Muhtasari wa Mpango wa Washirika wa YouTube uliopanuliwa

Tunapanua Mpango wa Washirika wa YouTube (YPP) kwa watayarishi wengi zaidi kwa kuwapa uwezo wa kufikia mapema vipengele vya Ununuzi na ufadhili kutoka kwa mashabiki. Mpango wa Washirika wa YouTube uliopanuliwa unapatikana kwa watayarishi wanaostahiki katika nchi au maeneo haya. Ikiwa unaishi katika mojawapo ya nchi au maeneo haya, unaweza kusoma makala yaliyo hapa chini ili upate maelezo zaidi kuhusu mabadiliko kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube.  

Ikiwa huishi katika mojawapo ya nchi au maeneo ambako mpango unapatikana, hakuna mabadiliko kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube yanayokuhusu. Unaweza kusoma makala haya ili upate muhtasari wa Mpango wa Washirika wa YouTube, masharti ya kujiunga na maagizo ya kutuma ombi yanayokufaa.

Angalia iwapo unastahiki kushiriki kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube uliopanuliwa. Iwapo bado hujastahiki, chagua Pata arifa katika sehemu ya Chuma mapato ya Studio ya YouTube. Tutakutumia barua pepe tutakapokusambazia Mpango wa Washirika wa YouTube (YPP) uliopanuliwa na utakapokuwa umetimiza masharti ya upeo wa kustahiki. 

Utangulizi wa jinsi ya Kuchuma Mapato kwenye YouTube

Mwaka 2022, tulitangaza kuwa tunaimarisha Mpango wa Washirika wa YouTube (YPP) ili tuzidi kuhakikisha kuwa YouTube ni jukwaa lenye manufaa kwa watayarishi. Kuanzia katikati ya mwezi Juni 2023, tutapanua Mpango wa Washirika wa YouTube kwa watayarishi wengi zaidi kwa kuwapa uwezo wa kufikia mapema ufadhili kutoka kwa mashabiki na vipengele mahususi vya Ununuzi.

Watayarishi katika nchi zinazotimiza masharti wanaweza kutuma maombi kujiunga na Mpango uliopanuliwa wa Washirika wa YouTube wanapofikia mojawapo ya viwango vilivyo hapa chini vya kutimiza masharti:

  • Kuwa na wafuatiaji 500 pamoja na kupakia video 3 za umma zinazotimiza masharti katika kipindi cha siku 90 zilizopita na kufikisha saa 3,000 za muda ambao video zimetazamwa hadharani kwa njia inayokubalika katika miezi 12 iliyopita au
  • Kuwa na wafuatiliaji 500 pamoja na kupakia video 3 zaa umma zinazotimiza masharti katika kipindi cha siku 90 zilizopita na ufikishe mara milioni 3 za kutazamwa kwa Video Fupi hadharani kwa njia inayokubalika katika siku 90 zilizopita.

Iwapo ungependa tukuarifu unapotimiza masharti, chagua Pokea arifa katika sehemu ya Chuma mapato ya Studio ya YouTube. Tutakutumia barua pepe baada ya Mpango wa Washirika wa YouTube uliopanuliwa kukufikia na uwe umetimiza masharti ya upeo yaliyotajwa hapo juu.

Watayarishi katika Mpango wa Washirika wa YouTube ambao pia wanatimiza masharti ya upeo yaliyo hapa chini wanaweza kupata manufaa zaidi kama vile ugavi wa mapato kutoka kwenye matangazo na YouTube Premium:

  • Kuwa na wafuatiliaji 1,000 pamoja na kufikisha saa 4,000 za muda ambao video zimetazamwa hadharani kwa njia inayokubalika katika miezi 12 iliyopita au
  • Kuwa na wafuatiliaji 1,000 pamoja na kufikisha mara milioni 10 za kutazamwa kwa Video Fupi hadharani kwa njia inayokubalika katika siku 90 zilizopita.

Kwa washirika ambao tayari wamejiunga na Mpango wa Washirika wa YouTube, hakuna mabadiliko yoyote kwenye manufaa yao ya mpango.

