-3 vya usakinishaji katika programu yao inayofunguka papo hapo.
  • Hawapaswi kutumia bango au mbinu nyingine inayofanana na matangazo kuwasilisha kidokezo cha usakinishaji kwa watumiaji.

Maelezo ya ziada ya programu inayofunguka papo hapo na mwongozo wa UX yanaweza kupatikana kwenye Mbinu Bora za Hali ya Utumiaji.

Kubadilisha Hali ya Kifaa

Programu zinazofunguka papo hapo hazipaswi kufanya mabadiliko kwenye kifaa cha mtumiaji ambayo yatadumu kwa zaidi ya kipindi ambacho programu inayofunguka papo hapo itatumika. Kwa mfano, programu zinazofunguka papo hapo hazipaswi kubadilisha mandhari ya mtumiaji au kuunda wijeti za skrini ya kwanza.

Kuonekana kwa Programu

Ni lazima wasanidi programu wahakikishe kwamba programu zinazofunguka papo hapo zinaonekana kwa mtumiaji, ili kwamba mtumiaji aweze kujua kila wakati programu inayofunguka papo hapo inapotumika kwenye kifaa chake.

Vitambulishi vya Vifaa

Programu zinazofunguka papo hapo haziruhusiwi kufikia vitambulishi vya vifaa ambavyo (1) vitaendelea kutumika baada ya programu inayofunguka papo hapo kufungwa na (2) mtumiaji hawezi kubadilisha mipangilio yake. Kwa mfano:

  • Nambari ya Muundo
  • Anwani za Mac za chipu zozote za mtandao
  • IMEI, IMSI

Programu zinazofunguka papo hapo zinaweza kufikia nambari za simu ikiwa zilipatikana kupitia ruhusa za muda ambao programu inatumika. Msanidi programu hapaswi kujaribu kukusanya maelezo ya vitambulishi hivi au mbinu nyingine ile kwa kusudi la kumtambua mtumiaji.

Trafiki ya mtandao

Trafiki ya mtandao kutoka ndani ya programu inayofunguka papo hapo inapaswa kusimbwa kwa njia fiche kwa kutumia itifaki ya TLS kama vile HTTPS.

Sera ya Android Emoji

Sera yetu ya emoji imebuniwa ili kuendeleza hali jumuishi na thabiti ya utumiaji. Ili ukamilishe hilo, programu zote lazima zitumie toleo jipya zaidi la Emoji za Unicode zinapotumika kwenye Android 12+. 

Programu ambazo zinatumia Emoji za Android chaguo msingi bila utekelezaji wowote maalumu tayari zinatumia toleo jipya zaidi la Emoji za Unicode zinapotumika kwenye Android 12+. 

Programu zenye utekelezaji wa emoji maalumu, zikijumuisha zile zilizotolewa na maktaba nyingine, ni lazima zitumie toleo jipya zaidi la Unicode zinapotumika kwenye Android 12+ ndani ya miezi minne baada ya kutolewa kwa Emoji mpya za Unicode.

Soma mwongozohuu ili ufahamu jinsi ya kutumia emoji ya kisasa.


Familia

Google Play huwapa wasanidi programu fursa ya kutangaza maudhui yao yenye ubora wa juu na yanayofaa watu wa umri wowote katika familia. Kabla ya kutuma programu kwenye mpango wa Programu za Familia Yote au kutuma programu ambayo inalenga watoto kwenye Duka la Google Play, una wajibu wa kuhakikisha kuwa programu yako inafaa watoto na inatii sheria zote husika.

Pata maelezo kuhusu mchakato wa programu za familia yote na ukague orodha hakikishi inayoshirikisha mtumiaji katika Mafunzo kwa Wasanidi wa Google Play.

Sera za Familia za Google Play

Matumizi ya teknolojia kama zana ya kuimarisha maisha ya familia yanaendelea kuongezeka. Wazazi wanatafuta maudhui salama na yenye ubora wa juu ili washiriki na watoto wao. Huenda unabuni programu zinazolenga watoto au huenda programu yako itawavutia. Google Play inataka kukusaidia uhakikishe kuwa programu yako ni salama kwa watumiaji wote, ikiwa ni pamoja na familia.

Neno "watoto" linaweza kuwa na maana mbalimbali kulingana na lugha na muktadha mbalimbali. Ni muhimu uwasiliane na mwakilishi wako wa kisheria ili akusaidie kubaini wajibu na/au masharti yanayotokana na umri ambayo huenda yanatumika katika programu yako. Unajua vyema jinsi programu yako inavyofanya kazi, kwa hivyo tunakutegemea utusaidie kuhakikisha programu zilizo kwenye Google Play ni salama kwa familia.

Programu zote zinazotii Sera za Familia za Google Play zinaweza kujijumuisha ili kukadiriwa katika Mpango wa Programu Zilizoidhinishwa na Walimu, lakini hatuwezi kukuhakikishia kuwa programu yako itajumuishwa kwenye Mpango wa Programu Zilizoidhinishwa na Walimu. 

Masharti ya Dashibodi ya Google Play

Maudhui na Hadhira Lengwa

Katika sehemu ya Maudhui na Hadhira Lengwa kwenye Dashibodi ya Google Play, ni lazima uonyeshe hadhira inayolengwa na programu yako kabla ya kuchapisha, kwa kuchagua kwenye orodha ya rika zilizopo. Bila kujali mambo ambayo unabaini katika Dashibodi ya Google Play, iwapo utachagua kujumuisha istilahi na picha katika programu yako ambayo inaweza kuchukuliwa kuwa inalenga watoto, hatua hii inaweza kuathiri tathmini ya Google Play ya hadhira lengwa uliyobainisha. Google Play inahifadhi haki ya kufanya ukaguzi wake wenyewe wa maelezo ya programu unayotoa ili kubaini ikiwa hadhira unayolenga ni sahihi.

Unapaswa tu kuchagua zaidi ya kikundi kimoja cha umri wa hadhira inayolengwa na programu yako iwapo umebuni programu yako na kuhakikisha kuwa programu yako inafaa watumiaji katika kikundi ulichochagua. Kwa mfano, programu zilizobuniwa kwa ajili ya watoto wachanga na wa chekechea zinapaswa kuchagua tu kundi lengwa la umri "Usiozidi miaka 5". Iwapo programu yako imebuniwa kwa ajili ya daraja mahususi la shule, chagua kikundi cha umri ambacho kinafaa zaidi daraja hilo la shule. Unapaswa tu kuchagua vikundi vya umri ambavyo vinajumuisha watoto na watu wazima iwapo kwa hakika umebuni programu kwa ajili ya umri wote.

Mabadiliko katika Sehemu ya Maudhui na Hadhira Lengwa

Unaweza kusasisha wakati wowote maelezo ya programu yako katika sehemu ya Maudhui na Hadhira Lengwa kwenye Dashibodi ya Google Play. Sasisho la programu linahitajika kabla maelezo haya yaonyeshwe kwenye Duka la Google Play. Hata hivyo, mabadiliko yoyote ambayo unafanya katika sehemu hii ya Dashibodi ya Google Play yanaweza kukaguliwa ili kubaini iwapo yanatii sera hata kabla ya kuwasilisha sasisho la programu.

Tunakushauri kwa dhati uwaruhusu watumiaji wako wa sasa wajue ukibadilisha kikundi lengwa cha umri cha programu yako au ukianza kutumia matangazo au ununuzi wa ndani ya programu, kupitia sehemu ya "Mambo Mapya" au ukurasa wa programu yako katika Google Play au kupitia arifa za ndani ya programu.

