Kuweka skrini za mwisho kwenye video

Unaweza kuweka skrini za mwisho kwenye sekunde 5–20 za mwisho kwenye video. Unaweza kuzitumia kutangaza video nyingine, kuwahimiza watazamaji wafuatilie kituo na mengineyo. Unaweza kuweka hadi vipengee vinne kwenye skrini yako ya mwisho kwenye video zilizo na uwiano wa kawaida wa 16:9. Uwiano mwingine unaweza kuruhusu vipengee vichache zaidi.

Kumbuka:

  • Ni lazima video yako iwe na urefu wa angalau sekunde 25 ili iweze kuwa na skrini ya mwisho.
  • Vipengee vingine vinavyowashirikisha watumiaji, kama vile vishawishi vya kadi na alama maalum za video, hubanwa wakati skrini ya mwisho inapojitokeza.
  • Skrini za mwisho hazipatikani kwenye video zilizobainishwa kuwa zinalenga watoto, katika programu ya YouTube music, video za flash, wavuti wa vifaa vya mkononi au video zinazozunguka digrii 360.

Skrini za Mwisho za Video zako

Kuweka skrini ya mwisho

  1. Ingia katika akaunti ya Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui.
  3. Bofya jina au kijipicha cha video ambayo ungependa kuhariri.
  4. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Kihariri.
  5. Chagua Skrini za mwisho  kisha uchague kipengee ambacho ungependa kuweka:
    • Kutumia kiolezo: Violezo vina vikundi vya vipengee ambavyo unaweza kubadilisha upendavyo ili uunde skrini ya mwisho.
    • Video: Angazia video uliyopakia hivi karibuni, video maarufu zaidi kwa watazamaji au video mahususi.
    • Orodha ya kucheza: Onyesha orodha ya kucheza ya YouTube ambayo ni wazi kwa umma.
    • Kufuatilia: Wahimize watazamaji wafuatilie kituo chako.
    • Kituo: Tangaza kituo kingine kwa kutumia ujumbe maalum.
    • Kiungo: Ikiwa umejiunga kwenye Mpango wa Washirika wa YouTube, unaweza kuunganisha kituo chako kwenye tovuti ya nje.
      • Kumbuka: Hakikisha kuwa tovuti yako ya nje uliyounganisha inatii sera zetu, ikiwa ni pamoja na Mwongozo wa Jumuiya na Sheria na Masharti yetu. Ukiukaji unaweza kusababisha kuondolewa kwa kadi au kiungo, maonyo au kufungwa kwa Akaunti yako ya Google.

  6. Bofya HIFADHI. 

Chaguo zaidi

  • Kuondoa aina ya kipengee: Bofya Futa kipengee ili uondoe aina ya kipengee. Unaweza kubofya Kipengee ili uchague kipengee kingine cha skrini ya mwisho.
  • Kubadilisha wakati wa kuonyesha kipengee: Bofya na uburute ncha za kihariri ili uweke wakati kipengee kitakapoanza na kumalizika. Unaweza pia kuweka wakati mahususi kwenye kisanduku kilicho karibu na kitufe cha Futa kipengee .
  • Kubadilisha mahali kipengee kilipowekwa: Bofya na uburute ndani ya kisanduku. Unaweza ​​kubofya gridi ndani ya kichezaji ili uonyeshe gridi juu ya onyesho la kukagua video. Unaweza pia kuchagua “Linganisha na gridi” na “Linganisha na kipengee” ili upate usaidizi wa mahali pa kuweka vipengee vyako.
  • Kuangalia onyesho la kukagua la skrini yako ya mwisho: Ili uone jinsi skrini yako ya mwisho inavyoonekana video yako inapocheza, chagua kitufe cha kucheza kwenye kicheza video.
  • Kuangalia vipimo vya skrini ya mwisho: Unaweza kuangalia utendaji wa skrini zako za mwisho katika ripoti ya kina kwenye Takwimu za YouTube.

