Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu Uhisani wa YouTube

Uhisani wa YouTube huwaruhusu watayarishi wasaidie mashirika ya misaada waliyochagua. Vituo vinavyostahiki vinaweza kuchangisha pesa kwa ajili ya mashirika yasiyo ya faida kwa kuweka kitufe cha kuchanga kwenye video na mitiririko yao mubashara. Watazamaji wanaweza kuchanga moja kwa moja kwenye ukurasa wa kutazama video au katika gumzo la moja kwa moja.

Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu Watayarishi na michango

Ni nani anastahiki kuchangisha pesa kwenye Uhisani wa YouTube?

Ili kuanzisha michango ya uhisani, ni sharti kituo chako kitimize masharti yafuatayo:

Kumbuka: Unaweza kuona uchangishaji kwenye vituo ambavyo havizingatii masharti ya kujiunga yaliyo hapo juu. Tunapanga kufanya Uhisani wa YouTube upatikane katika maeneo mengi baadaye.

Ni nchi au maeneo gani ambako unaweza kuweka mipangilio ya michango ya Uhisani wa YouTube?

Iwapo unaishi katika mojawapo ya nchi au maeneo yafuatayo, unaweza kuweka mipangilio ya Mchango wa Uhisani wa YouTube.

  • Ajentina
  • Austria
  • Ubelgiji
  • Bolivia
  • Kanada
  • Kolombia
  • Korasia
  • Estonia
  • Ufaransa
  • Ujerumani
  • Ghana
  • Hong Kong
  • Aisilandi
  • Indonesia
  • Ayalandi
  • Israeli
  • Italia
  • Kuwaiti
  • Lativia
  • Litwania
  • Lasembagi
  • Malesia
  • Meksiko
  • Montenegro
  • Uholanzi
  • Nyuzilandi
  • Norwe
  • Peruu
  • Ufilipino
  • Polandi
  • Pwetoriko
  • Romania
  • Slovakia
  • Hispania
  • Uswidi
  • Uswizi
  • Tailandi
  • Uturuki
  • Uingereza
  • Marekani

Ninaona kuwa ninaweza kufikia kipengele cha Uhisani wa YouTube. Je, utaratibu wa kuweka mipangilio ni upi?

Itakuwaje iwapo sioni kitufe cha kuchanga baada ya kuanzisha mchango?

Zifuatazo ni baadhi ya sababu zinazoweza kufanya kitufe cha kuchanga kisionekane kwenye mchango wako:
  • Hakikisha kuwa umeweka mipangilio ya mchango wa Uhisani wa YouTube.
  • Iwapo mchango una tarehe ya kuanza, kitufe cha kuchanga kitaonekana kwenye ukurasa wako wa kutazama au gumzo la moja kwa moja baada ya tarehe ya kuanza mchango.
  • Iwapo unachangisha kwenye mtiririko mubashara na umewasha gumzo la moja kwa moja, utaona kitufe cha kuchanga katika gumzo kwenye kifaa cha mkononi. Ni lazima vifaa vya mkononi viwe katika mkao wima ili uone gumzo la moja kwa moja. Pata maelezo zaidi kuhusu michango ya gumzo la moja kwa moja.
  • Iwapo umebainisha kuwa video au kituo chako "kinalenga watoto," kitufe cha kuchanga kitaondolewa. 

Ni nini maana ya michango ya jumuiya?

Michango ya jumuiya hukuruhusu ushirikiane na watayarishi wengine ili kuchangisha pesa kwa ajili ya lengo mlilonalo pamoja. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuanzisha au kujiunga na mchango wa jumuiya.

Ni nini kilifanyikia Super Chat for Good?

Super Chat for Good sasa ni Michango ya Gumzo la Moja kwa Moja. Bado watayarishi wanaweza kuandaa michango kwenye mitiririko yao mubashara na watazamaji wanaweza kuchanga moja kwa moja kupitia dirisha la gumzo. Super Chat na Super Stickers zitazimwa kwenye mitiririko mubashara yenye michango ili kuepuka mkanganyo. Unaweza kufuatilia michango ya watazamaji katika Ukurasa wa Kudhibiti Utiririshaji wa Moja kwa Moja kwenye Wijeti ya Shughuli za Mtazamaji.
Ili uwashe kipengele cha Michango ya Gumzo la Moja kwa Moja, weka mtiririko mubashara ulioratibiwa kwenye mchango wako. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuweka mipangilio ya mchango wa Uhisani wa YouTube. Mitiririko mubashara yenye gumzo la moja kwa moja itakuwa na aikoni ya kuchanga katika gumzo. Mitiririko mubashara isiyo na gumzo la moja kwa moja itakuwa na kitufe cha kuchanga karibu na au chini ya mtiririko.
Shukrani Moto hazipatikani kwenye video zilizo na Michango.

Je, bado ninaweza kuchuma mapato kwenye mitiririko mubashara au video ambazo zina mchango?

