Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi YouTube inavyokufaa

Iwe unafuatilia ari au biashara, tunafahamu unatumia muda na nguvu nyingi kutayarisha maudhui yanayowasilishwa kwenye YouTube. Ni muhimu kwako kuelewa jinsi maudhui yako yanavyogunduliwa pamoja na utendaji wake. Kama watayarishi, ninyi ni kiini cha jumuiya yetu, kwa hivyo kuwasiliana nanyi pamoja na uwazi husalia kuwa kipaumbele chetu. Tumejitolea kusaidia mafanikio yako. Ndiyo maana tumeunganisha rasilimali kadhaa nzuri zinazoelezea:

Maudhui yako kwenye YouTube

Utafutaji kwenye YouTube

Kipengele cha Utafutaji kwenye YouTube huvipatia kipaumbele vipengele vikuu vichache ili kukupatia matokeo bora zaidi ya utafutaji, ikijumuisha ufaafu, ushirikishaji na ubora. Ili kukadiria ufaafu, tunaaangalia vigezo vingi, kama vile jinsi jina, lebo, maelezo na maudhui ya video yanavyolingana na hoja ya utafutaji ya mtazamaji. Ishara za ushirikishaji ni njia muhimu ya kubaini ufaafu na tunajumuisha ishara za jumla za ushirikishaji kutoka kwa watumiaji. Kwa mfano, tunaweza kuangalia muda wa kutazama video fulani kwa hoja fulani ili kubaini ikiwa watumiaji wengine wanachukulia video hiyo kuwa inayofaa kwa hoja husika. Kuhusu ubora, mifumo yetu imebuniwa ili iweze kutambua ishara zinazoweza kubaini vituo vinavyoonyesha utaalamu na uaminifu kwenye mada husika. YouTube haikubali malipo ili kuweka maudhui katika nafasi bora kwenye matokeo halisi ya utafutaji.

Katika vipengele kama vile muziki au burudani, mara nyingi tunatumia vipengele vya ziada kama vile upya au umaarufu ili kusaidia mifumo yetu kuunganisha watumiaji kwenye maudhui bora watakayofurahia. Katika maeneo fulani ambapo uaminifu ni muhimu, ikiwa ni pamoja na habari, siasa na matibabu au maelezo ya kisayansi, tunafanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha kuwa mifumo yetu ya utafutaji inatanguliza kuonyesha maudhui yenye ubora wa juu na yanayoaminika kutoka vyanzo vya kuaminika.

Kadi Rasmi pia hufanya iwe rahisi kwa watumiaji kugundua maudhui kwa kuangazia nyenzo rasmi katika Utafutaji kwenye YouTube. Kadi hizi ni pamoja na video na machapisho rasmi kutoka vituo maarufu, kama vile vya watayarishi maarufu wa YouTube, watu mashuhuri na wasanii maarufu wa muziki. Video na machapisho pia hutoka kwenye maudhui yanayohusiana na timu za michezo, filamu na TV, muziki na matukio maalum. Kadi hizi hutolewa kiotomatiki na haziruhusu kuwekewa mapendeleo.

Lengo letu ni kukupa nyenzo za kukusaidia kuelewa mambo tunayozingatia ili kuwapatia watumiaji matokeo bora zaidi ya utafutaji.

Nyenzo zaidi

Video zinazopendekezwa

Tunaanza kwa kufahamu kuwa kila mtu ana mazoea ya kipekee ya utazamaji. Kisha mfumo wetu hulinganisha namna mtazamaji anavyotazama na tabia zinazofanana. Mfumo hutumia maelezo hayo kupendekeza maudhui mengine ambayo mtazamaji anaweza kutaka kutazama.

