Mabadiliko kwenye masharti ya utozaji wa Google Play kwa wasanidi programu wanaohudumia watumiaji nchini India

Kuanzia tarehe 13 Machi 2024, wasanidi programu wanaotoa mfumo mbadala wa utozaji kwa watumiaji nchini India, ni sharti watumie API za mfumo mbadala wa utozaji. Angalia maelezo hapa chini na utembelee mwongozo wetu wa ujumuishaji wa API ya mfumo mbadala wa utozaji ili uanze.

Kutokana na kanuni za hivi karibuni nchini India, sasa tunawapa wasanidi programu wote uwezo wa kutoa mfumo mbadala wa utozaji pamoja na mfumo wa utozaji wa Google Play kwa watumiaji wa kompyuta kibao na simu zao za mkononi nchini India. Ikiwa mtumiaji atalipa kupitia mfumo mbadala wa utozaji, ada ya huduma ya Google Play itapunguzwa kwa asilimia 4. Soma chapisho hili kwenye blogu na Sera ya malipo iliyosasishwa kwa maelezo zaidi.

Ikiwa hupangi kuweka mfumo mbadala wa utozaji, huhitaji kuchukua hatua yoyote iwapo programu yako tayari inatumia mfumo wa utozaji wa Google Play.

Kujumuisha mfumo mbadala wa utozaji

Ili kudumisha hali thabiti na salama ya utumiaji, wasanidi programu watahitaji kutimiza masharti kadhaa. Sasa wasanidi programu wanaweza kujumuisha API za mfumo mbadala wa utozaji, inayorahisisha utekelezaji wa masharti ya hali ya utumiaji na kuripoti. Pata maelezo zaidi kuhusu manufaa ya ziada ya API hapa.

Wasanidi programu ambao hawako tayari kujumuisha API za mfumo mbadala wa utozaji wana chaguo la kutekeleza skrini ya chaguo za mtumiaji wao wenyewe na kuripoti miamala hadi tarehe 13 Machi 2024.

Kujumuisha API za mfumo mbadala wa utozaji

Ikiwa ungependa kuwapa watumiaji nchini India mfumo mbadala wa utozaji pamoja na ule wa Google Play na utakuwa unatumia API za mfumo mbadala wa utozaji kuanzia tarehe utakayoanza kutoa mfumo huo, ni sharti ufuate hatua zifuatazo:

  1. Jaza fomu ya taarifa ya malipo, kubali Sheria na Masharti na ukamilishe hatua zozote za kuanza ushirikiano wa kimkataba zinazohitajika ili ujiandikishe kwenye mpango kupitia timu ya usaidizi ya Google (kwa mfano, unahitajika kuweka mipangilio ya taarifa zako za malipo).
  2. Fuata masharti ya uaminifu na usalama kwa kuthibitisha kutii masharti ya PCI DSS na kuwapa watumiaji njia ya kuripoti miamala ya kilaghai.
  3. Kamilisha mchakato wa ujumuishaji wa API za mfumo mbadala wa utozaji kama inavyoelezwa kwenye mwongozo huu wa ujumuishaji wa API.
  4. Dhibiti mipangilio ya mfumo mbadala wa utozaji wa Dashibodi yako ya Google Play, ili kujijumuisha au kujiondoa kwenye kila programu yako, kupakia nembo za njia ya kulipa na URL za kudhibiti usajili.
  5. Ripoti kwa Google Play miamala yote iliyoidhinishwa inayofanywa na watumiaji nchini India, ndani ya saa 24 ukitumia API za mfumo mbadala wa utozaji.
  6. Kwa usajili wowote unaoendelea ulioanzishwa ulipokuwa unatoa mfumo mbadala wa utozaji bila uwekaji otomatiki, utahitajika kuuhamisha kupitia ExternalTransactions API kabla ya kuripoti miamala inayorudiwa kupitia kwenye API. Uhamishaji huu wa mara moja lazima ufanyike kabla ya tarehe 13 Machi 2024, ambayo ni tarehe ya mwisho ya kuhamia kwenye API ya mfumo mbadala wa utozaji. Kwa maelezo zaidi, tembelea ukurasa wetu wa Maswali Yanayoulizwa Sana.
  7. Lipa ada ya huduma ya Google Play iliyorekebishwa, kwa miamala iliyotolewa ankara inayotumia mfumo mbadala wa utozaji, nje ya mfumo wa utozaji wa Google Play.

