Malalamiko mengine ya kisheria

YouTube huzingatia tu malalamiko ya kisheria wakati mhusika au mwakilishi wake wa kisheria aliyeidhinishwa amewasiliana nasi.

Mtu fulani akichapisha taarifa zinazokutambulisha binafsi au anapopakia video inayokuangazia bila wewe kujua, ikiwa ni pamoja na hali za faragha au nyeti, mwombe aliyepakia aondoe maudhui hayo. Aliyepakia asipokubali au iwapo hungependa kuwasiliana naye, wasilisha malalamiko kupitia mchakato ulio katika ukurasa wa Mwongozo wa Faragha kwenye YouTube. Taarifa binafsi zinaweza kuwa pamoja na picha yako, jina, namba ya kitambulisho cha taifa, namba ya akaunti ya benki, maelezo ya mawasiliano au taarifa nyingine zinazokutambulisha kimahususi. Pata maelezo zaidi kuhusu vigezo vya kuondoa maudhui kutokana na ukiukaji wa faragha.

Ikiwa malalamiko yako hayahusu faragha, chagua nchi au eneo la mzozo wako kwenye menyu kisha ufuate maagizo.

Jaza fomu hii.

Ikiwa hupati nchi au eneo lako kwenye menyu iliyo hapo juu

YouTube.com inasimamiwa na sheria ya Marekani. Kwa sababu hiyo, hatukubali malalamiko ya kisheria kutoka nchi au eneo ambako haki zako zinadaiwa. Tunapendekeza ufuatilie madai yoyote unayoweza kuwa nayo moja kwa moja dhidi ya mtu aliyechapisha maudhui. Unaweza kujaribu kuwasiliana na aliyepakia. Ikiwa mahakama itaamua kuwa mtu aliyechapisha maudhui ana makosa na ikiwa amri hiyo ya mahakama itatuhitaji tuondoe maudhui kwenye huduma yetu, tutachukua hatua ipasavyo.

Pata maelezo zaidi kuhusu Sera za YouTube, usalama na kuripoti.

Ukiukaji wa sera

Ikiwa una wasiwasi kuhusu ukiukaji wa sera za YouTube, unaweza kuripoti ukiukaji huo. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuripoti video, chaneli na maudhui mengine ambayo hayafai kwenye YouTube.

Unyanyasaji

Iwapo una wasiwasi kuwa mtagusano na mwanachama wa jumuiya umefikia kiwango cha unyanyasaji, unaweza kuripoti mtagusano huo. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuripoti video, chaneli na maudhui mengine ambayo hayafai kwenye YouTube.

Hakimiliki

Ikiwa una tatizo la hakimiliki, nenda kwenye Kituo chetu cha hakimiliki.

Malalamiko kuhusu faragha

Ikiwa video ina taarifa zinazokutambulisha binafsi bila idhini yako, unaweza kuwasilisha malalamiko kupitia mchakato ulio katika ukurasa wa Mwongozo wa Faragha kwenye YouTube. Taarifa binafsi zinaweza kuwa pamoja na picha yako, jina, namba ya kitambulisho cha taifa, namba ya akaunti ya benki, maelezo ya mawasiliano au taarifa nyingine zinazokutambulisha kimahususi.

Pata maelezo zaidi kuhusu vigezo vya kuondoa maudhui kutokana na ukiukaji wa faragha.

Amri za mahakama

Iwapo kuna amri ya mahakama ya Marekani inayohusu maudhui yaliyochapishwa kwenye www.youtube.com, unaweza kutuma amri hiyo ya mahakama kwa njia ya barua pepe kwenye anwani hii:

YouTube, Inc., Attn Legal Support

901 Cherry Ave., Second Floor

San Bruno, CA 94066

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
2355977925169817029
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false