Mfumo wetu wa mapendekezo unaendelea kubadilika, kwa kujifunza kila siku kutokana na zaidi ya vipengee bilioni 80 vya maelezo tunavyoviita ishara, vya msingi vikiwa:

  • Historia ya video ulizotazama: Mfumo wetu hutumia video za YouTube zinazotazamwa na watazamaji ili kuwapa mapendekezo bora zaidi, kukumbuka walikoachia kutazama na zaidi.
  • Historia ya mambo uliyotafuta:  Mfumo wetu hutumia mambo yanayotafutwa na mtazamaji kwenye YouTube ili kutoa mapendekezo ya siku zijazo.
  • Vituo unavyofuatilia: Mfumo wetu hutumia maelezo kuhusu vituo vya YouTube ambavyo mtazamaji anafuatilia ili kupendekeza video zingine ambazo huenda akazipenda.
  • Alama za imenipendeza: Mfumo wetu hutumia maelezo ya alama za imenipendeza ili kujaribu kutabiri uwezekano kwamba mtazamaji atavutiwa na video kama hizi katika siku zijazo.
  • Alama za haijanipendeza: Mfumo wetu hutumia video ambazo mtumiaji aliziwekea alama ya haijanipendeza ili kuzuia hatua ya kupendekeza video kama hizo katika siku zijazo.
  • Chaguo za maoni ya "Sijavutiwa": Mfumo wetu hutumia video ambazo watumiaji huziwekea alama ya "Sijavutiwa" ili kuamua ni maudhui gani ya kuzuia kupendekeza katika siku zijazo. 
  • Chaguo za maoni za “Usipendekeze kituo”: Mfumo wetu hutumia chaguo za maoni za “Usipendekeze kituo” kama ishara kwamba huenda maudhui ya kituo si kitu ambacho mtazamaji alifurahia kutazama.
  • Tafiti za kuridhika kwa watumiaji: Mfumo wetu hutumia tafiti za watumiaji ambazo huwaomba watazamaji wakadirie video walizotazama, jambo ambalo husaidia mfumo kuelewa kiwango cha kuridhika, si tu muda wa kutazama.

Vipengele tofauti vya YouTube hutegemea ishara fulani za mapendekezo kuliko vingine. Kwa mfano, tunatumia video ambayo mtazamaji anatazama kwa sasa kama ishara kuu tunapopendekeza video ya kucheza inayofuata. Ili kutoa mapendekezo ya video kwenye ukurasa wa kwanza, tunategemea historia ya video alizotazama mtazamaji. Watazamaji wanaweza kuzima na kufuta historia ya video walizotazama ikiwa hawapendi kuona mapendekezo kwenye ukurasa wao wa kwanza. Kwa watu waliozima kipengele cha historia ya video ulizotazama kwenye YouTube na wasio na historia ya kutosha ya video ulizotazama hapo awali, ukurasa wa kwanza utaendelea kuonyesha upau wa kutafutia na menyu ya upande wa kushoto ya Mwongozo. 

Kupunguza uenezaji wa maudhui yanayokaribia kukiuka sera na maelezo hatari ya kupotosha 

Wajibu wetu kuhusu uwazi unamaanisha kuwa tunaweza kuwa na maudhui yanayopatikana kwenye mfumo, yanayokaribia kukiuka sera zetu lakini hayakiuki. Tunafikiri kuwa ni muhimu kulinda uhuru wa kujieleza, lakini tumeweka kiwango cha juu kwa video tunazoonyesha mara kwa mara kwenye mapendekezo yetu katika ukurasa wa kwanza wa YouTube au kwenye kidirisha cha "Inayofuata". 

Ndiyo maana tunachukua hatua ya ziada ya kupendekeza video za kuaminika kwa watazamaji kuhusu mada kama vile habari, siasa, matibabu na maelezo ya kisayansi.

Tunategemea wakaguzi, waliopewa mafunzo kwa kutumia mwongozo unaopatikana hadharani, ambao hukagua ubora wa maelezo katika kila kituo na video. Ili kuamua iwapo video ni ya kuaminika, wakaguzi huangalia vigezo kama vile utaalamu na sifa ya anayezungumza au kituo, mada kuu ya video, na iwapo maudhui yanatimiza ahadi yake au kutimiza lengo lake. Kadri video inavyoaminika, ndivyo itakavyotangazwa katika mapendekezo. Tunajitahidi kila mara kuboresha mifumo yetu ili kukuza maudhui kutoka kwenye vyanzo vya kuaminika, kama vile vyombo vya habari na taasisi za afya. 

