Kuweka mipangilio ya akaunti ya AdSense katika YouTube ili upokee malipo kwenye YouTube

Kutokana na vita vinavyoendelea Ukraini, tutasimamisha kwa muda kuwapatia matangazo ya Google na YouTube watumiaji walio nchini Urusi. Pata maelezo zaidi.

Iwapo unachuma mapato kwenye YouTube, unapaswa kuunganisha akaunti iliyoidhinishwa ya AdSense katika YouTube ili uchume mapato na upokee malipo.

Muhimu: Unaweza tu kuwa na akaunti moja ya AdSense katika YouTube yenye jina sawa la anayelipwa kwa mujibu wa Sheria na Masharti ya AdSense katika YouTube. Akaunti zinazofanana za AdSense katika YouTube zilizofunguliwa kupitia YouTube hazitaidhinishwa na mchakato wa uchumaji mapato utazimwa kwenye Chaneli ya YouTube iliyounganishwa. Unapofungua akaunti mpya ya AdSense katika YouTube, fungua moja tu kupitia Studio ya YouTube. Ukifanya hivyo kwenye tovuti nyingine (kama vile kwenye ukurasa wa kwanza wa AdSense katika YouTube) haitafanya kazi.

Kufungua na kuunganisha akaunti ya AdSense katika YouTube

Kufungua akaunti ya AdSense katika YouTube na kuiunganisha kwenye chaneli yako ni hatua muhimu katika mchakato wa kupokea malipo kwenye YouTube. Kumbuka kuwa iwapo tayari upo katika Mpango wa Washirika wa YouTube, unaweza kubadilisha akaunti yako iliyounganishwa ya AdSense katika YouTube ukipenda kufanya hivyo. Unaweza pia kuchuma mapato kwenye zaidi ya chaneli moja ya YouTube kupitia akaunti sawa ya AdSense katika YouTube.

Kumbuka kwamba unaweza tu kubadili akaunti yako iliyounganishwa ya AdSense katika YouTube mara moja katika kipindi cha siku 32.

 AdSense kwa Watayarishi wa YouTube

 

Unaweza kufungua akaunti mpya ya AdSense katika YouTube na uiunganishe kwenye chaneli yako:

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Katika menyu ya kushoto, chagua kichupo cha Mapato.
  3. Bofya ANZA katika kadi ya Jisajili kwenye AdSense katika YouTube.
  4. Ukiombwa, weka nenosiri la akaunti yako ya YouTube kisha uthibitishe upya ikihitajika.
  5. Chagua akaunti ya Google ambayo ungependa kutumia kwenye AdSense katika YouTube.
    1. Kumbuka: iwapo tayari unatumia AdSense kwa sababu nyingine nje ya YouTube, ingia katika akaunti ukitumia akaunti ya Google uliyotumia kwenye akaunti yako iliyopo ya AdSense.
  6. Sasa umeingia kwenye AdSense katika YouTube. Ukishafika hapa, thibitisha kuwa anwani ya barua pepe ni sahihi katika sehemu ya juu ya ukurasa. Iwapo si sahihi, bofya Tumia akaunti tofauti ili ubadilishe akaunti.
  7. Endelea kuweka mipangilio ya akaunti yako. Weka maelezo yako ya mawasiliano kisha utume ombi lako la akaunti ya AdSense katika YouTube.

Baada ya kufuata hatua zilizo hapo juu, utaelekezwa kwenye Studio ya YouTube, ambapo utaona ujumbe unaothibitisha kuwa ombi lako la akaunti ya AdSense katika YouT u be limepokelewa. Tafadhali kumbuka kuwa iwapo hutaelekezwa kwenye Studio, ombi lako halikukamilika. Kagua akaunti yako ya AdSense katika YouTube ili uangalie ikiwa kuna hatua zozote ambazo hujakamilisha. AdSense katika YouTube itakuarifu kupitia barua pepe baada ya akaunti yako kuidhinishwa, shughuli ambayo kwa kawaida huchukua siku kadhaa lakini wakati mwingine inaweza kuchukua wiki 2 hadi 3. Baada ya kuidhinishwa, utaona ujumbe wa kuthibitisha katika Studio ya YouTube kwenye kadi ya Jisajili kwenye AdSense katika YouTube  unaosema kuwa akaunti yako ya AdSense katika YouTube imeidhinishwa na inatumika.

