Sera dhidi ya maudhui hatari au ya kuumiza

Kuanzia tarehe 18 Machi 2024, sera yetu kuhusu maudhui Hatari na ya Kuumiza itasasishwa ili kujumuisha msimamo mkali zaidi kuhusu makanusho ya hadhira na mwongozo uliosasishwa ili kutathmini vyema hatari ya madhara yanayoweza kutokana na kitendo husika.
YouTube hairuhusu maudhui yanayohimiza shughuli hatari au zinazokiuka sheria ambazo zinaweza kusababisha majeraha mabaya ya mwili au kifo.
 
Ikiwa utapata maudhui yanayokiuka sera hii, yaripoti

 

Ruka uende kwenye kifungu maalum cha makala haya:

Muhimu: Sera hii hutumika kwa video, maelezo ya video, maoni, mitiririko mubashara na bidhaa au vipengele vingine vyovyote kwenye YouTube. Sera hizi pia zinatumika kwenye viungo vya nje vilivyo katika maudhui yako. Viungo hivyo vinaweza kujumuisha URL za kubofya, kuwaelekeza watumiaji kwenye tovuti nyinginezo katika video kwa kutamka, pamoja na njia nyinginezo.

Sera dhidi ya maudhui hatari au ya kuumiza

Jinsi sera hii inavyokuathiri

Kumbuka: Orodha iliyo hapa chini haijakamilika. Ikiwa unafikiri kuwa maudhui yako yanaweza kukiuka sera hii, usiyachapishe.
Maudhui haya hayaruhusiwi kwenye YouTube:

Vitendo hatari au vyenye kuumiza, mashindano na mizaha

  • Mashindano ya hatari zaidi: Mashindano ya hatari yanayoweza kusababisha majeraha ya mwili.
  • Mizaha ya hatari au ya kutisha: Mizaha inayowafanya waathiriwa wahofie kuwa wapo katika hatari kubwa ya kimwili au inayosababisha mfadhaiko wa kihisia kwa watoto.
  • Vitendo vya hatari au vyenye kuumiza: Vitendo vinavyofanywa na watu wazima ambavyo vina uwezekano wa kusababisha madhara makubwa au kifo.
  • Watoto wakishiriki katika shughuli za hatari: Maudhui yanayohatarisha hali ya watoto kihisia na kimwili. Ili upate maelezo zaidi, soma Sera yetu ya usalama wa mtoto.

Maudhui ya silaha

  • Maagizo ya kuua au kudhuru: Maagizo yanayoonyesha au kuwaeleza watazamaji jinsi ya kutekeleza shughuli zinazolenga kuwaua au kuwadhuru wengine kwa kiasi kikubwa.
  • Vilipuzi: Kutoa maagizo ya kutengeneza vifaa vya vilipuzi au misombo inayolenga kuwajeruhi au kuwaua wengine.
  • Bunduki: Ili upate maelezo zaidi, soma Sera yetu ya bunduki.

Maudhui ya usalama wa kidijitali

  • Maagizo ya wizi: Video za maagizo ya wizi zilizochapishwa kwa nia ya moja kwa moja ya kuiba bidhaa halisi au kupata kitu bila malipo.
  • Udukuzi: Kuonyesha jinsi ya kutumia kompyuta au teknolojia ya habari kwa nia ya kuiba vitambulisho, kuhatarisha data binafsi au kusababisha madhara makubwa kwa watu wengine.
  • Kukwepa kulipia maudhui au huduma dijitali: Maudhui yanayoonyesha watazamaji jinsi ya kufikia maudhui, programu au huduma bila idhini ambazo kwa kawaida huhitaji malipo.
  • Wizi wa data binafsi: Maudhui yanayojaribu kupata au kutoa maagizo ya jinsi ya kupata taarifa isiyo ya umma inayomtambulisha mtu kutoka kwa watazamaji kwa kuwadanganya.
    • Wizi wa data binafsi unaotokana na sarafu ya dijitali: Maombi ya maelezo ya pochi ya sarafu ya dijitali au inayohusiana na sarafu ya dijitali kama sehemu ya mpango wa wizi wa data binafsi.