Uwakilishi wa uongo katika Dashibodi ya Google Play

Usipotoa maelezo sahihi kuhusu programu yako katika Dashibodi ya Google Play, ikiwa ni pamoja na sehemu ya Maudhui na Hadhira Lengwa, hali hii huenda ikasababisha kuondolewa au kusimamishwa kwa programu yako, kwa hivyo ni muhimu uweke maelezo sahihi.

Masharti ya Sera ya Familia

Iwapo mojawapo ya hadhira inayolengwa na programu yako ni watoto, ni sharti utii masharti yafuatayo. Iwapo hutii masharti hayo, programu yako inaweza kuondolewa au kusimamishwa.

  1. Maudhui ya programu: Maudhui ya programu yako ambayo yanafikiwa na watoto yanapaswa kuwafaa. Iwapo programu yako ina maudhui yasiyofaa duniani kote, lakini maudhui hayo yanachukuliwa kuwa yanafaa kwa watumiaji watoto katika eneo fulani, programu inaweza kupatikana katika eneo hilo (maeneo machache) lakini haitapatikana katika maeneo mengine.
  2. Utendaji wa programu: Programu yako haipaswi kuweka tu mwonekano wa wavuti wa tovuti au kuwa na lengo la msingi la kuelekeza watumiaji washiriki kwenye tovuti bila ruhusa ya mmiliki wa tovuti au msimamizi.
  3. Majibu kwenye Dashibodi ya Google Play: Ni lazima ujibu kwa usahihi maswali kwenye Dashibodi ya Google Play yanayohusu programu yako na usasishe majibu hayo yaonyeshe kwa usahihi mabadiliko yoyote kwenye programu yako. Hii inajumuisha lakini si tu, kutoa majibu sahihi kuhusu programu yako katika sehemu ya Hadhira Lengwa na Maudhui, Sehemu ya Usalama wa Data na Dodoso la Daraja la Maudhui la IARC.
  4. Kanuni za Data: Lazima ufumbue ukusanyaji wa taarifa yoyote ya binafsi na nyeti kutoka kwa watoto katika programu yako, ikiwa ni pamoja na kupitia API na SDK ulizotaja au ulizotumia katika programu yako. Maelezo nyeti kutoka kwa watoto ni pamoja na, lakini si tu, maelezo ya uthibitishaji, data ya vitambuzi vya maikrofoni na kamera, data ya kifaa, kitambulisho cha Android na data ya matumizi ya matangazo. Pia, unapaswa uhakikishe kwamba programu yako inafuata kanuni za data zilizo hapa chini:
    • Programu zinazolenga watoto pekee hazipaswi kutuma kitambulishi cha matangazo cha Android (AAID), Nambari ya Ufuatiliaji ya SIM, Nambari ya Ufuatiliaji ya Muundo, BSSID, MAC, SSID, IMEI na/au IMSI.
      • Programu zinazolenga watoto pekee hazipaswi kuomba ruhusa ya AD_ID zinapolenga Android kiwango cha API ya 33 au matoleo mapya zaidi.
    • Programu zinazolenga watoto pamoja na hadhira ya watu wazima hazipaswi kutuma AAID, Nambari ya Ufuatiliaji ya SIM, Nambari ya Ufuatiliaji ya Muundo, BSSID, MAC, SSID, IMEI na/au IMSI zinazotoka kwa watoto au watumiaji wenye umri usiojulikana.
    • Nambari ya simu ya kifaa haipaswi kuombwa kutoka kwenye TelephonyManager ya API ya Android.
    • Programu zinazolenga watoto pekee hazipaswi kuomba ruhusa ya mahali au kukusanya, kutumia na kutuma eneo mahususi.
    • Lazima programu zitumie Kidhibiti cha Vifaa Visaidizi (CDM) zinapoomba Bluetooth, isipokuwa programu yako inalenga tu matoleo ya Mfumo wa Uendeshaji (OS) wa kifaa, ambayo hayatumiki kwenye CDM.
  5. API na SDK: Ni lazima uhakikishe kuwa programu yako inatumia vizuri API na SDK.
    • Programu ambazo zinalenga watoto pekee hazipaswi kuwa na API au SDK zozote ambazo hazijaidhinishwa kwa ajili ya huduma zinazolenga watoto.
      • Kwa mfano, Huduma ya API inayotumia teknolojia ya OAuth kwa ajili ya uthibitishaji na uidhinishaji ambayo sheria na masharti yake yanafafanua kuwa haiidhinishwi kwa matumizi katika huduma zinazowalenga watoto.
    • Programu zinazolenga watoto na hadhira za watu wazima hazipaswi kutumia API au SDK ambazo hazijaidhinishwa kwa ajili ya matumizi katika huduma zinazolenga watoto isipokuwa zitumike kupitia skrini ya kuuliza umri au zitumike kwa njia ambayo haitasababisha ukusanyaji wa data kutoka kwa watoto. Programu zinazolenga watoto na hadhira za watu wazima hazipaswi kuhitaji watumiaji wafikie maudhui ya programu kupitia API au SDK ambayo haijaidhinishwa kwa huduma zinazolenga watoto.
  6. Uhalisia Ulioboreshwa (AR): Iwapo programu yako inatumia Uhalisia Ulioboreshwa, lazima ujumuishe onyo la usalama pindi baada ya kufunguka kwa sehemu ya uhalisia ulioboreshwa. Onyo linapaswa kuwa na yafuatayo:
    • Ujumbe unaofaa kuhusu umuhimu wa usimamizi wa wazazi.
    • Ujumbe wa kukukumbusha ujihadhari dhidi ya hatari zilizo katika ulimwengu halisi (kwa mfano, kuwa mwangalifu na mazingira yako).
    • Programu yako haipaswi kuomba kutumia kifaa ambacho hakijapendekezwa kutumiwa na watoto (kwa mfano, Daydream, Oculus).
  7. Vipengele na Programu za Kijamii: Iwapo programu zako zinaruhusu watumiaji kushiriki au kubadilishana habari, lazima ubainishe kwa usahihi vipengele hivi kwenye dodoso la daraja la maudhui katika Dashibodi ya Google Play.
    • Programu za Kijamii: Programu ya kijamii ni programu ambayo lengo lake kuu ni kuwezesha watumiaji kushiriki maudhui ya muundo wowote au kuwasiliana na makundi makubwa ya watu. Programu zote za kijamii ambazo zinajumuisha watoto katika hadhira yake lengwa, lazima zitoe kikumbusho cha ndani ya programu kuhusu kutumia mtandao kwa usalama na tahadhari kuhusu hatari halisi za mawasiliano ya mtandaoni kabla ya kuruhusu watoto kushiriki maelezo au maudhui ya muundo wowote. Lazima pia uombe kitendo cha mtu mzima kabla ya kuruhusu watoto kushiriki taarifa binafsi.
    • Vipengele vya Kijamii: Kipengele cha kijamii ni utendaji wowote wa ziada wa programu ambao huwezesha watumiaji kuwasiliana au kushiriki maudhui ya muundo wowote na makundi makubwa ya watu. Programu yoyote inayojumuisha watoto katika hadhira yake lengwa na ina vipengele vya kijamii, lazima itoe kikumbusho cha ndani ya programu kuhusu kutumia mtandao kwa usalama na tahadhari kuhusu hatari halisi za mawasiliano ya mtandaoni kabla ya kuruhusu watoto kushiriki maelezo au maudhui ya muundo wowote. Lazima pia utoe njia ya watu wazima kudhibiti vipengele vya kijamii kwa ajili ya watoto, ikiwa ni pamoja na, lakini si tu, kuwasha/kuzima kipengele cha kijamii au kuchagua viwango tofauti vya utendaji. Hatimaye, lazima uombe kitendo cha mtu mzima kabla ya kuwasha vipengele vinavyoruhusu watoto kushiriki taarifa binafsi.
    • Kitendo cha mtu mzima kinamaanisha mbinu ya kuthibitisha kuwa mtumiaji si mtoto na hakihimizi watoto kudanganya umri wao ili kupata uwezo wa kufikia maeneo ya programu yako yanayofaa kufikiwa na watu wazima (yaani, PIN, nenosiri, tarehe ya kuzaliwa, barua pepe ya kuthibitisha, kitambulisho chenye picha, kadi ya mikopo au SSN ya mtu mzima).
    • Programu za kijamii ambapo lengo kuu la programu ni kupiga gumzo na watu wasiojulikana hazipaswi kulenga watoto. Mifano ni pamoja na: programu za mtindo wa tovuti ya kupiga gumzo, programu za kuchumbiana, vyumba vya gumzo la wazi vya watoto, n.k.
  8. Kutii sheria: Ni lazima uhakikishe kuwa programu yako, ikiwa ni pamoja na API au SDK zozote ambazo zinataja au kutumia programu yako zinatii Sheria ya Marekani ya Ulinzi na Faragha ya Watoto Mtandaoni (COPPA), Sheria ya Jumla ya Ulinzi wa Data ya Nchi Washirika wa Umoja wa Ulaya (GDPR), na kanuni na sheria nyingine zinazotumika.
Ili kudumisha usalama na heshima kwenye mfumo wa Google Play, tumebuni viwango vinavyobainisha na kuzuia maudhui ambayo hayafai au yanayodhuru watumiaji wetu.
  • Programu ambazo zinatangaza michezo kwa ajili ya watoto katika ukurasa wa programu katika Google Play lakini maudhui ya programu hizo yanafaa tu watu wazima.
  • Programu ambazo zinatumia API ambazo zina sheria na masharti ambayo yanazuia matumizi yake katika programu zinazolenga watoto.
  • Programu ambazo zinahimiza matumizi ya pombe, tumbaku au bidhaa zinazodhibitiwa.
  • Programu ambazo zinajumuisha kamari halisi au iliyoigizwa.
  • Programu ambazo zinajumuisha ukatili au maudhui ya kutisha yasiyowafaa watoto.
  • Programu ambazo hutoa huduma za miadi ya kuchumbiana au kutoa mawaidha ya ngono au ndoa.
  • Programu ambazo zina viungo vinavyoelekeza kwenye tovuti ambazo huonyesha maudhui yanayokiuka Sera za Mpango wa Wasanidi Programu za Google Play.
  • Programu ambazo zinaonyesha matangazo ya watu wazima (kwa mfano, maudhui ya vurugu, maudhui ya ngono, maudhui ya kamari) kwa watoto. 

