Kuunda na kudhibiti shughuli za bidhaa zilizowekewa lebo

Ununuzi kwenye YouTube hukuruhusu uanzishe hali ya ununuzi inayokufaa wewe na watazamaji wako. Kwa kuweka lebo kwenye bidhaa, unaweza kutangaza bidhaa zako katika chaneli yako ya YouTube au ikiwa uko kwenye mpango wa Washirika, bidhaa za chapa nyingine pia. Ili kusaidia kuongeza hamasa kwa bidhaa zilizowekewa lebo, kuwapa watazamaji ofa na taarifa mpya kuhusu bidhaa, unaweza kutumia shughuli hizi:

Ofa na Punguzo za bei

Kipengele cha ofa na punguzo za bei huwaonyesha watazamaji ofa zilizo kwenye bidhaa ulizowekea lebo. Kuna aina tatu za ofa na punguzo za bei zinazoweza kuonyeshwa kwenye orodha ya bidhaa au bango la bidhaa lililobandikwa.

  1. Ofa ya Muuzaji: Ofa ambayo inajumuisha, lakini si tu:
    1. Asilimia fulani inayotolewa kwenye bei ya bidhaa kiotomatiki au kupitia msimbo wa punguzo
    2. Kiasi cha pesa halisi au cha viwango kinachotolewa kwenye bei ya bidhaa kiotomatiki au kupitia msimbo wa punguzo
    3. Ofa isiyo ya kiasi maalum, kama vile “Zawadi ya ununuzi” au “Nunua X Upate Y”
  2. Kidokezo cha bei ya mauzo: Bei ya bidhaa iliyopunguzwa.
  3. Punguzo la bei: Beji inayoonyeshwa wakati bei ya sasa ya bidhaa imeshuka chini ya bei ya marejeleo. Bei ya marejeleo ni bei ya chini kabisa iliyoorodheshwa katika kipindi cha siku 30 zilizopita.

Watayarishi wanaweza kuweka beji ya “Punguzo la bei” kwa kubadilisha bei ya bidhaa husika kwenye maduka yao. Watayarishi wanaweza kuunda na kuweka Ofa za Wauzaji na Vidokezo vya bei za mauzo kwa kutumia:

  1. Shopify, au
  2. Google Merchant Center (GMC) - Ikiwa tu una idhini ya kufikia ya moja kwa moja.

YouTube itawaonyesha watazamaji ofa kulingana na data ya wauzaji wa rejareja. Ikiwa bidhaa iliyowekewa lebo ina zaidi ya ofa moja, YouTube itaonyesha ofa kubwa zaidi inayopatikana. Bidhaa zilizowekewa lebo huonekana tu kwa watazamaji wanaotumia kifaa cha mkononi katika nchi au maeneo haya. Ikiwa bidhaa ulizowekea lebo hazionyeshwi kwa watazamaji wako, hakikisha kwamba wanatumia kifaa cha mkononi na wako katika nchi au eneo lililojumuishwa. Bidhaa zilizowekewa lebo zitaonekana tu iwapo zinaweza kusafirishwa kwenda nchi au eneo la mtazamaji.

Kutimiza masharti

Ili uweze kutumia kipengele cha ofa na punguzo za bei, muuzaji wako wa rejareja anatakiwa kutimiza masharti mengine ya kujiunga kulingana na aina ya ofa. Ijapokuwa hakuna masharti mengine yoyote kwa wauzaji wa rejareja yanayohusu Vidokezo vya bei za mauzo na Punguzo za bei, kuna masharti zaidi kwa wauzaji wa rejareja kuhusiana na Ofa za Wauzaji:

  • Ofa za Wauzaji (kutoka Shopify):
    • Kwa ofa zinazowekwa kiotomatiki (punguzo za kiotomatiki): Ni sharti duka lako la Shopify liwe katika mojawapo ya nchi au maeneo yafuatayo: Australia, Brazili, Kanada, Denmaki, Uhispania, Ufaransa, India, Italia, Japani, Korea, Uholanzi, Uingereza na Marekani.
    • Kwa ofa zinazowekwa kwa kutumia misimbo ya punguzo: Ni sharti duka lako la Shopify liwe Marekani.
    • Kwa ofa zisizo za kiasi maalum: Ofa za aina hii hazitumiki kwa sasa.
  • Ofa za Wauzaji (kutoka GMC): Ni sharti muuzaji wako wa rejareja anayetumika awe katika mojawapo ya nchi au maeneo yafuatayo: Australia, Brazili, Kanada, Denmaki, Uhispania, Ufaransa, India, Italia, Japani, Uholanzi, Korea, Uingereza na Marekani.

