Sera dhidi ya bidhaa au huduma haramu au zilizodhibitiwa


 
Usalama wa watayarishi, watazamaji na washirika wetu ndio kipaumbele chetu cha juu zaidi. Tunamtegemea kila mmoja wenu atusaidie kulinda jumuiya ya kipekee yenye hamasa ya hali ya juu. Ni muhimu kuelewa Mwongozo wetu wa Jumuiya pamoja na jukumu lake kwenye wajibu wetu wa pamoja wa kuifanya YouTube kuwa sehemu salama. Tenga muda usome kwa uangalifu sera iliyo hapa chini. Pia unaweza kuangalia ukurasa huu ili upate orodha kamili ya mwongozo wetu.

YouTube hairuhusu maudhui yanayolenga kuuza huduma au bidhaa fulani zinazodhibitiwa.

Ikiwa utaona maudhui yanayokiuka sera hii, yaripoti. Maagizo ya kuripoti ukiukaji wa Mwongozo wetu wa Jumuiya yanapatikana hapa. Iwapo umeona video au maoni machache ambayo ungependa kuyaripoti, unaweza kuripoti chaneli hiyo.

Unaweza pia kupata nyenzo za ziada.

Jinsi sera hii inavyokuathiri

Iwapo unachapisha maudhui

Usichapishe maudhui kwenye YouTube ikiwa yanalenga kuuza, kuunganisha au kuwezesha ufikiaji wa moja kwa moja wa huduma na bidhaa zozote zilizodhibitiwa zilizoorodheshwa hapa chini. Huruhusiwi kuuza bidhaa hizi au kuwezesha matumizi ya huduma hizi kwa kuchapisha viungo, anwani ya barua pepe, namba ya simu au njia nyingine za kuwasiliana na muuzaji moja kwa moja.

  • Pombe
  • Manenosiri ya akaunti za benki, kadi za mikopo zilizoibwa au maelezo mengine ya fedha
  • Sarafu au hati bandia
  • Dawa za kulevya na dawa nyingine zinazodhibitiwa
  • Vilipuzi
  • Viungo
  • Aina ya wanyama walio katika hatari ya kutoweka au sehemu za aina ya wanyama walio katika hatari ya kutoweka
  • Bunduki na vifuasi vya aina fulani za bunduki
  • Nikotini, ikijumuisha bidhaa za mvuke
  • Tovuti za kucheza kamari za mtandaoni ambazo bado hazijakaguliwa na Google au YouTube
  • Dawa ambazo hazijaagizwa na daktari
  • Huduma za ngono au usindikizaji
  • Huduma za matibabu ambazo hazijaidhinishwa
  • Ulanguzi wa binadamu

Kumbuka: Ikiwa unatoa viungo au maelezo ya mawasiliano kama vile namba za simu, barua pepe au njia nyingine za mawasiliano za mahali ambapo dawa za kulevya zinaweza kununuliwa au dawa za kawaida zinapoweza kununuliwa bila maagizo ya daktari, huenda chaneli yako ikasimamishwa. Angalia mifano hapa chini. 

Pia, maudhui yafuatayo hayaruhusiwi kwenye YouTube:

  • Matumizi au utengenezaji wa dawa za kulevya: Matumizi au utengenezaji wa dawa za kulevya, uuzaji au uwezeshaji wa uuzaji wa dawa za kulevya au zenye madhara madogo, uwezeshaji wa uuzaji wa dawa za kawaida zinazodhibitiwa bila maagizo ya daktari au kuonyesha jinsi ya kutumia steroidi katika maudhui yasiyo ya kielimu. 
  • Maagizo ya udanganyifu: Maudhui yanayotoa maagizo ya udanganyifu katika elimu.

Sera hii hutumika kwa video, maelezo ya video, maoni, mitiririko mubashara na bidhaa au vipengele vingine vyovyote kwenye YouTube. Kumbuka kuwa orodha hii haijataja kila kitu. Tafadhali kumbuka sera hizi pia zinatumika kwenye viungo vya nje vilivyo katika maudhui yako. Hii inaweza kujumuisha URL zinazobofyeka, kuwaelekeza watumiaji kwenye tovuti nyinginezo kwa kutamka kupitia video pamoja na njia nyinginezo. 

Mifano

Ifuatayo ni baadhi ya mifano ya maudhui yasiyoruhusiwa kwenye YouTube.

Kumbuka kuwa orodha hii haijataja kila kitu. 

