Unaweza kupakia video kwenye YouTube kwa kufuata hatua chache rahisi. Tumia maagizo yaliyo hapa chini ili upakie video zako kutoka kwenye kompyuta au kifaa cha mkononi. Huenda usiweze kupakia ikiwa matumizi yako yanasimamiwa kwenye YouTube. Pata maelezo zaidi hapa.
Kupakia video katika Studio ya YouTube
- Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
- Katika kona ya juu kulia, bofya UNDA Pakia video .
- Chagua faili ambayo ungependa kupakia. Unaweza kupakia hadi video 15 kwa wakati mmoja. Hakikisha unabofya Badilisha kwenye kila faili ili ubadilishe maelezo ya video yako.
Kumbuka: Video yako itageuzwa ili iwe ya ubora wa juu zaidi unaopatikana ili kuhakikisha inaweza kuchezwa kwenye mitandao na vifaa tofauti. Unaweza kuangalia muda unaokadiriwa wa uchakataji wa video za ubora wa SD, HD na 4K. Video za ubora wa juu zaidi kama vile 4K au HD zinaweza kuchukua muda mrefu zaidi kuchakatwa. Pata maelezo zaidi kuhusu ubora wa video baada ya kupakia na uwiano na ubora wa video. Ikiwa unatatizika, angalia mwongozo wetu wa hitilafu za kawaida za upakiaji.
Ukifunga hali ya upakiaji kabla ya kukamilisha kuchagua mipangilio yako, video yako itahifadhiwa kama ya faragha kwenye ukurasa wako wa Maudhui.
MaelezoMada |
Mada ya video yako. Kumbuka: Mada za video zinaruhusiwa kuwa na idadi ya juu ya herufi 100 na haziwezi kujumuisha herufi zisizoruhusiwa. |
Maelezo |
Maelezo yanayoonyeshwa chini ya video yako. Kwa maelezo ya video, tumia muundo ufuatao: [Jina la Kituo] |[Mada ya Video] [Kitambulisho cha Video] Kwa masahihisho katika video yako, weka “Sahihisho:” au “Masahihisho:”. Sahihisho au Masahihisho lazima yawe katika Kiingereza licha ya lugha ya video au maelezo yaliyosalia. Kwenye mstari tofauti, unaweza kuweka muhuri wa wakati na ufafanuzi wa sahihisho lako. Kwa mfano: Sahihisho: 0:35 Sababu ya sahihisho Sehemu hii inapaswa kuonekana baada ya sura zozote za video. Wakati hadhira inatazama video yako, kadi ya maelezo ya Angalia Masahihisho itaonekana. Ili ubadilishe muundo wa maandishi katika maelezo ya video zako, teua herufi nzito, italiki au muundo wa kukata kati kwenye chaguo zilizo chini ya kisanduku cha maelezo. Maelezo ya video yanaruhusiwa kuwa na idadi ya juu ya herufi 5,000 na hayawezi kujumisha herufi zisizoruhusiwa. Kumbuka: Iwapo kituo kina maonyo yoyote yanayoendelea, au iwapo huenda maudhui hayafai baadhi ya watazamaji, kipengele cha masahihisho hakitapatikana. |
Kijipicha | Picha ambayo watazamaji wataona kabla ya kubofya video yako. |
Orodha ya kucheza | Weka video yako kwenye mojawapo ya orodha zako zilizopo za kucheza, au utunge orodha ya kucheza. |
Hadhira | Ili kutii Sheria ya Kulinda Faragha ya Watoto Mtandaoni (COPPA), unapaswa kutufahamisha iwapo video zako zinalenga watoto. |
Mipaka ya umri | Weka mipaka ya umri kwenye video ambazo huenda hazifai hadhira fulani. |
Video Inayohusiana |
Video kutoka kwenye kituo chako ambayo ni kiungo chenye uwezo wa kubofyeka katika kichezaji cha Video Fupi ili kusaidia kuelekeza watazamaji kwenye Video zako Fupi kwenye maudhui yako mengine ya YouTube. Ukiwa na uwezo wa kufikia vipengele vya kina, unaweza kuhariri Video Fupi ili kujumuisha kiungo cha video kutoka kwa kituo chako. Unaweza kuunganisha Video, Video Fupi na maudhui ya Moja kwa Moja. Kumbuka: Video unayochagua inapaswa kuwa ya umma au iwe haijaorodheshwa na ni lazima ifuate Mwongozo wetu wa Jumuiya. |
Katika sehemu ya chini ya ukurasa wa Maelezo, teua ONYESHA ZAIDI ili uchague mipangilio yako ya kina.
