Kuelewa Ada ya Huduma ya Google Play

Wasanidi programu wanaweza kutozwa ada ya huduma ya Google Play kulingana na asilimia ya bei ya ununuzi au ununuzi wa bidhaa dijitali unaofanywa kwenye programu zao. 

Wasanidi programu hupokea thamani muhimu kutoka Android na Google Play na ada yetu ya huduma huonyesha thamani hii. Ada ya huduma pia ni jinsi tunavyochuma pesa kama biashara na kusaidia uwekezaji wetu kwenye Android na Google Play, ikiwa ni pamoja na kutuwezesha tusambaze huduma za Android bure na kutoa kifurushi cha zana na huduma zinazowasaidia wasanidi programu kujenga biashara zilizofanikiwa, huku tukiweka mifumo yetu salama kwa ajili ya mabilioni ya watumiaji ulimwenguni kote.

Maswali yanayoulizwa sana

Kwa nini Google Play hutoza ada ya huduma?

Ada ya huduma hutusaidia kuendeleza uwekezaji wetu kwenye Android na Google Play, huonyesha thamani iliyotolewa na Android na Google Play na ni njia tunayotumia kuchuma pesa kama biashara. Kama vile tu inavyogharimu pesa kusanidi, kuchapisha na kutangaza programu, inagharimu pesa kusanidi, kuchapisha na kutangaza mfumo wa uendeshaji na duka la programu. Huu ni muundo wa kawaida wa biashara wa maduka ya programu na michezo inayotolewa na Microsoft, Apple, Steam, Nintendo, Amazon na wengine.

Ada ya huduma ni kiasi gani?

Hakuna ada ya jumla ya huduma inayotozwa kwa sababu wasanidi programu wanapatikana katika hali mbalimbali ambazo zinahitaji viwango tofauti vya michango ili kukuza biashara za kudumu. Asilimia 99 ya wasanidi programu ambao wanaweza kutozwa ada ya huduma wanatimiza masharti ya kutozwa ada ya asilimia 15 au chini yake. Pata maelezo zaidi kuhusu ada yetu ya huduma kwenye makala haya ya Kituo cha Usaidizi .

Ni nani anayeweza kutozwa ada ya huduma?

Asilimia 3 tu ya wasanidi programu wanaolipisha programu zao au wanaotoa bidhaa dijitali ndio wanaotozwa ada ya huduma. Hii inamaanisha kuwa asilimia 97 ya wasanidi programu husambaza programu zao na kutumia huduma na zana zetu zote za wasanidi programu bila malipo.

Ada ya huduma hulipia nini?

Ada ya huduma husaidia kuendeleza uwekezaji wetu kwenye Android na Google Play, huonyesha thamani iliyotolewa na Android na Google Play, hutuwezesha kutoa huduma bora na za bei nafuu kwa watumiaji, husaidia wasanidi programu kufikia watumiaji na kukuza biashara za kudumu na hulinda usalama wa mfumo.

Sehemu kuu za uwekezaji zinajumuisha:

  • Android na Duka la Google Play: Mfumo wa uendeshaji wa Android bila malipo huwaruhusu watengenezaji wa maunzi kuunda aina mbalimbali za vifaa kwa bei tofauti ambazo huwapa watumiaji uchaguzi usio na kifani. Pia, Duka la Google Play hutoa fursa kubwa duniani ya kuchagua programu na michezo mbalimbali, hupatikana kwenye zaidi ya nchi 190 zenye mapendekezo maalumu na ugunduzi rahisi wa programu zenye ubora wa hali ya juu.
  • Mifumo mipya ya Android: Tunaunda mifumo kwa ajili ya maumbo mapya kama vile Auto na TV ili kuwasaidia wasanidi programu waongeze watu wanaowafikia katika njia mpya.
  • Ulinzi: Watumiaji wanaiamini Android na Google Play kwa sababu ya usalama wake, ukaguzi wa programu ili kuhakikisha zinatii sera za usalama na faragha, pamoja na ulinzi wa kiotomatiki wa Google Play Protect unaokagua zaidi ya programu bilioni 100 kwa siku.
  • Usambazaji wa programu: Wasanidi programu wanaweza kufikia papo hapo zaidi ya watumiaji bilioni tatu wa Android na uwezo wa kuboresha usambazaji wa programu kulingana na kifaa na utendaji na kutoa masasisho ya mara kwa mara.
  • Zana za msanidi programu: Wasanidi programu wanaweza kutekeleza majaribio, jaribio la beta, kuboresha kurasa za programu katika Google Play, kuchanganua utendaji na zaidi.
  • Mfumo wa utozaji: Watumiaji wanafurahia malipo yenye usalama na ya kuaminika, huku wasanidi programu wakiweza kufanya mialama kwa urahisi na watumiaji milioni 700 kwa kutumia kadi ya zawadi ya Google Play na njia faafu za kulipa katika eneo husika.
Wasanidi programu hunufaikaje kwenye Google Play?

