Mwongozo wa Jumuiya wa YouTube

Unapotumia YouTube, unajiunga na jumuiya ya watu kutoka ulimwenguni kote. Mwongozo ulio hapa chini husaidia kufanya YouTube iendelee kuwa sehemu ya burudani na furaha kwa kila mtu.

Ukiona maudhui ambayo unafikiri kuwa yanakiuka mwongozo huu, yaripoti.

Wakati mwingine, maudhui ambayo huenda yakakiuka Mwongozo wa Jumuiya yanaweza kusalia kwenye YouTube ikiwa yana muktadha wa Elimu, Hali Halisi, Sayansi au Sanaa (EDSA).. Katika hali hizi, maudhui yatapata ruhusa ya EDSA ya kutofuata kanuni.

Sera hizi zinatumika kwa aina zote za maudhui kwenye mfumo wetu, ikiwemo, kwa mfano maudhui yasiyoorodheshwa na ya faragha, maoni, viungo, Machapisho ya jumuiya na vijipicha. Orodha hii si kamili.

Kutayarisha kwa Kuzingatia Kanuni: Mwongozo wa Jumuiya ya YouTube

Taka na tabia za udanganyifu

Jumuiya ya YouTube imejengwa katika uaminifu. YouTube hairuhusu maudhui ambayo ni taka, yanayolenga kulaghai, kupotosha, au kudanganya watumiaji wengine.

Maudhui nyeti 

Tunatumai kuwalinda watazamaji, watayarishi na hasa watoto. Ndiyo maana tuna kanuni zinazohusu kuwalinda watoto dhidi ya maudhui ya ngono na uchi na kujijeruhi. Pata maelezo kuhusu kinachoruhusiwa kwenye YouTube na hatua za kuchukua ukiona maudhui ambayo hayafuati sera hizi.

Maudhui ya vurugu au hatari

YouTube hairuhusu matamshi ya chuki, tabia ya kunyatia, vurugu ya kuogofya, mashambulizi hasidi na maudhui yanayohimiza tabia hatari au za kudhuru.

Bidhaa zilizodhibitiwa

Huwezi kuuza bidhaa fulani kwenye YouTube. Pata maelezo kuhusu kinachoruhusiwa—na kisichoruhusiwa.

Maelezo ya kupotosha

YouTube hairuhusu aina fulani za maudhui yanayopotosha au ya udanganyifu yanayoweza kusababisha madhara mabaya sana. Hii ni pamoja na aina fulani ya maelezo ya kupotosha yanayoweza kusababisha madhara katika mazingira halisi, kama vile kutangaza suluhisho au matibabu hatari, aina fulani za maudhui yaliyobadilishwa kwa ujanja, au maudhui yanayoathiri michakato ya demokrasia.

 

Maudhui ya Kielimu, Hali Halisi, Kisayansi na Kisanaa (EDSA)

Mwongozo wetu wa Jumuiya unalenga kufanya YouTube iwe jumuiya salama. Wakati mwingine, maudhui ambayo huenda yakakiuka Mwongozo wa Jumuiya yanaweza kusalia kwenye YouTube ikiwa yana muktadha wa Elimu, Hali Halisi, Sayansi au Sanaa (EDSA). Katika hali hizi, maudhui yatapata ruhusa ya kutofuata kanuni za EDSA. 

Pata vidokezo vya watayarishi kuhusu mwongozo na sera za YouTube.

Tafadhali fuata kanuni hizi kwa umakini. Iwapo tabia ya mtayarishi wa YouTube kwenye na/au nje ya mfumo wa YouTube inadhuru watumiaji, jumuiya, wafanyakazi au mfumo wetu, tunaweza kuchukua hatua kulingana na vigezo kadhaa, ikiwa ni pamoja na lakini si tu, makali ya vitendo vyake na iwapo kuna mtindo fulani wa tabia hatari. Hatua tutakayochukua itaanzia kusimamisha manufaa ya mtayarishi hadi kufunga akaunti.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
17562748491024664114
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false