Kuanza kutumia Ununuzi kupitia YouTube

Vipengele vya Ununuzi kwenye YouTube vinawezesha Watayarishi waliotimiza masharti kutangaza bidhaa zao kwa urahisi kwenye maduka yao wenyewe au biashara nyingine kote kwenye YouTube. Kwa kutumia vipengele vya Ununuzi kwenye YouTube, unaweza:

  • Kuunganisha duka lako kwenye YouTube ili uangazie bidhaa zako katika maudhui yako.
  • Kuwekea lebo bidhaa za chapa zingine katika maudhui yako.
  • Kuangalia takwimu zako za Ununuzi katika Takwimu za YouTube ili uangalie utendaji wa bidhaa ulizowekea lebo.

Vipengele vya Ununuzi kwenye YouTube vinajumuisha:

  • Duka la chaneli yako
  • Bidhaa za duka lako lililounganishwa zinazoonyeshwa katika maelezo na rafu ya bidhaa 
  • Bidhaa zilizowekewa lebo kwenye video, Video Fupi na mitiririko yako mubashara

Kutangaza bidhaa zako

Ili utangaze bidhaa zako mwenyewe kwenye YouTube, unaweza:

  1. Kutimiza masharti ya kujiunga
  2. Kuunganisha duka lako kwenye YouTube
  3. Kuwekea lebo bidhaa za duka lako ili uziangazie katika maudhui yako

Ununuzi kwenye YouTube: Wekea lebo na Uuze Bidhaa kutoka kwenye Duka Lako

Watazamaji walio katika maeneo haya wanaweza kuvinjari na kununua bidhaa zako katika mifumo hii kwenye YouTube:

  • Kwenye duka la chaneli yako
  • Kama bidhaa kwenye maelezo ya video
  • Katika rafu ya bidhaa inayopatikana chini ya maudhui yako
  • Kwa kubofya kitufe cha Ununuzi kwenye maudhui yako 

Kumbuka: Tunaonyesha maelezo kamili ya bidhaa kwa watazamaji kulingana na nchi za mauzo ambazo duka huweka kwenye Google Merchant Center. Ikiwa video inaambatana na kanusho la "Usafirishaji wa Bidhaa Umezuiwa katika Baadhi ya Maeneo" kwenye nchi mahususi, basi inamaanisha kuwa muuzaji hajalenga nchi hii kwenye Google Merchant Center. Unaweza kuwasiliana na muuzaji wa rejareja au msimamizi wako wa duka la mtandaoni ili upate maelezo zaidi. Mifumo na wauzaji wa rejareja wana wajibu binafsi wa kuwezesha usafirishaji katika masoko ya ndani. Unaweza kuenda kwenye mfumo au tovuti ya muuzaji wa rejareja ili upate maelezo yaliyosasishwa kuhusu huduma yao ya usaidizi kwa usafirishaji wa ndani. Pia unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu jinsi wauzaji wanaweza kubadilisha nchi wanakouza.

Ustahiki wa chaneli ili kutangaza bidhaa zako

Ili kutangaza bidhaa zako kwenye YouTube, ni lazima chaneli yako itimize masharti haya ya msingi:

Baada ya kuthibitisha kwamba umetimiza masharti ya kujiunga, unaweza kuunganisha duka lakoili uwashe vipengele vya Ununuzi katika chaneli yako. Ikiwa hutimizi upeo wa Mpango wa Washirika wa YouTube (YPP) au wanaofuatilia, unaweza kukagua nyenzo hizi ili zikusaidie kukuza chaneli yako.

Kutangaza bidhaa kutoka biashara nyingine

Kuwekea lebo na Kuuza Bidhaa Zako Ukitumia Huduma ya Ununuzi kwenye YouTube! 🛍️

Unaweza kuwekea lebo na kutangaza bidhaa za biashara nyingine kwenye maudhui yako. Ili uweke lebo kwenye bidhaa za biashara nyingine katika maudhui yako, ni lazima:

  1. Utimize masharti ya kujiunga.
  2. Ufuate mwongozo wetu wa kuweka lebo.
  3. Kuweka lebo kwenye bidhaa katika maudhui yako.

Masharti ya chaneli kustahiki kutangaza bidhaa za biashara nyingine

Ili utangaze bidhaa za biashara nyingine kwenye maudhui yako, ni lazima chaneli yako itimize masharti haya ya msingi:

  • Uwe umejiunga katika Mpango wa Washirika wa YouTube
  • Uwe unaishi Korea Kusini au Marekani.
  • Chaneli yako iwe na zaidi ya watu 10,000 wanaoifuatilia.
  • Chaneli yako si chaneli ya muziki, Chaneli Rasmi ya Msanii au inayohusishwa na washirika wa muziki. Washirika wa muziki wanaweza kujumuisha studio za kurekodia muziki, wasambazaji, wachapishaji, au VEVO.
Mipangilio ya hadhira ya chaneli yako haijawekwa kuwa Inalenga Watoto na chaneli yako haina idadi kubwa ya video ambazo zimewekwa kuwa zinalenga watoto.