Nyenzo zaidi

Uhusiano wako na YouTube

Mkataba wako na YouTube

Matumizi yote ya huduma yanategemea Sheria na Masharti ya YouTube, Mwongozo wetu wa Jumuiya na Sera zetu za Mfumo.

Kumbuka kuwa sera zaidi zitatumika pia ukiwasha vipengele fulani kama vile uchumaji wa mapato, kutiririsha mubashara au Ununuzi. Usisahau kwamba ikiwa unatoa utangazaji au udhamini kwa huduma au unajumuisha matangazo yanayolipiwa kwenye maudhui yako, pia unakubali kufuata sera zetu za matangazo kwa watangazaji. Unaweza kusoma sera zetu zote wakati wowote kwa kutafuta kwenye Kituo chetu cha Usaidizi.

Unaweza kupata mikataba mingi ya sasa mtandaoni ambayo ilikubaliwa kwenye Studio ya YouTube.

Kuwasiliana na YouTube

Kama sehemu ya lengo letu linaloendelea la kuboresha uwazi na mawasiliano yetu na washirika wetu, tunajitahidi kila wakati kukuarifu kuhusu mabadiliko ambayo huenda tukahitaji kuyafanya ambayo yanaweza kukuathiri. Iwe unakabiliwa na tatizo mahususi, unahitaji usaidizi wa kusuluhisha masuala ya kiufundi au ungependa kufahamu jinsi ya kunufaika zaidi na YouTube, tuko hapa kukuhudumia. Unaweza kuwasiliana na timu ya Usaidizi kwa Watayarishi au Msimamizi wako wa Washirika. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu jinsi tunavyowasiliana nawe hapa.

Kuchuma mapato kwenye YouTube

Mpango wa Washirika wa YouTube

Tunapanua Mpango wa Washirika wa YouTube (YPP) kwa watayarishi wengi zaidi kwa kuwapa uwezo wa kufikia mapema vipengele vya Ununuzi na ufadhili kutoka kwa mashabiki. Mpango wa Washirika wa YouTube uliopanuliwa unapatikana kwa watayarishi wanaostahiki katika nchi au maeneo haya. Upanuzi utasambazwa mwezi ujao kwa watayarishi wanaostahiki nchini AE, AU, BR, EG, ID, KE, KY, LT, LU, LV, MK, MP, MT, MY, NG, NL, NO, NZ, PF, PG, PH, PT, QA, RO, RS, SE, SG, SI, SK, SN, TC, TH, TR, UG, VI, VN, and ZA. Soma makala haya ili upate maelezo zaidi kuhusu mabadiliko kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube.

Ikiwa huishi katika mojawapo ya nchi au maeneo yaliyotajwa hapo juu, hakuna mabadiliko kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube yanayokuhusu. Unaweza kusoma makala haya ili upate muhtasari wa Mpango wa Washirika wa YouTube, masharti ya kujiunga na maagizo ya kutuma ombi yanayokufaa.

Angalia iwapo unastahiki kushiriki kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube uliopanuliwa. Iwapo bado hujastahiki, chagua Pata arifa katika sehemu ya Chuma mapato ya Studio ya YouTube. Tutakutumia barua pepe tutakapokusambazia Mpango wa Washirika wa YouTube uliopanuliwa na utakapokuwa umetimiza masharti ya upeo wa kutimiza masharti. 


Ukiwa sehemu ya Mpango wa Washirika wa YouTube, unastahiki kufikia njia nyingi za mapato, ilimradi tu zinapatikana katika nchi au eneo uliko na unatimiza vigezo. Unaweza pia kufikia usaidizi wa watayarishi na Copyright Match Tool. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu mpango, jinsi unavyofanya kazi na jinsi ya kutuma ombi hapa.

