Angalia mapato yako ya YouTube

Kutokana na vita vinavyoendelea Ukraini, tutasimamisha kwa muda kuwapatia matangazo ya Google na YouTube watumiaji walio nchini Urusi. Pata maelezo zaidi.

Tunakuletea toleo jipya la beta linaloleta maelezo ya malipo kwenye kichupo cha 'Chuma mapato' cha programu ya vifaa vya mkononi ya Studio ya YouTube. Toleo hili la beta litawapatia watayarishi wanaostahiki mbinu rahisi ya kuelewa jinsi mapato yao yanavyobadilika kuwa malipo. Kwa kutumia toleo hili la beta, unaweza kuangalia:
  • Hatua ulizopiga kuelekea malipo yako yanayofuata
  • Historia yako ya malipo ya miezi 12 iliyopita ikijumuisha tarehe, kiasi ulicholipa na uainishaji wa malipo
Pata maelezo zaidi kwenye chapisho letu la jukwaa .

Ikiwa umejiunga kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube, kichupo cha Mapato katika Takwimu za YouTube huonyesha maudhui yanayochuma mapato mengi zaidi na vyanzo vya mapato vinavyoleta faida zaidi. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuchuma mapato kwenye YouTube.

Kidokezo: Kadiri vyanzo vyetu vya uchumaji wa mapato vinavyoendelea kubadilika, unaweza kuona mabadiliko kwenye kichupo cha Mapato katika Takwimu za YouTube, ikiwa ni pamoja na uchanganuzi wa kina zaidi wa mapato. Uchanganuzi huu huwapa watayarishi wa miundo anuwai fursa ya kutathmini kwa kina vyanzo vyao vya mapato na kuimarika ili kukuza biashara zao. Endelea kusoma ili upate maelezo zaidi.

Kumbuka: Huchukua siku 2 ili mapato yaonekane kwenye Takwimu za YouTube.

Tazama ripoti zako za mapato

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Katika menyu ya kushoto, chagua Takwimu .
  3. Kwenye menyu ya juu, chagua Mapato.

Kiasi cha mapato unayochuma

Ripoti hii inakuonyesha kiasi cha mapato ambacho chaneli yako imepata katika miezi 6 iliyopita, ikichanganuliwa kwa mwezi.

Kiasi cha pesa unachopata kinategemea marekebisho kutokana na:

Iwapo makadirio ya mapato yako yanabadilika, huenda ni kwa sababu ya marekebisho haya. Marekebisho haya hufanyika mara mbili baada ya mapato uliyopata kuonekana katika Takwimu za YouTube:

  • Marekebisho ya kwanza hufanyika baada ya wiki 1, ili kutoa makadirio kamili zaidi.
  • Marekebisho ya pili hufanyika katikati ya mwezi unaofuata na yanaonyesha mapato yako kwa ujumla.

Jinsi unavyochuma mapato

Ripoti hii inatoa muhtasari wa makadirio ya mapato kutoka kila chanzo cha mapato. Mifano ya vyanzo vya mapato ni pamoja na Matangazo kwenye Ukurasa wa Kutazama, Matangazo katika Mipasho ya Video Fupi, Uanachama, Supers, Maduka Yaliyounganishwa na Washirika wa Ununuzi. Unaweza kuchagua chanzo ili uone uchanganuzi wa kina wa mapato.

Utendaji wa maudhui

Ripoti hii inaonyesha mapato yaliyopatikana kwenye video, Video Fupi na mitiririko yako mubashara. Ripoti pia inajumuisha Mapato kwa Kila Mara Elfu Moja za Kutazamwa (RPM).

Ripoti hii pia hukuonyesha maudhui yaliyo na makadirio ya juu zaidi ya mapato, yaliyoainishwa kulingana na aina za muundo (video, Video Fupi, mitiririko mubashara).

Angalia mapato yako ya mwisho

Kuhusu mapato ya mwisho

  • Mapato yako ya mwisho yanaonekana tu kwenye akaunti yako ya AdSense katika YouTube.
  • Mapato ya mwisho kwenye AdSense katika YouTube yanaweza kuwa tofauti na mapato yako yanayokadiriwa katika Takwimu za YouTube. Kwa mfano, huenda hatua ya kuzuia kodi ikaathiri mapato yako ya mwisho, ikiwa itatumika. Hatua zozote za kuzuia kodi zitaonekana kwenye akaunti yako ya AdSense katika YouTube.
  • Mapato ya mwisho ya mwezi uliotangulia huwekwa kwenye salio la akaunti yako kati ya tarehe 7 na 12 ya kila mwezi.

Ili uangalie mapato yako ya mwisho kwenye AdSense katika YouTube:

  1. Ingia katika akaunti yako ya AdSense katika YouTube.
  2. Upande wa kushoto, chagua AdSense katika YouTube.
  3. Salio lako la sasa la mapato yako ya YouTube na kiasi cha malipo yako ya mwisho huonyeshwa. Unaweza pia kufikia nyenzo mahususi za YouTube.

