Hakimiliki ni nini?

Katika nchi nyingi, mtu anapotayarisha kazi halisi ambayo ni maudhui halisi yaliyotayarishwa na kuhifadhiwa kwenye kifaa halisi, anakuwa mwenye hakimiliki ya kazi hiyo kiotomatiki. Kama mwenye hakimiliki, ana haki maalum ya kutumia kazi hiyo. Mara nyingi, ni mwenye hakimiliki pekee anayeweza kuamua iwapo mtu mwingine ana ruhusa ya kutumia kazi hiyo. 

Ni aina zipi za kazi ambazo husimamiwa na hakimiliki?
  • Kazi za sauti na video, kama vile vipindi vya televisheni, filamu na video za mtandaoni
  • Tungo za muziki na rekodi za sauti
  • Kazi za uandishi, kama vile mihadhara, makala, vitabu na tungo za muziki
  • Kazi za picha, kama vile upakaji rangi, mabango na matangazo
  • Michezo ya video na programu ya kompyuta
  • Kazi za maigizo, kama vile michezo ya kuigiza na filamu za uimbaji

Mawazo, mambo ya kweli na michakato hayasimamiwi na hakimiliki. Kulingana na sheria ya hakimiliki, ili kustahiki kulindwa kwa hakimiliki, ni lazima kazi iwe ya ubunifu na lazima iwe maudhui halisi yaliyotayarishwa na kuhifadhiwa kwenye kifaa kinachoshikika. Majina na mada kivyake hazisimamiwi na hakimiliki.

Je, ninaweza kutumia kazi inayolindwa kwa hakimiliki bila ukiukaji?

Unaweza kutumia maudhui yanayolindwa kwa hakimiliki bila ukiukaji, kama vile katika hali zisizofuata kanuni za hakimiliki, kama vile matumizi ya haki na matumizi yasiyo ya biashara, au kwa kupata ruhusa ya kutumia maudhui ya mtu mwingine.

Ikiwa unafikiria kutumia muziki wa mtu mwingine kwenye video yako, pata maelezo zaidi kuhusu chaguo zako za kutumia muziki:

Machaguo ya kutumia muziki katika video zako

 

Pia, baadhi ya watayarishi wa maudhui huchagua kufanya kazi zao zipatikane ili zitumike tena na kuweka masharti fulani yanayoitwa leseni ya Creative Commons.

Je, YouTube inaweza kubaini ni nani mwenye hakimiliki?

Hapana. YouTube haiwezi kufanya upatanisho wa mizozo ya hakimiliki. Tunapopokea ombi kamili na sahihi la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki, tunaondoa maudhui hayo kwa mujibu wa sheria. Tunapopokea arifa sahihi ya kukanusha, tunaisambaza kwa mtu aliyetuma ombi la kuondoa maudhui. Baada ya hapo, ni jukumu la wahusika kutatua suala hilo mahakamani.

Je, hakimiliki ni sawa na chapa ya biashara?

Hapana. Hakimiliki ni aina moja tu ya mali ya uvumbuzi. Si sawa na chapa ya biashara, ambayo hulinda jina, kauli mbiu, nembo na vitambulishi vingine vya chanzo dhidi ya kutumiwa na watu wengine kwa madhumuni fulani. Hakimiliki pia ni tofauti na sheria ya hataza, ambayo hulinda kazi za uvumbuzi.

YouTube hutoa mchakato tofauti wa kuondoa video zinazokiuka sheria za chapa ya biashara au sheria nyingine.

Je, kuna tofauti gani kati ya hakimiliki na faragha?

Kwa sababu tu umeonekana kwenye video, picha au rekodi ya sauti haimaanishi kuwa wewe ni mwenye hakimiliki ya maudhui hayo. Kwa mfano, ikiwa rafiki yako alirekodi mazungumzo kati yenu, yeye ndiye anapaswa kuwa mwenye hakimiliki ya rekodi hiyo ya video. Maneno mnayosema nyinyi wawili hayasimamiwi na hakimiliki 'kando' bila video yenyewe, isipokuwa ikiwa yaliwekwa mapema.

Ikiwa rafiki yako au mtu mwingine alipakia video, picha au rekodi ambamo umo bila ruhusa yako na unahisi kuwa kitendo hicho kinakiuka faragha au usalama wako, unaweza kuzingatia kutuma malalamiko kuhusu faragha.

Dhana potofu za kawaida kuhusu hakimiliki

Zifuatazo ni baadhi ya dhana potofu za kawaida kuhusu hakimiliki na jinsi inavyofanya kazi kwenye YouTube. Kumbuka kwamba kufanya chochote kati ya yafuatayo hakutalinda maudhui yako dhidi ya maombi ya kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki au madai ya Content ID:

Dhana potofu ya 1: Kumtaja mwenye hakimiliki kunamaanisha kuwa unaweza kutumia maudhui yake

Kumtaja mwenye hakimiliki hakukupatii haki ya kiotomatiki ya kutumia kazi yake iliyo na hakimiliki. Unapaswa kuhakikisha kuwa umepata haki zote zinazohitajika za vipengele vyote vinavyolindwa kwa hakimiliki kwenye video yako kabla ya kuipakia kwenye YouTube.

