Majukumu ya Wadhibiti wa Maudhui na uwezo wa kufikia vipengele

Vipengele hivi vinapatikana tu kwa washirika wanaotumia Kidhibiti Maudhui cha Studio ya YouTube.

Nini kitatokea ikiwa utakiuka sera za YouTube

Wadhibiti wa maudhui wanaoshindwa kufuata sera za YouTube wanaweza kupokea maonyo rasmi iwapo YouTube itabaini kuwa wametumia vibaya vipengele vya CMS kwa ulegevu, kimakusudi au kwa njia hatari. Pia, YouTube inaweza kuondoa maudhui yoyote yaliyopangishwa au yaliyowasilishwa ambayo yanakiuka sheria na masharti au sera za YouTube. Arifa rasmi za tahadhari zinaweza kuathiri ustahiki wa kampuni yako kwenye programu fulani za YouTube na vipengele vya CMS, kwa hivyo ni muhimu uwe na udhibiti wa kutosha wa ndani ili kuzuia ufikiaji usioidhinishwa kwenye mifumo yako na kutii sera, mwongozo na masharti yote ya YouTube.

Kupoteza uwezo wa kufikia vipengele vya Mfumo wa Kudhibiti Maudhui (CMS)

Pamoja na maonyo rasmi, washirika wanaotumia vibaya vipengele vya Mfumo wa Kudhibiti Maudhui (CMS) wanaweza kupoteza uwezo wa kufikia vipengele hivyo au vipengele vingine vinavyohusiana. Kwa kawaida kizuizi hiki ni cha muda na huwepo kwa kipindi fulani cha muda kilichowekwa. Huenda pia tukakuzuia kwa muda kufikia vipengele vya Mfumo wa Kudhibiti Maudhui (CMS) ili kuzuia tishio la hatari kwenye mfumo huo. Kipindi cha muda ambao mshirika anahitaji kusubiri kabla ya kupata tena idhini ya kufikia kipengele hutegemea vigezo kadhaa, kama vile kiwango cha ukiukaji, sababu ya ukiukaji huo, athari kwa biashara ya mshirika na historia ya ukiukaji ya mshirika huyo. Katika baadhi ya matukio, tunaweza kuona kuwa kupoteza kabisa uwezo wa kufikia vipengele fulani unafaa. Msimamizi wako wa washirika atakuwa na taarifa kuhusu maelezo husika na hatua zitakazofuata. Ikiwa huna msimamizi wa washirika, unaweza kuwasiliana na timu ya Usaidizi kwa Watayarishi ili upate maelezo zaidi.

Majukumu yako ukiwa mdhibiti wa maudhui

Mfumo wa Kudhibiti Maudhui wa YouTube (CMS) ni kifurushi thabiti cha zana kinachoweza kudhuru mfumo wa YouTube kikitumiwa isivyofaa. Wadhibiti wa maudhui wana wajibu wa kuhakikisha kuwa maudhui yote yanayopangishwa na kuwasilishwa (kama vile chaneli, video, video za picha, metadata ya vipengee, marejeleo ya Content ID, n.k.) yanafuata sera na mwongozo wote wa YouTube, ikijumuisha Sheria na Masharti yetu, Mwongozo wa Jumuiya, masharti ya uchumaji mapato na sera za kidhibiti maudhui.

Ukiukaji uliopitiliza na wa mara kwa mara

Tunatilia maanani sana sera hizi. Washirika wanaokiuka sera zetu za kidhibiti maudhui mara kwa mara au kupita kiasi watawekewa vikwazo vikali. Vikwazo hivi vinaweza kuwa pamoja na kupoteza idhini ya kufikia vipengele vya ziada vya Mfumo wa Kudhibiti Maudhui (CMS), kupoteza idhini ya kufikia vipengele mahususi kwa muda mrefu zaidi au kupoteza kabisa uwezo wa kufikia Mfumo wa Kudhibiti Maudhui (CMS) na kusimamishwa kwa mikataba yoyote uliyoweka na YouTube.

Katika hali fulani, tunaweza kukupa “tahadhari ya mwisho” ya kutii sera zetu. Wadhibiti wa maudhui waliopewa arifa rasmi ya tahadhari ya mwisho watapoteza idhini ya kufikia vipengele vyao vingi vya Mfumo wa Kudhibiti Maudhui (CMS) hadi watakapopita ukaguzi wa matumizi mabaya unaofanywa mwaka unaofuata. Wakikiuka zaidi sera zetu za kidhibiti maudhui katika mwaka unaofuata na wakose kuomba na kupita ukaguzi wa matumizi mabaya, mikataba yao itakuwa katika hatari ya kusimamishwa.

Usimamizi wa Wamiliki Wengi wa Maudhui

Kumbuka kwamba ikiwa una wajibu wa usimamizi katika vidhibiti vingi vya maudhui kwenye YouTube, ukiukaji unaotokea kwenye kidhibiti kimoja cha maudhui unaweza kusababisha vikwazo kwenye vidhibiti vyote vya maudhui unavyomiliki. 