Matangazo yanayolipiwa | Waruhusu watazamaji na YouTube kujua kuwa video yako ina matangazo yanayolipiwa. |
Sura za kiotomatiki |
Unaweza pia kuweka mihuri za wakati na mada za sura za video zako ili kurahisisha utazamaji. Unaweza kubuni sura za video yako mwenyewe au utumie sura zinazozalishwa kiotomatiki kwa kuchagua kisanduku cha kuteua cha 'Ruhusu sura za kiotomatiki (wakati zipo na zinapostahiki)'. Sura zozote za video utakazoweka zitabatilisha sura za video zilizozalishwa kiotomatiki. |
Maeneo Yanayoangaziwa | Kipengele cha Maeneo Yanayoangaziwa (wakati kinapatikana na unapostahiki kukitumia) hutumia maeneo uliyoangazia kwa njia dhahiri katika maelezo, manukuu na fremu za video zako kuangazia maeneo muhimu katika utepe kwenye maelezo ya video yako. Ili ujiondoe kwenye kipengele cha Maeneo Yanayoangaziwa kiotomatiki, acha kuchagua kisanduku cha kuteua cha 'Ruhusu Maeneo Yanayoangaziwa kiotomatiki'. Kumbuka: Kipengele cha Maeneo Yanayoangaziwa hakitumii data ya mahali kifaa chako kilipo au kuathiri aina ya matangazo yanayoonyeshwa katika video yako (ikiwa unachuma mapato). |
Lebo |
Weka maneno muhimu yenye ufafanuzi ili usaidie kusahihisha makosa ya utafutaji. Lebo zinaweza kuwa muhimu iwapo maudhui ya video yako yana makosa ya tahajia. Vinginevyo, lebo huwa na umuhimu mdogo katika ugunduzi wa video yako. |
Uthibitishaji wa manukuu na lugha | Chagua lugha halisi ya video na uthibitishaji wa manukuu. |
Tarehe na mahali pa kurekodi | Weka tarehe na mahali ambapo video yako ilirekodiwa. |
Leseni na usambazaji | Chagua iwapo video yako inaweza kupachikwa kwenye tovuti tofauti. Ashiria iwapo ungependa kutuma arifa kwa wanaofuatilia video yako mpya. |
Kutumia sampuli kutunga Video Fupi | Waruhusu wengine watunge Video Fupi kwa kutumia sauti kwenye video yako. |
Aina |
Chagua aina ili watazamaji waweze kupata video yako kwa urahisi zaidi. Kwenye video za Elimu, unaweza kuteua chaguo zifuatazo:
|
Maoni na ukadiriaji | Chagua iwapo watazamaji wanaweza kutoa maoni kwenye video. Chagua iwapo watazamaji wanaweza kujua mara ambazo video yako imependwa. |
- Kuwasha au kuzima kipengele cha uchumaji wa mapato kwenye video yako
- Kuchagua muundo wako wa utangazaji
- Kudhibiti mapumziko ya matangazo yanayochezwa katikati ya video
Iwapo uko kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube, unaweza kutumia ukurasa wa ufaafu kwa matangazo kukadiria video zako ukilinganisha na mwongozo wetu wa maudhui yanayofaa watangazaji. Kitendo hiki hutusaidia kufanya maamuzi kuhusu uchumaji wa mapato kwa haraka na usahihi zaidi. Pata maelezo zaidi kuhusu Uthibitishaji unaojifanyia.
