Kuanzia tarehe 1 Februari, 2027, tutaleta masasisho kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube (YPP). Ili uendelee kuchuma mapato kikamilifu kutokana na maudhui yako, kagua na ukubali masharti yaliyosasishwa kwenye Studio ya YouTube kufikia tarehe 31 Januari, 2027.
Mpango wa Washirika wa YouTube (YPP) huwapa watayarishi ufikiaji mkubwa zaidi wa nyenzo na vipengele vya uchumaji wa mapato vya YouTube na ufikiaji wa timu zetu za Usaidizi kwa Watayarishi. Pia, unaruhusu ugavi wa mapato unaotokana na matangazo yanayoonyeshwa kwenye maudhui yako. Pata maelezo zaidi kuhusu vipengele, masharti ya kujiunga na maelezo ya kutuma ombi la kujiunga kwenye makala haya.
Utangulizi wa jinsi ya Kuchuma Mapato kwenye YouTube
Unachohitaji ili ujiunge
- Ufuate sera za uchumaji mapato kwenye chaneli za YouTube.
- Huu ni mkusanyiko wa sera na mwongozo unaokuruhusu kuchuma mapato kwenye YouTube na unahitaji kuutii unapokubali makubaliano ya ushirika na YouTube.
- Uishi katika nchi au eneo ambako Mpango wa Washirika wa YouTube unapatikana.
- Usiwe na maonyo yanayoendelea kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya kwenye chaneli yako.
- Uhakikishe kuwa umewasha Uthibitishaji wa Hatua 2 kwenye Akaunti yako ya Google.
- Uwe na ufikiaji wa vipengele vya kina kwenye YouTube.
- Uwe na akaunti moja ya AdSense katika YouTube inayotumika ambayo imeunganishwa na chaneli yako au uwe tayari kufungua akaunti kwenye Studio ya YouTube ikiwa bado huna akaunti (fungua tu akaunti ya AdSense katika YouTube kwenye Studio ya YouTube—pata maelezo zaidi).
Jinsi unavyoweza kutimiza masharti
Ukishaelewa hatua za kufuata ili ujiunge, chaneli yako inaweza kutimiza masharti ya kujiunga na Mpango wa Washirika wa YouTube kwa kutumia Video Fupi au video ndefu. Iwapo ungependa tukuarifu unapotimiza masharti, chagua Pokea arifa katika sehemu ya Chuma mapato ya Studio ya YouTube. Utapokea barua pepe baada ya kutimiza mojawapo ya masharti ya upeo yaliyo hapo chini.
1. Kuwa na wafuatiliaji 1,000 pamoja na kufikisha saa 4,000 za muda wa kutazama video unaotimiza masharti katika miezi 12 iliyopita au
2. Kuwa na wafuatiliaji 1,000 pamoja na kufikisha mara milioni 10 za kutazamwa kwa Video Fupi zinazotimiza masharti katika siku 90 zilizopita.
Maelezo zaidi kuhusu upeo wa ustahiki
Upeo huo hutusaidia kufanya uamuzi bora zaidi kuhusu iwapo chaneli yako inatimiza sera na mwongozo wetu. Ukishatuma ombi, chaneli yako itapitia mchakato wa kawaida wa ukaguzi ili kuona ikiwa inatimiza sera na mwongozo wetu. Ikiwa inatimiza sera na mwongozo wetu, tutairuhusu chaneli yako kujiunga na Mpango wa Washirika wa YouTube. Kumbuka kuwa tutaendelea kukagua chaneli katika Mpango wa Washirika wa YouTube ili kuhakikisha kuwa zinaendelea kutimiza sera na mwongozo wetu kadiri siku muda unavyosonga.
Mahali pa kutuma maombi
✨ MPYA✨ Ufikiaji wa Mapema wa Vipengele vya Mpango wa Washirika wa YouTube
Baada ya kupata unachohitaji na chaneli yako inatimiza masharti ya kutuma ombi, jisajili katika Mpango wa Washirika wa YouTube kwenye kompyuta ya mezani au kifaa cha mkononi:
- Ingia kwenye YouTube
- Katika sehemu ya juu kulia, bofya picha yako ya wasifu
Studio ya YouTube
- Kwenye menyu ya kushoto, bofya Chuma mapato
- Chagua Tuma Ombi Sasa ili uanze
- Bofya Anza ili usome na Ukubali Masharti ya msingi
- Bofya Anza ili ufungue akaunti ya AdSense katika YouTube au uunganishe akaunti iliyopo inayotumika
Ukimaliza, utaona hali ya Unaendelea kwenye hatua ya Kufanyiwa Ukaguzi, ikimaanisha kuwa tumepokea ombi lako!
