Chagua jinsi unavyotaka kuchuma mapato

Tunapanua Mpango wa Washirika wa YouTube (YPP) kwa watayarishi wengi zaidi kwa kuwapa uwezo wa kufikia mapema vipengele vya Ununuzi na ufadhili kutoka kwa mashabiki. Mpango wa Washirika wa YouTube uliopanuliwa unapatikana kwa watayarishi wanaostahiki katika nchi au maeneo haya. Upanuzi utasambazwa mwezi ujao kwa watayarishi wanaostahiki nchini AE, AU, BR, EG, ID, KE, KY, LT, LU, LV, MK, MP, MT, MY, NG, NL, NO, NZ, PF, PG, PH, PT, QA, RO, RS, SE, SG, SI, SK, SN, TC, TH, TR, UG, VI, VN, and ZA. Soma makala haya ili upate maelezo zaidi kuhusu mabadiliko kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube.

Ikiwa huishi katika mojawapo ya nchi au maeneo yaliyotajwa hapo juu, hakuna mabadiliko kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube yanayokuhusu. Unaweza kusoma makala haya ili upate muhtasari wa Mpango wa Washirika wa YouTube, masharti ya kujiunga na maagizo ya kutuma ombi yanayokufaa.

Angalia iwapo unastahiki kushiriki kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube uliopanuliwa. Iwapo bado hujastahiki, chagua Pata arifa katika sehemu ya Chuma mapato ya Studio ya YouTube. Tutakutumia barua pepe tutakapokusambazia Mpango wa Washirika wa YouTube uliopanuliwa na utakapokuwa umetimiza masharti ya upeo wa kutimiza masharti. 

Ikiwa upo katika Mpango wa Washirika wa YouTube (YPP), unaweza kuchuma mapato kupitia vipengele hivi vya uchumaji mapato ikiwa unatimiza upeo na masharti ya kujiunga:

Vigezo vya Kituo Vipengele vya Uchumaji wa Mapato
 • Watu 500 wanaofuatilia
 • Uwe umepakia video 3 za umma katika kipindi cha siku 90 zilizopita
 • Mojawapo ya hizi mbili:
  • Video zako ndefu ziwe zimetazamwa hadharani kwa muda wa saa 3,000 katika kipindi cha siku 365 zilizopita
  • Video zako Fupi ziwe zimetazamwa hadharani mara milioni 3 katika kipindi cha siku 90 zilizopita
 • Watu 1,000 wanaofuatilia
 • Mojawapo ya hizi mbili:
  • Video zako ndefu ziwe zimetazamwa hadharani kwa muda wa saa 4,000 katika kipindi cha siku 365 zilizopita
  • Video zako Fupi ziwe zimetazamwa hadharani mara milioni 10 katika kipindi cha siku 90 zilizopita

Kila kipengele cha uchumaji wa mapato kina masharti tofauti ya kujiunga. Makala haya yatakueleza jinsi unavyoweza kuwasha kila mojawapo ya vipengele hivi iwapo umetimiza masharti.

Utangulizi wa jinsi ya Kuchuma Mapato kwenye YouTube

Hakikisha kuwa umekamilisha hatua zote za kuwasha kipengele cha uchumaji wa mapato kwenye kituo chako cha YouTube ili ufikie mbinu za kuchuma mapato.

Kufikia mbinu za kuchuma mapato

Baada ya kujiunga kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube, washirika wanaweza kuchagua sehemu za mkataba ambazo wanastahiki ili wafungue fursa za kuchuma mapato. Pia, mbinu hii huwapa watayarishi uwazi na umakini mkubwa wa kuamua ni fursa zipi za uchumaji wa mapato zinafaa vituo vyao.

 1. Ingia katika akaunti kwenye Studio ya YouTube
 2. Katika menyu ya kushoto, chagua Chuma mapato.
 3. Bofya Anza kwa kila Sehemu isiyo ya lazima ili ukague na ukubali sheria na masharti.

Matangazo ya Ukurasa wa Kutazama

Kuanzia katikati ya mwezi Januari 2023, washirika walio katika Mpango wa Washirika wa YouTube (YPP) ni lazima wakague na kukubali masharti ya Sehemu ya Uchumaji wa Mapato kwenye Ukurasa wa Kutazama ili waendelee kuchuma mapato ya matangazo kwenye Ukurasa wa Kutazama.

