Sera ya mashirika yenye itikadi kali au ya kihalifu


Usalama wa watayarishi, watazamaji na washirika wetu ndio kipaumbele chetu cha juu zaidi. Tunamtegemea kila mmoja wenu atusaidie kulinda jumuiya ya kipekee yenye hamasa ya hali ya juu. Ni muhimu kuelewa Mwongozo wetu wa Jumuiya pamoja na jukumu lake kwenye wajibu wetu wa pamoja wa kuifanya YouTube kuwa sehemu salama. Tenga muda usome kwa uangalifu sera iliyo hapa chini. Pia unaweza kuangalia ukurasa huu ili upate orodha kamili ya mwongozo wetu.

YouTube hairuhusu maudhui yanayolenga kusifu, kutangaza au kusaidia mashirika yenye itikadi kali au ya kihalifu. Mashirika haya hayaruhusiwi kutumia YouTube kwa shughuli yoyote, ikiwa ni pamoja na kusajili wanachama.

Ikiwa utaona maudhui yanayokiuka sera hii, yaripoti. Maagizo ya kuripoti ukiukaji wa Mwongozo wetu wa Jumuiya yanapatikana hapa. Iwapo umeona video au maoni machache ambayo ungependa kuyaripoti, unaweza kuripoti chaneli hiyo.

Iwapo unaamini mtu yeyote yupo hatarini, unapaswa kuwasiliana na taasisi ya utekelezaji wa sheria ili uripoti hali hiyo mara moja.

Jinsi hali hii inavyokuathiri

Ikiwa unachapisha maudhui

Usichapishe maudhui kwenye YouTube ikiwa yanalingana na maelezo yoyote yaliyo hapa chini.

  • Maudhui yanayotayarishwa na mashirika yenye itikadi kali, au ya kihalifu au kigaidi
  • Maudhui yanayosifu au kuwaenzi magaidi au wahalifu mashuhuri au wenye itikadi kali ili kuwahamasisha watu wengine kutekeleza vitendo vya vurugu
  • Maudhui yanayosifu au kutetea vitendo vya vurugu vilivyofanywa na mashirika yenye itikadi kali, ya kihalifu au ya kigaidi
  • Maudhui yanayolenga kusajili wanachama wapya ili wajiunge na mashirika yenye itikadi kali, ya kihalifu au ya kigaidi
  • Maudhui yanayoonyesha mateka au kuchapishwa kwa nia ya kuomba, kutishia au kuogofya kwa niaba ya shirika la kihalifu, lenye itikadi kali au la kigaidi
  • Maudhui yanayoonyesha alama za cheo, nembo au ishara za mashirika yenye itikadi kali, ya kihalifu au kigaidi kwa nia ya kusifu au kutangaza mashirika hayo
  • Maudhui yanayochochea au kutangaza matukio ya vurugu yanayosikitisha, kama vile ufyatuaji wa risasi shuleni

YouTube inategemea mambo mengi, ikiwa ni pamoja na uteuzi wa serikali na mashirika ya kimataifa, ili kubainisha ni nini kinajumuisha mashirika ya uhalifu au ya kigaidi. Kwa mfano, huwa tunafunga chaneli yoyote ambayo tuna sababu za kutosha kuamini kwamba mmiliki wa akaunti ni mwanachama wa shirika linalofahamika la kigaidi, kama vile Kundi la Kigaidi la Kigeni (Marekani) au shirika lililobainishwa na Umoja wa Mataifa.

Ikiwa unachapisha maudhui yanayohusiana na ugaidi au uhalifu kwa malengo ya kielimu, kiuhalisia, kisayansi au kisanaa, kumbuka kutoa maelezo ya kutosha kwenye video au sauti yenyewe ili watazamaji waelewe muktadha. Video yenye utata au ya kuogofya ambayo ina muktadha unaojitosheleza inaweza kuwekewa mipaka ya umri au skrini ya onyo.

