Matatizo ya kulipa, kuripoti na kutamatisha maagizo

Unaweza kupata majibu ya maswali mengi kuhusu kulipa, kuripoti na kughairi maagizo katika Kituo cha Usaidizi wa Dashibodi ya Google Play, timu yetu ya usaidizi inaweza kutatua yaliyosalia.

Kunja Zote Panua Zote

Angalia ripoti za fedha na takwimu za programu

Kwenye Dashibodi ya Google Play, unaweza kupata maelezo ya kina kuhusu ripoti za fedha na takwimu. Maelezo hayo yanaweza kukusaidia kufahamu mengi kuhusu utendaji wa programu yako.

Unaweza kupata maelezo kuhusu jinsi ya kufikia ripoti hizi kwenye kurasa zifuatazo:

Maagizo yanaghairiwa

Katika hali fulani, mtumiaji anaweza kughairi maagizo au pesa zake zirejeshwe na Google. Pesa hurejeshwa kwa heshima ya watumiaji wako kama inavyotakiwa na sheria na hujumuishwa kwenye Mkataba wetu wa Usambazaji kwa Wasanidi Programu. Baada ya kughairi agizo, huwezi kulirejesha tena.

Yafuatayo ni baadhi ya matukio ambapo pesa zinaweza kurejeshwa:

  • Mtumiaji anarejesha programu inayolipishwa: Baada ya kununua programu, mtumiaji ana hadi saa 2 za kuirejesha ili arejeshewe pesa zote. Mtumiaji anaweza kurejesha programu mara moja pekee. Kama mtumiaji atanunua programu hiyo tena, hataweza kuirejesha mara ya pili.
  • Mtumiaji anaomba arejeshewe pesa: Watumiaji wanaweza kuomba warejeshewe pesa kwenye Google Play.
  • Ununuzi usiokusudiwa au ambao haujaidhinishwa: Katika hali zingine, timu yetu ya usaidizi inaweza kurejesha pesa za ununuzi uliofanywa kwa makosa au bila idhini ya mnunuzi.

Pia, iwapo Google itabaini kuwa agizo lina hatari kubwa au halifuati sera zetu. linaweza kughairiwa kwa usalama wako. Ili upate maelezo zaidi kuhusu jinsi Google inavyotambua na kusaidia kuzuia ulaghai, tembelea sehemu ya Ulinzi wa wauzaji dhidi ya ulaghai.

Ununuzi wa ndani ya programu ambao haujakamilika

Iwapo watumiaji wanatatizika kufanya ununuzi wa ndani ya programu, wanaweza kuwasiliana nawe ili wapate usaidizi. Iwapo huwezi kuwasaidia mwenyewe, unaweza kupata hatua zingine za utatuzi wa ununuzi wa ndani ya programu na matatizo ya malipo kwenye Kituo cha Usaidizi wa Google Play.

Iwapo watumiaji bado hawawezi kukamilisha ununuzi wa ndani ya programu, unaweza kuwasiliana na timu yetu ya usaidizi. Ili utusaidie tusuluhishe tatizo hili, hakikisha kuwa unajumuisha maelezo yafuatayo:

  • Picha ya skrini ya tatizo
  • Sampuli ya vitambulisho vya agizo lililo na tatizo
  • SKU zilizoathiriwa
  • Ni ombi lipi la API ya kutozwa kupitia Google ambalo halifanyi kazi?
  • Unaona misimbo gani ya hitilafu?
  • Ufafanuzi kuhusu jinsi unavyotumia huduma ya kutozwa kupitia Google: Je, unatumia uthibitishaji unaotegemea seva? Ni aina gani ya kipengee?
  • Ripoti ya hitilafu iliyozalishwa kwa kutumia Zana ya Android Debug Bridge
Badilisha sarafu katika akaunti ya Dashibodi ya Google Play

Iwapo ungependa kubadilisha akaunti yako ya Dashibodi ya Google Play ili utumie sarafu tofauti, utahitaji kufungua akaunti mpya ya Dashibodi ya Google Play ukitumia anwani tofauti ya barua pepe. Iwapo unahitaji kufungua Akaunti mpya ya Google, unaweza kuifungua wakati wowote.

Wakati wa kufungua akaunti yako mpya ya Dashibodi ya Google Play, unaweza kuchagua nchi tofauti ili ubadilishe sarafu ambayo akaunti yako inatumia. Baada ya kufungua akaunti mpya, timu yetu ya usaidizi inaweza kuhamishia programu zako kwenye akaunti yako mpya, na ikurudishie ada ya usajili wako wa awali.

Siwezi kuona au kurejesha pesa za maagizo mahususi

Ikiwa unamiliki akaunti, unaweza kufikia vipengele vya muuzaji katika Dashibodi yako ya Google Play.

Ili uwaruhusu watumiaji wengine kufikia vipengele hivi, wamiliki wa akaunti wanahitaji kuwapa watumiaji ruhusa za "Kuangalia data ya fedha" na "Kudhibiti maagizo."

Ikiwa una ruhusa zinazotakikana, unaweza kupata maagizo kwenye Dashibodi ya Google Play ili ukague maelezo ya maagizo au urejeshe pesa. Ukiona ujumbe kuwa umezuiwa kurejesha pesa au kughairi usajili, inamaanisha kuwa umefikia kima kinachoruhusiwa katika akaunti yako.

Sasisha mahali ambapo malipo yako yanatumwa

Ikiwa una programu inayolipishwa au unatoa huduma ya ununuzi wa ndani ya programu, unaweza kusasisha maelezo ya akaunti ya benki ambapo malipo yako yanatumwa. Ili urekebishe akaunti yako kwenye kituo cha malipo ya Google, tumia maagizo yafuatayo:

  1. Weka akaunti mpya ya benki.
  2. Thibitisha akaunti yako.
  3. Weka akaunti mpya iwe akaunti yako ya msingi ya malipo.

Kumbuka: Ikiwa una akaunti moja pekee ya benki iliyothibitishwa kwenye maelezo ya akaunti yako ya malipo, unaweza kuiondoa tu baada ya kuweka akaunti nyingine ya benki.

Omba ankara za kodi ya ongezeko la thamani (VAT)

Ikiwa kwa kawaida unatozwa kodi ya ongezeko la thamani unaponunua bidhaa kwenye Google Play, unaweza kuomba ankara ya VAT katika kituo cha malipo ya Google.

Pata stakabadhi yako ya usajili kwenye Dashibodi ya Google Play

Baada ya kujisajili kwenye akaunti ya Dashibodi ya Google Play, utapokea stakabadhi ya malipo katika barua pepe yako.

Ili upate stakabadhi ya malipo, ingia kwenye Akaunti ya Gmail uliyotumia kujisajili kwenye akaunti ya Dashibodi ya Google Play kisha utafute “Ada ya Usajili ya Msanidi Programu.”

Kumbuka: Iwapo huwezi kupata stakabadhi yako ya malipo na unahitaji kitambulisho cha muamala ili uhamishe programu, kagua miamala yako kwenye Kituo cha malipo ya Google.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
7299423668019786827
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false