Unaweza kuchuma mapato kutokana na matangazo yanayoonyeshwa kabla ya video kuanza, wakati video inacheza, baada ya video kuisha na katika video zako zilizo kwenye Ukurasa wa Kutazama. Unaweza pia kuchuma mapato mtumiaji aliyejisajili katika YouTube Premium anapotazama maudhui yako kwenye Ukurasa wa Kutazama.

Ukurasa wa Kutazama huwakilisha kurasa zilizo kwenye YouTube, YouTube Music na YouTube Kids zinazojikita katika maelezo na uchezaji wa video zako ndefu au zinazotiririshwa moja kwa moja. Ili uchume mapato ya matangazo na YouTube Premium kwenye video ndefu au zinazotiririshwa moja kwa moja, zilizotazamwa kwenye Ukurasa wa Kutazama au zinapopachikwa kwenye tovuti zingine katika Kicheza Video cha YouTube, ni sharti ukubali masharti ya Sehemu ya Uchumaji wa Mapato kwenye Ukurasa wa Kutazama.

Matangazo ya Mipasho ya Video Fupi

Kukubali masharti ya Sehemu ya Uchumaji wa Mapato kwenye Video Fupi huruhusu kituo chako kugawana mapato yanayotokana na matangazo yaliyotazamwa katikati ya video katika Mipasho ya Video Fupi. Ugavi wa mapato ya matangazo ya Video Fupi utaanza kutekelezwa kuanzia tarehe uliyokubali Sehemu hii. Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ugavi wa mapato ya matangazo unavyofanya kazi kwenye Video Fupi, soma Sera zetu za uchumaji wa mapato kwenye Video Fupi za YouTube.

Sehemu ya Bidhaa za Biashara

Sehemu ya Bidhaa za Biashara (na Masharti ya Ziada ya Bidhaa za Biashara yaliyokuwepo awali) hukuwezesha kuchuma mapato kupitia vipengele vya ufadhili kutoka kwa mashabiki huku ukiwasiliana na mashabiki wako. Vipengele vya ufadhili kutoka kwa mashabiki vinajumuisha uanachama katika kituo, Super Chat, Super Stickers na Shukrani Moto. Ili uchume mapato kupitia vipengele vya ufadhili kutoka kwa mashabiki, ni sharti ukubali masharti ya Sehemu ya Bidhaa za Biashara (CPM) na uwashe vipengele mahususi. Watayarishi waliotia sahihi kwenye Masharti ya Ziada ya Bidhaa za Biashara (CPA) hawahitaji kutia sahihi kwenye Sehemu mpya ya Bidhaa za Biashara. Ili upate maelezo zaidi kuhusu vipengele vya ufadhili kutoka kwa mashabiki na sera zinazotumika, soma sera za uchumaji mapato kwenye Bidhaa za Biashara kwenye YouTube.

Kuwasha matangazo ya Ukurasa wa Kutazama

Ikiwa video yako inatii mwongozo wetu wa maudhui yanayofaa watangazaji, unaweza kuwasha matangazo. Ikiwa huna uhakika iwapo video yako imetimiza masharti, angalia mwongozo wa uthibitishaji unaojifanyia na mifano kwenye ukurasa huo. Kuchagua kuwasha matangazo hakumaanishi kuwa matangazo yatafunguka kiotomatiki kwenye video. Kabla tangazo lolote halijaonekana, video itapitia mchakato wa kawaida ikiwa ni pamoja na ukaguzi wa kiotomatiki au unaofanywa na watu ili kuthibitisha kuwa inatii mwongozo wetu.

Kwa kuwasha matangazo katika video kwenye YouTube, unathibitisha kuwa una haki zote zinazostahili za vipengee vya kuona na sauti katika video hizi.

Kuwasha matangazo katika video mahususi

 Ili uwashe matangazo kwenye video moja ambayo umeshapakia:

 1. Nenda kwenye Studio ya YouTube.
 2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui .
 3. Karibu na video husika, bofya Uchumaji wa mapato .
 4. Bofya Washa katika menyu kunjuzi ya uchumaji wa mapato.
 5. Bofya Hifadhi.