Mitandao ya Chaneli Mbalimbali (MCN): Iwapo una chaneli ya mshirika inayoshirikiana na MCN, unapaswa kuunganisha akaunti yako ya AdSense katika YouTube kwenye chaneli yako. Kufikia akaunti ya mshirika mwingine ya AdSense katika YouTube, hata ukipewa ruhusa, ni ukiukaji wa Sheria na Masharti ya AdSense katika YouTube.

Sifahamu iwapo tayari nina akaunti ya AdSense au AdSense katika YouTube

Tafuta kwenye vikasha vyako barua pepe kutoka "adsense-noreply@google.com".
Unaruhusiwa tu kuwa na akaunti moja ya AdSense au AdSense katika YouTube yenye jina sawa la anayelipwa kwa mujibu wa Sheria na Masharti ya AdSense. Iwapo itabainika kuwa una akaunti nyingine, uidhinishaji wa akaunti yako ya AdSense katika YouTube utabatilishwa na utaombwa ufunge akaunti nyingine zinazohusiana.
Tayari nina akaunti iliyoidhinishwa ya AdSense au AdSense katika YouTube
  1. Ingia katika akaunti yako ya YouTube kisha uende kwenye https://studio.youtube.com/channel/UC/monetization
  2. Bofya Anza kwenye kadi ya "Jisajili kwenye AdSense katika YouTube".
  3. Utahitaji kuweka nenosiri la akaunti yako ya YouTube kisha uthibitishe upya. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuthibitisha upya akaunti yako ya YouTube.
  4. Chagua akaunti ya Google ambayo ungependa kutumia kuingia katika akaunti ya AdSense katika YouTube. Iwapo tayari una akaunti ya AdSense au AdSense katika YouTube, ni lazima uingie katika akaunti ukitumia akaunti ya Google unayotumia kufikia akaunti yako iliyopo. Huenda akaunti hii ikawa tofauti na vitambulisho vya kuingia katika akaunti unavyotumia kuingia katika YouTube.
  5. Utaelekezwa kwenye ukurasa wa kujisajili wa AdSense katika YouTube . Thibitisha kuwa barua pepe iliyo katika sehemu ya juu ya ukurasa ni sahihi. Iwapo akaunti ambayo imeonyeshwa si sahihi, bofya "Tumia akaunti tofauti" ili ubadilishe akaunti.
  6. Bofya Kubali Uunganishaji.
  7. Utaelekezwa kwenye Ukurasa wa mapato katika Studio ya YouTube.
  8. Baada ya kuunganisha akaunti yako ya AdSense katika YouTube, tutaweka alama ya kijani kwenye hatua hii ili kuonyesha kuwa “Imekamilika” kwenye kadi ya “Jisajili kwenye AdSense katika YouTube”.

