Kuwasha au kuzima huduma ya uanachama katika chaneli

Uanachama Katika Vituo
Kumbuka kuwa ni wajibu wako kutii sera, sheria na masharti ya YouTube pamoja na sheria na kanuni zote husika unapotumia uanachama katika chaneli.

Uanachama katika chaneli yako

Chaneli zinazotimiza masharti zinaweza kuwasha huduma ya uanachama katika chaneli

Ili uchume mapato kutokana na uanachama katika kituo, ni lazima wewe (na Mtandao wako wa Vituo Mbalimbali) kwanza mkubali Sehemu ya Bidhaa za Biashara (CPM). Ili upate maelezo zaidi kuhusu CPM, angalia sera zetu za uchumaji wa mapato katika Bidhaa za Biashara kwenye YouTube

Iwapo ungependa kutumia kompyuta ili uwashe uanachama katika kituo: 

  1. Kwenye kompyuta, ingia katika akaunti kwenye Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, bofya Chuma mapato.
  3. Bofya kichupo cha Uanachama. Kichupo hiki kitaonekana tu iwapo kituo chako kimetimiza masharti.
  4. Bofya Anza kisha ufuate maagizo yaliyo kwenye skrini.
  5. Iwapo ni mara yako ya kwanza katika sehemu ya Uanachama, fuata maagizo yaliyo kwenye skrini ili utie sahihi kwenye Sehemu ya Bidhaa za Biashara (CPM).

Iwapo ungependa kutumia kifaa chako cha mkononi ili uwashe uanachama katika kituo:

  1. Fungua programu ya Studio ya YouTube ya vifaa vya mkononi .
  2. Katika sehemu ya chini ya skrini, gusa Chuma mapato .
  3. Gusa kadi ya Uanachama kisha ufuate maagizo yaliyo kwenye skrini. Iwapo kadi ya Uanachama haitaonekana, gusa Anza katika sehemu ya “Uanachama”.
  4. Iwapo ni mara yako ya kwanza kuwasha uanachama, fuata maagizo yaliyo kwenye skrini ili utie sahihi kwenye Sehemu ya Bidhaa za Biashara (CPM).

Pata maelezo zaidi kuhusu kutimiza masharti na jinsi ya kudhibiti uanachama katika chaneli.

Kuzima kipengele cha uanachama katika chaneli

Kumbuka: Wakati umezima huduma ya uanachama katika chaneli, malipo yote yanayorudiwa yanayolipwa na wanachama yatakatishwa. Hutaweza kuwarejesha wanachama hawa kiotomatiki. Ni lazima watazamaji wajiunge tena kwa hiari yao kwenye mpango wa uanachama katika chaneli yako.
  1. Kwenye kompyuta, ingia katika Akaunti yako ya Google.
  2. Nenda kwenye ukurasa wa Uanachama.
  3. Bofya Mipangilio  kisha Zima Uanachama kisha Zima.

Kumbuka kwamba ukizima uanachama katika chaneli, viwango na manufaa hayatahifadhiwa.

Iwapo uanachama utasimamishwa kwenye chaneli kwa sababu ya kusimamishwa kwa chaneli, kuondolewa kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube au kutokana na matumizi mabaya, ulaghai au ukiukaji wa sera au sheria na masharti yetu, wanachama wote wanaoendelea kulipia uanachama watarejeshewa pesa za malipo yao ya mwezi wa mwisho. Mgawo wa chaneli wa mapato yatakayorejeshwa utakatwa kwenye chaneli.

Uanachama katika chaneli kwenye mtandao wako

Kuruhusu mtandao uwashe huduma ya uanachama katika chaneli

  1. Kwenye kompyuta, ingia katika akaunti kwenye Studio ya YouTube.
  2. Nenda kwenye Mipangilio.
  3. Bofya "Makubaliano" na ukubali Sehemu ya Bidhaa za Biashara.

Kughairi, kukatiza na kurejeshewa pesa

Iwapo wanachama wataomba kurejeshewa pesa, YouTube, kwa hiari yake, itatoa uamuzi kuhusu dai hilo. Tunapowarejeshea wanachama pesa, mgawo wako utakatwa kwenye akaunti ya AdSense katika YouTube ili tuwarejeshee wanachama pesa. Pata maelezo zaidi kuhusu sera ya kurejesha pesa ya YouTube kwa uanachama wa chaneli unaolipishwa.

Uanachama ukisimamishwa kwenye kituo kwa sababu kituo kimesimamishwa, wanachama wote wanaolipa watarejeshewa malipo yao ya mwisho. Sababu zingine za kurejesha pesa ni pamoja na kuondolewa kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube au kwa sababu ya matumizi mabaya, ulaghai au ukiukaji wa sheria na masharti au sera zetu. Mgawo wa chaneli wa mapato yatakayorejeshwa utakatwa kwenye chaneli.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
256197074894911605
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false