Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu ugunduzi na utendaji

Mfumo wa YouTube wa utafutaji na ugunduzi huwasaidia watazamaji wapate video ambazo kuna uwezekano mkubwa wa kuzitazama na kuzidisha kuridhika kwa watazamaji kwa muda mrefu. Pata majibu ya maswali yanayohusu utendaji wa chaneli na video yako katika sehemu inayofuata ya Maswali Yanayoulizwa Sana.

Utafutaji na Ugunduzi kwenye YouTube: Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu 'Algoriti' na Utendaji

Pata vidokezo vya kugundua video kwa watayarishi.

Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu Ugunduzi

YouTube huchagua vipi video za kutangaza?

Mfumo wetu wa mapendekezo hubainisha kundi bora zaidi la video za kuonyesha hadhira yako kwa kuzingatia:
  • Maudhui wanayotazama
  • Maudhui ambayo hawatazami
  • Maudhui wanayotafuta
  • Maudhui waliyopenda na wasiyopenda
  • Maoni ya ‘Sivutiwi’

Nitafanyaje ili video zangu zitangazwe kwa hadhira kubwa zaidi?

Si lazima uwe mtaalamu katika algoriti au takwimu ili ufanikiwe kwenye YouTube, badala yake, lenga kuifahamu hadhira yako. Mfumo wetu wa mapendekezo hautangazi video kwa hadhira yako lakini hutafuta video kwa ajili ya hadhira yako inapotembelea YouTube. Video zinaorodheshwa kulingana na utendaji na ufaafu wazo kwa hadhira yako, si video zote zimetimiza masharti ya kupendekezwa.

Video hupangwa vipi kwenye Ukurasa wa kwanza?

Ukurasa wa kwanza ni sehemu ambayo hadhira yako huona inapofungua programu ya YouTube au kutembelea YouTube.com. Ni sehemu ambako tunalenga kuweka mapendekezo yaliyowekewa mapendeleo, yanayofaa zaidi kwa kila mtazamaji. Wakati hadhira yako inatembelea Ukurasa wa kwanza, YouTube huonyesha video kutoka kwenye vituo inavyofuatilia. Video zilizotazamwa na watazamaji kama hawa na video mpya pia huonyeshwa. Uteuzi wa video unalingana na:
  • Utendaji -- Jinsi video yako inavyovutia na kuwaridhisha watazamaji kama hawa, miongoni mwa vigezo vingine.
  • Historia ya mambo uliyotafuta na video ulizotazama -- Mara ambazo hadhira yako hutazama kituo au mada na mara ambazo tayari tumeonyesha kila video.

Kumbuka kuwa si kila maudhui yametimiza masharti ya kupendekezwa kwenye Ukurasa wa Kwanza wa YouTube.

Video za sehemu ya Zinazovuma huchaguliwa vipi?

Angalia makala haya kuhusu utaratibu wa Video Zinazovuma.

Video hupangwa vipi katika sehemu ya Zinazopendekezwa chini ya ‘Inayofuata’?

Video Zinazopendekezwa hupendekezwa sambamba na video ambayo hadhira yako inatazama chini ya ‘Inayofuata’. Video Zinazopendekezwa hupangwa ili kuipa hadhira yako video ambazo zina uwezekano mkubwa wa kuzitazama baada ya inayocheza. Mara nyingi, video hizi zinahusiana na video ambayo hadhira yako inatazama, lakini pia zinaweza kuwekewa mapendeleo kulingana na historia ya video walizotazama.
Kumbuka kuwa si kila maudhui yametimiza masharti ya kupendekezwa kwenye kurasa za Tazama Video Inayofuata.

Video hupangwa vipi katika sehemu ya Utafutaji?

Jinsi ulivyo mtambo wa kutafuta wa Google, Utafutaji kwenye YouTube hulenga kuonyesha matokeo yanayofaa zaidi kulingana na utafutaji wa maneno muhimu. Video hupangwa kulingana na vigezo vifuatavyo:
  • Jinsi ambavyo mada, maelezo na maudhui ya video yanalingana na utafutaji wa mtazamaji.
  • Video zinazovutia watazamaji zaidi katika utafutaji.
Kumbuka: Matokeo ya utafutaji si orodha ya video zilizotazamwa zaidi katika utafutaji fulani.