Jinsi tunavyokagua ombi lako
Baada ya kukubali masharti ya Mpango wa Washirika wa YouTube na kuunganisha akaunti ya AdSense katika YouTube inayotumika, chaneli yako itawekwa kwenye foleni ya ukaguzi kiotomatiki. Mifumo ya kiotomatiki na wataalamu wetu watakagua chaneli yako kwa ujumla ili kuhakikisha kuwa inafuata mwongozo na sera zetu zote. Angalia tena kwenye sehemu ya Chuma mapato ya Studio ya YouTube wakati wowote ili uone hali ya ombi lako.
Tutawasiliana nawe tukufahamishe kuhusu uamuzi baada ya chaneli yako kukaguliwa (kwa kawaida huwa ndani ya takribani mwezi 1).
Kumbuka kuwa kunaweza kutokea ucheleweshaji wa kuchakata maombi kutokana na idadi kubwa ya maombi tunayopokea, matatizo ya mfumo au vizuizi vya nyenzo. Maombi yote ya Mpango wa Washirika wa YouTube yanashughulikiwa kulingana na tulivyoyapokea. Wakati mwingine chaneli huhitaji kufanyiwa ukaguzi mara nyingi, hasa wakati wakaguzi mbalimbali wana maoni tofauti kuhusu ufaafu wa chaneli yako kujiunga kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube. Hii inaweza kuongeza muda unaohitajika kufanya uamuzi.
Iwapo ombi lako la kwanza halikufanikiwa, usijali, unaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi huu ndani ya siku 21 au uendelee kupakia maudhui halisi na utaweza kutuma ombi tena baada ya kipindi cha siku 30. Iwapo hili si ombi lako la kwanza kukataliwa au ulituma tena ombi hapo awali, unaweza kujaribu tena baada ya kipindi cha siku 90. Huenda wakaguzi wetu waligundua kuwa sehemu kubwa ya chaneli yako haifuati sera na mwongozo wetu kwa sasa, hivyo hakikisha umekagua vipengele vinavyopingana na maudhui ya jumla ya chaneli yako na urekebishe chaneli yako kabla ya kutuma ombi tena. Pata maelezo zaidi kuhusu hatua unazoweza kuchukua ili kuboresha ombi lako wakati mwingine.
Kuchagua jinsi ya kuchuma mapato na kulipwa
Ukishajiunga na Mpango wa Washirika wa YouTube, anza kutumia Studio ya YouTube ukitumia Matangazo ya Ukurasa wa Kutazama na ya Mipasho ya Video Fupi, Uanachama, Super, Ununuzi na zaidi. Ili kuwasha vipengele vya uchumaji wa mapato, utahitaji kukagua na kukubali sheria na masharti ya sehemu husika. Pata maelezo zaidi kuhusu sehemu na chaguo zake hapa.
Baada ya kuchagua jinsi ambavyo ungependa kuchuma mapato, utaweza kudhibiti mapendeleo ya matangazo, kuwasha uchumaji wa mapato kwenye machapisho yako na zaidi. Ifuatayo ni orodha ya Maswali Yanayoulizwa Sana tunayoyapokea kutoka kwa watayarishi ambao wamejiunga hivi majuzi na Mpango wa Washirika wa YouTube.
Kupokea malipo
Tembelea Kituo chetu cha Usaidizi ili uelewe kwa urahisi kuhusu mapato yako kama mshirika wa YouTube, pata maelezo yote kuhusu AdSense katika YouTube (Mpango wa Google unaoruhusu watayarishi katika Mpango wa Washirika wa YouTube kulipwa) na kutatua matatizo ya kawaida ya malipo.
Kuendelea kutumia akaunti ili uendelee kuchuma mapato
Mpango wa Washirika wa YouTube unavyoendelea kuimarika, ni muhimu kudumisha mfumo wa chaneli ambao ni salama na unaotumika. Ili kuangazia usaidizi wetu kwa watayarishi ambao wana hamasa na wanawasiliana na jumuiya, tunaweza kuzima uchumaji wa mapato kwenye chaneli ambazo hazijapakia video au kuchapisha kwenye kichupo cha Machapisho kwa kipindi cha miezi 6 au zaidi.
Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu kutuma ombi na zaidi
Itakuwaje iwapo sitimizi upeo wa mpango?
Iwapo bado hujatimiza masharti, endelea kujitahidi kubuni maudhui halisi na kukuza hadhira yako. Zifuatazo ni baadhi ya nyenzo ambazo zinaweza kukusaidia kukuza chaneli yako:
- Pata suluhu kutoka kwa watumiaji wengine wa YouTube katika Mijadala ya Usaidizi ya YouTube.
- Gundua vidokezo rahisi na vya haraka vya jinsi ya kukuza na kujenga chaneli yako kwenye kituo chetu cha Vidokezo vya Mtayarishi.
