Mwongozo wa Jumuiya ni kanuni kuhusu tabia unazopaswa kufuata kwenye YouTube. Sera hizi zinatumika katika aina zote za maudhui kwenye mfumo wetu, ikiwa ni pamoja na maudhui ambayo hayajaorodheshwa na ya faragha, maoni, viungo, machapisho na vijipicha. Orodha hii si kamili. Iwapo maudhui yako yanakiuka Mwongozo wetu wa Jumuiya, chaneli yako inaweza kupewa onyo.
Kumbuka: Tunaweza kuondoa maudhui kwa sababu nyinginezo mbali na ukiukaji wa Mwongozo wa Jumuiya. Kwa mfano, malalamiko kuhusu faragha kutoka kwa mhusika au amri ya mahakama. Katika hali hizi, chaneli yako haitapokea onyo.
Kutayarisha kwa Kuzingatia Kanuni: Mwongozo wa Jumuiya ya YouTube
Kinachofanyika unapopewa onyo
Ukipewa onyo, utaarifiwa kupitia barua pepe. Unaweza pia kuchagua kutumiwa arifa kupitia kifaa cha mkononi na arifa za kompyuta na katika mipangilio ya chaneli yako. Pia, tutakufahamisha kuhusu:
- Maudhui yaliyoondolewa
- Sera zilizokiuka (kwa mfano unyanyasaji au vurugu)
- Jinsi inavyoathiri chaneli yako
- Hatua unayoweza kuchukua
Iwapo maudhui yako yanakiuka Mwongozo wa Jumuiya yetu, yataathiri chaneli yako kwa njia zifuatazo:
Tahadhari
Tunafahamu unaweza kukosea na hukiuki sera zetu kwa kukusudia — ndiyo sababu ukiukaji wa kwanza kwa kawaida hupokea tahadhari tu. Ili muda wa tahadhari hii uishe baada ya siku 90, unaweza kushiriki katika mafunzo ya sera yasiyo ya lazima. Hata hivyo, ikiwa maudhui yako yatakiuka sera ile ile ndani ya kipindi cha siku 90, huenda muda wa tahadhari hautaisha na chaneli yako inaweza kupewa onyo.
Wakati mwingine tukio moja la ukiukaji kwa kiasi kikubwa linaweza kusababisha kusimamishwa kwa chaneli bila tahadhari. Iwapo unafikiri kuwa tumekosea, unaweza kukata rufaa.
Mafunzo ya sera yasiyo ya lazima
Mafunzo ya sera ni elimu fupi ya ndani ya bidhaa inayolingana na sera mahususi ya Mwongozo wa Jumuiya ambayo umekiuka.
Ukipokea tahadhari kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya, unaweza kufikia mafunzo ya sera kupitia akaunti yako ya Studio popote ambapo kwa kawaida huwa unaangalia iwapo umekiuka sera. Hii inajumuisha dashibodi ya Studio na kichupo cha Maudhui. Pia, utaona kiungo cha kufungua mafunzo kupitia barua pepe na arifa za bango. Kumbuka: Si tahadhari zote za ukiukaji wa Mwongozo wa Jumuiya zinatimiza masharti ya mafunzo ya sera.
Ukikamilisha mafunzo ya sera yasiyo ya lazima, muda wa tahadhari uliyopewa utaisha baada ya siku 90. Kipindi cha siku 90 kitaanza baada ya mafunzo kukamilika, wala si wakati tahadhari imetolewa. Ukikiuka sera tofauti baada ya kukamilisha mafunzo, utapewa tahadhari nyingine.
Ukiukaji unaojirudia wa sera zetu – au tukio moja la ukiukaji mbaya sana– linaweza kusababisha kusimamishwa kwa akaunti yako. Huenda tukazuia watu wanaorudia kufanya makosa wasishiriki katika mafunzo siku zijazo.
