Dai la mtu mwenyewe ni nini?

Kwa sasa tunasambaza mabadiliko 2 kwenye Ukurasa wa maelezo wa Hakimiliki ya Video:

  1. Muundo wa ukurasa: Tumesasisha muundo wa ukurasa. Ikiwa unatafuta jina la mlalamikaji na maelezo ya sera ya madai , wekelea kiashiria juu ya safu mlalo ya "Athari kwenye video".
  2. Kichupo cha hakimiliki: Kwenye ukurasa wa Maelezo ya video, tumeongeza kichupo kipya cha Hakimiliki ili uweze kufikia maelezo ya hakimiliki kwa urahisi kupitia ukurasa wa Maelezo ya video yoyote.

Kumbuka kwamba maelezo yanayopatikana na chaguo za kujibu madai hazijabadilika.

Video inaweza kupata dai ambalo limewekwa na mwenyewe ikiwa mwenye hakimiliki atatumia zana ya Kuweka Dai Mwenyewe kutambulisha maudhui yake kwenye YouTube ambayo yametumiwa bila ruhusa yake.

Unachopaswa kujua kuhusu madai ya kuweka mwenyewe

  • Madai ya kuweka mwenyewe ni tofauti na madai ya Content ID. Madai ya Content ID huzalishwa kiotomatiki wakati video iliyopakiwa inalingana na video nyingine (au sehemu ya video) katika mfumo wa YouTube wa Content ID.
  • Zana ya kutumia unapodai mwenyewe inatumiwa na wenye hakimiliki ambao wameonyesha hitaji la kutumia zana hiyo na wana ujuzi wa kina kuhusu Content ID. Zana hii imewapa wenye hakimiliki njia ya kudai wenyewe video ambazo hazijalinganishwa na Content ID.
  • Madai ambayo mtu anaweka mwenyewe yanapaswa kuwa na muhuri sahihi wa wakati ili watayarishi wajue ni maudhui yapi haswa yanadaiwa. Wenye hakimiliki hawawezi kutumia zana ya kutumia Unapodai Mwenyewe kwa lengo lolote lingine.
Uwezo wa kufikia Zana ya Kutumia Unapodai Mwenyewe utabatilishwa au, ikihitajika, ushirikiano na YouTube utasimamishwa ikiwa wenye hakimiliki watachagua muhuri wa wakati usio sahihi kwa kurudia. Ikiwa unaamini kuwa muhuri wa wakati unaodaiwa kwenye video yako si sahihi, unaweza kuwasiliana na timu yetu ya Usaidizi kwa Watayarishi.

Ninaweza kufanya nini ikiwa kuna mtu ambaye ameweka dai mwenyewe kwenye video yangu?

Tools to Resolve Manual Content ID Claims - Copyright on YouTube

Kulingana na hali, una chaguo kadhaa ikiwa mtu ameweka dai mwenyewe kwenye video yako:

Usichukue hatua
Iwapo unaamini kwamba dai ni sahihi, unaweza kutochukua hatua yoyote na uache dai kwenye video yako. Unaweza pia kubadili uamuzi wako baadaye.
Kuondoa maudhui yanayodaiwa

Iwapo unaamini kuwa dai ni sahihi, unaweza kuondoa maudhui yanayodaiwa bila kupakia video mpya. Ukifanya hivyo, chaguo zozote kati ya hizi zitaondoa dai kiotomatiki:

  • Kata sehemu: Unaweza kuondoa sehemu inayodaiwa kwenye video yako.
  • Badilisha wimbo: Iwapo sauti katika video yako imedaiwa, unaweza kubadilisha wimbo wako wa sauti uweke sauti nyingine kutoka kwenye Maktaba ya Sauti katika YouTube.
  • Sitisha sauti ya wimbo: Iwapo sauti katika video yako imedaiwa, unaweza kusitisha sauti ambayo imedaiwa. Unaweza kuchagua iwapo ungependa kusitisha wimbo au sauti yote katika video.
Gawa mapato
Iwapo umejiunga katika Mpango wa Washirika wa YouTube na muziki ulio katika video yako umedaiwa, huenda ukaweza kugawana mapato na mchapishaji wa muziki.
Kupinga dai

Iwapo unaamini kuwa dai si sahihi, unaweza kupinga dai kama una uhakika una haki zote zinazohitajika za kutumia maudhui yanayodaiwa.

Iwapo unapanga kupinga dai na ulikuwa ukichuma mapato kwenye video yako, hakikisha kuwa unafahamu utaratibu wa uchumaji wa mapato wakati wa mzozo. Kumbuka kuwa YouTube haileti upatanisho wakati wa mizozo ya hakimiliki.

Ukipinga dai bila sababu halali, mwenye hakimiliki anaweza kuomba kuondolewa kwa video yako. Tukipata ombi halali la kuondoa video kwa kukiuka hakimiliki kwenye video yako, akaunti yako itapokea onyo la hakimiliki.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
10003116284038943427
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false