Sera za Jumla za Kidhibiti Maudhui

Sera hizi zinatumika kwa kila mshirika aliye na uwezo wa kufikia Mfumo wa Kudhibiti Maudhui wa YouTube

Sera kuhusu uwajibikaji wa chaneli

Ni wajibu wa wadhibiti wa maudhui kuhakikisha kuwa chaneli zote zilizounganishwa zinafuata mwongozo na sera za maudhui za YouTube. Sera hii inatumika kwa maudhui yaliyopakiwa kwenye chaneli Zinazomilikiwa na Kuendeshwa (O&O) na chaneli za Washirika. 

Masharti ya sera

  • Wadhibiti wa maudhui hawapaswi kuwa na zaidi ya matukio 30 ya matumizi mabaya (kama vile kusimamishwa, kusitishwa au kukomeshewa uchumaji wa mapato) katika kipindi cha siku 90. Sera hii inatumika kwa chaneli katika akaunti zako za washirika na zisizo za washirika. 
  • Wadhibiti wa maudhui hawapaswi kuwa na zaidi ya matukio 10 ya matumizi mabaya ya chaneli kwenye akaunti zao zisizo za washirika katika kipindi cha siku 90.

Ukiukaji wa sera

Kupitisha upeo huu kutachukuliwa kuwa ukiukaji mmoja wa sera hii. Ukiukaji wa kwanza katika kipindi cha siku 90 utasababisha kusimamishwa kwa mwezi 1. Katika kipindi cha kusimamishwa, huwezi kuunda au kuunganisha chaneli mpya kwenye Kidhibiti chako cha Maudhui. 

Ukiukaji wa pili katika kipindi cha siku 90 utasababisha kusimamishwa kwa miezi 2. Ukiukaji wa tatu na wa mwisho utasababisha vikwazo, ambavyo vinaweza kuwa pamoja na kusitishwa kwa muda mrefu au kusimamishwa kwa mikataba yako na YouTube.

Unachoweza kufanya ili ufuate sera hii

Sera kuhusu uwekaji wa chaneli
Wadhibiti wa maudhui wanatarajiwa kuwa na uhusiano na chaneli za watayarishi kabla ya kuweka vituo hivyo kwenye mitandao yao. Wadhibiti wa maudhui ambao, miongoni mwa vitu vingine, huwajumuisha watayarishi kupitia mbinu taka au danganyifu au kutumia vibaya mamlaka ya kuunganisha chaneli, wanaweza kupoteza idhini ya kufikia vipengele vya Mfumo wa Kudhibiti Maudhui (CMS).

Masharti ya sera:

  • Ni lazima wadhibiti wa maudhui wadumishe kiwango cha zaidi ya asilimia 90 cha kukubaliwa kwa mialiko yao ya kuunganisha chaneli kila mwezi.
  • Wadhibiti wa maudhui wasiofikisha kiwango cha kukubaliwa cha asilimia 90 wanaweza kuzuiwa kualika chaneli kwenye akaunti zao zote za wamiliki wa maudhui kwa mwezi 1.

Unachoweza kufanya ili ufuate sera hii:

  • Tuma mialiko yako mwanzoni mwa mwezi. Hatua hii huwapa watayarishi wako muda wa kutosha wa kukubali mialiko.
  • Tuma mialiko kwa chaneli unazofahamu pekee na ambazo una uhusiano wa kibiashara nazo.
  • Wasiliana na watayarishi na uwakumbushe kukubali mialiko yao, panapohitajika.
Sera kuhusu ukwepaji wa mifumo
Tunaamini kuwa wadhibiti wa maudhui watasimamia haki na maudhui kwa niaba ya wamiliki wao wa maudhui, watatue matatizo kwenye mitandao yao na watumie Mfumo wa Kudhibiti Maudhui wa YouTube kwa uwajibikaji. Tunatarajia yayo hayo kwenye vipengele vilivyojumuishwa kwenye Mfumo wa Kudhibiti Maudhui wa YouTube. Wadhibiti wa Maudhui wanaotumia vibaya vipengele hivi ili kukwepa mifumo au taratibu za YouTube zilizowekwa wanakiuka imani hiyo na kudhuru mfumo mzima wa YouTube.

Masharti ya sera:

  • Wadhibiti wa maudhui hawaruhusiwi kushiriki katika vitendo vinavyojaribu kukwepa au kuhitilafiana na mifumo, taratibu au sera za YouTube.
  • Kukiuka sera hii kunaweza kuchukuliwa kuwa matumizi mabaya kupita kiasi na kunaweza kusababisha kusimamishwa kwa akaunti zako zote za mmiliki wa maudhui.

