Kwanini uingie kwenye YouTube?

Ili kukusaidia ufurahie manufaa ya kuingia katika akaunti, tunafanyia majaribio njia za kuwakumbusha watu waingie katika akaunti. Kipengele hiki kina kidokezo cha kuingia katika akaunti kinachoonekana unapotumia YouTube. Ukiona kidokezo hiki na hutaki kuingia katika akaunti kwa wakati huu, unaweza kukiondoa.

Kuingia katika akaunti ya YouTube ukitumia Akaunti yako ya Google kunaweza kukusaidia kupata maudhui unayopenda, kuwasiliana na jumuiya ya YouTube, na zaidi. Haya ndiyo manufaa unayopata unapoingia katika akaunti:

Ona zaidi kutoka kwenye vituo unavyopenda kwa kufuatilia

Unaweza kufuatilia vituo na uchague kutumiwa arifa video mpya zinapopakiwa. Kwa chaguomsingi, tutakutumia mihtasari pekee kutoka kwenye kituo hicho.

Kubuni na kushiriki orodha za kucheza

Pata na utazame video unazopenda kwa kubuni orodha ya kucheza. Unaweza hata kuishiriki na marafiki na uwaalike washirikiane kwenye orodha hiyo ya kucheza.

Kuchangia kwenye jumuiya

Unaweza kutazama vituo na wasanii unaowapenda. Maoni yako kuhusu video na machapisho yatawafahamisha unachofikiri kuhusu video yao, kuuliza maswali, na kuwasiliana na mashabiki wengine.


Unaweza pia kusaidia kuboresha YouTube kwa ajili ya kila mtu kwa kutumia zana zetu za jumuiya kama vile ripoti na zuia.

Njia zisizo za lazima za kupata hata manufaa zaidi kutoka YouTube

Unaweza kupata manufaa zaidi kutoka YouTube ukitumia huduma hizi zinazolipiwa zisizo za lazima:

Kutazama kwa faragha ukitumia hali fiche

Ikiwa hutaki YouTube ihifadhi kumbukumbu ya shughuli zako, unaweza kutumia hali fiche. Kwa mfano, ukitazama video katika hali fiche, haitabadilisha video unazopendekezewa katika akaunti yako.


Kwenye kifaa cha mkononi, unaweza kupata hali fiche katika menyu ya akaunti. Au unaweza kutumia hali ya faragha ya kivinjari unachopenda. Pata maelezo zaidi kuhusuhali fiche.

Kudhibiti faragha yako

YouTube imejitolea kulinda faragha yako. Ukiwa umeingia katika akaunti, unaweza kufikia data yako kwenye YouTube ili uone ni data ipi inayohifadhiwa katika akaunti yako. Unaweza pia kunufaika na maelezo ya kina ya seti ya mipangilio ya faragha.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
11064808532468720914
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false