Ikiwa tayari unashiriki katika mpango na unahamia API za mfumo mbadala wa utozaji, unaweza kuruka hatua ya 1 hapo juu. Baada ya kukamilisha hatua zilizoainishwa hapo juu na kuanza kuripoti miamala kwa kutumia API, huhitaji tena kutuma miamala wewe mwenyewe.

Ujumuishaji bila uwekaji otomatiki

Ikiwa ungependa kuwapa watumiaji nchini India chaguo la mfumo mbadala wa utozaji pamoja na mfumo wa Google Play, lakini bado hujakuwa tayari kujumuisha API za mfumo mbadala wa utozaji, ni lazima ukamilishe hatua zifuatazo za kujiandikisha mwenyewe:

  1. Jaza fomu ya taarifa ya malipo, kubali Sheria na Masharti na ukamilishe hatua zozote za kuanza ushirikiano wa kimkataba zinazohitajika ili ujiandikishe kwenye mpango kwa usaidizi wa timu ya usaidizi ya Google (kwa mfano, unahitajika kuweka mipangilio ya taarifa zako za malipo).
  2. Bainisha programu ambazo utatoa chaguo mbadala la utozaji ukitumia fomu ya kujiandikisha ambayo utatumiwa kwa barua pepe baada ya kukamilisha fomu ya taarifa.
  3. Fuata masharti ya uaminifu na usalama kwa kuthibitisha kutii masharti ya PCI DSS na kuwapa watumiaji njia ya kuripoti miamala ya kilaghai.
  4. Fuata masharti yetu ya muda ya hali ya utumiaji ili uhakikishe kuwa chaguo la mfumo wa utozaji limewasilishwa kwa njia thabiti na linahakikisha kuwa watumiaji wanaelewa chaguo wanalofanya.
  5. Piga hesabu kamili na uripoti kwa Google Play kiasi cha miamala yote iliyolipwa kupitia mfumo mbadala wa utozaji kwa ajili ya kutuma ankara. Maagizo ya kuripoti kila mwezi yatatolewa kwa wasanidi programu waliojaza fomu ya taarifa na kukamilisha utaratibu wa kufahamu mazingira ya kazi katika mpango huu.
  6. Lipa ada ya huduma ya Google Play iliyorekebishwa, kwa miamala iliyofanywa kupitia mfumo mbadala wa utozaji nje ya mfumo wa utozaji wa Google Play.
  7. Kabla ya tarehe ya mwisho ya kuhama, jumuisha API za mfumo mbadala wa utozaji, hamisha usajili wowote unaoendelea ambao ulianza ulipokuwa unatoa mfumo mbadala wa utozaji bila uwekaji otomatiki na usasishe mipangilio ya mfumo mbadala wa utozaji kwenye Dashibodi ya Google Play. Baada ya kuhamisha usajili unaoendelea na kuanza kuripoti miamala kwa kutumia API, huhitaji tena kutuma miamala wewe mwenyewe. Uhamishaji huu wa mara moja lazima ufanyike kabla ya tarehe 13 Machi 2024, ambayo ni tarehe ya mwisho ya kuhamia kwenye API ya mfumo mbadala wa utozaji. Kwa maelezo zaidi, tembelea ukurasa wetu wa Maswali Yanayoulizwa Sana.

Nini kinachofuata

Baada ya kujaza fomu ya taarifa ya mfumo mbadala wa utozaji, tafadhali rejelea maagizo ambayo tutakutumia kwa njia ya barua pepe. Haya yanabainisha maelezo ambayo unapaswa kuripoti kwa Google na malipo unayopaswa kulipa kama ada ya huduma na kodi.

Ikiwa una maswali yoyote ya ziada, unaweza kuwasiliana na timu yetu ya usaidizi hapa.

Fungua fomu ya taarifa

Maswali yanayoulizwa sana

Kwa nini bado unahitaji mfumo wa utozaji wa Google Play pamoja na mfumo wa msanidi programu?

Google Play inaamini kuwa watumiaji wanapaswa kuwa na chaguo la kutumia mfumo wa utozaji wa Google Play wanapofanya ununuzi wa bidhaa dijitali kwenye programu zilizosakinishwa kutoka Google Play. Tumeunda mfumo wa utozaji wa Google Play kwa viwango vya juu vya usalama na faragha ili watumiaji wawe na uhakika wanapofanya ununuzi wa ndani ya programu. Pia, mifumo mbadala ya utozaji huenda isitoe viwango vya ulinzi au chaguo na vipengele vya malipo sawa na vya mfumo wa utozaji wa Google Play — kama vile vidhibiti vya wazazi, njia za kulipa za familia, udhibiti wa usajili, kadi za zawadi za Google Play na Pointi za Google Play.