Kuweka mipangilio ya AdSense katika YouTube kupitia akaunti ya Kidhibiti Maudhui

Iwapo umepewa haki za kusimamia akaunti ya Kidhibiti Maudhui, unaweza kuiunganisha na akaunti ya AdSense katika YouTube.
  1. Ingia katika akaunti yako ya Kidhibiti Maudhui.
  2. Nenda kwenye Mipangilio.
  3. Chini ya sehemu ya Muhtasari, utaona AdSense katika YouTube (huenda ukahitaji kusogeza ili uione).
  4. Bofya Badilisha.
  5. Bofya Endelea kwenye AdSense.
  6. Utahitaji kuweka nenosiri la akaunti yako ya YouTube kisha uthibitishe upya. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuthibitisha upya akaunti yako ya YouTube.
  7. Chagua akaunti ya Google ambayo ungependa kutumia kuingia katika akaunti ya AdSense katika YouTube. Iwapo tayari una akaunti ya AdSense au AdSense katika YouTube, ni lazima uingie katika akaunti ukitumia Akaunti ya Google unayotumia kufikia akaunti yako iliyopo.
  8. Ukiombwa, weka nenosiri la akaunti yako ya AdSense katika YouTube. Huenda maelezo haya yakawa tofauti na vitambulisho unavyotumia kuingia katika akaunti ya YouTube.
  9. Thibitisha chaneli ya YouTube unayounganisha na akaunti ya AdSense katika YouTube na uchague lugha ya msingi ya chaneli hiyo. Ingawa unachagua chaneli moja ya YouTube ili kukamilisha uunganishaji wa AdSense katika YouTube, YouTube itaonyesha matangazo kwenye chaneli zote zilizounganishwa kwenye Kidhibiti chako cha Maudhui.
  10. Bofya Kubali Uunganishaji na uweke maelezo yako ya malipo, ukiombwa.
Ukishamaliza mchakato huu, utaelekezwa kwenye YouTube. Pata maelezo zaidi kuhusu muda wa kusubiri ukaguzi wa ombi la AdSense.

Matatizo ya kawaida

Tumia maelezo yaliyo hapa chini ili utatue matatizo ya kawaida unapojaribu kuunganisha akaunti ya AdSense katika YouTube kwenye chaneli yako.

Nimefungua akaunti mpya ya AdSense katika YouTube, lakini haijaidhinishwa kwa sababu tayari nina akaunti iliyopo ya AdSense au AdSense katika YouTube

Unapaswa kuwa na akaunti moja tu ya AdSense au AdSense katika YouTube yenye jina sawa la anayelipwa kwa mujibu wa Sheria na Masharti ya AdSenseau Sheria na Masharti ya AdSense katika YouTube, kama yanavyotumika. Iwapo tutagundua kuwa una akaunti nyingine, hatutaidhinisha akaunti yako mpya uliyofungua ya AdSense katika YouTube.

Tafuta kwenye vikasha vya barua pepe yako iwapo kuna barua pepe yenye mada “Tayari una akaunti ya AdSense au AdSense katika YouTube”. Ujumbe huu utakuwa na maelezo kuhusu akaunti yako iliyopo ya AdSense au AdSense katika YouTube. Ukiwa na maelezo haya, una chaguo mbili za kurekebisha tatizo hili:

Tumia akaunti (ya zamani) iliyopo

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube kisha ubofye Badilisha Uunganishaji.
  2. Katika menyu ya kuchagua akaunti, teua Akaunti ya Google inayotumia akaunti yako iliyopo (ya zamani) ya AdSense au AdSense katika YouTube.
  3. Bofya Kubali Uunganishaji.

Utaelekezwa kwenye Studio ya YouTube, ambako utaweza kuona akaunti iliyounganishwa kwenye chaneli yako.

Kutumia akaunti mpya ambayo umefungua sasa hivi

Kwanza, utahitaji kufunga akaunti (ya zamani) iliyopo

  1. Ingia katika akaunti yako iliyopo ya AdSense au AdSense katika YouTube, kama inavyotumika.
  2. Fuata hatua hapa ili ufunge akaunti yako.

Ukishafunga, ingia katika akaunti yako mpya ya AdSense katika YouTube ili uthibitishe kuwa umefunga ile ya zamani.

Kumbuka: Inaweza kuchukua siku kadhaa kabla ya akaunti ya AdSense katika YouTube kuidhinishwa na kuunganishwa kwenye chaneli yako ya YouTube.

Matatizo ya Kuthibitisha Anwani (PIN)

Hatua ya kukamilisha uthibitishaji wa anwani (PIN) kwenye AdSense katika YouTube inahitajika ili udumishe mchakato wa uchumaji mapato kwenye chaneli na upokee malipo.

