Muhtasari na masharti ya kujiunga kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube

Tunapanua Mpango wa Washirika wa YouTube (YPP) kwa watayarishi wengi zaidi kwa kuwapa uwezo wa kufikia mapema vipengele vya Ununuzi na ufadhili kutoka kwa mashabiki. Mpango wa Washirika wa YouTube uliopanuliwa unapatikana kwa watayarishi wanaostahiki katika nchi au maeneo haya. Ikiwa unaishi katika mojawapo ya nchi au maeneo haya, soma makala haya ili upate maelezo zaidi kuhusu mabadiliko kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube. 

Ikiwa huishi katika mojawapo ya nchi au maeneo ambako mpango unapatikana, hakuna mabadiliko kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube yanayokuhusu. 

Angalia iwapo unastahiki kushiriki kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube uliopanuliwa. Iwapo bado hujastahiki, chagua Pata arifa katika sehemu ya Chuma mapato ya Studio ya YouTube. Tutakutumia barua pepe baada ya Mpango wa Washirika wa YouTube uliopanuliwa kukufikia na uwe umetimiza masharti ya upeo wa kustahiki. 
 

Mpango wa Washirika wa YouTube (YPP) huwapa watayarishi ufikiaji mkubwa zaidi wa rasilimali za YouTube na vipengele vya uchumaji wa mapato na ufikiaji wa timu zetu za Usaidizi kwa Watayarishi. Pia, unaruhusu ugavi wa mapato unaotokana na matangazo yanayoonyeshwa kwenye maudhui yako. Pata maelezo zaidi kuhusu vipengele, masharti ya kujiunga na maelezo ya kutuma ombi la kujiunga kwenye makala haya.

Utangulizi wa jinsi ya Kuchuma Mapato kwenye YouTube

Ungependa kutuma maombi ya kujiunga kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube, lakini unahitaji usaidizi kukuza hadhira kwanza? Angalia vidokezo vyetu kuhusu jinsi ya kuwa na mashabiki wengi na vidokezo vyetu vya Mpango wa Washirika wa YouTube.

Hatua za kufuata ili ujiunge

  1. Fuata Sera za Uchumaji Mapato kwenye Chaneli za YouTube.
    1. Huu ni mkusanyiko wa sera na mwongozo unaokuruhusu kuchuma mapato kwenye YouTube na utii wa sera unahitajika unapokubali makubaliano ya ushirika na YouTube.
  2. Uishi katika nchi au eneo ambako Mpango wa Washirika wa YouTube unapatikana.
  3. Usiwe na maonyo yanayoendelea kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya kwenye chaneli yako.
  4. Hakikisha kuwa umewasha kipengele cha Uthibitishaji wa Hatua 2 katika Akaunti yako ya Google.
  5. Uweze kufikia vipengele vya kina kwenye YouTube.
  6. Uwe na akaunti moja ya AdSense katika YouTube inayotumika ambayo imeunganishwa na chaneli yako au uwe tayari kufungua akaunti kwenye Studio ya YouTube ikiwa bado huna akaunti (fungua tu akaunti ya AdSense katika YouTube kwenye Studio ya YouTube, pata maelezo zaidi).

Jinsi unavyoweza kutimiza masharti

Ukishaelewa hatua za kufuata ili ujiunge, chaneli yako inaweza kutimiza masharti ya kujiunga na Mpango wa Washirika wa YouTube kwa kutumia Video Fupi au video ndefu. Iwapo ungependa tukuarifu unapostahiki, bofya Nijulishe ninapostahiki katika sehemu ya Kuchuma mapato ya Studio ya YouTube. Utapokea barua pepe baada ya kutimiza mojawapo ya masharti ya upeo yaliyo hapo chini.

1. Kuwa na wafuatiliaji 1,000 pamoja na kufikisha saa 4,000 za muda ambao video zimetazamwa hadharani kwa njia inayokubalika katika miezi 12 iliyopita, au
2. Kuwa na wafuatiliaji 1,000 pamoja na kufikisha mara milioni 10 za kutazamwa kwa Video Fupi hadharani kwa njia inayokubalika katika siku 90 zilizopita.