Kuweka mipangilio na kudhibiti ofa na punguzo za bei

Kuna njia tofauti za kuweka mipangilio ya ofa kulingana na ofa unayotoa. Baada ya ofa kukaguliwa na kuidhinishwa, unaweza kuiwekea bidhaa lebo.

Kumbuka: Ukiwekea bidhaa lebo, huwezi kuona ofa husika unapochagua bidhaa. Lakini, ofa hiyo itaonekana baada ya kuwekewa lebo.

 Tunapendekeza uweke mipangilio ya ofa zozote angalau siku 5 kabla ya kuzishiriki kwenye YouTube.

Ofa za Wauzaji

Kuweka au kubadilisha ofa ya muuzaji kupitia Shopify

Unaweza kuweka Ofa za Wauzaji kupitia Shopify, kwa kutumia punguzo la kiotomatiki la kiwango maalum au msimbo wa punguzo. Mtazamaji anaponunua bidhaa zinazotimiza masharti, punguzo za kiotomatiki za kiwango maalum hutumiwa kiotomatiki wakati wa kulipa. Unapobuni na kushiriki msimbo wa punguzo, ni sharti watazamaji waweke msimbo huo wakati wa kulipa ili wapate punguzo kwenye bidhaa zinazotimiza masharti.
Kumbuka: Ofa zisizo za kiasi maalum na ofa za kusafirishiwa kwa $0 haziwezi kutumika kwa sasa. Pata maelezo zaidi kuhusu aina za ofa zinazoweza kutumika kwenye Shopify.

Kuweka Ofa ya Muuzaji katika Shopify:

  1. Nenda kwenye Punguzo kisha Weka punguzo.
  2. Katika sehemu ya “Chagua aina ya punguzo”, chagua: “Kiwango cha punguzo kwenye bidhaa,” AU “Kiwango cha punguzo kwenye oda.”
  3. Kwenye sehemu ya “MBINU,” chagua aina ya punguzo unalotaka kutoa:
    1. Punguzo la kiotomatiki: Watazamaji huwekewa punguzo kiotomatiki wakati wa kulipa.
    2. Msimbo wa punguzo: Ni sharti watazamaji waweke msimbo wakati wa kulipa ili wapate punguzo.
  4. Weka maelezo ya ofa yako  kisha Hifadhi punguzo.
  5. Kusawazisha punguzo lako kwenye programu ya Kituo cha Google:
    1. Kwenye sehemu ya Punguzo, bofya punguzo husika.
    2. Katika sehemu ya Vituo vya mauzo , chagua programu ya Kituo cha Google.
    3. Bofya Hifadhi.

 Kuweka au kubadilisha ofa ya muuzaji katika Google Merchant Center (GMC)

Ili kuweka ofa ya muuzaji katika GMC:

  1. Weka na uwasilishe ofa yako ukitumia mojawapo ya mbinu zilizopo kwenye bidhaa husika:
    1. Zana ya kutayarisha ofa za Merchant Center
    2. Mipasho ya ofa
    3. Content API

Ofa za wauzaji hukaguliwa na kuthibitishwa kwa mujibu wa Masharti ya kanuni za uhariri na Sera za ofa za Google Merchant Center. Zikiidhinishwa, huchapishwa kwenye mifumo mbalimbali ya Google na YouTube.

Kidokezo cha Bei ya Mauzo

Ukiweka bei yako ya mauzo hakikisha inatimiza masharti mengine yote.

Kuweka au kubadilisha bei ya mauzo kupitia Shopify

Kuweka bei ya mauzo kupitia Shopify:

  1. Nenda kwenye Bidhaa  kisha Bofya bidhaa husika.
  2. Chini ya sehemu ya Bei, weka Bei ya kulinganishia iwe bei halisi ya bidhaa yako.
  3. Weka Bei ya bidhaa yako iwe bei mpya ya mauzo.

Kuweka au kubadilisha bei ya mauzo katika GMC

Ili kuweka bei ya mauzo katika GMC:

  1. Hakikisha kuwa bei halisi ya bidhaa yako imeorodheshwa kwenye sifa ya bei [bei].
  2. Wasilisha bei ya mauzo kwa kutumia sifa ya bei ya mauzo [bei ya mauzo] isiyo ya lazima.