Copyright & Ad-Suitability "Checks" in Upload Flow: Address Issues Before Your Video Goes Public
Manukuu | Weka manukuu kwenye video yako na ufikie hadhira pana. |
End screen | Weka vipengele vya video katika sehemu ya mwisho ya video yako. Lazima video yako iwe na urefu usiopungua sekunde 25 ili uweke skrini ya mwisho. |
Kadi | Weka maudhui yanayoshirikisha kwenye video yako. |
Tumia ukurasa wa Ukaguzi kuchunguza video yako ili kubaini matatizo ya hakimiliki na iwapo unafaa kwa matangazo kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube.
- Hakimiliki: Ukaguzi wa hakimiliki hutafuta maudhui yaliyo na hakimiliki katika video yako. Iwapo matatizo yatapatikana, unaweza kuondoa maudhui yanayodaiwa kwenye video yako au uchague kupinga dai.
- Ufaafu kwa matangazo: Ukaguzi wa kubaini ufaafu kwa matangazo utathibitisha iwapo video yako inafuata mwongozo wetu wa maudhui yanayofaa matangazo. Iwapo matatizo yatapatikana, unaweza kuomba tukague wenyewe kama unafikiri kuwa mifumo yetu ilikosea.
Ukaguzi huu unakusaidia kupata maelezo kuhusu vikwazo vinavyoweza kuwekwa ili uweze kurekebisha matatizo kabla ya video yako kuchapishwa. Ukaguzi unaweza kuchukua muda, lakini unafanyika chinichini, kwa hivyo unaweza kurejelea mchakato huu baadaye. Unaweza pia kuchapisha video yako wakati ukaguzi unaendelea na urekebishe matatizo baadaye.
Uonekanaji
- Hifadhi au uchapishe: Ili uchapishe video yako sasa, teua chaguo hili kisha uchague Ya Faragha, Haijaorodheshwa au Ya Umma kuwa mipangilio ya faragha ya video yako. Ukichagua kufanya video yako iwe ya umma, unaweza pia kuweka video yako kuwa Onyesho la Kwanza papo hapo. Kumbuka: Video yako inaweza kuchapishwa uchakataji wa ubora wa SD unapokamilika.
- Ratibu: Ili uchapishe video yako baadaye, teua chaguo hili kisha uchague tarehe ambayo ungependa video yako ichapishwe. Video yako itakuwa ya faragha hadi tarehe hiyo. Unaweza pia kuweka video yako kuwa Onyesho la Kwanza.
Tazama jinsi ya kupakia video
Angalia video ifuatayo kutoka kwenye Kituo cha Watayarishi wa Maudhui ya YouTube kuhusu jinsi ya kupakia video.
Jinsi ya Kupakia Video kwa Kutumia Studio ya YouTube
Pata maelezo zaidi kuhusu kupakia video
Idadi ya video unazoweza kupakia kwa sikuThere's a limit to how many videos a channel can upload each day across desktop, mobile, and YouTube API. To increase your daily limit, visit this article.
Kupakia faili za sauti
Huwezi kupakia faili za sauti ili kutayarisha video ya YouTube. Ifuatayo ni orodha ya aina za faili zinazoruhusiwa kwa maudhui yanayoweza kupakiwa kwenye YouTube.
Pata maelezo kuhusu tofauti kati ya “kupakia” na “kuchapisha”
Kupakia video wima
Fahamu ni kwa nini tarehe ya kupakiwa na tarehe ya kuchapishwa kwa video yako ni tofauti
- Tarehe ya kupakiwa: Tarehe ambapo ulipakia video yako. Huonekana karibu na video yako ya faragha au ambayo haijaorodheshwa kwenye ukurasa wa Maudhui yako.
- Tarehe ya kuchapishwa: Tarehe ambapo video yako ilifanywa kuwa ya umma. Huonekana chini ya video yako ya moja kwa moja na huwekwa kulingana na Saa za Kawaida za Pasifiki (PST).
Tarehe hizi mbili zinaweza kuwa tofauti iwapo ulipakia video yako kuwa ya faragha au ambayo haijaorodheshwa, kisha ukaifanya kuwa ya umma baadaye.