Mifano ya ukiukaji wa sera hii ni pamoja na:

  • Kutumia Mfumo wa Kudhibiti Maudhui (CMS) kuchuma mapato kwa njia isiyofaa kutokana na maudhui ambayo hayajatimiza masharti ya uchumaji wa mapato kwenye YouTube. Hii ni pamoja na maudhui yanayokiuka mwongozo wetu wa usalama wa jumuiya na chapa na pia maudhui yasiyoruhusiwa na sheria na kanuni zozote husika.
  • Kuweka mwenyewe umiliki wako kwenye vipengee vya Content ID ambavyo huna maslahi halali ya mali yake ya uvumbuzi, hata kwa muda mfupi.
  • Kutumia mchakato wa kudai mwenyewe Content ID ili kukwepa mchakato wa utatuzi wa mizozo kuhusu madai.
  • Kujumuisha chaneli yoyote kwenye Mfumo wako wa Kudhibiti Maudhui (CMS) ambayo haijaidhinishwa na YouTube katika hali ambazo idhini ya awali inahitajika.
  • Kutumia au kunufaika kutokana na unyemeleaji au kushiriki katika mbinu zilizoundwa ili kuongeza mapato yako kwenye YouTube kupitia njia batili au za ulaghai.        

Sera ya Kidhibiti Maudhui kuhusu maonyo ya hakimiliki
Chaneli inapopokea onyo la hakimiliki, vikwazo vya kiwango cha chaneli hutumika. Washirika wanapaswa kuepuka kuongezeka kwa maonyo ya hakimiliki kwenye chaneli zao zinazodhibitiwa. La sivyo, vikwazo vitawekwa kwenye vidhibiti vyao vya maudhui mbali na sera zilizopo za maonyo ya chaneli. Vikwazo vya maonyo ya washirika huzuia ufikiaji wa vipengele. Hali hii huathiri mmiliki wa maudhui na wamiliki wa maudhui wanaohusishwa naye.

Masharti ya sera:

Mshirika akipokea maonyo 10 ya hakimiliki kwenye chaneli zinazodhibitiwa katika kipindi cha siku 90, mshirika huyo anastahili kufanyiwa ukaguzi wa ziada. Matokeo ya ukaguzi huo yanaweza kuwa pamoja na kupoteza uwezo wa kuunganisha chaneli, kupoteza uwezo wa kupakia video na kusimamishwa kwa makubaliano ya ushirika. Baada ya siku 90, muda wa maonyo ya hakimiliki utakwisha na yataondolewa kwenye chaneli na kwenye jumla ya maonyo ya mmiliki wa maudhui. YouTube pia inahifadhi haki ya kutathmini na kushughulikia masuala ya matumizi mabaya wakati wowote, kwa hiari yake.

Unachoweza kufanya ili ufuate sera hii:

  • Kuwa mwangalifu unapochagua chaneli mpya za kudhibiti. Epuka kuweka chaneli zinazoweza kuongeza jumla ya maonyo yako.
  • Washirika wengi hufanya vyema zaidi wakidumisha idadi ya chaneli zinazomilikiwa na kuendeshwa na wamiliki wa maudhui chini ya 120.
  • Elimisha chaneli unazodhibiti kuhusu hakimiliki na uhakikishe kuwa zinafuata sera za YouTube.
  • Hakikisha unadumisha mifumo inayofaa ya udhibiti wa ndani kadri unavyoongeza idadi ya chaneli unazodhibiti.
Ikiwa unaamini kuwa maonyo yoyote husika si sahihi, huenda ukahitaji kupata maelezo zaidi kuhusu kuwasilisha arifa za kukanusha au kuomba ufutaji wa madai.
Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu Maonyo ya hakimiliki katika Kituo cha Usaidizi.
Sera kuhusu umiliki na ufikiaji kwa uwajibikaji
Katika juhudi za kuimarisha usalama wa mfumo wetu, YouTube inaweza kuzuia, kusimamisha au kusitisha akaunti za Mfumo wa Kudhibiti Maudhui (CMS) ambazo inaamini kuwa zimeathiriwa na wahusika wasiowajibika au wasioruhusiwa. 
  • Wadhibiti wa maudhui watawajibikia kila kitendo kinachotekelezwa kwa kutumia akaunti zao za Mfumo wa Kudhibiti Maudhui (CMS).
    • Hakikisha kuwa una kinga za kutosha zinazofuatilia ufikiaji wa wafanyakazi wako na utiifu wao wa sera zetu. Kampuni zitawajibikia vitendo vya wafanyakazi wao binafsi.
    • Sera hii inatumika pia kwa kampuni za wengine zilizoajiriwa ili kusimamia akaunti ya Mfumo wa Kudhibiti Maudhui (CMS).
  • Haturuhusu kabisa kuwapa wahusika wengine ambao si washirika au wasioruhusiwa idhini ya kufikia akaunti yako ya Mfumo wa Kudhibiti Maudhui (CMS) kwa madhumuni ya kufidiwa au kupata faida nyingine.
    • Usikodishe, kupangisha wala kuuza ufikiaji wa akaunti yako ya Mfumo wa Kudhibiti Maudhui (CMS).
    • Ikiwa umeshirikiana na mhusika mwingine ili asimamie akaunti yako ya Mfumo wa Kudhibiti Maudhui (CMS) kwa niaba yako, ni lazima shirika hilo liwe na makubaliano ya ushirika ya moja kwa moja nasi. 
    • Usitoe idhini ya kufikia akaunti yako ya Mfumo wa Kudhibiti Maudhui (CMS) kwa mashirika (au watu wanaohusishwa nayo) ambayo yana historia ya matumizi mabaya.
    • YouTube ikitambua kwamba mhusika ambaye si mshirika au asiyeruhusiwa amepata idhini ya kufikia akaunti yako ya Mfumo wa Kudhibiti Maudhui (CMS), YouTube inaweza kuchukua hatua. Kwa mfano, YouTube inaweza kubatilisha uwezo wa mtu wa kufikia au kusimamisha mikataba yoyote husika.
Kama mdhibiti wa maudhui, ni sharti uarifu YouTube ikiwa kampuni yako inanunuliwa na kampuni nyingine. Ikiwa umejipatia kampuni iliyo na idhini ya kufikia Mfumo wa Kudhibiti Maudhui (CMS), ni sharti pia uarifu YouTube. Ni lazima utume arifa hizo ndani ya siku 30 baada ya umiliki.
Sera ya upangishaji ya washirika wa muziki
Maudhui yasiyo ya muziki ni sharti yahusiane kwa kiwango kikubwa na vipengee vya muziki vilivyopo kwenye akaunti.
  • Kwa mfano, mahojiano ya wasanii yanaweza kuchukuliwa kuwa yanahusiana kwa kiwango kikubwa.
  • Washirika wa muziki walio na maudhui yasiyo ya muziki wanapaswa kujadili mbinu za usuluhishaji zinazowezekana na wasimamizi wao wa washirika ili kuzuia uwezekano wa kupoteza idhini ya kufikia vipengele, kama vile uwezo wa kuunganisha chaneli.