Punguzo la Bei

Beji ya “punguzo la bei” itaonyeshwa wakati bei thabiti iliyokuwepo ya bidhaa inashuka kwa kiwango kikubwa. Unaweza kubadilisha bei ya bidhaa yako ili Google ionyeshe beji ya “Punguzo la bei”. Ili beji ya “punguzo la bei” ionyeshwe, badilisha bei ya bidhaa yako kwenye duka lako. Bei mpya inapaswa kuwa chini ya bei ya wastani uliyoorodhesha hapo awali. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi vidokezo vya punguzo za bei vinavyofanya kazi.

Uzinduzi wa bidhaa

Ukiwa na kipengele cha uzinduzi wa bidhaa, unaweza kuongeza hamasa na kudumisha hali ya kusisimua unapozindua bidhaa mpya wakati wa mtiririko mubashara. Picha ya kishikilia nafasi iliyo na mfuko wa ununuzi huonyeshwa kwenye orodha ya bidhaa ya mtiririko wako mubashara, kwa hiyo watazamaji wanaweza kujua kwamba unazindua bidhaa yako hivi karibuni. Baada ya bidhaa kuonyeshwa kwenye mtiririko wako mubashara, watazamaji wanaweza kuinunua papo hapo.

Unaweza kuweka mipangilio ya uzinduzi wa bidhaa pamoja na au bila tarehe za kuchapishwa, kulingana na mahitaji na ustahiki wako.

  • Uzinduzi wa bidhaa wenye tarehe za kuchapishwa: Una masharti madhubuti ya kuzuia uvujaji na unahitaji kuwekwa kwa mipangilio mapema zaidi. Watayarishi wenye uwezo wa kufikia moja kwa moja duka lao la Shopify au huduma ya Google Merchant Center (GMC) ya duka lao lililounganishwa wanaweza kutumia tarehe za kuchapishwa.
  • Uzinduzi wa bidhaa bila tarehe za kuchapishwa:  Huwekwa unapowekea lebo bidhaa kwenye mtiririko wako mubashara. Uzinduzi huu hauzuii bidhaa yako kuonyeshwa kwenye YouTube mapema, lakini watazamaji wanaweza kupata bidhaa yako kwingineko. Ili kusaidia kuzuia uvujaji, unaweza kuacha kuorodhesha ukurasa wa bidhaa yako hadi uzinduzi ufanywe. Watayarishi walio kwenye mpango wa washirika au watayarishi walio na maduka yaliyounganishwa wanaweza kutumia kipengele hiki.

Baada ya kuandaa uzinduzi wa bidhaa yako, unaweza kuratibu mtiririko wako mubashara, kuweka uzinduzi wa bidhaa yako kwenye mtiririko na uizindue.

Kuandaa uzinduzi wa bidhaa bila tarehe za kuchapishwa

Ili uandae uzinduzi wa bidhaa yako bila tarehe za kuchapishwa, lazima:

Hakikisha umeweka bidhaa kwenye duka lako ili iweze kukaguliwa ili kubaini ikiwa inatii sera zetu na sera za Google Merchant Center. Mchakato huu kwa kawaida huchukua siku chache za kazi. Baada ya kuidhinishwa, bidhaa zako zitaonekana kwenye Studio ya YouTube ili uziweke kwenye mtiririko wako mubashara.

Kuandaa uzinduzi wa bidhaa na tarehe za kuchapishwa

Ili uandae uzinduzi wa bidhaa yako na tarehe za kuchapishwa, unahitaji uwezo wa kufikia moja kwa moja:

  • Google Merchant Center (GMC) ya duka lako lililounganishwa au
  • Ukurasa wa msimamizi wa duka lako la Shopify

Kama mbinu bora, andaa uzinduzi wa bidhaa yako angalau wiki 1 kabla ya mtiririko wako mubashara. Baada ya kuandaa uzinduzi wa bidhaa yako, unaweza kuratibu mtiririko wako mubashara na uweke bidhaa yako kwenye mtiririko mubashara ili uizindue.