- Nenda kwenye youtube.com/creators ili upate maelezo, ukuze chaneli yako na ufikie mipango, nyenzo na matukio.
- Angalia chaneli yetu ya Usaidizi kwa Wateja wa YouTube na chaneli ya Watayarishi wa maudhui ya YouTube ili utazame video za mafunzo, utatuzi na vidokezo kutoka kwa timu ya Usaidizi kwa Wateja wa YouTube.
Iwapo una maonyo yanayoendelea kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya kwenye chaneli yako, unaweza kutuma ombi baada ya muda wa maonyo yako kuisha. Unaweza pia kutuma ombi baada ya rufaa yako kukubaliwa ili maonyo kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya yaondolewe. Wanachama wa sasa wa mpango huu hawataondolewa watakapopokea maonyo kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya.
Muda wa kutazama video unaotimiza masharti
Kinachozingatiwa kuwa muda wa kutazama video unaotimiza masharti:
- Muda wa kutazama video unaotimiza masharti unaotokana na video ndefu ambazo umebainisha kuwa za umma
Muda wa kutazama video unaotokana na aina zifuatazo za video hauhesabiwi katika upeo wa Mpango wa Washirika wa YouTube:
- Video za faragha
- Video ambazo hazijaorodheshwa
- Video zilizofutwa
- Kampeni za utangazaji
- Video Fupi za YouTube
- Mitiririko mubashara ambayo haijaorodheshwa, imefutwa au haijageuzwa kuwa VOD (video iliyo tayari kutazamwa)
Mara za kutazamwa kwa Video Fupi zinazotimiza masharti
Kinachozingatiwa kuwa utazamaji wa Video fupi unaotimiza masharti:
- Utazamaji unaotimiza masharti kwenye Video Fupi ulizobainisha kuwa za umma unaoonekana kwenye Mipasho ya Video Fupi
Utazamaji wa Video Fupi unaotokana na aina zifuatazo za video hauhesabiwi katika upeo wa Mpango wa Washirika wa YouTube:
- Video Fupi za faragha
- Video Fupi ambazo hazijaorodheshwa
- Video Fupi zilizofutwa
- Kampeni za utangazaji
- Machapisho ya Picha yanayoonekana kwenye Mipasho ya Video Fupi
Kumbuka kuwa muda wowote wa kutazama video unaotimiza masharti kutokana na utazamaji wa Video Fupi katika Mipasho ya Video Fupi hauhesabiwi katika upeo wa muda wa kutazama video wa saa 4,000. Kwa maelezo kuhusu kutimiza masharti kwa utazamaji wa Video Fupi kulingana na jinsi tunavyokokotoa malipo, angalia sera zetu za uchumaji wa mapato kwenye Video Fupi za YouTube.
Je, iwapo ninatimiza upeo, nitajiunga kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube kiotomatiki?
Hapana. Kila chaneli ambayo inatimiza upeo itapitia mchakato wa kawaida wa ukaguzi. Timu yetu itakagua chaneli yako kikamilifu ili kubaini iwapo chaneli hiyo inatimiza sera zetu za uchumaji mapato wa chaneli kwenye YouTube. Lazima pia chaneli yako isiwe na maonyo yoyote yanayoendelea kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya ili utume ombi. Chaneli ambazo zinafuata sera na mwongozo wetu zinaweza kuchuma mapato.
Chaneli inatakiwa ikamilishe hatua zote za kujisajili kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube (ambazo kwa sasa zinajumuisha kusaini mkataba na kuunganisha akaunti ya AdSense katika YouTube) kabla ya kukaguliwa.
Iwapo chaneli haitumiki na haijapakia au kuchapisha machapisho ya Jumuiya kwa miezi 6 au zaidi, YouTube inahifadhi haki ya kuondoa uwezo wake wa kuchuma mapato.
Chaneli zitapoteza uwezo wa kuchuma mapato zikikiuka sera zozote za uchumaji mapato wa chaneli kwenye YouTube. Hali hii ya kupoteza uwezo wa kuchuma mapato itafanyika bila kujali muda wake wa kutazama video na idadi ya wanaofuatilia chaneli.
Kulingana na Sheria na Masharti yetu, YouTube inahifadhi haki ya kuonyesha matangazo kwenye maudhui yote katika mfumo. Iwapo bado hufikii vigezo vya juu vya kutimiza masharti ya kujiunga na Mpango wa Washirika wa YouTube, huenda bado ukaona matangazo yanaonyeshwa kwenye maudhui yako. Katika hali hii, bado hutimizi masharti ya kupokea mgawo wa mapato.
Baada ya kufikia vigezo vya juu vya kutimiza masharti ya kujiunga na Mpango wa Washirika wa YouTube, utaweza kupokea mgawo wa mapato yanayotokana na matangazo yaliyoonyeshwa kwenye maudhui yako.