Kutayarisha podikasti kwenye Studio ya YouTube

Pata maelezo kuhusu jinsi ya kutayarisha podikasti ukitumia Studio ya YouTube na kuweka podikasti yako kwenye YouTube Music.

Kutayarisha Podikasti kwenye Studio ya YouTube

Kwenye YouTube, podikasti ni orodha ya kucheza na vipindi vya podikasti ni video zilizo katika orodha hiyo ya kucheza. Podikasti yako inapaswa kujumuisha vipindi kamili pekee, vilivyopangwa kwa mpangilio ambao vinapaswa kutumiwa. Iwapo podikasti yako ina vipindi vingi, vijumuishe kwenye podikasti hiyohiyo.

Watayarishi wa podikasti wanastahiki manufaa yafuatayo:

  • Kujumuishwa kwenye YouTube Music
  • Beji za podikasti kwenye kurasa za Kutazama na Orodha ya kucheza
  • Kuangazia youtube.com/podcasts ili kuwavutia wasikilizaji wapya
  • Kadi Rasmi zenye Maelezo Kuhusu Mtumiaji.
  • Ugunduzi rahisi kwenye Ukurasa wa kutazama ili kuwasaidia wasikilizaji kupata vipindi vyako
  • Mapendekezo kwa wasikilizaji wapya wanaovutiwa na mambo sawa
  • Vipengele vya utafutaji vilivyoboreshwa ili kusaidia hadhira yako kupata podikasti yako
Kumbuka:
  • Baadhi ya orodha za kucheza hazistahiki kutumia vipengele vya podikasti, hata kama utazibainisha kama podikasti. Maudhui yasiyostahiki yanajumuisha, lakini sio tu, maudhui ambayo hayamilikiwi na mtayarishi.
  • Video Fupi iliyotayarishwa kutumika kwenye podikasti yako haitaonekana kwenye YouTube Music.
  • Youtube.com/podcasts inapatikana nchini Marekani pekee.
  • Podikasti za watayarishi hujumuishwa kwenye programu ya YouTube Music katika nchi au maeneo ambako podikasti zinapatikana. 

Pata maelezo kuhusu jinsi ya kutayarisha podikasti kwenye YouTube

Angalia mbinu zetu bora za watayarishi wa podikasti ili upate vidokezo zaidi vya kuboresha kituo chako au upate maelezo kuhusu jinsi ya kutayarisha podikasti kwenye Studio ya YouTube ukitumia maelezo yaliyo hapa chini. Iwapo wewe ni mtumiaji mpya wa YouTube, pata maelezo kuhusu jinsi ya kupakia video ziwe vipindi vya podikasti yako.

Kutayarisha podikasti mpya kwenye Studio ya YouTube

Ili utayarishe podikasti mpya:

  1. Ndani ya Studio ya YouTube, bofya Tayarisha kisha Podikasti mpya.
    • Unaweza kuombwa uthibitishe akaunti yako kabla ya kutayarisha podikasti mpya.
  2. Kwenye dirisha ibukizi, chagua Tayarisha podikasti mpya.
    • Chagua Weka orodha ya kucheza iliyopo iwe podikasti ikiwa ungependa kubadilisha orodha ya kucheza iliyopo iwe podikasti. Pata maelezo ya jinsi ya kuboresha orodha za kucheza zilizopo katika sehemu inayofuata.
  3. Weka maelezo ya podikasti yako, ikiwa ni pamoja na:
  4. Bofya Tayarisha ili uhifadhi.

Ukitayarisha podikasti yako, weka vipindi kwa kupakia video mpya au zilizopo kwenye podikasti yako. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuweka video kwenye podikasti yako katika sehemu inayofuata.

Kumbuka:

  • Kwenye YouTube, kila kipindi cha podikasti huwakilishwa na video. MP3 haiwezi kubadilishwa kuwa podikasti kwenye YouTube. Ili utayarishe podikasti, pakia au weka video kwenye orodha ya kucheza ya podikasti yako.
  • Ikiwa kipindi cha podikasti yako kinakiuka sera zetu za hakimiliki, maudhui yako hayataruhusiwa kutumia vipengele vya podikasti. Pata maelezo zaidi kuhusu matumizi ya haki na maudhui yaliyo na hakimiliki kwenye YouTube.
  • Video za podikasti zinapatikana kwa uchezaji wa sauti pekee. Ili uzime uchezaji wa sauti pekee kwenye video, lazima uiondoe video hiyo kwenye podikasti zote ndani ya mipangilio ya video zako.
Ili upate maelezo zaidi kuhusu kuboresha kipindi chako kwenye YouTube, angalia mbinu zetu bora ndani ya Vidokezo vya Watayarishi.

Weka video kwenye podikasti

Ili upakie video mpya kwenye podikasti yako:

  1. Ndani ya Studio ya YouTube, nenda kwenye Maudhui kisha Podikasti.
  2. Chagua podikasti yako.
  3. Bofya Weka video kisha Pakia video.
  4. Pakia video ambazo ungependa kuweka kwenye podikasti yako na uweke maelezo ya video.
  5. Bofya Tayarisha ili uhifadhi mabadiliko.

Ili uweke video zilizopo kwenye podikasti yako:

  1. Ndani ya Studio ya YouTube, nenda kwenye Maudhui kisha Podikasti.
  2. Chagua podikasti yako.
  3. Bofya Weka video kisha Weka video zako zilizopo.
  4. Chagua video ambazo ungependa uweke kwenye podikasti yako.
  5. Bofya Weka kwenye orodha ya kucheza na uchague podikasti yako kwenye orodha hiyo.
  6. Bofya Hifadhi ili uweke video kwenye podikasti yako.

