Kuanzisha mchango wa Uhisani wa YouTube

Uhisani wa YouTube huwaruhusu watayarishi wasaidie mashirika ya misaada waliyochagua. Vituo vinavyostahiki vinaweza kuchangisha pesa kwa mashirika yasiyo ya faida kwa kuweka kitufe cha kuchanga kwenye video na mitiririko yake mubashara. Watazamaji wanaweza kuchanga moja kwa moja kwenye ukurasa wa kutazama video au katika gumzo la moja kwa moja.

Uhisani wa YouTube haupatikani kwenye video zilizobainishwa kama zinazolenga watoto. Hutaona video zilizobainishwa kama zinazolenga watoto unapoweka video kwenye mchango wako. Kwa maelezo zaidi kuhusu ustahiki na upatikanaji, nenda kwenye sehemu ya Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu Uhisani wa YouTube.

Nafasi ya kipengele cha Super Chat for Good imechukuliwa na kipengele cha Michango ya Gumzo la Moja kwa Moja kama njia ya kuchangisha pesa kwenye gumzo la moja kwa moja. Angalia maelekezo yaliyo hapa chini kuhusu jinsi ya kuweka mchango wako kwenye mtiririko wako mubashara ulioratibiwa na gumzo la moja kwa moja.

Masharti ya kujiunga

Ili kutimiza masharti ya kuchangisha pesa kwa kutumia Uhisani wa YouTube, kituo chako lazima kitimize masharti yafuatayo:
Kidokezo: Unaweza kupata huduma ya kuchangisha pesa kwenye baadhi ya vituo ambavyo havitimizi masharti ya kujiunga yaliyo hapo juu. Tunapanga kufanya huduma ya Uhisani wa YouTube ipatikane katika maeneo mengi siku zijazo.

Maeneo Inakopatikana

Iwapo unaishi katika mojawapo ya nchi au maeneo yafuatayo, unaweza kuweka mipangilio ya Mchango wa Uhisani wa YouTube.

 • Ajentina
 • Austria
 • Ubelgiji
 • Bolivia
 • Kanada
 • Kolombia
 • Korasia
 • Estonia
 • Ufaransa
 • Ujerumani
 • Ghana
 • Hong Kong
 • Aisilandi
 • Indonesia
 • Ayalandi
 • Israeli
 • Italia
 • Kuwaiti
 • Lativia
 • Litwania
 • Lasembagi
 • Malesia
 • Meksiko
 • Montenegro
 • Uholanzi
 • Nyuzilandi
 • Norwe
 • Peruu
 • Ufilipino
 • Polandi
 • Pwetoriko
 • Romania
 • Slovakia
 • Hispania
 • Uswidi
 • Uswizi
 • Tailandi
 • Uturuki
 • Uingereza
 • Marekani

Kuanzisha Mchango wa Uhisani wa YouTube

Unaweza kuanzisha mchango wa Uhisani wa YouTube na kuuweka kwenye video au mitiririko yako mubashara. Kisha mashabiki wanaweza kuchanga pesa kwa kutumia kitufe cha kuchanga kwenye video iliyowekwa au kwenye gumzo la moja kwa moja.

 1. Ingia katika Studio ya YouTube.
 2. Katika menyu ya kushoto, chagua Chuma mapato kisha Uhisani kwenye YouTube.
 3. Bofya Anza kisha Anzisha mchango.
 4. Chagua shirika lisilo la faida la Marekani linalopatikana lililoanzishwa kwa mujibu wa sheria ya 501(c)(3) ambalo ungependa kulichangia. Ikiwa shirika lisilo la faida lililoanzishwa kwa mujibu wa sheria ya 501(c)(3) ambalo ungependa kuchangia halijaorodheshwa, chagua Omba shirika lisilo la faida. Pata maelezo zaidi kuhusu mashirika yasiyo ya faida yanayopatikana.
 5. Fuata maagizo ili uweke maelezo kwenye mchango, kama vile jina, maelezo na washirika. Tunapendekeza pia uweke lengo na kipindi cha mchango. Unaweza kubadilisha wakati wowote.
 6. Weka video au mitiririko mubashara iliyoratibiwa ambayo itakuwa na kitufe cha kuchanga.
 7. Chagua CHAPISHA.

Unaweza pia kuweka mchango wako unapoweka mtiririko wako mubashara kwenye Ukurasa wa Kudhibiti Utiririshaji wa Moja kwa Moja chini ya Mipangilio ya Kina. Pata maelezo zaidi hapa.

Kidokezo: Baada ya tarehe ya kuanza kwa mchango kufika, kitufe cha kuchanga kitaonekana kwenye ukurasa wa kutazama wa video yako au kwenye gumzo la moja kwa moja. Ikiwa umeanzisha mchango na video yako imebainishwa kuwa inalenga watoto, kitufe cha kuchanga hakitaonekana kwenye video yako au kwenye gumzo la moja kwa moja.

Ikiwa ungependa kukuza athari yako, anzisha mchango wa jumuiya. Hatua ya kusasisha sehemu ya “Washirika” itaruhusu kituo chochote kinachoweza kufikia huduma ya Uhisani wa YouTube kujiunga kwenye mchango wako.

Kitufe cha kuchanga kitaonekana kwenye ukurasa wa kutazama wa video yako au kwenye gumzo la moja kwa moja baada ya mchango wako kuanza.

Jiunge kwenye mchango uliopo

Unaweza pia kujiunga kwenye mchango wa jumuiya wa mtayarishi mwingine.

 1. Ingia katika Studio ya YouTube.
 2. Katika menyu ya kushoto, chagua Chuma mapato kisha Uhisani kwenye YouTube.
 3. Bofya Anza kisha Jiunge kwenye mchango.
 4. Chagua kwenye orodha ya michango ya jumuiya inayopatikana.
 5. Weka video au mitiririko mubashara iliyoratibiwa ambayo itakuwa na kitufe cha kuchanga.
 6. Chagua CHAPISHA.
Kidokezo: Utaanza kuona kitufe cha kuchanga kwenye ukurasa wa kutazama wa video yako au kwenye gumzo la moja kwa moja baada ya tarehe ya kuanza kwa mchango.

Kudhibiti mchango wako wa Uhisani wa YouTube

Kwenye "kichupo cha Uhisani kwenye YouTube", unaweza kuangalia kiasi cha pesa ambazo zimechangwa katika mchango. Unaweza pia kubadilisha kampeni, kiasi cha pesa kinacholengwa au kuondoa mchango wakati wowote.

Ili kubadilisha maelezo ya mchango wako:

 1. Ingia katika Studio ya YouTube.
 2. Katika menyu ya kushoto, chagua Chuma mapato kisha Uhisani kwenye YouTube.
 3. Karibu na mchango unaotaka kuubadilisha, chagua Zaidi  kisha Badilisha.

Ili ufute mchango wako na kuondoa kitufe cha kuchanga kwenye video zako, fuata hatua za hapo juu kisha uchague Futa.

Tazama jinsi ya kuanzisha mchango kwenye Uhisani wa YouTube

How to Set Up a Fundraiser | YouTube Giving

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Programu za Google
Menyu kuu