Kusaidia wasanidi programu kuwa wabunifu na kukua ni muhimu zaidi kwa dhamira yetu na tunaendelea kuwekeza kwenye mfumo, zana na huduma zetu ili kuwasidia. Tunawarahisishia wasanidi programu kusambaza programu zao kwa mabilioni ya watumiaji wa Android na kuchuma pesa kutoka kwa watu duniani kote kwa kutumia njia ya kulipa ya eneo wanalopendelea.

Pia, tunatoa zana na huduma ili kuwasaidia wasanidi programu kudhibiti machapisho ya programu zao, kampeni za matangazo na usakinishaji upya wa programu kwenye Duka la Google Play, zana za kutekeleza majaribio na kuboresha utendaji, takwimu za data, usaidizi wa kiufundi, mafunzo yasiyolipishwa katika Chuo cha Google Play na zaidi.

Ungependa kupata maelezo zaidi kuhusu baadhi ya huduma zinazotolewa na wasanidi programu?

Usanidi programu

Zana za Android

Tunatoa zana na nyenzo ili kuwasaidia wasanidi programu kutayarisha hali ya utumiaji ambayo watu huipenda, kwa haraka na kwa urahisi, kwenye kila kifaa cha Android. Kwa mfano, Android Studio ni programu rasmi ya Mfumo Jumuishi wa Usanidi kwa ajili ya Wasanidi wa Programu wa Android na inajumuisha kila kitu unachohitaji ili kusanidi programu za Android ikiwa ni pamoja na faharasa ya SDK ya vitegemezi maarufu, maarifa ya ubora wa programu kutoka Firebase Crashlytics na vifaa pepe vya viigaji.
 

Chuo cha Google Play 

Tunatoa mafunzo bila malipo kupitia Chuo cha Google Play kwa wasanidi programu, watu wa biashara na wafanyabiashara wa michezo na programu za Google Play. Chuo cha Google Play kinatoa fursa kwa wasanidi wapya wa programu wanaochipukia, kushiriki ujuzi na mbinu bora za kuanzisha biashara ya programu au michezo, pamoja na wasanidi programu kupata taarifa kuhusu mabadiliko katika zana zetu. Wasanidi programu pia hupata maelezo kuhusu jinsi ya kusanidi programu, kujiandaa kwa ajili ya uzinduzi na kuongeza uonekanaji kwa mtumiaji. Chuo cha Google Play pia hutoa mafunzo kwa wasanidi programu wanaotaka kupata masoko mapya kupitia kozi zetu za Go Global: Japani, Amerika Kusini, Kusini mashariki mwa Asia na Ulaya Magharibi.
 

Jaribio la programu

Tunawapa wasanidi programu uwezo wa kuzifanyia programu zao jaribio la beta kwa kutumia kikundi kidogo cha watumiaji, Wasanidi programu wanaweza kukusanya maoni ya faragha au kuwajibu moja kwa moja wachunguza programu kupitia dashibodi ya Google Play.  Hii inajumuisha kuchunguza matoleo mapya ya programu kabla ya kuzinduliwa. Pia, wasanidi programu wanaweza kufanya majaribio ya matoleo ya programu zao zinazopatikana kwa watumiaji kwenye Google Play ili kupata maoni ya awali au kufuatilia vipimo vya ndani ya programu kabla ya kuzinduliwa.
 