Matangazo na Uchumaji wa Mapato

Ikiwa unachuma mapato ya programu inayolenga watoto kwenye Google Play, ni muhimu programu yako ifuate Masharti yafuatayo ya Matangazo ya Familia na Sera ya Uchumaji wa Mapato.

Sera zilizo hapa chini zitatumika kwenye uchumaji wa mapato na utangazaji wote katika programu yako, ikiwa ni pamoja na matangazo, kutangaza katika vyombo mbalimbali vya habari (kwenye programu zako na za wengine), ofa za ununuzi wa ndani ya programu au maudhui mengine yoyote ya biashara (kama vile kulipia bidhaa zijumuishwe katika maudhui). Uchumaji wa mapato na utangazaji wote kwenye programu hizi lazima utii kanuni na sheria zote husika (ikiwa ni pamoja na mwongozo wa sekta au wa udhibiti).

Google Play inahifadhi haki ya kukataa, kuondoa au kusimamisha programu zozote zilizo na mbinu za kutangaza biashara kupita kiasi.

Masharti ya matangazo

 Ikiwa programu yako inaonyesha matangazo kwa watoto au watumiaji ambao umri wao haujulikani, ni lazima:

  • Utumie tu SDK za Matangazo ya Familia zenye Uthibitishaji wa Kujifanyia kwenye Google Play ili kuonyesha matangazo kwa watumiaji hao;
  • Uhakikishe kuwa matangazo yanayoonyeshwa kwa watumiaji hao hayajumuishi matangazo yanayotegemea mambo yanayomvutia mtumiaji (matangazo yanayolenga watumiaji walio na tabia fulani kulingana na shughuli zao za kuvinjari mtandaoni) au utangazaji tena (matangazo yanayolenga watumiaji binafsi kulingana na shughuli zao za awali kwenye programu au tovuti); 
  • Uhakikishe kuwa matangazo unayoonyesha watumiaji hao yanawasilisha maudhui ambayo yanawafaa watoto;
  • Uhakikishe kuwa matangazo unayoonyesha watumiaji hao yanafuata masharti ya muundo wa matangazo yanayolenga Familia; na
  • Uhakikishe kuwa umetii kanuni zote za kisheria na viwango vya sekta vinavyohusiana na matangazo yanayolenga watoto.

Masharti ya muundo wa tangazo

Uchumaji wa mapato na utangazaji katika programu yako haupaswi kuwa na maudhui yanayopotosha au kubuniwa kwa njia ambayo itasababisha watoto wayabofye bila kujua.

Ikiwa hadhira lengwa ya programu yako ni watoto pekee, mambo yafuatayo hayaruhusiwi. Ikiwa hadhira lengwa ya programu yako ni watoto na watu wazima, mambo yafuatayo hayaruhusiwi unapoonyesha matangazo kwa watoto au watumiaji wengine ambao umri wao hautambuliki:

  • Uchumaji wa mapato na utangazaji unaokatiza mtumiaji, ikiwa ni pamoja na uchumaji wa mapato na utangazaji ambao unatumia nafasi yote kwenye skrini au kukatiza matumizi ya kawaida na hautoi njia dhahiri ya kuondoa tangazo (kwa mfano, Matangazo ya skrini nzima).
  • Uchumaji wa mapato na utangazaji ambao unakatiza matumizi ya kawaida ya programu au mchezo, ikiwa ni pamoja na matangazo ya zawadi au ya kujijumuisha ambayo hayawezi kufungwa baada ya sekunde tano.
  • Uchumaji wa mapato na utangazaji ambao haukatizi matumizi ya kawaida ya programu au mchezo unaweza kuendelea kuonyeshwa kwa zaidi ya sekunde tano (kwa mfano, maudhui ya video yenye matangazo yaliyojumuishwa).
  • Uchumaji wa mapato na utangazaji unganishi unaoonyeshwa pindi unapofungua programu.
  • Kuonyesha matangazo mengi kwenye ukurasa mmoja (kwa mfano, matangazo ya bango ambayo yanaonyesha ofa nyingi kwenye bango moja au kuonyesha zaidi ya tangazo moja la bango au la video hakuruhusiwi).
  • Uchumaji wa mapato na utangazaji ambao hautofautishwi kwa njia dhahiri na maudhui ya programu yako, kama vile offerwall na hali nyingine za matangazo kwa mtumiaji.
  • Matumizi ya mbinu za kutisha au za ujanja ili kuhimiza utazamaji wa matangazo au ununuzi wa ndani ya programu.
  • Matangazo yanayopotosha yanayomlazimisha mtumiaji kubofya kwa kutumia kitufe cha kuondoa, au kwa kufanya matangazo yaonekane ghafla katika maeneo ya programu ambapo mtumiaji hugusa kwa utendaji mwingine.
  • Kukosa kutenganisha matumizi ya sarafu za michezo pepe na pesa halisi ili kufanya ununuzi wa ndani ya programu.
Ili kudumisha usalama na heshima kwenye mfumo wa Google Play, tumebuni viwango vinavyobainisha na kuzuia maudhui ambayo hayafai au yanayodhuru watumiaji wetu.
  • Uchumaji wa mapato na utangazaji ambao huhepa mtumiaji anapojaribu kuufunga
  • Uchumaji wa mapato na utangazaji ambao haumpi mtumiaji njia ya kufunga ofa baada ya sekunde tano (5) jinsi inavyoonyeshwa katika mfano ulio hapa chini:

     
  • Uchumaji wa mapato na utangazaji ambao hutumia nafasi kubwa ya skrini ya kifaa bila kumpa mtumiaji njia ya kuuondoa, kama inavyoonyeshwa katika mfano ufuatao:

  • Matangazo ya mabango yanayoonyesha ofa nyingi, kama inavyoonyeshwa katika mfano ulio hapa chini:
  • Uchumaji wa mapato na utangazaji ambao unaweza kuchukuliwa na mtumiaji kuwa maudhui ya programu, kama inavyoonyeshwa katika mfano ulio hapa chini:
  • Vitufe, matangazo au uchumaji mwingine wa mapato ambao unatangaza kurasa zingine za programu yako katika Google Play lakini hauwezi kutofautishwa na maudhui ya programu, kama inavyoonyeshwa katika mfano ulio hapa chini:

Ifuatayo ni baadhi ya maudhui ya matangazo yasiyofaa ambayo hayapaswi kuonyeshwa kwa watoto.

  • Maudhui ya Vyombo vya Habari ambayo Hayafai: Matangazo ya vipindi vya televisheni, filamu, muziki, albamu au maudhui mengine ambayo hayafai watoto.
  • Michezo ya Video na Programu Zinazoweza Kupakuliwa ambazo Hazifai: Matangazo ambayo hayafai watoto, yanayotokana na programu zinazoweza kupakuliwa na michezo ya video ya kielektroniki.
  • Bidhaa Hatari au Zinazodhibitiwa: Matangazo ya pombe, tumbaku, bidhaa zinazodhibitiwa, au bidhaa nyingine hatari.
  • Kamari: Matangazo ya kamari ya kuiga, matangazo ya mashindano au bahati nasibu, hata kama hulipishwi kushiriki.
  • Maudhui ya Watu Wazima au Yanayochochea Ngono: Matangazo yaliyo na maudhui ya ngono, yanayochochea ngono na ya watu wazima.
  • Kuchumbiana au Mahusiano: Matangazo ya kuchumbiana au tovuti za mahusiano ya watu wazima.
  • Maudhui ya Vurugu: Matangazo yenye maudhui ya vurugu na ya kuogofya ambayo hayafai watoto.

SDK za Matangazo

Ikiwa unaonyesha matangazo kwenye programu yako na hadhira lengwa inajumuisha watoto tu, basi unapaswa utumie matoleo ya SDK ya matangazo ya Familia yenye uthibitishaji wa kujifanyia pekee. Iwapo hadhira inayolengwa na programu yako inajumuisha watoto na watu wazima, ni lazima uweke hatua za kuchagua umri, kama vile skrini ya kuuliza umri na uhakikishe kuwa matangazo yanayoonyeshwa kwa watoto yanatoka tu kwenye matoleo ya SDK ya matangazo ya Google Play yenye uthibitishaji wa kujifanyia. 

Tafadhali rejelea ukurasa wa Sera ya Mpango wa SDK ya Matangazo ya Familia yenye Uthibitishaji wa Kujifanyia kwa maelezo zaidi kuhusu masharti hayo kisha rejelea hapa ili uone orodha ya sasa ya matoleo ya SDK ya matangazo ya Familia yenye uthibitishaji wa kujifanyia.

Iwapo unatumia AdMob, rejelea Kituo cha Usaidizi cha AdMob ili upate maelezo zaidi kuhusu bidhaa zao.

Ni wajibu wako kuhakikisha kwamba programu yako inatimiza masharti yote yanayohusu matangazo, ununuzi wa ndani ya programu na maudhui ya biashara. Wasiliana na watoa huduma wako wa SDK ya matangazo ili upate maelezo zaidi kuhusu sera zao za maudhui na kanuni za utangazaji.


Sera ya SDK ya Matangazo ya Familia yenye Uthibitishaji wa Kujifanyia

Google Play imedhamiria kukuza hali ya usalama kwa watoto na familia. Lengo kuu ni kuhakikisha watoto wanaona matangazo yanayofaa kwa umri wao na kwamba data yao inashughulikiwa ipasavyo. Ili kufanikisha lengo hili, tunahitaji SDK za matangazo na mifumo ya upatanisho ijithibitishe kuwa inawafaa watoto na inatii Sera za Mpango wa Wasanidi Programu wa Google Play na Sera za Google Play za Familia, ikiwa ni pamoja na Masharti ya Mpango wa SDK ya Matangazo ya Familia yenye Uthibitishaji wa Kujifanyia.

Mpango wa Google Play wa SDK ya Matangazo ya Familia yenye Uthibitishaji wa Kujifanyia wa ni njia muhimu kwa wasanidi programu kubaini aina ya SDK za matangazo au mifumo ya upatanisho iliyojithibitisha kuwa inafaa kutumiwa katika programu zilizosanidiwa mahususi kwa watoto. 

Usipotoa maelezo sahihi kuhusu SDK yako, ikiwa ni pamoja na kwenye fomu ya ombi uliyotuma, hali hii huenda ikasababisha kuondolewa au kusimamishwa kwa SDK yako katika Mpango wa SDK ya Matangazo ya Familia yenye Uthibitishaji wa Kujifanyia, kwa hivyo ni muhimu uweke maelezo sahihi.

Masharti ya sera

Iwapo SDK yako au mfumo unganishi unahudumia programu ambazo ni sehemu ya Programu za Familia za Google Play, ni sharti utii Sera zote za Wasanidi Programu wa Google Play ikiwa ni pamoja na masharti yafuatayo. Kushindwa kutii masharti yoyote ya sera kunaweza kusababisha programu yako iondolewe au kusimamishwa kwenye Mpango wa SDK ya Matangazo ya Familia yenye Uthibitishaji wa Kujifanyia.

Ni wajibu wako kuhakikisha kuwa SDK yako au mfumo unganishi unatii sera, kwa hivyo tafadhali hakikisha unasomaSera za Mpango wa Wasanidi Programu wa Google Play, Sera za Familia za Google Play naMasharti ya Mpango wa SDK ya Matangazo ya Familia yenye Uthibitishaji wa Kujifanyia.