Sera za Content ID

Sera hizi zinatumika kwa washirika walio na uwezo wa kufikia mfumo wa ulinganishaji wa Content ID. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu kutimiza vigezo vya Content ID katika Kituo cha Usaidizi.

Sera kuhusu maudhui yanayotimiza vigezo vya Content ID
Mfumo wa ulinganishaji wa Content ID ni zana thabiti ya kudhibiti haki zako kwenye YouTube. Kutokana na hali yake nyeti na changamano, ni lazima maudhui yatimize masharti fulani ili yatumiwe kama marejeleo. Ni wajibu wako kufuata masharti haya na kuhakikisha kuwa marejeleo yako yanadai tu video zilizo na mali yako ya uvumbuzi.

Masharti ya sera

  • Ni lazima uwe na haki za kipekee za maudhui yaliyo katika faili ya marejeleo kwa ajili ya maeneo ambako unadai umiliki.
    • Mifano ya maudhui ambayo hayatimizi masharti ya kutumiwa kama marejeleo:
      • Maudhui yaliyopewa leseni ya jumla kutoka kwa mhusika mwingine kama vile utangazaji wa kimaeneo wa tukio kuu la spoti.
      • Maudhui yaliyotolewa chini ya Creative Commons au leseni huria kama hizo.
      • Video, rekodi au tungo zilizo wazi kutumiwa na umma.
      • Klipu kutoka vyanzo vingine zinazotumiwa kwa mujibu wa kanuni za matumizi ya haki.
      • Maudhui yanayouzwa au kupewa leseni kwa kiwango kinachofaa ili yajumuishwe kwenye kazi zingine, kama vile muziki unaotumiwa katika uzalishaji wa video na sauti.

Masharti haya yanatumika kwa vipengee vyote viwili vya sauti na picha vya marejeleo yako. Kwa mfano, ikiwa marejeleo yako ya picha na sauti yana sauti ya wengine isiyo na leseni, maudhui hayo yanapaswa kuondolewa kabla ya uwasilishaji.

  • Ni lazima faili zote za marejeleo ziwe za kipekee kwa namna ya kutosha ili kuruhusu ulinganishaji sahihi.
    • Mifano ya maudhui ambayo hayatimizi masharti ya kutumiwa kama marejeleo:
      • Rekodi za karaoke, rekodi zilizoboreshwa na rekodi za kuiga.
      • Madoido ya sauti, sauti zinazotumiwa chinichini ya maudhui mengine au rekodi za kucheza zikirudia bila kukoma.
      • Rekodi za sauti za maudhui yaliyo wazi kutumiwa na umma au maudhui ya wengine ambayo yanafanana na rekodi nyingine za sauti za maudhui hayo, kama vile muziki wa jadi au miseto fulani.
  • Ni lazima faili zote za marejeleo ziwakilishe kipengee kimoja cha mali ya uvumbuzi.
    • Mifano ya maudhui ambayo hayatimizi masharti ya kutumiwa kama marejeleo:
      • Mikusanyiko ya nyimbo au maudhui ya video fupi.
      • Maudhui yaliyochanganywa au miseto ya mfululizo ya DJ.
      • Orodha za nyimbo bora au rekodi za sauti za albamu kamili.
  • Faili zote za marejeleo zinazotumiwa kuchuma mapato kutokana na maudhui ni lazima zitii sera za maudhui za YouTube.

