Pata maelezo kuhusu Machapisho ya jumuiya

YouTube Community Posts

Watayarishi walio na idhini ya kufikia Machapisho ya jumuiya wanaweza kuwasiliana na watazamaji wakitumia media wasilianifu. Machapisho ya jumuiya yanaweza kujumuisha kura, mijarabu, GIF, maandishi, picha na video. Machapisho ya jumuiya yanaweza kukuwezesha kuwasiliana na hadhira yako nje ya video unazopakia. Yanaonyeshwa kwenye Kichupo cha jumuiya na yanaweza kuonekana kwenye Ukurasa wa kwanza au Mpasho wa chaneli unazofuatilia.

Je, ninatimiza masharti ya Kichupo cha jumuiya?

Ili Kichupo cha jumuiya kipatikane, ni lazima uruhusu ufikiaji wa vipengele vya kina kwenye kituo chako. Unaweza kuchagua kati ya chaguo tatu ili upate idhini ya kufikia: historia ya chaneli, uthibitishaji kwa video au kitambulisho sahihi. Pata maelezo zaidi hapa. Inaweza kuchukua hadi saa 48 kabla ya Kichupo cha jumuiya kupatikana baada ya kuwasha kipengele cha ufikiaji wa vipengele vya Kina.

Uwezo wa kufikia machapisho ya jumuiya unaweza kubadilika kulingana na jukumu la kituo chako. Pata maelezo zaidi kuhusu ruhusa za kituo.

Ikiwa hadhira ya kituo chako imewekwa kuwa "Inayolenga Watoto," ni wewe pekee unayeweza kuona Kichupo cha jumuiya yako na si watazamaji wako. Pia, huwezi kutunga machapisho mapya, lakini unaweza kuangalia machapisho ya hapo awali. Pata maelezo zaidi kuhusu kuweka mipangilio ya hadhira yako.

Kumbuka: Huenda kipengele hiki kisipatikane kwa matumizi yanayosimamiwa kwenye YouTube. Pata maelezo zaidi hapa.

Ninaweza kupata wapi Machapisho ya jumuiya yangu?

Unaweza kupata Machapisho ya jumuiya yako kwenye Kichupo cha jumuiya cha chaneli yako chini ya sehemu ya Maudhui ya Studio ya YouTube. Ili ufikie machapisho yako katika Studio ya YouTube:

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui.
  3. Bofya kichupo cha Machapisho.

Iwapo umeratibu Machapisho ya jumuiya kwa tarehe ya kuchapishwa ya siku zijazo, yatakuwa katika Studio ya YouTube na kwenye sehemu ya "Yaliyoratibiwa" ya Kichupo cha jumuiya. Unaweza pia kupata machapisho yako ambayo muda wake wa kuonekana umeisha kwa kwenda katika sehemu ya "Yaliyowekwa kwenye kumbukumbu" ya Kichupo cha jumuiya. Ni wewe pekee unayeweza kuona sehemu hii.

Kumbuka: Machapisho ya jumuiya yanayokiuka Mwongozo wetu wa Jumuiya hayaruhusiwi kwenye YouTube. Iwapo chapisho lako litabainika kuwa linakiuka sera zetu, linaweza kuondolewa na chaneli inaweza kuwekewa onyo.

Je, watazamaji wangu wanaarifiwa ninapochapisha?

Ikiwa watazamaji wamechagua kupokea arifa za vituo wanavyofuatilia, watapata arifa za Machapisho ya jumuiya mara kwa mara.

Watazamaji wanaweza kuchagua kutopokea arifa za chapisho kwa kuchagua "Hakuna" katika mipangilio ya kengele.

Huenda tukatuma arifa kuhusu chapisho mara kwa mara kwa watazamaji ambao hawafuatilii lakini ambao mara nyingi hutazama video kwenye kituo chako. Pata maelezo zaidi kuhusu mipangilio ya arifa za mtazamaji.

Pata vidokezo vya watayarishi vya Machapisho ya jumuiya.

Kwa nini maoni yamezimwa kwenye Chapisho langu la jumuiya?

Hakikisha kuwa mipangilio chaguomsingi ya maoni ya chaneli yako haijawekwa kuwa "Zima maoni" kwa kufuata maagizo haya. Unaweza pia kuwasha maoni kwenye chapisho mahususi katika Studio ya YouTube kwenye kompyuta yako.

Huenda YouTube ilizima maoni kwa sababu za kiusalama, kama vile kuwalinda watoto wadogo au kwa sababu ya masuala mengine ya kiusalama. Pata maelezo zaidi kuhusu sababu za maoni kuzimwa.

Machapisho ya jumuiya ambayo hutuma video huonyesha mipangilio ya maoni ya video hizo. Unaposhiriki video katika chapisho na maoni ya video yamezimwa, maoni pia yatazimwa kwenye chapisho lako. Maoni yanaweza kuzimwa kwenye video kwa sababu:

Ikiwa wewe ndiwe mmiliki wa video unayoshiriki, unaweza kuchagua kuwasha au kuzima maoni kwenye video mahususi katika Studio ya YouTube. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuchagua mipangilio yako ya maoni.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
9291800849998037515
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false