  1. Maudhui ya tangazo:Maudhui ya tangazo lako yanayoweza kufikiwa na watoto yanapaswa kuwa yanayowafaa.
    • Ni lazima (i) ufafanue matendo na maudhui ya matangazo yasiyofaa na (ii) uyazuie kupitia sheria na masharti yako au sera. Ufafanuzi unapaswa kutii Sera za Mpango wa Wasanidi Programu wa Google Play.
    • Ni lazima pia utengeneze mbinu ya kukadiria faili za matangazo yako kulingana na makundi yanayoambatana na umri. Ni lazima makundi yanayoambatana na umri yajumuishe angalau makundi ya 'Kila Mtu' na 'Watu Wazima'. Mbinu ya ukadiriaji inapaswa kuafikiana na mbinu ambayo Google hutoa kwa SDK baada ya kujaza fomu ya ombi.
    • Ni lazima uhakikishe kuwa hali ya uwekaji zabuni katika wakati halisi inapotumika kuonyesha matangazo kwa watoto, faili za matangazo zimekaguliwa na zinatii masharti yaliyo hapo juu.
    • Aidha, lazima uwe na mbinu ya kutambua kihalisi faili za matangazo kwenye orodha yako (kwa mfano, kuweka alama maalum kwenye faili ya matangazo kwa kutumia nembo inayoonekana ya kampuni yako au utendaji kama huo).
  2. Muundo wa tangazo:Ni lazima uhakikishe kuwa matangazo yote yanayoonyeshwa kwa watumiaji watoto yanafuata masharti ya muundo wa tangazo linalolenga Familia na unapaswa uruhusu wasanidi programu wachague miundo ya tangazo inayotii Sera ya Familia ya Google Play.
    • Utangazaji haupaswi kuwa na maudhui yanayopotosha au kubuniwa kwa njia ambayo itasababisha watumiaji watoto wayabofye bila kujua. Matangazo yanayopotosha yanayomlazimisha mtumiaji kubofya kwa kutumia kitufe cha kuondoa, au kwa kufanya matangazo yaonekane ghafla katika maeneo ya programu ambapo mtumiaji hugusa kwa utendaji mwingine hayaruhusiwi.
    • Utangazaji wa kukatiza, ikiwa ni pamoja na utangazaji ambao unatumia nafasi yote kwenye skrini au kukatiza matumizi ya kawaida na hautoi njia dhahiri ya kuondoa tangazo (kwa mfano, Matangazo ya skrini nzima) hauruhusiwi.
    • Utangazaji unaokatiza matumizi ya kawaida ya programu au uchezaji wa mchezo, ikiwa ni pamoja na matangazo yanayotoa zawadi au ya kujijumuisha, lazima uweze kufungwa baada ya sekunde 5.
    • Huruhusiwi kuonyesha matangazo mengi kwenye ukurasa. Kwa mfano, matangazo ya bango ambayo yanaonyesha ofa nyingi kwenye bango moja au kuonyesha zaidi ya tangazo moja la bango au la video hakuruhusiwi.
    • Ni lazima utangazaji uweze kutofautishwa kwa urahisi na maudhui ya programu. Offerwall na hali za matangazo kwa mtumiaji ambayo hayatambuliwi kwa uwazi kama utangazaji na watumiaji watoto hayaruhusiwi.
    • Utangazaji hauruhusiwi kutumia mbinu za kutisha au za ujanja ili kuhimiza utazamaji wa matangazo.
  3. IBA/Utangazaji tena:Ni lazima uhakikishe kuwa matangazo yanayoonyeshwa kwa watumiaji watoto hayajumuishi matangazo yanayotegemea mambo yanayomvutia mtumiaji (matangazo yanayolenga watumiaji walio na tabia fulani kulingana na shughuli zao za kuvinjari mtandaoni) au utangazaji tena (matangazo yanayolenga watumiaji binafsi kulingana na shughuli zao za awali kwenye programu au tovuti).
  4. Kanuni za data:Wewe, mtoa huduma za SDK, unapaswa kuwa mwazi kuhusu jinsi unavyoshughulikia data ya watumiaji (kwa mfano, maelezo yanayokusanywa kutoka kwa mtumiaji au kuhusu mtumiaji ikijumuisha maelezo ya kifaa). Hii inamaanisha kufumbua uwezo wa kufikia wa SDK yako, kukusanya, kutumia na kushiriki data na kudhibiti matumizi ya data kwa madhumuni yaliyofumbuliwa. Masharti haya ya Google Play yanatumika pamoja na masharti yoyote yanayobainishwa na sheria husika za faragha na ulinzi wa data. Lazima ufumbue ukusanyaji wa maelezo yoyote ya binafsi na nyeti kutoka kwa watoto ikiwa ni pamoja na, lakini si tu maelezo ya uthibitishaji, data ya kitambuzi cha maikrofoni na kamera, data ya kifaa, kitambulisho cha Android na data ya matumizi ya matangazo.
    • Ni lazima uwaruhusu wasanidi programu kwa misingi ya kila ombi au kila programu, waombe ruhusa ya ichukuliwe kama inayowalenga watoto katika uonyeshaji wa matangazo. Hali kama hiyo ni lazima itii sheria na kanuni zinazotumika, kama vile Sheria ya Marekani ya Kulinda Faragha ya Watoto Mtandaoni (COPPA) na Sheria ya Jumla ya Ulinzi wa Data (GDPR) ya Umoja wa Ulaya.
      • Google Play inahitaji SDK za matangazo zizime matangazo yaliyowekewa mapendeleo, utangazaji unaotegemea mambo yanayomvutia mtumiaji na kutangaza tena kama sehemu ya hali ya 'ichukuliwe kama inayowalenga watoto'.
    • Ni lazima uhakikishe kuwa hali ya uwekaji zabuni katika wakati halisi inapotumika kuonyesha matangazo kwa watoto, viashirio vya faragha vinapaswa viwe vimetangazwa kwa wanaoweka zabuni.
    • Hupaswi kutuma AAID, Nambari ya Ufuatiliaji ya SIM, Nambari ya Ufuatiliaji ya Muundo, BSSID, MAC, SSID, IMEI na/au IMSI zinazotoka kwa watoto au watumiaji wenye umri usiojulikana.
  5. Mifumo Unganishi: Wakati wa kuonyesha matangazo kwa watoto, ni lazima:
    • Utumie tu SDK za Matangazo za Familia zenye Uthibitishaji wa Kujifanyia au uweke kinga zinazohitajika kuhakikisha kuwa matangazo yote yanayoonyeshwa kutoka kwenye upatanisho yanatii masharti haya; na
    • Utume maelezo yanayohitajika kwenye mifumo ya upatanisho ili kuashiria daraja la maudhui la tangazo na hali yoyote inayotumika ya 'ichukuliwe kama inayowalenga watoto'.
  6. Uthibitishaji unaojifanyia na Kutii:Ni lazima uipatie Google maelezo ya kutosha, kama vile maelezo yaliyobainishwa kwenye fomu ya ombi, ili ithibitishe sera ya SDK ya matangazo inatii masharti yote ya uthibitishaji wa kujifanyia ikiwa ni pamoja na, lakini si tu:
    • Kutoa toleo la Kiingereza la SDK yako au Sheria na Masharti ya Mfumo Unganishi, Sera ya Faragha na Mwongozo wa Ujumuishaji wa Mchapishaji
    • Kutuma sampuli ya programu ya majaribio inayotumia toleo la hivi karibuni la SDK ya matangazo inayotii masharti. Sampuli ya programu ya majaribio inapaswa kuwa APK ya Android iliyosanidiwa kikamilifu na inayoweza kutekelezwa, inayotumia vipengele vyote vya SDK. Masharti ya programu ya majaribio:
      • Ni lazima itumwe kama APK ya Android iliyosanidiwa kikamilifu na inayoweza kutekelezwa, iliyosanidiwa ili itumike kwenye umbo la simu.
      • Ni lazima itumie toleo la SDK ya matangazo ambalo ni jipya zaidi au linalokaribia kuchapishwa linalotii sera za Google Play.
      • Ni lazima itumie vipengele vyote vya SDK ya matangazo yako ikiwa ni pamoja na kutekeleza SDK ya matangazo yako ili kuleta na kuonyesha matangazo.
      • Ni lazima iwe na uwezo kamili wa kufikia hesabu zote za matangazo ya moja kwa moja au yanayoonyeshwa kwenye kituo kupitia faili za matangazo zilizoombwa kupitia programu ya jaribio.
      • Haipaswi kuzuiwa na mchakato wa kutambulisha mahali.
      • Iwapo orodha yako inalenga hadhira ya mseto, ni lazima programu yako ya jaribio iweze kutofautisha kati ya maombi ya faili za matangazo kutoka kwenye orodha kamili na orodha inayowafaa watoto au rika zote.
      • Haipaswi kudhibitiwa kwa matangazo mahususi katika orodha isipokuwa iwe inadhibitiwa na skrini ya kuuliza umri.
  7. Ni lazima ujibu kwa wakati unaofaa maombi yoyote ya maelezo yatakayofuata na ujithibitishie kuwa matoleo yote mapya yanatii Sera za hivi karibuni za Mpango wa Wasanidi Programu wa Google Play, ikiwa ni pamoja na Masharti ya Sera ya Familia.
  8. Kutii sheria: SDK za Matangazo za Familia zenye Uthibitishaji wa Kujifanyia zinapaswa zionyeshe matangazo yanayotii sheria na kanuni zote zinazohusu watoto ambazo zinaweza kutumika kwa wachapishaji husika.