Vikwazo maalum kwenye maudhui ya michezo ya video

  • Wachapishaji wa michezo ya video ndio tu wanaoweza kuwasilisha marejeleo yenye video za uchezaji au nyimbo halisi za michezo ya video. 
    • Nyimbo halisi za michezo ya video ni rekodi za sauti zilizoundwa kimahususi kwa ajili ya mchezo wa video, wala si nyimbo zilizopewa leseni ya kujumuishwa kwenye mchezo.
    • Sera hii inajumuisha Mfumo wa Kufikia Video Unapohitaji (VOD) wa maudhui ya michezo ya video yanayotiririshwa moja kwa moja. 
      • Tumia Copyright Match Tool au kipengele cha kudai mwenyewe ili ulinde maudhui haya.
  • Vipengee vyote vya rekodi za sauti vya matoleo mengine ya nyimbo halisi za michezo ya video (OST) ni lazima vitumie njia ya kukagua sera.
    • Kwenye vipengee hivi, ulinganishaji wa tuni kwenye tungo zilizopachikwa unaweza kusababisha madai mengi yasiyofaa ambayo yanaweza kukinzana na matamanio ya mchapishaji wa michezo ya video.
Sera kuhusu uwasilishaji wa marejeleo ya Content ID
Wadhibiti wa maudhui wanapaswa tu kuwasilisha faili za marejeleo ambazo zinafaa kwa ulinganishaji wa Content ID. Marejeleo yasiyofaa yana madhara kwa watayarishi na kwa mfumo wa kudhibiti haki wa YouTube. Unaweza kusoma zaidi kuhusu maudhui yanayotimiza vigezo vya Content ID katika Kituo cha Usaidizi.

Masharti ya sera:

  • Wadhibiti wote wa maudhui ni lazima wasiwe na marejeleo ya Content ID yasiyo sahihi yanayozidi asilimia 1 ya katalogi zao za mmiliki wa maudhui na wasipitishe marejeleo 500 yasiyo sahihi ndani ya kipindi cha siku 30.
  • Kwa wamiliki wa maudhui wanaopitisha kiwango hiki, kipengele cha kuwasilisha marejeleo kinaweza kuzuiwa au kuzimwa.
Sera kuhusu kipengele cha Content ID cha kudai mwenyewe

Kuhusu kipengele cha kudai mwenyewe

Kipengele cha kudai mwenyewe huwaruhusu wadhibiti wa maudhui kuweka madai wenyewe kwenye video zilizo na maudhui yao. Kinapaswa tu kutumiwa kusuluhisha matatizo ya kutoa madai katika hali ambapo maudhui yaliyotimiza vigezo vya Content ID hayakudaiwa kiotomatiki. Ikiwa aina ya maudhui haijatimiza vigezo vya Content ID, haipaswi kudaiwa kupitia kipengele cha kudai mwenyewe.


Washirika walioonyesha hitaji kubwa ndio tu wanaopewa idhini ya kufikia zana ya kutumia unapodai mwenyewe. Ili kudumisha mfumo bora wenye haki ambao unaambatana na aina nne za uhuru kwenye YouTube, kipengele cha kudai mwenyewe kina masharti makali ya matumizi.

Vikwazo kwenye maudhui unayopaswa kudai

 Kikwazo  Maelezo
Dai tu video ambazo zina maudhui yaliyo na hakimiliki ambayo unayamiliki peke yako. Dai tu maudhui ambayo yanapatikana ndani ya video iliyopakiwa.

Usidai mwenyewe maudhui (au sehemu za maudhui) ambayo huyamiliki.


Kutumia vibaya kipengele cha kudai mwenyewe kwa ajili ya udhibiti kunaweza kusababisha kupoteza kipengele hicho papo hapo au kabisa, pamoja na vikwazo vingine vinavyowezekana.

Tumia tu kipengele cha kudai mwenyewe ndani ya upeo wa maudhui yanayoweza kudaiwa kwa ulinganishaji wa Content ID.
 
Mfumo wa ulinganishaji wa Content ID unaruhusu tu kudai sauti, video na tuni zinazolingana kati ya video ya aliyepakia na maudhui ya marejeleo yaliyotolewa na mshirika. Madai yote unayotoa mwenyewe ni sharti yaambatane na utendaji huu wa msingi.

Usidai mwenyewe video kulingana na kijipicha au picha tuli.