Bidhaa au huduma haramu au zilizodhibitiwa

Mifano ya maudhui hatari au ya kuumiza

Ifuatayo ni baadhi ya mifano ya maudhui hatari au ya kuumiza isiyoruhusiwa kwenye YouTube. 

Kumbuka: Orodha iliyo hapa chini haijakamilika.

Mashindano ya hatari zaidi

  • Hali ya kushindwa kupumua: Shughuli yoyote inayozuia kupumua au inayoweza kumsababishia mtu ashindwe kupumua. Mifano ni pamoja na:
    • Michezo ya kukabana, kuzamishana au kujining'iniza
    • Ulaji wa vitu visivyolika
  • Matumizi mabaya ya silaha:: Kutumia silaha kama vile bunduki au visu, bila kuchukua tahadhari za usalama zinazofaa au kwa njia inayoweza kusababisha majeraha ya mwili. Mifano inajumuisha shindano la "No Lackin'".
  • Kula vitu hatari: Kula, kutumia au kuingiza vitu visivyolika au kemikali zinazoweza kusababisha ugonjwa au kuuathiri mwili kwa sumu. Mifano inajumuisha mashindano ya ulaji wa sabuni.
  • Kuungua, kugandisha na shoti za umeme: Shughuli zinazoweza kusababisha vidonda vinavyotokana na kuungua sana, kuganda, baridi kali au kupigwa shoti ya umeme. Mifano inajumuisha shindano la moto na la maji ya moto.
  • Kujihasiri na majeraha yanayotokana na kujigonga kwenye kitu butu: Mifano inajumuisha:
    • Kujihasiri
    • Kujiepusha na kanuni za kawaida za kiafya
    • Kuanguka, kudungwa, ajali, majeraha yanayotokana na kujigonga kwenye kitu butu au kupondwa

Kumbuka: Tunaweza kuweka mipaka ya umri kwenye maudhui ambayo yana muktadha wa kielimu au hali halisi.

Mizaha ya hatari au ya kutisha

  • Majeraha ya mwili ya kukusudia: Kuwadhuru waathiriwa wa mizaha. Mifano ni pamoja na:
    • Mashambulizi ya urushaji ngumi
    • Kuweka dawa kwenye chakula zinazosababisha kuhara
    • Mizaha ya kupigwa shoti ya umeme
  • Kumfanya mtu ajihisi kama vile yuko katika hali hatarishi:: Kuwalaghai watu waamini wapo katika hatari halisi, hata ikiwa hawajapata majeraha ya mwili. Mifano ni pamoja na:
    • Vitisho kwa kutumia silaha
    • Vitisho vya mabomu
    • Kuzipigia huduma za dharura (911) simu za uongo ili watume polisi
    • Uvamizi wa nyumbani au ujambazi bandia
    • Utekaji nyara bandia
  • Mfadhaiko wa kihisia kwa watoto au watu ambao wapo hatarini: Mzaha wowote unaosababisha mfadhaiko wa kihisia au tishio kwa usalama wa mwili, kwa watoto au watu wengine waliopo hatarini. Mifano ni pamoja na:
    • Vifo au matukio bandia ya kujiua
    • Vurugu bandia
    • Uigizaji ambao mzazi au mlezi atamtenga mtoto
    • Kuonyesha video ambazo mzazi au mlezi anamfedhehesha mtoto au anatamka maneno mabaya kwa mtoto

Kumbuka: Tunaweza kuweka mipaka ya umri kwenye maudhui ya mzaha yanayojumuisha watu wazima na ambayo hayakiuki sera zetu.