Kuchuma mapato kupitia Kituo cha YouTube Music

Iwapo wewe ni lebo, mchapishaji, msambazaji au mwanamuziki binafsi, YouTube inaweza kukusaidia kufikia mashabiki zaidi na kuongeza mapato. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi YouTube inavyoweza kukusaidia kuchuma mapato kutokana na muziki wako kupitia matangazo, usajili na vyanzo vingine vya mapato hapa. Pata maelezo zaidi kuhusu zana na mikakati inayoweza kunyumbuliwa ya kuwasilisha muziki wako na kudhibiti haki zako dijitali kwenye YouTube hapa.

Ufadhili kutoka kwa mashabiki 

Super Chat na Super Stickers ni njia za watayarishi kuwasiliana na mashabiki wakati wa mitiririko mubashara na Maonyesho ya Kwanza. Mashabiki wanaweza kununua Super Chats ili kuangazia ujumbe wao ndani ya gumzo la moja kwa moja au Super Stickers ili kupata picha ya uhuishaji inayoonekana katika gumzo la moja kwa moja. Iwapo unastahiki, pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuwasha Super Chat au Super Stickers na jinsi unavyoweza kudhibiti vipengele hivi.

Shukrani Moto huruhusu watayarishi kuchuma mapato kutoka kwa watazamaji wanaotaka kuonyesha shukrani za ziada kwa Video zao Fupi na ndefu. Mashabiki wanaweza kununua uhuishaji wa mara moja na kuchapisha maoni ya kipekee, yaliyowekewa mapendeleo kwenye sehemu ya maoni ya video au Video fupi. Iwapo unastahiki, fahamu jinsi ya kuwasha na kudhibiti Shukrani Moto kwenye kituo chako.

Uanachama katika kituo huwawezesha watazamaji kujiunga na kituo chako kupitia malipo ya kila mwezi na kupata manufaa ya wanachama pekee kama vile beji, emoji na manufaa mengine. Iwapo unastahiki, pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuwasha uanachama na jinsi unavyoweza kudhibiti uanachama katika kituo chako.

Kuuza bidhaa kwenye YouTube

Pia, tunawapa wamiliki wa vituo wanaostahiki fursa ya kuonyesha bidhaa zao na bidhaa rasmi zenye chapa kwenye YouTube. Kuanza kutumia Ununuzi kupitia YouTube.

Na iwapo wewe ni msanii wa muziki kwenye YouTube, unaweza pia kustahiki kuonyesha orodha ya matamasha yako yajayo kwenye YouTube. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuweka tiketi za tarehe za ziara yako kwenye video hapa.

Utendaji wako kwenye YouTube

YouTube ni sehemu ya Google na inatii kanuni na sera za faragha za Google. Unapotumia huduma zetu, iwe kama mtumiaji au kama mshirika, unaamini kuwa tutalinda taarifa zako. Tunaelewa jinsi data ilivyo muhimu katika kupima mafanikio yako kwenye YouTube. Tunahakikisha kuwa mbinu zetu zinalingana na Sera yetu ya Faragha ili kulinda faragha na usalama wa watumiaji na washirika wetu.

YouTube hutoa vifurushi vya zana vya kupima utendaji wako ili ikusaidie unufaike zaidi na data yako. Ukiiruhusu, tunatoa idhini ya kufikia data ya Takwimu za YouTube kwa wamiliki wa maudhui na chaneli ya YouTube. Pata maelezo zaidi kuhusu aina za ripoti zinazoweza kufikiwa na chaneli ya YouTube na wamiliki wa maudhui kupitia API hizi. Pia, tuna vipengele vya takwimu, Takwimu za YouTube na Takwimu za YouTube kwa Wasanii, vilivyoundwa moja kwa moja kwenye mfumo, ili kukuruhusu kufikia vipimo vya utendaji, kama vile: 

  • Muda wa kutazama: Muda ambao watazamaji wametazama video.
  • Wanaofuatilia: Idadi ya watazamaji wanaofuatilia chaneli yako.
  • Utazamaji: Idadi halali ya mara ambazo chaneli na video zako zilitazamwa.
  • Video maarufu: Video zinazofanya vizuri zaidi.
  • Muda wa kutazama: Tazama jinsi video yako inavyovutia hadhira yako.
  • Data ya Mtiririko MubasharaAngalia idadi ya watazamaji ambao wametazama mtiririko wako katika video yako yote.
  • Demografia: Watazamaji wako ni akina nani, ikijumuisha takwimu kuhusu umri, jinsia yao na mahali walipo.
  • Vyanzo vya watazamaji: Kipimo hiki hukusaidia uelewe jinsi watazamaji wako walipata maudhui yako.