Usitumie kipengele cha kudai mwenyewe kudhibiti matatizo ya chapa ya biashara, faragha au matatizo mengine yasiyo ya hakimiliki. 

Usidai mwenyewe video zilizo na maonyesho yaliyobuniwa na aliyepakia ya wahusika walio na hakimiliki.

Usidai mwenyewe rekodi za mashabiki za matukio ya moja kwa moja (kama vile michezo ya kuigiza, mifululizo ya vichekesho au michezo ya spoti) isipokuwa kama unamiliki haki za rekodi hiyo mahususi au wewe ni mchapishaji wa muziki anayedai utungo wa muziki. 

Content ID inaruhusu tu udhibiti wa haki kwa ajili ya tungo za muziki, wala si aina nyingine za kazi zilizoandikwa. 

Katika hali nyingine za matumizi, tunapendekeza utume ombi la kuondoa video la kisheria au malalamiko kuhusu faragha.

Usidai mwenyewe video ambazo kwa sasa zinadaiwa, au zilidaiwa hapo awali na kipengee kwa ajili ya maudhui sawa. Kizuizi hiki kinajumuisha kudai mwenyewe video ambazo zina dai la awali lililopingwa kwa ufanisi la maudhui sawa.

Hatua ya kutoa mwenyewe madai yanayofanana ambayo yanalenga maudhui sawa inaweza kuchukuliwa kuwa ukiukaji uliopitiliza wa sera yetu kuhusu Ukwepaji wa Mifumo. 
Usitumie kipengele cha kudai mwenyewe kuunda mpango usiofaa wa ugavi wa mapato miongoni mwa madai yaliyopo kwenye video. Kukiuka sera hii kunaweza kuchukuliwa kuwa ukiukaji uliopitiliza wa sera yetu kuhusu ukwepaji wa mifumo.
Usidai mwenyewe video ikiwa umiliki wako umepachikwa, au unapaswa kupachikwa kwenye vipengee vingine. Usitoe mwenyewe dai la utungo kwenye sehemu ya video ikiwa tayari imedaiwa na kipengee cha rekodi ya sauti kilicho na utungo wako. Umiliki wa tungo unapaswa kupachikwa kwenye rekodi za sauti panapowezekana.

Vikwazo vya jinsi ya kudai maudhui

Kikwazo Maelezo
Unahitaji kukagua mwenyewe maudhui unayodai kabla ya kuwasilisha dai unalotoa mwenyewe.
 
Haturuhusu kuweka otomatiki mchakato wa kudai mwenyewe. Angalia sera kuhusu hatua za kuchukua mwenyewe.
Vipengee vyote unavyotumia kudai mwenyewe ni sharti viwe na metadata sahihi, inayoweza kusomeka na binadamu na maudhui sahihi ya marejeleo. Hali pekee ambapo kanuni hii inaweza kukiukwa ni wakati nakala ya marejeleo ya maudhui yanayodaiwa haifai kwa ulinganishaji au hairuhusiwi na sera yetu ya marejeleo. 

Ijapokuwa vipengee hivi havihitaji marejeleo, ni lazima madai yote yawe ya maudhui sawa ya kipekee na yafafanuliwe kwa usahihi na metadata. (k.m. hakuna vipengee vya ‘kundi' au 'vya kukusanywa vyote').

Vipengee unavyotumia kudai mwenyewe ni sharti viangazie kwa usahihi upeo wa umiliki wako. Kwa mfano, ikiwa wewe ni mtangazaji katika eneo mahususi na unadai video zilizopakiwa upya za maudhui yaliyopewa leseni, huwezi kutumia kipengele cha kudai mwenyewe kuweka sera ya uzuiaji wa jumla ikiwa huna haki za jumla za maudhui hayo.

Zaidi ya hayo, huenda watangazaji wakawa na haki za kuonyesha maudhui yaliyopewa leseni katika eneo fulani, lakini hiyo haimaanishi kila wakati kuwa wana haki za kudai video zilizo na maudhui hayo katika eneo hilo.
Madai yote unayotoa mwenyewe ni lazima yajumuishe mihuri sahihi ya wakati inayobainisha mahali maudhui unayodai yalipo kwenye video. Sehemu mahususi zinazolingana ni lazima zibainishwe kwa mihuri ya wakati ya kipekee.