Kubadilisha skrini ya mwisho upendavyo

Vipengee ni vipande vya maudhui unavyoweka kwenye skrini yako ya mwisho. Kuna njia nyingi za kubadilisha vipengee kwenye skrini yako ya mwisho upendavyo. Unaweza kutumia violezo, kubadilisha muda wa kuonyesha vipengee vyako na kuamua mahali vipengee vitaonyeshwa kwenye video yako.

Kutumia kiolezo

Violezo vina vikundi vya vipengee ambavyo unaweza kubadilisha upendavyo ili uunde skrini ya mwisho.

  1. Ingia katika akaunti kwenye Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Maudhui.
  3. Bofya video ambayo ungependa kuhariri.
  4. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Kihariri.
  5. Bofya Weka kipengee  ili utumie kiolezo chako.
  6. Bofya HIFADHI.

Kuondoa aina ya kipengee

  1. Chagua kipengee kwa kukibofya kwenye safu mlalo ya skrini ya mwisho ya Kihariri.
  2. Upande wa kushoto wa video, bofya Futa kipengee .
  3. Bofya Weka kipengee  ili uchague kipengee kingine cha skrini ya mwisho.
  4. Bofya HIFADHI.

Kubadilisha wakati wa kuonyesha kipengee

Unaweza kuchagua wakati ambao ungependa vipengee vya skrini yako ya mwisho vionyeshwe kwenye video yako. Vipengee vya skrini ya mwisho vitaonyeshwa wakati sawa kwa chaguomsingi. Unaweza kubadilisha upendavyo vipengee mahususi ili vionyeshwe nyakati tofauti.

  1. Chagua kipengee kwa kukibofya kwenye safu mlalo ya skrini ya mwisho ya Kihariri.
  2. Upande wa kushoto wa video, tafuta visanduku vinavyoonyesha muda wa kuonekana kwa skrini ya mwisho.
  3. Sasisha wakati wa kuanza au wakati wa kumalizika kwa kipengee.
  4. Bofya HIFADHI.

Unaweza pia kubadilisha wakati wa kuonyesha kipengee cha skrini yako ya mwisho kwa kutumia vishale kukiburuta kwenye safu mlalo ya skrini ya mwisho ya Kihariri.

Kubadilisha mahali kipengee kilipowekwa

  1. Chagua kipengee kwa kukibofya kwenye safu mlalo ya skrini ya mwisho ya Kihariri.
  2. Kwenye kicheza video, buruta kipengee hadi mahali upendapo.
  3. Bofya HIFADHI.
Kidokezo: Bofya gridi  ndani ya kichezaji ili uonyeshe gridi juu ya onyesho la kukagua video. Unaweza pia kuchagua “Linganisha na gridi” na “Linganisha na kipengee” ili upate usaidizi wa mahali pa kuweka vipengee vyako.

Kuangalia onyesho la kukagua la skrini yako ya mwisho

Ili uone jinsi skrini yako ya mwisho inavyoonekana video yako inapocheza, chagua kitufe cha kucheza  kwenye kicheza video.

Kinachoweza kuonekana kwenye skrini yako ya mwisho

Vipengee ni vipande vya maudhui unavyoweka kwenye skrini yako ya mwisho. Unaweza kupanua au kutumia kiteuzi kuelea juu ya baadhi ya vipengee ili uone maelezo zaidi. Unaweza kuweka hadi vipengee vinne katika skrini yako ya mwisho kwenye video zenye uwiano wa kawaida wa 16:9. Uwiano mwingine unaweza kuruhusu vipengee vichache zaidi.