Unachohitaji ili ujiunge na Mpango wa Washirika wa YouTube uliopanuliwa

  1. Fuata sera za uchumaji mapato wa chaneli kwenye YouTube.
  2. Kuwa na chaneli katika mojawapo ya nchi au maeneo ambako mpango unapatikana.
  3. Hakikisha kuwa umewasha Uthibitishaji wa Hatua 2 kwenye Akaunti yako ya Google.
  4. Kuwa na akaunti moja ya AdSense katika YouTube inayotumika, utakayounganisha na chaneli yako. Ikiwa huna, uwe tayari kuifungua katika Studio ya YouTube wakati wa kutuma ombi. Hakikisha kuwa umefungua akaunti mpya ya AdSense katika YouTube kwenye Studio ya YouTube pekee.

Maeneo ambako Mpango wa Washirika wa YouTube uliopanuliwa unapatikana

Mpango wa Washirika wa YouTube uliopanuliwa unapatikana kwa watayarishi waliotimiza masharti katika nchi au maeneo yafuatayo:

  • Aljeria
  • Samoa ya Marekani
  • Ajentina
  • Aruba
  • Australia
  • Austria
  • Bahareni 
  • Belarusi
  • Ubelgiji
  • Bamuda
  • Bolivia 
  • Bosnia na Hezegovina
  • Brazili
  • Bulgaria
  • Kanada
  • Visiwa vya Cayman
  • Chile
  • Kolombia
  • Kostarika
  • Korasia 
  • Kuprosi
  • Jamhuri ya Zechia
  • Denmaki 
  • Jamhuri ya Dominika 
  • Ekwado
  • Misri
  • Elsavado
  • Estonia
  • Ufini
  • Ufaransa
  • Guyana ya Ufaransa
  • Polinesia ya Ufaransa
  • Ujerumani
  • Ugiriki
  • Guadalupe
  • Guam
  • Gwatemala
  • Hong Kong
  • Hondurasi
  • Hangaria
  • Aisilandi
  • India
  • Indonesia
  • Ayalandi
  • Israeli
  • Italia
  • Japani
  • Yordani
  • Kenya
  • Kuwaiti
  • Lativia
  • Lebanoni
  • Lishenteni
  • Litwania
  • Lasembagi
  • Masedonia
  • Malesia
  • Malta
  • Moroko
  • Meksiko
  • Uholanzi
  • Nyuzilandi
  • Nikaragwa
  • Naijeria 
  • Visiwa vya Mariana Kaskazini
  • Norwe
  • Omani
  • Panama
  • Papua
  • Peru
  • Ufilipino
  • Polandi 
  • Ureno
  • Pwetoriko
  • Paragwai
  • Katari
  • Romania
  • Saudia
  • Senegali 
  • Sabia
  • Singapoo
  • Slovakia
  • Slovenia
  • Afrika Kusini
  • Korea Kusini
  • Uhispania
  • Uswidi
  • Uswizi
  • Taiwani
  • Tailandi 
  • Uturuki 
  • Turki na Kaikosi 
  • Uganda
  • Falme za Kiarabu
  • Uingereza
  • Marekani
  • Urugwai
  • Visiwa vya Virgin vya Marekani
  • Vietnamu

Mahali pa kutuma ombi la kujiunga na Mpango wa Washirika wa YouTube uliopanuliwa

Baada ya kupata unachohitaji na chaneli yako inatimiza masharti ya kutuma ombi, jisajili katika Mpango wa Washirika wa YouTube kwenye kompyuta au kifaa cha mkononi:

  1. Tumia kompyuta ili uingie katika akaunti kwenye Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, bofya Chuma mapato.
  3. Bofya Tuma Ombi Sasa ili ukague na Ukubali masharti ya msingi.
  4. Bofya Anza ili ufungue akaunti ya AdSense katika YouTube au uunganishe akaunti iliyopo inayotumika.

Ukimaliza, utaona hali ya Inaendelea kwenye hatua ya Kufanyiwa Ukaguzi, ikimaanisha kuwa tumepokea ombi lako!

Tunachokagua

Mifumo yetu ya kiotomatiki na wataalamu watakagua chaneli yako kwa ujumla ili kuhakikisha kuwa chaneli yako inafuata mwongozo na sera zetu zote. Angalia tena kwenye sehemu ya Chuma mapato ya Studio ya YouTube wakati wowote ili uone hali ya ombi lako.