Kuwasha matangazo kwenye video nyingi

Ili uwashe matangazo kwenye video nyingi ambazo umeshapakia tayari:

 1. Nenda kwenye Studio ya YouTube.
 2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui .
 3. Teua kisanduku cha kijivu kilicho upande wa kushoto wa kijipicha cha video yoyote unayotaka kutumia kuchuma mapato.
 4. Bofya menyu kunjuzi ya Badilisha katika upau mweusi ulio juu ya orodha ya video kisha Uchumaji wa mapato.
 5. Bofya Washa katika menyu kunjuzi ya uchumaji wa mapato.
  • Ili ubadilishe mipangilio ya matangazo yanayochezwa katikati ya video kwa wingi: Bofya Badilisha kisha Mipangilio ya matangazo kisha Teua kisanduku karibu na “Weka matangazo wakati video inacheza (katikati ya video)” na uamue ikiwa unataka matangazo yanayochezwa kiotomatiki katikati ya video bila mapumziko ya matangazo au video zote.
 6. Bofya Sasisha video kisha Teua kisanduku kilicho karibu na “Ninaelewa matokeo ya kitendo hiki” kisha Sasisha video.

Kuwasha matangazo ya Mipasho ya Video Fupi

Ni lazima maudhui yote yanayochuma mapato kupitia matangazo yafuate mwongozo wetu wa maudhui yanayofaa watangazaji. Kwenye Video Fupi, utazamaji wa maudhui unaofuata mwongozo wetu wa maudhui yanayofaa watangazaji ndio tu utakaostahiki katika ugavi wa mapato. Ili ushiriki katika ugavi wa mapato yanayotokana na matangazo yaliyotazamwa katikati ya video katika Mipasho ya Video Fupi, kagua na ukubali masharti ya Sehemu ya Uchumaji Mapato katika Video Fupi kwenye sehemu ya Chuma mapato ya Studio ya YouTube.​​​​​​

Kuwasha kipengele cha uanachama katika kituo

Kipengele cha uanachama katika kituo huwawezesha watazamaji kujiunga na kituo chako kupitia malipo ya kila mwezi na kupata manufaa ya wanachama pekee unayotoa, kama vile beji, emoji na bidhaa nyinginezo. Pata maelezo zaidi kuhusu masharti ya kujiunga na jinsi unavyoweza kuwasha kipengele cha uanachama katika kituo.

Kuwasha kipengele cha Ununuzi

Kipengele cha Ununuzi huwawezesha watayarishi kuunganisha maduka yao kwenye YouTube na kuangazia bidhaa zao, huku wakichuma mapato. Ikiwa umetimiza masharti, unaweza pia kutangaza bidhaa kutoka chapa zingine katika maudhui yako na uchume mapato. Pata maelezo zaidi kuhusu masharti ya kujiunga na jinsi kipengele cha Ununuzi kinavyofanya kazi.

Kuwasha Super Chat na Super Stickers

Super Chat na Super Stickers ni njia za kuunganisha mashabiki na watayarishi, wakati wa mitiririko mubashara na Maonyesho ya kwanza. Mashabiki wanaweza kununua Super Chat ili waangazie ujumbe wao ndani ya gumzo la moja kwa moja au Super Stickers ili wapate picha ya uhuishaji inayoonekana katika gumzo la moja kwa moja. Pata maelezo zaidi kuhusu masharti ya kujiunga na jinsi unavyoweza kuwasha Super Chat na Super Stickers.

Kuwasha kipengele cha Shukrani Moto

Shukrani moto huwaruhusu watayarishi kuchuma mapato kutoka kwa watazamaji wanaotaka kuonyesha shukrani za ziada kutokana na video zao. Mashabiki wanaweza kununua uhuishaji wa mara moja na kupata uwezo wa kuchapisha maoni ya kipekee, yaliyoangaziwa kwa rangi na yaliyowekewa mapendeleo katika sehemu ya maoni ya video. Pata maelezo zaidi kuhusu masharti ya kujiunga na jinsi unavyoweza kuwasha kipengele cha Shukrani Moto.

Kuwasha mapato ya YouTube Premium

Iwapo mtazamaji aliyejisajili kwenye YouTube Premium atatazama maudhui yako, utapata sehemu ya ada anayolipa kwenye YouTube Premium. Maudhui yote unayochapisha (yanayofuata Mwongozo wetu wa Jumuiya) yanatimiza masharti ya kuchuma mapato ya YouTube Premium. Ili uchume mapato ya YouTube Premium kwenye:

 • Video ndefu: Kubali masharti ya Sehemu ya Uchumaji wa Mapato kwenye Ukurasa wa Kutazama na uwashe matangazo ya Ukurasa wa Kutazama
 • Video Fupi: Kubali masharti ya Sehemu ya Uchumaji wa Mapato kwenye Mipasho ya Video Fupi

Pata maelezo zaidi kuhusu YouTube Premium.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Programu za Google
Menyu kuu