Kufanya orodha ya kucheza iliyopo iwe podikasti

  1. Ndani ya Studio ya YouTube, nenda kwenye Maudhui kisha Orodha za Kucheza.
  2. Elea juu ya orodha ya kucheza unayotaka kuifanya iwe podikasti.
  3. Bofya Menyu kisha Ifanye iwe podikasti.
  4. Kagua maelezo ya podikasti yako na uweke kijipicha cha mraba mdogo cha podikasti. Maelezo ya podikasti yanajumuisha jina, maelezo na anayeweza kutazama podikasti yako kwenye YouTube.
  5. Bofya Nimemaliza ili uthibitishe mabadiliko uliyofanya.

Kumbuka:

Hakikisha kuwa orodha zako za kucheza zilizopo zimeboreshwa kwa ajili ya kuchapisha na kusambaza podikasti kwenye YouTube. Ili upate maelezo zaidi, angalia mbinu zetu bora ndani ya Vidokezo vya Watayarishi.

Kuipatia podikasti yako jina

Wakati wa kuweka mipangilio, ipe podikasti yako jina linalojieleza. Usiweke maneno ya ziada kwenye jina la podikasti yako (ikiwa ni pamoja na ‘podikasti,’ isipokuwa iwe ni sehemu ya jina la podikasti yako).

Epuka majina ya jumla ya podikasti, kama vile "Vipindi Kamili," "Vipakiwa Vipya," "Podikasti," n.k. Iwapo jina la orodha yako ya kucheza si dhahiri, YouTube itabadilisha jina la podikasti yako na kuweka jina la kituo chako kwenye programu ya YouTube Music.

Kumbuka:
  • Baadhi ya orodha za kucheza hazistahiki kutumia vipengele vya podikasti, hata kama utazibainisha kama podikasti. Maudhui yasiyostahiki yanajumuisha, lakini sio tu, maudhui ambayo hayamilikiwi na mtayarishi.
  • Video Fupi iliyotayarishwa kutumika kwenye podikasti yako haitaonekana kwenye YouTube Music.
  • Youtube.com/podcasts inapatikana nchini Marekani pekee.
  • Podikasti za watayarishi hujumuishwa kwenye programu ya YouTube Music katika nchi au maeneo ambako podikasti zinapatikana. 

Kubadilisha maelezo ya podikasti yako

Ili ubadilishe maelezo ya podikasti yako:

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Nenda kwenye Maudhui kisha Podikasti.
  3. Wekelea kiashiria kwenye podikasti ambayo ungependa kuibadilisha kisha ubofye .
  4. Kwenye Ukurasa wa maelezo, badilisha jina, maelezo, kijipicha cha podikasti cha mraba mdogo, uonekanaji au mpangilio wa video wa podikasti yako.
  5. Bofya Hifadhi.

Kuondoa vipengele vya kuchapisha na kusambaza podikasti katika orodha

  1. Ndani ya Studio ya YouTube, nenda kwenye Maudhui kisha Podikasti.
  2. Wekelea kiashiria juu ya orodha ya kucheza unayotaka kuondoa isiwe podikasti.
  3. Bofya kwenye Menyu karibu na podikasti unayotaka kuondoa vipengele.
  4. Chagua Badilisha isiwe podikasti.
  5. Bofya Ndiyo ili uthibitishe.

Kupanga upya vipindi kwenye podikasti yako

Ili ubadilishe mpangilio ambao vipindi vyako vinatumika, utatakiwa kuvipangilia upya ndani ya orodha yako ya kucheza ya podikasti.

  1. Ndani ya Studio ya YouTube, nenda kwenye Maudhui kisha Podikasti.
  2. Bofya Badilisha kwenye podikasti ambayo ungependa kusasisha.
  3. Kwenye ukurasa wa maelezo ya podikasti, bofya menyu ya Mpangilio Chaguomsingi wa Video na uchague jinsi unavyotaka video zako zipangwe.
  4. Bofya Hifadhi kwenye kona ya juu kulia ili uthibitishe mabadiliko.
  • Iwapo podikasti yako ina mfululizo wa vipindi, panga video zako kuanzia kipindi kipya zaidi hadi cha zamani zaidi.
  • Iwapo podikasti yako ni ya mfululizo, panga orodha yako ya kucheza kuanzia kipindi cha zamani zaidi hadi kipya zaidi.

Kupima utendaji wa podikasti yako kwenye YouTube

Ili uelewe utendaji wa jumla wa podikasti yako:

  1. Fungua Studio ya YouTube.
  2. Kwenye kichupo cha Takwimu , bofya Muhtasari.
  3. Chagua podikasti husika kwenye kadi ya Podikasti Zako upande wa chini kulia mwa ukurasa.

Kumbuka: Ikiwa una podikasti moja pekee kwenye YouTube, hili litakuwa chaguo pekee.

Ndani ya muhtasari huu, unaweza kupata data ya utazamaji, muda wa kutazama na data ya podikasti yako. Iwapo una podikasti mbalimbali, orodha zako za kucheza zitaonekana katika mzunguko.

Ili kuelewa zaidi kuhusu utendaji wa podikasti yako:

  1. Fungua Studio ya YouTube.
  2. Kwenye kichupo cha Takwimu , bofya Muhtasari.
  3. Chagua Angalia Takwimu za Podikasti.

Kwenye mwonekano huu, utapata:

  • Muhtasari wa utendaji wa podikasti yako
  • Vyanzo vya watazamaji
  • Demografia za hadhira
  • Vipimo vya muda wa kutazama
  • Data ya mapato
  • Na zaidi

Iwapo una podikasti mbalimbali, bofya jina la podikasti ambayo ungependa kuichanganua.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
6851513784194853685
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false