Maombi yote ya Mpango wa Washirika wa YouTube hushughulikiwa kulingana na tulivyoyapokea. Tutawasiliana nawe tukufahamishe kuhusu uamuzi baada ya chaneli yako kukaguliwa (kwa kawaida huwa ndani ya takribani mwezi 1).
 
Kumbuka kuwa kunaweza kutokea uchelewaji kutokana na:
  • Idadi ya maombi
  • Hitilafu za mfumo
  • Vikwazo vya nyenzo
  • Chaneli zinazohitaji kufanyiwa ukaguzi mara kadhaa, hasa wakati wakaguzi mbalimbali wana maoni tofauti kuhusu ufaafu wa chaneli wa kujiunga na Mpango wa Washirika wa YouTube

Iwapo ombi lako la kwanza halikufanikiwa, usijali, endelea kupakia maudhui halisi na unaweza kujaribu tena baada ya kipindi cha siku 30. Iwapo hili si ombi lako la kwanza kukataliwa, unaweza kujaribu tena baada ya kipindi cha siku 90. Huenda wakaguzi wetu waligundua kuwa sehemu kubwa ya chaneli yako haifuati sera na mwongozo wetu kwa sasa. Kwa hivyo, hakikisha umekagua sera na mwongozo wetu ukilinganisha na maudhui ya jumla ya chaneli yako kisha urekebishe chaneli yako kabla ya kutuma ombi tena. Pata maelezo zaidi kuhusu hatua unazoweza kuchukua ili uimarishe chaneli yako kwa ajili ya wakati mwingine.

Kuchagua jinsi ya kuchuma mapato na kupokea malipo

Baada ya kujiunga na Mpango wa Washirika wa YouTube, unaweza kuanza kuchuma mapato kupitia vipengele vya ufadhili kutoka kwa mashabiki na Ununuzi. Ili uwashe vipengele vya ufadhili kutoka kwa mashabiki na Ununuzi, kagua na ukubali masharti ya Sehemu ya Bidhaa za Biashara. Pata maelezo zaidi kuhusu sehemu hiyo na jinsi ya kuwasha vipengele vya ufadhili kutoka kwa mashabiki na Ununuzi.

Vipengele vya ufadhili kutoka kwa mashabiki na Ununuzi

Ukijiunga na Mpango wa Washirika wa YouTube ukiwa na wafuatiliaji 500 katika chaneli yako, unaweza kuchuma mapato kupitia vipengele vifuatavyo vya uchumaji wa mapato ikiwa unatimiza masharti ya kuvitumia:

  • Uanachama katika chaneli: huwawezesha watazamaji kujiunga na chaneli yako kupitia malipo ya kila mwezi na kupata manufaa ya wanachama pekee unayotoa, kama vile beji, emoji na bidhaa nyinginezo.
  • Super Chat na Super Stickers: mashabiki wanaweza kununua Super Chat ili waangazie ujumbe wao ndani ya gumzo la moja kwa moja au Super Stickers ili wapate picha nzuri ya uhuishaji inayoonekana katika gumzo la moja kwa moja.
  • Shukrani Moto:  hukuwezesha kuchuma mapato kutoka kwa watazamaji wanaotaka kuonyesha shukrani za ziada kutokana na video zako.
  • Ununuzi: hukuwezesha kuunganisha duka lako rasmi la bidhaa kwenye YouTube na kuangazia bidhaa zako.

Kupokea malipo

Nenda kwenye sehemu ya "Pokea malipo" ya Kituo chetu cha Usaidizi ili:

  • Ufahamu kwa urahisi zaidi kuhusu mapato yako ukiwa mshirika wa YouTube
  • Upate maelezo zaidi kuhusu AdSense katika YouTube (mpango wa Google unaowaruhusu watayarishi katika Mpango wa Washirika wa YouTube kulipwa)
  • Ufahamu jinsi ya kutatua matatizo ya kawaida ya malipo

Endelea kutumia chaneli yako ili uendelee kuchuma mapato

Kwa vile Mpango wa Washirika wa YouTube unaendelea kukua, ni muhimu kudumisha mfumo wa chaneli zenye shughuli. Tunaweza kuzima uchumaji wa mapato kwenye chaneli ambazo hazijapakia video au kuchapisha kwenye kichupo cha Jumuiya kwa kipindi cha miezi 6 au zaidi.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
15833046267820597231
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false