Ripoti za kabla ya uzinduzi

Msanidi programu anapofanya majaribio ya programu kwa kikundi kidogo au kikubwa, wasanidi programu wanaweza kuweka na kutekeleza ripoti za kabla ya uzinduzi ili kubaini matatizo yoyote kwenye programu kabla ya kuchapishwa. Ripoti ya kabla ya uzinduzi hubainisha matatizo yanayoweza kutokea kwenye programu yanayoweza kuathiri hali ya utumiaji kama vile uthabiti, utendaji na usalama wa programu.
 

Uboreshaji wa utendaji wa programu 

Tunatoa zana ya maarifa kuhusu utendaji iliyobuniwa kwa ajili ya wasanidi programu ili kupima na kuboresha utendaji wa programu na michezo ili iwe na video za ubora wa juu na kufanya kazi kwa haraka. Huduma hii inaruhusu wasanidi programu kuchanganua data kwenye vifaa mbalimbali vya Android.

Usalama

Faragha ya mtumiaji na usalama 

Tunatoa mazingira salama ya kupakua programu, hatua hii inaongeza uaminifu kwa watumiaji wa programu. Programu zote zinasambazwa kupitia Google Play, ikiwa ni pamoja na zinazomilikiwa na Google, zinategemea Sera za Google Play. Sera za Google Play zinajumuisha sera zinazohusiana na matumizi na kushughulikia data ya mtumiaji. Tunachapisha maelezo ili kuwasaidia watumiaji kuelewa ni taarifa gani zinakusanywa, kwa nini zinakusanywa na jinsi watumiaji wanavyoweza kusasisha, kudhibiti, kuhamisha au kufuta taarifa zao.
 

Programu huchanganua ili kuzuia usakinishaji wa programu hasidi

Google Play Protect huchanganua vifaa vya Android ili kuwatahadharisha watumiaji iwapo programu ina programu hasidi zinazotambulika, bila kujali ikiwa zilipakuliwa kupitia Google Play, duka la programu za wengine au upakiaji kutoka kifaa kingine.

Pia, tunawapatia wasanidi programu API ili kuwasaidia kuhakikisha kuwa seva zao zinatumia toleo halisi la programu ya msanidi kwenye vifaa halisi vya Android. Hali hii husaidia kuwalinda wasanidi programu dhidi ya ulaghai na hatari za kiusalama kupitia SafetyNet.
 

Usambazaji wa programu 

Usambazaji wa kimataifa 

Kupitia Google Play, wasanidi programu wanaweza kusambaza programu na masasisho ya programu kwa zaidi ya watumiaji bilioni tatu kwenye maelfu ya vifaa kutoka kwa mamia ya kampuni halisi zilizotengeneza kifaa (OEM) katika zaidi ya nchi 190, pia kuweza kusambaza programu katika nchi mahususi. Kwa mfano, wasanidi programu wanaweza kuunda hadi kurasa 50 maalum za programu katika Google Play ili kuweka mapendeleo ya kuorodheshwa kwa programu zao katika Google Play kwenye nchi mahususi. Wasanidi programu pia wanaweza kuweka mapendeleo ya programu kwa kubadilisha wapendavyo kurasa za programu katika Google Play na kulenga hadhira mahususi kwa kubadilisha mwonekano wa programu.

Wasanidi programu pia wanaweza kusambaza masasisho kwenye programu zao kwa ufanisi na usalama kwa kutumia vipengele na utendaji mpya. Masasisho ya programu huwasaidia wasanidi programu kuwafanya watumiaji washiriki na kuusaidia mfumo wa usalama kukabiliana na hatari mpya zinapotokea.
 

Upakuaji wa programu kulingana na nchi

Wasanidi programu wanaweza kupata maarifa kuhusu nchi maarufu ambako programu zimesanikishwa pamoja na maarifa kuhusu upakuaji wa lugha mahususi. Wasanidi programu wanaweza kukagua ripoti kuhusu usakinishaji wa programu, uondoaji, ukadiriaji, mapato na kuacha kufanya kazi kupitia Dashibodi ya Google Play ili kusaidia kufuatilia utendaji wa programu zao. 