Utendaji na mapato ya ununuzi

Bidhaa kutoka maduka uliyounganisha

Unaweza kuangalia utendaji wa kiwango cha juu wa bidhaa ulizowekea lebo katika sehemu ya Ununuzi ya Studio ya YouTube au kwa kutumia ripoti za kina kwenye Takwimu za YouTube. Ili upate maelezo ya kina na yaliyosasishwa kuhusu mapato, nenda kwenye tovuti ya mfumo wako wa bidhaa za matangazo au muuzaji wa rejareja Kumbuka, malipo yote yanayotokana na mauzo ya bidhaa za matangazo na bidhaa zingine yanafanywa kupitia mfumo au muuzaji anayeshughulikia bidhaa zako. YouTube na AdSense hazihusiki.

Bidhaa za biashara nyingine

Unaweza kutumia ripoti zilizopanuliwa kwenye Takwimu za YouTube ili kupima hali ya kushirikisha katika bidhaa zako zilizowekewa lebo na ufahamu idadi ya watazamaji inayotokana na kurasa za bidhaa.

Sera

Bidhaa kutoka maduka uliyounganisha

Muuzaji wako anayeshughulikia bidhaa au mfumo wako rasmi (si Google) ndiye anawajibikia vipengee vyote vya mauzo ya bidhaa za biashara, ikiwa ni pamoja na, lakini si tu:

  • Kutangaza bidhaa na/au huduma
  • Uwekaji Boharini
  • Kufikisha agizo
  • Kurejesha pesa
  • Huduma kwa wateja
  • Usimamizi wa orodha ya vitu
  • Malipo kwa mtayarishi au msanii

Kushiriki data kati ya wauzaji wa rejareja au mifumo na Google

Data inayohusiana na mauzo ya bidhaa na mara ambazo wateja wametembelea chaneli, itashirikiwa kati ya wauzaji wa rejareja na Google kwa ajili ya kuboresha bidhaa na kukupa takwimu faafu. Kwa mfano, tunaweza kushiriki data tunayopata kutoka kwa muuzaji wako wa rejareja kuhusu jumla ya mauzo ya kila mwezi ya bidhaa kwenye Studio yako ya YouTube. Pia, tunaweza kutumia data hii kutathmini iwapo vipengele vipya vinasaidia kuongeza mauzo katika chaneli yako. Wauzaji wa rejareja hupata data inayohusiana na wanaotembelea kutoka katika vipengele vya Ununuzi kwenye YouTube kwa ajili ya takwimu zao.

Muuzaji wako wa rejareja atashughulikia au kutumia data ya mauzo kwa mujibu wa sheria na masharti yake, ikiwa ni pamoja na sera ya faragha. Google itatumia au kushughulikia data hiyo ya Mauzo kwa mujibu wa Sera yetu ya Faragha. Hakikisha kuwa unasoma na kuelewa sera hizi.

Bidhaa za biashara nyingine

Unapoangazia bidhaa za biashara nyingine, miamala na shughuli zozote kwenye tovuti ya muuzaji wa rejareja zitafanywa kwa mujibu wa sheria na masharti ya muuzaji wa rejareja, ikiwa ni pamoja na sera zake za faragha. Muuzaji wa rejareja atabainisha bei ya mwisho na kodi pamoja na ada zinazotozwa. Muuzaji wa rejareja atashughulikia oda yote, ikiwa ni pamoja na:

  • Kutekeleza oda
  • Usafirishaji
  • Malipo
  • Usaidizi (ikiwa ni pamoja na kurejeshwa kwa bidhaa na pesa)

Watazamaji wanaweza kuwasiliana na muuzaji wa rejareja iwapo wana matatizo au maswali yoyote yanayohusiana na oda, ikiwa ni pamoja na kurejeshwa kwa bidhaa na pesa.

Orodha za bidhaa za kipekee kwenye chaneli

Wauzaji wanaostahiki wanaweza kutuma orodha ya bidhaa kwa chaneli mahususi za YouTube kwa upekee kutoka ndani ya akaunti zao za Google Merchant Center au kwa mtiririko maalum ndani ya mfumo wa Cafe24. Wauzaji wanaweza kufanya hivyo kwa kuonyesha ni chaneli zipi zinashughulikia uorodheshaji wa bidhaa mahususi kama sehemu ya mipasho yao ya kuorodhesha. Kwa kutumia kipengele hiki, wauzaji wanathibitisha kuwa bidhaa au matangazo hayo ya bidhaa ni ya kipekee kwa chaneli mahususi ya YouTube na hayapatikani kwenye chaneli zingine za mauzo au kwa watayarishi wengine wa YouTube. Uorodheshaji umetiwa alama kuwa wa kipekee kwenye chaneli hiyo kwa muda wote wa uorodheshaji na umeangaziwa kwa watazamaji ikiwa una bei ya punguzo na/au umewekwa kuwa wa muda mfupi. Uorodheshaji wa kipekee unategemea sheria na masharti ya muuzaji, ikijumuisha sera zake za faragha. Muuzaji anabainisha na kuwajibika kwa bei ya mwisho na masharti ya ununuzi.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
315152589466602654
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false