Kutokana na vita vinavyoendelea Ukraini, tutasimamisha kwa muda kuwapatia matangazo ya Google na YouTube watumiaji walio nchini Urusi. Pata maelezo zaidi.
Mpango wa Washirika wa YouTube huwawezesha watayarishi kuchuma mapato kutokana na maudhui yao kwenye YouTube. Watayarishi wanaweza kugawana mapato yanayotokana na matangazo yaliyo kwenye video zao au kwa kutumia vipengele vingine vya uchumaji wa mapato. Tumia ukurasa huu kuelewa jinsi unavyochuma mapato, jinsi unavyolipwa na wakati unaweza kulipwa.
Ninachumaje mapato?Mapato ya utangazaji
Chini ya makubaliano ya ushirika ya YouTube, hakuna dhamana zozote kuhusu kiasi utakacholipwa au iwapo utalipwa. Mapato huzalishwa kulingana na mgawo wa mapato ya utangazaji kutoka kwa watazamaji wanaotazama video yako. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi matangazo yanavyoonekana kwenye video unazotumia kuchuma mapato.
Vipengele vingine vya uchumaji wa mapato
Ugavi wa mapato unarejelea asilimia yako ya mapato yote iliyobainishwa katika makubaliano ya ushirika wako mahususi na YouTube. Unaweza kuangalia makubaliano yako ili upate maelezo mahususi kuhusu kiwango chako cha ugavi wa mapato:
- Ingia katika akaunti kwenye Studio ya YouTube
- Kwenye menyu ya kushoto, chagua Mipangilio
- Chagua Makubaliano
- Bofya Angalia makubaliano karibu na kila mkataba ili upate maelezo kuhusu kiwango chako cha ugavi wa mapato
Pata maelezo zaidi kuhusu mahali pa kupata makubaliano yako.
Viwango vya ugavi wa mapato
Kuna Sehemu mahususi katika Studio ya YouTube ambazo washirika wanaweza kuchagua kwa hiari. Wakati wa kukagua sheria na masharti ya kila Sehemu, washirika wanaweza kupata maelezo zaidi kuhusu viwango vya ugavi wa mapato.
Sehemu ya Bidhaa za Biashara
Mshirika akiwasha vipengele vya ufadhili kutoka kwa mashabiki kwa kukagua na kukubali masharti ya Sehemu ya Bidhaa za Biashara, YouTube itamlipa asilimia 70 ya mapato halisi yanayotokana na vipengele vya uanachama katika chaneli, Super Chat, Super Stickers na Shukrani Moto.
Sehemu ya Uchumaji wa Mapato kwenye Ukurasa wa Kutazama
Mshirika akiwasha Matangazo ya Ukurasa wa Kutazama kwa kukagua na kukubali masharti ya Sehemu ya Uchumaji wa Mapato kwenye Ukurasa wa Kutazama, YouTube itamlipa asilimia 55 ya mapato halisi yanayotokana na matangazo yaliyoonyeshwa au yaliyotiririshwa katika video zake za umma kwenye Ukurasa wake wa Kutazama maudhui. Kiwango hiki cha ugavi wa mapato hutumika pia video zake za umma zinapotiririshwa ndani ya Kicheza Video cha YouTube kwenye tovuti au programu zingine.
Sehemu ya Uchumaji Mapato katika Video Fupi
Mshirika akiwasha Matangazo ya Mipasho ya Video Fupi kwa kukagua na kukubali masharti ya Sehemu ya Uchumaji Mapato katika Video Fupi, YouTube itamlipa asilimia 45 ya mapato aliyogawiwa kulingana na mgawo wake wa utazamaji katika Jumla ya Mapato ya Watayarishi yanayotokana na Video Fupi.
Takwimu za YouTube
Unaweza kuangalia makadirio ya mapato yako ya YouTube ukitumia Takwimu za YouTube.
- Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
- Kwenye menyu ya kushoto, chagua Takwimu.
- Kwenye menyu ya sehemu ya juu, chagua Mapato.
Katika mwonekano huu, unaweza kuangalia ripoti mbalimbali za mapato zinazohusiana na mapato yako. Pata maelezo zaidi kuhusu kutumia Takwimu za YouTube kuangalia mapato yako.
Makadirio ya mapato ya kila mwezi
Kumbuka kuwa makadirio ya mapato ya kila mwezi kama yanavyoonyeshwa katika Takwimu za YouTube yanaweza kubadilika:
AdSense katika YouTube
Mapato yako ya mwisho yanaonekana tu katika akaunti yako ya AdSense katika YouTube. Mapato halisi ya mwezi uliopita huwekwa kwenye salio la akaunti ya AdSense katika YouTube kati ya tarehe 7 na 12 ya kila mwezi.
Unaweza kupata mapato yako ya mwisho ndani ya akaunti yako ya AdSense katika YouTube.
- Ingia kwenye akaunti yako ya AdSense katika YouTube.
- Kwenye upande wa kushoto, chagua Mipangilio Malipo. Utaona jumla ya mapato yako ya kipindi ulichochagua na miamala yako ya mwisho.
Hatua ya Kuzuia kodi inaweza kuathiri mapato yako ya mwisho (ikiwa kodi inazuiwa) na kiasi kilichozuiwa kinaonekana tu katika akaunti yako ya AdSense katika YouTube.
Masharti ya kodi ya Marekani
Google huzuia kodi za Marekani kwenye mapato unayochuma kutokana na watazamaji nchini Marekani. Wasilisha taarifa zako za kodi ya Marekani katika akaunti yako ya AdSense katika YouTube ikiwa bado hujafanya hivyo ili Google iweze kubaini kiwango chako sahihi cha kodi ya zuio. Iwapo hutatoa taarifa za kodi, Google inaweza kuhitajika kuzuia kima cha juu zaidi cha kodi.
Watayarishi wote wanaochuma mapato wanatakiwa kuwasilisha taarifa za kodi ya Marekani, bila kujali mahali waliko duniani. Washirika wapya walio na akaunti mpya za AdSense katika YouTube wanatakiwa pia kuwasilisha taarifa hizo za kodi kabla hawajapata malipo yao ya kwanza. Pata maelezo zaidi kuhusu masharti ya kodi ya Marekani kwenye mapato ya YouTube na jinsi ya kuwasilisha taarifa zako za kodi ya Marekani kwa Google.
Dhima nyingine ya kulipa kodi
Kumbuka kuwa unaweza kuwajibika kulipa kodi kwa nchi au eneo unakoishi kwa mapato yoyote uliyochuma kutokana na video zako kwenye YouTube. Wasiliana na mamlaka ya kodi ya eneo husika ili upate mwongozo wa kina.
AdSense katika YouTube
Nyenzo muhimu
- AdSense katika YouTube
- Kufungua akaunti ya AdSense katika YouTube ili upokee malipo kwenye YouTube
- Kuweka njia yako ya malipo ya AdSense katika YouTube
- Hatua za kulipwa
- Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu malipo
Mtandao wa Chaneli Mbalimbali (MCN)
Malipo ya Ununuzi
Ratiba za malipo
- Mapato yako yakifikisha kima cha juu cha malipo cha eneo lako.
- Hakuna malipo yaliyosubirishwa kwenye akaunti yako.
- Umewasilisha taarifa zako za kodi ya Marekani.
- Uchumaji wa mapato haujasimamishwa au kusitishwa kwenye chaneli yako.
- Unatii sera za uchumaji wa mapato kwenye YouTube.