Sera kuhusu unyanyasaji na uchokozi wa mtandaoni

Usalama wa watayarishi, watazamaji na washirika wetu ndio kipaumbele chetu cha juu zaidi. Tunamtegemea kila mmoja wenu atusaidie kulinda jumuiya ya kipekee yenye hamasa ya hali ya juu. Ni muhimu kuelewa Mwongozo wetu wa Jumuiya pamoja na jukumu lake kwenye wajibu wetu wa pamoja wa kuifanya YouTube kuwa sehemu salama. Tenga muda usome kwa uangalifu sera iliyo hapa chini. Pia unaweza kuangalia ukurasa huu ili upate orodha kamili ya mwongozo wetu.

Haturuhusu maudhui yanayomlenga mtu kwa matusi au kashfa refu kulingana na maumbile yake au kwa kuwa katika kikundi cha watu wanaolindwa, kama vile umri, ulemavu, kabila, jinsia, mwelekeo wa kingono au mbari. Pia haturuhusu tabia zingine zenye madhara, kama vile vitisho au upekuzi na utangazaji wa taarifa binafsi. Kumbuka kuwa tunachukua hatua kali zaidi dhidi ya maudhui yanayolenga watoto.

Ikiwa utaona maudhui yanayokiuka sera hii, yaripoti. Maagizo ya kuripoti ukiukaji wa Mwongozo wetu wa Jumuiya yanapatikana hapa. Iwapo utapata maoni au video nyingi ambazo ungependa kuripoti, unaweza kuripoti chaneli. Ili upate vidokezo kuhusu jinsi ya kuwa salama, kudumisha usalama wa akaunti yako na kulinda faragha yako, angalia Kituo cha Usalama cha Watayarishi na Kuimarisha usalama wako kwenye YouTube.

Ikiwa vitisho mahususi vitatolewa dhidi yako na unahisi hauko salama, ripoti moja kwa moja kwa taasisi ya utekelezaji wa sheria, mahali uliko.

Jinsi sera hii inavyokuathiri

Ikiwa unachapisha maudhui

Usichapishe maudhui kwenye YouTube ikiwa yanalingana na maelezo yoyote yaliyo hapa chini.

