Kuanza kutumia Takwimu za YouTube

Unaweza kutumia takwimu ili uelewe vyema utendaji wa chaneli na wa video yako mahususi kupitia vipimo na ripoti muhimu kwenye Studio ya YouTube. Ili ufahamu zaidi, unaweza kutumia Hali ya Kina kuangalia ripoti ya takwimu za kina ambapo unaweza kupata data mahususi, kulinganisha utendaji na kuhamisha data. Pata maelezo zaidi kuhusu ripoti za takwimu za kina.

Kumbuka: Baadhi ya data, kama vile jiografia, vyanzo vya watazamaji au jinsia inaweza kudhibitiwa. Pata maelezo zaidi kuhusu data inayodhibitiwa katika Takwimu za YouTube.

Takwimu katika Studio ya YouTube

Fahamu mambo ya msingi

Kwenye makala haya:

Nenda kwenye Takwimu za YouTube

Kuangalia ripoti kwenye kiwango cha chaneli

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, bofya Takwimu .

Kuangalia ripoti kwenye kiwango cha video

  1. Ingia katika Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui .
  3. Elekeza kiteuzi kwenye video yako kisha uchague Takwimu .

Pata maelezo kuhusu vichupo kwenye Takwimu za YouTube

Kwenye Takwimu za YouTube, unaweza kupata vichupo mbalimbali vinavyokusaidia kuelewa data yako.

Kumbuka: Huenda baadhi ya ripoti zisipatikane kwenye vifaa vya mkononi.

Kichupo cha Muhtasari (kiwango cha chaneli au video)

Kichupo cha Muhtasari hukuonyesha muhtasari wa utendaji wa chaneli na video zako. Unaweza kupata data hii katika kiwango cha chaneli au video. Unaweza kuangalia ripoti kama vile za utendaji wa Kawaida na katika Muda halisi. Pata maelezo zaidi kuhusu kichupo cha Muhtasari.

Katika kiwango cha video, unaweza kupata maelezo kuhusu jinsi ya kupima matukio makuu ya muda wa kutazama.

Kichupo cha Maudhui (kiwango cha chaneli)

Kichupo cha Maudhui hukupatia muhtasari wa jinsi hadhira yako inavyopata pamoja na kutagusana na maudhui yako na maudhui yanayotazamwa na hadhira hiyo. Unaweza kupata data hii katika kiwango cha chaneli kisha uichuje kulingana na aina ya maudhui ili uangalie ripoti kama vile maonyesho na jinsi yalivyochangia muda wa kutazama na maudhui maarufu. Pata maelezo zaidi kuhusu ushirikishaji na ufikiaji wa maudhui yako.

Kumbuka: Maonyesho ya Chaneli yanagawanywa kulingana na watumiaji Wapya na Wanaorudi.

Kichupo cha Ufikiaji (kiwango cha video)

Kichupo cha Ufikiaji hukupatia muhtasari wa jinsi hadhira yako inavyogundua chaneli yako. Unaweza kupata vipimo vya Ufikiaji katika kiwango cha video. Kadi ya vipimo muhimu huonyesha maonyesho yako, asilimia ya mibofyo kwenye maonyesho, mara za kutazamwa na watazamaji wa kipekee. Pata maelezo zaidi kuhusu ufikiaji wa video yako kisha uangalie muda wa kutazama na maonyesho yako.

Ushirikishaji (kiwango cha video)

Kichupo cha Ushirikishaji hukupatia muhtasari wa muda ambao hadhira yako inatazama video zako. Unaweza kupata vipimo vya Ushirikishaji katika kiwango cha video. Kadi ya vipimo muhimu huonyesha muda wa kutazama na wastani wa kipindi cha kutazama maudhui yako. Pata maelezo kuhusu ushirikishaji wa hadhira yako na jinsi ya kupima matukio makuu ya muda wa kutazama.

Hadhira (kiwango cha chaneli au video)

Kichupo cha Hadhira hukupatia muhtasari wa aina ya watazamaji wa video zako. Kadi ya vipimo muhimu huonyesha wanaofuatilia pamoja na watazamaji wanaorudi, wapya na wa kipekee. Pata maelezo zaidi kuhusu hadhira yako na uelewe watazamaji wako wa kipekee.
Kumbuka: Unaweza kupata vipimo vya Hadhira katika kiwango cha chaneli au video.

Mapato (kiwango cha chaneli au video)

Iwapo umejiunga na Mpango wa Washirika wa YouTube, kichupo cha Mapato hukusaidia kufuatilia mapato yako kwenye YouTube. Unaweza kupata vipimo vya Mapato katika kiwango cha chaneli au video. Kadi ya vipimo muhimu huonyesha kadirio lako la mapato. Mapato ya mwisho huonekana kwenye Takwimu za YouTube baada ya malipo yako kuwekwa kwenye AdSense katika YouTube, kwa kawaida kati ya siku ya 7 na ya 12 ya mwezi unaofuata. Pata maelezo zaidi kuhusu Ratiba za malipo ya AdSense kwenye YouTube. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuangalia mapato yako.

Kumbuka:

  • Kuzuia kodi kunaweza kuathiri mapato yako ya mwisho, iwapo kuna uzuiaji wa kodi. Kiasi kilichozuiwa kinaonekana tu kwenye akaunti yako ya AdSense katika YouTube.
  • Unaweza pia kupata utendaji wa mapato yako katika kiwango cha video.
  • Kwenye kadi ya RPM katika kiwango cha video, mapato yako huenda yasilingane na jumla ya mapato yaliyokadiriwa. Hii ni kwa sababu baadhi ya vyanzo vya mapato havihusishwi na video mahususi. Kwa mfano, uanachama katika chaneli hauhusishwi na video mahususi.

Zinazovuma (kiwango cha chanel)

Kichupo cha Zinazovuma hukupatia muhtasari wa maudhui ambayo hadhira na watazamaji wako kwenye YouTube wanatafuta. Unaweza kupata maarifa yanayovuma katika kiwango cha chaneli. Maarifa kwenye kichupo cha Zinazovuma yanaweza kukusaidia kugundua upungufu wa maudhui kwenye video na Video Fupi pamoja na mawazo kuhusu video ambazo huenda watazamaji wangependa kutazama. Pata maelezo ya jinsi ya kutumia kichupo cha Zinazovuma.

Pata vidokezo vya Takwimu za YouTube kwa Watayarishi.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
11856992472908703140
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false