Mwongozo wa Shughuli kwenye YouTube

Mbinu bora za kuweka marejeleo

Vipengele hivi vinapatikana tu kwa washirika ambao hutumia Kidhibiti Maudhui cha Studio ya YouTube. Wasiliana na Msimamizi wako wa Washirika wa YouTube ili uweze kuvitumia.
Ili Content ID iweze kulinganisha maudhui vizuri na kwa ufanisi kadri iwezekanavyo, ni muhimu kudumisha faili za marejeleo ambazo ni sahihi na zinatumika. Bila udumishaji huu, uko katika hatari ya kujipata ukiwa na vikwazo kwenye akaunti, mahusiano hasi ya umma kwenye kampuni yako na miradi ya usafishaji inayochukua muda mwingi.

Tumia mbinu bora zilizoorodheshwa hapa chini ili ufaulu kudumisha faili zako za marejeleo ipasavyo:

Wasilisha faili za marejeleo ambazo ni sahihi na za kipekee

Ni lazima uwe na haki za kipekee katika eneo moja au zaidi kwenye faili za marejeleo unazowasilisha. Masharti haya yanatumika kwa vipengee vyote viwili vya sauti na picha vya marejeleo yako. Kwa mfano, ikiwa marejeleo yako picha na video yana sauti ya wengine isiyo na leseni, maudhui hayo yanapaswa kuondolewa kabla ya uwasilishaji. Faili ya marejeleo ikitambuliwa kuwa huenda si sahihi na inaweza kuzalisha madai yasiyo sahihi, utapata arifa katika Kidhibiti Maudhui cha Studio. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuthibitisha faili za marejeleo ambazo huenda si sahihi.

Kumbuka kwamba aina zifuatazo za maudhui hazijatimiza vigezo vya ulinganishaji wa Content ID:

  • Video za wengine zilizopachikwa
  • Maudhui ya PD
  • Maudhui ambayo hayajapewa leseni ya kipekee
  • Maudhui ambayo kwa kiwango kikubwa si ya kipekee au ni ya kuigwa (kama vile rekodi za karaoke, rekodi zilizoboreshwa au miseto fulani)
  • Maudhui ambayo ni ya jumla sana

Pata maelezo zaidi kuhusu maudhui yanayotimiza vigezo vya Content ID.

Jumuisha metadata ya kipengee ambayo ni kamili na sahihi

Mpakiaji wa video kwenye YouTube anapopata dai la Content ID, anahitaji maelezo ya kutosha kuhusu maudhui yanayodaiwa na mmiliki wa maudhui hayo. Kwa sababu hii, ni lazima marejeleo yawe na metadata kamili na sahihi.

  • Ni lazima vipengee vyote viwe na kichwa chenye maelezo (si “Wimbo wa 4” au nambari ya ufuatiliaji wa ndani, kwa mfano).
  • Vipengee vya muziki uliorekodiwa ni lazima pia viwe na maelezo ya msanii na studio ya kurekodia.

Tenga sehemu zenye maudhui ya wengine

Ni lazima uwe na haki za kipekee kwenye faili za marejeleo ambazo umewashia kipengele cha ulinganishaji wa Content ID.

Ikiwa marejeleo yako yanajumuisha maudhui ya wengine, kama vile video iliyo wazi kutumiwa na umma, unapaswa kutenga sehemu hizo zisizingatiwe wakati wa ulinganishaji wa Content ID. Mifano mingine ya maudhui ya wengine inaweza kujumuisha klipu fupi zilizotumiwa kwa mujibu wa kanuni za matumizi ya haki, matangazo ya biashara au sauti zinazojirudia zisizo za kipekee.

Unaweza kuwasilisha maudhui yatakayotengwa kwenye marejeleo kwa kutumia kiolezo cha CSV au mipasho ya DDEX.

Weka sera maalum za zinazolingana

Sera za zinazolingana hubainisha hatua ambayo Content ID inapaswa kuchukua kuhusiana na video unazodai. Unaweza kuweka sera maalum za zinazolingana zinazoeleza Content ID idai video kiotomatiki kulingana na:

  • Kiwango cha video ya mtumiaji kinacholingana: Urefu au asilimia ya video iliyopakiwa inayolingana na faili yako ya marejeleo.
  • Kiwango cha faili ya marejeleo kinacholingana: Urefu au asilimia ya faili yako ya marejeleo inayolingana na video iliyopakiwa.
  • Aina ya mlingano: Aina ya maudhui yanayolingana na faili yako ya marejeleo: sauti pekee, video pekee au zote mbili.

Unaweza pia kuteua chaguo la kuelekeza video unazodai ili uzikague mwenyewe ili ushughulikie mwenyewe maudhui yanayolingana ambayo huenda yanatiliwa shaka. Kupitia mchakato huu kunaweza pia kukusaidia kutambua marejeleo yoyote ambayo huenda si sahihi. Pata maelezo zaidi kuhusu kuweka sera.

 Tumia faili za urefu kamili

Tunapendekeza utumie faili za urefu kamili, wala si klipu, kama faili zako za marejeleo. Faili za marejeleo za urefu kamili huleta viwango vya juu zaidi vya uchumaji wa mapato na ulinganishaji wa Content ID wenye ufanisi zaidi.

Ikiwa faili yako ya marejeleo ya urefu kamili inajumuisha maudhui ya wengine, kama vile video iliyo wazi kutumiwa na umma, unapaswa kutenga sehemu hizo zisizingatiwe wakati wa ulinganishaji wa Content ID.
Kumbuka: Unaweza kuwasilisha faili ya marejeleo ya urefu kamili hata wakati hutaki maudhui yote yatazamwe kwenye YouTube. Faili ya marejeleo si video ya YouTube inayoweza kutazamwa na umma.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
113472934115912562
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false