Muhtasari na masharti ya kujiunga na mpango wa washirika wa Ununuzi kwenye YouTube

Mpango wa Washirika wa Ununuzi kwenye YouTube 🛍️

Mpango wa washirika wa Ununuzi kwenye YouTube hukupatia njia ya kuchuma mapato kwenye YouTube huku ukiisaidia hadhira yako kupata bidhaa wanazopenda. Kupitia mpango huu unaweza:

  • Kusaidia mashabiki wako kufanya ununuzi: Unapowekea bidhaa lebo katika maudhui yako, mashabiki wanaweza kuangalia kwa haraka maelezo muhimu kama vile bei na waendelee kutazama video yako huku wakilipia kwenye tovuti ya muuzaji wa rejareja.
  • Kunufaika zaidi kutokana na biashara yako kwenye YouTube: Mpango wa washirika unasaidia kuonyesha maudhui yako bora ya ununuzi kwa chapa na watazamaji zaidi kote kwenye YouTube -- hali inayofanya uwezekano wa mapato yako ya jumla kuongezeka ukitumia YouTube. Pia, utapata asilimia nzuri ya faida mashabiki wanaponunua.
  • Kutumia muda zaidi kutayarisha maudhui: Kwa kuwa unaweza kuwekea bidhaa lebo, kupata maarifa na kukagua mapato kwenye Studio ya YouTube, unaweza kutumia muda zaidi kutayarisha maudhui ambayo watu wanapenda na muda mchache kudhibiti viungo.
Kumbuka: Kwa sasa, mpango huu unapatikana tu kwa watayarishi walioko Marekani ambao wametimiza masharti. Ikiwa ungependa kutuma ombi la kujiunga mapema au kupendekeza chapa mahususi, tafadhali jaza fomu hii. Kujaza fomu hakuhakikishi mwaliko.

Mpango wa washirika wa Ununuzi kwenye YouTube

Masharti ya kujiunga

Ili ualikwe kwenye mpango, ni lazima utimize masharti haya ya msingi ya kujiunga:

  • Chaneli yako iwe katika Mpango wa Washirika wa YouTube
  • Ni lazima chaneli yako iwe na zaidi ya wafuatiliaji 15,000
  • Uwe unaishi Marekani
  • Chaneli yako si chaneli ya muziki, Chaneli Rasmi ya Msanii au inayohusishwa na washirika wa muziki. Washirika wa muziki wanaweza kujumuisha lebo za muziki, wasambazaji, wachapishaji au VEVO.
  • Mipangilio ya hadhira ya chaneli yako haijawekwa kuwa Inalenga Watoto na chaneli yako haina idadi kubwa ya video zilizobainishwa kuwa zinalenga watoto
  • Chaneli yako haina maonyo yoyote kwa kukiuka Mwongozo wa Jumuiya ambayo hayajashughulikiwa

Jinsi ya kujiunga

Ukishatimiza masharti ya kujiunga na mpango, unaweza kujisajili kwenye Studio ya YouTube.

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Katika menyu ya kushoto, chagua Chuma mapato.
  3. Katika Mipango, bofya Jiunge Sasa.
  4. Kagua na ukubali Sheria na Masharti ya Mpango wa Washirika wa Ununuzi kwenye YouTube.
  5. Umejiunga! Unaweza kuanza kuwekea bidhaa lebo katika maudhui yako. Hakikisha unafuata mwongozo wa kuweka lebo.

Wauzaji washirika na ofa

Ukishakuwa sehemu ya mpango, unaweza kuweka lebo kwenye orodha inayokua ya wauzaji wanaoshiriki na uone asilimia za mgawo wa faida wanazotoa. Unaweza kujiunga kwa kuomba sampuli za bidhaa bila malipo, kuangalia bidhaa zinazouzwa na kupokea asilimia za juu zaidi za faida kutoka kwa wauzaji. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuwekea bidhaa lebo kwenye maudhui yako

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube. 
  2. Kwenye menyu ya kushoto, bofya Chuma Mapatokisha Ununuzi kisha Gundua ofa za washirika

  3. Chini ya “Jiunge ili uzipate,” unaweza kubofya Asilimia ya Faida, Ofa au Sampuli

  • Kumbuka: Unaweza kubofya muuzaji ili upate maelezo zaidi. Unaweza pia kupanga wauzaji kialfabeti au kulingana na kiwango cha juu zaidi cha asilimia ya mgawo wa faida wanazotoa.