Ikiwa unaamini kuwa matumizi yako ya maudhui yanayolindwa kwa hakimiliki yastahiki kutofuata kanuni za hakimiliki, kama vile matumizi ya haki au matumizi yasiyo ya biashara, kumbuka kwamba, hata ikiwa utaweka maudhui halisi kwenye kazi ya mtu yenye hakimiliki, huenda video yako isistahiki kutofuata kanuni za hakimiliki. Hakikisha kuwa umetathmini kwa makini maudhui yako na upate ushauri wa kisheria ikihitajika, kabla ya kupakia.

Dhana potofu ya 2: Kudai kuwa “si ya faida” inamaanisha unaweza kutumia maudhui yoyote

Kutojaribu kuchuma pesa kutokana na kazi inayolindwa kwa hakimiliki hakuzuii madai ya hakimiliki. Ukibainisha tu kuwa maudhui uliyopakia ni “ya madhumuni ya burudani pekee” au “si ya faida,” kwa mfano, haitoshi kivyake.

Kuhusiana na hali zisizofuata kanuni za hakimiliki, kama vile matumizi ya haki au matumizi yasiyo ya biashara, Mahakama itaangalia kwa makini madhumuni ya matumizi yako katika kutathmini iwapo yanastahiki kutofuata kanuni za hakimiliki. Kwa mfano, matumizi “yasiyo ya faida” hupendelewa katika uchanganuzi wa matumizi ya haki, lakini hayatoshi kutumiwa kujitetea kivyake.

Dhana potofu ya 3: Watayarishi wengine wanafanya hivyo, kwa hivyo nawe pia unaweza kufanya vile vile

Hata kama kuna video kwenye tovuti ambazo zinaonekana kufanana na ile uliyopakia, haimaanishi kuwa pia wewe una haki ya kuchapisha maudhui hayo.

Wakati mwingine, mwenye hakimiliki huidhinisha baadhi lakini si kazi zake zote ili zionekane kwenye tovuti yetu. Wakati mwingine, video zinazofanana sana na hizo humilikiwa na wenye hakimiliki tofauti. Wengine wanaweza kutoa ruhusa na wengine wakatae.

Dhana potofu ya 4: Unaweza kutumia maudhui uliyonunua kwenye iTunes, CD au DVD

Kununua maudhui hakumaanishi kwamba unamiliki haki za kupakia maudhui hayo kwenye YouTube. Hata ukimtambua mwenye hakimiliki kwenye video au maelezo ya video, kuchapisha video zenye maudhui uliyonunua bado kunaweza kukiuka sheria ya hakimiliki.

Dhana potofu ya 5: Maudhui uliyorekodi mwenyewe kutoka kwenye televisheni, filamu au redio ni sawa

Kurekodi kitu mwenyewe hakumaanishi kuwa unamiliki haki zote za kukipakia kwenye YouTube. Ikiwa ulichorekodi kinajumuisha maudhui ya mtu mwingine yanayolindwa kwa hakimiliki, kama vile muziki wenye hakimiliki unaocheza chinichini, basi bado utahitaji kupata ruhusa kutoka kwa wenye hakimiliki.

Dhana potofu ya 6: Kusema “sikuwa na nia ya kukiuka hakimiliki”

Kauli na makanusho kama vile “haki zote ni za mtunzi,” “sina nia ya kukiuka hakimiliki” au “Similiki” hayamaanishi kuwa una ruhusa ya mwenye hakimiliki kuchapisha maudhui yake, wala kumaanisha kiotomatiki kuwa matumizi ya maudhui hayo yamestahiki kutofuata kanuni za hakimiliki, kama vile matumizi ya haki au matumizi yasiyo ya biashara.

Dhana potofu ya 7: Ni sawa kutayarisha maudhui yaliyo na hakimiliki yanayocheza kwa sekunde chache tu

Kiasi chochote cha maudhui yanayolindwa kwa hakimiliki kitakachotumiwa bila ruhusa ya wenye hakimiliki, hata kama ni ya sekunde chache tu, kinaweza kusababisha video yako kupata madai ya hakimiliki. Ikiwa unaamini kwamba matumizi yako ya maudhui yamestahiki kutofuata kanuni za hakimiliki, kama vile matumizi ya haki au matumizi yasiyo ya biashara, kumbuka kwamba ni Mahakama pekee inayoweza kubaini hali hiyo.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
10019630280665112974
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false