Matangazo hayataathiriwa unapoweka mchango kwenye mitiririko mubashara au video zako. Ili kuepuka mkanganyo, Super Chat na Super Stickers hazipatikani kwenye mitiririko mubashara iliyo na Michango ya Gumzo la Moja kwa Moja. Watayarishi hawawezi kuandaa gumzo la moja kwa moja la wanachama pekee lililo na kitufe cha kuchanga. Shukrani Moto hazipatikani kwenye video zilizo na Michango.

Mashirika Yasiyo ya Faida hupata vipi michango?

Google hushirikiana na Network for Good ili kukusanya na kusambaza michango kupitia ombi la Google. Kiasi chote cha mchango hutumwa kwa shirika lisilo la faida na YouTube italipia ada za miamala. Kama inavyotakiwa na Huduma ya Mapato ya Ndani ya Marekani, Network for Good ina udhibiti wa kipekee wa kisheria kwa michango inapotolewa. Iwapo Network for Good haiwezi kusambaza pesa hizo kwa shirika lisilo la faida lililochaguliwa na mtayarishi wa YouTube, Network for Good itasambaza pesa hizo kwa shirika lingine lisilo la faida la Marekani ambalo linastahiki. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi mchakato wa kusambaza pesa wa Network for Good hufanya kazi.

Itakuwaje iwapo shirika lisilo la faida linalolengwa kupokea mchango wangu litaacha kutimiza masharti?

Iwapo Network for Good, mshirika wa ufadhili wa Google, haiwezi kusambaza pesa za mradi kwa shirika lisilo la faida linalolengwa kwa sababu yoyote (ikiwemo kuwa shirika lisilo la faida si shirika halali la Marekani kwa mujibu wa 501(c)(3)), Google itashirikiana na Network for Good kuchagua shirika lingine lisilo la faida ambalo linastahiki.
Nitaonaje michango katika gumzo langu la moja kwa moja?
Utaona michango katika dirisha la gumzo. Unaweza pia kufuatilia michango ya gumzo la moja kwa moja katika Ukurasa wa Kudhibiti Utiririshaji wa Moja kwa Moja wenye Wijeti ya Shughuli za Mtazamaji.

Upau wa shughuli na jumla ya pesa huwakilisha nini?

Jumla ya pesa huwakilisha pesa zilizotolewa katika mchango huo kwa jumla, kutoka kwenye vituo na video zinazoshiriki katika mchango huo. Unaweza kupata jumla ya pesa au upau wa shughuli chini ya Kitufe cha kuchanga.

Ninaweza kupata wapi takwimu kuhusu mchango wangu?

Ili upate takwimu kuhusu mchango wako:

  1. Ingia katika akaunti ya YouTube kwenye kompyuta.
  2. Nenda kwenye Studio ya YouTube.
  3. nenda kwenye Chuma mapato.
  4. Chagua Uhisani kwenye YouTube.
  5. Chini ya "Jumla ya Pesa Zilizotolewa" utaona data ya msingi ya mchango karibu na kampeni ambayo umeanzisha au kujiunga nayo.
  6. Fanya kiteuzi kielee juu ya kiasi kilichotolewa ukitumia kipanya chako ili uone maelezo zaidi kuhusu mchango wako.

Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu Mashirika yasiyo ya Faida

Ni Mashirika gani Yasiyo ya Faida yanatimiza masharti ya kupokea michango kutoka Uhisani wa YouTube?
Ili kutimiza masharti ya kupokea pesa kutoka kwenye Mchango wa Uhisani wa YouTube, shirika lisilo la faida linapaswa:
Kumbuka: Kwa sasa taasisi zisizo za faida zenye chanzo kimoja cha ufadhili haziruhusiwi. 

Itakuwaje iwapo sioni shirika lisilo la faida ambalo ningependa kuchagua kwenye zana ya kutuma ombi?

Hizi ni baadhi ya sababu zinazoweza kufanya shirika lisilo la faida ambalo unatafuta likose kuonekana kwenye zana ya kutuma ombi:
  • Shirika lisilo la faida halijajumuishwa kwenye mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida. Shirika lisilo la faida linaweza kutuma ombi la kufungua akaunti ya Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida.
  • Shirika lisilo la faida halijasajiliwa na Guidestar kwa mujibu wa sheria ya Marekani ya 501(c)(3). Angalia kwenye guidestar.org ili uthibitishe kama shirika lisilo la faida linapatikana hapo.
  • Shirika lisilo la faida limejiondoa kwenye michango mtandaoni. Ni lazima Mashirika Yasiyo ya Faida yaruhusu wafadhili wayachangie mtandaoni. Pata maelezo zaidi kuhusu kuchangisha pesa za shirika lisilo la faida kwenye YouTube.

Nilituma ombi kwa shirika lisilo la faida ambalo ningependa kulisaidia. Itachukua muda gani kulijumuisha?

Baada ya kutuma ombi la kujumuisha shirika lisilo la faida linalostahiki, tutakutumia barua pepe ili kukufahamisha kuhusu hali ya ombi lako. Baadhi ya maombi yanaweza kuchukua hadi siku 5 za kazi. Ili kusaidia kuharakisha mchakato huu, hakikisha kuwa shirika unalochagua linatimiza masharti ya kujiunga.

