Chuma mapato kwenye mtiririko wako mubashara

Taarifa za hivi karibuni

Unaweza kuchuma mapato kwenye mitiririko yako mubashara kwa:

Baadhi ya chaneli zinaweza pia kufikia uanachama katika chaneli wa watazamaji wao.
Kumbuka: Ikiwa kichezaji kimepachikwa kwenye tovuti ya nje yenye kipengele cha kuanza kucheza kiotomatiki, matangazo yatazimwa kwenye mtiririko wako mubashara.

Matangazo kwenye mitiririko mubashara

Iwapo kituo chako kinachuma mapato na mtiririko wako mubashara unastahiki, YouTube itaonyesha matangazo kwenye maudhui yako. Hakuna uhakika kwamba matangazo yataonyeshwa na baadhi ya watazamaji huenda wasione tangazo. Mitiririko mubashara inaweza kutimiza masharti ya:

  • Matangazo ya kabla ya video huonyeshwa kabla ya mtiririko mubashara. Unaweza kutazama matangazo haya kwenye kifaa cha mkononi na kompyuta. Matangazo ya kabla ya video huwashwa kiotomatiki katika mitiririko mubashara.
  • Matangazo yanayochezwa katikati ya video huonyeshwa wakati wa mtiririko mubashara. Matangazo haya yanaweza kuwekwa kiotomatiki au na mtayarishi mwenyewe.
  • Matangazo ya maonyesho huonyeshwa kando au juu ya maudhui. Unaweza kutazama matangazo haya kwenye kompyuta.

Kuweka matangazo yanayochezwa katikati ya video

Weka matangazo yanayochezwa katikati ya video kwenye mtiririko mubashara:

  1. Fungua Studio ya YouTube.
  2. Bofya Tayarisha kisha Tiririsha mubashara.
  3. Anzisha mtiririko mubashara sasa kwenye kichupo cha 'Tiririsha' au uratibu mtiririko mubashara kwenye kichupo cha 'Dhibiti'.
  4. Kwenye sehemu ya juu, bofya Badilisha kisha Uchumaji wa mapato.
  5. Hakikisha Umewasha Uchumaji wa Mapato.
  6. Chagua mipangilio ya matangazo ya mtirirko wako mubashara:
    1. Ruhusu YouTube ikuwekee matangazo: YouTube huonyesha matangazo yanayochezwa katikati ya video kwa watazamaji katika wakati unaofaa wakati wa mtiririko mubashara na uchague mara za kujirudia za mapumziko ya matangazo:
      1. Kiwango cha chini: kujirudia mara chache zaidi na uwezekano wa mapato ya chini zaidi
      2. Wastani: kujirudia kwa wastani na uwezekano wa wastani wa kuchuma mapato
      3. Kiwango cha juu: kujirudia mara nyingi zaidi na uwezekano wa juu zaidi wa kuchuma mapato
      4.  Kumbuka: Bado tutakufahamisha tangazo linapokaribia kuonyeshwa kwa watazamaji, ikiwa ungependa kuliruka
    2. Chagua jinsi matangazo yatakavyoonekana: Unaweza kuchagua mwenyewe kila pumziko la tangazo linalochezwa katikati ya video AU uchague kiwango cha muda unaopenda upite baina ya matangazo. Ukichagua kuweka matangazo kulingana na muda, unaweza kuchagua kati ya dakika 6, 12, 18, 24 au 30.
      1. Kumbuka: Uwezekano wako wa kuchuma mapato unaweza kuwa chini zaidi unaporuhusu YouTube ikuwekee matangazo.
  7. Bofya Inayofuata kisha uendelee kuweka mipangilio ya mtiririko wako mubashara.
Vidokezo:
  • Hakuna uhakika kwamba watazamaji wote wataona tangazo linalochezwa katikati ya video. Ikiwa hakuna tangazo linaloonyeshwa, watazamaji wataendelea kutazama mtiririko wako mubashara.  
  • Mtazamaji akiruka tangazo au tangazo likiisha, ataendelea kutazama mtiririko mubashara.

Ucheleweshaji wa tangazo linalochezwa katikati ya video

Ukichagua kuruhusu YouTube ikuwekee matangazo yanayochezwa katikati ya video, unaweza kuchelewesha matangazo yanayochezwa katikati ya video wakati wa matukio muhimu ambapo hutaki watazamaji wakatishwe.

Kwenye Ukurasa wa Kudhibiti Utiririshaji wa Moja kwa Moja, nenda kwenye sehemu ya juu kulia kisha ubofye Chelewesha matangazo . Matangazo yanayochezwa katikati ya video yanacheleweshwa kuonekana kwa watazamaji kwa dakika 10. Kihesabu muda uliosalia cha sekunde 5 kitaonekana kwenye LCR kabla matangazo hayajaendelea.

Kumbuka: Matangazo yanayowekwa katikati ya video bado yataonyeshwa wakati kipengele cha kuchelewesha matangazo kimewashwa.

Mipangilio ya kiwango cha chaneli ya matangazo yanayochezwa katikati ya video

Chaneli zinazochuma mapato zisizo na udhibiti wa haki zinaweza kuweka mipangilio chaguomsingi ya tangazo linalochezwa katikati ya video kwenye mitiririko mubashara ya baadaye katika kiwango cha chaneli. Mipangilio ya kiwango cha chaneli inakuruhusu uchague mipangilio ya uchumaji wa mapato itakayokuwa chaguomsingi kwa mitiririko mubashara yoyote mipya itakayoanzishwa.

Ili uchague mipangilio ya kiwango cha chaneli: Fungua Ukurasa wa Kudhibiti Utiririshaji wa Moja kwa Moja kisha Kwenye kona ya chini kushoto, bofya Mipangilio .

Mapato ya matangazo kwenye mitiririko mubashara

Unaweza kuangalia mchanganuo wa mapato ya matangazo yako kwenye mitiririko mubashara na mitiririko mubashara iliyochezwa tena katika Takwimu za YouTube. Ili uangalie mchanganuo wa mapato ya matangazo yako kwenye mitiririko mubashara, changua kichujio cha Mubashara .

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
10379622211813465644
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false