Kumbuka kuwa muda wowote ambao video zimetazamwa hadharani kutokana na utazamaji wa Video Fupi katika Mipasho ya Video Fupi hautahesabiwa katika upeo wa muda ambao video imetazamwa hadharani wa saa 4,000.

Maelezo zaidi kuhusu upeo wa ustahiki

Upeo huo hutusaidia kufanya uamuzi bora zaidi kuhusu iwapo chaneli yako inatimiza sera na mwongozo wetu. Ukishatuma ombi, chaneli yako itapitia mchakato wa kawaida wa ukaguzi ili kuona ikiwa inatimiza sera na mwongozo wetu. Ikiwa inatimiza sera na mwongozo wetu, tutairuhusu chaneli yako kujiunga na Mpango wa Washirika wa YouTube. Kumbuka kuwa tutaendelea kukagua chaneli katika Mpango wa Washirika wa YouTube ili kuhakikisha kuwa zinaendelea kutimiza sera na mwongozo wetu kadiri siku muda unavyosonga.

Mahali pa kutuma maombi

✨ MPYA✨ Ufikiaji wa Mapema wa Vipengele vya Mpango wa Washirika wa YouTube

Baada ya kupata unachohitaji na chaneli yako inatimiza masharti ya kutuma ombi, jisajili katika Mpango wa Washirika wa YouTube kwenye kompyuta ya mezani au kifaa cha mkononi:

  1. Ingia kwenye YouTube
  2. Katika sehemu ya juu kulia, bofya picha yako ya wasifu kisha Studio ya YouTube
  3. Kwenye menyu ya kushoto, bofya Chuma mapato
  4. Chagua Tuma Ombi Sasa ili uanze
  5. Bofya Anza ili usome na Ukubali Masharti ya msingi
  6. Bofya Anza ili ufungue akaunti ya AdSense katika YouTube au uunganishe akaunti iliyopo inayotumika

Ukimaliza, utaona hali ya Unaendelea kwenye hatua ya Kufanyiwa Ukaguzi, ikimaanisha kuwa tumepokea ombi lako!

Jinsi tunavyokagua ombi lako

Baada ya kukubali masharti ya Mpango wa Washirika wa YouTube na kuunganisha akaunti ya AdSense katika YouTube inayotumika, chaneli yako itawekwa kwenye foleni ya ukaguzi kiotomatiki. Mifumo ya kiotomatiki na wataalamu wetu watakagua chaneli yako kwa ujumla ili kuhakikisha kuwa inafuata mwongozo na sera zetu zote. Angalia tena kwenye sehemu ya Chuma mapato ya Studio ya YouTube wakati wowote ili uone hali ya maombi yako.

Tutawasiliana nawe tukikupa uamuzi baada ya chaneli yako kukaguliwa (kwa kawaida ndani ya takribani mwezi 1). 

Kumbuka kuwa kunaweza kutokea uchelewaji wa kuchakata maombi kutokana na idadi kubwa ya maombi tunayopokea, matatizo ya mfumo au vizuizi vya rasilimali. Maombi yote ya Mpango wa Washirika wa YouTube yanashughulikiwa kulingana na tulivyoyapokea. Wakati mwingine chaneli huhitaji kufanyiwa ukaguzi mara nyingi, hasa wakati wakaguzi mbalimbali wana maoni tofauti kuhusu ufaafu wa chaneli yako kujiunga kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube. Hii inaweza kuongeza muda unaohitajika kufanya maamuzi.