Orodha za wauzaji washirika

Ukishakuwa sehemu ya mpango, unaweza kuanza kuwekea lebo bidhaa zilizo katika orodha yetu inayokua ya wauzaji inayojumuisha:

Kuelewa mapato yako

Kila chapa na muuzaji wa rejareja anayeshiriki ataweka viwango vyake vya asilimia ya faida na kipindi cha ununuzi kwa kila bidhaa. Asilimia za faida zitaonyeshwa kulingana na kila ofa ya bidhaa. Utalipwa asilimia inayoonyeshwa. Utapata asilimia ya faida mtazamaji akibofya bidhaa uliyoiwekea lebo na kufanya ununuzi. Unaweza kutumia Takwimu za YouTube ili uangalie mapato yako ya YouTube.

Kumbuka: Asilimia ya faida uliyopata italipwa kupitia AdSense katika YouTube ndani ya siku 60 hadi 120 baada ya ununuzi ili kushughulikia urejeshaji bidhaa unaofanywa na mteja. Ikiwa mteja atarejesha bidhaa, asilimia ya faida itatenduliwa.

Kulipia bidhaa zitangazwe katika maudhui, udhamini na maudhui yaliyoidhinishwa

Ukijumuisha bidhaa zinazolipiwa ili zitangazwe katika maudhui, maudhui yaliyoidhinishwa, udhamini au maudhui mengineyo yanayohitaji ufumbuzi kwa watazamaji katika video zako, unatakiwa kufuata sera za YouTube zinazohusu kulipia bidhaa ili zitangazwe katika maudhui. Tafadhali rejelea makala haya ili upate maelezo zaidi.

Kutatua matatizo ya kujisajili

Zifuatazo ni baadhi ya mbinu za kawaida za kutatua hitilafu unazoweza kukumbana nazo wakati wa kujisajili:

  • Huenda chaneli yako haijatimiza masharti. Soma masharti ya kujiunga yaliyo hapo juu ili uthibitishe ikiwa chaneli yako imetimiza masharti.
  • Ikiwa chaneli yako inasimamiwa na mmiliki wa maudhui, ni lazima mmiliki huyo wa maudhui akubali makubaliano kwa niaba yako.
  • Huenda umeingia katika Chaneli ya YouTube isiyo sahihi. Badilisha ili utumie chaneli unayoamini imetimiza masharti kisha ujaribu tena.

Kumbuka: Baada ya kuthibitisha kuwa tatizo lako halipo kati ya mojawapo ya hali zilizo hapo juu, wasiliana na Kituo cha Usaidizi kwa Watayarishi ili upate usaidizi zaidi.

Mbinu bora na nyenzo

Ili unufaike zaidi na mpango wa washirika kuanzia mwanzo, tunapendekeza:

  • Ujumuishe mapunguzo na matangazo ya bidhaa maarufu: Angalia ikiwa bidhaa unayotaka kujumuisha inapatikana kwa asilimia ya faida na upange maudhui yako kwa kuzingatia mapunguzo na matangazo yanayokufaa zaidi. 
  • Wekea lebo bidhaa zinazofaa na utumie mwito wa kuchukua hatua ili uongeze mauzo: Uwekee maudhui yako lebo ukitumia bidhaa zilizojumuishwa ndani ya video au Video yako fupi na utumie mwito wa kuchukua hatua ili uifahamishe hadhira yako kuwa inaweza kununua.
    • Tumia kipengele cha Kuweka Lebo katika Bidhaa Nyingi ili uwekee bidhaa lebo kwenye video zote kwa pamoja: Katika sehemu ya Chuma mapato ya Studio ya YouTube, nenda kwenye kichupo cha Ununuzi and then Wekea Bidhaa Lebo  and then Kagua video zilizo na mapendekezo ya bidhaa za kuwekea lebo, zinazopatikana kwenye maelezo ya video.
      • Ili uweke lebo kwenye bidhaa fulani, bofya picha ya bidhaa and then bofya WEKEA LEBO karibu na bidhaa husika au WEKEA ZOTE LEBO kwa bidhaa zote.
      • Ili uwekee bidhaa lebo kwenye video moja au zaidi, chagua video husika au uchague video zote and then WEKEA LEBO.
  • Pata hamasa kutoka kwa watayarishi na chapa: Angalia maudhui ya washirika kutoka kwa watayarishi wa YouTube ili upate hamasa ya kutayarisha maudhui.

Mwongozo wa Mtayarishi Kuanzia

Kifurushi chenye nyenzo muhimu kilichojaa nyenzo kama vile vidokezo vya kuweka mipangilio, mbinu bora na vibandiko vya kuburudisha vya kuweka kwenye maudhui yako.

Orodha ya video ya mtayarishi mshirika

Pata hamasa hapa kutoka kwa watayarishi wengine kwa kuangalia maudhui yao ya washirika kwenye YouTube!

Bonasi ya utendaji ya washirika wa Ununuzi kwenye YouTube

Kumbuka: Bonasi ya utendaji ya washirika wa Ununuzi kwenye YouTube ilikamilika 2023.

Bonasi ya utendaji ya washirika wa Ununuzi kwenye YouTube huwapa watayarishi wanaotimiza masharti fursa ya kipekee ya kuongeza mapato kwa kuziwekea bidhaa lebo kwenye maudhui yako. Unaweza kupata bonasi kulingana na jumla ya mauzo ya bidhaa ulizoziwekea lebo kati ya tarehe 27 Oktoba hadi 30 Novemba na tarehe 1 Desemba hadi 31 Desemba, 2023. Bonasi hii haichukui nafasi ya marupurupu yanayoendelea ya chapa na muuzaji wa rejareja na ni pamoja na asilimia ya faida iliyopatikana kutokana na mauzo.

Ni lazima watayarishi waliotimiza masharti wakidhi viwango vifuatavyo vya mauzo ili wapate bonasi moja kwa mwezi (kiasi kwa USD):

  • Bonasi ya $30 kwa kuongeza mauzo ya $300 katika jumla ya mauzo ya bidhaa
  • Bonasi ya $120 kwa kuongeza mauzo ya $1,000 katika jumla ya mauzo ya bidhaa
  • Bonasi ya $750 kwa kuongeza mauzo ya $5,000 katika jumla ya mauzo ya bidhaa
  • Bonasi ya $3,000 kwa kuongeza mauzo ya zaidi ya $15,000 katika jumla ya mauzo ya bidhaa

Malipo ya bonasi uliyopata yatakokotolewa kulingana na jumla ya mauzo yako, ukiondoa thamani ya marejesho yoyote yaliyofanywa ndani ya siku 45 baada ya muda wa bonasi kuisha. Malipo ya bonasi uliyopata yataonekana katika akaunti yako ya AdSense katika YouTube ndani ya siku 120 za muda wa mpango kuisha kila mwezi.

Kumbuka: Bonasi ya utendaji ya washirika wa Ununuzi kwenye YouTube inasimamiwa na Sheria na Masharti ya Mpango wa Washirika wa YouTube. Google inaweza kusimamisha bonasi ya utendaji ya washirika wa Ununuzi kwenye YouTube wakati wowote kwa kutoa notisi. Google inahifadhi haki ya kukataa malipo kwa sababu zinazojumuisha miamala inayozalishwa kwa njia ya udanganyifu, matumizi mabaya, kwa ulaghai au njia nyingine zisizo sahihi kama inavyobainishwa na Google. 

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
9255187272941236769
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false