Kudhibiti uanachama katika chaneli

Tunafanya mabadiliko machache kuhusu jinsi tunavyokusanya na kutumia data katika maudhui ya watoto kwenye YouTube. Kwa hivyo, baadhi ya maagizo katika makala haya yanaweza kuwa yamebadilika. Pata maelezo zaidi.

Pata maelezo zaidi kuhusu manufaa ambayo unaweza kuwapatia wanachama wako na watazamaji wako wanavyotumia uanachama.

Kila chaneli inayoshiriki katika mpango wa uanachama, ikiwa ni pamoja na manufaa yake, ina wajibu wa kutii sera na masharti yetu. Sera hizi zinajumuisha Mwongozo wa Jumuiya wa YouTube pamoja na sheria na kanuni zote zinazotumika.

Uanachama Katika Vituo

 

Kuna sehemu tofauti katika Studio ya Watayarishi ambapo unaweza kudhibiti na kufuatilia mpango wako wa uanachama:

Kichupo cha Uanachama

Baada ya kuanzisha uanachama, unaweza kupata kichupo hiki katika Studio chini ya Chuma mapato kisha Uanachama

Hapa unaweza kufuatilia:

  1. Jumla ya wanachama: Wanachama wote wa sasa ambao wanaweza kufikia manufaa. Ikiwa ni pamoja na wanachama ambao wametamatisha usajili lakini wanaweza kufikia manufaa kwa muda uliobakia wa kipindi chao cha bili.
  2. Wanachama wanaoendelea: Wanachama wote walio na usajili unaotumika tu. Usajili unaotumika hukokotolewa kwa kutoa wanachama walioondolewa kwenye jumla ya wanachama.
  3. Mapato: Unaweza kufuatilia mapato ya kipindi cha mwisho cha bili na ulinganishe na kipindi cha bili kilichotangulia
  4. Wanachama kulingana na kiwango cha uanachama: Fuatilia idadi ya wanachama (wanachama wote au wanaoshiriki) kulingana na kiwango cha uanachama katika kipindi fulani cha muda
  5. Wanaojisajili na wanaotamatisha usajili: Angalia ni watumiaji wangapi wamejisajili kuwa wanachama au wametamatisha uanachama katika kipindi cha bili kilichopita na ulinganishe na kipindi cha bili kilichotangulia.
  6. Maoni ya Kutamatisha Usajili: Baadhi ya watumiaji hutoa maoni kuhusu sababu ya kutamatisha usajili, katika chaguo zetu za kuteua jibu moja zilizobainishwa mapema. Kwa kuwekelea kiashiria juu ya ‘Usajili uliotamatishwa’ unaweza kuona jinsi watumiaji walivyojibu wakati wanatamatisha usajili kwenye chaneli yako.
Kumbuka: Kipindi cha bili kinaweza kuwa siku 28, 30 au 31 kulingana na kalenda ya sasa ya mwezi. Kwa mfano, uanachama uliolipiwa mwezi Septemba utapewa siku 30 za kutumia kabla ya malipo yanayofuata.

Kusimamia wanachama wako

Unaweza kuona orodha ya wanachama wako wote wa sasa ikiwa ni pamoja na:

  1. Jumla ya muda wa uanachama (inajumuisha muda wa vipindi vyote vya uanachama).
  2. Sasisho la mara ya mwisho: Siku zilizopita tangu wakati mwanachama alipojiunga, kujiunga upya, kupandisha au kushusha kiwango cha uanachama wake.

Ili uhamishie muhtasari wa maelezo haya kwenye faili ya CSV, bofya Pakua katika kona ya upande wa kulia. Mchakato wa kuhamisha unaweza kuchukua dakika kadhaa kukamilika. Unaweza kufunga dirisha hili wakati unasubiri.

Kukusanya maelezo kutoka kwa wanachama wako:

Kwa kutumia huduma hii ya washirika wengine ya uunganishaji wa IFTTT, unaweza kubuni fomu salama na maalum yenye wanachama wa chaneli yako ili kukusanya maelezo yatakayokusaidia kutoa manufaa. Unawajibikia data yoyote iliyokusanywa kutoka kwa wanachama. YouTube haiwezi kufikia data hii.

Kumbuka: Huduma ya washirika wengine ya uunganishaji wa IFTTT kwa sasa inapatikana tu katika lugha ya Kiingereza.

Kudhibiti manufaa, viwango na bei zako

Bofya kadi ya Ofa kwa Wanachama ili udhibiti na ubadilishe manufaa na viwango vyako vya uanachama. Hapa utapata mapendekezo na mbinu bora kwa aina ya manufaa ambayo huenda ukataka kutoa kwa kila kiwango cha bei.