Vipengee vinaweza kuangazia aina tofauti za maudhui:

  • Video au orodha ya kucheza:
    • Angazia video uliyopakia hivi karibuni.
    • Ruhusu YouTube ichague video inayomfaa mtazamaji zaidi kwenye kituo chako.
    • Chagua video au orodha yoyote ya kucheza (ya umma au ambayo haijaorodheshwa) kutoka kwenye kituo chako au chochote kingine.
  • Kufuatilia: Wahimize watazamaji wafuatilie kituo chako.
  • Kituo: Tangaza kituo kingine kwa kutumia ujumbe maalum.
  • Tovuti za nje: Ikiwa umejiunga na Mpango wa Washirika wa YouTube, unaweza kuunganisha kituo chako kwenye tovuti ya nje.
Kumbuka: Hakikisha kuwa tovuti yako ya nje uliyounganisha inatii sera zetu, ikiwa ni pamoja na Mwongozo wa Jumuiya na Sheria na Masharti yetu. Ukiukaji unaweza kusababisha kuondolewa kwa kadi au kiungo, maonyo au kufungwa kwa Akaunti yako ya Google.
Mbinu bora za kuunda skrini za mwisho
  • Angazia vipengee ambavyo vinafaa video husika.
  • Wahimize watazamaji kubofya ukitumia miito ya kuchukua hatua kwenye vipengee tofauti vya skrini ya mwisho.
  • Ikiwa unatumia picha maalum, tunapendekeza utumie picha ambayo ina upana wa angalau pikseli 300 x 300.
  • Hakikisha umeacha nafasi na muda wa kutosha mwishoni mwa video kwa ajili ya skrini ya mwisho. Hakikisha umezingatia sekunde 20 za mwisho kwenye video unapoihariri.
  • Unaweza pia kubadilisha wakati ambapo vipengee tofauti vya skrini ya mwisho vinaonekana ili vionyeshwe nyakati tofauti.
Kuangalia vipimo vya skrini ya mwisho

Unaweza kuangalia utendaji wa skrini zako za mwisho kwenye kichupo cha Kushiriki cha Takwimu za YouTube.

  1. Ingia katika akaunti kwenye Studio ya YouTube.
  2. Kwenye menyu ya kushoto, chagua Takwimu.
  3. Kwenye menyu ya juu, chagua Kushiriki.

Ikiwa unaangalia takwimu za kituo chako chote:

  • Ili ulinganishe ufanisi wa aina tofauti za vipengee, tumia kadi ya “Aina maarufu za vipengee vya skrini ya mwisho”.
  • Ili uone video zenye skrini za mwisho ambazo watazamaji walibofya sana, tumia kadi ya “Video maarufu kulingana na skrini ya mwisho”.

Ikiwa unaangalia takwimu za video mahususi:

  • Ili uone mara ambazo watazamaji wanabofya vipengee vya skrini yako ya mwisho, tumia kadi ya “Kiwango cha kubofya vipengee vya skrini ya mwisho”.

Masharti ya skrini za mwisho kwa watazamaji

Watazamaji hawawezi kuona skrini zako za mwisho katika sehemu hizi:

  • Kwenye wavuti wa vifaa vya mkononi (isipokuwa: wavuti wa vifaa vya mkononi vya iPad).
  • Katika programu ya YouTube Music au YouTube Kids.
  • Katika video za Flash.
  • Katika video zinazozunguka digrii 360.

Skrini za mwisho na video zilizobainishwa kuwa zinalenga watoto

Skrini za mwisho hazipatikani kwenye video zilizobainishwa kuwa zinalenga watoto.
Hata kama hapo awali uliweka skrini ya mwisho kwenye video yako, watazamaji hawataona skrini za mwisho hadhira yako ikibainishwa kuwa inalenga watoto.

Kumbuka: Huenda skrini yako ya mwisho isionyeshwe kila wakati au huenda ikaonyeshwa katika muundo tofauti na ulioweka. Tofauti hii hutokea tunapojitahidi kuboresha skrini za mwisho kulingana na utendaji, tabia ya watazamaji, kifaa na muktadha.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
14566896932279303428
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false