Kutoa kimakusudi au mara kwa mara mihuri ya wakati inayopotosha kunaweza kuchukuliwa kuwa ukiukaji mkubwa wa sera zetu.
Usidai mwenyewe maudhui yaliyo na sera ya 'kuchuma mapato' ambayo yanakiuka mwongozo wa YouTube wa usalama wa jumuiya au chapa. Hali hii inaweza kuchukuliwa kuwa ukiukajii wa sera yetu kuhusu Ukwepaji wa Mifumo. Soma maelezo zaidi hapa.
Madai unayotoa mwenyewe kuhusu maudhui ya sauti yanayopatikana kwenye sehemu ndogo ya video yanaweza tu kutumia sera ya kuchuma mapato katika hali chache mno. Kwa jumla, madai unayotoa mwenyewe kuhusu matumizi mafupi ya maudhui ya sauti yanaweza tu kutumia sera ya kuzuia au kufuatilia isipokuwa kama maudhui unayodai:
​Ni sehemu ya mkusanyiko wa video, orodha ya muziki bora, au shindano lenye maudhui ya muziki.
  • Ni sehemu ya maudhui ya utangulizi au utamatishaji yanayotumiwa na chaneli maalum.
  • Yapo kwenye video ambayo tayari ina dai sahihi lililopo la Content ID lenye sera ya kuchuma mapato.
  • Yapo kwenye video iliyopakiwa kwenye Chaneli Rasmi ya Msanii inayowakilishwa na mlalamikaji.
  • Yanachukua sehemu kubwa ya video.
Madai unayotoa mwenyewe kuhusu “matumizi yasiyo ya kimakusudi” ya maudhui ya sauti hayawezi kutumia sera ya 'kuchuma mapato', lakini bado unaweza kutumia kwa jumla sera ya 'kufuatilia' au 'kuzuia' kwenye matumizi yoyote ya maudhui yako. Kwa madhumuni ya sera hii, tunafasili “matumizi yasiyo ya kimakusudi” kuwa matukio ambapo:
  • Maudhui hayakuwekwa kwenye video na mtayarishi NA
  • Hakuna uhusiano kati ya mtayarishi na maudhui.

Baadhi ya mifano ya “matumizi yasiyo ya kimakusudi” ni:

  • Runinga inayosikika kutoka chumba kingine cha nyumba au ofisi ya mtayarishi.
  • Muziki kutoka gari lipitalo.

Mifano ya hali ambapo matumizi hayachukuliwi kuwa si ya kimakusudi ni pamoja na:

  • Kuimba, kucheza densi au ngoma kwa kutumia muziki husika.
  • Maudhui yoyote yanayowekwa baada ya kurekodi au kwenye programu za kuhariri.
  • Muziki unaocheza chinichini katika eneo ambapo mtayarishi ana udhibiti wa moja kwa moja wa muziki huo, au kusudi la video ni kunasa sauti, kama vile tamasha.

Content ID na kuzuia mwenyewe maudhui ya ukosoaji

YouTube hairuhusu kuchukua hatua mwenyewe kwenye Content ID kwa madhumuni ya kuzuia maudhui ya ukosoaji. Usichukue hatua mwenyewe kwenye Content ID zinazosababisha kuzuiwa kwa maudhui ambayo 1) yanakukosoa wewe au wateja unaowakilisha na 2) yana madondoo ya kazi yako inayolindwa kwa hakimiliki.
  • Neno “ukosoaji” linamaanisha kuwa madhumuni ya kutumia maudhui hayo ni kukosoa na/au kuonyesha maudhui, wahusika wake, watayarishi wake, au wenye haki za maudhui hayo kwa njia hasi au isiyopendeza.
  • “Hatua za kuchukua mwenyewe” ni pamoja na, lakini si tu, kutumia kipengele cha kudai mwenyewe au kubadilisha sera ya dai lililopo iwe ya kuzuia.
  • Ikiwa unaamini maudhui yamekiuka kazi yako inayolindwa kwa hakimiliki, tuma ombi la kuondoa video la DMCA (Sheria ya Milenia ya Hakimiliki Dijitali) badala yake.
  • Ombi lako la kuondoa video la DMCA (Sheria ya Milenia ya Hakimiliki Dijitali) likikataliwa, bado huruhusiwi kuchukua mwenyewe hatua za kudai maudhui. Hii ni pamoja na, lakini si tu, kudai mwenyewe na kuweka sera ya uzuiaji kwenye maudhui.
Content ID na udhibiti wa kisiasa
Hatua ya kutumia Content ID kuzuia maudhui ya kisiasa ambayo huna haki zinazohitajika ni ukiukaji uliopitiliza na hairuhusiwi kwenye YouTube. Jaribio lolote la kufanya hivyo linaweza kusababisha kusimamishwa kwa akaunti zote za mmiliki wa maudhui za mdhibiti wa maudhui.

Vidokezo vya kuepuka matatizo:

  • Fuatilia madai yako ya “kuzuia tu” na uripoti matatizo yoyote utakayoona moja kwa moja kwa msimamizi wako wa washirika.
Sera kuhusu hatua za kuchukua mwenyewe kwenye Content ID
Content ID hutegemea hatua kadhaa za ukaguzi zinazochukuliwa na wadhibiti wa maudhui wenyewe. Hatua hizi ni pamoja na, lakini si tu:
  • Kutatua umiliki tatanishi wa vipengee na nakala za marejeleo.
  • Kukagua madai ya hakimiliki yanayoweza kuibuka na yanayopingwa.