Kadi na zana nyingine kwenye kichupo cha Uanachama:

  1. Nyenzo: Kadi maalum ambayo itaonyesha desturi bora, viungo vya nyenzo nyingine na majaribio maalum ya uanachama ya kujijumuisha na kujiondoa.
  2. Video za hivi majuzi ambazo wanachama walitumia kujiunga: Fuatilia video zilizo na utendaji wa juu ambazo watazamaji wanafuatilia.
  3. Maoni ya wanachama ya hivi karibuni: Pata kwa urahisi maoni mapya ya mwanachama ili uweze kuyapatia kipaumbele cha kuyajibu.
  4. Video ya Utangulizi: Pakia video ya kuonyeshwa kwenye skrini ya ofa kwa wanachama wako. Watazamaji wataona video ya utangulizi wanapobofya kitufe cha JIUNGE ili kujisajili kwenye uanachama.

Takwimu za YouTube

Unaweza pia kuangalia data zaidi kuhusu wanachama wako kwenye YTA.

  1. Hadhira: Bofya Takwimu za YouTube kisha Takwimu kisha Hadhira, kisha bofya kadi ya ‘Jumla ya Wanachama’ ili uone jumla ya wanachama na wanachama wanaoendelea kwa kipindi cha muda fulani. Ukibofya ‘Angalia Zaidi’ itaonyesha data zaidi kuhusu wanachama wako. Unaweza kurekebisha vipindi vya wakati ili kuangalia utendaji wa vipimo vifuatavyo katika kipindi maalum:
    • Jumla ya wanachama na Wanachama wanaoendelea
    • Wanachama Wapya
    • Wanachama Walioondolewa
    • Wanachama Uliowapoteza (wanachama waliotamatisha usajili ambao hawawezi tena kupata manufaa kwa sababu ya kukamilika kwa kipindi chao cha bili)
  2. Mapato: Bofya kwenye Takwimu kisha Mapato kisha ubofye kadi ya ‘Mapato ya Miamala’. Ukiwa hapa, unaweza kuona idadi ya miamala iliyofanywa katika kipindi maalum. Miamala ni wanachama wapya waliojisajili au wanachama waliojisajili tena.
Kumbuka: Ili uangalie uchanganuzi wa kina wa data ya mapato ya uanachama:
  1. Nenda kwenye Studio ya YouTube.
  2. Chagua Takwimu.
  3. Chagua Mapato.
  4. Tafuta na uchague kadi ya Jinsi ya kuchuma mapato.
  5. Chagua Uanachama ili upate mwonekano wa kina wa mapato yako ya uanachama. Unaweza kuweka kipindi cha muda maalum au kuchuja kulingana na muundo wa video.

Kuangalia wanachama wako

Ukipata mwanachama mpya ukiwa nje ya mtandao hutapokea arifa. Unaweza kuona wanachama wako wote wanaoendelea, muda ambao wamekuwa wanachama na idadi ya wanaowafuatilia kwenye kichupo cha Uanachama katika Studio ya YouTube. Wanachama wanaweza kutamatisha uanachama wao wakati wowote.

Ikiwa unatiririsha mubashara mtazamaji mpya anapojiunga na uanachama katika chaneli yako, ujumbe wa "Karibu" wenye rangi ya kijani inayong'aa utatumwa katika gumzo la moja kwa moja. Ujumbe huu utabandikwa juu ya gumzo kwa dakika 5.

Unaweza pia kuona jumla ya idadi ya wanachama kwa siku katika kichupo cha Hadhira katika Takwimu za YouTube. ‘Kadi ya vipimo muhimu’ huonyesha chati ya idadi ya wanachama waliojiunga au kujiondoa kwa kipindi fulani.

Kutangaza uanachama

Unaweza kuongeza /join katika sehemu ya mwisho ya URL ya chaneli yako ili uunganishe moja kwa moja na kidirisha cha ofa kwa wanachama.
Unaweza kuweka kiungo hiki:
  • Kwenye maelezo ya video yako.
  • Kwenye kadi na skrini za mwisho katika video zako.
Uanachama Unaotolewa kama Zawadi

 Memberships Gifting

Uanachama unaotolewa kama zawadi unakuwezesha wewe au wanachama wa chaneli yako kununua fursa zinazofanya watazamaji wafikie manufaa ya uanachama katika chaneli. Wewe au wanachama wa chaneli yako mnaweza kununua uanachama unaotolewa kama zawadi wakati wa mitiririko mubashara au Maonyesho ya kwanza.

