Kupakia video za YouTube

Kipengele kipya cha kina kwenye YouTube: Kuanzia tarehe 17 Agosti, 2023, badilisha Video zako Fupi ili ujumuishe kiungo kwenye video nyingine moja kutoka katika kituo chako. Kiungo kitaonekana kwenye kichezaji cha Video Fupi na kitasaidia kuelekeza watazamaji kutoka kwenye Video Fupi kwenda katika maudhui yako mengine ya YouTube. Unaweza kuunganisha Video, Video Fupi na maudhui ya Moja kwa Moja. Video unayochagua inapaswa kuwa ya umma au iwe haijaorodheshwa na isikiuke Mwongozo wetu wa Jumuiya. Badiliko hili litasambazwa taratibu na huenda lisipatikane kwenye vituo au kwa watazamaji wote hadi kipengele kitakaposambazwa kabisa.

Unaweza kupakia video kwenye YouTube kwa kufuata hatua chache rahisi. Tumia maagizo yaliyo hapa chini ili upakie video zako kutoka kwenye kompyuta au kifaa cha mkononi. Huenda usiweze kupakia ikiwa matumizi yako yanasimamiwa kwenye YouTube. Pata maelezo zaidi hapa.

Kupakia video katika Studio ya YouTube

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Katika kona ya juu kulia, bofya UNDA  kisha Pakia video .
  3. Chagua faili ambayo ungependa kupakia. Unaweza kupakia hadi video 15 kwa wakati mmoja. Hakikisha unabofya Badilisha kwenye kila faili ili ubadilishe maelezo ya video yako.

Kumbuka: Video yako itageuzwa ili iwe ya ubora wa juu zaidi unaopatikana ili kuhakikisha inaweza kuchezwa kwenye mitandao na vifaa tofauti. Unaweza kuangalia muda unaokadiriwa wa uchakataji wa video za ubora wa SD, HD na 4K. Video za ubora wa juu zaidi kama vile 4K au HD zinaweza kuchukua muda mrefu zaidi kuchakatwa. Pata maelezo zaidi kuhusu ubora wa video baada ya kupakia na uwiano na ubora wa video. Ikiwa unatatizika, angalia mwongozo wetu wa hitilafu za kawaida za upakiaji.

Ukifunga hali ya upakiaji kabla ya kukamilisha kuchagua mipangilio yako, video yako itahifadhiwa kama ya faragha kwenye ukurasa wako wa Maudhui.

Maelezo
Weka maelezo muhimu kwenye video yako. Kumbuka: Unaweza kubofya TUMIA MAELEZO TENA ili unakili maelezo mahususi kutoka kwenye video uliyopakia awali.
Mada

Mada ya video yako.

Kumbuka: Mada za video zinaruhusiwa kuwa na idadi ya juu ya herufi 100 na haziwezi kujumuisha herufi zisizoruhusiwa.

Maelezo

Maelezo yanayoonyeshwa chini ya video yako. Kwa maelezo ya video, tumia muundo ufuatao: [Jina la Kituo] |[Mada ya Video] [Kitambulisho cha Video]

Kwa masahihisho katika video yako, weka “Sahihisho:” au “Masahihisho:”. Sahihisho au Masahihisho lazima yawe katika Kiingereza licha ya lugha ya video au maelezo yaliyosalia. Kwenye mstari tofauti, unaweza kuweka muhuri wa wakati na ufafanuzi wa sahihisho lako. Kwa mfano:

Sahihisho:

0:35 Sababu ya sahihisho

Sehemu hii inapaswa kuonekana baada ya sura zozote za video. Wakati hadhira inatazama video yako, kadi ya maelezo ya Angalia Masahihisho itaonekana.

Ili ubadilishe muundo wa maandishi katika maelezo ya video zako, teua herufi nzito, italiki au muundo wa kukata kati kwenye chaguo zilizo chini ya kisanduku cha maelezo.

Maelezo ya video yanaruhusiwa kuwa na idadi ya juu ya herufi 5,000 na hayawezi kujumisha herufi zisizoruhusiwa.