Masharti ya sera

  • Hatua za kuchukua mwenyewe zinahitaji ukaguzi wa binadamu na haziwezi kuwekwa kiotomatiki au kwa usanidi.
  • Hatua zote za kuchukua mwenyewe, kama vile kuthibitisha madai yanayoweza kuibuka au yanayopigwa, ni lazima:
    • Ziangazie kwa usahihi upeo wa umiliki wako.
    • Zitii sheria na kanuni zote zinazotumika.
    • Zitii sera zote za YouTube, kama vile masharti ya kujiunga na mpango wa uchumaji mapato.

Vikwazo

  • Usichukue hatua mwenyewe kwenye Content ID zinazosababisha kuzuiwa kwa maudhui ambayo 1) yanakukosoa wewe au wateja unaowakilisha na 2) yana madondoo ya kazi yako inayolindwa kwa hakimiliki.
    • Neno “ukosoaji” linamaanisha kuwa madhumuni ya kutumia maudhui hayo ni kukosoa na/au kuonyesha maudhui, wahusika wake, watayarishi wake, au wenye haki za maudhui hayo kwa njia hasi au isiyopendeza.
    • “Hatua za kuchukua mwenyewe” ni pamoja na, lakini si tu, kutumia kipengele cha kudai mwenyewe au kubadilisha sera ya dai lililopo iwe ya kuzuia.
    • Tafadhali tuma ombi la kuondoa video la DMCA (Sheria ya Milenia ya Hakimiliki Dijitali) ikiwa unaamini kuwa maudhui yanakiuka kazi yako inayolindwa kwa hakimiliki.
    • Ombi lako la kuondoa video la DMCA (Sheria ya Milenia ya Hakimiliki Dijitali) likikataliwa na uombwe uzingatie hali zisizofuata kanuni za hakimiliki, bado huruhusiwi kuchukua mwenyewe hatua zozote za kuweka madai ya uzuiaji kwenye maudhui. Hii ni pamoja na, lakini si tu, kudai mwenyewe na kuweka sera ya uzuiaji kwenye maudhui.
Sera kuhusu udhibiti wa vipengee kwenye Content ID kwa uwajibikaji
Vipengee visivyo sahihi, visivyosomeka au vyenye nakala vinaweza kuleta matatizo kwenye mfumo wa Content ID. Kwa sababu hii, YouTube inatarajia wadhibiti wa maudhui wawe wasimamizi wazuri wa vipengee wanavyomiliki. Wadhibiti wa maudhui wasiofanya hivyo wanaweza kuzuiwa kufikia vipengele vya Mfumo wa Kudhibiti Maudhui (CMS) au wawekewe vikwazo vingine.

Masharti ya sera

  • Vipengee vyote ni lazima viwe na metadata sahihi, isiyobadilika na inayoweza kusomeka na binadamu.
    • Aliyepakia anapaswa kuelewa bayana maudhui yanayodaiwa, na kufahamu mmiliki wa maudhui hayo. Kiwango cha chini zaidi cha metadata unayohitaji kujumuisha kinategemea aina ya maudhui:
      • Rekodi ya sauti au video ya muziki: jumuisha ISRC, jina, msanii na studio ya kurekodia.
      • Utungo wa muziki: jumuisha jina na mwandishi.
      • Kipindi cha runinga: jumuisha jina la onyesho na jina au nambari ya kipindi.
      • Filamu: jumuisha jina na waelekezi.
      • Utangazaji wa spoti: jumuisha majina ya wanaoshindana au timu na tarehe ya tukio.
      • Vipengee vingine vya wavuti: unapaswa kufafanua kwa usahihi maudhui ya marejeleo yanayohusishwa.
    • Ni wajibu wa washirika wa muziki kuhakikisha usahihi wa metadata wanayojumuisha kwa madhumuni ya uwasilishaji wa maudhui na utayarishaji wa Video za Picha.
    • Ikiwa metadata unayowasilisha haitimizi viwango vyetu vya ubora, tunahifadhi haki ya kuzuia au kusitisha uwasilishaji wako wa maudhui.
  • Wadhibiti wa maudhui ni sharti watumie aina ya kipengee inayofaa.
    • Kwa mfano, washirika hawapaswi kuunda vipengee vya wavuti kwa ajili ya maudhui ya muziki. Vipengee vya video za muziki haviwezi kutumiwa kwenye rekodi za maonyesho mubashara ambayo hayakutayarishwa na lebo ya muziki.
  • Usiunde nakala za vipengee vya maudhui ikiwa tayari kuna kipengee cha maudhui hayo kwenye mfumo wa Content ID. 
    • Weka umiliki wako kwenye vipengee vilivyopo badala ya kuunda vipya.
  • Usiweke umiliki wako kwenye kipengee ikiwa huna umiliki halisi wa mali hiyo ya uvumbuzi. 

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
12251531200897787208
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false