Kwa nini bado mnatoza ada ya huduma?

Ada ya huduma ya Google Play haijawahi kamwe kuwa ada ya uchakataji wa malipo tu. Huonyesha thamani inayotolewa na Android na Google Play na huduma zote za wasanidi programu tunazotoa, ikiwa ni pamoja na usambazaji wa programu na upatikanaji, mfumo wa biashara, zana za wasanidi programu, takwimu, mafunzo na zaidi. Tembelea makala haya kwa maelezo zaidi kuhusu ada ya huduma.

Ni kwa aina gani ya bidhaa ninaweza kuwapatia watumiaji nchini India chaguo la mfumo mbadala wa utozaji?

Mifumo mbadala ya utozaji inaweza kutumiwa kwa ununuzi wa ndani ya programu na usajili unaouzwa kwa watumiaji wa kompyuta kibao na simu za mkononi. Tafadhali rejelea Sera ya malipo kwa maelezo zaidi.

Ni kiasi gani cha ada ya huduma kinatozwa kwa miamala dijitali inayofanywa kupitia mfumo mbadala wa utozaji?

Wasanidi programu ni lazima wailipe Google ada za huduma zinazotumika. Mtumiaji anapochagua kutumia mfumo mbadala wa utozaji, ada ya kawaida ya huduma ambayo msanidi programu hulipa itapunguzwa kwa asilimia 4 kwa watumiaji waliochagua mfumo wa utozaji wa Google Play, ada ya huduma haitabadilika. Ada ya huduma itakayotozwa kwa wasanidi programu wanaoendelea kutumia mfumo wa utozaji wa Google Play pekee haibadiliki, ambapo asilimia 99 ya wasanidi programu wanatimiza masharti ya kutozwa ada ya huduma ya asilimia 15 au chini yake.

Je, ninatumaje miamala iliyofanywa kupitia mfumo mbadala wa utozaji?

Kuanzia tarehe 14 Novemba 2023, miamala iliyofanywa kupitia mfumo mbadala wa utozaji inaweza kuripotiwa kupitia API za mfumo mbadala wa utozaji na ni sharti iripotiwe ndani ya saa 24 ya malipo kuidhinishwa. API hizi zinafanya iwe rahisi kwa wasanidi programu kuripoti na pia kuruhusu miamala kupitia mfumo mbadala wa utozaji ionekane kwenye Chati Maarufu za Google Play.

Ikiwa bado hujajumuisha API za mfumo mbadala wa utozaji, bado unaweza kuendelea kuripoti miamala wewe mwenyewe hadi terehe 13 Machi 2024. Ukiripoti mwenyewe, unatakiwa uripoti mwenyewe kiasi cha miamala iliyolipwa mara moja kwa mwezi kufikia siku ya 5 ya kazi ya kila mwezi. Kwa mfano, ripoti ya miamala iliyofanywa mwezi Oktoba 2023 itapaswa kuripotiwa kufikia tarehe 7 Novemba 2023. Baada ya kujaza fomu ya taarifa, tutakagua maelezo yako na kukutumia maagizo kuhusu jinsi ya kuripoti miamala yako iliyolipiwa na malipo unayopaswa kulipia kwa ada za huduma na kodi zozote zinazokatwa.

Je, ada ya huduma inakokotolewa na ankara zake kutumwa vipi kwa miamala inayofanywa kupitia mfumo mbadala wa utozaji?

Ada ya huduma hutathminiwa kulingana na miamala iliyolipwa kutoka kwa watumiaji wa kompyuta kibao na simu za mkononi nchini India. Utapokea ankara yenye tarehe ya kukamilisha na maagizo ya malipo.

Je, ninahitaji kuonyesha bei sawa kwenye mfumo mbadala wa utozaji kama iliyo kwenye mfumo wa utozaji wa Google Play?

Hapana, wasanidi programu wanaweza kuweka bei tofauti kwenye kila mfumo wa utozaji wakipenda.

Ikiwa ninapanga kutoa chaguo mbadala la utozaji au ikiwa tayari nimeutoa, ninapaswa kutimiza masharti ya hali ya utumiaji yaliyobainishwa kwenye ukurasa huu kufikia lini?

