Kuvinjari programu ya YouTube kwenye televisheni yako

Programu ya YouTube inapatikana kwenye televisheni zinazoweza kuunganisha kwenye intaneti, vifaa vya kutiririsha na vifaa vingi vya michezo ya video. Ingia katika akaunti kwenye programu, angalia vituo unavyofuatilia, tafuta maudhui na utumie kifaa chako cha mkononi kama kidhibiti cha mbali. Unaweza pia kutazama YouTube kwenye televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti kwa kuunganisha vifaa vyako

Angalia iwapo programu ya YouTube inapatikana katika eneo unakoishi.

Maeneo inakopatikana

Ajentina

Lasembagi

Australia

Malesia

Austria

Malta

Azabajani

Meksiko

Bahareni

Montenegro

Bangladeshi

Moroko

Belarusi

Nepali

Ubelgiji

Uholanzi

Bolivia

Nyuzilandi

Bosnia na Hezegovina

Nikaragua

Brazili

Naijeria

Bulgaria

Masedonia Kaskazini

Kanada

Norwe

Chile

Omani

Kolombia

Pakistani

Kostarika

Panama

Korasia

Papua

Kuprosi

Paragwai

Zechia

Peru

Denmaki

Ufilipino

Jamhuri ya Dominika

Polandi

Ekwado

Ureno

Misri

Pwetoriko

Elsavado

Katari

Estonia

Romania

Ufini

Urusi

Ufaransa

Saudia

Jojia

Senegali

Ujerumani

Sabia

Ghana

Singapoo

Ugiriki

Slovakia

Gwatemala

Slovenia

Hondurasi

Afrika Kusini

Hong Kong

Korea Kusini

Hangaria

Uhispania

Aisilandi

Srilanka

India

Uswidi

Indonesia

Uswisi

Iraki

Taiwani

Ayalandi

Tanzania

Israeli

Tailandi

Italia

Tunisia

Jamaika

Uturuki

Japani

Uganda

Yordani

Ukraini

Kazakistani

Uingereza

Kenya

Marekani

Kuwaiti

Urugwai

Lativia

Venezuela

Lebanoni

Vietnamu

Libya

Yemeni

Lishenteni

Zimbabwe

Litwania

 

Jinsi ya Kuingia Kwenye YouTube katika Televisheni Yako

Fahamu jinsi ya kutumia programu ya YouTube kwenye televisheni

Kuingia au kuondoka katika akaunti ya programu ya YouTube

Unaweza kuingia katika akaunti ya YouTube kwenye televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti, kifaa cha kutiririsha au kifaa cha michezo ya video. Unaweza pia kuondoka katika akaunti ya programu au kuondoa akaunti kwenye programu.

Kubadilisha kati ya akaunti moja na nyingine

Katika programu ya YouTube kwenye televisheni yako, unaweza kuingia katika akaunti nyingi na kubadili akaunti hizi kwa urahisi.

Kumbuka: Ukichagua wasifu wa mtoto wako au wasifu wa mgeni kwenye YouTube Kids, utaingia katika YouTube Kids. Pata maelezo zaidi kuhusu hali hii ya utumiaji.

Wanafamilia wako wanaweza kuweka akaunti zao na wageni wanaweza kuingia katika Akaunti ya mgeni. Akaunti za wageni zinakuwezesha kutumia YouTube kwenye televisheni yako bila kuingia katika akaunti na maudhui yoyote unayotazama bila kuingia katika akaunti hayataathiri maudhui yanayopendekezwa kwenye akaunti yako.

Kutafuta video za kutazama

Una njia kadhaa za kutafuta video katika programu:
Kwenye huduma ya Tafuta
  • Unaweza kutumia huduma ya Tafuta kwenye menyu ya kushoto.

Kwenye kichupo cha ukurasa wa Mwanzo

  • Pitia gridi ya video zinazopendekezwa kwenye kichupo cha Ukurasa wa Mwanzo .
  • Chagua menyu ya kushoto ili ufungue sehemu ya ziada ya viungo muhimu. Unaweza kupitia vichupo tofauti, kama vile Zinazopendekezwa, Zinazovuma, au Muziki.

Kwenye kichupo cha Vituo unavyofuatilia

  • Pitia gridi ya video zinazopendekezwa kwenye vituo unavyofuatilia.
  • Pitia vituo unavyofuatilia ili kuona video au orodha mpya zaidi za kucheza kwenye kituo.

Kwenye Ukurasa wa kutazama

  • Nenda chini kisha uchague Tafuta .

Hifadhi video kwenye orodha za kucheza

Unaweza kuweka video kwenye orodha za kucheza ambazo umeshaziunda kwenye vifaa vingine. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuunda na kudhibiti orodha za kucheza.
Ili uhifadhi video kwenye orodha ya kucheza:
  1. Kwenye ukurasa wa kutazama wa video, chagua Hifadhi video .
  2. Chagua orodha ya kucheza ambako ungependa kuhifadhi video.

Kufikia Maktaba Yako

Kwenye kichupo cha Maktaba , unaweza kupata vichupo vya Historia yako, Video zangu, Video za kutazama baadaye, Filamu na vipindi vyako vya televisheni na Orodha za kucheza.

Kusasisha Mipangilio Yako

Ili ufikie mipangilio ya akaunti yako, chagua Mipangilio katika menyu ya kushoto. , unaweza kubadilisha mipangilio ya kucheza kiotomatiki, hali yenye mipaka na kuunganisha televisheni yako kwenye kifaa chako cha mkononi.

Kutumia kifaa kingine kama kidhibiti chako cha mbali

Tumia simu, kishikwambi au kompyuta yako kama kidhibiti cha mbali. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuunganisha kifaa chako ili ukitumie katika programu ya YouTube kwenye televisheni yako.

Kudhibiti foleni ya televisheni yako

Weka, angalia na uondoe video kwenye foleni ya televisheni yako unapounganisha simu, kishikwambi au kompyuta kwenye televisheni yako kupitia mchakato wa kutuma maudhui.

Kuweka video kwenye Foleni ya Televisheni yako

  1. Gusa Zaidi '' karibu na video unayotaka kuweka.
  2. Gusa Weka kwenye Foleni.

Angalia Foleni ya Televisheni Yako

Foleni ya televisheni yako itakuwa kwenye dirisha lililopunguzwa katika sehemu ya chini ya ukurasa wa YouTube kwenye simu yako. Telezesha kidole juu kwenye dirisha lililopunguzwa ili ufungue na uangalie foleni yako.

Kuondoa video kwenye Foleni ya televisheni yako

  1. Angalia Foleni ya Televisheni Yako.
  2. Gusa Zaidi '' karibu na video unayotaka kuondoa.
Gusa Ondoa kwenye Foleni.

Utatuzi na maoni

Utatuzi

Ikiwa unakumbwa na tatizo la kutazama YouTube kwenye televisheni yako, fuata mwongozo wetu wa utatuzi.

Kutuma maoni kwenye YouTube

Tunalenga kuboresha bidhaa zetu kila wakati na tunathamini maoni yako. Ili utume maoni kuhusu hali ya utumiaji wa bidhaa mpya, nenda kwenye https://www.youtube.com/tv_feedback katika simu, kishikwambi au kompyuta ya kupakata.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
2088076985055456257
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false