Onyo la Kwanza
Tukibaini kuwa maudhui yako hayafuati sera zetu kwa mara ya pili, utapata onyo.
Onyo hili linamaanisha kuwa hutaruhusiwa kufanya yafuatayo kwa wiki 1:
- Kupakia video au kuanzisha mitiririko mubashara
- Kuanzisha mtiririko mubashara ulioratibiwa
- Kuratibu video ili iwe ya umma
- Kuanzisha Onyesho la Kwanza
- Kuweka kionjo cha Onyesho la kwanza au mtiririko mubashara ujao
- Kuunda machapisho na vijipicha maalum
- Kutayarisha, kubadilisha au kuweka washirika katika orodha
- Kuweka au kuondoa orodha kwenye ukurasa wa kutazama kwa kutumia kitufe cha “Hifadhi”
Maudhui yako ya umma yaliyoratibiwa yanawekwa kuwa ya “faragha” kwa kipindi cha adhabu. Unapaswa kuyaratibu upya kipindi cha kusitishwa kitakapoisha.
Kumbuka: Adhabu huanza tarehe ya kuthibitisha.
Baada ya kipindi cha wiki 1, tutarejesha manufaa kamili kiotomatiki, lakini onyo litasalia kwenye chaneli yako kwa siku 90.
Onyo pia linaweza kusababisha upoteze idhini ya kufikia vipengele vya kina. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kupata tena idhini.
Onyo la Pili
Ukipata onyo la pili kabla ya kuisha kwa siku 90 tangu onyo la kwanza, hutaruhusiwa kuchapisha maudhui kwa wiki 2. Iwapo hamna masuala ya zaida, baada ya kipindi cha wiki 2, tutarejesha manufaa kamili kiotomatiki. Muda wa kila onyo hautaisha hadi kukamilika kwa siku 90 kuanzia wakati lilipotolewa.
Onyo la Tatu
Maonyo 3 katika kipindi kimoja cha siku 90 yanaweza kusababisha chaneli yako kuondolewa kabisa kwenye YouTube. Muda wa kila onyo hautaisha hadi kukamilika kwa siku 90 kuanzia wakati lilipotolewa.
Kumbuka: Kufuta maudhui yako hakuondoi onyo. Tunaweza pia kutoa onyo kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya kwenye maudhui yaliyofutwa. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu wakati tunahifadhi maudhui yaliyofutwa katika Sera yetu ya faragha.
Iwapo Chaneli yako Rasmi ya Msanii itapokea onyo kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya, itasimamishwa na kubadilishwa kuwa chaneli ya kawaida. Pata maelezo zaidi.
Hatua unazoweza kuchukua ukipata onyo
Tungependa kukusaidia uendelee kutumia YouTube, kwa hivyo kumbuka kufanya yafuatayo:
- Pata maelezo kuhusu Mwongozo wa Jumuiya yetu ili uhakikishe kuwa maudhui yako yanafuata sera zetu.
- Iwapo chaneli yako ilipata onyo na unafikiri tumekosea, tufahamishe. Unaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo hapa.
Kwa hiari yake, YouTube pia inahifadhi haki ya kudhibiti uwezo wa mtayarishi wa kubuni maudhui. Huenda chaneli yako ikafungwa au kudhibitiwa isitumie vipengele vyovyote vya YouTube.
Iwapo hili litatokea, huruhusiwi kutumia, kufungua wala kujipatia chaneli nyingine ili kukwepa vizuizi hivi. Marufuku haya yanatumika wakati wote ambapo chaneli yako ya YouTube imewekewa vizuizi. Ukiukaji wa vizuizi hivi unazingatiwa kuwa ukwepaji chini ya Sheria na Masharti yetu na unaweza kusababisha kufungwa kwa chaneli zako zote zilizopo za YouTube, chaneli zozote mpya unazofungua au kujipatia na chaneli ambapo unatajwa au kuangaziwa sana.