Kuandaa uzinduzi wa bidhaa na tarehe za kuchapishwa kupitia Shopify

Ikiwa umeunganisha duka lako la Shopify kwenye YouTube, andaa uzinduzi wa bidhaa yako kwenye Shopify:

  1. Pakia ofa ya uzinduzi wa bidhaa kwenye Shopify.
  2. Ratibu tarehe na muda sawa kwa programu ya Kituo cha Google na Duka la Mtandaoni la Shopify:
    • Duka la mtandaoni: Katika sehemu ya Bidhaa, ratibu tarehe na muda wa upatikanaji katika duka lako la Mtandaoni. Tarehe na muda huu ni wakati ambapo bidhaa yako itaonekana na kuweza kununuliwa kwenye Shopify.

    • Programu ya Kituo cha Google: Chini ya sehemu ya Kituo na programu za mauzo ratibu tarehe na muda kwenye Google. Tarehe na muda huu ni wakati ambapo bidhaa yako itaonekana na kuweza kununuliwa kwa watazamaji wa YouTube.

    • Hakikisha kuwa tarehe na muda wa uzinduzi wa bidhaa (ikiwa ni pamoja na saa za eneo za UTC) zinalingana katika Programu ya Kituo cha Google na Duka la Mtandaoni la Shopify.
  3. Bidhaa yako itakaguliwa kuhakikisha inatii sera zetu na sera za Google Merchant Center. Mchakato huu kwa kawaida huchukua siku chache za kazi. Baada ya kuidhinishwa, bidhaa yako itaonekana kwenye Studio ya YouTube.

Kuandaa uzinduzi wa bidhaa na tarehe za kuchapishwa kupitia Google Merchant Center

Ikiwa una uwezo wa kufikia moja kwa moja huduma ya Google Merchant Center (GMC) ya duka lako lililounganishwa, unaweza kuandaa uzinduzi wa bidhaa yako na tarehe za kuchapishwa:

  1. Tumia mipasho ya msingi au ya ziada ili kuwasilisha data ya bidhaa inayozinduliwa, ukitumia sifa ya "disclosure_date".
  2. Hakikisha kuwa maelezo ya tarehe na muda wa uzinduzi wa bidhaa (ikiwa ni pamoja na saa za eneo za UTC) vimewekwa kwa usahihi.
  3. Bidhaa yako itakaguliwa kuhakikisha inatii sera zetu na sera za Google Merchant Center. Mchakato huu kwa kawaida huchukua siku chache za kazi. Baada ya kuidhinishwa, bidhaa zako zitaonekana kwenye Studio ya YouTube.

Kuweka uzinduzi wa bidhaa kwenye mtiririko wako mubashara

Baada ya kuandaa uzinduzi wa bidhaa, ratibu mtiririko wako mubashara na uweke lebo kwenye uzinduzi wa bidhaa kwenye mtiririko mubashara:

  1. Kwenye Studio ya YouTube, ratibu mtiririko wako mubashara.
  2. Katika Ukurasa wa kudhibiti utiririshaji wa moja kwa moja, weka lebo kwenye uzinduzi wa bidhaa na bidhaa zozote husika kwenye video inayotiririshwa mubashara. 
  • Ikiwa ulitumia tarehe za kuchapishwa: Uzinduzi wa bidhaa yako utakuwa na beji ya “Uzinduzi wa bidhaa” karibu nayo na tarehe itakayopatikana. Hakikisha kuwa maelezo ya tarehe na muda wa uzinduzi wa bidhaa (ikiwa ni pamoja na saa za eneo za UTC) vimewekwa kwa usahihi. 
    • Kumbuka: Maelezo ya tarehe na muda wa uzinduzi wa bidhaa yanapaswa kuwa sawa na maelezo yaliyo kwenye Ukurasa wa kudhibiti utiririshaji wa moja kwa moja, GMC au Shopify na kwenye ukurasa wa kutua wa uzinduzi wa bidhaa yako. Ni lazima ukurusa wa kutua upatikane (umeorodheshwa na unaweza kutafutwa) kufikia wakati wa kuzindua bidhaa. Vinginevyo, watazamaji watapata ujumbe kuhusu hitilafu.
  • Ikiwa hukutumia tarehe za kuchapishwa: Bofya “Andaa uzinduzi wa bidhaa”  karibu na bidhaa. Bidhaa yako itafichwa hadi utakapokuwa tayari kuizindua.
  1. Ukitaka uzinduzi wa bidhaa yako uonekane kama kipengee cha kwanza katika rafu yako ya bidhaa inapozinduliwa, panga upya bidhaa zako.
  2. Bofya HIFADHI
Vidokezo vya Kuweka Lebo: Ikiwa bidhaa yako ina vibadala (kwa mfano, bidhaa inapatikana katika ukubwa au ukurasa tofauti), kila kibadala kinaweza kuwekewa lebo kivyake. 
  • Ikiwa bidhaa yako haina vibadala vingi, unaweza kuwekea lebo vibadala vyote. 
  • Ikiwa bidhaa yako ina vibadala vingi, unaweza kuwekea lebo vibadala vya bei tofauti. 
  • Sasisha jina la kila bidhaa iliyowekewa lebo ili tofauti kati ya vibadala iwe wazi. 