Pia, tunachapisha baadhi ya takwimu za chaneli na video, kama vile idadi iliyojumlishwa ya wanaofuatilia chaneli na mara ambazo video imetazamwa, hadharani kwenye ukurasa wa chaneli yako, ukurasa wa kutazama, tovuti zinazovuma za YouTube, Takwimu za YouTube kwa Wasanii, Maarifa na chati za muziki na kupitia huduma za API. Pia, tunaweza kushiriki data iliyojumlishwa, isiyotambulisha majina ya kituo na video na watangazaji, washirika wa mauzo na wenye hakimiliki, kulingana na Sera ya Faragha ya Google. Kwa mfano, tunaweza kusema kwamba idadi ya video zinazohusu siha imeongezeka mara mbili kwa mwaka uliopita katika nchi au eneo fulani..

Aina mahususi za data pia zinaweza kushirikiwa unapochagua kutumia vipengele fulani vya YouTube. Kwa mfano, ukimuunganisha muuzaji wako rasmi wa bidhaa za rejareja na chaneli yako ya YouTube, data ya takwimu inayohusiana na mauzo na mara za utembeleaji itashirikiwa baina ya Google na muuzaji wa rejareja. Tutakujulisha kila wakati jinsi data inavyoweza kushirikiwa pamoja na sheria na masharti ya programu yako.

Timu fulani za YouTube, kama vile zile zinazohusika katika utekelezaji wa uaminifu na usalama wa YouTube, zinaweza kuwa na idhini ya kufikia takwimu za kituo na video ambazo ni tofauti au zenye maelezo zaidi kuliko zile zinazotolewa kupitia mfumo wa Takwimu za YouTube au huduma za API. Kwa mfano, mifumo ya YouTube ya kugundua taka na ukiukaji wa usalama inaweza kukagua chanzo cha watazamaji wa tovuti na takwimu kwa kina ili kugundua tabia isiyo ya kawaida na kupata watu wanaojaribu kuongeza hesabu za mara za utazamaji wa video au idadi ya wanaofuatilia katika ukiukaji wa Sheria na Masharti ya YouTube.

Tunaendelea kubuni mbinu mpya za kuzipa biashara na watangazaji maarifa sahihi na yanayoweza kutekelezwa, hasa utazamaji unapobadilika kwenye mifumo na vifaa mbalimbali. Tunahakikisha kuwa mbinu hizi zinafuata Sera yetu ya Faragha ili kulinda faragha na usalama wa watumiaji wetu. Unaweza kusoma maelezo zaidi kuhusu jinsi tunavyohifadhi data hii ikiwa utaacha kutumia huduma zetu kama sehemu ya sera yetu ya kuhifadhi data.

Unaweza kufikia usaidizi kuhusu jinsi ya kunufaika zaidi na data yako kwa kuwasiliana na timu ya Usaidizi kwa Watayarishi. Kila wakati tunakubali maoni kutoka kwako kuhusu zana unazofaidika nazo zaidi.

Jinsi tunavyosaidia vipaji vipya

Kama sehemu ya ahadi yetu ya kusaidia watayarishi na wasanii wetu wanaochipukia, tunatekeleza mipango mara kwa mara ili kusaidia ukuaji wao. Hii inaweza kujumuisha kutoa idhini ya kufikia studio zetu nzuri kwenye Studio za YouTube, kambi za mafunzo kama vile NextUp na ufadhili mahususi wa biashara mpya ili kusaidia utayarishaji wa maudhui mapya. Ili kupata usaidizi huu, watayarishi na wasanii wetu wanaahidi kutengeneza maudhui ya kipekee ya YouTube ili watumiaji wetu wafurahie.

Nyenzo zaidi

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
10708950745428879231
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false