Ikiwa unatoa chaguo mbadala la utozaji lenye ujumuishaji wa API za mfumo mbadala wa utozaji, masharti ya hali ya utumiaji yatatimizwa kwa kujumuisha na kutumia API za upande wa kiteja. Kuanzia tarehe 14 Machi 2023, wasanidi programu wote wanaoshiriki watahitajika kujumuisha API za mfumo mbadala wa utozaji ili kutekeleza skrini ya chaguo la mtumiaji na kuripoti miamala.

Je, wasanidi programu wanaweza kutangaza mfumo mbadala wa utozaji ndani ya programu zao?

Ndiyo, wasanidi programu wanaotumia mfumo mbadala wa utozaji wanaweza kutangaza mfumo huo mbadala wa utozaji ndani ya programu zao, lakini lazima pia wafuate mwongozo wetu wa UX au watoe mfumo mbadala wa utozaji kwa kutumia API za mfumo mbadala wa utozaji ili kuhakikisha watumiaji wanaelewa chaguo lililotolewa na wanakuwa na hali thabiti ya utumiaji.

Je, mpango huu unaruhusu viungo vya ununuzi wa maudhui dijitali kwa watumiaji?

Ndiyo, mpango huu unaruhusu wasanidi programu kutumia malipo yanayofanywa kwenye wavuti kama njia mbadala ya kulipa katika mwonekano wa wavuti uliopachikwa ndani ya programu zao. Kama zilivyo njia mbadala nyingine za kulipa, malipo haya yatategemea masharti ya mpango yaliyoorodheshwa kwenye ukurasa huu, ikijumuisha masharti ya usalama, uaminifu wa mtumiaji pamoja na ada ya huduma.

Programu yangu imeandikishwa kwenye jaribio la chaguo mbadala la utozaji kwa watumiaji nchini India. Je, ninapaswa kujisajili tena ili kushiriki kwenye mpango wa mfumo mbadala wa utozaji nchini India?

Ikiwa programu yako iliandikishwa kwenye jaribio la chaguo mbadala la utozaji kwa watumiaji nchini India kabla ya tarehe 22 Februari, 2023, huhitaji kujiandikisha tena kupitia mpango wa mfumo mbadala wa utozaji nchini India. Hata hivyo, unahitajika kuwasilisha fomu ya kujiandikisha iliyosasishwa ya kifurushi cha programu iwapo utabadilisha utoaji wa mfumo mbadala wa utozaji katika nchi kwa kifurushi cha programu husika

Nimewasilisha fomu ya kujiandikisha ya kifurushi cha programu ili kubainisha nchi zitakazotumia chaguo mbadala la utozaji kwa programu yangu. Ninawezaje kuitaarifu Google kuhusu mabadiliko yoyote ya chaguo za kujiandikisha za kifurushi cha programu yangu?

Iwapo unatoa mfumo mbadala wa utozaji bila uwekaji otomatiki, unahitaji kuwasilisha fomu ya kujiandikisha ukibadilisha utoaji wa mfumo mbadala wa utozaji katika soko mahsusi kwa kifurushi fulani cha programu. Tafadhali kumbuka kuwa, masasisho yoyote yataanza kutumika tu tarehe moja ya mwezi unaofuata, majira ya (UTC), ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya ada husika za huduma.

Iwapo unatoa mfumo mbadala wa utozaji ukitumia API za mfumo mbadala wa utozaji, unaweza kubadilisha utoaji wa mfumo mbadala wa utozaji katika soko mahususi kwenye kifurushi cha programu fulani kupitia kwa mipangilio ya mfumo mbadala wa utozaji kwenye Dashibodi ya Google Play. Masasisho yoyote yataanza kutumika mara moja ikiwa ni pamoja na ada husika za huduma.

API za mfumo mbadala wa utozaji zina manufaa yapi? Ninaweza kujumuisha API za mfumo mbadala wa utozaji kwa ajili ya kutekeleza skrini ya chaguo za mtumiaji kabla ya kutumia API kuripoti miamala?

Ili kurahisisha hali ya utumiaji ya msanidi programu, API za mfumo mbadala wa utozaji zimeundwa ili kujumuishwa na kutumiwa pamoja. API za mfumo mbadala wa utozaji zina manufaa yafuatayo:

  • Skrini za mfumo mbadala wa utozaji zinazotekelezwa na Google Play, hii inamaanisha kuwa huhitaji kuunda na kutunza skrini ya maelezo wewe mwenyewe.
  • Mchakato wa kuripoti miamala uliorahisishwa, ambao huondoa hitaji la kugusa kwa mikono na hukabili hitilafu za ujumuishaji au ulinganishaji.
  • Miamala ya mfumo mbadala wa utozaji iliyoripotiwa kupitia API itaonyeshwa kwenye Chati Maarufu za Google Play.