Tafadhali rejelea ukurasa wa Mpango wa SDK ya Matangazo ya Familia yenye Uthibitishaji wa Kujifanyia ili upate maelezo zaidi kuhusu masharti ya Mpango.


Utekelezaji

Kuepuka ukiukaji wa sera ni bora kuliko kudhibiti ukiukaji ukishatokea, lakini ukiukaji unapotokea, tunajitahidi kuhakikisha wasanidi programu wanaelewa jinsi wanavyoweza kutii sera katika programu zao. Tafadhali tufahamishe iwapo utaona ukiukaji wowote au iwapo una maswali yoyote kuhusu kudhibiti ukiukaji.

Mpango wa Sera

Sera zetu za Maudhui hutumika kwa maudhui yoyote yanayoonyeshwa au kuunganishwa na programu yako, ikiwa ni pamoja na matangazo yoyote inayoonyesha kwa watumiaji na maudhui yoyote yanayotokana na mtumiaji inayopangisha au kuunganisha. Zaidi ya hayo, yanatumika kwa maudhui yoyote kutoka kwa akaunti ya msanidi programu yanayoonyeshwa hadharani katika Google Play, ikiwa ni pamoja na jina lako la msanidi programu na ukurasa wa kutua wa tovuti yako ya msanidi programu iliyoorodheshwa.

Haturuhusu programu zinazowaruhusu watumiaji kusakinisha programu zingine kwenye vifaa vyao. Programu zinazotoa idhini ya kufikia programu zingine, michezo au programu zisizohitaji kusakinishwa, ikijumuisha vipengele na huduma zinazotolewa na washirika wengine, lazima zihahakikishe kwamba maudhui yote ambako zinatoa idhini ya kufikia yanatii Sera za Google Play na huenda pia yakapitia ukaguzi wa ziada wa sera.

Masharti yanayotumika katika sera hizi yana maana sawa na Mkataba wa Usambazaji kwa Wasanidi Programu (DDA). Mbali na kutii sera hizi na DDA, maudhui ya programu yako lazima yakadiriwe kulingana na Mwongozo wetu wa Ukadiriaji wa Maudhui.

Haturuhusu programu au maudhui ya programu ambayo yanadunisha imani ya watumiaji katika mfumo wa Google Play. Kwa kukagua iwapo tutajumuisha au kuondoa programu kutoka Google Play, tunazingatia vigezo kadhaa, ikiwa ni pamoja na, lakini si tu mtindo wa madhara au hatari kubwa na matumizi mabaya. Tunatambua hatari ya utumiaji mbaya ikiwa ni pamoja na, lakini si tu vipengee kama vile malalamiko yanayolenga programu na msanidi programu, kuripoti habari, historia ya ukiukaji wa awali, maoni ya watumiaji na matumizi ya chapa, herufi na vipengee vingine maarufu.

Jinsi Google Play Protect hufanya kazi

Google Play Protect hukagua programu unapozisakinisha. Pia hukagua kifaa chako mara kwa mara. Ikipata programu inayoweza kudhuru, inaweza:

  • Kukutumia arifa. Ili uondoe programu, gusa arifa, kisha uguse Ondoa.
  • kuzima programu hadi utakapoiondoa.
  • Kuondoa programu kiotomatiki. Katika hali nyingi, iwapo programu yenye madhara imetambuliwa, utapokea arifa itakayokuarifu kuwa programu iliondolewa.

Jinsi ya kutumia ulinzi dhidi ya programu hasidi

Ili kukulinda dhidi ya programu hatari za kampuni nyingine, URL na matatizo mengine ya usalama, Google inaweza kupokea maelezo kuhusu:

  • Muunganisho wa mtandao wa kifaa chako 
  • URL zinazoweza kuleta madhara 
  • Mfumo wa uendeshaji na programu zilizosakinishwa kwenye kifaa chako kupitia Google Play au vyanzo vingine.

Unaweza kupata onyo kutoka Google kuhusu programu au URL ambayo si salama. Programu au URL inaweza kuondolewa au kuzuiwa isisakinishwe na Google iwapo inatambuliwa kuwa hatari kwa vifaa, data au watumiaji.

Unaweza kuchagua kuzima baadhi ya vipengele hivi vya usalama kwenye mipangilio ya kifaa chako. Lakini Google inaweza kuendelea kupokea maelezo kuhusu programu zinazosakinishwa kupitia Google Play na programu zilizosakinishwa kwenye kifaa chako kutoka vyanzo vingine zinaweza kuendelea kukaguliwa ili kubaini matatizo ya usalama bila kutuma maelezo kwa Google.

Jinsi arifa za Faragha hufanya kazi

Google Play Protect itakuarifu programu ikiondolewa kwenye Duka la Google Play kwa sababu programu inaweza kufikia taarifa yako binafsi na utakua na chaguo la kuiondoa. 


Mchakato wa Utekelezaji

Tunapokagua maudhui au akaunti ili kubaini iwapo si halali au zinakiuka sera zetu, tunazingatia maelezo mbalimbali tunapofanya uamuzi, ikiwemo metadata ya programu (kwa mfano, kichwa cha programu, maelezo), hali ya utumiaji ya ndani ya programu, maelezo ya akaunti (kwa mfano, historia ya matukio ya awali ya ukiukaji wa sera) na maelezo mengine yaliyotolewa kupitia mbinu za kuripoti (panapohusika) na ukaguzi wa kujifanyia.

Ikiwa programu au akaunti yako ya msanidi programu itakiuka sera zetu zozote, tutachukua hatua mwafaka kama ilivyobainishwa hapa chini. Pia, tutakupa maelezo yanayofaa kuhusu hatua tuliyochukua kupitia barua pepe pamoja na maagizo ya jinsi ya kukata rufaa iwapo unaamini kuwa uamuzi wetu una hitilafu.