Ikiwa unatoa kiwango cha uanachama cha chini ya $5, huenda ukapata ofa za uanachama unaotolewa kama zawadi ili uzisambaze kwa watazamaji kila mwezi. Ofa za uanachama unaotolewa kama zawadi hupatikana bila malipo na huchumi mapato kutokana na uanachama huu unaotolewa kama zawadi. Ofa za uanachama unaotolewa kama zawadi zinapatikana tarehe moja ya kila mwezi na hauhamishwi mwezi hadi mwezi. Ni lazima usambaze ofa za uanachama unaotolewa kama zawadi kabla uweze kuwanunulia watazamaji wako uanachama unaotolewa kama zawadi. Unaweza kusambaza ofa za uanachama unaotolewa kama zawadi katika seti za 5, kwa namna sawa na unavyosambaza uanachama unaotolewa kama zawadi unaonunua wakati wa mitiririko mubashara au Maonyesho ya kwanza: Ili uone ofa yako ya uanachama unaotolewa kama zawadi, nenda kwenye mtiririko mubashara au gumzo la moja kwa moja la Onyesho la kwanza kisha Uchague  kisha Zawadi za uanachama  kisha Toa zawadi 5 sasa.

Kumbuka: Ofa za uanachama unaotolewa kama zawadi hazipatikani katika akaunti za biashara kwa sasa. Endelea kufuatilia tunapopanua upatikanaji mpana zaidi katika miezi ijayo.

Wewe au mwanachama wa chaneli yako mnaponunua uanachama unaotolewa kama zawadi, sehemu ya gumzo inayoonyesha muda uliosalia itaangazia ununuzi huo kwenye gumzo la moja kwa moja kwa kipindi kifupi. Kipindi cha muda kinategemea gharama. Gumzo la moja kwa moja au mtiririko mubashara ukiisha kabla ya zawadi kutangazwa, bado itasambazwa kwa watazamaji.

Watazamaji lazima wajijumuishe ili kutimiza masharti ya uanachama unaotolewa kama zawadi. Mtazamaji anapojijumuisha ili kuruhusu zawadi kutoka kwenye chaneli yako, anatimiza masharti ya kupata uanachama unaotolewa kama zawadi kwa zawadi zozote zilizopo au zitakazotolewa baadaye kwenye chaneli yako.

Unaweza kuwahimiza watazamaji wajijumuishe ili kupata zawadi kwa kushiriki URL yako maalum ya kujijumuisha kwenye chaneli na maudhui yako:

  • www.youtube.com/channel/{external_channel_id}/allow_gifts, OR
  • www.youtube.com/channel/{channel_name}/allow_gifts

Unaweza kupata kitambulisho maalum cha nje cha chaneli yako hapa.

​​Ununuzi wa uanachama unaotolewa kama zawadi unachukuliwa kuwa umekamilika baada ya YouTube kutoa zawadi ya kwanza kwa mtazamaji. Unaweza kupata ripoti ya uanachama unaotolewa kama zawadi kwenye Takwimu za YouTube. Chagua 'Aina ya Uanachama' ili uangalie idadi ya uanachama unaotolewa kama zawadi ulionunuliwa na kutumiwa katika kipindi kilichochaguliwa.

Kuwazuia wanachama wasitoe maoni
Huwezi kumwondoa mtu yeyote ambaye amejiunga kuwa mwanachama, lakini unaweza kuzuia maoni yake. Ili kuzuia maoni kutoka kwa watazamaji mahususi, utahitaji kuweka vichujio vya maoni na gumzo la moja kwa moja.

Kuweka na kudhibiti video yako ya utangulizi

Weka video ya utangulizi kwa ajili ya wanachama watarajiwa
Yeyote anayebofya kitufe cha Jiunge ataona video yako ya utangulizi.

Unachopaswa kujua kabla ya kuweka video ya utangulizi

  • Matangazo hayataonyeshwa kwenye video za utangulizi.
  • Video yako ya utangulizi lazima ifuate Mwongozo wa Jumuiya ya YouTube.
  • Video yako ya utangulizi haipaswi kuwa na madai ya hakimiliki ya wengine.
  • Video yako ya utangulizi haipaswi kuwa na madai ya muziki.
  • Video yako ya utangulizi haipaswi kubainishwa kuwa inalenga watoto.
  • Iwapo ungependa kutaja bei mahususi za viwango vyako vya uanachama, kumbuka kuwa bei zinaweza kutofautiana kulingana na mfumo na nchi.

Jinsi ya kuweka au kuhariri video ya utangulizi

  1. Buni video yako ya utangulizi na uhakikishe unaichapisha kama video ambayo Haijaorodheshwa.
  2. Nenda kwenye studio.youtube.com.
  3. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Chuma mapato kisha bofya Uanachama.
  4. Bofya Weka video ya Utangulizi kwenye kadi ya Ofa zako kwa wanachama.
  5. Ili kuhariri au kufuta video ya utangulizi iliyopo, bofya Hariri  karibu na video ya utangulizi kwenye kadi Ofa zako kwa wanachama.

