Kutatua tatizo la kuondolewa kwa video

Lengo la maudhui haya ni kutoa usaidizi kwa video zilizoondolewa kwenye YouTube. Ikiwa unahitaji usaidizi wa kuondoa video, pata maelezo kuhusu jinsi ya kufuta video zako au kuripoti maudhui yasiyofaa.

Endapo utaona ujumbe wa "Video imeondolewa" karibu na mojawapo ya video ulizopakia, hii inamaanisha kwamba video yako imebainika kuwa imekiuka sera zetu na imeondolewa kwenye YouTube. Bofya sehemu iliyo hapo chini ili ufahamu hatua unazoweza kufuata ili kutatua tatizo. 

Sababu za kuondolewa na hatua unazoweza kuchukua

Maudhui yasiyofaa

Endapo utaona ujumbe wa "Video imeondolewa: Maudhui yasiyofaa" karibu na mojawapo ya video ulizopakia, hii inamaanisha kwamba video husika imebainika kuwa imekiuka Mwongozo wetu wa Jumuiya.

Jinsi ya kutatua tatizo

Imekiuka Sheria na Masharti

Endapo utaona ujumbe wa "Video imeondolewa: Ukiukaji wa Sheria na Masharti" karibu na mojawapo ya video zako, huenda video hiyo imekataliwa kutokana na ukiukaji wa Sheria na Masharti au hakimiliki. Soma Sheria na Masharti yetu na maelezo haya ya msingi ya hakimiliki kwa maelezo zaidi.

Inajumuisha maudhui yaliyo na hakimiliki

Endapo utaona mojawapo kati ya ujumbe hapa chini karibu na video zako, inamaanisha kwamba mmiliki wa maudhui amedai maudhui kwenye video yako kupitia mfumo wa YouTube wa Content ID:

  • Inajumuisha maudhui yaliyo na hakimiliki
  • Tumezima sauti kutokana na maudhui yaliyo na hakimiliki
  • Imezuiwa kote duniani
  • Imezuiwa katika baadhi ya nchi au maeneo

Chagua maandishi yanayotokea karibu ya video yako. Kiungo hiki kitakupeleka kwenye ukurasa wenye maelezo zaidi kuhusu madai ya hakimiliki yanayoathiri video yako. Chini ya "Maelezo ya Hakimiliki," utaona taarifa kuhusu maudhui yaliyotambuliwa katika video yako. 

Fahamu madai ya Content ID ni nini na jinsi yanavyoathiri video yako.

Video imeondolewa

Video yako imeondolewa kwenye YouTube kwa sababu mwenye hakimiliki ametutumia ombi kamili la kisheria la kuiondoa. Pia, umepokea onyo la hakimilki. Pata maelezo kuhusu jinsi maonyo ya hakimilki yanavyoweza kuathiri akaunti yako

Kuna njia tatu za kusuluhisha onyo lako la hakimilki. Hatua ya kufuta video yenye onyo haitasuluhisha onyo lako.

Tatizo la chapa ya biashara

Iwapo utaona ujumbe wa "Video imeondolewa - tatizo la chapa ya biashara", hii inamaanisha kwamba video husika imekiuka sera yetu ya chapa ya biashara.

Soma sera zetu za chapa za biashara ili uhakikishe unafahamu maudhui yanayokubaliwa kupakiwa kwenye YouTube.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
17640105856905326839
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false