Tafadhali kumbuka kuwa huenda ilani za uondoaji au za usimamizi zisionyeshe kila tatizo la ukiukaji wa sera lililopo kwenye akaunti, programu au orodha ya programu zako. Ni wajibu wa wasanidi programu kushughulikia matatizo yoyote ya sera na kufanya uhakiki wa ziada ili kuhakikisha kuwa programu au akaunti zao zilizosalia zinatii sera kikamilifu. Kushindwa kushughulikia matatizo ya ukiukaji wa sera kwenye akaunti na programu zako zote kunaweza kusababisha utekelezaji wa hatua za ziada.

Ukiukaji wa mara kwa mara au uliokithiri (kama vile programu hasidi, ulaghai na programu ambazo zinaweza kudhuru mtumiaji au kifaa) wa sera hizi au wa Mkataba wa Usambazaji kwa Wasanidi Programu (DDA) utasababisha kufungwa kwa akaunti mahususi au zinazohusiana na akaunti za Msanidi Programu wa Google Play.

Vitendo vya Utekelezaji 

Hatua tofauti za utekelezaji zinaweza kuathiri programu zako kwa njia tofauti. Tunatumia mchanganyiko wa tathimini ya binadamu na kiotomatiki ili kukagua programu na maudhui ya programu ili kutambua na kuchunguza maudhui yanayokiuka sera zetu na ni hatari kwa watumiaji na mfumo wa Google Play kwa ujumla. Matumizi ya mifumo ya kiotomatiki hutusaidia kutambua matatizo zaidi ya ukiukaji na kutathmini haraka matatizo yanayoweza kutokea, hatua inayosaidia kudumisha usalama wa Google Play kwa ajili ya kila mtu. Maudhui yanayokiuka sera huondolewa na mifumo yetu ya kiotomatiki au, wakati ambapo uamuzi bayana zaidi unahitajika, huripotiwa ili yakaguliwe zaidi na wahudumu na wachanganuzi wenye ujuzi ambao hufanya tathmini ya maudhui, kwa mfano, kwa sababu uelewaji wa muktadha wa sehemu ya maudhui unahitajika. Kisha matokeo ya ukaguzi huu wa binadamu hutumiwa kutengeneza data ya mafunzo ili kuboresha zaidi mifumo yetu ya mashine kujifunza.

Sehemu ifuatayo inaelezea baadhi ya hatua ambazo Google Play inaweza kuchukua na athari zake kwa programu yako na/au kwenye akaunti yako ya Msanidi Programu wa Google Play.

Isipobainishwa vinginevyo kwenye mawasiliano ya utekelezaji, hatua hizi huathiri maeneo yote. Kwa mfano, ikiwa programu yako imesimamishwa, haitapatikana katika maeneo yote. Pia, isipobainishwa vinginevyo, hatua hizi zitaendelea kutekelezwa usipokata rufaa dhidi ya hatua hiyo na rufaa yako ikubalike.

Kukataliwa

  • Programu mpya au sasisho la programu lililotumwa ili likaguliwe halitapatikana kwenye Google Play. 
  • Iwapo sasisho la programu iliyopo lilikataliwa, toleo la programu lililochapishwa kabla ya sasisho bado litapatikana kwenye Google Play.
  • Hali za kukataliwa haziathiri ufikiaji wako wa usakinishaji, takwimu na ukadiriaji wa programu iliyokataliwa ya mtumiaji aliyepo. 
  • Hali ya kukataliwa haiathiri hadhi ya akaunti yako ya Msanidi Programu wa Google Play.

Kumbuka: Usijaribu kutuma tena programu iliyokataliwa hadi urekebishe matukio yote ya ukiukaji wa sera.

Kuondoa

  • Programu, pamoja na matoleo yake ya awali, yameondolewa kwenye Google Play na hayataweza tena kupakuliwa na watumiaji.
  • Kwa sababu programu imeondolewa, watumiaji hawataweza kuona ukurasa wa programu katika Google Play. Maelezo haya yatarejeshwa utakapotuma sasisho linalotii sera la programu iliyoondolewa.
  • Watumiaji hawataweza kufanya ununuzi wowote wa ndani ya programu au kutumia vipengele vyovyote vya Kutozwa kupitia Google Play kwenye programu hadi toleo linalotii sera liidhinishwe na Google Play.
  • Matukio ya kuondolewa kwa programu hayaathiri mara moja hadhi ya akaunti yako ya Msanidi Programu wa Google Play lakini matukio mengi ya kuondolewa kwa programu yanaweza kusababisha kusimamishwa kwa akaunti.

Kumbuka: Usijaribu kuchapisha tena programu iliyoondolewa hadi urekebishe matatizo yote ya ukiukaji wa sera.

Kusimamishwa

  • Programu, pamoja na matoleo yake ya awali, yameondolewa kwenye Google Play na hayataweza tena kupakuliwa na watumiaji.
  • Hatua ya kusimamishwa inaweza kusababishwa na ukiukaji mwingi au uliokithiri wa sera, pamoja na matukio ya mara kwa mara ya kuondolewa au kukataliwa kwa programu.
  • Kwa sababu programu imesimamishwa, watumiaji hawataweza kuona ukurasa wa programu katika Google Play. Maelezo haya yatarejeshwa utakapotuma sasisho linalotii sera.
  • Huwezi tena kutumia APK au App Bundle ya programu iliyosimamishwa.
  • Watumiaji hawataweza kufanya ununuzi wowote wa ndani ya programu au kutumia vipengele vyovyote vya kutozwa kupitia Google Play hadi toleo linalotii sera liidhinishwe na Google Play.
  • Matukio ya kusimamishwa huhesabiwa kama maonyo dhidi ya hadhi nzuri ya akaunti yako ya Msanidi Programu wa Google Play. Maonyo mengi yanaweza kusababisha kufungwa kwa akaunti mahususi na akaunti husika za Msanidi Programu wa Google Play.

Kumbuka: Usijaribu kuchapisha tena programu iliyosimamishwa isipokuwa Google Play iwe imekueleza ufanye hivyo.

Matukio Machache ya Kuonekana

  • Uwezo wa kutambuliwa kwa programu yako kwenye Google Play umedhibitiwa. Programu yako itaendelea kupatikana kwenye Google Play na inaweza kufikiwa na watumiaji kwa kutumia kiungo cha moja kwa moja cha ukurasa wa programu katika Google Play. 
  • Hatua ya kuweka programu yako Ionekane na Wachache haiathiri hadhi ya akaunti yako ya Msanidi Programu wa Google Play. 
  • Hatua ya kuweka programu yako Ionekane na Wachache haiathiri uwezo wa watumiaji kuona ukurasa wa sasa wa programu katika Google Play.

Maeneo Machache

  • Programu yako inaweza kupakuliwa na watumiaji kupitia Google Play pekee katika maeneo fulani.
  • Watumiaji wanaopatikana katika maeneo mengine hawataweza kupata programu kwenye Duka la Google Play.
  • Watumiaji waliosakinisha programu awali wanaweza kuendelea kuitumia kwenye vifaa vyao lakini hawatapokea tena masasisho.
  • Udhibiti wa maeneo hauathiri hadhi ya akaunti yako ya Msanidi Programu wa Google Play.