Mapato, bei na urejeshaji wa pesa za uanachama katika chaneli

Ugavi wa mapato

Watayarishi hupata asilimia 70 ya mapato ya uanachama baada ya kodi na ada husika kukatwa. Kwa sasa, gharama zote za miamala (ikijumuisha ada za kadi za mikopo), zinashughulikiwa na YouTube.
Ugavi wa mapato kwa watayarishi katika Mitandao ya Chaneli Mbalimbali
Iwapo umejiunga na Mtandao wa Chaneli Mbalimbali, unapaswa kuwasiliana na mtandao wako. Baadhi ya Mitandao ya Chaneli Mbalimbali inaweza kuchukua mgawo wa ziada wa mapato. Hii inamaanisha kuwa huenda mapato yako ya uanachama yakawa chini ya 70% iwapo upo katika Mtandao wa Chaneli Mbalimbali.
Ni wajibu wako na Mtandao wa Chaneli Mbalimbali (panapohitajika) kutii sheria zote za kodi zinazotumika katika mapato yenu ya uanachama.

Kuripoti mapato

Unaweza kuona ripoti za mapato katika Takwimu za YouTube > Ripoti za Mapato ya Miamala. Utapokea mapato ya uanachama jinsi unavyopokea mapato ya matangazo kwenye AdSense katika YouTube.

Kutamatisha, kusimamisha na kurejeshewa pesa

Wanachama wanaweza kutamatisha uanachama wao wakati wowote.
Iwapo mwanachama ataomba kurejeshewa pesa, YouTube inaweza kuamua kwa hiari yake pekee uhalali wa dai hilo na inaweza kukata kiasi hicho kwenye mgawo ambao chaneli itapata. Pata maelezo kuhusu sera ya kurejesha pesa ya YouTube kwa uanachama unaolipiwa.

Uanachama ukisimamishwa kwenye kituo kwa sababu kituo kimesimamishwa, wanachama wote wanaolipa watarejeshewa malipo yao ya mwisho. Sababu zingine za kurejesha pesa ni pamoja na kuondolewa kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube au kwa sababu ya matumizi mabaya, ulaghai au ukiukaji wa sheria na masharti au sera zetu. Mgawo wa chaneli wa mapato yatakayorejeshwa utakatwa kwenye chaneli.

Maswali Yanayoulizwa Sana

Huenda kuna sababu kadhaa zinazosababisha hali hii, ikiwa ni pamoja na:
  • Kipengelee hiki hakijazinduliwa kwenye chaneli yako.
  • Kipengele hiki hakijazinduliwa katika nchi zote.
  • Video yako imebainisha kuwa inalenga watoto.
  • Kitufe cha "Jiunge" bado hakijazinduliwa kwenye baadhi ya mifumo. Hata hivyo, watazamaji wanaweza kujiunga kupitia kompyuta ya mezani. Bado unaweza kufikia manufaa kwenye mifumo yote inayopatikana ikiwa utajisajili kupitia kompyuta ya mezani.
  • Kitufe cha "Jiunge" kitaonekana tu kwenye kurasa za kutazama za video zinazotimiza masharti za chaneli zinazoshiriki. Kwa mfano, haturuhusu kurasa za kutazama za video zinazodaiwa na washirika fulani wa muziki.
  • Kitufe cha "Jiunge" hakionekani kwa watazamaji ambao hawajajisajili, wanaotumia vifaa vya mkononi. Watazamaji wanaotumia vifaa vya mkononi lazima wajisajili kwenye chaneli yako kwanza, ili kitufe cha "Jiunge" kionekane.

Ikiwa watazamaji wako hawaoni kitufe cha kujiunga, unaweza kuwakumbusha mbinu hizi za utatuzi kila wakati:

  • Wakumbushe watazamaji kwamba wanaweza kuwa wanachama kwa kubofya kitufe cha Jiunge kwenye ukurasa wa kwanza wa chaneli yako.
  • Watazamaji wanaweza kuongeza /join katika sehemu ya mwisho ya URL ya chaneli yako ili kujiunga moja kwa moja na dirisha lako la ofa kwa wanachama.
  • Unaweza pia kuongeza katika kiungo chako cha /join kwenye maelezo ya video yako.
Ninawezajie kupata data zaidi kuhusu wanachama wangu?
Tuna Members API inayokuwezesha kufikia maelezo yafuatayo kuhusu wanachama wako. Ikiwa unatumia kampuni ya wengine kutoa manufaa, unaweza kuwatumia maelezo haya kuhusu wanachama wako ili uweze kutoa manufaa ya uanachama.
  • The member's channel URL 
  • The name of the member's channel
  • A link to the member's profile picture
  • When the member joined your channel 
Note: The Members API Service currently does not provide information about a member’s level.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
10202375510742098651
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false