Masuala mengine ya kisheria

Malalamiko ya Kisheria na Amri za Korti

Ikiwa unahisi kuwa maudhui fulani kwenye tovuti yanakiuka haki zako au sheria zinazotumika, unaweza kuwasilisha malalamiko ya kisheria chini ya mitiririko ya malalamiko ya chapa ya biashara, kashfa, bandia, au malalamiko mengine ya kisheria . Ikiwa una amri ya mahakama dhidi ya aliyepakia, unaweza kuambatisha nakala ya amri ya mahakama kama jibu kwa jibu la kiotomatiki unalopata baada ya kuwasilisha malalamiko sahihi ya kisheria. Kila amri ya mahakama huchunguzwa na kutathminiwa kwa kutumia vigezo vya eneo na vya kimataifa.

Kumbuka pia kuwa una nyenzo nyingine za kuripoti maudhui. Kwa mfano, ikiwa unahisi maudhui hayatii mwongozo wa jumuiya, tafadhali yaripoti. Pia, zingatia iwapo video inakidhi vigezo vya kuondolewa chini ya sera ya faragha au unyanyasaji kabla ya kufungua malalamiko ya kisheria.

Ukwepaji wa Hatua za Kiteknolojia

Tunaposema ukwepaji wa hatua za kiteknolojia, tunarejelea zana zinazowaruhusu watumiaji kukwepa itifaki ya leseni ya programu. Hii inaweza kumaanisha namba za ufuatiliaji, vizalisha funguo, manenosiri na mbinu nyingine za kudukua programu au michezo.

Nini tofauti kati ya CTM na hakimiliki?

CTM ni zana inayowapa watumiaji njia ya kufikia programu. Hakimiliki inajihusisha na onyesho la programu au njia ya kuipata. Ikiwa kiolesura cha programu kipo katika video, au kuna kiungo cha kupakua programu katika video au maelezo ya video, huenda ukahitaji kutuma ombi la kuondolewa kwa video inayokiuka hakimiliki .

Dai la CTM linafaa wakati maudhui yanayokiuka hayapo katika video (au hayajaunganishwa moja kwa moja), lakini video inawapa watumiaji njia ya kuifikia isiyo halali.

Ikiwa unaamini una dai halali la CTM, tafadhali jaza fomu yetu ya wavuti.

Wasilisha malalamiko ya Ukwepaji wa Hatua za Kiteknolojia

Manukuu

Ikiwa umepata arifa inayokufahamisha kuwa video yako inakiuka Sheria ya Mawasiliano na Ufikiaji Video,  huenda ulipakia maudhui ambayo yalionyeshwa awali kwenye TV yakiwa na manukuu. Sheria ya Mawasiliano na Ufikiaji Video (CVAA) inahitaji kuwa maudhui yote ya video yaliyorekodiwa mapema ambayo yamewekewa manukuu kwenye TV pia yawe na manukuu kwenye intaneti. Ikiwa unaamini unaruhusiwa kutofuata masharti ya CVAA, unaweza kuchagua  cheti cha maudhui yako.

Ikiwa unaamini video inahitajika na CVAA iwe na manukuu, lakini aliyepakia hajaweka manukuu, tafadhali tuma ombi kupitia  fomu ya wavuti.

Kanuni ya Kudhibiti Maudhui ya Kigaidi Mtandaoni (“TCO”)

Ukipata maudhui ambayo unafikiri yanakiuka Mwongozo wetu wa Jumuiya na ungependa kuyawasilisha ili yakaguliwe, ripoti maudhui. Ili kupata maelezo zaidi kuhusu sera za YouTube, unaweza kusoma Mwongozo wetu wa Jumuiya. Unaweza pia kuondoa maudhui iwapo unaamini yanafaa kuondolewa kwa sababu za kisheria.

Ikiwa wewe ni mamlaka ya kiserikali yaliyoidhinishwa, unaweza kuwasiliana na YouTube ili upate maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuwasiliana na Mtu wa Kuwasiliana Naye kwa amri za kuondoa maudhui chini ya Kifungu cha 3 cha TCO. Kwa madhumuni haya, Google hukubali mawasiliano kwa Kiingereza.

Kwa maelezo zaidi kuhusu Kanuni ya Kudhibiti Maudhui ya Kigaidi Mtandaoni ya Umoja wa Ulaya (EU 2021/784), soma maandishi ya Kanuni rasmi ya Umoja wa Ulaya.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
9230936568193874623
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false