Hali ya Kuzuiwa kwa Akaunti

  • Akaunti yako ya msanidi programu ikiwa katika hali ya kuzuiwa, programu zote zilizo kwenye orodha ya programu zako zitaondolewa kwenye Google Play na hutaweza tena kuchapisha programu mpya au kuchapisha tena programu zilizopo. Bado utaweza kufikia Dashibodi ya Google Play.
  • Kwa sababu programu zote zimeondolewa, watumiaji hawataweza kuona ukurasa wa programu yako katika Google Play na wasifu wako wa msanidi programu.
  • Watumiaji wako wa sasa hawataweza kufanya ununuzi wowote wa ndani ya programu au kutumia vipengele vyovyote vya kutozwa kupitia Google Play vya programu zako.
  • Bado unaweza kutumia Dashibodi ya Google Play kutoa maelezo zaidi kwa Google Play na kurekebisha maelezo ya akaunti yako.
  • Utaweza kuchapisha tena programu zako utakaporekebisha matatizo yote ya ukiukaji wa sera.

Kufungwa kwa Akaunti

  • Akaunti yako ya msanidi programu inapofungwa, programu zote katika orodha yako zitaondolewa kwenye Google Play na hutaweza tena kuchapisha programu mpya. Hii pia inamaanisha kuwa akaunti zozote zinazohusiana na Akaunti ya Msanidi Programu wa Google Play zitafungwa kabisa.
  • Matukio mengi ya kusimamisha akaunti au kusimamishwa kutokana na ukiukaji wa sera kupita kiasi kunaweza pia kusababisha kufungwa kwa akaunti yako ya Dashibodi ya Google Play.
  • Kwa sababu programu zilizo kwenye akaunti iliyofungwa huondolewa, watumiaji hawataweza kuona ukurasa wa programu yako katika Google Play na wasifu wako wa msanidi programu.
  • Watumiaji wako wa sasa hawataweza kufanya ununuzi wowote wa ndani ya programu au kutumia vipengele vyovyote vya kutozwa kupitia Google Play vya programu zako.

Kumbuka: Akaunti yoyote mpya utakayojaribu kufungua pia itafungwa (bila kurejeshewa ada ya usajili wa msanidi programu), kwa hivyo tafadhali usijaribu kufungua akaunti mpya ya Dashibodi ya Google Play iwapo mojawapo ya akaunti zako nyingine imefungwa.

Akaunti Zisizotumika

Akaunti zisizotumika ni akaunti za wasanidi programu ambazo hazifanyi kazi au zimetelekezwa. Akaunti zisizotumika haziko katika hadhi nzuri kwa mujibu wa Mkataba wa Usambazaji kwa Wasanidi Programu.

Akaunti za Wasanidi Programu wa Google Play zinalenga wasanidi walio na akaunti zinazotumika wanaochapisha na kuendelea kudumisha programu. Ili kuzuia matumizi mabaya, tunafunga akaunti ambazo hazitumiki au hazifanyi kazi au vinginevyo zisizotumika mara kwa mara (kwa mfano, kwa uchapishaji pamoja na kusasisha programu, kufikia takwimu au kudhibiti kurasa za programu katika Google Play).

Hatua ya kufunga akaunti isiyotumika itafuta akaunti yako na data yoyote inayohusiana na akaunti hiyo. Utapoteza na hutarejeshewa ada ya usajili. Kabla tufunge akaunti isiyotumika, tutakuarifu kupitia maelezo ya mawasiliano uliyotoa kwenye akaunti hiyo. 

Kufungwa kwa akaunti isiyotumika hakutakuzuia kufungua akaunti mpya baadaye ikiwa utaamua kuchapisha katika Google Play. Hutaweza kuifungua upya akaunti yako na data au programu zozote za awali hazitapatikana katika akaunti mpya.  


Kudhibiti na Kuripoti Ukiukaji wa Sera

Kukata Rufaa Dhidi ya Hatua ya Utekelezaji

Tutarejesha programu iwapo hitilafu ilifanywa, na tukibaini kuwa programu yako haikiuki Sera za Mpango na Mkataba wa Usambazaji kwa Wasanidi Programu wa Google Play. Iwapo ulikagua sera kwa umakini na unahisi kuwa huenda uamuzi wetu ulikuwa na hitilafu, tafadhali fuata maagizo yaliyotolewa kwenye arifa ya barua pepe au bofya hapa ili ukate rufaa dhidi ya uamuzi wetu. 

Nyenzo Zaidi

Iwapo unahitaji maelezo zaidi kuhusu hatua ya utekelezaji au ukadiriaji/maoni kutoka kwa mtumiaji, unaweza kurejelea baadhi ya nyenzo zilizo hapa chini au uwasiliane nasi kupitia Kituo cha Usaidizi cha Google Play. Hatuwezi, hata hivyo, kukupa ushauri wa kisheria. Iwapo unahitaji ushauri wa kisheria, tafadhali wasiliana na mshauri wako wa kisheria.


Masharti ya Dashibodi ya Google Play

Google Play inataka kutoa hali salama na bora kwa watumiaji na fursa nzuri itakayowasaidia wasanidi programu wetu wote wafanikiwe. Tunajitahidi kuhakikisha kuwa mchakato wa kufanya programu yako ipatikane kwa watumiaji ni rahisi iwezekanavyo.

Ili kukusaidia kuepuka ukiukaji wa mara kwa mara, hakikisha kuwa unafanya yafuatayo unapowasilisha maelezo kupitia Dashibodi ya Google Play na wasifu wowote ambao umeunganishwa kwenye akaunti yako ya msanidi programu katika Dashibodi ya Google Play.

Kabla utume programu yako, lazima:

  • Utoe maelezo sahihi ya akaunti yako ya msanidi programu, ikiwa ni pamoja na maelezo yafuatayo:
    • Jina la kisheria na anwani
    • Nambari ya D-U-N-S, ikiwa unajisajili kama shirika
    • Anwani ya barua pepe na nambari ya simu ya unayewasiliana naye
    • Anwani ya barua pepe ya msanidi programu na nambari ya simu inayoonyeshwa kwenye Google Play inapohitajika
    • Mbinu za malipo inapohitajika
    • Taarifa ya malipo kwenye Google iliyounganishwa na akaunti yako ya msanidi programu
  • Ikiwa unajisajili kama shirika, hakikisha kwamba maelezo ya akaunti yako ya msanidi programu yamesasishwa na yanalingana na maelezo yaliyohifadhiwa kwenye wasifu wako wa Dun & Bradstreet
  • Utoe maelezo na metadata yote ya programu kwa usahihi
  • Upakie sera ya faragha ya programu yako na ujaze Sehemu ya masharti ya usalama wa data
  • Uweke akaunti ya onyesho inayotumika, maelezo ya kuingia katika akaunti na nyenzo zingine zote zinazohitajika ili Google Play ikague programu yako (hasa, vitambulisho vya kuingia katika akaunti, misimbo ya QR, n.k.)

Kama kawaida, unapaswa kuhakikisha kuwa programu yako inatoa hali ya utumiaji ambayo ni thabiti, inashirikisha na inaweza kubadilika; hakikisha kuwa kila kitu kwenye programu yako, ikiwa ni pamoja na mitandao ya matangazo, huduma za takwimu na SDK za wengine, zinatii Sera za Mpango wa Wasanidi Programu wa Google Play; na iwapo hadhira lengwa ya programu yako inajumuisha watoto, hakikisha kuwa inatii Sera yetu ya familia.

Kumbuka, ni wajibu wako kukagua Mkataba wa Usambazaji kwa Wasanidi Programu na Sera zote za Mpango wa Wasanidi Programu ili kuhakikisha kuwa programu yako inatii masharti kikamilifu.


Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
10373716551026790312
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false