Matendo ya hatari au ya kuumiza

  • Kufanya vitendo vinavyoweza kusababisha madhara makubwa au kifo: Tabia inayoonyesha watu wazima wakifanya vitendo vinavyoweza kusababisha madhara makubwa ya mwili au kifo, hasa ikiwa mtu anayetazama anaweza kuiga kitendo hatari au ikiwa maudhui yanahimiza au kusifu kitendo hatari. Vitendo hatari vinajumuisha, lakini si tu kitendo chochote kwenye aina zilizoorodheshwa kwenye Mashindano Hatari Zaidi hapo juu, kama vile hali ya kushindwa kupumua au kupigwa shoti ya umeme.
    • Pia, haturuhusu maudhui yanayoonyesha vitendo hatari vya watoto. Hii inajumuisha maudhui yanayoonyesha watoto:
      • Wakinywa pombe
      • Wakitumia vivukisho, sigara za kielektroniki, tumbaku au marijuana
      • Wakitumia vibaya fataki
      • Wakitumia bunduki bila kudhibitiwa
  • Uendeshaji wa gari kwa hatari sana: Kutumia gari katika njia inayoleta hatari ya kujeruhiwa vibaya au kifo kwa dereva au watu wengine. Mifano ni pamoja na:
    • Video ya simu ya mkononi inayoonyesha mwendeshaji wa pikipiki akiingia upande wa magari yanayotoka upande mwingine kwa mwendo wa kasi. Masimulizi yanasikika yakisema "Lo, hiyo ilikuwa bomba!"
    • Kuendesha gari kwa mwendo wa kasi kando ya njia ya wanaotembea kwa miguu.

Maagizo ya kudhuru

  • Utengenezaji wa mabomu: Kuwaonyesha watazamaji jinsi ya kutengeneza mabomu kwa lengo la kuwajeruhi au kuwaua wengine. Mifano ni pamoja na:
    • Mabomu ya paipu
    • Kifurushi cha mabomu kinachotumwa kwa mtu mahususi
    • Vifaa vya kujilipua
    • Kokteli ya molotov
  • Vurugu zinazohusisha watoto:: Mapigano au vurugu zozote halisi kati ya watoto. Ili upate maelezo zaidi, soma sera yetu ya Usalama wa Mtoto.

Kumbuka: Tunaweza kuweka mipaka ya umri kwenye maudhui ambayo yana muktadha wa hali halisi au kielimu.

Maudhui yenye mipaka ya umri

Kumbuka: Orodha iliyo hapa chini haijakamilika.
Wakati mwingine maudhui hayakiuki sera zetu, lakini huenda hayafai kwa watazamaji walio na umri wa chini ya miaka 18.
Huenda tukadhibiti badala ya kuondoa ikiwa maudhui yanayoonyesha kitendo hatari yanatimiza kigezo kimoja au vigezo zaidi kati ya vifuatavyo:
  • Kuna muktadha wa kielimu, kihalisia, kisayansi au kisanii, kama vile kutoa taarifa kuhusu hatari za kitendo husika. Kwa mfano, hali hii inaweza kujumuisha muktadha unaoeleza aina za majeraha yanayoweza kutokea kwa sababu ya kufanya kitendo hatari au kueleza jinsi ulivyoumia kutokana na kitendo hatari. Inaweza pia kujumuisha muktadha unaoeleza aina za tahadhari za usalama au mafunzo yanayohitajika ili kufanya kitendo husika kwa usalama na kuepusha majeraha. Kusema, “Usijaribu hili ukiwa nyumbani” si muktadha wa kutosha.
  • Kitendo kilichoonyeshwa hakiwezi kusababisha majeraha mabaya.
  • Maudhui hayatangazi kitendo kilichoonyeshwa. Utangazaji unajumuisha aina yoyote ya kuhimiza au kusifu kitendo au kutoa maagizo ya jinsi ya kutenda kitendo.

Pata maelezo kuhusu maudhui yenye mipaka ya umri na jinsi ya kutazama video zenye mipaka ya umri.

Mifano ya maudhui yenye mipaka ya umri

  • Maudhui ya mzaha yanayoangazia watu wazima wanaotumia damu bandia nyingi au majareha bandia yanayoogofya.
  • Kuonyesha video ya watu wakishiriki kwenye shindano hatari ikiwa na maoni yanayoelezea idadi ya watu waliojeruhiwa vibaya kutokana na shindano husika.
  • Maudhui yanayoonyesha watu wazima wakitumia vibaya fataki.
  • Maudhui yanayoonyesha watu wazima wakitumia vifaa vya kushtua kwa umeme kwa washiriki walio radhi au wao wenyewe.
  • Maudhui yanayoonyesha mwanariadha anayecheza mchezo wa parkour akitoa maoni kuhusu video za vitendo hatari zaidi vya wanariadha chipukizi na akitoa maoni kuhusu uwezekano wa madhara.

