Mwongozo wa Faragha wa YouTube

Mwongozo wa Faragha wa YouTube

Tunachukulia kwa umakini usalama wa watumiaji wetu kwa kushughulikia masuala yanayoweza kuathiri faragha yao. Mwongozo wetu wa faragha unalenga watumiaji wote ulimwenguni. Yaani, ingawa huenda video husika haijakiuka sheria za faragha za nchi uliko, inaweza kuwa imekiuka mwongozo wa faragha wa YouTube.

Mwongozo wa Faragha wa YouTube unalenga kulinda faragha ya watumiaji huku ukiweka uwiano kati ya masilahi ya umma na ustahiki wa habari. Iwapo unaamini kuwa maudhui yanakiuka kanuni nyingine za Mwongozo wa Jumuiya ya YouTube, tunakuhimiza upate maelezo kuhusu jinsi ya kuripoti maudhui yasiyofaa.

Je, YouTube huamua vipi kama maudhui yanafaa kuondolewa kwa kukiuka faragha?

Ili tuzingatie kuondoa maudhui, ni lazima mhusika atambulike kimahususi na malalamiko tuliyoyapokea kutoka kwa mhusika huyo au mwakilishi wake wa kisheria ni lazima yamtambulishe mhusika kupitia picha, sauti, jina kamili, namba ya kitambulisho cha kitaifa, namba ya akaunti ya benki, maelezo ya mawasiliano (kama vile anwani ya nyumbani, anwani ya barua pepe), au maelezo mengine yanayoweza kumtambulisha kimahususi. Aidha tunazingatia maslahi ya umma, ustahiki wa habari, idhini na iwapo maelezo husika yanapatikana kwa umma vinginevyo wakati wa kubaini kama maudhui yanapaswa kuondolewa kwa kukiuka faragha. YouTube inahifadhi haki ya kutoa uamuzi wa mwisho unaobaini kama ukiukaji wa mwongozo wake wa faragha umetokea.

Ni nini maana ya kutambulishwa kimahususi?

Ili video ichukuliwe kwamba inakutambulisha kimahususi, ni lazima iwe na maelezo ya kutosha yanayowawezesha watu wengine kukutambua. Kumbuka kuwa hata kama unaweza kujitambua katika video, haimaanishi kuwa watu wengine wanaweza kukutambua kimahususi. Kwa mfano, jina la kwanza bila muktadha zaidi au picha zinazopita haraka, haziwezi kuchukuliwa kuwa zinakutambulisha kimahususi.

Utaratibu wa faragha kwenye YouTube

Ikiwa umewasilisha malalamiko kuhusu faragha, YouTube inaweza kumpa aliyepakia video nafasi ya kuiondoa au kubadilisha taarifa ya faragha yaliyo katika video hiyo. Tutamtaarifu aliyepakia video kuhusu uwezekano wa ukiukaji wa faragha na huenda tukampa saa 48 za kuchukua hatua kuhusu malalamiko hayo. Kwa wakati huu, mtayarishi anaweza kutumia zana za Kupunguza au Kutia Ukungu zinazopatikana kwenye Studio ya YouTube. Iwapo aliyepakia video amechagua kuondoa video badala yake, malalamiko yatafungwa. Iwapo video ambayo huenda imekiuka faragha itaendelea kuwepo, Timu ya YouTube itakagua malalamiko hayo.

Utaratibu wetu wa Kuwasilisha Malalamiko kuhusu Faragha huzingatiwa pia katika hali ambazo zinahitaji data binafsi au ya kifedha iondolewe haraka.

Kuripoti ukiukaji wa faragha

Ili utume malalamiko kuhusu faragha, fuata Utaratibu wa Kuwasilisha Malalamiko kuhusu Faragha. Ukiwa mlalamishi, tunaheshimu faragha yako katika mchakato huu. Hatutatoa utambulisho wako wala maelezo yako ya mawasiliano kwa aliyepakia video bila idhini yako. Utapokea mawasiliano kuhusu mchakato huu kupitia anwani ya barua pepe uliyotupatia. Weka @support.youtube.com (kwa mfano, privacy+abcdefg123456@support.youtube.com)kwenye kichujio chako cha taka ili uhakikishe kuwa unapokea barua pepe hizi.

