Kupakia video za YouTube

Kipengele kipya cha kina kwenye YouTube: Kuanzia tarehe 17 Agosti, 2023, badilisha Video zako Fupi ili ujumuishe kiungo kwenye video nyingine moja kutoka katika kituo chako. Kiungo kitaonekana kwenye kichezaji cha Video Fupi na kitasaidia kuelekeza watazamaji kutoka kwenye Video Fupi kwenda katika maudhui yako mengine ya YouTube. Unaweza kuunganisha Video, Video Fupi na maudhui ya Moja kwa Moja. Video unayochagua inapaswa kuwa ya umma au iwe haijaorodheshwa na isikiuke Mwongozo wetu wa Jumuiya. Badiliko hili litasambazwa taratibu na huenda lisipatikane kwenye vituo au kwa watazamaji wote hadi kipengele kitakaposambazwa kabisa.

Unaweza kupakia video kwenye YouTube kwa kufuata hatua chache rahisi. Tumia maagizo yaliyo hapa chini ili upakie video zako kutoka kwenye kompyuta au kifaa cha mkononi. Huenda usiweze kupakia ikiwa matumizi yako yanasimamiwa kwenye YouTube. Pata maelezo zaidi hapa.

Kupakia video

Tumia programu ya YouTube kwenye Android kupakia video kwa kurekodi video mpya au kuchagua iliyopo.

Kupakia kwenye YouTube kupitia kompyuta kibao au simu yako ya Android

Programu ya YouTube

  1. Fungua programu ya YouTube .
  2. Gusa Tayarisha  kisha Pakia video.
  3. Chagua faili ambayo ungependa kupakia kisha uguse ENDELEA.
    • Iwapo video yako ina urefu usiozidi sekunde 60 na ina uwiano wa mraba au wima, itapakiwa kama Video Fupi. Pata maelezo zaidi.
    • (Si lazima) Iwapo video yako ina urefu wa zaidi ya sekunde 60 na ina uwiano wa mraba au wima, unaweza kugusa “Badilisha iwe Video Fupi” ili upunguze video yako na uipakie kama Video Fupi. Pata maelezo zaidi.

​Ukifunga hali ya upakiaji kabla ya kukamilisha kuchagua mipangilio yako, video yako itahifadhiwa ikiwa rasimu kwenye ukurasa wako wa Maudhui.

Programu ya Studio ya YouTube

Kumbuka: Huwezi kuthibitisha mwenyewe ukadiriaji wa video zako kupitia programu ya Studio ya YouTube.
  1. Fungua programu ya Studio ya YouTube .
  2. Kwenye sehemu ya juu, gusa Tayarisha  kisha Pakia video
  3. Chagua faili ambayo ungependa kupakia
  4. Weka maelezo kwenye video yako, kama vile jina (lisizidi herufi 100), mipangilio ya faragha na mipangilio ya uchumaji wa mapato. 
  5. Gusa Endelea
  6. Chagua hadhira yako, "Ndiyo, inalenga watoto" au "Hapana, hailengi watoto." Pata maelezo zaidi kuhusu video zinazolenga watoto.
  7. Gusa Pakia video ili uchapishe video yako.  

Maelezo

Weka maelezo muhimu kwenye video yako.
Kijipicha Picha ambayo watazamaji wataona kabla ya kubofya video yako.
Mada

Mada ya video yako.

Kumbuka: Mada za video zinaruhusiwa kuwa na idadi ya juu ya herufi 100 na haziwezi kujumuisha herufi zisizoruhusiwa.

Maelezo

Maelezo yanayoonyeshwa chini ya video yako. Kwa maelezo ya video, tumia muundo ufuatao:

[Jina la Kituo]|[Mada ya Video]|[Kitambulisho cha Video].

Ili ubadilishe muundo wa maandishi, angazia maandishi ambayo ungependa kubadilisha na uteue chaguo kwenye upau wa kubadilishia. Unaweza kutumia herufi nzito, italiki au kukata maandishi kati.

Maelezo ya video yanaruhusiwa kuwa na idadi ya juu ya herufi 5,000 na hayawezi kujumisha herufi zisizoruhusiwa.

Uonekanaji

Chagua mipangilio ya faragha ya video yako ili udhibiti sehemu ambapo video yako inaweza kuonekana na wanaoweza kuitazama.

Iwapo uko katika Mpango wa Washirika wa YouTube, unaweza kuweka video yako kuwa ambayo haijaorodheshwa au ya faragha hadi ukaguzi ukamilike. Ili uarifiwe baada ya ukaguzi kukamilika, unaweza kujijumuisha kupokea arifa katika programu ya Studio ya YouTube. Kumbuka: Tunasambaza kipengele hiki polepole. ​​

Mahali Weka mahali ambapo video yako ilirekodiwa.
Orodha ya kucheza Weka video yako kwenye mojawapo ya orodha zako zilizopo za kucheza, au utunge orodha ya kucheza.