Wasanidi programu wanaweza kutumia zana ya utafiti shirikishi ya Google (“Think with Google”) ili kupata:

  • mwongozo wa jinsi ya kuelewa tabia ya watumiaji;
  • vidokezo vya masoko;
  • zana za wasanidi programu ili kukuza hadhira ya programu kwa kuelewa demografia ya watumiaji wa programu; na
  • takwimu za wasanidi programu kuhusu vitu wanavyopendelea watumiaji katika eneo au nchi mahususi, miongoni mwa vitu vingine.
 

Huduma za tafsiri ili kusaidia kujanibisha programu za kimataifa

Kupitia huduma za tafsiri za Google, programu zinaweza kutafsiriwa kwa hadi lugha 48. Pia, tunawapa wasanidi programu mapendekezo kuhusu vipengele vya ndani ya programu ambapo wasanidi programu wangependa kuzipa kipaumbele tafsiri zilizojanibishwa. Tumefungua ukurasa wenye vidokezo vya kufanikiwa katika maeneo mahususi (APAC, EMEA, Amerika Kusini na Amerika Kaskazini). Makala haya yanafafanua jinsi ya kujanibisha programu kwa kuchapisha katika mojawapo ya lugha za maeneo mahususi na kutoa ofa wakati wa matukio ya sikukuu.
 

Maoni na ukadiriaji wa programu

Tunatoa zana kwa wasanidi programu ili waboreshe programu zao kwa kutumia maoni kutoka kwa watumiaji kupitia maoni na ukadiriaji. Kwa mfano, tunawapa wasanidi programu muhtasari wa ukadiriaji wa programu, maoni ya watumiaji binafsi na data iliyopangwa kwa makundi kuhusu maoni ya programu.  Pia, tunatoa mwongozo kwa wasanidi programu kuweka mipangilio ya kiotomatiki ya ilani ya mtumiaji kukadiria na kuweka maoni kwenye programu. Pia, tunatoa zana zinazowasaidia wasanidi programu kujaribu kipengele hiki.

 

Uchanganuzi wa jinsi mtumiaji anavyotumia programu

Mnamo Machi 2021, Dashibodi ya Google Play ilizindua vipimo vipya ili kutathmini programu na michezo. Hali hii inahakikisha kuwa wasanidi programu wanaweza kutathmini ushiriki wa programu au michezo yao na mienendo ya uchumaji wa mapato kulingana na vigezo. Vipimo hivi vinajumuisha takwimu kuhusu idadi ya watumiaji wanaofungua programu kila mwezi na takwimu za idadi ya watumiaji wanaoongezeka kila mwezi. Hii ni pamoja na ripoti na data zingine ambazo wasanidi programu wana ufikiaji kwenye Dashibodi ya Google Play.
 

Ugunduzi wa programu 

Tunatoa vidokezo vya kufanya programu zigunduliwe kwenye Google Play ikiwa ni pamoja na jinsi ya kuanzisha ukurasa wa programu katika Google Play, jinsi ya kufanya programu iwe na mwonekano wenye picha nzuri na jinsi ya kuainisha makundi ya hadhira yako. Pia, tunatoa maelezo kuhusu jinsi programu zinavyoweza kugunduliwa zaidi na jinsi programu zinavyopewa nafasi kwenye matokeo ya utafutaji.

Pia, tunasaidia ugunduzi wa programu kwa kulenga utangazaji wa programu na kuwasaidia watumiaji kugundua programu na michezo wanayoweza kufurahia kutoka katika mamilioni inayopatikana kwenye Google Play. Tunazingatia mambo kadhaa wakati wa kupanga na kuzipa nafasi programu na michezo, ikijumuisha, ufaafu kwa mtumiaji, hali ya utumiaji na thamani ya uhariri.

Pia, tunawasaidia watumiaji kwa kuwapa mapendekezo yanayofaa wanapotembelea Google Play. Hii huwasaidia wasanidi programu kufikia watumiaji wapya.
 