  • Maudhui yaliyo na maneno ya kukashifu au matusi mengi kulingana na sifa na maumbile ya mtu. Sifa hizi ni pamoja na hali yake ya kuwa katika kikundi cha watu wanaolindwa, maumbile au hali yake kama mwathiriwa wa unyanyasaji wa kingono, usambazaji wa picha za kimapenzi bila idhini ya mhusika, unyanyasaji nyumbani, unyanyasaji wa watoto na zaidi.
  • Maudhui yaliyopakiwa kwa kusudi la kumwaibisha, kumhadaa au kumtukana mtoto. Hii inamaanisha kunuia kufanya mtoto awe na hisia zisizopendeza, kama vile mateso, fedheha au kudhalilika, kukusudia kumfanya afanye mambo yanayoweza kumdhuru au kudhuru mali yake au kutumia majina ya kukera dhidi yake. Mtoto ni mtu aliye chini ya umri wa miaka 18.
Aina nyinginezo za maudhui yanayokiuka sera hii
  • Maudhui yanayoshiriki, yanayotishia kushiriki na yanayohimiza wengine kushiriki taarifa za faragha zinazoweza kumtambulisha mtu binafsi (PII). 
    • PII inajumuisha, lakini si tu, anwani za nyumbani, anwani za barua pepe, vitambulisho vya kuingia katika akaunti, kama vile jina la mtumiaji au nenosiri, namba za simu, namba za pasipoti, rekodi za matibabu au taarifa za akaunti ya benki.
    • Hali hii haijumuishi uchapishaji wa taarifa za umma zinazopatikana kwa watu wengi, kama vile namba rasmi ya simu ya ofisi ya kiongozi au namba ya simu ya biashara. 
    • Sera hii inatumika katika hali ambapo unashiriki Taarifa Binafsi Zinazoweza Kukutambulisha, kushiriki Taarifa Binafsi Zinazoweza Kumtambulisha Mtu mwingine na unaposhiriki Taarifa Binafsi Zinazoweza Kumtambulisha Mtu bila kukusudia.
    • Maudhui lazima yaonyeshe wazi wakati PII bandia inaposhirikiwa. Kwa mfano, kutumia kitambulisho bandia cha kuingia katika akaunti kama sehemu ya mafunzo.
  • Maudhui yanayohimiza tabia mbaya, kama vile mashambulizi ya pamoja mtandaoni. Mashambulizi ya pamoja mtandaoni yanatokea wakati mtu binafsi anahimiza watu kuungana kumtukana mtu anayetambulika kwenye YouTube au nje ya YouTube.
  • Maudhui ambayo yanatangaza nadharia hatari za njama au yanayomlenga mtu kwa kudai kuwa mtu huyo ni sehemu ya nadharia hatari ya njama. Nadharia hatari ya njama ni ile ambayo imehusishwa na vitisho vya moja kwa moja au vitendo vya ukatili.
  • Maudhui yanayomtisha mtu anayetambulika au mali yake. Hii inajumuisha vitisho dhahiri ambavyo havibainishi wakati au mahali mahususi, lakini vinaweza kuhusisha silaha, kwa mfano.
  • Maudhui yanayoonyesha tukio lililopangwa ambapo mtu binafsi anayetambulika anashutumiwa kushiriki na mtoto matendo yasiyofaa, bila polisi kuwepo.
  • Maudhui ya kufurahia au kudhihaki majeraha mabaya au kifo cha mtu anayetambulika.
  • Maudhui yanayoiga kihalisia watoto waliofariki au waathiriwa wa matukio hatari au matukio makubwa ya vurugu yaliyorekodiwa yanayoelezea vifo vyao au vurugu walizopitia.
  • Maudhui yanayoonyesha watayarishi wakiiga vitendo vya vurugu mbaya dhidi ya wengine. Kwa mfano, mauaji, mateso, kulemaza, kupiga na mengine.
  • Maudhui yanayohusu unyatiaji wa mtu anayetambulika.
  • Maudhui yanayokataa au kupunguza hali ya kuhusika kwa mtu kama mwathiriwa kwenye tukio kubwa la vurugu lililorekodiwa.
  • Maudhui yaliyo na mawasiliano ya kimapenzi bila ridhaa ya mtu anayetambulika. Hii inajumuisha:
    • Maudhui yanayomweleza mtu kwa njia chafu, ya kudhalilisha na ya ngono dhahiri
    • Maudhui yanayoshiriki, kuomba au kuonyesha jinsi ya kusambaza picha ya kimapenzi inayoshirikiwa bila idhini ya mhusika
    • Maudhui yanayoonyesha hali ya kuwaza kuhusu, kutisha au kuunga mkono unyanyasaji wa kingono

Sera hii hutumika kwa video, maelezo ya video, maoni, mitiririko mubashara na bidhaa au vipengele vingine vyovyote kwenye YouTube. Kumbuka kuwa orodha hii haijataja kila kitu. Kumbuka kuwa sheria hizi pia zinatumika kwenye viungo vya nje katika maudhui yako. Hii inaweza kujumuisha URL unazoweza kubofya, kuwaelekeza watumiaji kwenye tovuti nyingine katika video na njia zingine.