Kumbuka: Iwapo kituo kina maonyo yoyote yanayoendelea, au iwapo huenda maudhui hayafai baadhi ya watazamaji, kipengele cha masahihisho hakitapatikana.

Kijipicha Picha ambayo watazamaji wataona kabla ya kubofya video yako.
Orodha ya kucheza Weka video yako kwenye mojawapo ya orodha zako zilizopo za kucheza, au utunge orodha ya kucheza.
Hadhira Ili kutii Sheria ya Kulinda Faragha ya Watoto Mtandaoni (COPPA), unapaswa kutufahamisha iwapo video zako zinalenga watoto.
Mipaka ya umri Weka mipaka ya umri kwenye video ambazo huenda hazifai hadhira fulani.

Video kutoka kwenye kituo chako ambayo ni kiungo chenye uwezo wa kubofyeka katika kichezaji cha Video Fupi ili kusaidia kuelekeza watazamaji kwenye Video zako Fupi kwenye maudhui yako mengine ya YouTube. 

Ukiwa na uwezo wa kufikia vipengele vya kina, unaweza kuhariri Video Fupi ili kujumuisha kiungo cha video kutoka kwa kituo chako. Unaweza kuunganisha Video, Video Fupi na maudhui ya Moja kwa Moja.

Kumbuka: Video unayochagua inapaswa kuwa ya umma au iwe haijaorodheshwa na ni lazima ifuate Mwongozo wetu wa Jumuiya.

Katika sehemu ya chini ya ukurasa wa Maelezo, teua ONYESHA ZAIDI ili uchague mipangilio yako ya kina.

Matangazo yanayolipiwa Waruhusu watazamaji na YouTube kujua kuwa video yako ina matangazo yanayolipiwa.
Sura za kiotomatiki

Unaweza pia kuweka mihuri za wakati na mada za sura za video zako ili kurahisisha utazamaji. Unaweza kubuni sura za video yako mwenyewe au utumie sura zinazozalishwa kiotomatiki kwa kuchagua kisanduku cha kuteua cha 'Ruhusu sura za kiotomatiki (wakati zipo na zinapostahiki)'.

Sura zozote za video utakazoweka zitabatilisha sura za video zilizozalishwa kiotomatiki.

Maeneo Yanayoangaziwa Kipengele cha Maeneo Yanayoangaziwa (wakati kinapatikana na unapostahiki kukitumia) hutumia maeneo uliyoangazia kwa njia dhahiri katika maelezo, manukuu na fremu za video zako kuangazia maeneo muhimu katika utepe kwenye maelezo ya video yako. Ili ujiondoe kwenye kipengele cha Maeneo Yanayoangaziwa kiotomatiki, acha kuchagua kisanduku cha kuteua cha 'Ruhusu Maeneo Yanayoangaziwa kiotomatiki'. Kumbuka: Kipengele cha Maeneo Yanayoangaziwa hakitumii data ya mahali kifaa chako kilipo au kuathiri aina ya matangazo yanayoonyeshwa katika video yako (ikiwa unachuma mapato). 
Lebo

Weka maneno muhimu yenye ufafanuzi ili usaidie kusahihisha makosa ya utafutaji.

Lebo zinaweza kuwa muhimu iwapo maudhui ya video yako yana makosa ya tahajia. Vinginevyo, lebo huwa na umuhimu mdogo katika ugunduzi wa video yako.

Uthibitishaji wa manukuu na lugha Chagua lugha halisi ya video na uthibitishaji wa manukuu.
Tarehe na mahali pa kurekodi Weka tarehe na mahali ambapo video yako ilirekodiwa.
Leseni na usambazaji Chagua iwapo video yako inaweza kupachikwa kwenye tovuti tofauti. Ashiria iwapo ungependa kutuma arifa kwa wanaofuatilia video yako mpya.
Kutumia sampuli kutunga Video Fupi Waruhusu wengine watunge Video Fupi kwa kutumia sauti kwenye video yako.
Aina

Chagua aina ili watazamaji waweze kupata video yako kwa urahisi zaidi. Kwenye video za Elimu, unaweza kuteua chaguo zifuatazo:

  • Aina: Chagua shughuli, muhtasari wa dhana, jinsi ya kufanya jambo fulani, kutoa mafunzo, mwongozo wa kutatua tatizo, matumizi katika maisha halisi, jaribio la kisayansi, vidokezo au nyingine kama aina yako ya video ya elimu. 
  • Matatizo: Weka muhuri wa wakati na swali linalojibiwa katika video yako. Kumbuka: chaguo hili linapatikana tu katika aina ya video ya elimu ya mwongozo wa kutatua tatizo.
  • Mfumo wa elimu:  Chagua nchi au eneo ambalo video yako inaendana nalo. Hatua hii hukuwezesha kubainisha zaidi kiwango na mtihani, kozi au kiwango cha elimu. Kumbuka: Mfumo wa elimu unaweza kuchaguliwa kiotomatiki kulingana na nchi au eneo chaguomsingi la kituo chako.
  • Kiwango: Chagua kiwango cha video yako, kama vile Darasa la 9 au elimu ya juu.
  • Mtihani, kozi au kiwango: Tafuta kwenye hifadhidata yetu ili uweke kiwango cha elimu, mtihani au kozi inayohusiana na video yako. 
Maoni na ukadiriaji Chagua iwapo watazamaji wanaweza kutoa maoni kwenye video. Chagua iwapo watazamaji wanaweza kujua mara ambazo video yako imependwa.
Uchumaji wa mapato
Ikiwa upo kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube, unaweza
Ufaafu kwa matangazo

Iwapo uko kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube, unaweza kutumia ukurasa wa ufaafu kwa matangazo kukadiria video zako ukilinganisha na mwongozo wetu wa maudhui yanayofaa watangazaji. Kitendo hiki hutusaidia kufanya maamuzi kuhusu uchumaji wa mapato kwa haraka na usahihi zaidi. Pata maelezo zaidi kuhusu Uthibitishaji unaojifanyia.

Copyright & Ad-Suitability "Checks" in Upload Flow: Address Issues Before Your Video Goes Public

Vipengee vya video
Weka kadi na skrini za mwisho ili uonyeshe hadhira yako video zinazohusiana, tovuti na miito ya kuchukua hatua.
Manukuu Weka manukuu kwenye video yako na ufikie hadhira pana.
End screen Weka vipengele vya video katika sehemu ya mwisho ya video yako. Lazima video yako iwe na urefu usiopungua sekunde 25 ili uweke skrini ya mwisho.
Kadi Weka maudhui yanayoshirikisha kwenye video yako.
Ukaguzi

Tumia ukurasa wa Ukaguzi kuchunguza video yako ili kubaini matatizo ya hakimiliki na iwapo unafaa kwa matangazo kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube.

Ukaguzi huu unakusaidia kupata maelezo kuhusu vikwazo vinavyoweza kuwekwa ili uweze kurekebisha matatizo kabla ya video yako kuchapishwa. Ukaguzi unaweza kuchukua muda, lakini unafanyika chinichini, kwa hivyo unaweza kurejelea mchakato huu baadaye. Unaweza pia kuchapisha video yako wakati ukaguzi unaendelea na urekebishe matatizo baadaye.

Kumbuka: Matokeo ya ukaguzi wa Hakimiliki na Ufaafu kwa matangazo si ya mwisho. Kwa mfano, madai ya baadaye ya Content ID unayofanya mwenyewe, maonyo ya hakimiliki na mabadiliko kwenye mipangilio ya video yako yanaweza kuathiri video yako.