Biashara kwenye Google Play

Zana za uchumaji wa mapato

Mfumo wa utozaji wa Google Play huwasaidia wasanidi programu kuuza bidhaa dijitali na maudhui ndani ya programu zao kwa urahisi, ikiwa ni pamoja na maudhui ya ndani ya programu kama vile sarafu za ndani ya mchezo au usajili. 
 

Maelezo ya bei yanayoeleweka na kuaminika

Tunawapa wasanidi programu zana za kuwasaidia kuweka bei za programu zao, kuruhusu wasanidi programu kuweka bei kwa nchi mahususi au ya kimataifa na kutumia kiolezo cha bei kurahisisha uwekaji bei za programu kwenye Dashibodi ya Google Play.

Kwa mfano, wasanidi programu wanaweza kuweka bei ya programu, kubadilisha uwekaji bei wa programu na kuanzisha punguzo au ofa za programu. Wasanidi programu pia wanaweza kuweka mipangilio ya usajili na kubadilisha bei za vipengee vilivyo ndani ya programu. Hali hii inawapa wasanidi programu urahisi wa kuboresha ofa wanazotoa na kuendana na mabadiliko.

 

Usimamizi wa usajili wa Google Play

Tunawaruhusu watumiaji kughairi, kusimamisha au kubadili usajili kwenye Google Playkwa urahisi. Hii ni mojawapo ya huduma zilizounganishwa kwenye mfumo wa utozaji wa Google Play.
 

Usaidizi wa kurejeshewa malipo kwa Wateja wa Google 

Wasanidi programu wanaweza kudhibiti oda za programu kwa urahisi na kushughulikia urejeshaji wa pesa kwa watumiaji kwa haraka. Kwa kutumia tovuti au programu ya Dashibodi ya Google Play, wasanidi programu wanaweza kuangalia oda za programu, kurejesha pesa na kudhibiti ughairi wa usajili wa vipengee ambavyo watumiaji wamenunua.
 

Usimamizi 

Muhtasari wa masasisho ya programu

Kupitia Dashibodi ya Google Play, wasanidi programu wanaweza kuangalia data kulingana na matoleo ya programu kwa kituo cha usambazaji. Wasanidi programu pia wanaweza kupata muhtasari wa kusasisha historia ya programu zao. Wasanidi programu wanaweza kutumia maelezo haya kuendelea kuboresha ofa za programu zao.
 

Dashibodi ya Google Play iliyowekewa mapendeleo

Kulingana na maoni ya wasanidi programu, tumeunda njia kwa wasanidi programu kuweka mapendeleo ya onyesho la vipimo vinavyopatikana katika Dashibodi ya Google Play ili kupima utendaji wa programu zao. Wasanidi programu wanaweza kubandika vipimo wanavyopenda. Hali hii hutoa mbinu ya haraka na rahisi kwa wasanidi programu kufuatilia na kujibu vipimo wanavyojali.
 

Kiolesura thabiti cha kimataifa cha msanidi programu

Dashibodi ya Google Play hutoa kiolesura thabiti cha kimataifa kwa wasanidi programu kupakia na kudhibiti programu zao. Wasanidi programu hunufaika kutokana na vipengele vinavyosaidia kuboresha ubora wa programu, kushirikisha hadhira ya programu, kupata mapato na zaidi.
 

Zana za kulinganisha kikundi cha programu zingine

Wasanidi programu wanaweza kulinganisha programu zao kwa urahisi na programu zingine wanazochagua. Wanaweza kufanya hivi kwa kuweka mipangilio ya kikundi cha programu zilizochaguliwa na mtumiaji, kwa kuchagua kikundi mahususi cha programu na kulinganisha programu zao na programu za kikundi hicho mahususi. Wasanidi programu wanaweza kuhariri kikundi cha programu zilizochaguliwa na mtumiaji ili kulinganisha Android vitals hadi mara tatu kwa mwezi. Hatua hii inawapa wasanidi zana muhimu za kushughulikia programu zao nyingine.

Pia, tunatoa mapendekezo kuhusu jinsi ya kutumia takwimu za kulinganisha programu ili kuchanganua utendaji wa programu.