Je, hatua ya kubadilisha mada au kijipicha cha video hubadilisha nafasi ya video katika algoriti?

Labda, lakini ni kwa sababu mifumo yetu huchukua hatua kulingana na jinsi watazamaji wanavyotazama video yako kwa njia tofauti, kando na hatua ya kubadilisha mada au kijipicha cha video. Video ikionekana kuwa tofauti na watazamaji, itabadilisha jinsi watazamaji wanavyochukua hatua wanapoonyeshwa video hiyo. Hatua ya kubadilisha mada na kijipicha cha video yako inaweza kuwa njia bora ya kufanya video itazamwe zaidi, lakini haibadilishi kinachofanya kazi.

Ninawezaje kuboresha mada na kijipicha changu kwa ajili ya ugunduzi?

Unaweza kutumia vidokezo hivi kuboresha mada na kijipicha chako kwa ajili ya ugunduzi:

  • Hakikisha kuwa kijipicha chako kinafuata sera yetu ya vijipicha.
  • Tumia mada zinazoshawishi kwenye video zako na mada hizo ziwakilishe maudhui yako kwa njia sahihi.
  • Buni vijipicha vinavyowakilisha maudhui yako kwa njia sahihi.
  • Usitumie vichwa na vijipicha ambavyo:
    • Vinadanganya, kupotosha, vinashtua au ni vyambo vya kubofya: Vinavyowakilisha maudhui ya video visivyo
    • Vinashtua: Vinavyojumuisha lugha chafu au ya kufedhehesha
    • Vinavyochukiza: Vilivyo na picha mbaya au za kuudhi
    • Vilivyo na vurugu iliyokithiri: Vinavyotangaza vurugu au dhuluma isiyofaa
    • Vinavyoaibisha: Vinavyoashiria mambo yanayochochea ngono au tabia ya uzinifu
    • Vimetiwa chumvi: Vinavyotumia HERUFI KUBWA ZOTE au alama ya !!!!! kusisitiza mada kupita kiasi

Mbinu hizi zinaweza kuwafukuza watazamaji watarajiwa kwenye maudhui yako na katika hali nyingine zinaweza kusababisha maudhui yaondolewe kutokana na ukiukaji wa Mwongozo wa Jumuiya.

Je, hali ya uchumaji wa mapato (aikoni ya manjano) inaathiri ugunduzi wa video yangu?

Hapana, mfumo wetu wa utafutaji na mapendekezo haufahamu video ambazo zinatumiwa kuchuma mapato na ambazo hazitumiwi. Tunalenga kupendekeza video ambazo hadhira yako itaridhika nazo, bila kujali hali yake ya kuchuma mapato. Iwapo video yako ina maudhui ya vurugu au ya kuogofya, huenda tukakomesha uchumaji wake wa mapato. Huenda pia isipendekezwe kwa watazamaji wengi kwa sababu haifai. Katika mfano huu, si hatua ya kukomesha uchumaji wa mapato inayosababisha video ipendekezwe mara chache, lakini maudhui yaliyo ndani ya video.

Lebo ni muhimu kwa kiasi kipi?

Si muhimu. Lebo hutumiwa kimsingi ili kusaidia kurekebisha makosa ya kawaida ya tahajia (kwa mfano YouTube badala ya U Tube au You-tube).

Je, hatua ya kuweka mipangilio ya kituo changu ilenge mahali au nchi mahususi itanisaidia kuwafikia watazamaji zaidi katika eneo hilo? (km. Kubadilisha eneo kuwa Marekani hata kama niko Brazili)

Hapana, mipangilio ya mahali haitumiwi kuelezea jinsi video zinavyopendekezwa kwenye YouTube.