Iwapo ombi lako la kwanza halikufanikiwa, usitie shaka, unaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi huu ndani ya siku 21 au uendelee kupakia maudhui halisi na utaweza kutuma ombi tena baada ya kipindi cha siku 30. Iwapo hili si ombi lako la kwanza kukataliwa au ulituma tena ombi hapo awali, unaweza kujaribu tena baada ya kipindi cha siku 90. Huenda wakaguzi wetu waligundua kuwa sehemu kubwa ya chaneli yako haifuati sera na mwongozo wetu kwa sasa, hivyo hakikisha umekagua vipengele vinavyopingana na maudhui ya jumla ya chaneli yako na urekebishe chaneli yako kabla ya kutuma ombi tena. Pata maelezo zaidi kuhusu hatua unazoweza kuchukua ili kuboresha ombi lako wakati mwingine.

Kuchagua jinsi ya kuchuma mapato na kulipwa

Ukishajiunga na Mpango wa Washirika wa YouTube, anza kutumia Studio ya YouTube ukitumia Matangazo ya Ukurasa wa Kutazama, Matangazo ya Mipasho ya Video Fupi, Uanachama, Supers, Ununuzi na zaidi. Ili kuwasha vipengele vya uchumaji wa mapato, utahitaji kukagua na kukubali sheria na masharti ya sehemu husika. Pata maelezo zaidi kuhusu sehemu na chaguo zake hapa.

Baada ya kuchagua jinsi ambavyo ungependa kuchuma mapato, utaweza kudhibiti mapendeleo ya matangazo, kuwasha uchumaji wa mapato kwenye machapisho yako na zaidi. Ifuatayo ni orodha ya Maswali Yanayoulizwa Sana tunayoyapokea kutoka kwa watayarishi ambao wamejiunga hivi majuzi kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube.

Kulipwa

Tembelea Kituo chetu cha Usaidizi ili uelewe kwa urahisi kuhusu mapato yako kama mshirika wa YouTube, pata maelezo yote kuhusu AdSense katika YouTube (Mpango wa Google unaoruhusu watayarishi katika Mpango wa Washirika wa YouTube kulipwa) na kutatua matatizo ya kawaida ya malipo.

Endelea kutumia chaneli yako ili uendelee kuchuma mapato

Mpango wa Washirika wa YouTube unavyoendelea kuimarika, ni muhimu kudumisha mfumo wa chaneli ambao ni salama na unaotumika. Ili kuangazia usaidizi wetu kwa watayarishi ambao wana hamasa na wanawasiliana na jumuiya, tunaweza kuzima uchumaji wa mapato kwenye chaneli ambazo hazijapakia video au kuchapisha kwenye kichupo cha Jumuiya kwa kipindi kisichopungua miezi 6.

Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu kutuma ombi na zaidi

Itakuwaje iwapo sitimizi upeo wa mpango?

Iwapo bado hujatimiza masharti, endelea kujitahidi kubuni maudhui halisi na kukuza hadhira yako. Zifuatazo ni baadhi ya nyenzo ambazo zinaweza kukusaidia kukuza chaneli yako:

Iwapo una maonyo yanayoendelea kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya kwenye chaneli yako, unaweza kutuma ombi baada ya muda wa maonyo yako kuisha. Unaweza pia kutuma ombi baada ya rufaa yako kukubaliwa ili maonyo kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya yaondolewe. Wanachama wa sasa wa mpango huu hawataondolewa watakapopokea maonyo kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya.

Je, nini maana ya “muda ambao video imetazamwa hadharani kwa njia halali” na "utazamaji halali wa Video Fupi za umma"?

Muda ambao video imetazamwa hadharani kwa njia halali

Kinachozingatiwa kama muda ambao video imetazamwa hadharani kwa njia halali:

  • Muda wa kutazama unaotokana na video ndefu ambazo umebainisha kuwa za umma

Muda wa kutazama video unaotokana na aina zifuatazo za video hauhesabiwi katika upeo wa Mpango wa Washirika wa YouTube:

  • Video za faragha
  • Video ambazo hazijaorodheshwa
  • Video zilizofutwa
  • Kampeni za utangazaji
  • Video Fupi za YouTube
  • Mitiririko mubashara ambayo haijaorodheshwa, imefutwa au haijageuzwa kuwa Mfumo wa Kufikia Video Unapohitaji (VOD)