Je, wasanidi programu wote wanatakiwa kulipa ada ya huduma?

Tumejitolea kuwa na muundo wa biashara unaoturuhusu kuendelea kuwekeza kwenye Android na Google Play, lakini tunaelewa kwamba wasanidi programu wote hawafanani na kutumia mbinu moja kwa wasanidi programu wote hakuwezi kufanya kazi. Kwa mapato mengi ya Google Play, muundo wa biashara hiyo ni ada yetu ya huduma.  Wasanidi programu wanaouza programu zinazolipishwa pekee au wenye uwezo wa ndani ya programu wa kufikia huduma au maudhui dijitali, wanapaswa kulipa ada ya huduma na zaidi ya asilimia 99 ya wasanidi programu hao wanatimiza masharti ya kutozwa ada ya huduma ya asilimia 15 au chini yake. Idadi ndogo ya wasanidi programu wanaowekeza zaidi moja kwa moja kwenye Android na Google Play wanaweza kuwa na ada tofauti za huduma kama sehemu ya ushirika mpana unaojumuisha uwekezaji mkubwa wa kifedha na miunganisho ya bidhaa katika maumbo tofauti. Ushirika huu muhimu wa uwekezaji unaturuhusu kupata watumiaji zaidi kwenye Android na Google Play kwa kuendelea kuboresha matumizi kwa watumiaji wote na kuunda fursa mpya kwa wasanidi programu wote.

Pia, kuna baadhi ya mazingira ambapo hatutozi ada ya huduma kwenye miamala ya ndani ya programu au inayohitaji kutumia mfumo wa utozaji wa Google Play, kwa mfano, punguzo la bidhaa au huduma halisi, kati ya kompyuta katika mtandao mmoja, ufadhili usiotozwa kodi au miamala ya kamari.

Je, athari za sheria za hivi karibuni nchini Korea Kusini ni zipi?

Kutokana na matokeo ya sheria, tunawapa wasanidi programu wote uwezo wa kutoa mfumo mbadala wa utozaji pamoja na mfumo wa utozaji wa Google Play kwa watumiaji wa Korea Kusini wanaofanya ununuzi wa ndani ya programu katika programu zinazosambazwa na Google Play kwenye simu za mkononi na kompyuta kibao.

Wasanidi programu bado watatozwa ada ya huduma kwa miamala inayotumia mfumo mbadala wa utozaji, lakini ada ya huduma imepunguzwa kwa asilimia 4. Kwa mfano, wakati ada ya huduma ni asilimia 15 kwa miamala kupitia mfumo wa utozaji wa Google Play, ni asilimia 11 kwa miamala inayofanywa kupitia mfumo mbadala wa utozaji. Pata maelezo zaidi kuhusu utoaji wa mfumo mbadala wa utozaji kwa watumiaji walio Korea Kusini katika makala hii ya Kituo cha Usaidizi.

Je, athari za agizo la Tume ya Ushindani ya India ni zipi?

Kutokana na agizo la Tume ya Ushindani ya India, kuanzia mwezi Februari, tutawapa wasanidi programu wote uwezo wa kutoa mfumo mbadala wa utozaji pamoja na mfumo wa utozaji wa Google Play kwa watumiaji walio nchini India wanaofanya ununuzi wa ndani ya programu katika programu zinazosambazwa na Google Play kwenye simu za mkononi au kompyuta kibao.

Wasanidi programu bado watatozwa ada ya huduma kwa miamala inayotumia mfumo mbadala wa utozaji, lakini ada ya huduma imepunguzwa kwa asilimia 4. Kwa mfano, wakati ada ya huduma ni asilimia 15 kwa miamala kupitia mfumo wa utozaji wa Google Play, ni asilimia 11 kwa miamala inayofanywa kupitia mfumo mbadala wa utozaji. Maelezo zaidi yatatolewa hivi karibuni.

Maudhui yanayohusiana

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?

Je, unahitaji usaidizi mwingine?

Jaribu hatua zifuatazo:

true
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
8690378467079493687
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
92637
false
false