Sera hii hutumika kwa video, maelezo ya video, maoni, mitiririko mubashara na bidhaa au vipengele vingine vyovyote kwenye YouTube. Kumbuka kuwa orodha hii haijataja kila kitu. Tafadhali kumbuka kuwa sera hizi pia zitatumika kwa viungo vya nje katika maudhui yako. Hii inaweza kujumuisha URL unazoweza kubofya, kuwaelekeza watumiaji kwenye tovuti nyingine katika video kwa kutamka, pamoja na njia zingine.

Mifano

Ifuatayo ni baadhi ya mifano ya maudhui yasiyoruhusiwa kwenye YouTube.

  • Upakiaji upya wa maudhui ghafi na ambayo hayajarekebishwa yaliyotayarishwa na mashirika ya kigaidi, kihalifu, au yenye itikadi kali
  • Kuenzi viongozi wa magaidi au uhalifu wao kupitia nyimbo au kufanya kumbukizi
  • Kuenzi mashirika ya kigaidi au kihalifu kupitia nyimbo au kufanya kumbukizi
  • Maudhui yanayoelekeza watumiaji kwenye tovuti zinazounga mkono itikadi za ugaidi, zinazotumika kusambaza maudhui yaliyopigwa marufuku au zinazotumiwa kusajili wanachama
  • Video iliyorekodiwa na mhalifu wakati wa tukio hatari au kubwa la vurugu, ambapo silaha, vitendo vya vurugu au waathiriwa waliojeruhiwa wanaonekana au wanasikika
  • Viungo vya tovuti za nje zilizo na matamko ya wavamizi wenye vurugu
  • Maudhui ya mchezo wa video ambayo yamebuniwa au yameboreshwa ("yamerekebishwa") ili kutukuza tukio la vurugu, wahalifu au kuunga mkono mashirika ya uhalifu, itikadi kali au ugaidi
  • Kuhamasisha vurugu dhidi ya raia
  • Kuchangia mashirika hatari ya kihalifu, yenye itikadi kali au ya kigaidi

Tafadhali kumbuka kuwa hii ni baadhi ya mifano tu na usichapishe maudhui iwapo unaona kuwa yanaweza kukiuka sera hii.

Hatua zinazochukuliwa iwapo maudhui yanakiuka sera hii

Iwapo maudhui yako yatakiuka sera hii, tutaondoa maudhui hayo na kukutumia barua pepe ili kukufahamisha.

Ikiwa hii ni mara yako ya kwanza kukiuka Mwongozo wetu wa Jumuiya, huenda ukapokea tahadhari. Vinginevyo, tunaweza kukipa kituo chako onyo. Ukipata maonyo 3 ndani ya siku 90, kituo chako kitafungwa. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu mfumo wetu wa maonyo hapa.

Hali ya ukiukaji inaweza kusababisha kipengele cha uchumaji wa mapato kizimwe kwenye akaunti zako zozote kwa mujibu wa sera za uchumaji mapato wa vituo kwenye YouTube Hatua hii inaweza kujumuisha maonyo. Iwapo unafikiri kuwa tumekosea, unaweza kukata rufaa. Ukiukaji huo ukibatilishwa, unaweza kutuma ombi la uchumaji wa mapato mara tu utakapotimiza masharti katika Studio ya YouTube.

Tunaweza kusimamisha chaneli au akaunti yako kwa ukiukaji wa mara kwa mara wa Mwongozo wa Jumuiya au Sheria na Masharti. Tunaweza pia kusimamisha chaneli au akaunti yako baada ya tukio moja la ukiukaji kwa kiasi kikubwa au chaneli ikikiuka sera mara kwa mara. Huenda tukazuia watu wanaorudia kufanya makosa wasishiriki katika mafunzo ya sera siku zijazo. Pata maelezo zaidi kuhusu kufungwa kwa chaneli au akaunti.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
95246390690661589
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false