Je, matukio ya Kupenda au Kutopenda video yangu huathiri jinsi inavyopendekezwa?

Kwa kiasi fulani. Matukio ya Kupenda na Kutopenda video ni baadhi ya mamia ya ishara tunazozingatia wakati wa kuorodhesha katika nafasi. Mfumo wetu wa mapendekezo hujifunza kutokana na iwapo watazamaji wanachagua au hawachagui kutazama video. Mifumo hii hujifunza kiasi cha video ambacho watazamaji wanatazama na iwapo wanaridhishwa. Utendaji wa jumla wa video yako hubainishwa na mseto wa vigezo hivi.

Iwapo nitapakia video katika mipangilio ya haijaorodheshwa na baadaye nibadilishe iwe ya umma, je hatua hiyo itaathiri vibaya utendaji wa video yangu?

Hapana, la muhimu ni jinsi watazamaji wanavyochukua hatua baada ya video kuchapishwa.

Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu Utendaji

Iwapo utendaji wa mojawapo ya video zangu utakuwa wa chini, je, hali hiyo itaathiri vibaya kituo changu?

La muhimu ni hatua za watazamaji kwenye kila video wanapopendekezewa. Mifumo yetu hutegemea zaidi ishara za viwango vya hadhira na video ili kuamua mapendekezo bora zaidi ya video kwa hadhira yako. Kinachoweza kusababisha kupungua kwa mara ambazo kituo kinatazamwa kwa jumla ni wakati watazamaji wanaacha kutazama video zako nyingi wanapopendekezewa.

Je, utendaji wa chaneli yangu utaathiriwa vibaya iwapo nitaacha kupakia video kwa muda?

Tunakuhimiza uache kupakia kwa muda unapohitaji kufanya hivyo. Tumefanya utafiti kuhusu maelfu ya vituo ambako video ziliacha kupakiwa kwa muda na hatukupata uhusiano wowote kati ya muda wa kuacha kupakia na mabadiliko katika mara ambazo kituo kimetazamwa. Kumbuka kuwa huenda ikachukua muda “kuvutia” hadhira yako tena inaporudi katika hali za kawaida za utazamaji.

Je, ninahitaji kupakia kila siku au angalau mara moja kwa wiki?

Hapana, tumefanya uchanganuzi kwa miaka mingi na tumebaini kuwa kuongezeka kwa mara ambazo kituo kimetazamwa, katika matukio mengi ya upakiaji, hakuhusiani na muda kati ya matukio ya kupakia video. Watayarishi wengi wameimarisha uhusiano na hadhira zao kupitia ubora wa video badala ya wingi wa video. Tunakuhimiza ujiepushe na uchovu. Jambo hili ni muhimu kwa hadhira na masilahi yako.

Wakati bora zaidi wa kuchapisha video ni upi?

Hamna ushahidi wa kuonyesha kuwa wakati wa kuchapisha video huathiri utendaji wa video kwa muda mrefu. Mfumo wetu wa mapendekezo unalenga kutoa video sahihi kwa watazamaji wanaofaa, licha ya wakati ambapo video hiyo ilipakiwa. Hata hivyo, wakati wa kuchapisha ni muhimu kwa miundo kama vile video za Mubashara na Maonyesho ya Kwanza. Angalia Ripoti kuhusu wakati watazamaji wako wamefungua YouTube katika Takwimu za YouTube ili ufahamu wakati wa kupanga Onyesho la Kwanza, au kupanga mtiririko mubashara unaofuata.
Kuchapisha video wakati hadhira yako imechangamka sana kunaweza kuleta manufaa kwa ajili ya utazamaji wa mapema, lakini hakuna ushahidi wa kuonyesha kuwa kutaathiri utazamaji wa video kwa muda mrefu.

Ni nini muhimu kati ya wastani wa asilimia iliyotazamwa na wastani wa kipindi cha kutazama?

