Pata maelezo kuhusu madai ya Content ID

Dai la Content ID huzalishwa kiotomatiki wakati video iliyopakiwa inalingana na video nyingine (au sehemu ya video) katika mfumo wa YouTube wa Content ID. Kulingana na mipangilio ya Content ID ya mwenye hakimiliki, madai ya Content ID yanaweza:
  • Kuzuia video isitazamwe
  • Kuchuma mapato kwenye video kwa kuonyesha matangazo, wakati mwingine kushiriki mapato na aliyepakia
  • Kufuatilia takwimu za watazamaji wa video

Hatua yoyote kati ya hizi inaweza kutegemea eneo mahususi la kijiografia. Kwa mfano, video iliyo na dai la Content ID inaweza kuchumiwa mapato katika nchi au eneo moja na kuzuiwa au kufuatiliwa katika nchi au eneo tofauti.

Kumbuka:
  • Video inayodaiwa inapofuatiliwa au kuchuma mapato inaendelea kuonekana kwenye YouTube ikiwa na dai linaloendelea la Content ID. Kwa kawaida, wenye hakimiliki huchagua kufuatilia au kuchuma mapato kwenye video, wala si kuzizuia.
  • Madai ya Content ID huwa tofauti na maombi ya kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki na maonyo ya hakimiliki.
  • Madai ya Content ID huathiri video, lakini kwa kawaida hayaathiri chaneli au akaunti yako.

Katika video hii, utapata maelezo kuhusu jinsi ya kukagua iwapo video yako ina dai la Content ID na hatua utakazoweza kuchukua:

Kukagua iwapo video yako ina dai la Content ID

YouTube itakutumia barua pepe iwapo video yako itapokea dai la Content ID. Unaweza pia kutumia YouTube Studio kuangalia iwapo video yako ina dai la Content ID.

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui .
  3. Bofya upau wa kichujio kisha Hakimiliki.
  4. Tafuta video husika.
  5. Katika safu wima ya Vizuizi, wekelea kiashiria juu ya Hakimiliki.
    • Hakimiliki: Video ina dai la Content ID.
    • Hakimiliki – Uondoaji: Video inaathiriwa na ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki, inayofahamika pia kama "uondoaji".
Kwa maelezo zaidi, bofya ANGALIA MAELEZO kwenye maandishi yaliyowekelewa kiashiria ili ufungue ukurasa wa Maelezo ya hakimiliki ya video.

Angalia aliyedai video yako

  1. Fuata hatua zilizo hapa juu ili upate video iliyo na dai la Content ID.
  2. Katika safu wima ya Vikwazo, bofya ANGALIA MAELEZO kwenye maandishi yaliyowekelewa kiashiria.
  3. Chini ya safu wima ya Athari kwenye video, wekelea kiashiria juu ya safu mlalo ili uone maelezo ya mwenye hakimiliki.

Iwapo humtambui mwenye hakimiliki, si lazima iwe inamaanisha kuwa dai si sahihi. Pia, iwapo video yako ina dai kutoka kwenye "jamii moja au zaidi za kukusanya mirabaha ya haki za kuchapisha muziki", huenda ungependa kupata maelezo zaidi kuhusu jamii za kukusanya mirabaha.

Kumbuka:
  • Unaweza kupata madai kutoka kwa wenye hakimiliki tofauti kuhusu sehemu tofauti za video yako.
  • Iwapo maudhui yana wenye hakimiliki tofauti katika nchi au maeneo tofauti, unaweza kupata madai mengine kwenye video au sehemu sawa.

Kudhibiti madai ya Content ID

Kulingana na hali, una chaguo chache za kujibu dai la Content ID:

Usichukue hatua
Iwapo unaamini kwamba dai ni sahihi, unaweza kutochukua hatua yoyote na uache dai kwenye video yako. Unaweza pia kubadili uamuzi wako baadaye.
Kuondoa maudhui yanayodaiwa

Iwapo unaamini kuwa dai ni sahihi, unaweza kuondoa maudhui yanayodaiwa bila kupakia video mpya. Ukifanya hivyo, chaguo zozote kati ya hizi zitaondoa dai kiotomatiki:

  • Kata sehemu: Unaweza kuondoa sehemu inayodaiwa kwenye video yako.
  • Badilisha wimbo: Iwapo sauti katika video yako imedaiwa, unaweza kubadilisha wimbo wako wa sauti uweke sauti nyingine kutoka kwenye Maktaba ya Sauti katika YouTube.
  • Sitisha sauti ya wimbo: Iwapo sauti katika video yako imedaiwa, unaweza kusitisha sauti ambayo imedaiwa. Unaweza kuchagua iwapo ungependa kusitisha wimbo au sauti yote katika video.
Gawa mapato
Iwapo umejiunga katika Mpango wa Washirika wa YouTube na muziki ulio katika video yako umedaiwa, huenda ukaweza kugawana mapato na mchapishaji wa muziki.
Kupinga dai

Iwapo unaamini kuwa dai si sahihi, unaweza kupinga dai kama una uhakika una haki zote zinazohitajika za kutumia maudhui yanayodaiwa.

Iwapo unapanga kupinga dai na ulikuwa ukichuma mapato kwenye video yako, hakikisha kuwa unafahamu utaratibu wa uchumaji wa mapato wakati wa mzozo. Kumbuka kuwa YouTube haileti upatanisho wakati wa mizozo ya hakimiliki.

Ukipinga dai bila sababu halali, mwenye hakimiliki anaweza kuomba kuondolewa kwa video yako. Tukipata ombi halali la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki kwenye video yako, akaunti yako itapokea onyo la hakimiliki.

Maswali Yanayoulizwa Sana (FAQs)

Je, nipo taabani iwapo video yangu ina dai la Content ID?

Labda hapana. Wenye hakimiliki ndio wanaoamua iwapo watu wengine wanaweza kutumia upya maudhui yao yanayolindwa kwa hakimiliki. Mara nyingi wanaruhusu maudhui yao yatumiwe katika video zinazodaiwa na waonyeshe matangazo kwenye video hizo. Huenda matangazo yakaonyeshwa kabla ya video au wakati video inacheza (iwapo video ina urefu wa zaidi ya dakika 8).

Iwapo wenye hakimiliki hawangependa maudhui yao yatumiwe upya, wanaweza:

  • Kuzuia video: Wenye hakimiliki wanaweza kuzuia video, hali inayomaanisha kuwa haitaweza kutazamwa kwenye YouTube. Video inaweza kuzuiwa kote duniani, au katika nchi au maeneo fulani.

  • Kudhibiti mifumo fulani: Wenye hakimiliki wanaweza kudhibiti programu au tovuti ambako maudhui yao yanaonekana. Kudhibiti hakubadilishi upatikanaji wa video kwenye YouTube.

Ninaweza kuchukua hatua gani iwapo dai la Content ID si sahihi?
Iwapo unaamini kuwa dai si sahihi, unaweza kupinga dai kama una uhakika kuwa una haki zote zinazohitajika za kutumia maudhui yanayodaiwa.
Kumbuka kuwa ukipinga dai bila sababu sahihi, mwenye hakilimiki anaweza kuomba kuondolewa kwa video yako. Iwapo ombi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki ni sahihi, onyo la hakimiliki litawekwa kwenye chaneli yako.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
7393947731247033155
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false