Una chaguo chache za kufikia vipengele:
- Vipengele vya kawaida: Kufungua chaneli kunakupa vipengele hivi mara moja mradi huna maonyo yanayoendelea kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya. Tumia vipengele hivi kuanza kukuza hadhira yako na kuendeleza chaneli yako.
- Vipengele vya wastani: Unaweza kuchagua kufikia vipengele vya wastani, iwapo ungependa kuwa na seti kubwa ya zana ili uendelee kukuza hadhira yako. Ili ufanye hivyo, ni lazima uthibitishe namba yako ya simu.
- Vipengele vya kina: Watayarishi wengi wanaochapisha maudhui ambao wanataka kutumia vipengele vya kina kwa mara ya kwanza watatimiza masharti kiotomatiki, kwa kuwa tayari wamejenga historia ya kutosha ya chaneli.
- Baadhi ya watayarishi wapya au wale ambao wangependa kufikia vipengele vya kina moja kwa moja wanaweza kuchagua kuthibitisha utambulisho wao kwa kutumia kitambulisho halali au kupitia uthibitishaji kwa video. Soma zaidi hapa kuhusu jinsi maelezo kutoka kwenye kitambulisho chako au uthibitishaji kwa video unavyotumika.
Vipengele |
Hamna uthibitishaji |
Uthibitishaji kupitia nambari ya simu |
Uthibitishaji kupitia historia ya chaneli AU utambulisho |
|
Kawaida |
|
Kikomo kidogo cha kila siku |
Kikomo cha juu cha kila siku |
|
Wastani |
Video ndefu (zaidi ya dakika 15) |
|||
|
Kikomo kidogo cha kila siku |
Kikomo cha juu cha kila siku |
||
Kikomo kidogo cha kila siku |
Kikomo cha juu cha kila siku |
|||
Tayarisha podikasti | ||||
Kina |
||||
|
||||
Weka viungo vinavyobofyeka kwenye maelezo yako ya video ndefu na Machapisho ya jumuiya | ||||
Weka Video Inayohusiana kwenye Video yako Fupi ya YouTube | ||||
Machapisho ya jumuiya |
Kikomo kidogo cha kila siku |
Kikomo cha juu cha kila siku |
||
Bandika maoni kwenye video na Machapisho ya jumuiya | ||||
Kupakia RSS | ||||
Weka viungo vinavyobofyeka katika maelezo ya chaneli yako kwenye ukurasa wa kutazama |
Kumbuka: Mbali na maelezo yaliyo hapa juu, hakikisha kuwa unafuata Mwongozo wa Jumuiya ya YouTube. Ukiukaji wa sera zetu unaweza kusababisha onyo au kuzuia uwezo wako wa kufikia vipengele.
Kuona vipengele unavyoweza kufikia
Unaweza kuona vipengele unavyoweza kufikia sasa kwa kufuata maagizo yaliyo hapa chini.
- Kwenye kompyuta, ingia katika Studio ya YouTube.
- Bofya Mipangilio.
- Bofya Chaneli.
- Bofya ustahiki wa Kipengele.
Utaona “Kimewashwa” karibu na vipengele unavyoweza kufikia. Kumbuka kuwa si vipengele vyote vya YouTube hudhibitiwa ndani ya kichupo cha Ustahiki wa kipengele na baadhi ya vipengele vinaweza kuwa na masharti tofauti ya kujiunga. Ili upate maelezo zaidi kuhusu vipengele vingine, tembelea Ukurasa wa hali na vipengele.
Kuthibitisha utambulisho wako ili utumie vipengele
Kwa maagizo kuhusu jinsi ya kufikia vipengele vya wastani na vipengele vya kina, angalia makala haya ya Kituo cha Usaidizi. Kumbuka kuwa uthibitishaji kwa kitambulisho na video haupatikani kwa watayarishi wote.