Maudhui ya kielimu, hali halisi, kisayansi au kisanaa

Wakati mwingine, maudhui ambayo huenda yanakiuka sera hii yanaruhusiwa kusalia kwenye YouTube ikiwa yana muktadha wa Kielimu, Hali halisi, Kisayansi au Kisanaa (EDSA). Pata maelezo kuhusu jinsi YouTube inavyotathmini maudhui yenye muktadha wa EDSA.

Kumbuka: Katika hali fulani, maudhui yenye muktadha wa EDSA yanaweza kuwekewa mipaka ya umri. Maudhui fulani hayaruhusiwi kwenye YouTube hata ikiwa yamewekewa muktadha wa EDSA, kama vile maudhui yanayouza dawa za kulevya au dawa zinazodhibitiwa bila maagizo ya daktari.

Mifano ya maudhui yenye muktadha wa EDSA

  • Kipande cha habari kuhusu hatari za michezo ya kukabana kinaweza kufaa, lakini kuchapisha video nje ya muktadha kutoka kwenye makala sawa si sahihi.
  • Video ambayo mtaalamu wa madahiro anafanya kitendo hatari cha kurusha pikipiki inayoonyesha watazamaji tahadhari za usalama zinazochukuliwa katika maandalizi, kama vile wafanyakazi wa matibabu ya dharura waliopo na matumizi ya vifaa vya kujilinda.
  • Makala ya hali halisi yanayoonyesha athari ya matumizi ya dawa za kulevya katika jumuiya fulani ambayo, japo yanaonyesha watumiaji matumizi ya dawa za kulevya, yanawakatisha tamaa watazamaji kutumia dawa za kulevya na hayatoi maelezo kuhusu jinsi ya kuyanunua.
  • Video inayoonyesha uendeshaji wa hatari au ajali za magari katika mazingira yanayodhibitiwa ili kuwaelimisha watazamaji kuhusu mbinu bora za uendeshaji salama au vipengele vya usalama wa gari.

Kitakachofanyika iwapo maudhui yanakiuka sera hii

Iwapo maudhui yako yanakiuka sera hii, tutaondoa maudhui hayo na kukutumia barua pepe ili kukufahamisha. Ikiwa hatuwezi kuthibitisha kuwa kiungo ulichochapisha ni salama, huenda tukakiondoa. Kumbuka kuwa URL zinazokiuka sera zinazochapishwa kwenye video husika au katika metadata ya video zinaweza kusababisha tuondoe video husika.

Ikiwa hii ni mara yako ya kwanza kukiuka Mwongozo wetu wa Jumuiya, huenda ukapewa tahadhari bila adhabu kwenye chaneli yako. Utakuwa na fursa ya kushiriki katika mafunzo ya sera ili kuruhusu muda wa tahadhari uliopewa uishe baada ya siku 90. Hata hivyo, ikiwa utakiuka sera hiyo tena ndani ya kipindi hicho cha siku 90, muda wa tahadhari hautaisha na chaneli yako itapewa onyo. Ukikiuka sera tofauti baada ya kukamilisha mafunzo, utapewa tahadhari nyingine.

Ikiwa utapokea maonyo 3 katika kipindi cha siku 90, chaneli yako itasimamishwa. Pata maelezo zaidi kuhusu mfumo wetu wa maonyo.

Tunaweza kusimamisha chaneli au akaunti yako kwa ukiukaji wa mara kwa mara wa Mwongozo wa Jumuiya au Sheria na Masharti. Tunaweza pia kusimamisha chaneli au akaunti yako baada ya tukio moja la ukiukaji kwa kiasi kikubwa au chaneli ikikiuka sera mara kwa mara. Huenda tukazuia watu wanaorudia kufanya makosa wasishiriki katika mafunzo ya sera siku zijazo. Pata maelezo zaidi kuhusu kufungwa kwa chaneli au akaunti.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
5514897630728695745
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false