Bofya ENDELEA ili uchague hadhira yako. 

Hadhira Ili kutii Sheria ya Kulinda Faragha ya Watoto Mtandaoni (COPPA), unapaswa kutufahamisha iwapo video zako zinalenga watoto.
Mipaka ya umri Weka mipaka ya umri kwenye video ambazo huenda hazifai hadhira zote. 

Ukaguzi

Ukaguzi wa matatizo ya hakimiliki na ufaafu wa kuwekwa matangazo 

Iwapo uko katika Mpango wa Washirika wa YouTube, ukaguzi unakuruhusu kuchunguza video zako ili kubaini matatizo ya hakimiliki na ufaafu wa kuwekwa matangazo. 
Ukaguzi huu unakusaidia upate maelezo kuhusu vikwazo vinavyoweza kuwepo ili uweze kurekebisha matatizo kabla ya video yako kuchapishwa. 
Kumbuka: Matokeo ya ukaguzi wa Hakimiliki na Ufaafu kwa matangazo si ya mwisho. Kwa mfano, madai ya baadaye ya Content ID unayofanya mwenyewe, maonyo ya hakimiliki na mabadiliko kwenye mipangilio ya video yako yanaweza kuathiri video yako.

Kudhibiti arifa zako za ukaguzi

Unaweza kuwasha arifa za programu ili ufahamu kwa urahisi ukaguzi wa video zako unapokamilika. 

Kumbuka: Hakikisha kuwa umewasha arifa kwenye vifaa vyako vya mkononi na umeingia katika akaunti sahihi.

Programu ya Studio ya YouTube

  1. Fungua programu ya Studio ya YouTube .
  2. Gusa picha yako ya wasifu kisha Mipangilio .
  3. Chini ya “Arifa,” gusa Arifa za programu .
  4. Washa au uzime kipengele cha “Sera”. 

Pata maelezo zaidi kuhusu kupakia video

Idadi ya video unazoweza kupakia kwa siku

There's a limit to how many videos a channel can upload each day across desktop, mobile, and YouTube API. To increase your daily limit, visit this article.

Sehemu ya “Yanayoangaziwa katika video hii” kwenye Android

Iwapo video yako inaangazia mtayarishi anayetafutwa zaidi, watazamaji kwenye Android wanaweza kupata kiungo kwenye ukurasa wa kutazama kinachoelekeza katika kituo cha mtayarishi huyo anayeangaziwa. Watazamaji pia watakuwa na chaguo la kufuatilia watayarishi wanaoangaziwa. Kipengele hiki hufanya iwe rahisi kwa watazamaji kugundua watayarishi wapya na kufuatilia vituo vyao.

Kikundi kipana cha watayarishi wanaotafutwa zaidi kwenye YouTube huwekewa lebo kiotomatiki. Huwezi kuwekea watayarishi lebo mwenyewe.

Jinsi ya kuondoa lebo

Iwapo ulibuni video, unaweza kugusa jina la mtayarishi anayeangaziwa na uchague kumwondoa kwenye video.

Iwapo umewekewa lebo katika video, unaweza kugusa jina lako kwenye ukurasa wa kutazama na uchague kujiondoa kwenye video hiyo. Unaweza pia kuchagua kujiondoa kwenye video ambako umetajwa katika kituo hiki.

Kupakia kupitia mtandao wa simu ikilinganishwa na Wi-Fi

Unaweza kubadilisha aina ya muunganisho unaotumiwa kupakia video zako.

  1. Gusa picha ya wasifu wako .
  2. Gusa Mipangilio kisha Jumla.
  3. Gusa Ulizopakia.
  4. Chagua kati ya kupakia video kupitia Wi-Fi au mtandao wako wa simu.

Pata maelezo kuhusu tofauti kati ya “kupakia” na “kuchapisha”

Unapopakia video, faili ya video hupakiwa kwenye YouTube.
Unapochapisha video, itaweza kutazamwa na mtu yeyote aliye na idhini ya kuitazama.
Kupakia video wima
Unapopakia video yako, YouTube itabaini njia bora zaidi ya kuonyesha maudhui. Ili upate hali bora zaidi, usiweke pau nyeusi pembeni mwa video yako wima. Iwe video ni ya wima, mraba au mlalo, video hiyo itatoshea kwenye skrini.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
8014378246268412364
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false