  • Kuunganisha kwenye tovuti ya uchezaji kamari mtandaoni au tovuti ya kamari ya michezo ambayo haijaidhinishwa.
  • Kuuza pasipoti bandia au kutoa maelezo kuhusu kutengeneza hati rasmi bandia.
  • Utangazaji wa huduma za usindikizaji, ukahaba au kukandwa mwili kimahaba.
  • Maudhui yanayoelekeza jinsi ya kununua dawa kwenye mtandao fiche.
  • Video ya mtumiaji anayefanya ununuzi kwa kutumia programu ambayo inazalisha namba za kadi bandia za mikopo.
  • Kujumuisha kiungo cha kuelekeza kwenye duka la dawa mtandaoni ambalo halihitaji maagizo ya daktari.
  • Maudhui yanayotangaza bidhaa ambayo ina dawa za kulevya, nikotini au dawa zinazodhibitiwa.
  • Uonyeshaji wa matumizi ya dawa za kulevya: Maudhui yasiyo ya kielimu yanayoonyesha udungaji wa dawa za kulevya katika mishipa kama vile heroini, kuvuta au kunusa gundi au kumeza vidonge vyenye asidi.
  • Kutengeneza dawa za kulevya: Maudhui yasiyo ya kielimu yanayofafanua jinsi ya kutengeneza dawa za kulevya.
  • Watoto kutumia pombe au dawa za kulevya: Kuonyesha video za watoto wakinywa pombe, wakitumia vivukisho, sigara za kielektroniki, tumbaku au bangi au kutumia vibaya fataki.
  • Matumizi ya steroidi: Maudhui yasiyo ya kielimu yanayoonyesha jinsi ya kutumia steroidi kwa madhumuni ya kujistarehesha kama vile kujenga misuli.
  • Kuuza dawa zenye madhara kidogo: Kama vile kutoa viungo vinavyoelekeza kwenye tovuti zinazowezesha uuzaji wa bangi au salvia.
  • Kuuza dawa za kulevya: Video zinazoangazia dawa za kulevya kwa lengo la kuziuza. Baadhi ya aina za dawa za kulevya ni pamoja na (kumbuka kuwa hii si orodha kamili na huenda dawa hizi zikawa zinafahamika kwa majina tofauti):
    • Amfetamini
    • Kokeni
    • Dekstromethofani (DXM)
    • Flunitranzipamu
    • Fentanol
    • GHB
    • Heroini
    • Kitamini
    • K2
    • LSD
    • MDMA/ekstasi
    • Meskalini
    • Methamfetamini
    • Aisotonaitazini (ISO)
    • Afyuni
    • PCP
    • Sailosaibini na Sailosaibu (uyoga wa maajabu)

Kumbuka: Ikiwa unatoa viungo au maelezo ya mawasiliano kama vile namba za simu, barua pepe au njia nyingine za mawasiliano za mahali ambapo dawa za kulevya zinaweza kununuliwa au dawa za kawaida zinapoweza kununuliwa bila maagizo ya daktari, huenda chaneli yako ikasimamishwa.

Tafadhali kumbuka kuwa hii ni baadhi ya mifano tu na usichapishe maudhui iwapo unaona kuwa yanaweza kukiuka sera hii.

Maudhui yenye mipaka ya umri

Wakati mwingine maudhui hayakiuki sera zetu, lakini huenda hayafai kwa watazamaji walio na umri wa chini ya miaka 18. 

Mifano ya maudhui yenye mipaka ya umri

  • Maudhui yanayotangaza kituo cha kuuza bangi.
  • Maudhui yanayotoa maoni kuhusu chapa za sigara za kieletroniki zenye nikotini.

Kitakachofanyika iwapo maudhui yanakiuka sera hii

Iwapo maudhui yako yanakiuka sera hii, tutaondoa maudhui hayo na kukutumia barua pepe ili kukufahamisha. Ikiwa hatuwezi kuthibitisha kuwa kiungo ulichochapisha ni salama, huenda tukakiondoa. Kumbuka kuwa URL zinazokiuka sera zinazochapishwa kwenye video husika au katika metadata ya video zinaweza kusababisha tuondoe video husika.

Ikiwa hii ni mara yako ya kwanza kukiuka Mwongozo wetu wa Jumuiya, huenda ukapewa tahadhari bila adhabu kwenye chaneli yako. Utakuwa na fursa ya kushiriki katika mafunzo ya sera ili kuruhusu muda wa tahadhari uliopewa uishe baada ya siku 90. Hata hivyo, ikiwa utakiuka sera hiyo tena ndani ya kipindi hicho cha siku 90, muda wa tahadhari hautaisha na chaneli yako itapewa onyo. Ukikiuka sera tofauti baada ya kukamilisha mafunzo, utapewa tahadhari nyingine.

Ikiwa utapokea maonyo 3 katika kipindi cha siku 90, chaneli yako itasimamishwa. Pata maelezo zaidi kuhusu mfumo wetu wa maonyo.

Tunaweza kusimamisha chaneli au akaunti yako kwa ukiukaji wa mara kwa mara wa Mwongozo wa Jumuiya au Sheria na Masharti. Tunaweza pia kusimamisha chaneli au akaunti yako baada ya tukio moja la ukiukaji kwa kiasi kikubwa au chaneli ikikiuka sera mara kwa mara. Huenda tukazuia watu wanaorudia kufanya makosa wasishiriki katika mafunzo ya sera siku zijazo. Pata maelezo zaidi kuhusu kufungwa kwa chaneli au akaunti.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
10677626258347160177
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false