Unatakiwa uwasilishe madai yako mwenyewe.

Hatukubali madai yanayotolewa kwa niaba ya watu wengine isipokuwa katika hali zifuatazo:

  • Mhusika ambaye faragha yake imekiukwa hana uwezo wa kufikia kompyuta
  • Mhusika ambaye faragha yake imekiukwa ni mtu ambaye yupo hatarini
  • Dai linatolewa na mzazi au mlezi anayetambulika kisheria wa mtu binafsi ambaye faragha yake imekiukwa
  • Dai linatolewa na mwakilishi wa kisheria wa mtu ambaye faragha yake imekiukwa
  • Ombi limetumwa na mwanafamilia wa karibu kwa niaba ya mtu aliyeaga dunia

Hatutakubali malalamiko kuhusu faragha yanayowasilishwa kwa niaba ya:

  • Wanafamilia wengine (kama vile mume, mke, binamu, ndugu wa kiume au wa kike)
  • Wafanyakazi wenza au waajiriwa (ni lazima kila mtu atume ripoti yake mwenyewe)
  • Kampuni

Vidokezo vya jinsi ya kuwasilisha malalamiko kamili kuhusu faragha

  • Toa maelezo mafupi na dhahiri ili Timu ya YouTube iweze kukutambua kwenye video.
  • Tumia mihuri ya wakati kuonyesha matukio yote ambapo unaonekana kwenye video.
  • Katika sehemu ya maelezo, bainisha mavazi uliyovaa au mambo unayoyafanya, ambayo yanakutofautisha na watu wengine kwenye video.
  • Hakikisha kuwa umeweka URL ya video katika ripoti yako. Ikiwa unaripoti chaneli nzima hutahitaji kutuma URL.
  • Ikiwa unaripoti maoni yaliyotolewa katika sehemu ya maoni ya video, yaandike katika sehemu ya maelezo. Weka jina la aliyetoa maoni katika sehemu ya jina la mtumiaji.

Kupokea taarifa ya ukiukaji wa faragha

YouTube inaweza kukupa wewe, uliyepakia video, nafasi ya kuondoa au kubadilisha taarifa za faragha zilizo kwenye video yako. Katika hali hii, tutakutumia barua pepe kuhusu uwezekano wa ukiukaji wa faragha na kukupa saa 48 za kuchukua hatua kuhusu malalamiko hayo. Ukiondoa video inayodaiwa kukiuka faragha kwenye tovuti ndani ya saa 48, tutafunga malalamiko yaliyowasilishwa. Ikiwa video iliyoripotiwa kwamba inakiuka faragha itaendelea kuwa kwenye tovuti baada ya saa 48, Timu ya YouTube itakagua malalamiko hayo.

Tukiondoa video yako kwa sababu ya kukiuka faragha, usipakie toleo lingine linaloangazia watu wao hao. Watu hao wanaweza kuwasilisha malalamiko mengine kuhusu faragha au wakuripoti kwa unyanyasaji. Tuko makini kuhusu kulinda watumiaji wetu na huwa tunasimamisha akaunti ambazo zinakiuka faragha ya wengine.

Ninaweza kuchukua hatua gani kuhusu malalamiko?

  • Unaweza kuondoa kabisa maudhui yaliyoripotiwa kwenye tovuti.
  • Ikiwa umeweka jina kamili au taarifa binafsi za mtu mwingine kwenye kichwa, ufafanuzi au lebo za video yako, unaweza kubadilisha maelezo haya kwa kwenda kwenye Video kisha ubofye kitufe cha 'Badilisha' kwenye video iliyoripotiwa.
  • Unaweza kutia ukungu kwenye nyuso za watu ambao wanaonekana kwenye video.  

Hatukubali mbinu za uondoaji ambazo si kamili kama vile:

  • Kufanya video iwe ya faragha, kwa sababu aliyeipakia anaweza kubadilisha hali hiyo kutoka ya faragha na kuifanya ionekane kwa umma wakati wowote.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
16215691114429625719
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false