Content ID ni mfumo nyumbufu wa YouTube wa kiotomatiki unaowawezesha wenye hakimiliki kutambua video za YouTube zenye maudhui wanayoyamiliki.
YouTube huwapa Content ID wenye hakimiliki ambao tu wanatimiza vigezo mahususi. Ili uidhinishwe, ni lazima umiliki haki za kipekee za kiwango kikubwa cha maudhui halisi ambayo hupakiwa mara kwa mara na jumuiya ya watumiaji wa YouTube.
YouTube huweka pia mwongozo dhahiri kuhusu jinsi ya kutumia Content ID. Sisi hufuatilia matumizi na mizozo ya Content ID mara kwa mara ili kuhakikisha kuwa mwongozo huu unafuatwa.
Kama mwenye hakimiliki, unaipa YouTube nakala ya marejeleo yenye maudhui yako yanayotimiza vigezo. YouTube hutumia marejeleo hayo kukagua kama video zilizopakiwa zina maudhui yanayolingana. Maudhui yanayolingana yanapopatikana, YouTube hutumia sera unayopendelea: kuchuma mapato, kufuatilia au kuzuia video husika.
Hatua kuu za kutumia Content ID ni:
-
Kuweka mmiliki wako wa maudhui.
Unapoidhinishwa kutumia Content ID, msimamizi wako wa washirika kwenye YouTube hukuwekea mmiliki wa maudhui, anayekuwakilisha kwenye mfumo wa kudhibiti maudhui wa YouTube na kukupa idhini ya kufikia zana za Kidhibiti Maudhui katika Studio ya Watayarishi. Unahitaji kuweka mipangilio ya akaunti yako ya mmiliki wa maudhui. Kwa kutegemea mahitaji yako, unaweza kuhusisha akaunti ya AdSense katika YouTube na mmiliki wa maudhui au uwape watumiaji wa ziada idhini ya kufikia zana za Kidhibiti Maudhui.
-
Kuwasilisha maudhui kwenye YouTube.
Unaweka maudhui yako yaliyo na hakimiliki kwenye mfumo wa kudhibiti maudhui wa YouTube kwa kuwasilisha faili za marejeleo (sauti, video au sauti na video) na metadata inayofafanua maudhui hayo na maeneo ambako unayamiliki.
Kwa kila maudhui unayowasilisha, YouTube huunda kipengee kwenye mfumo wa kudhibiti maudhui. Kwa kutegemea aina ya maudhui au mbinu ya uwasilishaji uliyochagua, YouTube hubuni pia video ya YouTube inayoweza kutazamwa, marejeleo kwa ajili ya ulinganishaji wa Content ID au yote mawili.
-
Content ID hukagua video zilizopakiwa na watumiaji na kutambua maudhui yanayolingana.
Content ID hulinganisha kwa mfululizo video mpya zinazopakiwa na marejeleo ya vipengee vyako. Video zinazolingana hudaiwa kiotomatiki kwa niaba ya kipengee na sera ya zinazolingana uliyobainisha hutumiwa kwenye video zilizodaiwa kabla hazijachapishwa kwenye YouTube.
Content ID hufanya pia "ukaguzi wa maudhui ya zamani" ili kutambua video zinazolingana zilizopakiwa kabla ya kipengee chako kuwekwa. Video zilizopakiwa hivi karibuni na video maarufu hukaguliwa kwanza. -
Kudhibiti na kufuatilia maudhui yako.
Kidhibiti Maudhui kina orodha ya Majukumu yenye vitendo kama vile kukagua madai na kutatua mizozo ya umiliki. Pia, una uwezo wa kufikia takwimu, ripoti za mapato na orodha kamili ya zana za kudhibiti maudhui.