Hali zisizofuata kanuni za sera

Tunaweza kuruhusu maudhui yenye maudhui ya unyanyasaji ikiwa yana lengo la msingi la kuelimisha, kuelezea hali halisi, ya kisayansi au kisanaa. Hali hizi zisizofuata kanuni za sera si kibali cha kumnyanyasa mtu. Baadhi ya mifano ni pamoja na:

  • Mijadala inayohusiana na viongozi au wafanyakazi wa nyadhifa za juu: Maudhui yanayoangazia mijadala au majadiliano kuhusu mada mbalimbali zinazohusu watu binafsi walio na vyeo vya uongozi, kama vile wafanyakazi wa serikali katika nyadhifa za juu au Maafisa Wakuu Watendaji (CEO) wa mashirika makubwa ya kimataifa.
  • Maonyesho ya uigizaji: Matusi yanayotolewa katika muktadha wa sanaa kama vile tashtiti kwenye maigizo, vichekesho vya jukwaani au muziki (kama vile wimbo wa kushambulia). Kumbuka: Hali hii ya kutofuata kanuni za sera si kibali cha kumyanyasa mtu na kudai kuwa “Nilikuwa natania.”
  • Elimu au hamasisho kuhusu unyanyasaji: Maudhui yanayoangazia unyanyasaji halisi au wa kuigwa kwa nia ya kutayarisha makala au kwa kutumia wahusika waliojitolea (kama vile waigizaji) ili kupambana na uchokozi wa mtandaoni au kuwahamasisha watu.

Kumbuka: Tunashughulikia kwa uzito maudhui yanayomtukana vibaya mtu fulani kulingana na hali yake ya kuwa katika kikundi cha watu wanaolindwa bila kujali iwapo mtu huyo anashikilia nyadhifa ya juu au la.

Uchumaji wa mapato na adhabu nyinginezo

Katika baadhi ya matukio ambayo ni nadra sana kutokea, tunaweza kuondoa maudhui au kutoa adhabu nyinginezo pale mtayarishi:

  • Anapohimiza tabia mbaya kwa hadhira mara kwa mara.
  • Anapolenga, kutukana na kufedhehesha mtu binafsi anayetambulika kulingana na sifa na maumbile yake, kwenye video kadhaa alizopakia.
  • Anapomweka mtu binafsi hatarini kupata majeraha ya mwili kutokana na muktadha wa kijamii au kisiasa katika eneo aliko.
  • Anapotayarisha maudhui yanayoathiri jumuiya ya YouTube kwa kuendelea kuchochea uhasama dhidi ya watayarishi kwa manufaa binafsi ya kifedha.

Mifano

Ifuatayo ni baadhi ya mifano ya maudhui ambayo hayaruhusiwi kwenye YouTube:

  • Kuonyesha picha za mtu fulani mara kwa mara na kutoa kauli kama vile “Angalia meno ya kiumbe huyu, yanachukiza mno!” na maoni kama hayo yanayolenga sifa na maumbile kwenye video nzima.
  • Kumlenga mtu binafsi kulingana na hali yake ya kuwa katika kikundi cha watu wanaolindwa, kwa mfano kwa kusema: “Mwangalie huyu [neno la kufedhehesha linalolenga kikundi cha watu wanaolindwa]!”
  • Kumlenga mtu binafsi na kutoa madai kuwa anahusika na vitendo vya ulanguzi wa watu katika muktadha wa nadharia hatari ya njama ambapo njama inahusishwa na vitisho vya moja kwa moja au vitendo vya vurugu.
  • Kutumia matusi makali kumdhalilisha mtu binafsi kulingana na sifa na maumbile yake mahususi. Kwa mfano: “Angalia jibwa hili la mwanamke! Huyu si binadamu hata - labda awe jinamizi au mnyama fulani!”
  • Kulenga mtu binafsi na kuelezea kutamani kifo chake au jeraha baya: "Ninamchukia sana. Naomba agongwe na lori afe."
  • Kuonyesha mtu binafsi anayetambulika akiuawa au kujeruhiwa vibaya. Kwa mfano: Video ina klipu kutoka kwenye filamu fulani, ambapo mhusika mmoja anapigwa risasi kikatili na kuuawa. Video hiyo imehaririwa ili picha ya mtu halisi ionekane juu ya uso wa mhusika huyo.
  • Kutishia usalama wa mwili wa mtu fulani. Hii inajumuisha vitisho dhahiri kama, “Nikikuona Jumamosi nitakuua.” Hii pia inajumuisha kudokeza vurugu kwa kusema vitu kama, “Chunga sana, nakukujia” huku ukionyesha silaha.
  • Kuchapisha taarifa za faragha zinazoweza kumtambulisha mtu binafsi, kama vile namba ya simu, anwani ya nyumbani au anwani ya barua pepe, kuelekeza watumiaji au mtazamo mbaya upande wake. Kwa mfano, kusema, “Nimepata namba yake ya simu. Piga simu na kutuma ujumbe hadi atakapojibu!”
  • “Kushambulia” au kuelekeza uhasidi kwa mtu binafsi anayetambulika kupitia gumzo za sauti za ndani ya mchezo au ujumbe mtiririko unapoendelea.
  • Kuelekeza watumiaji kuandika maoni yasiyofaa kwenye sehemu ya maoni ya mtayarishi mwingine.
  • Kuunganisha kwenye tovuti za nje ya mfumo zinazopangisha au kuangazia picha ya kimapenzi inayoshirikiwa bila idhini ya mhusika.
  • Kuwaomba watumiaji wengine wawasiliane nawe ikiwa wangependa kushiriki picha ya kimapenzi inayoshirikiwa bila idhini ya mhusika.
  • “Kupiga simu za uongo” au simu nyingine za mzaha kwa huduma za dharura au kuwahimiza watazamaji washiriki katika kitendo hiki au tabia nyingine yoyote ya unyanyasaji.
  • Kunyatia au kujaribu kuwatisha watumiaji kwa vitendo vya usaliti.
  • Maudhui ya mchezo wa video ambayo yamebuniwa au yameboreshwa ("yamerekebishwa") ili kutangaza tukio la vurugu dhidi ya mtu binafsi.

Kumbuka, orodha hii haijakamilika. Usichapishe maudhui iwapo unafikiri kuwa huenda yatakiuka sera hii.

Kitakachofanyika iwapo maudhui yanakiuka sera hii

Iwapo maudhui yako yanakiuka sera hii, tutaondoa maudhui hayo na kukutumia barua pepe ili kukufahamisha. Ikiwa hatuwezi kuthibitisha kuwa kiungo ulichochapisha ni salama, huenda tukakiondoa. Kumbuka kuwa URL zinazokiuka sera zinazochapishwa kwenye video husika au katika metadata ya video zinaweza kusababisha tuondoe video husika.

Ikiwa hii ni mara yako ya kwanza kukiuka Mwongozo wetu wa Jumuiya, huenda ukapewa tahadhari bila adhabu kwenye chaneli yako. Utakuwa na fursa ya kushiriki katika mafunzo ya sera ili kuruhusu muda wa tahadhari uliopewa uishe baada ya siku 90. Hata hivyo, ikiwa utakiuka sera hiyo tena ndani ya kipindi hicho cha siku 90, muda wa tahadhari hautaisha na chaneli yako itapewa onyo. Ukikiuka sera tofauti baada ya kukamilisha mafunzo, utapewa tahadhari nyingine.

Ikiwa utapokea maonyo 3 katika kipindi cha siku 90, chaneli yako itasimamishwa. Pata maelezo zaidi kuhusu mfumo wetu wa maonyo.

Tunaweza kusimamisha chaneli au akaunti yako kwa ukiukaji wa mara kwa mara wa Mwongozo wa Jumuiya au Sheria na Masharti. Tunaweza pia kusimamisha chaneli au akaunti yako baada ya tukio moja la ukiukaji kwa kiasi kikubwa au chaneli ikikiuka sera mara kwa mara. Huenda tukazuia watu wanaorudia kufanya makosa wasishiriki katika mafunzo ya sera siku zijazo. Pata maelezo zaidi kuhusu kufungwa kwa chaneli au akaunti.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
6380181028055685422
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false