 

Uonekanaji

Kwenye ukurasa wa Uonekanaji, chagua wakati ambao ungependa video yako ichapishwe na hadhira ambayo ungependa ipate video yako. Unaweza pia kushiriki video yako kwa faragha.
Kumbuka: Mipangilio chaguomsingi ya faragha ya video kwa watayarishi walio na umri wa kati ya miaka 13 hadi 17 ni ya faragha. Iwapo una umri usiopungua miaka 18, mipangilio chaguomsingi ya faragha ya video hubainishwa kuwa ya umma. Kila mtu anaweza kubadilisha mipangilio hii ili afanye video yake iwe ya umma, ya faragha au ambayo haijaorodheshwa.
  • Hifadhi au uchapishe: Ili uchapishe video yako sasa, teua chaguo hili kisha uchague Ya Faragha, Haijaorodheshwa au Ya Umma kuwa mipangilio ya faragha ya video yako. Ukichagua kufanya video yako iwe ya umma, unaweza pia kuweka video yako kuwa Onyesho la Kwanza papo hapo. Kumbuka: Video yako inaweza kuchapishwa uchakataji wa ubora wa SD unapokamilika.
  • Ratibu: Ili uchapishe video yako baadaye, teua chaguo hili kisha uchague tarehe ambayo ungependa video yako ichapishwe. Video yako itakuwa ya faragha hadi tarehe hiyo. Unaweza pia kuweka video yako kuwa Onyesho la Kwanza.
Kagua mabadiliko uliyofanya na uhakikishe yanafuata sera za YouTube, kisha ubofye HIFADHI.
Kumbuka: Iwapo akaunti yako ina onyo kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya, video yako iliyoratibiwa haitachapishwa katika kipindi cha adhabu. Video yako imewekwa kuwa ya “faragha” katika kipindi cha adhabu na unapaswa kuratibu upya uchapishaji wa video baada ya kipindi cha adhabu kukamilika. Pata maelezo zaidi kuhusu mambo ya msingi kuhusu maonyo kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya.
Pata vidokezo vya kupakia video kwa watayarishi.

Tazama jinsi ya kupakia video

Angalia video ifuatayo kutoka kwenye Kituo cha Watayarishi wa Maudhui ya YouTube kuhusu jinsi ya kupakia video.

Jinsi ya Kupakia Video kwa Kutumia Studio ya YouTube

Pata maelezo zaidi kuhusu kupakia video

Idadi ya video unazoweza kupakia kwa siku

There's a limit to how many videos a channel can upload each day across desktop, mobile, and YouTube API. To increase your daily limit, visit this article.

Kupakia faili za sauti

Huwezi kupakia faili za sauti ili kutayarisha video ya YouTube. Ifuatayo ni orodha ya aina za faili zinazoruhusiwa kwa maudhui yanayoweza kupakiwa kwenye YouTube.

Ili uweke maudhui yako kwenye YouTube, jaribu kubadilisha faili yako ya sauti iwe faili ya video kwa kuweka picha. YouTube haina zana ya kupakia faili za sauti, lakini unaweza kujaribu programu nyingine ya kuhariri video.

Pata maelezo kuhusu tofauti kati ya “kupakia” na “kuchapisha”

Unapopakia video, faili ya video hupakiwa kwenye YouTube.
Unapochapisha video, video hiyo huweza kutazamwa na mtu yeyote.

Kupakia video wima

Unapopakia na kuchapisha video yako, YouTube itabaini njia bora zaidi ya kuonyesha maudhui. Ili upate hali bora zaidi, usiweke pau nyeusi pembeni mwa video yako wima. Iwe video ni ya wima, mraba au mlalo, video hiyo itatoshea kwenye skrini.

Fahamu ni kwa nini tarehe ya kupakiwa na tarehe ya kuchapishwa kwa video yako ni tofauti

  • Tarehe ya kupakiwa: Tarehe ambapo ulipakia video yako. Huonekana karibu na video yako ya faragha au ambayo haijaorodheshwa kwenye ukurasa wa Maudhui yako.
  • Tarehe ya kuchapishwa: Tarehe ambapo video yako ilifanywa kuwa ya umma. Huonekana chini ya video yako ya moja kwa moja na huwekwa kulingana na Saa za Kawaida za Pasifiki (PST).

Tarehe hizi mbili zinaweza kuwa tofauti iwapo ulipakia video yako kuwa ya faragha au ambayo haijaorodheshwa, kisha ukaifanya kuwa ya umma baadaye.

Kidokezo: Unaweza kuratibu video yako ichapishwe wakati mahususi.

Viungo vinavyohusiana

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
13429960242479401801
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false