Iwapo umeunganisha akaunti mpya ya AdSense katika YouTube kwenye chaneli yako, utatumiwa kadi ya kuthibitisha PIN kwenye anwani ya mahali halisi ulipo utakapofikisha salio la $10. Kadi hii ya uthibitishaji wa PIN itajumuisha namba ya PIN unayopaswa kuweka katika akaunti yako ili uthibitishe anwani yako.

Iwapo umeunganisha na akaunti iliyopo ya AdSense au AdSense katika YouTube, huenda ukahitaji kusubiri angalau wiki 3 kabla ya kadi ya kuthibitisha PIN kuwasili kupitia barua. Iwapo hujaipokea kadi hiyo baada ya wiki 3, unaweza kuomba kupokea kadi mpya ya kuthibitisha PIN.

Hakikisha kuwa anwani iliyo kwenye akaunti ya AdSense katika YouTube inalingana na anwani inayotambuliwa na ofisi ya posta iliyo karibu nawe. Kuwa na anwani sahihi husaidia ofisi ya posta ya karibu kufikisha barua yako. Iwapo hazifanani, unahitaji kubadilisha anwani ya malipo katika akaunti yako ili zifanane.

Iwapo unahitaji usaidizi wa uthibitishaji wa anwani (PIN), rejelea nyenzo hizi za Usaidizi:

Nini kitafanyika iwapo sitathibitisha anwani yangu?

Iwapo hutathibitisha anwani yako ndani ya miezi 4, uchumaji wa mapato utasitishwa kwenye chaneli yako. Hii inajumuisha kusitisha uwezo wa kufikia vipengele kama vile:

  • Uanachama katika chaneli
  • Super Chat na zaidi

Uchumaji wa mapato utaendelea kwenye chaneli yako baada ya kuthibitisha anwani yako.

Matatizo mengine

Nimeonyeshwa arifa ya “Sahamani, hitilafu fulani imetokea” katika Studio ya YouTube

Ujumbe huu kuhusu hitilafu unaweza kuonekana wakati unajaribu kufanya mabadiliko kupitia barua pepe ambazo hazitambuliwi na Studio ya YouTube. Ili utatue matatizo haya, jaribu yafuatayo:

  • Wakati unaunganisha akaunti ya AdSense katika YouTube, Studio ya YouTube itakuomba Uthibitishe Kuwa ni Wewe. Hakikisha kuwa unafanya hivyo ukitumia anwani ya barua pepe unayotumia kuingia katika akaunti ya YouTube.

    Kisha utaombwa uchague Akaunti ya Google ambayo ungependa kutumia kuendelea kwenye AdSense katika YouTube. Katika hali hii, unaweza kuchagua anwani ya barua pepe iliyo tofauti na unayotumia kuingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  • Iwapo chaneli yako imeunganishwa kwenye Akaunti ya Biashara, unapaswa kuingia katika akaunti kwa kutumia anwani ya barua pepe uliyotumia kufungua chaneli. Iwapo huwezi kuingia katika akaunti kwa kutumia anwani hiyo ya barua pepe, rejesha akaunti yako kwa kufuata vidokezo vyetu vya kukamilisha hatua za kurejesha uwezo wa kufikia akaunti.

AdSense katika YouTube inaniomba URL ya tovuti ili nijisajili

Wakati unaunganisha akaunti yako mpya ya AdSense katika YouTube kwenye chaneli yako ya YouTube, usiende kufungua kwenye google.com/adsense au adsense.com kwa madhumuni haya. Ukifanya hivyo, akaunti yako haitaidhinishwa na uchumaji wa mapato utazimwa kwenye chaneli yako. Badala yake, fungua akaunti ya AdSense katika YouTube kwenye Studio ya YouTube moja kwa moja.

Hitilafu nyingine

Iwapo unakumbwa na matatizo mengine ya kiufundi ambayo hayajabainishwa kwenye ukurasa huu, jaribu yafuatayo:

  • Funga vichupo vyote vya kivinjari.
  • Futa vidakuzi na akiba ya kivinjari chako.
  • Tumia dirisha la faragha au dirisha fiche (ili kuhakikisha kuwa hujaingia katika akaunti nyingine za Google).

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
6324250292419502324
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false