Fahamu jinsi ya kutumia Kidhibiti Maudhui cha Studio

Vipengele hivi vinapatikana tu kwa washirika wanaotumia Kidhibiti Maudhui cha Studio ya YouTube.

Kidhibiti Maudhui cha Studio ya YouTube ni zana ya wavuti inayotumiwa na washirika wa YouTube kudhibiti maudhui na haki zao kwenye YouTube. Kutegemea jukumu lako, utapata vipengele kadhaa au vyote kwenye menyu ya kushoto unapoingia katika akaunti ya Kidhibiti Maudhui:

 Dashibodi

Fuatilia matatizo tofauti yanayohitaji uchukue hatua, kama vile madai na mizozo kuhusu umiliki. Unaweza pia kufuatilia vituo vilivyo na maonyo ya hakimiliki, mialiko ya vituo ambayo haijajibiwa, na vituo vilivyosimamishwa kuchuma mapato.

 Video

Angalia orodha ya video zilizopakiwa au kutiririshwa mubashara na vituo vinavyohusishwa na Kidhibiti chako cha Maudhui. Hapa, unaweza kupakua video, kufuta video kadhaa mara moja, au kufanya masasisho mengi kwenye video zako kwa wakati mmoja. Unaweza pia kuchuja  ili uone video zilizo na madai ya hakimiliki, maonyo, na zilizoainishwa vinginevyo.

 Vipengee

Pata muhtasari kuhusu vipengee vinavyohusishwa na Kidhibiti chako cha Maudhui. Unaweza kuhamisha data ya vipengee, kuangalia na kubadilisha metadata ya vipengee na kubadilisha vipengee vingi kwa wakati mmoja. Ili upate kipengee unachotafuta, chuja  kulingana na aina ya kipengee, madai na vigezo vingine. Pata maelezo zaidi kuhusu vipengee.

 Lebo za vipengee

Tazama orodha ya lebo za vipengee vinavyohusishwa na Kidhibiti chako cha Maudhui. Unaweza pia kuangalia madai yanayojumuisha vipengee vilivyo na lebo fulani. Pata maelezo zaidi kuhusu lebo za vipengee.

 Matatizo

Shughulikia matatizo yanayohitaji uchukue hatua na ambayo huenda yanaathiri vipengee, marejeleo au madai yako. Pata maelezo zaidi kuhusu madai ambayo huenda yakatokea, yaliyopingwa, na yaliyokatiwa rufaa, mizozo kuhusu umiliki na uhamishaji, marejeleo batili na ukinzani wa kulingana kwa marejeleo.

 Vituo

Angalia orodha ya vipimo na ruhusa za vituo vinavyohusishwa na Kidhibiti chako cha Maudhui. Kidhibiti chako cha Maudhui kinaweza kuunganisha vituo vingi kwa kuanzisha vituo au kualika vituo vingine kujiunga kwenye akaunti yako ya Kidhibiti Maudhui.

 Video Zinazodaiwa

Angalia orodha ya video zinazodaiwa pamoja na vipengee vinavyohusishwa nazo. Madai dhidi ya video fulani huwekwa pamoja ili kukuwezesha kukagua na kushughulikia madai hayo kwa ufanisi. Pata maelezo zaidi kuhusu video zinazodaiwa.

 Sera

Kagua na ubadilishe sera zako maalum au buni sera mpya ili udhibiti zaidi maudhui yako. Unaweza pia kuongeza sera zilizoratibiwa ambazo zitaanza kutumika saa na tarehe iliyobainishwa. Pata maelezo zaidi kuhusu sera.

 Takwimu

Pata maelezo zaidi kuhusu utendaji wa maudhui yako kote kama vile kwenye video, vituo au vipengee. Unaweza kufuatilia mapato, demografia ya hadhira, vyanzo vya watazamaji, na maelezo mengine kupitia vipimo na ripoti zilizosasishwa. Pata maelezo zaidi kuhusu Takwimu.

 Kampeni

Angalia orodha ya kampeni za awali, za sasa na zijazo na vipengee husika katika kampeni hizo. Unaweza kutumia vipengee kuanzisha kampeni ili kukuwezesha uteue kipengee mahususi, au unaweza kutumia lebo kuanzisha kampeni ili kukuwezesha uteue vipengee vinavyohusishwa na lebo mahususi za vipengee. Pata maelezo zaidi kuhusu kampeni.

 Orodha ya walioruhusiwa

Orodha ya walioruhusiwa huonyesha vituo ambavyo vimeondolewa madai kiotomatiki kuhusiana na vipengee vya Kidhibiti chako cha Maudhui. Unaweza pia kuweka chaneli zaidi kwenye orodha yako ya walioruhusiwa ukitumia kitambulisho au URL ya chaneli. Pata maelezo zaidi kuhusu orodha za walioruhusiwa.

 Ripoti

Angalia na upakue ripoti za mapato, video, vipengee, marejeleo, madai na kampeni. Ripoti hizi zinapatikana kila wiki au kila mwezi. Pata maelezo zaidi kuhusu ripoti.

 Uwasilishaji wa Maudhui

Tazama na upakue vifurushi vya maudhui yaliyopakiwa kwenye Kidhibiti chako cha Maudhui. Violezo vya kupakia vifurushi hivyo, na kuwasilisha na kusasisha maudhui vinapatikana katika ukurasa huu. Pata maelezo zaidi kuhusu kuwasilisha faili kwenye YouTube.

Mipangilio

Angalia na ubadilishe mipangilio ya akaunti kama vile arifa za barua pepe na mapendeleo ya mtumiaji. Ili kudhibiti ruhusa za akaunti, unaweza kuunda na kubadilisha majukumu tofauti ya watumiaji. Pata maelezo zaidi kuhusu Mipangilio ya akaunti ya Kidhibiti Maudhui.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
6331484788473135387
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false