Zaidi ya hayo, pia tumefanya maboresho yafuatayo ili kufanya iwe rahisi kwako kutumia mfumo mbadala wa utozaji:

  • Udhibiti wa hali ya kujihudumia katika mipangilio ya mfumo mbadala wa utozaji kupitia Dashibodi ya Google Play, kama vile kuwasha au kuzima kipengele cha chaguo mbadala la utozaji kwa kila programu inayotimiza masharti kwa kila soko, kudhibiti nembo za njia ya kulipa na URL za kudhibiti usajili.
  • Ripoti zinazoweza kuhamishwa za miamala za mfumo mbadala wa utozaji ambazo zimeripotiwa kupitia API zilizo na maelezo ya ziada kama vile kiwango cha ubadilishaji kilichotumika, kitambulisho cha kifurushi cha programu husika na kiwango cha ada ya huduma.
Ninaweza kupata wapi maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kujumuisha API za mfumo mbadala wa utozaji?

Ni rahisi kupanua ujumuishaji wako uliopo wa mfumo wa utozaji wa Google Play ili utumie API za mfumo mbadala wa utozaji. API za mfumo mbadala wa utozaji zimeundwa kwa kutumia kanuni na miundo ile ile ya usanifu, sawa na Maktaba yetu ya Malipo kupitia Google Play na API za Msanidi Programu wa Google Play. Hii inamaanisha API hizi zinaoana na usanifu uliopo na timu zako zitakuwa na ufahamu nazo.

Katika mwongozo wetu wa ujumuishaji, tunatoa mwongozo wa kina na nyenzo kuhusu jinsi ya kuanza na kushughulikia masuala mbalimbali yanayohusu matumizi ya mfumo mbadala wa utozaji ikiwa ni pamoja na ununuzi wa mara moja na unaorudiwa. Kuna vijisehemu vya msimbo vya mfano ya kufanya iwe rahisi kutekeleza. Tunakaribisha maoni kutoka kwa wasanidi programu kuhusu API hizi na nyenzo za ziada ambazo zitakuwa za manufaa. Ukiwa na maswali yoyote au maoni kuhusu API za mfumo mbadala wa utozaji, tafadhali wasiliana nasi hapa.

Tayari ninashiriki kwenye chaguo mbadala la utozaji, ninahitaji kufanya nini ili nianze kutumia API za mfumo mbadala wa utozaji?

Kabla ya tarehe ya mwisho ya kuhama, ambayo ni tarehe 13 Machi 2024, kamilisha hatua zilizoainishwa kwenye Ujumuishaji wa API za Mfumo Mbadala wa Utozaji. Baada ya kuhamisha usajili wowote unaoendelea kutoka kipindi cha kuripoti wewe mwenyewe na kuanza kuripoti miamala kwa kutumia API, huhitaji tena kutuma miamala wewe mwenyewe.

Je, ninaweza kuripoti vipi miamala inayorudiwa, kupitia API za mfumo mbadala za utozaji kwa usajili unaoendelea ambao ulianza nilipokuwa nikitoa mfumo mbadala wa utozaji bila uwekaji otomatiki?

Kwa usajili wowote unaoendelea ulioanzishwa ulipokuwa unatoa mfumo mbadala wa utozaji bila kuripoti kiotomatiki, utahitajika kuuhamisha kupitia ExternalTransactions API kabla ya kuripoti miamala inayorudiwa kupitia kwa API. Uhamishaji huu wa mara moja lazima ufanyike kabla ya tarehe 13 Machi 2024, ambayo ni tarehe ya mwisho ya kuhamia kwenye API ya mfumo mbadala wa utozaji. Baada ya kuhamisha, unahitaji tu kuripoti miamala inayorudiwa kupitia API na huhitaji tena kuripoti kupitia mfumo wa kuripoti mwenyewe.

Ikiwa bado hujahamisha usajili unaoendelea, bado unatakiwa kuendelea kuripoti miamala inayorudiwa kupitia maagizo yaliyopo ya kuripoti mwenyewe.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

true
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
7344412793621860069
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false