Bidhaa Bandia

Google inapiga marufuku uuzaji au utangazaji wa mauzo ya bidhaa bandia katika bidhaa zake, ikiwa ni pamoja na YouTube. Bidhaa bandia zina nembo au chapa ya biashara ambayo inafanana na chapa halisi au huwezi kutofautisha kwa urahisi chapa hizo. Bidhaa bandia huiga vipengele vya chapa ya bidhaa halisi ili ziweze kuonekana kama bidhaa halisi ya mmiliki wa chapa hiyo.

Chaneli zinazotangaza na kuuza bidhaa bandia huenda zikafungwa.

Ikiwa unaamini video au kituo kinauza au kutangaza bidhaa bandia, unaweza kufungua Malalamiko kuhusu bidhaa bandia kupitia fomu yetu ya mtandaoni.

Tuma malalamiko kuhusu bidhaa bandia

Ni sharti tupokee malalamiko katika muundo huu ili tuchunguze. Timu yetu itachunguza malalamiko yako na kuondoa maudhui iwapo yanakiuka sera ya Google dhidi ya bidhaa bandia.

Tutakubali pia malalamiko kuhusu bidhaa bandia yasiyofuata mpangilio, yaliyotumwa kupitia barua pepe, faksi na barua.

Kumbuka kwamba matumizi mabaya ya fomu zetu za kisheria yanaweza kusababisha kufungwa kwa akaunti yako ya YouTube.

Je, maelezo haya yamekufaa?

Tunawezaje kuboresha?
Tafuta
Futa utafutaji
Funga kisanduku cha kutafutia
Menyu kuu
10522679336549388152
true
Tafuta kwenye Kituo cha Usaidizi
true
true
true
true
true
59
false
false