Utazamaji wa Video Fupi za umma kwa njia halali

Kinachozingatiwa kuwa utazamaji wa Video Fupi za umma kwa njia halali:

  • Utazamaji wa Video Fupi uliyoiweka hadharani unaoonekana katika Mipasho ya Video Fupi
Kumbuka kuwa muda wowote ambao video imetazamwa hadharani kutokana na utazamaji wa Video Fupi katika Mipasho ya Video Fupi hautahesabiwa katika upeo wa muda ambao video imetazamwa hadharani wa saa 4,000. Kwa maelezo kuhusu ustahiki wa utazamaji wa Video Fupi kulingana na jinsi tunavyokokotoa malipo, angalia sera zetu za uchumaji wa mapato kwenye Video Fupi za YouTube.

Iwapo ninatimiza upeo, je nitajiunga kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube kiotomatiki?

Hapana. Kila chaneli ambayo inatimiza upeo itapitia mchakato wa kawaida wa ukaguzi. Timu yetu itakagua chaneli yako kikamilifu ili kubaini iwapo chaneli hiyo inatimiza sera zetu za uchumaji mapato wa chaneli kwenye YouTube. Lazima pia chaneli yako isiwe na maonyo yoyote yanayoendelea kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya ili utume ombi. Chaneli ambazo zinafuata sera na mwongozo wetu zinaweza kuchuma mapato.

Itakuwaje iwapo hesabu zangu zitapungua na kuwa chini ya upeo baada ya kutuma ombi?

Tutaagiza chaneli yako ikaguliwe baada ya kutimiza upeo wa muda ambao video imetazamwa hadharani kwa njia halali na idadi ya wanaofuatilia. Kwa hivyo haijalishi iwapo idadi ya wanaofuatilia au muda wa kutazama unapungua chini ya upeo unaposubiri ukaguzi. Iwapo umetimiza upeo na umetuma ombi la kujiunga kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube, bado tutakagua chaneli yako ili kubaini ufaafu wa kujiunga kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube. Kumbuka kwamba chaneli inatakiwa ikamilishe hatua zote za kujisajili kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube (ambazo kwa sasa zinajumuisha kusaini mkataba na kuunganisha akaunti ya AdSense katika YouTube) kabla ya kukaguliwa.

Iwapo chaneli haitumiki na haijapakia au kuchapisha machapisho ya Jumuiya kwa miezi 6 au zaidi, YouTube inahifadhi haki ya kuondoa uwezo wake wa kuchuma mapato.

Chaneli zitapoteza uwezo wa kuchuma mapato zikikiuka sera zozote za uchumaji mapato wa chaneli kwenye YouTube. Hali hii ya kupoteza uwezo wa kuchuma mapato itafanyika bila kujali muda wake wa kutazama video na idadi ya wanaofuatilia chaneli.

Sipo tena kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube (au sikuwahi kujiunga kwenye mpango huu) na ninaona matangazo kwenye video zangu. Je, nitachuma mapato kutokana na matangazo hayo?

YouTube inaweza kuonyesha matangazo kwa maudhui yote kwenye mfumo. Iwapo awali ulikuwa mwanachama wa Mpango wa Washirika wa YouTube (na sasa haupo kwenye mpango huo), huenda bado ukaona matangazo yanayoonyeshwa kwenye maudhui yako. Katika hali hii, hupati mgawo wa mapato.

Iwapo utajiunga tena kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube, unaweza kupata mgawo wa mapato kutokana na matangazo yanayoonyeshwa kwenye maudhui yako baada ya kujiunga tena. Katika hali hiyo, unapotuma tena ombi la kujiunga kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube, hakikisha kuwa chaneli yako inatimiza masharti ya kujiunga yaliyobainishwa kwenye ukurasa huu.

 

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
false
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
3888248783344572843
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false