Watazamaji wanapochagua kibadala wanachokipenda, watapelekwa kwenye tovuti yako kwa kutumia maelezo ya kibadala yaliyochaguliwa mapema. Wakitaka, wanaweza kuchagua kibadala tofauti kwenye tovuti yako.

Unaweza kubandika bidhaa yako kwenye mtiririko wako mubashara kabla ya kuzinduliwa ili kuiangazia kwa udhahiri zaidi. Kabla ya tarehe ya kuzinduliwa, bango la "Inazinduliwa hivi karibuni" litaibukia. Saa moja kabla bidhaa yako kuzinduliwa, kipima muda kitaibukia karibu na bango. Baada ya bidhaa yako kuzinduliwa, kipima muda kitabadilika kiotomatiki kuwa ubandikaji wa kawaida wa bidhaa na bidhaa itaonekana kwenye Google na YouTube.

Kudhibiti uzinduzi wa bidhaa yako

Vidokezo vya kuzuia uvujaji wa uzinduzi wa bidhaa 

Kuwa mwangalifu kuhusu mahali ambapo ukurasa wa kutua wa bidhaa yako na URL za picha zimeunganishwa kabla ya uzinduzi wa bidhaa. Kwa usalama wa ziada, watayarishi wenye uwezo wa kufikia moja kwa moja duka lao la Shopify au Google Merchant Center (GMC) ya duka lao lililounganishwa wanaweza:

  1. Kusubiri hadi wakati wa mtiririko mubashara ili kuchapisha ukurasa wa bidhaa yako 
  2. Kuwasilisha uzinduzi wa bidhaa yako wakitumia tarehe za kuchapishwa angalau wiki 1 mapema

Kubadilisha muda wa uzinduzi wa bidhaa yako

Unaweza kusasisha muda ulioratibiwa wa kuzindua bidhaa kwa jinsi sawa na ulivyouratibu. Inachukua takribani saa 1 kwa muda mpya ulioratibiwa kuanza kutumika. Ili uangalie muda uliosasishwa, ni lazima upakie upya Studio ya YouTube. Pia, unapaswa kuweka upya lebo kwenye bidhaa ikiwa na wakati uliosasishwa unaoutaka.

Ikiwa mtiririko wako mubashara unachelewa na hutaki uzinduzi wa bidhaa uonekane mapema, uondoe katika orodha ya bidhaa. Unapokuwa tayari kuizindua kwenye mtiririko wako mubashara, unaweza kuiwekea lebo tena katika Ukurasa wa kudhibiti utiririshaji wa moja kwa moja ili uonekane.

Kumbuka: Ukiondoa uzinduzi wa bidhaa kwenye mtiririko wako mubashara, hautaonekana kwenye rafu ya bidhaa ya mtiririko wako mubashara. Lakini, bado utaonekana kwenye mifumo mingine ya YouTube kwa muda ulioratibiwa.

Kuzindua bidhaa yako mpya wakati wa mtiririko wako mubashara

Katika kichupo cha Ununuzi cha Ukurasa wa kudhibiti utiririshaji wa moja kwa moja, unaweza kuamua ikiwa unataka kuweka kipima muda au kuzindua bidhaa yako moja kwa moja: 

  1. Karibu na uzinduzi wa bidhaa yako, chagua kipima muda . Ikiwa ulitumia tarehe za kuchapishwa kwa uzinduzi wa bidhaa yako, unaweza kuchagua kipima muda baada ya muda na tarehe ya kuchapishwa kupita.
  2. Chagua iwapo unataka kuweka kipima muda cha dakika 1:00 au Uzinduzi wa papo hapo. 
  3. Bofya WEKA
  4. Ikiwa umechagua kipima muda, bofya ANZA ukiwa tayari kuanzisha kipima muda. Huwezi kubadilisha au kusitisha kipima muda baada ya kubofya anza, kwa hivyo hakikisha uko tayari kuzindua bidhaa.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
7860776462468686684
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false