Pesa zinasambazwaje kwa Mashirika Yasiyo ya Faida?

Huwa tunashirikiana na Network for Good, shirika lililosajiliwa kwa mujibu wa sheria ya Marekani ya 501(c)(3) na shirika la ufadhili ili kukusanya na kusambaza pesa kwenye Mashirika Yasiyo ya Faida. Kwa kawaida, Network for Good hutuma pesa kila mwezi. Iwapo mchango hauzidi $10, pesa hizo hutumwa kila mwaka. Pata maelezo zaidi kuhusu usambazaji wa pesa kutoka Network for Good.

Ninaweza kupata vipi maelezo zaidi kuhusu Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida?

Pata maelezo zaidi kuhusu Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida na masharti ya kujiunga kwenye mpango huu. 

Ninaweza kupata vipi maelezo zaidi kuhusu kuchangisha pesa kama shirika lisilo la faida kwenye YouTube? 

Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu Wafadhili

Ninaona kitufe cha kuchanga kwenye ukurasa wa kutazama video. Utaratibu wake ni upi?

Ni nini maana ya Michango ya Gumzo la Moja kwa Moja?

Wakati mtayarishi anaongeza mchango kwenye mtiririko mubashara au onyesho la kwanza linaloruhusu gumzo la moja kwa moja, watazamaji wanaweza kuona kitufe cha kuchanga katika gumzo. Mtazamaji akichanga kupitia Michango ya Gumzo la Moja kwa Moja, anaweza kuchagua kuweka jina lake kwenye mchango wake katika gumzo la moja kwa moja. Pata maelezo zaidi kuhusu Michango ya Gumzo la Moja kwa Moja.
Ni nchi au maeneo gani ambayo yanaweza kutoa michango ya Uhisani wa YouTube?

Iwapo unaishi katika nchi au maeneo yafuatayo, unaweza kutoa michango.

  • Ajentina
  • Austria
  • Ubelgiji
  • Bolivia
  • Kanada
  • Kolombia
  • Korasia
  • Estonia
  • Ufaransa
  • Ujerumani
  • Ghana
  • Hong Kong
  • Aisilandi
  • Indonesia
  • Ayalandi
  • Israeli
  • Italia
  • Korea
  • Kuwaiti
  • Lativia
  • Litwania
  • Lasembagi
  • Malesia
  • Meksiko
  • Montenegro
  • Uholanzi
  • Nyuzilandi
  • Norwe
  • Peruu
  • Ufilipino
  • Polandi
  • Pwetoriko
  • Romania
  • Slovakia
  • Korea Kusini
  • Uhispania
  • Uswidi
  • Uswizi
  • Taiwani
  • Tailandi
  • Uturuki
  • Uingereza
  • Marekani

Je, ninaweza kuondoa mchango wangu kwenye pato linalotozwa kodi?

Angalia maelezo ya kodi za wafadhili kulingana na eneo hapa.

Ni kiasi gani cha mchango wangu kitatumwa kwa shirika lisilo la faida?

Pesa zote unazochanga zitatumwa kwa shirika lisilo la faida. YouTube hulipia pia ada za miamala ya kadi za mikopo.

Je, ninaweza kurejeshewa pesa za mchango wangu?

Huwezi kurudishiwa pesa unazochangia kwa hiari mashirika yasiyo ya faida. Iwapo unatatizika kulipa, unaweza kuwasiliana na timu yetu ya usaidizi.

Ni maelezo gani ambayo yanashirikiwa na mashirika yasiyo ya faida ninapotoa mchango?

Unapotoa mchango, maelezo yako ya mawasiliano hayashirikiwi na mtayarishi au shirika lisilo la faida. Iwapo utafanya mchango wako uwe wa "umma" wakati unautoa kwenye gumzo la moja kwa moja, mtayarishi ambaye ni mwenyeji wa mtiririko mubashara anaweza kuona jina la akaunti yako na pesa ulizochanga. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi maelezo yako hutumika.
Ni nini maana ya michango ya nje ya YouTube, ya kampuni na ya mtumiaji?
  • Michango ya watumiaji: Pesa zinazotolewa na watumiaji wa YouTube.
  • Michango ya kampuni: Pesa zinazotolewa na YouTube au kampuni nyingine, jinsi inavyothibitishwa na shirika lisilo la faida.
  • Michango inayotolewa nje ya YouTube: Pesa zinazokusanywa na mwandalizi na kuthibitishwa na shirika lisilo la faida kwenye tovuti isiyo YouTube kama sehemu ya kampeni hii.
Utaratibu wa kulinganisha kampuni ni upi?
Iwapo kampuni imeahidi kulinganisha michango, itachanga $1 kwa kila $1 inayotolewa kama mchango kupitia kitufe cha kuchanga cha YouTube. Ulinganifu huu utaendelea hadi ulinganishaji ukamilike au hadi mwisho wa kampeni, lolote litakalotangulia.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
1814530662645747765
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false