Vipimo unavyopaswa kujua

Mapato ya matangazo kwenye Ukurasa wa Kutazama Makadirio ya mapato kutoka AdSense katika YouTube, matangazo ya DoubleClick na YouTube Premium katika kipindi na eneo lililochaguliwa. Idadi hii haijumuishi mapato yanayotokana na matangazo yoyote ya mpango wa matangazo yanayouzwa na washirika.
Mapato ya matangazo ya Mipasho ya Video Fupi Makadirio ya mapato kutoka kwenye matangazo ya Mipasho ya Video Fupi na YouTube Premium kwa kipindi kilichochaguliwa.
Mapato ya uanachama Makadirio ya mapato kutoka kwenye uanachama na uanachama unaotolewa kama zawadi kwa kipindi kilichochaguliwa.
Mapato ya Supers Makadirio ya mapato kutoka Supers, kama vile Super Chat, Super Stickers na Shukrani Moto.
Mapato ya washirika wa ununuzi Makadirio ya mapato yanayotokana na bidhaa za chapa zingine zinazoangaziwa katika maudhui yako.
Jumla ya mauzo Makadirio ya mauzo kutoka kwa washirika wa uuzaji wa rejareja.
Oda Makadirio ya idadi ya oda zinazowekwa kutoka kwa washirika wa uuzaji.
Idadi ya mibofyo kwenye bidhaa Jumla ya idadi ya mibofyo kwenye bidhaa inayofanywa na watazamaji kwenye bidhaa zilizowekewa lebo.
Bidhaa maarufu Bidhaa zako zilizoorodheshwa kulingana na idadi ya mibofyo kwenye bidhaa.
Maudhui yanayokupa mapato zaidi Bidhaa zako zilizoorodheshwa kulingana na makadirio ya mapato yanayopatikana.
Mapato ya Kuweka Lebo kwenye Bidhaa Makadirio ya mapato kutoka katika Hazina ya Ununuzi kwenye YouTube kwa kipindi kilichochaguliwa.
Kichezaji cha YouTube cha Elimu Makadirio ya mapato kutoka kwenye maudhui yako yakitazamwa kwenye mifumo ya teknolojia ya elimu.
Makadirio ya mapato (mapato) Jumla ya makadirio ya mapato yako (mapato halisi) kutoka katika vyanzo vya mapato vya YouTube kwa kipindi na eneo lililochaguliwa.
Makadirio ya mapato (mshirika) Asilimia za faida unazopata kutokana na mauzo ya awali ambazo bado hazijaidhinishwa ili ulipwe. Kiasi hiki cha pesa hukokotolewa kwa kuondoa bidhaa zilizorejeshwa kutoka katika asilimia za faida inayosubiri kushughulikiwa. Kwa kawaida dirisha la kurejesha bidhaa huchukua muda wa siku 30 hadi 90.
Asilimia za faida zilizoidhinishwa Asilimia za faida unazopata kutokana na mauzo ya awali ambazo zimeidhinishwa ili ulipwe.

Miamala

Idadi ya miamala kutoka Supers kwa kipindi na eneo lililochaguliwa.

Makadirio ya uchezaji wa video unaochuma mapato

Uchezaji wa video unaochuma mapato ni wakati ambapo mtazamaji anatazama video yako na kuonyeshwa angalau onyesho moja la tangazo. Inaweza pia kuonyesha mtazamaji anapoacha kutazama wakati wa tangazo la mwanzo bila kufikia video yako.

Utazamaji

Idadi halali ya mara ambazo chaneli na video zako zilitazamwa.

Wastani wa kipindi cha kutazama

Makadirio ya wastani wa dakika zilizotazamwa kwa kila tukio la kutazama katika kipindi na video uliyochagua.

Muda wa kutazama (saa)

Muda waliotumia watazamaji kutazama video yako.

Kiasi ambacho watangazaji hulipia Mapato yako kwa kila mara 1,000 za uchezaji wa video unaochuma mapato ambapo tangazo moja au zaidi yanaonyeshwa.
Mapato kulingana na aina ya tangazo Mapato yamegawanywa kulingana na aina ya tangazo, kama vile matangazo ya video yanayoweza kurukwa, matangazo yenye maudhui anuai, matangazo ya bamba na matangazo yasiyorukika.
Viwango vya uanachama Mapato yamegawanywa kulingana na kiwango cha uanachama, kama vile kiwango cha mfuatiliaji, shabiki mkuu na VIP.
Jumla ya wanachama Mapato yako kwa jumla ya wanachama na wanachama wanaoendelea. Wanachama wanaoendelea hukokotolewa kwa kuondoa wanachama waliokatisha uanachama kwenye jumla ya wanachama. Pata uchanganuzi wa jumla ya wanachama ikijumuisha:
  • Wanachama walio na uanachama unaojirudia
  • Wanachama walio na uanachama unaotolewa kama zawadi (wa muda mfupi)
Sehemu ambapo wanachama hujiunga Angalia ni maudhui gani yanayoleta idadi kubwa zaidi ya uanachama, pamoja na kutoa beji za “wanachama pekee” kwa wanachama katika chaneli.
Sababu ya kuacha uanachama Pata maarifa ikiwa watazamaji wa kutosha hujibu utafiti wanapoacha uanachama wao.
Jinsi vipengele vya Supers vinavyochuma mapato Mapato hugawanywa kulingana na Super Chat, Super Stickers na Shukrani Moto.
Bidhaa maarufu Bidhaa ulizotangaza zilizopata mibofyo zaidi.
Maonyesho ya duka lililounganishwa Idadi ya maonyesho yaliyokuwa kwenye duka lako lililounganishwa.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
13414660512889276697
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false