Muhtasari wa Mpango wa YouTube kwa Mashirika Yasiyo ya Faida

Mpango wa YouTube kwa Mashirika Yasiyo ya Faida huyapa mashirika yasiyo ya faida idhini ya kufikia vipengele maalum vya YouTube ili yaweze kuwasiliana na mashabiki, wanaojitolea na wafadhili.

Katika hali nyingi, video ni muundo mpya na muhimu wa kusimulia hadithi. Kwa kuwa YouTube hupata watazamaji bilioni moja kila mwezi, mashirika yote yasiyo ya faida yanaweza kutumia video kwenye YouTube kushiriki hadithi zao na hadhira ya kimataifa. Unaweza kuangalia nyenzo zetu zote kwenye tovuti ya Mpango wa YouTube kwa Mashirika Yasiyo ya Faida.

Mahitaji ya mpango

Ili kubaini ikiwa shirika lisilo la faida linatimiza mahitaji ya kushiriki katika Mpango wa YouTube kwa Mashirika Yasiyo ya Faida, kagua mwongozo wa mahitaji ya kujiunga kwenye Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida.

Vipengele vya mpango

Kama mshirika katika Mpango wa YouTube kwa Mashirika Yasiyo ya Faida, unaweza kufikia vipengele mahususi vilivyoundwa kwa ajili ya wahusika:

Tumia kadi za michango kwenye video

Mashirika yasiyo ya faida nchini Marekani yanaweza kuchanga pesa kwa kuweka kadi za michango kwenye video zao za YouTube na kutumia zana ya kutangaza kadi za michango ili kuwaunganisha mashabiki na watayarishaji.

Unganisha moja kwa moja kwenye tovuti yako kutoka video zako

Kadi za Kuunganisha Popote

Unaweza kuwaelekeza watazamaji wako kwenye kurasa za kutua za nje za kampeni ukitumia kadi za Kuunganisha Popote, aina maalum ya kadi ambazo hukuruhusu kuunganisha kwenye URL za nje. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kuweka kadi za Kuunganisha Popote kwenye video zako.

Matangazo yenye mwito wa kuchukua hatua yaliyowekelewa juu ya video

Unaweza kuunda matangazo yanayowekelewa juu ya video zako, ambayo yanaonekana wakati video inapoanza kucheza. Watumiaji wanapobofya matangazo hayo, wanaelekezwa kwenye tovuti ya nje au tovuti nyingine ambayo unachagua.

Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuwekelea tangazo lenye mwito wa kuchukua hatua juu ya video yako ili watazamaji waweze kubofya na kutembelea tovuti yako au kuchangia shirika lako.

Boresha maudhui yako 

Tumia nyenzo zetu kuboresha maudhui ya shirika lako lisilo la faida, kituo na vipengele vingine vinavyotumiwa na mashirika yasiyo ya faida:

Tumia nyezo zetu za uchapishaji

Unaweza kupata idhini ya utayarishaji ili urekodi au uhariri video zako kwenye studio ya watayarishaji katika mji wa Los Angeles au New York. Tembelea tu tovuti ya Space LA au Space NY na ubofye kitufe cha Tuma ombi sasa.

Usaidizi thabiti wa kiufundi

Nyezo za Watayarishaji wa YouTube

Pata maelezo kuhusu jinsi ya kupata usaidizi kupitia nyenzo za watayarishaji wetu ili uweze kuboresha kituo cha shirika lako lisilo la faida.

Usaidizi thabiti wa kiufundi

Ikiwa una matatizo yoyote ya kuweka kituo cha shirika lako lisilo la faida, wanachama wa Mpango wa Shirika Lisilo la Faida hupata usaidizi thabiti kupitia barua pepe ili wahakikishe kuwa matatizo ya kiufundi yanatatuliwa haraka. Tumia tu fomu hii kutueleza kuhusu matatizo haya na tutaweza kukusaidia.

 
Hakikisha kuwa unaangalia aina mbalimbali zavipengele vya kituo cha watayarishaji wa YouTube vinavyopatikana kwa ajili ya watayarishaji wote wa Mpango wa YouTube kwa Mashirika Yasiyo ya Faida.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
14338330355450228709
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false