Mfumo wetu wa ugunduzi hutumia muda halisi na muda linganifu wa kutazama kama ishara wakati wa kuamua kushirikishwa kwa hadhira na tunakuhimiza ufanye vivyo hivyo. Hakika, tungependa video fupi na ndefu zifanikiwe, kwa hivyo tunakuhimiza utunge video zako katika urefu unaofaa kulingana na maudhui. Kwa jumla, muda linganifu wa kutazama ni muhimu zaidi kwa video fupi na muda halisi wa kutazama ni muhimu zaidi kwa video ndefu. Unaweza kutumia kipimo cha muda wa kutazama ili ufahamu muda ambao watazamaji wangependa kutazama na ubadilishe maudhui yako ipasavyo.

Kwa nini mara ambazo video zimetazamwa ni chini kuliko idadi ya wanaofuatilia?

Idadi ya wanaofuatilia chaneli yako huonyesha idadi ya watazamaji ambao wanafuatilia chaneli yako cha YouTube. Idadi hiyo haiwakilishi idadi ya watazamaji wanaotazama video zako. Kwa wastani, watazamaji hufuatilia vituo kadhaa na huenda wasirudi kutazama kila video mpya unayopakia katika vituo ambavyo wanafuatilia. Ni kawaida pia kwa watazamaji kuendelea kufuatilia vituo ambavyo hawatazami tena. Fahamu hadhira yako kupitia Takwimu za YouTube.

Kwa nini kituo changu kinapata watazamaji wachache kwenye sehemu za Ukurasa wa Kwanza au Video Zinazopendekezwa?

Kuna sababu nyingi zinazofanya mara ambazo kituo kimetazamwa kuongezeka au kupungua kadri muda unavyopita. Zifuatazo ni baadhi ya sababu za kawaida zaidi zinazosababisha kupungua kwa watazamaji kwenye sehemu ya mapendekezo:
  • Hadhira yako inatazama vituo na video nyingine zaidi kwenye YouTube.
  • Hadhira yako inatumia muda mdogo kwenye YouTube.
  • Ulikuwa na video chache zenye utendaji wa juu zaidi au video “ilivuma zaidi” lakini watazamaji hao hawakurudi kutazama zingine.
  • Unapakia video mara chache kuliko kawaida.
  • Umaarufu wa mada ambayo video zako zinalenga unapungua.
Kumbuka kuwa mambo yanayovutia hadhira yako yanaweza kubadilika kadri muda unavyosonga. Ni muhimu uendelee kujaribu mada na miundo mipya kila wakati. Ili kukuza hadhira, watayarishi wanahitaji kudumisha watazamaji waliopo na kuvutia wapya.

Kwa nini video ya zamani imetazamwa zaidi hivi majuzi?

Ni kawaida kwa watazamaji kuanza kuvutiwa na video za zamani. Watazamaji wengi hawatazami video kulingana na mpangilio wa wakati zilipakiwa wala kuamua cha kutazama kulingana na wakati video ilichapishwa. Iwapo watazamaji wanavutiwa na video ya zamani, huenda ni kwa sababu:
  • Umaarufu wa mada ya video yako unaongezeka.
  • Watazamaji wapya wanagundua kituo chako na ‘wanatazama kwa mfululizo’ video zako nyingi za zamani.
  • Watazamaji zaidi wanachagua kutazama video yako wanapoonyeshwa kwenye mapendekezo.
  • Ulibuni video mpya katika mfululizo, hali inayowafanya watazamaji warudi kutazama vipindi vya zamani.
Wakati video ya zamani inaanza kupata watazamaji wengi, tafakari kuhusu aina ya video utakayotoa ambayo itawavutia watazamaji hawa warudi kutazama video zaidi.

Ubainishaji wa ‘Inalenga Watoto’ unaathiri vipi utendaji wa video yangu?

Kuna uwezekano mkubwa wa video ambazo zinalenga watoto kupendekezwa pamoja na video zingine za watoto. Huenda maudhui ambayo hayajajibainisha kwa njia sahihi yasipendekezwe pamoja na video nyingine zinazofanana.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
8525385205033820352
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false